HADITH ZA MTUME s.a.w.w. NA MA-IMAMU a.s.

 

 

  

 

 

Zimekusanywa na kutarjumiwa na

AMIRALY M.H.DATOO

BUKOBA - TANZANIA

 

700.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt.”

 

701.  Imenakiliwa riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Itakapo tokea miongoni mwenu mtu akazingirwa kabisa kwa hali mbaya, basi inambidi awajulishe jamaa na ndugu zake na asiiweke nafsi yake katika shida.”

 

702.  Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. amesema katika Nahaj –ul – Balagha kuwa:

“Mtu yeyote atakayemwambia mahitaji yake dharura zake kwa muumin basi ajue kuwa ameweka habari zake hizo kwa Allah swt, na yeyote yule atakayeleta dharura na mahitajio yake kwa kafiri basi ajue kuwa amekwenda kinyume na maamrisho ya Allah swt.”

 

703.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Katika hali tatu tu ndipo kunapo ruhusiwa kuomba ama sivyo hairuhusiwi.

·         Kwanza katika kujinusuru mtu mwenyewe,

·         kujinusuru na hasara kubwa kabisa ya mali na

·         tatu iwapo kwa kutokuomba kutakuja kumpatia udhalilisho wa hali ya juu sana. Yaani mtu katika vitu hivyo vitatu kujiokoa na hali hizo tatu mtu anaweza kuomba msaada kwa wengine.”

 

704.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Mtu mmoja alimwijia Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. na kuomba chochote: Kwa hayo Imam a.s. akamwambia haistahiki kuomba isipokuwepo hizo sura tatu.

·               Kwanza ama kuzuia umwagikaji wa damu,

·               ama mtu akiwa na shida ya hali ya juu kabisa au

·               kujizuia kuja kudhalilika vibaya sana.

 

Sasa hebu wewe niambie wewe upo katika sura ipi kati ya hizi tatu? 

 

Yeye akasema ‘Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Katika sura tatu ulizozitaja ipo mojawapo. Basi bila kusita kwa haraka sana Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akamtolea dinar elfu hamsini na kumpa, na  Al Imam Hussein ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akampa dinar elfu arobaini na tisa  na ‘Abdulah bin Ja’afar akampa dinar elfu arobaini na nane.”

 

705.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Heshima ya muumin ni kule kuamka kwa ajili ya sala za usiku, na vile vile heshima yake ni kule kutokuwa mwombaji wa watu.”

 

706.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa amesema:

“Wewe lazima uwe na moyo wa kuishi vyema na watu na kuwaheshimu na kutosheka nao. Na kuishi nao vyema ni kule kuongea nao kwa upole na utamu na uwe na uso wenye tabasamu na uishi nao vile kwamba kila wakuonapo uwe ukionyesha furaha usoni mwako na hivyo utakuwa umejiwekea heshima katika jamii.”

 

706.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Iwapo kutatokezea miongoni mwenu anayemtegemea Allah swt azikubalie kila dua zake anazoziomba basi awe akiishi na watu wote kwa wema na kamwe asimtegemee mtu yeyote isipokuwa Allah swt peke yake na atakapo jiona kuwa yeye kwa hakika anao moyo kama huo basi atambue wazi kuwa chochote kile atakachomwomba Allah swt atampatia na kumjaalia.”

 

707.  Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema kuwa:

“Iwapo mtu atataka wema wote kwa ajili yake ni kwamba yeye ajiepushe mbali na tamaa za kila aina ya kutamani yale waliyonayo watu, na kama yeye ana matamanio yoyote au maombi yoyote basi asiwategemee hawa watu bali zote azielekeze kwa moyo mkunjufu na halisi kwa Allah swt na lazima Allah swt atazikubalia dua na maombi yake na atamtimizia.”

 

708.  Abul A’ala bin A’ayan anasema kuwa mimi nimemusikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

“Enyi watu nyie mtajidhuru pale mtakapo peleka maombi yenu na mahitaji yenu kwa watu, na kwa hakika inafukuzia mbali heshima na adabu. Mkae na watu katika hali ya kuridhika na kuwa na uhusiano nao mzuri na kwa hakika hiyo ndiyo kwa ajili ya usalama. Kwa hakika tamaa yenu ndiyo dalili ya ufakiri wenu.”

 

709.  Ahmad bin Muhammad bin Abi Nassr anasema kuwa yeye siku moja alimwambia Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Ninaomba uniandikie barua moja kwa Ismail bin Daud, ili kwamba niweze kupata chochote kutoka kwake. Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. akamwambia iwapo mimi kitu unachokitaka au cha kukutosheleza wewe ningekuwa nimekukataa, ndipo ningekuandikia, ama sivyo uchukue kile nilicho nacho mimi kwangu na ukitegemee hicho.”

 

710.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kwa hakika yale waliyonayo watu katika uwezo wao na kuridhika nayo ndimo humo kuna heshima ya muumin ya imani yake, je nyie hamjaisikia kauli ya Hatim?  Hatim alisema kuwa pale mtakapoona nafsi zenu zimevutiwa kwa mali za watu wengine basi muelewe kuwa shida na taabu ziko zinawakaribia, na kwa hakika tamaa ni ufakiri ulio dhahiri.”

 

711. Abdullah Bin Sinan anasema kuwa yeye amemsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

“Kwa ajili ya muumin mapendezi ya dunia na akhera yako katika mambo matatu.

Kwanza ni sala katika sehemu ya mwisho wa usiku,

kutokuvutiwa na kutokuwa na husuda na mali na miliki wanayomiliki watu wengine na

 kuwa mwaminifu na mtiifu kwa ukamilifu wa Ahlul Bayt a.s. na mapenzi yao.”

 

712.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Alikuwapo mtu mmoja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na akamwuliza, ‘Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! naomba unionyeshe unieleze jambo moja nilifanye jambo ambalo Allah swt atakuwa radhi pamoja nami. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimujibu:

Udumishe amani na upendo katika utamaduni wa dunia, jambo ambalo kimatokeo utapata mapenzi ya Allah swt na usiwe na kijicho na wivu wala tamaa kwa mali na miliki za watu jambo ambalo litahifadhi heshima yako machoni na mioyoni mwao.”

 

713. Ja’bir bin Yazid ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa amesema:

“Usiwe na wivu choyo wala tamaa kwa mali za watu kwa hakika ni jambo jema kabisa kwa kuitakasisha nafsi yako kuliko hata kutoa mhanga wa mali. Vile vile wakati wa shida na dhiki fanya subira. Kuhifadhi heshima yako na utakatifu wako, mambo haya ni afadhali hata kuliko kugawa mali kwa watu. Kwa hakika kuwa na imani kamili juu ya Allah swt na kutotaka kutovutiwa kutokuwa na wivu au kijicho au tamaa kwa mali waliyonayo watu wengine ndio hayo mambo yaliyo bora kabisa katika maisha ya mwanadamu.”

 

714. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Allah swt amechukia hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema na kuvisema.”

 

715.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Baada ya kutenda mema mtu atakapovizungumzia hayo basi atayateketeza mema yake yote.”

 

716. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad

      Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Allah swt hakupendezewa na mambo sita na mimi vile vile katika kizazi changu Maimam wote sikupenda kutokezee sifa hizo, na vile vile Maimam pia nimewahusia kuwa wasizipende sifa hizo ziwepo katika muumin. Hivyo kila muumin anabidi ajiepushe na sifa hizo. Katika sifa hizo sita mojawapo ni ile baada ya kumfanyia mtu wema mtu anaanza kuyazungumzia huku na pale.”

 

717. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Allah swt hapendi sifa sita na hizo sifa sita mimi sikupendezewa kwa ajili ya mawasii watakao nifuata na waumini wote watakaonifuatia.

Kwanza kusali isivyo kwa makini,

 pili katika hali ya saumu kujamiiana na mwanamke,

tatu baada ya kutoa sadaka kutangaza na kuonyesha.

Nne kuingia msikitini katika hali ya Janaba,

kuwa na shauku ya kutaka kujua mambo ya watu majumbani mwao kunatendeka na kunaendelea nini, na

sita kucheka makaburini mtu anapokuwa baina ya makaburi mawili.”

 

718. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mamlaka yake amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Mtu yeyote atakaye msaidia muumin ndugu yake na baadaye akaja akamwambia kuhusu wema huo akausema basi Allah swt hulirudisha tendo hilo halikubalii. Basi mtoaji atabakia na uzito juu yake na kwa lile jema alilolitenda hana malipo yoyote kutoka kwa Allah swt.”

 

Na Imam a.s. aliendelea kusema: “Kwa sababu Allah swt anasema kuwa yeye ameiharamisha Jannat kwa ajili ya yule anayesema baada ya kutenda tendo jema na bahili na mchonganishi.

 

Muelewa wazi kuwa yule mtoa sadaka, hata anayetoa kiasi cha Dirham moja, basi Allah swt humlipa zaidi ya ukubwa wa mlima wa Uhud kwa neema za Jannat na yeyote yule atakaye saidia kufikisha hiyo sadaka kwa yule ambaye anahitaji basi Allah swt atamlipa mema hayo hayo, na kamwe hakutakuwa na punguzo lolote katika neema za Allah swt kwa ajili ya wote hao.”

 

719. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba yake alisema:

“Yeyote yule atakaye tenda wema na kuwawia wema ndugu wenzake, na akaanza kutanganza mema aliyoyafanya basi matendo ya watu kama hawa yatatupiliwa mbali na hayatakuwa na maana yeyote.

 

Allah swt amewaharamishia Jannat watu wafuatao:

·         Kwanza ni wale wanao tangaza mema waliyowafanyia watu wenzao, na

·         Wale wanaowapotosha watu wengine,

·         wafitini,

·         wanywaji wa pombe,

·         wale wanao tafuta makosa ya watu na aibu za watu,

·         wale wenye tabia mbaya,

·         wale walio makatili kwa wenzao na vile vile

·         wale watu wanao watuhumu watu wengine kwa tuhuma za kuwazushia maovu.”

 

720. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa mababu zake kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Allah swt amewazuieni nyinyi kwa matendo maovu takriban ishirini na manne na mojawapo ni jambo lile ambalo baada ya kutoa sadaka mtoaji anamwambia maneno aliyempatia.”

 

721. Bwana Abu Zahar Al Ghafar amenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Kuna aina tatu ya watu ambao Allah swt kamwe hatazungumza nao siku ya Qiyama.

Kwanza ni yule mtu ambaye hatoi kitu chochote bila ya kumsema au kumwambia yule anayempa, na

pili ni yule ambaye hachukui jukumu wala haoni umuhimu wa kuficha zehemu zake za siri na wa

tatu ni yule ambaye anauza mali yake na kutaka faida kupindukia kiasi.”

 

722. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mtu yeyote baada ya kumsaidia muumin atamuudhi kwa kumwambia au kwa kumsengenya kiasi kwamba roho yake ikaumia basi Allah swt huibatilisha sadaka na wema kama huo.”

 

723.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Aina tatu ya watu kamwe hawataingia Jannat.

Moja ni yule ambaye wazazi wake wamemfanya Aak, wa

pili mnywaji wa pombe (daima anakunywa pombe) na

tatu ni yule baada ya kufanya mema huanza kusema na kutangaza.”

 

724.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. siku moja alimtumia mifuko mitano za Tende za Baqi’ (Jannatul Baqi’, ipo Madina ). Mtu huyo alikuwa muhtaji mwenye shida na daima alikuwa akitegemea msaada kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s., na kamwe alikuwa harefushi mikono yake kwa wengine kwa ajili ya kuomba kwa watu wengineo. Mtu mmoja alipo yaona hayo basi alimwambia Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s.:

 

“Kwa kiapo cha Allah swt, huyu mtu hajakuomba chochote wewe kwa hivyo badala ya kumpa mifuko mitano mfuko mmoja tu ulikuwa ukitosha, na kwa hayo Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. akamwambia:

 

“Allah swt asiongezee idadi ya muumin kama wewe humu duniani!  Wewe mtu wa ajabu sana, mimi ndiye ninayempa lakini ubahili unaufanya wewe!  Kumbuka kuwa mtu mwenye shida na anaye kutegemea wewe hakuombi, Je ni haki kuwa mwenye shida asipoomba basi asisaidiwe mpaka lazima aombe? Basi hapa inaonyesha heshima yake. Uso ule ambao unawekwa juu ya udongo kwa ajili ya ibada ya Allah swt katika hali ya sujuda itakuwa basi mimi nimeubadilisha ule sura badala ya kumwangukia Allah swt utakuwa umeniangukia mimi ! Na jambo ambalo silitaki mimi na wala silifanyi hivyo.”

 

 

725.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako.”

 

726.  Yas’ab bin Hamza anasema kuwa:

“Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim a.s., watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, “Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka.

 

Imam a.s. akamwambia:

“Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam a.s. aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja’afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam a.s. kwa kuniangalia mimi akasema:

“Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?”

 

Suleiman akasema

“Allah swt aiendeleze amri yako”.

 

Hapo Imam a.s. aliinuka na kuelekea katika  chumba chake a baada ya muda si muda akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema, je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?”

 

Hapo mimi nikamjibu:

“Ya Imam a.s.! Mimi niko hapa.”

Na kwa hayo Imam a.s. akamwambia”

“Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka  ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso. Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake.”

 

Seleiman Al-Ja’afar akauliza:

“Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume s.a.w.w.! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?”

 

Kwa hayo Imam a.s. akamjibu

“Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo amesema, kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe.”

 

727.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako.”

 

728.  Yas’ab bin Hamza anasema kuwa:

“Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim a.s., watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, “Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka.

 

Imam a.s. akamwambia:

“Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam a.s. aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja’afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam a.s. kwa kuniangalia mimi akasema:

“Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?”

 

Suleiman akasema

“Allah swt aiendeleze amri yako”.

 

Hapo Imam a.s. aliinuka na kuelekea katika  chumba chake a baada ya muda si muda akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema, je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?”

 

Hapo mimi nikamjibu:

“Ya Imam a.s.! Mimi niko hapa.”

Na kwa hayo Imam a.s. akamwambia”

“Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka  ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso. Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake.”

 

Seleiman Al-Ja’afar akauliza:

“Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume s.a.w.w.! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?”

 

Kwa hayo Imam a.s. akamjibu

“Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo amesema, kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe.”

 

729.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Jambo jema kabisa linalonisaidia mimi katika kufanya wema katika kuwasaidia ni mkono ambao unawafikishia na mkono mwingine unashirikiana naye. Na kwa hakika hao wanaokuja kuomba wanakuja na maombi yao ndipo wanapokuwa karibu nami zaidi. Kwa hakika nimeona kuwa wale wanao sahau waliyoyatenda mema kabla na baada ya kuurudisha mkono wao nyuma huonekana kuwa wao wanaanza kuyasahau mema yote. Kwa hakika moyo wangu kamwe haukuniruhusu kuwafukuza na kuwakatalia waombaji. Na baada ya hapo Imam a.s. alisoma mashairi ifuatayo:

 

Wakati unapokuijia mtihani kwako kwa heshima zako pia inabidi uombe,

Basi uende kwa mtu mmoja aliye mkuu na aliye Sharifu kwa ajili ya kuomba kwake.

Kwa hakika, huyo mtu Sharifu na mkuu atakapokusaidia basi humo ndani hakutakuwa na maonyesho wala masengenyo, na badala yake ndani kutakuwa na unyenyekevu na kuhuzunika pamoja nawe.

 

Kumbuka wakati utakapotaka kupima katika mzani uombaji na utoaji sadaka  na mema basi utaona sahani ya mzani ya uombaji utakuwa daima ni mzito kuliko nyingine yote.”

 

730.  Warram bin Abi Faras ameandika riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Wenye imani dalili zao ni nne,

kwanza nyuso zao huwa zina bashasha,

 ndimi zao zinakuwa zenye ukarimu na mapenzi,

nyoyo zao zinakuwa zimejaa huruma, na

wanakuwa na mkono wenye kutoa mkono unaopendelea kutoa sadaka  na misaada nk.”

 

731. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad

Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Kila kila aina ya wema na huruma ni sadaka.”

 

732.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akizungumzia neno Ma’arufu katika Qur’an Tukufu, Surah Nisaai, 4, Ayah 114:

 

Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa Sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhai ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

 

733.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa ma’arufu kuna maanisha kule mtu kutimiza wajibu wake aliofaradhishiwa.”

 

734.  Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwasaidia waombaji

watatu na wa nne alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema:

“Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka  bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka  au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua:

“Ewe Allah swt naomba unipe riziki.”

Basi hapo atajibiwa, “Je mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki?”

 

735.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Bora ya sadaka  zote ni ile kufanya wakati mtu anapofanya katika hali unapokuwa sawa.”

 

736.  Hisham bin Al Muthanna anasema:

“Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuhusu tafsiri ya ayah Surah An A’Am, 6, Ayah 141:

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala mstumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu,

“Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu.”

 

737.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Baada ya mtu kujitolea kile kiasi alicho na dharura nacho kwa mujibu wa mahitaji yake na baadaye katika kiasi kinachobaki akitoa sadaka basi hiyo sadaka  ni bora kabisa.”

 

738.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Mojawapo katika Nasiha na Mawaidha ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ilikuwa ni kila aina ya wema ni sadaka  mojawapo, na sadaka  iliyo bora kabisa ni pale kutoa wakati mtu ameshajitimizia wajibu wake na ametosheka, na mkumbuke kuwa muwape wale ambao kwao nyie mnawajibika kuwatimizia mahitaji yao.

 

Mkono wa mtoaji ni afadhali kuliko mkono wa mpokeaji. Kwa hakika mtu ambaye anachuma kwa uwezo wake na kutumia kwa ajili yake na kuwatimiza mahitaji yao basi Allah swt kamwe hatamlaumu.”

