rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

Haja Ya Dini

Kimeandikwa na : Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Kimetafsiriwa na : Maalim Dhikiri Omari Kiondo

UTANGULIZI

(KWA MANENO YA MFASIRI)

Namshukuru Mwenyezi Mungu Tabarakal Lahu wa Taala, kwa kunipa muda wa kuanza hadi kumaliza tafsiri ya kijitabu hiki kilichoandikwa na Mwalimu wangu Maulana Sayyed Saeed Akhtar Rizvi, ambaye pia ni Chief Missionary wetu.

Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu chake kiitwacho "Need of Religion" alichokiandika kwa lugha ya Kiingereza, kwa ajili ya vijana wa Kiislamu wanaochukua "Diploma" ya Elimu ya Kiislamu kwa Njia ya Posta.

Nimeona kuwa kitabu hiki kitawasaidia sana ndugu zangu Waislamu wa hapa Afrika ya Mashariki, iwapo nitakitarajumu kwa Lugha ya Kiswahili, lugha ambayo hutumiwa sana hapa kwetu.

Kila mtu hupenda kitu na kukithamini sana baada ya kukiona kuwa ni cha faida kake. Kadiri ya faida ya kitu hicho itakavyozidi ndio jinsi mtu huyo atakavyozidi kukithamini na kukipenda kitu hicho.

Dini nayo ni hivyo hivyo, Mtu ataipenda tu, baada ya kuzielewa faida zake kwake.

Katika kijitabu hiki Allamah Sayyed Saeed Akhtar Rizvi, kwanza anaeleza Dini ni nini, kisha anaelezea faida zake, anakanusha hoja za wale wasemao kuwa dini ni kitu kipingacho sayansi n.k.

Analinganisha dini na "Maendeleo na Mabadiliko a viumbe", halafu anakanusha hoja za wale wasioamini kuwepo kwa siku ya Ufufuo. Mwisho kabisa anamalizia kwa kuzitaja sifa muhimu za dini.

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu aliyemjaalia ndugu yetu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa elimu na akatunufaisha sisi Waislamu wa hapa Afrika Mashariki na duniani pote kwayo.

Mwenyezi Mungu atujalie Waislamu, tuzidi kupata "Alim" kama huyu ndugu yetu. Tuwe wasikivu wa mahubirio yao, na Atuongoze katika Njia iliyonyooka Amin.

Allahuma Swali alaa Muhammadin wa-aali Muhammad.

Mallam: Dhikiri U. M. Kiondo.