rudi maktaba >Akida >

Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Hiyo ndiyo Jannat tutayowarithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu

Vile vile twaambiwa katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Hujurat ,49, Ayah 13 :

Enyi watu ! Hakika Sisitumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa na mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Allah swt ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi….

3. Ihsani na matendo mema

Yaani kuwafanyia watu mambo mema na matendo yetu yawe mema kwa ujumla na kwa hakika haya ndiyo mambo mema na bora kabisa na ndiyo sababu za kuingia Jannat. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maidah,5, Ayah 85 :

Basi Allah swt atawalipa, kwa yale waliyoyasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema.

4. Jihadi na kuwa shahidi

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9, Ayah 111

Hakika Allah swt amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Jannat. Wanapigana katika Njia ya Allah swt – wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'an. Na nani atimizae ahadi kuliko Allah swt ? Basi furahini kwa biashara yenu mliy fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

5. Kutokufuata nafsi yake

Yaani mtu hafuati matamanio ya nafsi yake na badala yake anaikhilafu. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Naziat, 79, Ayah 40 – 41 :

Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt Mlezi, na akijizuilia nafsi yake na matamanio,

Basi huyo, Jannat itakuwa ndiyo makaazi yake !

6. Kushindania katika kuleta Imani

Allah swt atuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al- Waqia, 56, Ayah 10 – 13 :

Na wa mbele watakuwa mbele.

Hao ndio watakao karibishwa

Katika Bustani zenye neema.

7. Hijrah na Jihad

Tumeshaona kuwa Jihadi imeshatajwa hapo mwanzoni ( Jihadi na kuwa Shahidi, nam. 4 ) hapa Jihadi imekuja lakini pamoja na Hijrah. Yaani Hijra ni Jihadi mojawapo kwa ajili ya Mumin. Tumeona kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliiacha Makkah na kwenda Madina, hii ilikuwa ndiyo Jihadi mojawapo ambayo ndiyo kwa ajili ya Allah swt na Dini.

Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9, Ayah 20-22 :

Wale walioamini na wakahama, na wakapigana Jihadi katika njia ya Allah swt kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Allah swt . Na hao ndio wenye kufuz.

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu.

Watadumu humo milele. Hakika kwa Allah swt yapo malipo makubwa.

8. Subira na Ustahimilivu wakati wa shida

Kufanya Subira na Ustahimilivu wakati mtu anapopatwa na shida na matatizo mbalimbali ama yakupoteza mali, kufiwa, kuugua n.k Katika vitabu tunapata habari kuwa Mitume a.s na Maimamu a.s. pia wamepitia shida kali kali ambazo wao wamezifanyia subira na ustahimilivu kwa ajili ya furaha ya Allah swt . Qur’ani Tukufu , Sura al-Dahar, 76, Ayah 12 :

Na atawajaza Bustani za Jannat na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ra’d, 13, Ayah 24 :

Hao ndio watu wa Jannat, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.(Wakiwaambia) Assalamu ‘Alaikum ! amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.

9. Kuwa imara katika Dini

Inambidi mtu awe madhubuti katika Dini kama ukuta wa Shaba yaani awe na uwezo wa kukabiliana na kila sura itakayojitokeza mbele yake kiasi kwamba kamwe hataweza kulega lega katika dini na kamwe hataweza kurudi nyuma katika msimamo wake wa Dini. Allah swt anasema katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ahqaf, 46, Ayah 13 – 14 :

Hakika waliosema:Mola wetu Mlezi ni Allah swt ; kisha wakatengenea, hawatajuwa na khofu, wala hawatahuzunika.

10. Kumtii Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Inatubidi sisi kumtii Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ili kuwa mustahiki wa Jannat . Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 13 :

…. Na anayemtii Allah swt na Mtume wake, Yeye atamtia katika Jannat zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

11. Ikhlas (Uhalisi )

Iwapo kama hakutakuwapo na uhalisi katika kila jambo basi hakutakuwa na usahihi wa kitu au jambo hilo. Uhalisi lazima uwepo katika Imani, matendo na akili na fahamu zetu na kwa hakika huu ndio ufunguo wa kuingia Jannat na ndivyo maana Allah swt ameweka sharti hili la kumwezesha mtu kuingia Jannat na Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Safaat, 37, Ayah 39 – 43 :

Wala hamlipwi ila hayo hayo mliyokuwa mkiyafanya.