 

739.  Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na

  kumlalamikia kuhusu njaa:

“Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimtuma mmoja wa wake zake naye alipowaendea wakamwambia kuwa wao walikuwahawana chochote isipokuwa maji ya kunywa tu, na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia, je kuna yeyote yule atakaye mchukua mtu huyu kuwa mgeni wake kwa usiku huo?”

 

Na kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema,

“Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nakubali kumchukua huyu kama mgeni wangu kwa usiku wa leo.” Na walipofika nyumbani kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam a.s. alimwuliza Bi. Fatimah az-Zahra a.s. “Je nyumbani kuna chakula chochote?”

 

Kwa kusikia hayo Bi. Fatimah az-Zahra a.s. akasema, tuna chakula kiasi cha kuwalisha watoto wetu tu lakini na mgeni pia ana haki yake.”

 

Na hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema

“Wewe walaze watoto, na uizime taa.”

 

Asubuhi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipokuja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwelezea kisa kilivyotokea na wakati bado akiwa anaelezea kisa hicho ayah ifuatayo iliteremshwa Surah Al Hashri, 59, ayah ya 9:

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

740.  Muhammad bin Yaqub Kuleiyni amenakili riwaya kutoka Abu

Nasar kuwa yeye amesoma barua ambayo Al Imam 'Ali ibn Abi  Talib a.s. alimwandikia Abu  Ja’afar (Mutawakili, mtawala wa Ki Abbasi). Humo kulikuwa kumeandikwa:

“Ewe Abu Ja’afar ! nimepata habari kuwa wewe unapotoka nje wakati umekaa juu ya usafiri wako basi wafanyakazi wako wanakutoa nje kwa kupitia mlango mdogo, ili kwamba yule ambaye ana shida na mwenye kuuhitaji msaada wako asiweze kufaidika hivyo.

 

Mimi kwa kiapo cha haki yangu ninakusihi kuwa kutoka kwako na kuingia kwako uwe kupitia mlango mkubwa na uwe na wingi wa dhahabu, fedha na mali ili atakapo tokezea mbele yako mwombaji mwenye shida uweze kumsaidia. Wajomba zako wanapokuomba uwape Dinar hamsini na wake zao wanapokuomba uwape Dinar ishirini na tano na usiwape chini ya hapo kama utawapa zaidi basi hilo ni shauri lako.

 

Na hii nakuambia kwa sababu iwapo wewe utafuata hivyo basi Allah swt atakuwia wema, hivyo utumie na usiwe na shaka katika ahadi na neema za Allah swt mmiliki wa malimwengu yote.”

 

741.  Safwan anasema kuwa siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.

  alimwuliza mmoja wa wahudumu wake:

“Je leo mmetoa chochote katika njia ya Allah swt ?”

 

Naye alijibu hapana, leo sijatoa chochote bado.”

 

Kwa hayo Imam a.s. alisema

“Sasa usipotoa hivyo unategemea Allah swt atupe baraka kwa misingi gani? Lazima utoe kwa njia ya Allah swt hata kama itakuwa ni Dirham moja.”z

 

742.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Ayah ya Qur'an

Surah Al-Hajj, 22, Ayah ya 28:

Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.

 

“Allah swt katika ayah hii anamaanisha kuwalisha wale walio na shida na kuwasaidia, ambapo wao kwa heshima zao wenyewe hawajitokezi nje mbele ya watu kuomba.”

 

743.  Isack bin Ammar amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer

as-Sadiq a.s. kuwa:

“Utafika wakati mmoja ambapo waombaji wanaorefusha mikono yao kwa watu watakuwa wakiishi kwa starehe na wale watakao kaa kimya kwa kutunza heshima zao watakuwa wakifa kwa shida zitakazo kuwa zikiwakabili.

 

Kwa hayo mimi nikamwuliza Imam a.s.,

“Ewe Maula ! Je yakitokea hayo katika zama za uhai wangu mimi nifanyeje?”

 

Kwa hayo Imam a.s akamjibu,

“Kwa hakika kile ulichonacho wewe uwasaidie hao watu kwa hali na mali na kwa hata cheo chako ulicho nacho na kwa wadhifa wako ulio nao uwasaidie ipasavyo.”

 

744.  Abu Basir anasema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliitolea

maelezo Ayah ya Qur'an Tukufu Surah Al Baqara, 2, ayah ya 267       isemayo:

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

amesema Kuwa:

“Zama kabla ya Islam watu walikuwa wamejilimbikizia mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali (kwa njia zilizo haramu) na baada ya wao kusilimu, walikuwa wakidhani kuwa kwa kutoa mali iliyo patikana kwa njia haramu, watakuwa wametakasisha mali yao iliyo halali, kwa hivyo Allah swt alitoa amri kuwa sadaka  itolewe kutoka mali iliyo halali tu.”

 

745.  Kwa kuzungumzia ayah hiyo ya juu Shahab amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Ambamo amesema kulikuwa na kaumu moja ambayo walikuwa na mali nyingi iliyo chafu  (iliyopatikana kwa njia za haramu ). Wakati wao walipoukubalia Islam walianza kuchukizwa na malimbikizo yao hayo machafu na wakataka kutoa kwa njia za sadaka. Allah swt aliwaonya kwa kuwaambia kuwa sadaka  hutolewa kutokea mali iliyo halali tu.”

 

746.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo watu watachuma au watajipatia mali kwa mujibu wa hukumu za Allah swt na wakaitumia kinyume na hukumu za Allah swt au iwapo watachuma kwa njia zilizo kinyume na hukumu za Allah swt na wakazitumia kwa mujibu wa hukumu za Allah swt; katika hali zote mbili Allah swt hazikubalii.

 

Katika kutaka kukubaliwa sharti ni kwamba mapato hayo yawe yamepatikana kwa njia zilizo halali na zitumiwe katika njia zilizo halali vile vile.”

 

747.  Halabi anasema kuwa mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer

as-Sadiq a.s. kuhusiana na ayah hii katika Qur'an Tukufu Surah Al Baqarah, 2, ayah ya 267:

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema:

“Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kuingia katika Uislam bado wameendelea kubakia na mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali. Na humo kulikuwa na mmoja ambaye kwa makusudi alianza kutoa sadaka kutoa mali hiyo isiyo halali. Na Allah swt alimzuia kufanya hivyo yaani sadaka  haiwezi kutolewa isipokuwa kutokea mali iliyotokana kwa njia halali.”

 

748.  Katika Ma’anil Akhbar Al Imam Hassan al-'Askari a.s. kwa

kupitia sanad amenakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer

as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Wale ambao wanajiona utukufu na wakubwa na ambao wanatenda matendo kwa mujibu wa nafsi zao, mfano wake ni wa yule mtu ambaye mimi nilisikia watu wakimsifu sana na kumheshimu sana, na hivyo mimi nikawa na shauku ya kutaka kuonana na mtu huyo lakini katika hali ambayo yeye hataweza kunitambua. Siku moja mimi nilimwona alikuwa amezingirwa na watu. Baada ya muda mchache kupita mimi nikamwona yeye ametoka humo na akawa anaondoka, basi mimi nilimfuata nyuma yake.

 

Tulipita katika duka la muuza mikate, huyo mtu kwa kuficha macho yake na kificho ficho akaiba mikate miwili. Kwa hakika mimi nilistaajabishwa mno, na nikadhani kuwa labda wao wana maelewano fulani kabla ya tukio hilo.

 

Tukaendelea mbele yeye akamghafilisha mfanya biashara huyo na akaiba makomamanga mawili humo. Na hapa pia nikafikiria kwa labda wao watakuwa na maelewano kama hayo kabla ya kutokea tukio hili, nikiwa hapo nikaingiwa na wazo kuwa je iwapo watakuwa na maelewano kama hayo basi kwa nini achomoe vitu kimafichoficho?

 

Basi mimi niliendelea kumfuata nyuma yake, tukafika njiani akamwona mtu mmoja mgonjwa basi huyo akasimama kwa mgonjwa huyo na akatoa ile mikate miwili na hayo makomamanga mawili, akampa huyo mgonjwa.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza huyo mtu kulikuwa na dharura gani kwa kufanya hivyo. Mtu huyo kwa kuniona mimi akasema je wewe ni Ja’afar bin Muhammad ? Nami nikamjibu naam, basi yeye hapo akaanza kusema nasikitika sana kwa kutokujitambulisha kwako hapo kuja kukufikishia faida (kwa sababu Imam a.s. alikuwa hakujionyesha kuwa yeye ni Imam bali alikuwa amejiweka kama yeye ni mtu wa kawaida)

 

Imam a.s. akamwambia kwa hakika matendo yako hayo yana aibisha.

 

Basi yeye akasema kuwa Allah swt anasema katika Qur'an Tukufu Surah An A’Am, 6, Ayah 160:

Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa.

 

Ama kwa mujibu wa ayah ya Qur'an Tukufu mimi nimeiba mikate miwili hivyo nimetenda madhambi mawili na nimeiba makomamanga mawili hivyo nimetenda madhambi wawili na kwa ujumla nimetenda madhambi manne.

 

Na pale mimi nilipompa mgonjwa sadaka  mimi kwa kila wema nimepata malipo kumi ya thawabu hivyo jumla nimepata malipo ya thawabu arobaini. Na kutoka arobaini ukitoa nne ninayo mema thelathini na sita bado.”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu:

“Mama yako akae kwenye kilio chako! Wewe kwa hakika umeitoa maana isivyo ya Ayah za Qur'an Tukufu. Je wewe huelewi ayah ya Qur'an Tukufu isemayo Surah Al Ma’ida, 5, Ayah ya 30:

 

Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika.

 

Kwa mujibu wa ayah hiyo wewe umeiba mikate miwili umetenda madhambi mawili na kwa kuiba makomamanga mawili umetenda madhambi mawili mengine na hivyo jumla umetenda madhambi manne, na pale ulipotoa hiyo mali yaani mikate na makomamanga, kama sadaka  bila idhini ya mwenye mali basi umetenda madhambi mengine manne. Kwa hivyo umetenda madhambi nane kwa pamoja. Sasa wewe unafikiria mema hayo arobaini yametoka wapi?”

 

Kwa hakika mtu huyo aliduwaa, akimwangalia Imam a.s. na akajiondokea zake.

 

Baada ya hapo Imam a.s. akasema kwa kujitolea maana potofu ya ayah za Qur'an Tukufu vile isivyo sahihi ndio matokeo yake haya na vile vile kuwapotosha watu wengine pia.”

 

749.  Katika tafsiri Ayyashi Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.

amenakiliwa akitoa tafsiri ya ayah Surah Al Baqara, 2,  ayah ya 267:

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

Imam a.s. akaelezea:

“Miongoni mwa watu kulikuwa kumelimbikwa mali iliyopatikana kwa riba na njia zingine zisizo za halali, basi wao walinuia kutoa sadaka  humo, na ndipo Allah swt alipowakataza kufanya hivyo (kutoa sadaka  kutoka mali iliyopatikana kwa njia za haramu hairuhusiwa).”

 

750.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. ameripoti riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Katika vitu vya kuleta uokovu mojawapo ni kuwalisha chakula wale wenye kuwa na shida na dhiki, na pili mtu awe ni mwanzilishi awe ni mwanzo wa kutoa salamu na vile vile wakati watu wamelala usingizi mtu anaamka kwa ajili ya kusali na kufanya ‘ibada.”

 

751.  Muhammad  Yakub amenakili kutoka ‘Ali bin Ibrahim ambaye

naye amenakili kutoka Muhammad bin ‘Isa bin ‘Ubaid ambaye naye amenakili kutoka Ahmad bin Muhammad naye amenakili kutoka ibn Fazzal Ma’aruf naye kutokea Tha’alaba bin Maymun ambaye naye pia amenakili riwaya hiyo kutoka kwa Zararah, kuwa

 

752.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Allah swt hupendezewa mno kulishwa chakula wale wenye dhiki na shida na njaa, na vile vile hupendezewa kutolewa kwa dhabihu (qurbani).”

 

753.     Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:

“Yeyote yule ambaye hakubahatika kutufanyia sisi wema basi ni wajibu wake kuwafanyia mema na kuwatimizia mahitaji ya marafiki zetu.  Na yeyote yule ambaye hakubahatika kudhuru makaburi yetu basi adhuru makaburi ya wafuasi na marafiki zetu.”

 

754.     Muhammad bin Ali bin Hussein Jamil amenakili riwaya moja kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Miongoni mwenu mtu aliye bora kabisa ni yule mwenye moyo mkarimu yaani mwenye moyo wa kutoa na mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili. Na usafi wa imani dalili yake ni kwamba huwawia kwa wema muumin wenzake na kuwatimizia dharura na mahitajio yao. Bila shaka yeyote yule anayewafanyia hisani ndugu zake katika imani basi ndiye mpenzi wa Allah swt kwa sababu katika kufanya wema huko kuna mambo mengi yanayomzuia mtu asiingie katika mitego ya Sheitani na vile vile asiingie Jahannam, na kwa matokeo yake ndiye mtu anayeingia Jannat.”

 

Baada ya hapo Imam a.s. alimwambia Jamil, “Ewe Jamil! Habari hizi uwafikishie wenzako.

 

Kwa hayo mimi nikasema, “Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Niwe fidia juu yako. Je ni watu gani hao?”

 

Imam a.s. akasema: “Hao ni wale ambao wanawafanyia wema ndugu zao katika imani wakati wa shida huwa pamoja nao na vile vile wakati wa furaha pia huwa nao.”

 

755.     Sheikh Sadduq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye amesema kuwa:

“Yeyote yule ambaye hakupata fursa kufanya wema nasi, basi awafanyie wema wapenzi na wafuasi wetu basi atapata thawabu za kutufanyia wema sisi. Na vile vile ambaye hakubahatika kutuzuru sisi katika uhai wetu na uhai wake basi awazuru wapenzi na wafuasi wetu, basi atapata thawabu kama za kutuzuru sisi.”

 

756.     Safwan Al-Jammal anasema kuwa siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia Mu’alla bin Hunais:

“Ewe Mu’alla! Uwe wa Allah swt, ili Allah swt aweze kukutunza na kukuhifadhi.

 

Kwa hayo Mu’alla alianza kusema:

“Je hivyo inawezekanaje?”

 

Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu, uwe na hofu ya Allah swt, uwe daima ukimwona yeye katika mawazo yako, kwa hiyo yeye atakifanaya kila kitu kiwe kikikuogopa wewe, na vile vile kitakuwa kikikuwazia wewe na kukujali wewe. Ewe Mu’alla ili kujipatia mapenzi ya Allah swt lazima uwatendee watu matendo mema, na utambue wazi wazi kuwa Allah swt anapendezewa sana na moyo wa ukarimu na huchukizwa sana na ubahili na huwa na uadui nao.

 

Angalia !  Wewe kama utaniomba chochote na mwisho wake wewe ukaaza kufanya mapenzi nami, na badala yake mimi nitafurahishwa sana iwapo wewe hautaniomba chochote na hautapata chochote kutoka kwangu na baada ya hayo wewe bado ukawa na mapenzi nami.

 

Na kwa hakika ukiniuliza mema yote naweza kuyafanya kwa ajili yako basi ukweli ni kwamba sifa zote ni za Allah swt kwa sababu yeye amekupitishia neema yake kwa mikono yangu mimi nimekuwa ni kipitishio tu kwa ajili yako kwa hiyo yeye ndiye anayestahiki sifa zote.”

 

Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia, “Nyamaza!”

Wale mafukara ambao wanawajali ndugu na jamaa zao na kuwawia wema wenzao, Allah swt huwapa ujira mzuri sana, kwa sababu Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Surah Sabaa, 34,

ayah 37:

Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.

 

757.     Sheikh Quleyni amenakili riwaya kutoka kwa Ahmad bin ‘Isa kuwa Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

 

758.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa kwa neno ‘Innama’ inamaanisha kuwa katika kazi zenu au shughuli zenu zote, mwenye kuwa na haki zaidi kuliko yeyote juu ya nafsi zenu na mali zenu ni Allah swt, baada yake ni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na baada yake ni, Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na hadi kufikia Qiyama Maimamu a.s. kutokea kizazi chake.

 

Vile vile Allah swt ameelezea fadhila zao kwa kusema

Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

 

Kisa katika ayah hii ni kwamba Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akisali sala ya Dhuhuri, alipomalizia raka’a ya pili tu akatokezea mwombaji. Siku hiyo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa amevaa  Khullah yenye thamani ya Dirham elfu moja ambayo alikuwa amepewa zawadi na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Na Imam a.s. alipokuwa katika hali ya Ruku’u, kulitokezea maskini mmoja ambaye akasema, “Ewe Walii wa Allah swt na muumin halisi, iwe salamu juu yako, naomba unipe mimi maskini sadaka yoyote. Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliinamisha chini Hulla na kwa ishara akamwambia huyo maskini aichukue.”

 

Kwa tukio hili ndipo Allah swt alipoteremsha ayah hii kwa ajili yake na kwa ajili ya kizazi chake na kuonyesha fadhila na kufuzu kwao. Fadhila zao kuwa wanagawa sadaka  hata kama watakuwa katika hali ya Rukuu.

 

Kwa hakika imekuja kujulikana kuwa yule maskini aliyekuja kuomba alikuwa si mtu bali alikuwa ni Malaika ambaye alikuja kuomba, na vile vile katika kizazi kizima cha Maimam a.s. pia tumeona mara nyingi sana Malaika huwa wanakuja kuomba katika sura ya maskini.

