rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

DINI, MABADILIKO NA MAENDELEO

Inasemekana kuwa "Mabadiliko na maendeleo", vimethibitisha kuwa hakuna ulazima wa kuwepo Mwenyezi Mungu katika utaratibu wa Ulimwengu.

Ingawa jambo hili lafaa kuzungumziwa katika sehemu ya pili (Mungu wa Uislamu) ya masomo haya, ningependelea kutoa maoni machache ili mwanafunzi ayafikirie.

Kwanza, ni lazima ieleweke wazi kuwa, sizungumzii kuhusu ukweli au uongo wa maelezo yahusuyo mabadiliko na maendeleo, kwani hapa sio mahali pafaapo kulizungumzia zaidi jambo hili.

Pili, ni lazima ieleweke kuwa mabadiliko tu yatokeayo kwa viumbe asili vyenye uhai si 'Mabadiliko ya maendeleo'.

Kitabu cha maarifa yote kijulikanacho kwa jina la "World Book Encyclopaedia" cha 1966 kimeandikwa yafuatayo: "Ufafanuzi wa 'Mabadiliko na maendeleo ya viumbe vyenye uhai hujumlisha mawazo haya matatu yafuatayo:

1. Viumbe vyenye uhai hubadilika kizazi hadi kizazi vikitoa vizazi vyenye tabia zitofautianazo na zile za wahenga wao.

2. Tendo hili limetendeka kwa muda mrefu sana hata likazalisha vikundi vyote na aina zote za viumbe viishivyo sasa, na vile vilivyoishi zamani, ambavyo vimekwisha kufa au vimekwisha potea.

3. Hivi viumbe tofauti tofauti vyenye uhai vina uhusiano wa kiasili kati yao.

Tatu, ieleweke kuwa, ingawa kuna thibitisho hizo, maelezo kuhusu "Mabadiliko na maendeleo', bado ni makisio (theory) tu, wala sio ukweli (fact).

"Ukweli" kama Kamusi la Lugha ya Kiingereza lijulikanalo kwa jina la "Websters Third New International Dictionary", liufafanuavyo ni "Tukio halisi, katika muda au nafasi", ni "Habari zilizothibitishwa".

Hivi kuna uthibitisho gani juu ya maelezo haya ya 'Mabadiliko na Maendeleo?'

Mtaalamu mmoja wa 'Mabadiliko na Maendeleo' aliyejulikana sana, Bwana W. Le Gros Clark, ameandika katika kitabu chake kiitwacho "The Fossil Evidence for Human Evolution" hivi.

"Uwezekano wa kupata mabaki ya zamani ya miili ya wajenga halisi, au hata mfano tu wa Kikundi cha kijiografia cha mahali maalum, ambavyo ndivyo vilivyotoa wahenga hasa ni wa kubuniwa tu, kiasi ambacho haustahili hata kidogo kuufikiria ukweli wake.

"Ufafanuzi wa ushahidi kuhusu 'Maendeleo na mabadiliko' ya binaadamu wa zamani sana ulitokana na uchimbuzi wa sehemu walizoishi binaadamu wa zamani, ambao wameelezwa katika sura iliyopita ni ufafanuzi wa muda tu, kwa sababu ya kutotimilika kwa ushahidi huo haiwezekani kuwa vinginevyo zaidi ya hivi".

Gazeti liitwalo "Science News Letter" la mwaka 1965 lilisema hivi: "Kuna ugomvi baina ya wanasayansi kuhusu tu, jinsi mwanadamu alivyobadilika na kuendelea: ni lini alifanya hivyo na alivyokuwa kabla."

Bwana Clark tuliyemtaja hapo juu aliandika hivi, "Ni nini chanzo asili cha mwanaadamu?....Kwa bahati mbaya, majibu yo yote yawezayo kutolewa hivi hapa kuhusu maswali kama haya yanategemea ushahidi usio wa dhahiri kabisa, na kwa hivyo mengi ya majibu hayo ni makisio tu."

Rais wa zamani wa "Shirika la Umarikani Ia Maendeleo ya Sayansi aliandika katika gazeti liitwalo "Science Magazine" haya yafuatayo ili 'kuunga mkono' mabadiliko na Maendeleo:

Hebu njoo sasa, kama unaweza, katika safari ya kukisia ya nyakati za zamani sana zisizo na kumbukumbu za kuaminika. Tufikirie wakati ambao jamii ya viumbe vyenye akili vimetokea kutokana na aina ifananayo na.....; fanya hima katika muda wa maelfu ya miaka, muda ambao habari za sasa zautegemea, kwa ajili ya sehemu kubwa ya makisio ya ufafanuzi wa wakati wa kwanza wa kumbukumbu zilizoandikwa, ambazo kutokana nazo, uhakika fulani fulani waweza kuokotezwa."