Isipokuwa waja wa Allah swt walio khitariwa.

Haom ndio watakaopata riziki maalumu,

Matunda, nao watahishimiwa.

12. Ukweli

Kwa hakika sharti hili ni la umuhimu wa aina yake kwani kila jambo tulifanyalo linahitaji ukweli na kama hakuna ukweli basi kila kitu kitaharibikiwa. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maidah,5, Ayah 119 :

Allah swt atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Allah swt amewawia radhi, nao awe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa.

13. Kujitakasisha mwenyewe

Inambidi kila mtu atulie na kujitakasisha nafsi yake mwenyewe kwa kila jambo na hivyo alete mapinduzi ndani mwake. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ta-Ha, 20, Ayah 75– 76 :

Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu.

Bustani za milele zipitazo mito kati yake,wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.

14. Kutoa katika njia ya Allah swt na kuomba Tawba

Allah swt anatutaka sisi tule na tuwalishe wengine pia tuwe wakarimu na kamwe tusiwe mabakhili na tuombe Tawba kwa ajili ya madhambi yetu. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ali Imran, 3, Ayah 133-136 :

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Jannat ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyowekwa tayari kwa wachamungu,

Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allah swt huwapenda wafanyao wema;

Na ambao pindiwafanyapo uchafu au wakjidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah swt na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao – na nai anayefuta dhambi isipokuwa Allah swt ? – na wla hawapendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.

Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mto kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.

15. Hofu ya Allah swt

Kuna msemo kwamba Mwogopeni yule mtu ambaye hamwogopi Allah swt ! Na wala musimwogope yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt ! Kwa sababu yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt kamwe hatakudhuru nyuma yako na atakuwa akijua kuwa Allah swt hatafurahishwa na hatua yoyote ile ya kukuletea madhara. Ndiyo maana tunaambiwa kuwa tusiwaogope Waumini, tuongee nao waziwazi bila ya kuwa na hofu ya aina yoyote, lakini bila ya kuwatuhumu. Lakini yule asiye na hofu ya Allah swt atatafuta kila hila na mbinu za kukudhuru wewe kwa sababu hana hofu ya Allah swt. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Rahman, 55, Ayah 46 :

Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt atapata Jannat (Bustani) mbili

Vile vile nitapenda kuwaleteeni Hadith ya Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. amesema katika Majma’ul Bayan :

“Mtu yeyote ambaye anajua na kutambua wazi kuwa mimi nifanyapo jema au baya, basi Allah swt yupo anashuhudia matendo yangu haya, basi mtu kama huyu daima atakachokuwa akikifanya basi atakuwa mwangalifu mno katika matendo yake na atajiambia kuwa lau nitafanya kazi hii njema basi Allah swt atalipa mema kadha na kadha na lau nitafanya maasi na madhambi, basi Allah swt ataniandikia adhabu kadha wa kadha. Kwa hivyo watu kama hawa wamewekewa Bustani mbili katika Jannat.”

16. Tawalla na Tabarra

Ama kuhusu mtu atakaye fuata masuala haya mawili basi Allah swt atamjaalia Jannat na uthibitisho wake ni kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu , Sura al-Mujadilah, 58, Ayah 21 :

Allah swt ameandika : Hapana shaka Mimi na Mtume wang tutashinda. Hakika Allah swt ni Mwenye nguvu, mwenye kushinda.

Tawalla maana yake ni kuwa rafiki wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahl al-Bayt a.s. na Tabarra inamaana ya kujiepusha na kujiweka mbali na kutokuwa na uhusiano wowote pamoja na wale maadui wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja Ahl al-Bayt a.s.