 

759.     Katika kitabu kiitwacho Ihtijaj humo Tabarasi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameelezea kuhusu ayah hiyo kuwa:

 “Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika hali ya sala akiwa katika Ruku’u alitimiza wajibu wake na akatoa Zaka na Allah swt ndipo alipoiteremsha hiyo ayah na makusudio yake yalikuwa ni kupata ridhaa ya Allah swt.”

 

760.     Ali bin Ibrahim katika kitabu chake Tafsir ananakili riwaya kutoka kwa baba yake Ma’arifat Safwan kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokuwa amekaa pamoja na ‘Abdullah bin Salam kulikuwa na kikundi cha Mayahudi pia. Na wakati huo ikateremshwa ayah ya Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

 

Baada ya hapo mara Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akatoka nje haraka na akaelekea msikitini na huko njiani alikutana na mwombaji mmoja na hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:

“Je kuna mtu aliyeweza kukusaidia?”

 

Basi huyo mwombaji akasema,

“Naam, kuna mtu anayesali msikitini humo ndiye aliyenisaidia.”

 

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyoukaribia msikiti akamwona huyo mtu si mwingine bali ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.

 

Na riwaya hii vile vile imenakiliwa na Abu Hamza ambaye ameandika katika Tafsir Ayyashi.

 

761.     Muhammad bin Ali bin Hussein katika kitabu cha Amali amenakili riwaya kutoka Abul Ja’rud Ma’rifat kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amenakiliwa riwaya kuwa amezungumzia kuhusu ayah Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

 

kama ifuatavyo:

“Katika Mayahudi ambaye mnafiki mmoja alipoukubalia Uislam akaanza kuiga:

“Ewe Mtume wa Allah swt! Je ni nani Wasii na Khalifa wako? Na nani huyo atakaye kuwa Walii baada yako?”

 

Ndipo hapo ayah hiyo ilipoteremshwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akawaambia inukeni, basi hao wote wakainuka na wakaanza kuelekea msikitini. Walipofika msikitini wakakutana na maskini mmoja akitoka nje na hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuuliza, “Je kuna mtu yeyote aliyekupa chochote ?” Huyo akasema “Kwa nini isiwe hivyo pete hii je niliyoipata?” Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema,”Je ni nani aliyekupa?”

 

Huyo mwombaji akasema “Huyo mtu ambaye bado anasali.”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema

“Je alipokupa hiyo pete alikuwa katika hali gani?”

 

Huyo mwombaji akasema alikuwa katika hali ya Ruku’u. Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipopaaza sauti ya Takbira yaani Allahu Akbar na wale wote waliokuwepo pamoja naye nao pia walitoa Takbira kwa nguvu na sauti na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndipo alipowaambia wote:

“Mtambue wazi kuwa baada yangu Walii ni huyu Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na wa si mwingine”

 

Karta anasema kuwa

“Kwa mujibu wa riwaya zilizopatikana kuwa katika sala moja aliitoa Hullah, na katika sala ya pili alitoa pete basi inadhihirika kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anatoa sadaka katika hali ya sala zaidi ya mara moja ndivyo inavyothibitika kwa mujibu wa riwaya zinazopatikana.”

 

762.     Ayyashi katika Tafsir yake ananakili riwaya moja kutokea kwa mwana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa Ammar Yasir amesema:

“Siku moja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipokuwa akisali sala ya Sunnah aliahirisha tendo moja kiasi kwamba mpaka akavua pete yake kwa ajili ya kumpa aliyekuja kuomba. Na pale Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokuja basi alimwelezea hivyo. Na wakati huwo iliteremshwaayah yake hadi kufikia :

Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitusomea ayah hiyo na akasema,

 

“Yeyote yule ambaye mimi ni Mawla wake basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni Mawla wake. Ewe Allah swt! Uwe na mapenzi na yule ambaye anawapenda wao, na uwe na uadui na yule ambaye anafanya uadui pamoja nao.”

 

763.     Halabi anasema kuwa yeye alipomwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. basi Imam a.s. akamjibu:

“Naam kabisa! Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. aligawa nusu ya mali yake katika njia ya Allah swt – hadi kwamba nguo kwa nguo, Dinar kwa Dinar, alivigawa vyote katika njia ya Allah swt, na alikwenda Hija ishirini kwa kutembea na miguu.”

 

764.     Mtume Muhammad  s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah,

J. 6, Uk. 13:

“Umma wangu utaendelea kuishi kwa heri pale watapokuwa waaminifu miongoni mwao,

watakapokuwa wakirejesha amana watakazokuwa wakiachiana, na

watakapokuwa wakitoa sadaka kutoka mali zao;

Lakini, Iwapo wao hawatatimiza wajibu hizo, basi watakumbwa na ukame na baa la njaa.”

 

765.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha, uk.512, Msemo 254 :

“Enyi wana wa Adam ! Muwe wawakilishi wenu wenyewe katika mali yenu na mfanye kile chochote kile mnachotaka kufanyiwa nyie baada ya kifo chenu.”

 

Tanbih

 Iwapo mtu atataka baada ya kifo chake sehemu fulani ya mali utajir wake utumike katika kutoa sadaka au misaada, basi asisubiri mpaka afe bali aitumie popote pale atakapo katika uhai wake kwa sababu inawezekana kuwa baada ya kifo chake warithi wake wasiweze kutekeleza kwa mujibu wa vile alivyotaka au usia wake na labda inawezekana asipate wakati wa kuandika usia hivyo akakosa fursa hiyo.”

 

766.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Kanz-ul-

'Ummal, J. 6, Uk. 371:

“Toeni sadaka na muwatibu wagonjwa wenu kwa hayo, kwa sababu sadaka [1] kwa hakika inatoa balaa na magonjwa; na inaongezea umri wenu ukawa mrefu na kuongezeka kwa thawabu zenu.”

 

767.     Imenakiliwa kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

akisema, Al-Ithna-'Asheriyyah, Uk. 85:

“Nilipokuwa nimekwenda mbinguni, mimi niliona mistari mitatu imeandikwa juu ya mlango wa Jannat:

Mstari wa kwanza ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Mimi ni Allah swt na hakuna Allah swt mwingine isipokuwa mimi na Rehema zangu zinazidi adhabu zangu.

Mstari wa pili ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Sadaka inalipwa kwa mara kumi (10) na mkopo unalipwa mara kumi na nane (18), na kuwajali maJama’a na ndugu kunalipwa mara thelathini (30).

Mstari wa tatu ulisomwa yeyote yule anayeelewa wadhifa Wangu na Ukuu wangu basi kamwe asinishutumu mimi katika maswala ya maisha.”

 

768.     Taus-ibn-il-Yamani anasema kuwa yeye alimsikia Al Imam

Zaynul 'Abediin a.s. akisema sifa za muumin ni tano na pale alipoombwa kuzitaja alijibu, Khisal-i-Sadduq, Uk. 127:

“Ucha Allah swt katika hali ya upweke,

 kutoa sadaka wakati unaohitajika,

Subira anapopatwa na matatizo au anapokuwa na shida,

uvumilivu wakati wa ghadhabu,

 ukweli ponapokuwa na hofu.”


KUTOA SADAKA NA UBAHILI:

 

769. Mali ya mchoyo huliwa na warithi wake au hupeperuka bila

        kujulikana.

770. Hakuna mtu mwenye upweke vile alivyo bahili.

771. Mchoyo ni mweka/mtunzi hazina wa warithi wake.

772. Ubahili na uchoyo huangamiza upendo wa urafiki wa kweli.

773. Ubahilifu ni kujipatia ubadhirifu.

774. Kuwa mchoyo kwa kile ulichonacho ni kutomwamini Allah swt.

775. Sifa ya upole na wema huangamizwa kwa ubahili.

776. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo atenganapo nayo.

777. Maovu hufichwa kwa ukarimu.

778. Bora wa watu ni yule afaaye watu

779. Hakutakuwa kuwafadhili watu kwa mifuko mitupu.

780. Fadhila huuliwa kwa matumizi fidhuli.

781. Uachie ngome ya Sadaqa iilinde ufanisi wako.

782. Kutoa baada ya kughairi ni bora zaidi kuliko kughairi baada ya kutoa.

783. Uso ulio mcheshi ni mojawapo ya ne’ema mbili.

784. Usimuudhi mtu yeyote yule pale akutakiapo kila la kheri.

785. Fadhila na ukarimu hupatiwa sifa.

786. Fadhila ya kweli (kwa moyo safi) huondoa dhiki zote

787. Makosa ya mwenye kutoa fadhila ni afadhali kuliko dharau ya mchoyo.

788. Fadhila isiongozwe kwa uoga wala kuwa na matumainio ya kupata chochote (tamaa).

 


 

KUWAJALI NDUGU NA MAJAMA’A.

 

789.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar

al-Anwaar, J. 74, Uk. 89:

“Yeyote yule anayetaka kuongezewa riziki na baraka na siku yake ya mauti icheleweshwa, basi inambidi awajali ndugu na maJama’a zake.”

 

790.     Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., Bihar al-Anwaar, J. 73,

Uk. 138:

“Mali haiwezi kulimbikana kupita kiasi isipokuwa kwa njia tano:

Ubahili kupita kiasi,

matarajio makubwa sana,

 uroho kupita kiasi,

 kuvunja uhusiano pamoja na ndugu na maJama’a za mtu mwenyewe, na

 kuijali na kuipenda dunia hii kuliko Akhera.”

 

791.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Usul-i- Kafi , J. 2, Uk. 150:

“Kuwajali Jama’a na ndugu kunaleta faida tano:

Kutakasika na kukubalika kwa matendo ya mtu

Kuongezeka katika utajiri na mali

Kuondoa balaa na shida mbalimbali

Kurahisisha maswala yake katika Akhera

Umri kuwa mrefu.”

 

792.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Khisal

Uk. 179:

“Kuna makundi matatu ya watu ambao hawataruhusiwa kuingia Jannat:

Wanywaji wa pombe,

Wachawi [2], na

wale wanaokana Jama’a na ndugu zao.


 

KUWAHURUMIA WAZAZI.

 

793.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mustadrak

Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 15, Uk. 176:

“Furaha ya Allah swt ipo katika furaha ya wazazi wa mtu (kama ndio hivyo ni kweli, basi adhabu na ghadhabu zake pia zipo katika ghadhabu za wazazi wa mtu).”

 

794.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar,

 J. 74, Uk. 85:

“Bora ya matendo ni:

Kusali kwa wakati wake,

kuwa mwema na mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa wazazi wake, na

kuchangia katika vita vitakatifu vya Jihad (dhidi ya Mapagani) katika njia ya Allah swt.”

 

795.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Safinat-ul-Bihar,

J. 2, Uk. 553:

“Iwapo mtu anataka Allah swt ampunguzie makali ya mauti, basi lazima awajali Jama’a na ndugu zake, na awawie wema wazazi wake. Na pale mtu anapofanya hivyo, basi Allah swt atampunguzia makali ya mauti na kamwe hatapata umaskini katika maisha yake.”

 

796.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Usul-i- Kafi,

J. 2, Uk. 349:

“Yeyote yule anayewatazama wazazi wake kwa macho ya ghadhabu, hata kama wao hawakuwa waadilifu kwake, basi Allah swt hatazikubalia ibada za mtu huyo (hadi hapo atakapofanya Tawba).”

 

797.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 5, Uk. 554:

“Watendee wazazi wako kwa huruma ili na watoto wako waje wakutendee vivyo hivyo; na uwe mcha Allah swt kwa wake wa watu wengine ili wake zako wabakie wacha Allah swt.”

 

798.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2, Uk. 162:

“Safari moja mtu alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwuliza namna ya kuwashughulikia wazazi. Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu

uwe mwenye huruma kwa mama yako:

uwe mwenye huruma kwa mama yako na

uwe mwenye huruma kwa mama yako;

 Uwe mwenye huruma kwa baba yako

uwe mwenye huruma kwa baba yako; na

 uwe mwenye huruma kwa baba yako lakini huruma hiyo uianzie kwa mama yako kabla ya baba yako.”

 


HAKI ZA WATOTO.

 

799.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al Imam

'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 31, Uk. 290:

“Ewe Ali ! Allah swt huwalaani wazazi wale wanao wafanya watoto wao wasiwe watiifu kwao kwa sababu ya kuwalaani kwao.”

 

800.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia mmoja ya wafuasi

wake, Nahjul Balagha Uk. 536, Msemo, No. 352:

“Usiupitishe wakati wakati wako mwingi pamoja na mke wako na watoto wako waliokuwa wakubwa, kwa sababu kama mke wako na watoto wako ni wampendao Allah swt, basi Allah swt hatawaacha wapenzi wake bila ya kuwajali, iwapo watakuwa ni maadui wa Allah swt, basi kwa nini wewe uwe na wasiwasi na ujiweke mashughuli kwa ajili ya maadui wa Allah swt.

 

Na mambo mawili yanayoweza kuchukuliwa katika wanaume katika kuhusiana na kuwapatiapo familia zao.  Moja ni kutokutimiza wajibu wake kwao,  na pili kinachotajwa hapa ni kulimbikiza kupita kiasi kwa mali kwa ajili yao.”

 

801.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 6, Uk. 47:

“Chukueni hatua za kuwafundisha watoto wenu riwaya na ahadith za Ahlul Bayt a.s. kabla watoto wenu hawajaharibika na hawajachafuliwa akili zao.”

 

802.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 483:

“Heri ya mtu kwa mtoto wake ni kule kwa mtoto wake kuwa heri kwa wazazi wake.”

 

803.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha,

Msemo 399:

“Haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kwamba apewe jina[3] zuri kabisa, afundishwe adabu njema na afundishwe Qur'an kwa kanuni zake.”

 

804.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi J. 6,

 Uk. 47:

“Wafundisheni watoto wenu kuogelea na kulenga shabaha.”

 

805.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 16, No. 45, 330:

“Watoto wenu wanapokua kufikia umri wa miaka saba, wafundisheni sala, wanapokuwa na umri wa miaka kumi, muwalazimishe kusimamisha sala; na mutenganishe vitanda vyao vya kulalia.”

 

806.     Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. : Man la Yahdharul

 Faqih, J. 2, Uk. 622:

“Haki ya mtoto wako ni kwamba wewe utambue wazi kuwa yeye amekuja humu duniani kwa kukupitia wewe, kwa hiyo yaliyo sahihi na yaliyo mabaya yanatokana na wewe. Wewe unawajibika kumpa mafunzo na elimu bora, kumwelekeza kwa Allah swt, na kumsaidia katika kumtii Allah swt. Kwa hivyo iwapo utamsaidia utamfanyia hisani mtoto wako, basi utaweza kufikia malengo hayo; na kama wewe utamwia kiovu, basi hayo yatakurejea wewe mwenyewe.”

 

807.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 104, Uk. 95:

“Muwaheshimu watoto wenu na muwafundishe kuwa wema, mtasamehewa na Allah swt.”

 


KUNYOYESHA MAZIWA

 

808.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Man la

Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 561:

“Naam malipo ya mwanamke wakati wa mimba yake hadi kuzaa mtoto, na wakati pale anapolea mtoto ni sawa na kuwekwa askari katika kituo cha kulinda mipaka ya Waislam dhidi ya hujuma za makafiri, kwa ajli ya Allah swt.  Kwa hivyo iwapo atakufa katika kipindi hiki, basi mwanamke huyo atakuwa katika daraja la mashahidi.”

 

809.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah,

J. 21, Uk. 452:

“Hakuna maziwa yenye faida zaidi kwa mtoto isipokuwa maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake.”

 

810.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 104, Uk. 106:

“Wakati mwanamke anaposhika mimba basi atakuwa ni kama mpiganaji ambaye anafunga saumu wakati wa mchana na anakesha usiku kucha katika ‘ibada, na amejitolea mhanga maisha yake na mali yake katika njia ya Allah swt. Hivyo anapozaa anapata malipo makubwa sana ambayo hakuna mtu anayeelewa isipokuwa Allah swt mwenyewe. Na pale anaponyonyesha mtoto maziwa basi atapata thawabu za kumfanya mtoto mmoja kuwa huru kutoka katika kizazi cha Mtume Ismail a.s. kwa kila mara atakapo nyonyesha. 

 

Na wakati ufikapo kipindi cha kumuachisha mtoto kunyonya, basi malaika aliyekaribu naye humwambia kuanza matendo kwa mara nyingine tena kwani kwa hakika yeye sasa hivi alipo ni katika hali ya kusamehewa kikamilifu (yaani ashike mimba na kuzaa na kunyonyesha tena kwa mara nyingine).”

 

811.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Mustadrak-

ul-Wasa'il, sehemu ya 48:

“Hakuna maziwa yaliyo bora kabisa kwa mtoto isipokuwa maziwa ya mama yake.”


NDOA ‘IBADA KUU.

 

812.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Man la

Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384:

“Raka’a mbili za sala zinazosaliwa na mtu aliyeoa ni nzito kuliko yule asiyeoa ambaye anakesha usiku kucha katika ibada na kufunga saumu nyakati za mchana.”

 

813.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Usingizi wa mtu aliyeoa ni afadhali mbele ya Allah swt kuliko ibada afanyazo mtu asiyeoa usiku kucha na anayefunga saumu nyakati za mchana.”

 

814.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Wengi wa watendao wema katika ‘ummah wangu ni wale waliooa na kuolewa wakati watendao maovu wengi wao ni wale wasio oa au kuolewa.”

 

815.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema, Bihar al-Anwaar,

J. 103, Uk. 217:

“Siku moja mtu mmoja alimwijia baba yangu naye a.s. alimwuliza iwapo alikuwa ana mke naye akajibu alikuwa hana.  Hapo baba yangu a.s. alimjibu kuwa yeye hawezi kulala usiku mmoja bila ya mwanamke hata kama atapewa badala yake dunia nzima na yale yote yaliyomo ndani yake.