Mwanasayansi mmoja wa Kiingereza, Bwana L. M. Davies wakati fulani alisema hivi:

"Imekisiwa kuwa, vifungu vya maneno visivyopungua 800 katika maneno yaonyeshayo wazo Ia kukisia (maneno kama vile "Tuchukulie tu," au Tunaweza kudhania kuwa" n.k) vinaonekana kati ya majalada ya kitabu cha Bwana Darwin kiitwacho "Origin of Species" (Asili ya viumbe vyenye asili moja), peke yake."

Ukivifikiria vifungu vya maneno tulivyoviandika hapo juu, na hasa maneno yale tuliyoyapigia mistari, utaamua kuwa "Mabadiliko na maendeleo si ukweli uliodumishwa ila ni maelezo tu miononi mwa maeIezo mengi yaliyokuwepo tangu mwanzoni mwa binaadamu, ili kuieleleza asili ya ulimwengu, Mengi ya maelezo ya namna hii, sasa yamedharauliwa, lakini hapo mwanzoni yalikuwa na nguvu akilini mwa watu kama yalivyo haya maelezo ya mabadiliko na maendeleo hivi sasa. Na nguvu zake hizi, katika akili ya watu, hazifanyi mawazo haya kuwa ya ukweli zaidi.

Hakika, mwanasayansi mmoja, Dakta T. N. Tahmisian, ambae ni mtaalamu wa mambo ya viumbe vyenye uhai, wa Tume ya Nguvu za Atomiki, alisema, "Wanasayansi waendao huku na huku na kufundisha kuwa maelezo kuhusu mabadiliko na maendeleo ni ukweli uliothibitika wa masiha ni wadanganyifu wakuu na hadithi watoazo kuyaeleza mabadiliko na maendeleo, hazina ukweli hata kidogo. Aliuita uelezaji wa mabadiliko na maendeleo kuwa ni "fumbo la mchezo wa mchanganyiko wa dhana na mazingaumbwe ya matumizi ya nambari."

Mwanasayansi mwingine aliyekuwa mkuu wa idara ya sayansi katika chuo kimoja, Bwana J. W. Klotz, alisema mnamo mwaka 1965 Masihiya kwamba, "kuyakubali maelezo ya mabadiliko na maendeleo bado kunategemea tu, kuwa ni imani zaidijuu yajambo hilo.

Na juu ya hapo maelezo haya mpaka sasa yanawajibikiwa kutafuta ushahidi utoshao kuyaunga mkono. Basi vipi maelezo haya yawezavyo kutumika kupinga maelezo ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu?

Mwisho kabisa, hata wanamabadiliko na maendeIeo wenyewe wanakubali kuwa kunahitajika kuwepo, "Mwenyezi Mungu Mwenye kuishi milele, Mjuzi wa yote, Mwenye nguvu zote." Katika utaratibu wa Ulimwengu kama inavyoelezwa katika maelezo ya "Mabadiliko na maendeleo."

Lakini, hapo mwanzo wanasayansi walikukataa kuwepo Mwenyezi Mungu; na kuzihusisha sifa njema hizi na "Asili", wanasema kuwa "Asili" ilichukua kile, na "Asili" ilifanya kile.

Hata hivyo hebu tutazame hii 'Asili' ni nini? Asili ni wazo la kuwazika tu, lililo katika ubongo wa watu, baada ya kujifunza kwa makini tabia za vitu. Asili yaweza kuonekana katika vitu; lakini si yenye kuishi yenyewe. Na kwa hali yoyote, hakunia kumbukumbu ya mkutano wo wote uliofanyika kuhusu asili za vitu mbali mbali; ili kuamua kuhusu jinsi ya kupatanisha kazi zao. Maua hayafanyi kazi pamoja na nyuki ili kutafuta ushirika wa nyuki katika uzalishaji wao, na kuwapa nyuki asali kama ujira wao. Bali twajua wazi kuwa nyuki hawawezi kuishi hata kwa siku moja tu, bila ya maua, na kuwa maelfu ya maua yangelipotea kama si sababu ya nyuki.

Hivyo basi, unaona kuwa wana mabadiliko na maendeleo wanatambua umuhimu wa Mtengenezaji na "Msanii". Lakini kimafundisho, wanafundisha kwa kurudia rudia kuwa, huyo Mtengenezaji na Msanii alikuwa ni "Asili" (fundisho ambalo ni oni la kuwazika tu) au "Jauhari" ambayo ni kitu kisicho na "Akili wala Uhai".