rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

KUTOIELEWA DINI

Mara kwa mara tunasikia maneno mabaya yakisemwa wazi wazi, ili kuipinga "Dini". Maneno haya yanatumiwa sana siku hizi, na Makomyunist. Maneno hayo ni:

(i) Dini inapinga sayansi

(ii) Dini ni dawa iliyogunduliwa na mabeparili kuwatuliza watu wa tabaka linalodhulumiwa, na kuwafanya watosheke na hali yao hiyo ya kimaskini, kwa usemi mwingine dini ilikuwa kasumba ya kuwalazia watu.

(iii) Dini huonelewesha maendeleo ya kimwili na kiakili.

Basi hebu ngoja tuzichunguze hoja hizi. Habari hizi hizi zimesemwa na Wazungu wengi toka Karl Marx hadi Bertrand Russel) ambao walikuwa na ujuzi wa dini moja tu, nayo ni Ukristo, hakika wametenda dhambi kubwa ya kiakili, kwa kuona dini fulani, na kudhania kuwa dini zote (hata Uislamu) ni lazima ziwe na fikara hizo hizo.

Hakika kwa vyo vyote vile maneno yao hayo kama si fikara zilizotolewa kwa shabaha maalum, ni udanganyifu mtupu.

Ili kuueleza kinaga naga usemi huo hapo juu, inatulazimu kuieleza kwa muhtasari tu hali ya fikara za Kimasihia ilivyokuwa kuhusu ujuzi na maendeleo.

Tangu karne ya kumi na sita ya baada ya Nabii Isa [a], ulitokea ugomvi kati ya Kanisa na sayansi. Ugomvi huu mbaya sana haukuanzwa na wanasayansi, ila ulianzwa na viongozi wa Kimasihia; ambao walihofu kuwa dini yao ilikuwa katika hatari kubwa ya kupoteza nguvu zake miongoni mwa Wamasihia. Ngome ya mafundisho yao ilikuwa katika hatari ya kuanguka. Madhehebu zote mbili (Wakatoliki na Maprotestanti) ingawa zilikuwa zikigombana zenyewe kwa zenyewe, zilikuwa na msimamo mmoja kuhusu mapambano baina ya mafundisho yao na njia za kimapinduzi za kisayansi, za Bwana Cupernicus, na mwenzie bwana Galileo. Walifanya kile kile ambacho kila mdhalimu anayeogopa unyoge wake wa kiasili angeliweza kukitenda. Mateso makali sana yalitolewa kwa wanasayansi washupavu waliolipinga Kanisa na ambao walisema kuwa kile wakijuacho kilikuwa ukweli mtupu.

(1) "Kwanza hatuna budi tumchukue Bwana Cupernicus (Nicolaus Koppernigh) aliyeishi kati ya mwaka 1473-1545, maana yeye alikuwa ndiye aliyeanzisha jambo hilo, Bwana huyu kwa muda mrefu hakuthubutu hata kuchapisha kitabu chake kijulikanacho kwa jina la "On the Revolution of Heavenly Bodies" (katika mzunguko wa sayari za Angani)." Kwa ajili ya kuliogopa Kanisa. Mwishoni alifaulu kulituliza Kanisa kwa kukiandika kitabu hicho kwa heshima ya Papa (afisa wa cheo cha juu sana wa Kanisa Katoliki). Mchapishaji wa kitabu hiki aliandika utangulizi kuthibitisha kuwa maelezo juu ya mzunguko wa dunia ni jambo linalokubaliwa tu, wala si jambo Iililothibitishwa kabisa. Kwa maneno ya Bwana Bertrand Russel, "Kwa muda fulani, mbinu hizi zilitosha, na ni kutokana na wito wa kijasiri wa Bwana Galileo (wa kuwaita wana dini kuja kushindana na Wanasayansi) ambao ulileta shutma za wakati uliopita wa Bwana Cupernicus (rejea katia kitabu kiitwacho "Religion and Science").