 

Na hapo Imam a.s. alimwambia kuwa Raka’a mbili anazosali mtu aliyeoa ni bora kuliko ibada ya yule asiyeoa kwa kukesha usiku kucha na kufunga saumu katika nyakati za mchana. Na baadaye Imam a.s. alimpa Dinar za dhahabu saba na akamwambia akaolee kwa hayo.”


 

KUWAPA HIMA KWA AJILI YA KUOA.

 

816.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5,

Uk. 328 :

“Mtu anayeoa hujipatia nusu ya imani yake, na nusu ya imani inayobakia lazima awe na Taqwa.”

 

817.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema: Man la

Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384:

“Wengi wa watu wa Jahannam watakuwa wale wasioolewa (bila kujali mwanamme au mwanamke).”

 

818.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., At-Tahdhib,

J. 7, Uk. 239:

“Wengi wa wapotofu na walio haribika katika wale walio kufa miongoni mwenu ni wale wasioolewa na wasiooa.”

 

819.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Man la

Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385:

“Yeyote yule anayetaka awe msafi na aliye takasika wakati atakapo onana na Allah swt, basi aoe na awe na mke.”

 

820.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. : Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Oeni, ama sivyo mtahesabiwa miongoni mwa Rahbani  au ndugu wa maShaytani.”

 


NDOA NI UFUNGUO WA REHEMA ZA ALLAH SWT NA BASHARA NJEMA.

 

821.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Milango ya Jannat kwa rehema itafunguliwa katika nyakati nne:

Pale inaponyesha mvua,

wakati mtoto anapoangalia kwa huruma nyuso za wazazi wake,

pale wakati mlango wa Al Ka’aba tukufu inapofunguliwa, na

pale ndoa inapofanyika.”

 

822.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema: Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 222:

“Waunganisheni watoto wenu wavulana kwa wasichana kwa ndoa kwa sababu, humo Allah swt huwajaalia tabia njema, na huwazidishia katika riziki na heshima zao.”

 

823.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5,

Uk. 328:

“Muolewe na muwaoze mabinti zenu, kwa sababu ni bahati nzuri kwa Mwislamu mwanamme kumtoa au kuwapa mtoto wake aliyekua au dada yake kwa ajili ya ndoa.”

 

824.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi J. 5,

Uk. 328:

“Hakuna kilicho kipenzi mbele ya Allah swt kuliko ile nyumba ambayo kuna maamrisho ya Islam yanatekelezwa kwa ndoa; na hakuna kitu chochote kinacho mghadhabisha Allah swt kuliko nyumba ile ambamo kunatokea talaka na ufarakano na utengano kati ya bibi na bwana.”

 


HARAKISHENI KUOA

 

825.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5,

Uk. 337:

“Kwa hakika bikira ni kama matunda ya mtini; matunda hayo yanapokomaa na kama hayakuchumwa, basi mwanga wa jua una waharibu na upepo unawatawanya. Hivyo bikira wapo katika hali hiyo hiyo. Na pale wanapo tambua kile anachohisi mwanamke, basi hakuna dawa yao yoyote isipokuwa kuolewa na bwana. Iwapo wao hawataozwa, basi hawataweza kuepukana na uchafuzi, kwa sababu wao ni binaadamu, vile vile. (kwa sababu wao pia wanahisia na matakwa kama binaadamu wengineo).”

 

826.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Kijana yeyote anayeoa mwanzoni mwa ujana wake, Shaytani wake analia na kujuta kabisa kuwa yeye ameikomboa sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutoka kwa Shaytani.”

 

827.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Mustadrak

 Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 14, Uk. 153:

“Ewe kijana ! Iwapo kuna yeyote miongoni mwenu anayeweza kuoa, basi afanye hivyo, kwa sababu ni vizuri kwa macho yenu (msiwachungulie wanawake wengine) na inahifadhi sehemu zenu za siri (ili muendelee kubakia wacha Allah swt).”

 

828.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Mustadrak Al-Wasa'il-

ush-Shiah, J. 14, Uk. 248:

“Allah swt ameharamisha hali ya kutokuoa, na amewaharamishia wanawake kutokujitenga bila kuolewa (hivyo lazima na wanawake pamoja na kuwa wacha Allah swt lazima waolewe).”

 


 

KUWASAIDIA NA KUINGILIA KATI KATIKA NDOA ZILIZO HALALI.

 

829.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Yeyote yule anayefanya jitihada za kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa iliyo halali ili waweze kuoana kwa sheria takatifu za Allah swt, basi Allah swt atamjaalia kwa ndoa hiyo Hur ul-‘Ain mwenye macho meusi katika Jannat, na atamjaalia thawabu za ibada za mwaka mmoja kwa kila hatua atakayochukua au neno atakalolizungumza.”

 

830.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., At-Tahdhib, J. 7,

Uk. 415 na Al-Kafi J. 5, Uk. 331:

“Ibada bora kabisa ni kule wewe kuingilia kati ya watu wawili kwa ajili kuoana ki halali kwa mujibu wa amri za Allah swt.”

 

831.     Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 74, Uk. 356:

“Katika siku ya Qiyamah, ambapo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha rehema za Allah swt, basi kutakuwa na aina tatu ya watu ambao watapewa kivuli hicho cha ‘Arish ya  Allah swt:

Mtu yule aliye sababisha kusaidia kufunga ndoa ya Mwislamu mwenzake, au

yule ambaye amemhudumia, au

yule ambaye amemfichia siri zake kwa ajili ya suala lake hilo.”

 

832.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, At-Tahdhib, J. 7,

Uk. 404:

“Yeyote yule anayewaunganisha wasioolewa katika ndoa basi wao watakuwa miongoni mwa wale watu ambao Allah swt atawatazama kwa rehema Zake siku ya Qiyamah.”

 

833.     Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 74, Uk. 356:

“Katika siku ya Qiyamah, kutakuwa na kivuli maalum cha Allah swt ambamo hakutakuwapo na wengine isipokuwa

Mitume a.s au vizazi vyao, au

Muumin anayemfanya huru mtumwa, au

Muumin anayelipa deni la muumin mwingine, au

Muumin ambaye anawaunganisha waumini ambao katika ndoa (waumini ambao hawajaoana).”

 

834.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 20, Uk. 46:

“Yeyote yule anayejaribu kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa kwa mujibu wa sheria za Allah swt, basi Allah swt atampatia Hur ul-‘Ain elfu moja (wahudumu wanaokaa Jannat wakiwa na macho meusi makubwa) katika ndoa na ambapo kila mmoja wao atakuwa katika ngome ya Malulu na Almas na Rubi.”


 

MWANAMKE NA MAHARI.

 

835.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 58, Uk. 321:

“Ubashiri mbaya wa mwanamke ni kuwa mahari yake ya juu kabisa na ghadhabu zake.”

 

836.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.   a.s Amesema,

“Waizi huwa wa makundi matatu:

La kwanza wale wanaozuia kutoa sadaka; 

pili wale wanao jiwekea mahari ya mwanamke na kujihalalishia kwa ajili yao wenyewe;

tatu wale wanaochukua mikopo na hawajaamua kurudisha mikopo hiyo kwa ajili ya kulipa madeni yao.”

 

837.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 387:

“Kwa hakika moja ya baraka za Allah swt kwa mwanamke ni mahari yake kutokuwa juu, na moja ya maovu ya mwanamke ni kuwa na mahari kubwa.”

 

838.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah,

J. 21, Uk. 253:

“Msifanye mahari ya wanawake ikawa nzito, kwa sababu hiyo inaleta uhasama na uadui.”

 

839.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar,

 J. 64, Uk. 268:

“Kuna madhambi maovu kabisa ya aina tatu:

Kuwatesa wanyama wakati wa kuwachinja,

Kuchelewesha na kutokulipa mahari ya mwanamka, na

Kutokulipa mishahara ya wafanyakazi.”

 


 

AFADHALI MAHARI NDOGO.

 

840.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 16, Uk. 299:

“Ndoa ile imebarikiwa ambayo ina gharama ndogo.”

 

841.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 236 [4]:

“Wanawake bora kabisa katika umma wangu ni wale ambao nyuso zao ni zenye urembo na mahari yao huwa ni ndogo.”

 

842.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 16, Uk. 321[5]:

“Oeni hata kama mtakuwa na pete ya chuma (kama mahari).

 

843.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 16, Uk. 321:

“Yeyote yule anayetoa hata kiasi cha tonge moja ya nafaka au tende kama mahari (kwa kukubaliwa na mwenzake), basi kwa hakika ndoa yake ni halali na sahihi kabisa.”

 

844.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Wasa'il ush-Shi'ah,

J. 21, Uk. 251:

“Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alitoa mahari ya Zirah moja yenye thamani ya Dirham thelathini katika ndoa ya binti yake Fatimah az- Zahra a.s. akiwaolewa na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.”

 


 

NDOA KWA KUJALI IMANI NA UAMINIFU.

 

845.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. bila kujali daraja la

kizazi cha mtu, amesisitiza na kusema, At-Tahdhib, J. 7, Uk. 394:

“Mtu yeyote anapokuletea habari za kutaka kukuoa na wewe kwa kuridhika unakubalia, kwa adabu zake na dini yake, basi ungana naye kwa ndoa. Na iwapo hutafanya hivyo, basi wewe utakuwa umesababisha fitina na ufisadi mkubwa kabisa juu ya ardhi.”

 

846.     Imam Jawad a.s. ameandika katika barua, Al-Kafi J. 5, Uk.

347 na Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 393 na At-Tahdhib, J. , Uk. 394:

“Mtu yeyote akutakaye wewe katika ndoa anayetaka kukuoa na wewe unakuwa umeridhika na dini na uadilifu wake, basi ungana naye kwa ndoa.”

 

847.     Siku moja mtu mmoja alimwambia Al Imam Hussein ibn

'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa, Al-Mustadrak, J. 2, Uk. 218:

“Yeye alikuwa na binti wake na alimwuliza Imam a.s. kuwa yeye amwoze binti wake kwa nani, kwa hayo Imam a.s. alimjibu: Muoze binti wako kwa yule ambaye ana imani na ni mcha Allah swt: Kwa sababu atampenda na kumheshimu huyo binti wako, na iwapo yeye atakuwa mkali juu ya binti yako, basi hatamdhuru.”

 

848.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-

    Muhajjat-ul-Baidha, J. 3, Uk. 94:

“Yeyote yule atakaye muoza binti wake kwa mtu ambaye si mcha Allah swt basi kwa hakika amevunja uhusiano wake pamoja naye.”

 


 

AZMA YA MWANAMME KATIKA NDOA.

 

849.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, At-Tahdhib,

J. 7, Uk. 399:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa urembo wake tu (bila ya kujali imani yake), basi yeye hataambulia kile alichokitaka; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya mali na utajiri wake (basi Allah swt atampa hiyo mali na utajiri tu peke yake.) Kwa hivyo ni juu yenu nyie kutafuta mwanamke aliye katika dini na mcha Allah swt.”

 

850.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 333:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa matarajio ya utajiri, basi Allah swt anampa utajiri na mali peke yake.”

 

851.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, At-Tahdhib,

J. 7, Uk. 399:

“Yeyote anayeoa mwanamka kwa utajiri wake, Allah swt humwachia hayo tu; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake na uzuri wake, basi yeye atayaona yale ndani ya mwanamke yale asiyoyapenda; lakini yule anayeoa mwanamke kwa misingi ya imani na dini yake, basi Allah swt atamjazia kila aina ya sifa ya mambo hayo kwa ajili yake.”

 

852.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 20, Uk. 53:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake tu, basi Allah swt atamjaalia uzuri wake na uzuri wa mwanamke huyo utamdhuru na kumletea matatizo huyo mwanamme.”

 

853.     Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s., Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 385:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt, na kuungana naye kwa wema basi Allah swt atamjaalia taji la heshima na ufanisi.”

 

854.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w.,

Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 3, Uk. 85:

“Msioe wanawake kwa ajili ya urembo wao tu kwa sababu urembo wao unaweza kusababisha wale wasiwe wacha Allah swt wala si kwa ajili ya mali yao kwa sababu mali yao inaweza ikawasababisha wakawa wasiwe watiifu; lakini muwaoe kwa misingi ya imani ya dini yao.”

 

 


 

KUTAFUTA RIZIKI.

 

855.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Man la

 Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 168:

“Amelaaniwa, amelaaniwa yule ambaye hawajali wale anaotakiwa kuwalisha ambao wanamtegemea, kwa hakika amelaaniwa kwa mara nyingi.”

 

856.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Man la

Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 16:

“Mwanamme yule ambaye anafanya subira kwa hasira mbaya za mke wake, na anatafuta ile subira kwa Allah swt, basi Allah swt anamjaalia thawabu na ujira mkubwa sana kwa wale wenye kushukuru.”

 

857.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 168 na Al-Kafi, J. 5, Uk. 88:

“Yeyote yule anayevumilia taabu za kutafuta pesa kwa ajili ya kumtimizia haja ya mke wake, ni sawa na yule anayepigana vita vya Jihadi katika njia ya Allah swt.”

 

858.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Man la Yahdharul
Faqih, J. 3, Uk. 168:

“Ni dhambi moja kubwa kabisa inamtosheleza mtu yule ambaye anawapuuzia wale wanaomtegemea yeye kwa kuwapatia riziki. (Dhambi hili kubwa linaweza kumteketeza huyo mtu).”

 

859.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 168:

“Mtu mwenye furaha ni yule ambaye anasimamia na kuratibu maswala ya mke na watoto wake.”

 

 


 

WAKE KUWAWIA WEMA WAUME ZAO.

 

860.     Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu,

Sura Ar-Rum, 30, Ayah ya 21.

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.

 

861.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alipopata habari

kutoka kwa Ummi Salama kuhusu Uthman ibn Mazu’un, basi aliondoka kuelekea wafuasi wake na huku akiwaambia kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 93, Uk. 73:

“Je nyie mnajitenga na wake zenu ? Kwa hakika, mimi mwenyewe huwaendea wanawake, huwa ninakula chakula nao mchana, na kulala nao usiku. Kwa hakika yeyote yule anayejitenga na maisha ninavyoishi mimi basi hatakuwa miongoni mwangu yaani atakayeipa mgongo.”

 

862.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Man la Yahdharul

Faqih, J. 3, Uk. 385:

“Yeyote yule anayeikataa ndoa na kuipuuzia kwa hofu ya gharama itakayo mfikia, basi anaondoa imani yake juu ya Allah swt kwani inamaanisha kuwa yeye hamwamini Allah swt.”

 

863.     Imeripotiwa kutoka kwa Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 219:   

“Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa kumjibu wa mwanamke ambaye alikuwa hataki aolewe ili abaki bila kuolewa, kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu

“ usifanye hivyo, kwa sababu iwapo ndivyo ingekuwa ni kutukuka huko, basi Bi Fatimah az-Zahara a.s. angekuwa ni mwanamke wa kwanza kutokuolewa kuliko wewe (kwa sababu yeye alikuwa na wadhifa mmoja mkubwa sana akiwa ni binti wake Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w.), na kwa hakika hakuna mwanamke yeyote duniani ambaye anaweza kuwa na utukufu zaidi ya Bi Fatimah az-Zahara a.s.”

 

864.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa kusema kuwa, Al-

Kafi J. 5, Uk. 496:

“Wanawake watatu walimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kusema kuwa waume zao wamekataa kula nyama au kutumia manukato au kuwakaribia wake zao. Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. (Akikaripia matendo yao) alikwenda haraka juu ya Mimbar na baada ya Kumhimidi Allah swt alisema: Je wamekuwaje baadhi ya watu kuwa hawataki kula nyama, na wala hawataki kutumia manukato, na wameacha kuwakaribia wake zao?.”

 

865.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 494:

“Kuwa wakati mke wa Uthman ibn Mazu’un, alipomwelezea Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. kuwa bwana wake daima amekuwa akifunga saumu siku za mchana na kusali wakati wa usiku alikuwa hajali maisha yake na wala alikuwa hamjali mke wake pia, kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliondoka akaenda moja kwa moja nyumbani kwake na akamkuta yuko anasali. Wakati Uthman alipomaliza sala zake, Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alimwambia: “Ewe Uthman, Allah swt hakunituma mimi kuwa Ruhbani (Kuwa kama Mapadre kwa kikirsto) bali amenituma mimi kwa ajili ya dini iliyo rahisi ambayo inalinda haki za mwili na roho. Mimi hufunga saumu, huwa nikidumisha sala, na huwa nikichanganyikana na kujumuika pamoja na familia yangu kwa ukamilifu. Na yeyote yule anayependa Sunnah yangu na mwenendo wangu basi lazima afuate mwenendo wa maisha yangu, na Sunnah yangu; Na kwa hakika ndoa ikiwa ni mojawapo ya Sunnah zangu.”


 

KUWAHESHIMU WAKE ZENU.

 

866.     Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili kutoka kwa baba yake hadi kufikia kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 8,

 Uk. 310:

“Amelaaniwa mwanamke yule ambaye anamfanya mme wake akasirike, na mwanamke mwenye furaha ni yule ambaye humridhisha bwana wake kwa furaha.”

 

867.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 7, Uk. 214:

“Yeyote yule aliye na wanawake wawili na kama hawawii kwa haki kwa nafsi na mali yake miongoni mwao, basi siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa amefungwa kwa minyororo na nusu ya mwili wake hautakuwa wima hadi kule atakapo tumbukizwa Jahannam.”

 

868.     Imam Muhammad al-Baqir a.s. Amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 103, Uk. 224:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke lazima amheshimu kwa heshima zote, kwa sababu mwanamke kwa mtu yeyote anamaanisha raha na mustarehe, kwa hiyo yeyote anayemwoa mwanamke asimharibu wala kumdhalilisha yeye (Kwa kutojali haki zake zinazostahili).”

