rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

MADHEHEBU KATIKA UKRISTO

Japo Uislamu pia umegawanyika katika makundi mawili ya Sunni na Shia, lakini mgawanyiko huu ni wa kisiasa, sio wa kidini. Katika Ukristo mgawanyiko ni wa kidini. Japo wote wanamuamini Mungu, lakini tusimsahau Yesu - - - mambo yanakhitilafiana kuanzia hapa.

Ingawa idadi kamili haieleweki, ninafahamu takribani madhehebu hamsini ndani ya Ukristo, tukianzia na wa - Amish, ambao wameamua kujitenga na ulimwengu na mambo yote yanayorahisisha maisha (ya kisasa) kama vile umeme na magari, na kumalizia na Unitarians ambao wanaonekana mbele ya wakristo walio wengi kuwa sio wakristo kwa sababu hawaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu wala hawaamini utatu Mtakatifu.

Waromani Katoliki, ambao ni dhehebu la kikristo kubwa kuliko yote ulimwenguni leo, wanawatukuza watakatifu (saints) na mama wa Yesu. Mliwaji (yaani mkate) wakati wa kumunio inasemekana kwamba huwa ni mwili halisi wa Yesu, divai huwa ni damu halisi inapobarikiwa na padri.

Kwa sababu ya kutoridhishwa kwao na imani ya kutooa au kutoolewa (celibacy), kanisa la Orthodox lilijitenga kutoka Roma katika zama za kati (middle ages) na sasa hivi kanisa hili lina wafuasi wengi katika Ulaya ya Mashariki. Wanaendelea na mapambo katika makanisa yao kama yale ya kanisa katoliki lakini wana sikukuu tofauti na wanaapa kiapo cha utii kwa "Baba Mtakatifu" mwingine asiye kuwa Yule wa Roman Katoliki.

Mnamo mwaka 1517, kanisa la kiprotestanti lilianzishwa, kwa sababu ya kutokubaliana na baadhi ya mambo (vitendo) ndani ya kanisa katoliki. Baadhi ya mambo hayo ni:

1) Wakatoliki wanapamba na kuyanakshi makanisa yao. Waprotestanti wanayafanya kuwa rahisi.

2) Maandiko Matakatifu ya Wakatoliki yanajumuisha vitabu vya "Apocrypha" (vitabu vilivyofichikana ). Waprotestanti hawakubali kitabu chochote katika vitabu hivi.

3) Wakatoliki wana vinyago katika makanisa yao, majumba yao, katika magari yao. Pia wanavichimbia vinyago hivi mbele ya bustani za nyumba wanazotaka kuziuza, na wa misalaba iliyopambwa kwa umbo la Yesu akiwa amesulubiwa. Waprotestanti wanashutumu jambo hili kuwa ni "ibada ya masanamu" kwa hiyo wengi hawana hata msalaba mtupu (usiokuwa na sanamu ya Yesu) ndani ya makanisa yao.

Ndani ya tawi hili la Ukristo la Kiprotestanti kuna madhehebu mengine lukuki (mengi sana).

Walutherani wanafuata mafundisho ya Martin Luther. Baadhi ya Wakristo kutoka katika makanisa yaliyofanya Mageuzi (Reformed Churches). Hata hivyo waliona kuwa Martin Luther hakuwa mwangalifu na makini vya kutosha, hivyo waliamua kufuata mafundisho ya John Calvin.

Wa-Baptisti, ambao wanaamini kuwa watu wazima - - sio watoto - - ndio wanaotakiwa kubatizwa, waliuawa kikatili na wakatoliki na Waprotestanti katika Zama za Kati (Middle Ages) lakini sasa hivi wamekuwa miongoni mwa madhehebu makubwa ya Ukristo.

Kamwe Wakatoliki hawakuwa wa pole kuhusiana na harakati za Waprotestanti, na lilikuwa ni hitajio la uhuru wa kidini lililowahamisha Wazungu kutoka miji yao na kwenda katika nchi za ugenini. Wa-puritan walipohamia Amerika, katika karne ya kumi na saba, kundi la zima la madhehebu ya kikristo lilianza kuwepo katika miaka michache iliyofuatia.

Wa-shaker walikuwa na imani kali juu ya imani ya kutokuoa (ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu). Dhehebu hili leo limeshakufa (kutokana na ubovu wa imani na misingi yake).

Wapentekoste wanadai "kuzungumza kwa ndimi" (kuzungumza kwa Roho mtakatifu). Huduma zao za kanisa inasemekana zinafurahisha sana. Pia wanaamini kuwa Biblia ndani yake haina makosa hata kidogo - - - yaani haina kasoro au dosari japo ile ndogo kabisa. Kutokana na nyadhifa zao tumekuja kuwajua watu "maarufu" kama akina Jimmy Swaggert, Jim na Tammy Fay Bakker.

Mashahidi wa Yehova wanatumia muda wao mwingi kutafakari kitabu cha Ufunuo, wakiiota siku ambayo kila na mtu na kila kitu kitakhiliki (kitaangamia) isipokuwa wao.

Wa-Mormon walikuwa na mtume wao, Joseph Smith, ambaye aliwaletea kitabu cha maandiko ambacho wanaamini kuwa ni kitakatifu kama Biblia. Sera yao ya "ndoa za mbinguni" (yaani wake wengi bila mpaka) ilipelekea mwisho wa kuendelea kufanywa kuwa taifa (state) katika nchi hii.

Wanasayansi wa kikristo pia wana kitabu chao cha Maandiko mbali na Biblia; Mary Baker Eddy, mtume wao (wa kike) aliwaambia wafuasi wake kuwa imani na sayansi hushinda vyote - - - hata matamanio ya ngono (sexual desires).

Madhehebu mengi tofauti tofauti yakiwa na vitendo vingi tofauti tofauti, yote yameungana na kukubaliana kwamba imani yao ya Ukristo ndiyo "imani pekee ya kweli". Kiapo hiki cha kishahidi kwenye dini imekuwa ndio sababu ya matukio mengi ya ukatili na utumiaji wa nguvu usioelezeka dhidi ya wale wenye imani tofauti na hii. Matukio haya ni kama vile vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades). Upelelezi na hata Maangamizi ya moto ya Nazi (Nazi Holocaust). Kutovumiliana ni kitu chenye kutisha sana na hasa kunapotokana na ushabiki.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia waislamu kuwa:

"Shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarakiane". (3:103)

Ni lazima:

"Subirini na muwashinde makafiri, na kuweni imara (nyoyo zenu) na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu". (Quran 3:200)

Kwa sababu:

"Yeyote anayejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu, na akafanya mambo mazuri, kwa hakika ameshika kishiko imara kisichokuwa na kukatika: na mwisho wa yote ni kwa Mwenyezi Mungu". (Quran 31:22)