17. Kudumisha Sala

Katika maana yake ni kwamba inambidi kila Mwislamu awe akisali sala zote zilizofaradhishwa juu yake kwa kuzingatia umuhimu na nyakati zake. Zipo Sala nyingi ambazo tumefaradhishiwa katika Islam kwa mfano Sala tano za siku, Sala za matukio kama mitetemeko, kupatwa kwa jua au mwezi, n.k. (rejea vitabu vya fiq-hi). Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Ma’arij, 70, Ayah 22 -34 :

Isipokuwa wanaosali,

Ambao wanadumisha Sala zao,

Na ambaokatika mali yao iko haki maalumu

Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba;

Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,

Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.

Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo

Na ambao anahifadhi tupu zao.

Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi –

Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka.

Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,

Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,

Na ambao wanazihifadhi sala zao.

Hao ndio watakao hishimiwa Jannat.

2.JAHANNAM

( Motoni )

Maelezo juu ya Jahannam ( Motoni )

Waislamu wanatimiza nguzo ya Sumu kwa sababu waweze kuepukana na adhabu za Jahannam . Je Jahannam ni mahala pa namna gani na humo kuna adhabu za aina gani ?

Kumeandikwa vitabu vingi vikizungumzia swala hili. Qur’an Tukufu inayomaelezo ya kutosha yanayozungumzia mateso na adhabu za kiakili na kimwili kwa ajili ya wale watakaoingizwa humo kwa kutokana kwao kutoishi vile alivyotaka Allah swt, kwa sababu wao hawakutimiza ahadi yao pamoja na Allah swt alivyokuwa amewapa, ambao hawakutimiza makusudi ya kuumbwa kao yaani kumwabudu Allah swt na si mwingine.

Adhabu kama hizo zinaweza kuangaliwa na kurejewa katika Surah zifuatazo :

al-Baqarah,Aali-’Imran, alMaaida, al-An" am, al-A’raf, al-Anfal, Younus, Hud, al-Ra’d, al-Hijr, al-NahI, Maryam, Taha, al-Hajj, al-Muminoon, al-Noor, al-Furqan, al‘Ankabut, Luqman, al-Sajdah, al-Ahzab, Saba, al-Zumar, Ohafir, al-Tur, al-Hashr, al-Ma’arij, al-furuj, al-Fajr, al-Nisaa..., Katika Surah nyingi, kwa hakika Qur’an imeteremka kuwaonya wanaadamu dhidi ya moto wa Jahannam na kuwaelekeza katika furaha ya kudumu milele : Ufalme usiokwisha kamwe.

Je Jahannam ina umbo gani la kuonekana ? Tupitie Ayah ya Qur’an Tukufu Surah ya Al-Balad, 90, Ayah ya 19-20 zisemazo :

Lakini waliokanusha Aya Zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao.

“Kufungiwa inamaanisha kufunikwa; Jahannam inaweza kulinganishwa kama mtungi, wenye kifuniko, juu ya jiko, kwamba chungu kinachomwa ndani na nje. Maana itakuwa wazi zaidi tusamapo Ayah zifuatazo za Qur’ani Tukufu Surah al-Humazah, 104, Ayah 5 – 9 :

Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika (Moto unaoitwa) Hutama. Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini ( Huo Moto unaoitwa ) Hutama ? Ni Moto wa Allah swt uliowashwa (kwa ukali barabara ). Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) watafungiwa (wewemo ndani yake ). Kwa magogo marefu marefu

“Kufunikwa juu yao” inamaanisha sawa na vile ilivyo katika Ayah ya 90 : 20 hapo juu. Na mistari yake inaweza kumaanisha kwenda undani zaidi, na mistari hiyo ‘inaongezeka,’ kiurefu, na kwa hakika Allah swt ndiye ajuaye zaidi.

Je miale ya moto wa Jahannam iko yenye ukubwa kiasi gani ? Jibu lake tunapewa na Muumba wetu na Jahannam Qur’ani Tukufu Surah al-Mursalat, 77: Ayah ya 32: "Hakika (Moto huo) hutoa macheche yaliyo kama majumba."

Milango ya Jahannam

Katika mlango wa kwanza wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Yeyote yule atakayekuwa na matumaini katika Allah swt basi daima atakuwa mtu mwenye furaha na mafanikio; Yeyote anayekuwa na khofu ya Allah swt basi anajaaliwa usalama; mtu mwovu na aliyepotoka na mstahiki wa adhabu za Allah swt ni yule ambaye hana matumaini yoyote kwa Allah swt na wala hana khofu ya aina yoyote ile ya Allah swt.