 

869.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 103, Uk. 223:

“Kwa hali yoyote ile na katika sura yoyote ile lazima mpatane na wake zenu, na muongee nao vyema kwa kutumia maneno mema mazuri, na hivyo matendo yao yatakuwa mema na watabadilika kuwa wake wema na wazuri kwa ajili yenu.”

 

870.     Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kwa kumnakili

baba a.s. yake ambao wamemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema, Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 228:

“Kiasi chochote cha imani cha mtu kitakachoongezeka basi na kumjali kwa mke wake pia kutaongezeka.”

 

871.     Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa,

Al Khisal, Uk. 183 na Bihar al-Anwaar, J. 76, Uk. 141:

“Kutokana na vitu vya duniani, mimi huwajali wanawake na manukato zaidi, lakini ibada ni nuru ya macho yangu, (mapenzi na ibada ya Allah swt).”


MWANAMKE KUMRIDHISHA MUME WAKE

 

872.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema , Bihar al-Anwaar, j.81, uk 385

“Siku ya Qiyamah mwanamke hataokolewa na hatapata uokovu wowote kutoka kwa Allah swt bila ya idhini ya bwana wake.”

 

873.  Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. ameripoti kutoka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye amesema, Al-kafi, j5, uk.324 :

“Bora wa wanawake miongoni mwenu ni yule ambaye ana sifa tano

Mwanamke asiye na matatizo, Mtiifu, Mnyenyekevu, Mwenye matumizi madogo

Mvumilivu wakati bwana wake anapokasirika

Mshiriki mwema na msaidizi wakati wa shida,

Mpaji wa hima kwa bwanake anapokuwa amezongwa na mawazo na shida

Mtunzaji wa mhifadhi wa nyumba ya bwana wake anapokuwa hayupo.

 

Kwa hivyo mwanamke kama huyo ni wakala wa mawakala wa Allah swt na kwa hivyo mawakala wa Allah swt hawatakuwa wenye hasara (yeye anapata matumaini sahihi).

 

874.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.5, Uk.507

“Mwanamke yeyote yule anayepitisha usiku ambapo mume wake amemkasirikia na kumghadhibikia, ibada zake hazikubali hadi pale huyo mwanamke atakuwa amemridhisha bwana wake.”

 

875. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Makarim-ul-Akhlaq,J.2, Uk. 246 :

“Haki za bwana kwa mke wake ni kuziwasha taa, kutayarisha na kupika chakula na kumpokea mume wake anapokuja mlangoni kwa maneno mazuri na kamwe asimkatalie mume wake anapomhitaji yeye binafsi ( kujamiiana) isipokuwa anapokuwa sababu zake.[6]

 

876. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,Mustadrak-Al-Wasa'il-ush-Shiah, J.14, Uk. 257 : 

“Mwanamke kamwe hatatekeleza haki za Allah swt hadi yeye ametekeleza haki za mume wake.”

 

877.  Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.,Wasa'il ush-Shi'ah, J.10, Uk. 527

“Siku moja mwanamke mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Allah swt ! Je bwana haki gani kwa mke wake ?’

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu:  Mwanamke amtii mume wake na wala asimuasi.’”

 


 

TALAKA NA ATHARI ZAKE.

 

878.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi,

J. 6, Uk. 54:

“Kwa hakika Allah swt hapendi kabisa au humlaani mwanamme au mwanamke yeyote ambaye anakuwa na nia ya talaka au anaoa kwa ajili ya kustarehe tu.”

 

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameirejea kauli hii mara tatu kusisitiza kuwa mwanamme yeyote yule anayempa mke wake talaka kwa ajili ya kuoa mwanamke mwingine na kutaka kustarehe starehe za ndoa mwanmke mpya na vile vile mwanamke yeyote yule anayeomba talaka kwa sababu kama hizo hizo na kuolewa na mwanamme mwingine, basi wote hawa wanajitumbukiza katika laana za Allah swt.[7]

 

879.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 104, Uk. 107:

“Wanawake katika umma wangu ambao wanafuata sunnah nne (mambo mema manne) basi wataingizwa Jannat:

Iwapo yeye atalinda utukufu wake,

 Anamtii mme wake,

Anatimiza sala zake tano, na

Anafunga saumu katika mwezi wa Ramadhani.”

 


 

KUPELEKA MACHO CHINI NA KULINDA HESHIMA.

 

880.     Allah swt anatwambia katika Qur'an Tukufu, Sura An Nuur, 24, ayah ya 30.

Waambieni waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah swt  anazo khabari za wanayo yafanya.

 

881.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anatuambia, Man la Yahdharul

Faqih, J. 4, Uk. 18:

“Kutazama kiharamu kwa wale walio haramishwa kwetu ni sawa na mshale kutoka upinde wa Shaytani ambayo imejaa sumu. Yeyote anayejiepusha naye kwa ajili ya Allah swt, na wala si kwa sababu zinginezo, basi Allah swt atampa imani ambamo yeye ataipata furaha ndani mwake.”

 

882.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 5,

Uk. 559:

“Zinaa ya macho ni kuangalia yale yaliyo haramishwa, kwa mtazamo wa matamanio,

Zinaa ya midomo ni kuwabusu wale walio haramishwa (wasio maharimu), na

 Zinaa ya mikono ni kuwagusa (mikono na sehemu zingine za wale walio haramishwa Wasio-maharimu ) bila kujali iwapo atakuwa na hamu au hatakuwa na hamu ya kujamiiana.”

 

883.     Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi, J. 5,

Uk. 559:

“Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amemlaani yule mtu ambaye anaangalia sehemu za siri za mwanamke ambaye si halali kwake, na vile vile ememlaani yule mtu ambaye anafanya khiyana pamoja na mke wa ndugu yake, na vile vile yule mtu ambaye anachukua rushwa kwa watu kwa msaada wanaohitaji kutoka kwake.”

 

MWANAMKE NA KUJIPAMBA.

 

884.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Wasa'il ush-

Shi'ah, Volume 14, Uk. 10:

“Neno asemalo mwanamme kumwambia mke wake:

‘Nakupenda  basi kamwe halitatoka moyoni mwa mke wake’.”

 

885.     Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi, J. 4,

Uk. 119:

“Haijali chochote au vyovyote vile mwanamke ajirembavyo kwa ajili ya bwana wake.”

 

886.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Man la Yahdharul

Faqih, J. 4, Uk. 6:

“Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kujiremba kwa mwanamke kwa ajili ya mwanamme mwingine mbali na mume wake mwenyewe na akasema:

‘Na kama atafanya hivyo, basi ni haki ya Allah swt kumchoma moto katika Jahannam. (Hadi hapo atakapofanya Tawba[8] )”

 

887.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Wasa'il ush-Shi'ah,

 J. 14, Uk. 11:

“Yeyote yule anayezidisha mapenzi yetu (Ahlul Bayt a.s.) basi na atazidisha mapenzi yake kwa mke wake vile vile.”

 

888.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 20, Uk. 30:

“Bora katika wake zenu ni yule ambaye ni mcha Allah swt na mtiifu kwa mume wake katika mapenzi na kujirembesha (lakini sio kuwavutia wanaume wengine).”


 

ZINAA NA ATHARI ZAKE MBAYA.

 

889.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi,

J. 5, Uk. 554:

“Imeandika katika Tawrat:

Mimi ni Allah swt, muuaji wa wauaji na muadhibu wa wazinifu.”

 

890.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 5,

Uk. 541:

“Ziko athari sita za zinaa, tatu ambazo zinapatikana humu duniani na tatu zitapatikana huko akhera.

Zile zitakazoonekana duniani:

Itaondao heshima ya mtu na kumdhalilisha;

Itamfanya mtu awe maskini; na

Itafupisha umri wa maisha yake (yaani atakufa haraka).

 

Na zile zitakazo patikana Akhera ni:

Adhabu za Allah swt,

Hali ngumu kabisa katika utoaji wa hesabu, na

Kutumbukizwa katika Jahannam kwa ajili ya milele.”

 

891.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Kutokea

Tawrat, Al-Kafi, J. 5, 554:

“Kuwa enyi watu msizini kwa sababu mkifanya hivyo wake zenu pia watafanya vivyo hivyo. Kile mkipandacho ndicho mtakacho kivuna. (kila ufanyavyo na wewe utafanyiwa hivyo).”

 

892.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Man la

Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 14:

“… yeyote yule amkumbatiaye mwanamke, ambaye ameharamishiwa kwake, basi atafungwa kwa minyororo ya mioto pamoja na Shaytani na wote kwa pamoja watatupwa katika Jahannam.”

 

893.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. wakati mmoja aliulizwa na

Amar ibn Mussa kuhusu kufanya tendo la kujamiiana pamoja na wanyama au kujitoa manii kwa mkono au kwa kutumia sehemu zinginezo za mtu mwenyewe, na Imam a.s. alimjibu, Al-Kafi, J. 5, Uk. 541:

“Hali yoyote katika hizi na vyovyote vile ambavyo mwanamme humwaga maji yake, inachukuliwa kuwa ni zinaa (na imeharamishwa).”

 

894.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi,

J. 2, Uk. 270:

“Amelaaniwa! Amelaaniwa yule mtu ambaye anafanya tendo la kuwaingilia wanyama.”

 

895.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 5, Uk. 316 ;

“(Zinaa miongoni mwa jamii moja) mwanamme kwa mwanamme au mwanamke kwa mwanamke (ni zinaa).”


ULAWITI.

 

896.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

“Kuingiza (uume) mwanzoni mwa nafasi ya haja kubwa ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika sehemu ya mbele ya siri ya mwanamke. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut[9] a.s. kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi za zinaa.”

 

897.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa !  Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt  humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo.”

 

898.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi

“Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu  bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri).”

 

899.  Hudhaifa ibn Mansur anasema :

“Mimi nilimwuliza  al-Imam as- Sadique a.s. kuhusu Dhambi Kuu.

 

900.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa.”

 

901.  Nikamwuliza tena,

“Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?”

 

902.  Al-Imam as- Sadique a.s. alinijibu :

“Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad s.a.w.w. (Qur’an tukufu ).”

 

903.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Qur’an Tukufu, Surah Hud, 11, Ayah 82, isemayo :

‘Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka.’

 

904.  Al-Imam as- Sadique a.s. alimjibu:

“Yupo mtu ambaye anaiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, lakini Allah swt anampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokea watu wa Mtume Lut a.s.[10]

 

Walivyoadhibiwa Umma wa Mtume Lut a.s.

905. Qur’an tukufu imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut a.s. .

  • Sauti kubwa ya kutisha na mayowe ya kusikitisha na makubwa mno
  • Kupigwa kwa kutupiwa mawe juu yao
  • Kupindua ardhi juu chini

 

906.  Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud, 11 : 83 

‘(Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)’

 

 

907.  Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. amesema : katika  Fiqh-i-Ridha

“Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa  kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera.”

 

908.  Qur’an tukufu imetumia neno ‘utovu wa adabu, uchafu’ kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A’araf, 7, : Ayah 80 - 81

‘Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:”Je ! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu.’

 

“Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.’

 

909.  Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika maudhui yanayozungumzia zanaa.  Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Wasa’il al-Shiah

“Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu.”

 

910.  Ni haraam kumbusu kijana wa kiume kwa kuashiki.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika  Al-Kafi kwa kumnakili Mtume Muhammad s.a.w.w. :

“Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama) , Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto.”

 

911.  Al-Imam ar-Ridha a.s. amesema katika Fiqh-i-Ridha :

“Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu  wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno.”

 

912.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Mustadrakul

     Wasail :

“Allah swt atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi.”

 

913.  Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi au shuka moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.

 

914.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti  kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja."

 

915.  Kwa mujibu wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.,

“Mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.

 

916. Tunakuleteeni hadith ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliyoisema :

“Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti.”

 

917. Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia sehemu za haja kubwa), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake :

  • mama wa kijana huyo,
  • dada na
  • binti yake huyo kijana kwa maisha yake yote. 
  • Yaani, mtu huyu (mlawiti) kamwe hataweza kumwoa mama yake, au dada au binti ya huyo kijana.

 

918.  Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:

 "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera. 

Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-

·        Wanapoteza nuru 

·        Wanakuwa maskini

Maisha yao yanakuwa mafupi.

 

Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-

·        Allah swt atakuwa amewakasirikia mno

·        Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali

·        Wataishi milele Jahannam.

 

919.  Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

"Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."

 

(2413)      Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe.  Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme  umeingia katika sehemu za haja kubwa au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

 

(2414)      Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamlawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

 

       


 

USAFI KATIKA ISLAM.

 

920.     Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Ithna-

'Asheriyyah, Uk. 92:

“Kuna mema matatu ambayo Allah swt huyapenda katika watu:

Ufupi katika uzungumzaji,

usingizi mfupi, na

 ulaji mdogo;

 

Na mambo matatu ambayo hayamfurahishi Allah swt:

Kuzungumza kupita kiasi

Kulala kupita kiasi, na

 Kula kupita kiasi.”

 

921.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Kanz-ul-

'Ummal, Hadithi no. 26002:

“Jaribuni kuwa wasafi kila muwezavyo. Kwa hakika Allah swt ameweka misingi ya Islam juu ya usafi; hivyo kamwe mtu mchafu hawezi kuingia Jannat mpaka awe msafi.”

 

922.     Al Imam Amiril Muuminin 'Ali ibn Abi Talib a.s., Amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 356:

“Kula kupita kiasi kunasababisha wingi wa magonjwa.”

 

923.     Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Khisal-i-Sadduq,

Uk. 125:

“Zipo Sunnah tano kuhusu kichwa na tano zingine kuhusu mwili.

Sunnah tano zinazohusiana na kichwa ni:

Kuosha mdomo,

kunyoa mashurubu,

kuchana nywele,

kupitisha maji kupita mdomo na

pua.

 

Sunnah tano zinazohusiana na mwili ni:

Kukaa jando,

kunyoa nywele za sehemu za siri,

kunyoa nywele kwenye mabega,

kupunguza na kukata makucha, na

 kusafisha na kuosha sehemu za siri (kwa maji au kwa karatasi, kwa kitambaa, au chochote kile kinachoweza kukufaa n.k.)”

 

924.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia Al Imam Hasan

ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il  ush-Shi'ah, J. 24, Uk. 245:

“Je nikufundishe mema manne ambayo hautahitaji dawa ya matibabu ya aina yoyote ?

“Naam” alijibu Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. 

 

Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu:

Usikae kula chakula hadi uwe una njaa;

Na usiondoke juu ya meza ya chakula bila ya kubakiza njaa kidogo;

Tafuna chakula chako vyema mdomoni mwako;

Na unapotaka kwenda kulala, uende ukajisaidie haja.

 

Iwapo utatekeleza haya basi kamwe hautahitaji matibabu ya aina yoyote.”

 


 

BIASHARA NA UHUSIANO WA KIJAMII.

 

925.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Amesema Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 89:

“Iwapo mtu atanunua mali ambayo katika vyakula ambacho ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na kama atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi kama fedha zote atazigawa katika sadaka kwa na wenye kuhitaji misaada maskini, basi hiyo haitapunguza adhabu yoyote mbele ya Allah swt kwa kile alicho kitenda (kuhujumu uchumi).”

 

926.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 103, Uk. 93:

“Yeyote yule anayefanya biashara bila ya kuzingatia sheria na kanuni za Islam, basi kwa hakika ataingia katika riba, (bila ya yeyemwenyewe kujijua).”

 

927.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ananakili kutoka Mtume

Muhammad  Mustafa s.a.w.w.  kuwa Amesema, Khisal-i-Sadduq,

J. 1, Uk. 286:

“Yeyote yule aliye katika biashara na anayenunua na kuuza vitu lazima ajiepushe mambo matano, ama sivyo asinunue wala asiuze kitu chochote:

Riba,

Kula kiapo,

Kuficha ubaya na kasoro za mali,

Kusifu kitu kama hakistahili hivyo wakati wa kuuza; na

kutafuta kasoro au ubaya wakati wa kununua.[11]

 

928. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Kafi, J. 5,

Uk. 78:

“Yeyote yule anayetafuta riziki humu duniani ili aondokane na shida za kutegemea watu katika mahitaji yake, na ili kuwalisha na kuwasaidia wananyumba wake, na kueneza mapenzi yake kwa majirani zake basi atakutana na Allah swt siku ya Qiyamah huku uso wake ukiwa uking’ara kama mwezi.”

 


 

KUGHUSHI KATIKA BIASHARA.

 

929.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Safinat-ul-

Bihar, J. 2, Uk. 318:

“Yeyote yule anaye lala huku akiwa amepanga njama dhidi ya Muislam mwenzake moyoni mwake, basi amelala katika adhabu za Allah swt, na atabakia katika hali hiyo hadi pale afanye Tawba.”

 

930.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 17, Uk. 283:

“Na yeyote yule anayemlaghai ndugu yake Mwislam, basi Allah swt humwondoshea riziki kwa wingi na huharibu maisha yake na kumwachia katika hali yake mwenyewe.[12]

 

931.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., At-Tahdhib, J. 7,

Uk. 13:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kuchanganywa kwa maji katika maziwa wakati wa kuuza.”

 

932.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema,

“Yeyote yule anayewaghushi Waislam kwa ujumla basi huyo hayupo nasi.”

 

933.     Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 80:

“Mtu yeyote anaye walaghai Waislam wenzake katika kununua au kuuza kitu chochote, hayupo miongoni mwetu, na siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa miongoni mwa Wayahudi, kwa sababu wao wamekuwa daima wakiwadanganya na kuwaghushia Waislam.”

 


 

MATAMANIO NA TAMAA ZISIZO HALALI.