(2) Bwana Luther pia, aliupinga 'utaratibu' wa Bwana Cupernicus kwa kutumia njia za Kitheolojia (za kiujuzi wa Sifa na Tabia za Mwenyezi Mungu).

(3) Mwanasayansi mwingine, Bwana Galileo Galilei aliyeishi kati ya mwaka 1564-1642 Masihiy, ingawa alikuwa rafiki wa Papa Urban VllI, alitiwa katika jela ya Mahakama ya kuhukumu kesi za wazushi wa mambo ya kidini, kwa amri ya Papa huyo huyo na kutishiwa atapata mateso makali kama hataacha mafundisho yake hayo. Makosa ya Galileo yalikuwa kuunga mkono mafundisho ya Copernicus kutokana na uchunguzi alioufanya kwa darubini yake. Kwa upande wa Kanisa, uchunguzi huu ulikuwa mgumu zaidi kupambana nao, kuliko ile elimu ya kimaandishi tu ya Bwana Copernicus.

(4) Mwana Sayansi mwingine Bwana Giardino Bruno aliyeishi kati ya mwaka 1549-1600 Masihiy, alikuwa madhabuha mwingine wa ukatili uliotendewa wanasayansi. Bwana huyu alichomwa hali ya kuwa yu hai, Hababi Bertrand Russel, ameandika katika kitabu chake kiitwacho "Religion and Science" hivi: Wataalamu wa Elimu Lahuuti hawakuchelewa kusema kuwa, mafundisho hayo mapya yatafanya yale mafundisho ya kuchukua umbo la kiutu (incarnation, kwa mfano Yesu kuwa ni Mungu aliyegeuka katika umbo la Binaadamu) kuwa ni vigumu kuaminika.

(Rejea katika kitabu kiitwacho "Religion and Science").

"Hivyo mahakama ya hukumu za wazushi wa Kidini, ilitangizia haya yafuatayo kuwa ndiyo ukweli. "Usemi wa kwanza, kuwajua ndio kitovu (centre) cha Ulimwengu na kuwa jua haliizunguki dunia ni wa kijinga, kipuuzi, usio kweli hata kidogo katika Elimu lahuuti na ambao ni uzushi mtupu, maana hauafikiani na maandishi Matakatifu..... Usemi wa pili usemao kuwa dunia si kitovu cha ulimwengu na kwa hiyo dunia ina lizunguka jua ni upuuzi, ni uwongo katika elimu ya hekima (filosofia) na kwa upande wa elimu Lahuuti, kwa ujumla haitofautiani na imani sahihi." (Rejea katika kitabu kiitwacho "Religion and Science".)

Na kwa kuongezea zaidi, Kasisi wa Kanisa la Jesuit aliyeitwa Melchoir Inchofer ilimbidi aongezee kusema wazo lihusulo mzunguko wa dunia ni uzushi mtupu, lichukizalo zaidi, lenye madhara zaidi na lenye kuaibisha zaidi. Kutulia kwa dunia ni kutakatifu mara tatu; hivyo basi hoja zipingazo maisha ya milele ya roho, kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na wa Mungu kuchukua umbo Ia kiutu ni lazima zikubaIiwe upesi kuliko hoja zithibitishazo kuwa dunia inasogea. (Reja kitabu kiitwacho "ReIigion and Science).

Kwa sababu ya kukabiliwa na dhuluma kali, Wanasayansi waliueleza Ukristo, kuwa ni "imani isiyo pendelea mambo ya kiakili na isiyopendelea mambo ya Kisayansi; ni ushirikina na ni kitu kirudishacho nyuma maendeleo ya binaadamu." Jambo la kustaajabisha ni kuwa wameichukulia kila dini kwa ujumla kuwa ni sawa na Ukristo. Kwa hakika Uislamu hauwezi kuwekwa miongoni mwa dini 'zisizoafikiana na sayansi, zisizo za kihoja, au zisizoafikiana na maendeleo ya kibinaadamu.'