Katika mlango wa pili wa Jahannam kumeandikwa yafuatayo: Yeyote yule asiyetaka kufanywa uchi Siku ya Qiyama, basi awavalishe nguo wale walio uchi humu duniani, Yeyote yule asiyetaka kupatwa na kiu Siku ya Qiyamah, basi awanywishe wale wenye kiu humu duniani, Yeyote yule asiyetaka kupatwa na njaa Siku ya Qiyamah, basi awalishe wale wenye njaa humu duniani.

Katika mlango wa tatu wa Jahannam kumeandikwa : Allah swt huwalaani wale wasemao uongo, Allah swt huwalaani wale walio mabakhili, Allah swt huwalaani wale wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wanyong.

Katika mlango wa nne wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Allah swt humdhalilisha yule ambaye anaidharau Dini ya Islam, Allah swt humdhalilisha yule anayewakashifu Ahl al-Bayt a.s. ya wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ; Allah swt humdhalilisha yule ambaye anawasaidia wadhalimu katika kuwadhulumu watu.

Katika mlango wa tano wa Jahannam kumeandikwa sentenso : Msiendekeze matamanio yenu, kwani matamanio yanapingana na tendo la kusadikisha;Musiyaongelee zaidi yale yasiyowahusu kwani mtaondoka katika Baraka za Allah swt; na kamwe msiwe wasaidizi wa madhalimu.

Katika mlango wa sita wa Jahannam kumeandikwa sentenso: Mimi nimeharamishiwa kukubalia Mujtahid (hawa ni wale ambao wamefikia upeo wa Ijtihad, uwezo wa kutoa fatwa. Rejea vitabu vya Fiqh ndipo utakapoweza kupata ilimu zaidi katika somo hili). Mimi nimeharamishiwa kukubalia wale wanaofunga saumu.

Katika mlango wa saba wa Jahannam kumeandikwa sentenso tatu: Ujihisabie mwenyewe matendo yako kabla hujafanyiwa hisabu ya matendo yako; ikaripie nafsi yako kabla wewe hujakaripiwa; na mwabudu, Allah swt aliye Mkuu na aliyetukuka, kabla ya wewe hujafika mbele yake na ambapo hautaweza tena kumwabudu na kumtukuza.

Kwa kuwa marejeo kuhusu Jahannam yapo yanapatikana kwa wingi kutoka Qur’ani Tukufu, sisi sasa tutajaribu kurejea mapokezi na maelezo kuhusu Jahannam kutokea Ahadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. kuhusu adhabu,vitisho vya Jahannam , mahala palipojaa joto la hali ya juu yenye kuumiza, mahala ambapo moto wake unawekewa vipande vya kiberiti au mrututu ambayo kila moja ni kubwa kama milima mikubwa kabisa ulimwenguni. Zipo sehemu kubwa kabisa kama hizo ambapo wale waliokwisha adhibiwa hupelekwa kupoozwa na kugandishwa kama barafu. Kwa maneno mengine, wanatolewa kutoka hali moja ya mto mkali kabisa na kupelekwa katika hali nyingine ya bariki kabisa. Katika sayari yetu kuna milima yenye theluji na milima yenye kutoa volkeno ambayo hutoa miyeyuko ya mawe kama lava; na hivyo ndivyo ilivyo hali ya Jahannam : kuna hali zote mbili za joto kali na baridi kali.

Katika uk.309 ya kitabu cha al-Selek, The Divine Traditions, mkusanyiko wa Ahadith al-Qudsi, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amenakiliwa akisema kuwa siku moja Jahannam ilimlalamikia Allah swt kwa kusema, : “Ewe Mola! Hata sehemu zangu zinateketezana!” na kwa hayo Allah swt aliiruhusu kupumua mara mbili, mara moja katika majira ya baridi na mara nyingine katika majira ya joto kali. Kwa sababu ya kupumua kwake huku ndiko kumetokezea misimu hii miwili yenye joto kali na baridi kali. Iwapo Allah swt angalikuwa ameruhusu zaidi ya mara mbili basi kusingalikuwapo na maisha ulimwenguni humu.