 

934.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi,

J. 2, Uk. 79:

“Baada yangu mimi, ninawahofia umma wangu katika vitu vitatu:

Upotofu baada ya kuelimika,

 matamanio yanayo potosha na

Tamaa ya tumbo na sehemu za siri.”

 

935.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Al-Kafi, J. 2,

Uk. 80:

“Hakuna ‘ibada ya Allah swt iliyo na thamani zaidi kuliko usafi, uhalisi wa tumbo la mtu na sehemu zake za siri kutokana na matamanio au tamaa.”

 

936.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makarim-ul- Akhlaq, 429 :

“Kwa mtu ambaye anakuwa na matamanio na maovu yanapokuwa daima yako tayari na yeye anayaepukana nayo kwa sababu ya hofu ya Allah swt,  basi Allah swt atamharamishia moto wa Jahannam na atamhakikishia kuwa hatakuwa na tishio kubwa ….”

 

937.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema: Al-Muhajjat-ul-Baidha

“Yeyote yule anayejinusuru na maovu ya

tumbo,

ulimi, na

sehemu zake za siri basi kwa hakika amejinusuru kutoka madhambi.”

 

938.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha

U. 553:

“Kumbuka (wakati wa kutenda dhambi), kuwa raha zinapotea wakati matokeo ( yatakayotokea )yake yanabakia.”

 

939.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 5,

 Uk. 548:

“Yeyote yule anayembusu kijana wa kiume kwa matamanio ya kitamaa, basi Allah swt atamadhidhibisha na kumchapa kwa miale ya moto.”

 

940.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2,

Uk. 79:

“Je kuna jitihada gani iliyo afadhali kuliko usahihi wa tumbo na wa sehemu za siri.”

 


 

MALI YA DUNIA NA ULIMBIKIZAJI KWA UROHO.

 

941.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 71, Uk. 173:

“Kwa yeyote yule ambaye siku zake mbili za maisha yakawa sawa (hakuna maendeleo ya kiroho) kwa hakika yupo katika hasara.”

 

942.     Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 311:

“Mfano wa dunia hii ni sawa na maji ya bahari. Kiasi chochote yule anywacho mwenye kiu kutoka bahari, kiu chake kitaendelea kuongezeka hadi kinawez kumuua.”

 

943.     Al Imam Muhammad at-Taqi a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 368:

“Watu wanaheshimiwa humu duniani kwa kuwa na mali na Akhera watu wataheshimiwa kwa kuwa na matendo mema.”

 

944.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makusanyo
ya Waram:

“Maangamizo ya wanawake wangu yako katika mambo mawili:

Dhahabu na

mavazi yasiyo ya heshima;

 

Na maangamizo ya wanaume wafuasi wangu yapo katika

kuiacha elimu na

 kukusanya na kulimbikiza mali.”

 

DUNIA INAYO HADAA, MAVUTIO NA SUMU YAKE.

 

945.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-

Anwaar, J. 6, Uk. 161:

“Wakati Jeneza maiti ya mtu inapoinuliwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa, basi Ruh yake inaifuata maiti na katika hali ya masikitiko makubwa inasema:

‘Enyi watoto na Jama’a zangu ! Jitahadharisheni sana kuwa ulimwengu huu hauwahadai nyie kama mulivyonifanyia mimi.

 

Mimi nimekusanya mali yote hii bila ya kujali uhalali au uharamu wake na nimeiacha nyuma huku kwa ajili ya wengine.

 

 Sasa mimi nimeondoka na mzigo juu yangu (kwa sababu ya kutenda kila aina ya madhambi ya uhalali na uharamu) wakati matunda yake wanafaidi watu wangineo; kwa hivyo, mujiepushe na hayo ambayo sawa na yaliyo nifika mimi.”

 

946.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 73, Uk. 166:

“Iwapo huyu mtu angeweza kuiona mauti yake na kasi yake inavyo mwelekea yeye basi kwa hakika angechukia na kuiacha dunia na matumaini yake yote.”

 

947.     Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 311:

“Mfano wa dunia ni kama nyoka ambaye ngozi yake ya nje ni laini na nyororo kwa kugusa wakati kuna sumu kali mno inayoua ndani mwake. Aliye na hekima wanajaribu kujiepusha nayo (lakini watoto wasio na fahamu kamili) wanapendezewa na kuvutiwa nayo na wanatamani kugusa na kucheza kwa mikono yao.[13]

 

948.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 2,Uk. 315:

“Mapenzi ya dunia hii itakayo angamia ndiyo chanzo cha maovu yote.”

 


 

WATUMWA WAPUUZAJI WA DUNIA HII INAYO HADAA.

 

949.     Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.,  Tuhaful-'Uqul na Bihar al-Anwaar, J. 44, Uk. 374:

“Kwa hakika, watu ni watumwa wa dunia na imani yao haina misingi yoyote, ipo katika ndimi zao tu. Wao wanaitilia maanani ili mradi wanapata mahitaji yao wanayoyahitaji, lakini pale wanapojaribiwa, basi idadi ya waumini halisi inakwenda ikipungua.”

 

950.     Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 84:

“Mimi nastaajabishwa kuhusu yule mtu ambaye yuko mashughuli kwa ajili ya kula tu lakini hafikirii kwa ajili ya chakula cha akili yake. Hivyo yeye anajiepusha na kile kinachomdhuru tumboni mwake na papo hapo anaiachia akili yake ijae kwa yale yanayoangamiza.”

 

 


 

ULAFI NA MATUMAINI YA KIPUUZI.

 

951.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha

Barua no. 52:

“Ingawaje uchoyo, uoga na uroho ni vitu vyenye sifa tofauti, lakini vyote viko sawa katika mambo ya kufikiria kwao kuhusu Allah swt.”

 

952.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Man la Yahdharul

Faqih, J. 4, Uk. 418:

“Iwapo mwanaadamu atakuwa na mabonde mawili ambamo kumejazwa dhahabu na fedha, basi yeye hatatosheka nayo bali atakwenda kuitafuta ya tatu.”

 

953.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Usul-i- Kafi, J. 2,

Uk. 320:

“Yeyote yule anaye uendekeza moyo wake kwa dunia hii basi atapatwa na hali tatu:

Mateso yasiyoisha,

kiu ya matamanio isiyoisha na

matumaini yasiyo timika.”

 

954.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam,

Uk. 240:

“Wako kiasi gani cha watu ambao ni waovu na siku zao ziko zinahesabika lakini bado wanaendelea kwa juhudi zao zote za kuitafuta hii dunia.”

 


 

MAJIVUNO NA KIBURI.

 

955.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Tasnif-i-Ghurar-ul-

Hikam,Uk. 443:

“Msiwe wakaidi (na msing’ang’anie kufuata vile mfikiriavyo nyie wenyewe), kwa sababu watu kama hawa hukumbana na maangamizo.”

 

956.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Tasnif-i-Ghurar-ul-

Hikam,Uk. 308 na Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 91:

“Yeyote yule ajionaye kuwa yeye ndiye mkubwa kabisa (hana mfano mwingine) basi si kitu chochote kile mbele ya Allah swt.”

 

957.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 72, Uk. 39:

“Mambo mawili yanasababisha watu kuangamia (na kutumbukizwa katika Jahannam):

Kuogopa umaskini, na

Kutaka ukubwa kwa kupitia majivuno.”

 

958.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 298:

“Mjiepushe na kujifakharisha wenyewe, kwa kutegemea yale muyaonayo mazuri ndani mwenu na kwa kupenda kuzidishiwa sifa kwa sababu hayo ndiyo majukumu makubwa yakutegemewa na Shaytani.”

 

959.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 310:

“Yeyote yule aliye na kiburi hata kidogo moyoni mwake basi hataruhusiwa kuingia Jannat.”

 


 

KUBANA MATUMIZI.

 

960.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

 J. 71 Uk. 346:

“Yeyote yule anaye panga matumizi yake basi kamwa hatakuwa fakiri.”[14]

 

961.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 182:

“Sera bora kabisa ni katika kutekeleza ukarimu.”

 

962.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 15, Uk. 271:

“Matumizi ya kupita kiasi cha kile kinachohitajika, ni ufujaji.”

 

963.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

 J. 66, Uk. 334:

“Lau watu wangekuwa na tabia ya kula kwa kiasi, basi miili yao ingekuwa na nguvu.”

 

964.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Irshad-ul-

Qulub…………:

“Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia:

‘Ewe uliye ghafilika ! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe.’”

 


 

USHAURIANO.

 

965.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Irshad-ul-

Qulub…………:

“Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia:

‘Ewe uliye ghafilika ! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe.’”

 

966.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Manhaj-us-Sadiqiin,Tafsiri, J. 2, Uk. 373:

“Iwapo watawala wenu ni watenda wema, na matajiri ni wale wenye kukushukuruni, na mambo yenu yanakwenda kwa ushauriano miongoni mwenu, basi kwenu nyinyi kuishi duniani ni vyema kuliko chini yake. Lakini iwapo watawala wenu ni waovu kwenu nyie, na matajiri ni mabakhili miongoni mwenu, na mambo yenu yanakwenda bila kushauriana, kwa hivyo kwenu nyie kutakuwa afadhali kuwa ndani ya ardhi kuliko kuishi juu yake.”

 

967.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 336:

“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na wenye busara na akili, kwa ajili ya kupata mwangaza ili aweze kupata mwanga katika masuala yake (na ataweza kuona sahihi kile kilicho sawa kutoka na kile kilicho potofu).”

 

968.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 75, Uk. 105:

“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na watu wa maelewano, basi huonyesha maendeleo yake….”

 

969.    Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Nahaj-ul-Falsafa, Uk. 533;

“Hakuna muumin atakaye kuwa mwovu kwa ushauriano, na wala hakuna atakayefaidika kwa ukaidi wake.”

 


 

KUFANYA KAZI NA KUKAA BURE.

 

970.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema At-Tahdhib, J. 6, Uk. 324:

“Ibada imegawanyika katika matawi sabini, na bora ni kule mtu kujitafutia riziki halali.”

 

971.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam Uk. 197:

“Kamwe, Kamwe hakutapatikana raha na starehe za maisha kwa kubakia bila kazi au kuwa mvivu.”

 

972.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 175:

“Jiepusheni uvivu na kutokuridhika. Na haya mawili ndio ufunguo wa kila aina ya maovu.”

 

973.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. aliambiwa na Sa’ad Ansari kuwa mikono yake imekufa ganzi au imekuwa ngozi ngumu ni kwa sababu ya kufanya kazi kwa kutumia kamba na koleo kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kutumia  yeye, mke na watoto wake.

 

   Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. aliibusu mikono yake (akionyesha heshima) na akasema, Usd-ul-Ghabah, J. 2, Uk. 269:

“Kwa hakika huu ndio mkono ambao moto wa Jahannam kamwe hautaugusa.”

 

 


 

SHAHIDI NA SHAHADA.

 

974.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 10, Uk. 100:

“Kuna jema kwa kila jema hadi wakati mtu anapouawa katika njia ya Allah swt na zaidi ya hapo hakuna tena jema lingine juu yake. (Kupigana dhidi ya maadui Waislam ambao wanawaua Waislam)”

 

975.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Furu'i al-Kafi, J. 5,

Uk. 54:

“Yeyote yule anayeuawa katika njia ya Allah swt kama shahidi, basi yeye kamwe hataulizwa chochote kuhusu madhambi yake. (Madhambi yake yote yatakuwa yamesamehewa kwa ujumla).”

 

976.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 149:

“……………. kwa kiapo cha yule ambaye maisha na roho yangu iko mikononi mwake, iwapo viumbe vyote vya duniani na angani vikijumuika pamoja kumuua muumin ambaye hana kosa hata moja au watakapo shawishiwa kufanya hivyo, basi Allah swt atawatia wote kwa pamoja katika moto wa Jahannam.”

 

977.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah, J. 15, Uk. 14:

“Hakuna tone ambalo linalopendwa na Allah swt kuliko tone la damu ya yule, linalomwagika akiwa anakuwa shahidi katika njia ya Allah swt.”

 

 


 

MTARAJIWA AL-MAHDII A.S. NA UTAWALA WAKE WA HAKI.

 

978.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Sunan Abi Daud, J. 4, Uk. 107;

“Al Mahdi anatokana na kizazi changu kutokea kwa wana wa Fatma Bi Zahra a.s.[15]

 

979.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 129:

“Mwenye furaha ni yule ambaye ataweza kumfikia Al-Qaim a.s. wa Ahlul Bayt a.s. na kumfuata kabla ya kudhihiri kwake. Mtu huyu atawapenda wapenzi wa Imam Al Mahdi a.s. na atawachukia maadui wake, na atakubalia uongozi wa Maimam a.s. kabla ya kudhihiri kwake. Na hawa ndio marafiki zangu, na kwa hakika hawa ni watu halisi katika umma wangu ambao mimi ninawatukuza sana.”

 

980.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Musannif, J. 11 Uk. 371:

“Allah swt atamwinua mtu mmoja kutokana na kizazi changu, kutokea Ahlul Bayt a.s.  yangu, kwa kuja kwake ardhi hii itajazwa kwa uadilifu kama vile ilivyojaa sasa hivi kwa dhuluma na kukosekana kwa haki.”

 

981.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 2, Uk. 83 na J. 3, Uk. 446  na J. 4, Uk. 96; Sahih Bukhari, J. 5, Uk. 13 na Sahih Muslim, J. 6, Uk. 21, na No. 1849 ya Riwaya–25 na Marajeo mengine ambayo yameelezwa na Wanazuoni wa Kisunni:

“Mtu yeyote atakayekufa bila kumjua Imam wa Zama zake (Imam wa zama zetu hizi ni Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.) Basi atakuwa amekufa kama vile walivyo kuwa wakifa katika zama za Ujahiliyyah.”

 

982.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 316:

“Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mbingu itanyesha mvua, ardhi itaotesha miti yake, uadui utakwisha kutoka mioyo ya waja (ili kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mapenzi ya kindugu), na wawindaji na wanyama wataendelea kuishi kwa amani kwa pamoja…………”

 

983.  Abil Jarudi amesema, Al-Kafi, J. 1, Uk. 34:

“ Mimi nilimwuliza Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. iwapo yeye alikuwa akijua kuhusu mapenzi yangu na utiifu wangu kwake, naye alinijibu kuwa alikuwa akijua. Nami nikamwambia kuwa nilikuwa na swala nililokuwa nikitaka kumwuliza ili aweze kunijibu, kwa sababu mimi nilikuwa kipofu na nilikua nikitembea kwa uchache sana, na hivyo nilikuwa siwezi kumtembelea kila mara. Naye alinitaka mimi nimwulize swala nililokuwa nikitaka kumwuliza. Hivyo mimi nilimwomba anijulishe dini au madhehebu yeye na Ahlul Bayt a.s. wanayoifuata na ambayo inapendwa na Allah swt, ili nami niweze kufanya ‘ibada ya Allah swt kwa mujibu wa madhehebu hayo.”

 

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alinijibu:

“Kwa hakika wewe umeniuliza swala kubwa sana, ingawaje umeniuliza kwa kifupi sana. Kwa kiapo cha Allah swt mimi ninakujibu kuhusu dini yangu na dini ya mababu zangu kupitia huyo tunavyomwabudu Allah swt. Nayo ni:

‘Kwa kukiri imani yetu kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa ni Allah swt, na kwamba Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. ni Mtume wa Allah swt, na kusadiki kuwa chochote kile kilichomteremkia yeye (Qur'an Tukufu) ni kutoka kwa Allah swt, na kuwa na mapenzi (yetu) ya wapenzi wetu na watiifu kwetu (Ahlul Bayt a.s.) na kuwachukia maadui wetu, kujisalimisha kwa njia yetu, na kumsuburi Al Qaim a.s. (Imam wa kumi na mbili ambaye atadhihiri pale itakapotokea amri ya Allah swt), na kutaka (kudumisha yale yaliyofaradhishwa na mambo yaliyo halalishwa) na kwa kuwa mcha Allah swt halisi (kwa kujiepusha na yale yote ambayo ni haramu).

 

984.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Yaumul-Khalas, Uk. 269:

“Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mikono yake itakuwa juu ya vichwa vya waumini, naye atawapa maendeleo ya kiakili na kukamilisha subira yao na kile wanacho kiangalia mbele. Baada ya hapo Allah swt ataongezea nuru yao macho na uwezo mkubwa wa kusikiliza ili kwamba kamwe kusitokezee vizuizi baina yao na Al Qaim a.s. pale atakapo amua kuongea nao, na watakapomsikiliza, wataweza kumwona ilhali atakuwa mahala pake.”

 

985.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema  Bihar al-Anwaar,

J. 52, Uk. 391:

“Wakati wa Al Qaim a.s. muumin atakaye kuwa mashariki ataweza kumwona muumin mwenzake aliye magharibi, na vivyo hivyo muumin aliye magharibi ataweza kumwona muumini aliye mashariki.

 

Tanbih.

Ndugu msomaji ! Kwa hakika sasa hivi tunayo ala za mawasiliano mbalimbali kama vile Satellite, Television yafuatayo ambayo yanaweza kuwa yenye manufaa makubwa kwetu ili kuwaza kuangalia vyema na kuelewa hiyo riwaya vitu ambavyo havikuwapo wakati maneno matukufu ya riwaya hiyo yalipokuwa yakisemwa.

 

986.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 7:

“Huyu Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. atakuwapo mahala ambapo ni karibu na Al Ka’aba Tukufu baina ya nguzo na nafasi ya kusimamia ya Mtume Ibahim a.s. na atatoa mwito, atakapo kuwa akisema:

‘Enyi watu wangu hasa ambao Allah swt amewawekeni kwa kuwatayarisha nyinyi kwa ya furaha ya kudhihiri kwangu juu ya ardhi hii ! Njooni kwangu kwa utiifu. Na kwa hakika kauli hii itawafikia wale wote watakapokuwa nafasi wanaposalia na hata kama watakuwa vitandani wakiwa mashariki ya ardhi au magharibi yake. Na watamsikiliza kwa mwito wake huo mmoja tu ambayo yatafikia kila sikio la kila mtu, nao watajitayarisha kwa ajili ya kuja kwake. Kwa hakika haitawachukua muda wowote isipokuwa pumzi tu kiasi kidogo kukusanyika hapo baina ya mlingoti na nafasi ya kusimama ya Mtume Mtume Ibahim a.s., wakimwitikia Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.’”

 

987.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia mfuasi wake aliyekuwa halisi, Mufadhdhal, mambo fulani kutokea kisa cha Al Imam Muhammad al-Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. na kudhihiri kwake,

“Ewe Mufadhdhal ! Waambie wafuasi wetu habari za Al-Mahdi ili wasiwe na shaka katika Dini yao.”

Bihar-ul-Anwaar, J. 53, Uk. 6.

 

988.     Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s., amesema Kamal-ud-Din, Uk. 445:

“Mimi ni Al Mahdi na mimi ni yule ambaye bado nipo hai na ambaye nitaijaza ulimwengu kwa haki na uadilifu kama vile ilivyojazwa kwa maovu na dhuluma.

 

Kwa hakika ardhi haitabakia bila ya kuwa na mbashiri, na watu kamwe hawataisha bila ya kuwa na kiongozi. Na hii ni amana na hivyo msiwaambie wote wale Waislam wenzenu isipokuwa wawe ni watu wa Allah swt (wawe katika haki).”

 

989.     Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. amesema, Kamal-ud-Din, Uk. 484:

“Kwa mambo yanayotokea kwa Waislam, murejee katika riwaya zetu, ( yaani Wanazuoni au Ma’ulamaa), kwa sababu wao ndio wawakilishi wangu kwenu na mimi ni Hujjatullah juu yao.”

 

990.     Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. alimwandikia barua Sheikh Al Mufid, Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 175:

“Sisi tunaelewa hali yako na mazingara yako na hakuna jambo lolote lako lililojificha kwetu sisi.”

 

991.     Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. alimwandikia barua Sheikh Al Mufid, Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 175:

“Si kwamba sisi hatukujali wewe au tumekusahau, kwa sababu kama ingekuwa hivyo, matatizo na balaa zingekuwa zimekuondokea wewe na maadui wako wangekuwa wameisha kumaliza. Hivyo, muogope Allah swt na uwe mtiifu kwake, asifiwe Allah Jalli Jalalahu.”

 

 

Dua :

Tunamwomba Allah swt aharakishe kudhihiri kwa Imam wetu wa kumi na mbili Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. ili aweze kudumisha usawa, ukweli, na haki katika ulimwengu mzima.  Amina.

 


 

UMMA WA WAISLAM KATIKA ZAMA ZA MWISHO.

 

992.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Waqayi-ul-Ayyam, Uk. 439:

“Kutakuja zama kutakuja wakati katika zama miongoni mwa watu kuwa:

Wao hawatawaheshimu Wanazuoni wao (yaani Maulamaa) ila kwa mavazi yao mazuri;

wao hawatasikiliza Qur'an Tukufu ila kwa sauti ya kuvutia;

Na wao hawatamwabudu Allah swt isipokuwa katika mwezi wa Ramadhani tu;

 wanawake wao hawatakuwa na aibu,

maskini miongoni mwao hawatakuwa na subira, na

matajiri wao hawatakuwa wakarimu, kwani wao hawataridhirika kwa kidogo na wala hawatakinai kwa wingi.

Wao hawatashiba kwa kingi, wao watafanya kila jitihada kwa ajili ya matumbo yao;

 dini yao itakuwa ni mapesa (mali na utajiri); na

 wake zao ndio watakuwa Qiblah zao (tunapoelekea kusali huko Al-Ka’abah tukufu); na

majumba yao ndio itakuwa Misikiti yao;

wao watakimbia kutoka Maulamaa wao kama vile kondoo anavyo kimbia kutoka kwa mbwa mwitu.

 

Hapo watapokuwa kama hivyo (basi Allah swt atawatumbukiza katika mambo matatu). 

Atawaondolea baraka katika mali zao.

Watatawaliwa na mtawala dhalimu.

Watakufa (kutoka humu duniani) wakiwa hawana imani iliyo halisi.”

 

993.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 23, Uk. 22:

“Utafika wakati katika umma wangu kwamba :

watawala wao watakuwa wakatili na wadhalimu,

Maulamaa na Wanazuoni wao watakuwa waroho wa mali na utajiri na watakuwa na imani kidogo,

waumini wao watakuwa ni wanafiki,

wafanya biashara wao watakuwa wakijishughulisha kwa kutoa na kupokea riba na kuficha maovu na kasoro ya vitu wanavyonunua na kuuza na

wanawake wao watakuwa wamejihusisha mno na mambo ya kujirembesha ya dunia. 

 

Hivyo, wakati huo,

mwovu kuliko wote miongoni mwao ndio watakaokuwa wakiwaongoza wao, na

wema miongoni mwao watakuwa wakiwaita watu lakini hakuna mtu atakaye wajibu.”

 

994.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Ithna-'Asheriyyah, Uk. 202:

“Utafika wakati katika Umma wangu ambapo wao watakuwa wakipenda vitu vitano na kuvisahau vitu vitano:

Wao watakuwa wakiipenda dunia na kuipuuzia Akhera.

Wao watapenda mali na kusahau hesabu ya siku ya Qiyamah

Waume zao watawapenda wanawake waovu na kuwasahau Hur al-‘Ayn

Wao watapenda majumba na watayasahau makaburi yao.

Wao watajipenda wenyewe kupita kiasi na kumsahau muumba wao.

 

Kwa hakika watu kama hawa hawanipendi mimi na mimi pia siwapendi wao.”


 

UMRI WETU TUUTUMIE VYEMA.

 

995.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alimwambia Abu Dhar, Bihar al-Anwaar, J. 77, Uk. 77:

“Ewe Aba Dhar ! Faidi vitu vitano kabla ya vitu vitano:

Ujana kabla ya uzee,

Siha yako kabla ya magonjwa,

Utajiri wako kabla ya umaskini,

Ufaragha wako kabla hujawa mashughuli, na

 maisha yako kabla ya kifo chako.”

 

996.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, 

Uk. 257:

“Itakapofika siku ya Qiyamah,  kikundi cha watu kitasimama na kuja kubisha hodi katika mlango wa Jannat. Nao wataulizwa ni nani wao, nao watajibu: Sisi ni watu wa subira na kwa hayo wataulizwa ni kitu gani walichokifanyia subira, nao watajibu sisi tumefanya subira kwa ajili ya Allah swt dhidi ya kumwasi Allah swt. Kwa hivyo Allah swt atasema kuwa hao ni wasema ukweli na atawaruhusu waingie Jannat. Kwani Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu:

Sura Az-Zumar, 39, Ayah 10:

‘Sema: Enyi waja wangu mlio amini ! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Allah swt  ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.’”

 

997.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 206:

“Aliye na furaha ni yule ambaye hana matamanio na matarajio makubwa katika maisha yake na anafaidi kila fursa anayoipata.”


 

DINI NA KUSOMEA MAMBO YAKE.

 

998.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 1, Uk. 176:

“Ole wake yule Mwislam ambaye habakizi siku moja katika juma zima kwa ajili ya kujifunza masuala ya dini yake na wala kujaribu kufanya uchunguzi na utafiti wa dini yake.”

 

999.     Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 1, Uk. 15:

“Yeyote yule anayesomea dini ya Allah swt, basi kwa hakika ana uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yake na kumpatia yeye riziki kutokea mahala ambapo yeye alikuwa hata hajaweza kuwazia.”

 

1000.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Bihar al-Anwaar,

J. 1, Uk. 214:

“(Vijana wa Kish’ia lazima wawe na program au utaratibu wa kujifunza masuala ya dini). Mimi ninapomwona kijana wa Kishi’a ambaye hana program au utaratibu kama huu basi mimi nitamfundisha somo.”

 

1001.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 29:

“Wajulishe wafuasi wetu kuwa kwa hakika bila shaka wao watakuwa miongoni mwa wale watakao okoka siku ya Qiyamah kwa masharti iwapo wao watakuwa watimizaji wa yale wanayo amrishwa.”

 

1002.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 153:

“Yeyote yule kutokea Ummah wangu atakaye hifdhi ( kariri ) hadithi arobaini ambazo zinahitajiwa na watu katika maisha yao ya kidini (kwa ajili ya Tabligh na muongozo), basi Allah swt atamwinua akiwa hakimu kutoka waliokufa Siku ya Qiyamah.”

 


UPOLE NA MATOKEO YAKE MAZURI

 

1003.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ,Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 373:

“Kwa hakika mja anaweza kujipatia daraja la yule anayefunga saumu katika nyakati za mchana na anayesali usiku kucha, kwa tabia zake nzuri za upole.”

 

1004.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. ,Bihar al-Anwaar, J. 78,

Uk. 111:

“Ewe Mwanangu !

Hakuna utajiri uliona thamani kuliko akili na

hakuna umasikini uliosawa na ujahili;

hakuna ugaidi ulio mbaya kabisa kama kiburi,na

hakuna maisha yenye raha kuliko kuwa mpole.”

 

1005.   Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Khisal-i-Sadduq, Uk. 29:

“Kwa hakika, bora ya bora zote ni tabia njema.”

 

1006.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 71, Uk. 394:

“Tabia njema ipo katika njia tatu:

Kujiepusha na vitu vilivyo haramishwa,

kutafuta yale yaliyo halalishwa, na

kutendea haki wana nyumba wake.”

 

1007.   Al Imam Zaynul 'Abediin a.s., amesema Khisal-i-Sadduq, Uk. 317:

“Kauli njema huongezea mali, utajiri, na riziki, na huahirisha ajali, na hutengeneza mapenzi miongoni mwa wenye nyumba, na humfanya mtu akaingia Jannat.”

 

1008.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 103:

“Yapo mambo matatu ambayo yeyote yule atakayezifikisha kwa Allah swt, basi Allah swt atamfaradhishia Jannat kwa ajili yake:

Kutoa mchango katika umaskini,

desturi nzuri pamoja na watu wote, na

 kujitendea haki nafsi yake.”

 

1009.   Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk, 100:

“Kwa mambo ambayo umma wangu utajipatia Jannat ni hasa kwa mema yote, na desturi nzuri.”

 

 


 

ATHARI MBAYA ZA HASIRA NA TABIA MBAYA.

 

1010.   Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 302:

“Hasira inaiharibu imani kama vile siki(huwa chachu) inavyoharibu asali.”

 

1011.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Ghadhabu ni ufunguo wa kila aina ya shari.”

 

1012.   Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili kutoka kwa mzazi wake a.s. ambaye amenakili kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye Amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 27:

“Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. ili afundishwe tendo ambalo litaondoa kizuizi baina yake na Jannat.

 

Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alimwambia:

Usiwe mkali;

usiwaombe watu vitu,

watakie watu kile ujitakiacho wewe mwenyewe.”

 

1013.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Yeyote yule anayezuia ghadhabu zake, basi Allah swt atazificha siri zake.”

 

1014.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema  Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Ghadhabu ni kitu kinacho teketeza moyo wa hakimu; kwani yeyote yule asiyeweza kudhibiti vyema ghadhabu yake basi kamwe hawezi kuitumia busara yake.”

 

 


 

KUOMBA TAWBA YA Allah swt.

 

1015.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 22 :

“Mjipake manukato ya Istighfar ili hata tone na mabaki ya madhambi yenu yasiwadhalilishe nyie.”  

 

1016.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimfundisha mtu mmoja kwa kumwomba Allah swt dua kwa kumwambia, Bihar al-Anwaar,

J. 94, Uk. 242 :

“Sifa zote ni za Allah swt kwa kila neema; na mimi ninamwomba kila la kheri na kila la wema; na naomba Allah swt aniepushe na kila aina ya shari; na ninamwomba Allah swt msamaha kwa madhambi yote.”

 

1017.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa, Khisal-i-Sadduq, Uk. 317:

“Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. aliulizwa kuwa bora wa waja ni nani, naye alijibu:    Wao ni:

  • Wanapofanya mema wanafurahia hayo; 
  • wanapofanya mabaya basi wanaomba Tawba na Istighfar ; 
  • wanapojaaliwa chochote wanashukuru; 
  • wanapokuwa katika hali ngumu, wanaonyesha subira; 
  • wao wanapo mghadhabikia mtu, humsamehe.”

 

1018.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Makarim-ul-Akhlaq, Uk. 313:

“Anapozidisha muumin Mwislam kwa kuomba Istighfar ya Allah swt, basi rikodi ya matendo yake mema yataongezeka na yatakuwa yaking’ara.”

 

 


 

SALAA YA JAMA’A.

 

1019.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 4:

“Allah swt huheshimu sana yule mja anayesali sala kwa Jama’a na baada yake anapoomba kitu chochote basi Allah swt lazima humtimizia.”

 

1020.   Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 88, Uk. 4 na Wasa'il ush-Shi'ah, J. 8, Uk. 290:

“Fadhila za sala ya Jama’a kwa sala ya mtu anayesali peke yake ni kila raka’a moja katika Jama’a ni bora kuliko raka’a elfu moja (1000) zinazosaliwa na mtu peke yake.”

 

1021.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 6, Uk. 446:

“Sala moja ya mtu katika Jama’a ni bora kuliko sala za miaka arobaini anazosali akiwa nyumbani kwake (peke yake).”

 

1022.   Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 6:

“Safu ya mistari katika sala ya Jama’a inayosaliwa juu ya ardhi ni sawa na safu za Malaika huko mbinguni; na Raka’a moja inayosaliwa katika Jama’a ni sawa na Raka’a ishirini na nne na kila raka’a moja inayosaliwa na wapenzi wa Allah swt kuliko sala za miaka arobaini. Hivyo, siku ya Qiyamah ambayo ni siku ya uadilifu wakati Allah swt atakapo wakutanisha wanaadamu wote kuanzia mwanzoni hadi mwisho, basi hakutabakia na muumin yeyote ambaye amesali sala ya Jama’a, kwamba Allah swt atampunguzia shida zake za siku ya Qiyamah na ataambiwa aingie Jannat.”

 

1023.   Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. siku moja aliijiwa na Kipofu mmoja ambaye alisema, At-Tahdhib, J. 3, Uk. 266:

“Kulikuwa hakuna mtu yeyote wa kumchukua Msikitini ili aweze kushiriki katika sala ya Jama’a pamoja na Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. pale aliposikia Adhana ikitolewa.

 

Hapo Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. alimwambia:

“Funga kamba kutoka nyumbani kwako hadi Msikitini na ushiriki katika sala ya Jama’a.”

 

1024.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 11:

“Mtu yeyote ambaye anaiacha sala ya Jama’a bila ya kuwa na Udhuri inayokubalika bali bila sababu yoyote, kwa misingi ya kutotaka kushiriki katika mkusanyiko wa Waislam, basi atakuwa hana Sala yoyote.”

 

1025.   Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 12:

“Kwa hakika sala ya Jama’a imefaradhishwa ili kuwepo imani halisi katika umoja, katika Islam, na katika kumwabudu Allah swt kiwazi wazina ambayo imedhihirishwa kuwa bayana, kwa sababu, ili iweze kuwadhihirikia watu wa mashariki na wa magharibi (wa dunia hii).

 

Hivyo ukweli na asili wa Uislam utadhihirika na kujulikana na makafiri na mapagani kabla ya Uislam utakuwa ni kama kiza mbele ya nuru, kiza ambacho hatimaye kinapotea.

 

Vile vile sala ya Jama’a husababisha watu kutambuana na kuelewana na inawezekana wengine wakawa mashahidi kuhusu wengineo kuhusu Uislam wao, ambamo kuna uwezekano na vile vile kushirikiana katika mambo mema na ya kumfurahisha Allah swt mambo ambayo yanawazuia wasimuasi Allah swt kupita kiasi.”

 


NEEMA NNE ZA ALLAH swt

 

1026.   Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema kuwa kila asubuhi, kila Mwislamu anatakiwa azikumbuke neema nne za Allah swt.  Hofu yangu ni kwamba asipozikumbuka, kuna hatari ya kuzipoteza neema hizo:

·         Namshukuru Allah swt ambaye amenisaidia kumtambua Yeye na hakuuacha moyo wangu gizani.

·         Namshukuru Allah swt ambaye ameniweka pamoja na wafuasi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

·         Namshukuru Allah swt ambaye ameiweka riziki yangu kwake Yeye na si mikononi  mwa watu.

·         Namshukuru Allah swt ambaye amezifunika dhambi zangu na aibu zangu na hakunidhalilisha mbele ya watu.

 

1027.  Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.,Nur al-Absaar

Shablanji.

“Mwovu wa watu ni yule anayewawekea pingamizi na anakuwa mkali kwa watu wake wa nyumbani.”

 

1028.   Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu :

“Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate vyayo za Shaytani;  kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri.”

 


SIFA ZA KUPENDEZA ZA MWANAMKE

 

1029.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il

ush-Shi'ah,Vo. 20, Uk.172

“Malipo ya mwanamke mcha Allah swt kwa kumpa mume wake bilauri moja ya maji ni zaidi ya kufanya ibada mwaka mzima ambamo mchana anafunga saumu na usiku zake anakesha katika kufanya ibada.”