Chakula cha watu wa Jahannam na Jannat

Wakati wakazi wa Jannat watakuwa wakila kila aina ya matunda mazuri na yenye ladha tamu, wakazi wa Jahannam watakuwa wakila chakula kama miiba ambayo itakuwa ikiwasakhama katika koo zao, kamwe haitawafikia tumboni mwao, na wala hawataweza kutapika. Na hii ndiyo chakula mojawapo ya watu wa Jahannam . Aina nyingine ya chakula kinachotayarishwa kwa ajili ya wakazi wa Jahannam ni usaha wa majeraha ya wale wanaopata mateso katika Jahannam , na kuchemshwa katika joto la kupasua matumbo yao.

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amenakiliwa katika uk.145, J.1 ya al-Zamakhshari’s Rabee’ al-Abrar akiwa amemwuliza Malaika Jibrail a.s., “Je ni kwa nini mimi kamwe sijamwona Malaika Mikaili a.s. akicheka au kutabasamu?” Malaika Jibraili a.s. alimjibu: “Mikaili kamwe hakucheka wala kutabasamu kuanzia pale Jahannam ilipoumbwa. ” Anas, Allah swt airehemu rohoyake, amenakiliwa na al-Zamakhshari akisema kuwa mfano wa kiwango kidogo kabisa cha adhabu ya Jahannam ni kama kwamba mtu anatengenezewa pea ya viatu ambavyo anapovaa bongo inachemka na kutokota. Habari zaidi kuhusu sehemu hii ya kutisha zinapatikana katika al-Zamakhshari, ambazo ni kama zifuatazo :

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, “Katika safari yangu ya usiku wa (‘Israa), mimi nilisikia sauti kubwa mno, hivyo nilimwuliza Malaika Jibrail a.s., ‘Je sauti hii kubwa ni ya nini, Ewe Jibraili ?’ Naye alinijibu, ‘Ni jiwe lililotupwa kutokea juu kuangukia ndani mwa Jahannam , na imekuwa ikianguka kwa muda wa vipindi sabini vya baridi, na sasa ndipo ilipofika chini.”

Abu ‘Asim ‘Ubayd ibn ‘Umayr ibn Qatadah al-Laythi, Hakimu wa Makkah (d. 68 A.H.), amesema, “Jahannam hupumua mara moja kwa sababu yake Malaika na Mitume a.s. yote hutetemeka, kiasi kwamba hata Mtume Ibrahim a.s. hupiga magoti na kusema, “Ewe Mola wangu ! Nakuomba uniokoe!”

Abu Sa’eed al-Khudri amenakiliwa akisema, “iwapo milima itapigwa kwa rungu mara moja inayotumiwa na Malaika wa Jahannam , basi itavunjika vipande vipande na kuwa vumbi.”

Tawoos ibn Keesan al-Khawlani amenakiliwa akisema, “Wakati Jahannam ilipoumbwa, Malaika walishtushwa mno, na wakati nyie wanaadamu mulipoumbwa, basi walitulia.”

Al-Hasan ibn Yasar al-Basir amesema, “Kwa kiapo cha Allah swt! Hakuna hata mja mmoja wa Allah swt anayeweza kustahimili joto la Jahannam ! Tumeambiwa iwapo mtu atasimama Mashariki na Jahannam ikawa upande wa magharibi na ikafunuliwa kidogo tu, basi bongo ya mtu huyo aliye Mashariki itachemka. Iwapo kama kiasi cha ndoo moja ya usaha wa Jahannam ukimwagwa juu ya ardhi hii ya dunia, basi hakuna hata kiumbe kimoja kingalibakia hai.”

Hisham ibn al-Hassan al-Dastoo’i alikuwa hazimi taa wakati wa usiku, na wakati wananyumba yake walipompinga kwa kumwambia, “Sisi hatuwezi kutofautisha baina ya usiku na mchana !” Yeye aliwajibu, “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi ninapozima taa wakati wa usiku, hukumbuka kiza kikali cha kaburini, na hivyo sipati usingizi.”

Adhabu katika Jahannam itakuwa kwa mujibu wa aina za madhambi zilizofanywa wakati wa maisha ya mtu humu duniani. Kwa mfano, Wale ambao walilimbikiza mapesa humu duniani bila ya kutoa Zaka na kodi zinginiezo za kidini, basi hao watachomwa kwenye paji la uso kwa yale waliyoyalimbikiza, pembeni mwao, na migongoni mwao. Kwa maneno mengine, sehemu zote za mwili wao.

Abu Zar al-Ghaffari, Allah swt amwie radhi, alikuwa akisema, “Waambieni wale ambao hupenda kulimbikiza utajiri wao kuwa watachomwa nayo juu ya paji la uso wao, pembeni mwao, na migongoni mwao hadi watakapokuwa wamejaa kwa mioto.”

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, kama vile tuambiwavyo katika uk.243, J.8, ya Bihar al-Anwar, “Hakuna Mja wa Mwenyezi Mungu mwenye utajiri au mali na hataki kulipa Zaka isipokuwa kwamba atachomwa kwa vipande hivyo vya mapesa vitakavyokuwa vimepashwa moto katika moto wa Jahannam na kwamba watatumbukizwa katika adhabu hizo kuanzia juu ya vipaji vyao vya nyuso zao na migongo yao hadi pale Allah swt atakapokuwa amemaliza kupokea mahisabu na adhabu za waja wake Siku ya Qiyamah, muda ambao ni wa maelfu ya miaka kwa mujibu wa mahisabu yetu. Hapo ndipo watakapotumwa ama kuingia Jannat au Jahannam .”

Abu Umamah anamnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akielezea aina na vinywaji watakaopewa wakazi wa Jahannam . Anasema, “Italetwa mbele yake, naye atachukizwa nayo; na itakapoletwa karibu yake, itauchoma uso wake na kifuvu kitadondoka. Iwapo ataweza kunywa hata kidogo kutokamo, basi matumbo yake yatakatika vipandevipande na kutokezea sehemu za nyuma ya kutokezea choo.”

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameripotiwa akisema, “Sala za mtu anayekunywa pombe hazikubali kwa siku arobaini; na iwapo atakufa huku pombe ikawamo tumboni mwake, basi Allah swt atamlazimisha anywe sadiid, maji yatokayo kwenye sehemu za uchi wa malaya ambayo yatakusanywa katika birika huko Jahannam na kupewa watu hawa, na kwayo matumbo na ngozi zao zitachomwa.”

Riwaya hii imeelezwa na Shu’ayb ibn Waqid ambaye anamnakili al-Husain ibn Zayd ambaye anamnakili Imam Ja’fer al-Sadiq a.s. kama ilivyoelezwa katika uk. 244, J. 8, ya Bihar al-Anwar, “Wale wenye madhambi mbali na zinaa au mauaji, watapewa vinywaji vya risasi na shaba iliyoyeyushwa”, kama vile Ibn Mas’ud anavyonakiliwa katika Bihar al-Anwar akisema.

Mujahid anasema kuwa hayo yatakuwa ni usaha na damu za wale walioadhibiwa, ambapo Ibn Jubayr anasema ni ‘maji meusi; kwani Jahannam ni nyeusi, miti yake ni meusi, na nyuso na miili ya wakazi wake pia inakuwa imegeuka kuwa nyeusi.

Hoja hii inachukuliwa na al-Dhahhak. Adhabu za ziada zitakazokuwa zikitolewa Jahannam zitakuwa za nyoka na nge ambao makucha yao yatakuwa, kwa mujibu wa Ibn ‘Abbas na wengineo wanaripoti hivyo, makubwa na marefu kama minazi. Nyoka watakuwa wanene kama tembo, na nge watakuwa wakubwa kama punda weusi. Na mara kwa mara wakazi wa Jahannam watakuwa wakipigwa vipigo kwa makonde yao kama marungu: Iwapo wao watakuwa katika tabaka za juu za Jahannam , basi vipigo hivyo vitawaangusha katika tabaka zinginezo, na kila tabaka litakuwa na joto na mateso makali kuliko tabaka lililotangulia, kwa muda wa miaka sabini. Mara watakapofikia tabaka la chini, miale mikali ya moto itawatupa tena, na vivyo hivyo itakavyokuwa ikiendelea. Hakutakuwa na muda wa kuomba msamaha kwa ajili yao.

Je ni mahala gani palipo pabaya zaidi katika Jahannam ?

Ibn Mas’ud na Ibn ‘Abbas wamenakiliwa katika uk.241 – 242, J.8, ya al-Majlisi Bihar al-Anwar anasema kuwa wanafiki watawekwa katika tabaka la chini kabisa la Jahannam ambapo kuna adhabu kali kuliko zote. Watafungwa katika vyumba kama majiko yaliyojaa mioto mikali.

Kwa sasa turejee Nahjul Balagha na tuangalie vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anavyotupatia picha ya Jahannam , tumwombe Allah swt asitutumbukize humo :

‘Janga kubwa kwa mtu ni kule kutumbukia katika Jahannam ; yeye atajihisi kuwa anachemshwa mzimamzima, na ataona mateso yake yasiyona mwisho, na kiumbe fulani kinakoroma na kupumua, viumbe vyote vilivyo humo hukosa raha na kamwe hawapati fursa ya kupumzika, na kamwe hawatapata kupumzika kutokana na adhabu zake au mauti ya uhakika. Yeye hasinzii hata kidogo wala hakutakuwa na mapumziko katiko mateso yake : Kutakuwa na maumivu yakudumu kiasi ambacho tunamwomba Allah swt atunusuru na kutusaidia .’ ( Hotiba 83 ).

‘Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa kuliko sehemu yoyote ile, mahala ambapo mikono ya wakazi wake yanakuwa yamefungwa shingoni mwaio, na vichwa vyao vimefungwa na miguu yao kwa minyororo na mavazi yao yametengenezwa kwa lami. Mashati yao yametengenezwa kwa moto wakati ambapo adhabu zao za moto usiozimika kamwe hazitakwisha kwamwe mahala ambapo mlango wake utakuwa umejazwa watu, katika moto mkali kabisa kiasi kwamba sauti zao zinasikitisha na kutisha, na miale ya moto ikipaa na kufikia kila sehemu na wala hakuna kujitoa kutoka humo na wala hakuna muda utakaokwisha,na wala haina mwisho wake kwa wale wanaotekeezwa na kuchomwa humo.’ ( Hotuba 109 ).

‘Joto lake ni kali mno, kufikia chini kwake ni mbali mno, sakafu yake ni chuma, vinywaji vyake ni usaha.’ (Hotuba 120 )

‘Siku ya Qiyamah, madhalimu wote wataletwa bila ya kuwapo na mtu yoyote wa kuwasaidia au kuwatetea, na hivyo watatumbukizwa katika moto wa Jahannam na humo atasagwasagwa kama vile machine za kusaga zifanyavyo, hadi hapo atakapojigonga kichwa katika sakafu ya chini kabisa.’ ( Hotuba 164 )

‘Iwapo Malik (msimamizi wa Jahannam) atakuwa mkali, husababisha sehemu yake moja kuminyana na sehemu zingine, anapogombeza, milango yake huruka juu na chini (hutema kama volkano). (Hotuba 183 )

Mazungumzo juu ya Jahannam yanatudhihirishia wazi kuwa umbali, mahala na nafasi ni vitu vya uhakika katika maisha yajayo kama vile yalivyo katika maisha yetu haya. Ushahidi wa kusema kuwa Jahannam itasogezwa au kupelekwa sehemu moja kutokea sehemu nyingine, unapatikana katika Ayah ya 23 ya Surah al-Fajr (Surah namba 89 ) na katika Ayah zinginezo pia :

Basi Siku hiyo italetwa Jahannam. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini ?

Kwa hakika wale watakaokuwa wakiihamisha Jahannam kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa Amri ya Allah swt, hawatakuwa wenfgine isipokuwa ni Malaika ambao sisi hatuwaoni duniani humu lakini punde tutakapo kufa, tutaanza kuwaona, naomba mazungumzo haya juu ya Malaika tuyaachilie hapa kwani yatahitaji kutungiwa kitabu kingine, na kwa sasa hivi somo hili litatuchukua mbali, Insha-Allah, tutaweza kuwatungieni kitabu kingine juu ya Malaika.

Lazima ikumbukwe kuwa picha yote iliyotolewa kuhusu Jahannam hatujaelezea kuhusu mateso na adhabu yanayotokana kuwa pamoja na Mashetani, Pepo mbaya na Majini waliolaaniwa ambao wote hao watakuwa pamoja na wanaadamu waliolaaniwa. Tukiangalia mateso wanayopewa viumbe hivi, makelele yao, sehemu zao zikivutwa na kunyofolewa, na wakichunwa ngozi kutoka miili yao … yanatisha mno kama Jahannam yenyewe. Kumbuka vile Allah swt alivyomwelezea mwanadamu kuwa ameumbwa kwa ubora wote. Wanaadamu watakaotumbukizwa katika Jahannam wataelewa vyema zaidi kuliko wengine, wakati ambapo wale watakaokuwa wameongoka watakuwa wamepona uhakika wa kuteswa.

Wale ambao wamesoma masimulizi ya Saint Joan of Arc (1412 – 1431 ), Mfaransa mashuhuri, mbali na umri wake wa kati, aliwaongoza Wafaransa katika ushindi dhidi ya majeshi ya Waingereza huko Orleans, kumbuka kuwa yeye alikuwa ni Pepo mbaya, na anapendelea kutembea juu ya miti iwakayo moto kutokea ncha moja ya dunia hadi nyingine kuliko kuangalia tu. Sasa hebu fikiria kuwa nao katika Pepo za milele. (Yeye haoni ajabu kutembea juu ya moto, je na wewe unaomsimamo kama huo…?)

Kwa kifupi hivyo ndivyo ilivyo Jahannam na adhabu na mateso yake. Kama tungaliweza kuangalia hata mara moja au kuwaangalia wakazi wake, basi kwa hakika tusingalijali kufunga saumu kila siku ya maisha yetu, na wala si katika mwezi wa Ramadhani tu, Mwezi wa Allah swt, mwezi wa msamaha na baraka, lakini maisha yetu yote.

Sababu zimfanyazo mtu kuingia Jahannam

1. Kufr na Nifaq

Hoja hii ipo ya kwanza katika mfululizo wa sababu za kumfanya mtu aingie Jahannam na sababu zote zifuatazo ndizo matawi ya Kufr na Nifaq na Allah swt amewafanyia makhususi Jahannam watu wenye sifa hizi mbili. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 140 :

Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Allah swt zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano waohao. Hakika Allah swt atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 145 :

Hakika wabnafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahannam , wala hutompata yeyote wa kuwanusuru.

2. Kuwazuia wale wanaotenda kazi katika njia ya Allah swt

Kuna watu wengi ambao wanatabia ya kuzua uzushi na kuwazuia kwa njia mbali mbali wale wanaofanya tabia na kutenda matendo mema kwa mujibu wa Sunnah na tabia ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahl al-Bayt a.s. kwa hivyo watu kama hawa ndio waliowekwa katika sababu ya kwanza ya kuingizwa Jahannam . Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 55 :

Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.

3. Kutomtii Allah swt

Leo kila mzazi anataka watoto wake wamfuate na kumtii vile atakavyo yeye mwenyewe akiwa kama mzazi na vile vile kila atengenezacho mtu hutegemea kuwa kitu hicho kitamfaa na kumfanyia kazi kwa makusudio ya kukitengeneza na ndivyo vivyo hivyo Allah swt ametuumba sisi pamoja viumbe vingine vyenye uhai na visivyo na uhai kwa sababu na makusudio maalumu, nayo ni utiifu kwa Amri Zake na kumfuata Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahl al-Bayt a.s.

Hivyo kwa kutomtii Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahl al-Bayt a.s. ni dhambi kuu na ndicho kitakachotutumbukiza Jahannam moja kwa moja. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Jinn, 72 , Ayah 23 :

….. Na wenye kumuasi Allah swt na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannam wadumu humo milele.

Vile vile twaambiwa na Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 115 :

Rudi nyuma Yaliyomo endelea