 

1030.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi, J.5,

Uk. 508:

“Ni kwa mwanamke kujiweka msafi kabisa kwa kujipaka manukato bora kabisa na kuvaa mapambo ambayo yatamfanya yeye amvutie bwana wake na ajiweke tayari kwa ajili ya bwana wake usiku na mchana.” [16]

 

1031. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha,

Msemo 494:

“Jihadi ya mwanamke (vita katika njia ya Allah swt ) ni kuwa na uhusiano mwema na kuwa mshiriki wa bwana wake.”

 

1032. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Usuli kafi, J. 5,

Uk. 327

“Iwapo ningetaka kukusanya mema yote ya dunia hii na Aakhera kwa ajili ya Mumin basi mimi ningeziweka kwa ajili ya

moyo mnyenyekevu,

 ulimi wenye shukurani na isemayo mema,

mwili ufanyao subira wakati wa shida na dhiki.

 

(Kwa ajili ya mwanamme Mimi ningempa) Mke mcha-Allah swt ili anapouona uso wake anajawa na furaha na yeye (mwanamke) anaihifadhi na kulinda mali yake, pale bwana wake anapokuwa hayupo.”

 

1033. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J.103, Uk. 252

“Amelaaniwa! Amelaaniwa kabisa mwanamke yule ambaye anautonesha moyo wa mume wake na kumfanya akasirike.

 

Lakini amebahatika kabisa mwanamke yule ambaye anamheshimu bwana wake wala hamghadhabishi na huwa mtiifu kwa bwana wake.”

 

1034.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema Bihar al-Anwaar,

J.103, Uk. 235

“Bora ya mwanamke ni yule anayezaa, mvutiaji kimapenzi, mtunza siri zenu, na mcha-Allah swt. Na humtii bwana wake na hupendwa na Jama’a na ndugu zake. Pale anapokuwa pamoja na bwana wake, anamwonyesha urembo na mavazi yake ambayo kwa hakika huyaficha kwa ajili ya wanaume wengine isipokuwa mume wake tu.

 

Kwa hakika huwa msikivu na mnyenyekevu kwa mazungumzo yake na huzitii amri zake. Pale anapokuwa faragha anavaa vizuri kabisa na kutimiza mahitaji ya bwana wake kutoka kwake. Daima huwa anakuwa amevaa vizuri na kujirembesha kwa ajili ya bwana wake tu na kamwe huwa si mtu aliyejisahau kwa ajili ya bwana wake            ( hujiweka tayari kwa ajili ya bwana wake.).”

 

1035. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar,

J.104, Uk. 98:

“Kutokea kwa furaha ya mwanamme Mwislamu ni kwamba

ana mke mcha-Allah swt na

nyumba kubwa ya kukidhi wananyumba,

 usafiri mzuri na

watoto wema.”

 

1036.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema

“Vita vya Jihad kwa ajili ya mwanamke ni kuwa na uhusiano na kuwa mwema kwa mume wake na haki za mwanamme kwa mke wake ni zaidi ya haki za wote juu yake.”


1037.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu Surah Al-Baqara, 2,

Ayah ya 231:

Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao,  basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Allah swt kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Allah swt juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anachokuonyeni kwacho. Na mcheni Allah swt , na jueni kwamba hakika Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.

 

1038. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah,

J.22, uk.9:

“Muoe na wala msitoe talaqa kwa sababu ‘Arshi Ilahi hutetemeka kwa talaka.”

 

1039.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema  Al-Kafi, J. 6, Uk. 54

“Allah swt hufurahishwa mno kwa nyumba ile ambamo harusi huwapo na hughadhabishwa kwa nyumba ile ambamo huwa na talaka. Na hakuna kinachomkerehesha Allah swt kama talaka.”

 

 


 

SEMI ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

 

 

UADILIFU.

 

1040.  Taji la mfalme ni uadilifu wake mwenyewe.

1041.  Utatawala iwapo nawe utakuwa mwadilifu.

1042.  Uadilifu huangamiza ulafi , uroho na tamaa.

1043. Ngome ya Utukufu (ya Allah swt) huikinga nchi yenye mtawala mwadilifu.

 

SHURUTISHO NA SHARI

 

1044.  Kulazimisha/Kushurutisha kunaifanya akili iwe kipofu.

1045.  Shari kunamfanya mtu awe mwoga wa uadilifu (ataiongopea)

1046.  Uchokozi ni hatua ya kukaribia maangamizi.

1047.  Kinachodhulumu haki ni kule kusaidia vilivyo batilifu.

1048.  Udhalimu kwa mwenye dhiki ni dhuluma kubwa kuliko zote zile.

1049.  Allah swt huharakisha kuanguka kwa wachokozi.

1050.  Ushidi wa mshari ni kushindwa kwa nafsi yake.

1051.   Kustarehe humu duniani kwa fidia ya akhera ni kujidhulumu nafsi yako.

1052.   Kuwakandamiza yatima na wajane kunaleta magonjwa na kupotea kwa ne’ema.

 

 

ULIMI NA USEMI:

 

1053.  Mtu amehifadhika chini ya ulimi wake.

1054.  Ulimi mtamu/mzuri hupata marafiki wengi.

1055. Ulimi wako utasema kile kilichozoeshwa. (Kwa hivyo jihadhari kabla ya kusema).

1056.   Akili ni busara. Akili ya mpumbavu ipo chini ya ulimi  wake(anasema kabla ya kufikiri).

1057.  Ulimi ni mkalimani wa akili.

1058.  Ulimi wa mtu ni uzani wake mwenyewe.

1059.  Ulimi unaathari za kuchoma zaidi ya mkuki.

1060.  Usemi wa kweli ni ulimi mtukufu.

1061.  Jihadhari na ulimi, kwani ni sawa na mshale unaoweza kufyatuka  kutoka upinde.

1062.   Mtu bila kusema (ulimi useme mema na kukataza mabaya) ni ama sanamu au mnyama.

1063. Ulimi  wa mwenye busara ipo akilini mwake (huongea na akili yake na hufikiria zaidi na kusema kwa uchache kwani ni yenye manufaa).

1064.  Kuujaribu (kucheki) ulimi ni afadhali kuliko kulitazama tumbo.

1065.  Yeyote yule asiye uhifadhi ulimi wake basi ataujutia mbeleni.

 


UKIMYA NA KUSEMA.

 

1066.   Kila vile busara ya mtu iongezekavyo ndivyo vivyo hivyo maneno yake hupunguavyo.

1067.  Ukimya ni majibu ya maswali mengi sana.

1068.  Ukimya ni jibu bora kabisa kwa mpumbavu.

1069.  Mazungumzo bora ni yale yaliyo mafupi na yenye manufaa.

1070.  Bora ya misemo ni ile iliyochujwa na kuhakikishwa.

1071.  Ukae kimya ili ukae salama.

1072.  Kusema kupita kiasi kunamdharaulisha mtu.

1073.  Urefu wa mazungumzo huidhoofisha hotuba.

1074.   Hotuba ni kama dawa; kiasi kidogo kinaponya na kwa kuzidi kiasi kunaweza kumwua mgonjwa.

1075. Usimpuuzie yule asemaye bali wewe uyatilie maanani yale ayasemayo.

1076.  Kusema kidogo ndivyo kukosolwa kidogo.

 


KIFO (MAUTI).

 

1077.  Watu wako wamelala hali wako hai na huwa macho baada tu ya kufa.

1078. kujielekeza kwa mabaki ya matamanio ya mtu ndiko kujiuwa  haraka.

1079.  Ufe kabla ya kifo kukuijia.

1080.  Mauti inaidhihaki tamaa.

1081.   Mauti ni kutenganisha toka kitakachoisha na kuelekea kule pasipokwisha.

1082. Kuikumbuka mauti kila mara kutampunguzia mtu tamaa za duniani.

1083.  Wale watembeao juu ya ardhi siku moja watazikwamo.

1084.  Tamaa hukuongoza katika njia ya upotofu.

1085.  Wakati hatuna matumaini huwa hatuhuzuniki.

1086.  Kufadhaika huwa pamoja na tamaa.

1087.  Kinachoipatia madhara na hasara dini ni tamaa.

1088.  Waroho ni watumwa wa matilaba yao.

1089.  Kutokuwa na mategemeo kunaituliza na kuipumzisha roho.

1090.  Uroho huuangamiza uadilifu

1091.   Ubinadamu ni wa aina mbili; wale wenye matamanio matupu na   wale watakao kuja kuwa wasioridhika.

1092.  Tamaa huingamiza hadhi ya mtu bila ya kuongezeka kwa bahati   yake.

1093.  Hata kama wakiwa uchi na wenye njaa, hao walioridhika huwa ni  wenye furaha.

1094.  Kuridhika ni hazina isiyo na kifani.

1095.  Kuridhika ni hadhi na heshima isiyodidimia milele.

1096.  Mwenye kuridhika tu ndiye aishiee kwa amani na usalama.

 


USTAHIMILIVU, UVUMILIVU NA UTULIVU.

 

1097. Kutokuwa na saburi ya akili ni yenye madhara kuliko ustahimilivu.

1098.  Chifu ya sababu ya Islam ni utulivu kwa Allah swt

1099.  Ustahimilivu ni matunda ya Imani.

1100.  Ujue kuwa utulivu ni hatua ya awali katika dini halisi na uaminifu ni mwili

1101.  Kwa ustahimilivu, bahati mbaya huwa sivyo tena bahati mbaya.

1102. Ule uwezo wa uvumilivu wa ghadhabu (hasira) ni bora kuliko kuchukua kisasi.

 


MALI (UTAJIRI).

 

1103.  Mapenzi ya mali inachochea tamaa na kuharibu wema.

1104.  Usia unawafariji warithi

1105.  Mali ni chanzo cha hamaki.

1106.  Bora ya akiba ni pale ambapo kazi zinatawanywa vyema.

1107. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo anapotengana nayo.

 

AKILI NA UPUMBAVU.

 

1108.  Uadui ni kazi ya wapumbavu.

1109.  Dhana ya mwenye akili ni mafumbo.

1110. Kwa kumtii Allah swt ni sawa kwa hisa ya akili na hekima ya mtu.

1111.  Kupigana vita dhidi ya matakwa yake mtu ni jihad kubwa kabisa.

1112.  Sababu ya busara na akili ni kukubalia ujinga wake mwenyewe.

1113.  Mwerevu hulenga pale na thabiti.

1114.  Mpumbavu hulenga pale penye mali.

1115.  Dhana ya mtu inategemea akili yake ilivyo.

1116. Dhana ya mwenye busara na hekima ni sahihi kabisa kuliko  kithibitisho cha mpumbavu

1117. Kwa kujitenganisha na vitu vya muda na kujiweka tayari kwa maisha ya kudumu ndiko kunako busara na hekima hisa kubwa.

1118.   Mtu huyo ni mwenye busara ambaye matendo yake yanathibitisha  yaliyoyasema.

1119. Mtu mwenye busara hasemi ila pale penye dharura au penye sababu.

1120. Kila mtu aliye mwenye busara na hekima huwa yuko masikitikoni.

1121.  Mwenye busara ni mwenye faida hata kama akiwa katika hali gani ile.

1122.  Kujihusisha na wapumbavu  ni kuitesa Roho.

1123.  Mpumbavu yupo peke yake hata kama akiwa katika jamii.

1124. Kutoka kupata hekima (matakwa yake) hayawezi kufidiwa na fedha.

1125.  Hakuna ugojwa ulio mbaya kabisa kuliko kutokwa kwa hekima.

 

UWEMA NA MATENDO MEMA.

 

1126.  Kwa uwema mtu anaweza kumteka mtu aliye huru.

1127.  Wema haufi kamwe.

1128.  Kazi iliyo bora zote ni kujijumuisha pamoja na walio wema.

1129.  Kuwa mwema kwa mema ni uwema na hii ndiyo fahamu ya mtu ya hali ya juu.

1130.  Thamani ya mtu inategemea uzani wa uadilifu wake.

1131.  Angukia ndani kwa wema na uangukie nje kwa matakwa.

 

TAMAA

 

1132. Mapenzi ya mali (utajiri) yanachochea tamaa na kuupoteza uwema.

1133.  Tamaa haielewi mipaka yake.

1134.  Kuwa na imani ya Allah swt ni jitihada iliyo bora kabisa.

1135. Tamaa iliyo kuuu kabisa ya wanyama ni kule kushibisha tumbo lao wenyewe.

1136. Tamaa iliyo kuu ya wanyama porini kule kuwanyanyasa wengineo.

1137.  Tamaa kuu ya mwanamke ni kuivutia dunia kwake na kuchochea fujo humo.

1138. Jitihada kuu kabisa ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.humu duniani ni kuiongoza dunia.

1139.  Tamaa yako iwe ni ile kwa ajili ya akhera na hapo utajirekebisha.

1140.  Thamani ya mtu inategemea utukufu wa jitihada zake.

1141.  Ukuu na ufahari wa mtu unategemea utukufu wa jitihada zake na wala sio pale penye kuozapo mifupa ya mababu zetu.

 

REHEHMA NA MSAMAHA:

 

1142.  Kusamehe ni taji la ukubwa na fahari.

1143.  Rehema inaitukuza nguvu.

1144. Itakuwa ni vyema iwapo rehema itashirikishwa pamoja na ukubwa.

1145. Itakuwa ni adhabu kubwa itakayotolewa mbali na kuombwa   msamaha.

1146.  Unyenyekevu inatangaza ukubwa.

1147.  Unyenyekevu ni matunda ya elimu na hekima.

1148. Unyenyekevu bila ya kutazama panapostahili ni sawa na huna uwezo.

1149.  Majivuno huangamiza na kumharibia sifa mtu.

1150.  Kwa kuwa na majivuno au kiburi ni sawa na kuipa akili sumu.

1151.  Kiburi hukandamiza mwenendo wa maendeleo.

1152.  Majivuno huua na kuudhalilisha ukubwa.

1153.  Unyenyekevu ni sawa na wavu uliotandwa kwa ukubwa.

1154.   Kujivuna na kule kujideka ni matokeo ya wale wenye akili kasoro.

 

ULIMWENGU:

 

1155.  Ulimwengu huu ni sawa na daraja ituvushayo kwenda akhera.

1156.  Dunia hii ni sawa na duka la maovu.

1157.  Mapenzi ya dunia ni chanzo (mizizi) cha matatizo na maovu yote.

1158.  Ufahari wa wapumbavu na walio wajinga ni mapenzi ya dunia.

1159.  Dunia ni chungu mno zaidi kuliko ule utamu wake ulio nao.

1160.  Kuipatia dunia hii talaka ni sawa na kupanga harusi na Akhera.

1161.  Dunia hii ni sumu na wale wailao sumu ni majahili.

1162. Uishi kwa kiwiliwili chako humu duniani na uifanyishe kazi nafsi(imani) yako kwa ajili ya akhera.

 

WATU

 

1163. Watu ni zaidi ya vile walivyokuwa awali na huishi zaidi ya walivyokuwa wakiishi mababu zao.

1164. Mtu aliye jasiri kuliko wengine ,atulizaye matamanio yake (subira).

1165.  Itakuwa ni jambo la upuuzi iwapo nafsi itakuwa imedhoofika hali mwili wa mtu bado ana siha nzuri na iliyo njema.

1166.  Yule aijuaye na kuelewa ubinadamu huchagua upweke.

1167.  Yule ampandae Allah swt hupigana na aibu za watu.

1168.  Yeyote yule asiyejifikiria na kujithamini mwenyewe basi amepotoka.

 


MATAKWA YA SUBIRA

 

1169. Hekima iliyo kuu kabisa ni kule kupingana na matakwa na matamanio ya mtu.

1170.  Atakuwa ni mtu mwenye furaha kuu iwapo ataishinda nafsi yake mwenyewe.

1171.  Adui wa kupindukia wa mtu ni yale matakwa yake.

1172.  Vita vilivyo bora kuliko vyote ni vile vita dhidi ya nafsi ya mtu.

1173. Ulafi wa sehemu zetu za siri ndizo nyavu zilizo tegwa na Shaytani.

 


MADHAMBI.

 

1174. Kuishi kwako hapa (mbali na utukufu) na dhambi lisiloweza  kusamehewa.

1175. Usiogopeshwe na chochote kile isipokuwa madhambi yako mwenyewe.

1176.  Madhambi yanaharibu ibada ya Allah swt.

1177.  Uharibifu ni matunda ya madhambi.

1178.  Madhambi yanampotezea mtu utukufu wake.

1179.  Kujiepusha na madhambi ni afadhali kuliko kutenda mema .

1180.  Kutenda madhambi ni ugonjwa na dawa yake ni kujiepusha nayo na kufanya tawaba

 


MAFUNZO YA TAHADHARI.

 

1181.  Kila mtazamo wako wa fahamu ni fundisho kwako

1182.  Walio kufa wamewachia mafunzo kwa ajili ya walio hai.

1183. Nijia walizozipitia wale waliokufa na waliotutangulia ni zenye kutufunza na kututahadharisha sisi tuzifuatazo.

1184.  Uhakika wa mambo ni mkufunzi wa kutosha kabisa.

1185.  Umri mkubwa ni mkufunzi aliye bora kabisa .

 

SHAURI

1186.  Kutoa onyo la upole katika umati wa watu ni jambo lililo bure.

1187. Mtoa mashauri asiye na uwema ni sawa na vile upinde  unavyokuwa bila uzi.

1188.  Mshauri aliye bora kuliko wengine ni yule akuelezeaye makosa na dosari zako.

 

UAMINIFU,UADILIFU

 

1189.  Ulimi mtukufu ni ule ulio adilifu.

1190. Kwa kutimiza ahadi ni mfano ulio bora kabisa wa uaminifu na uadilfu.

1191. Ukweli ina maana ya kwamba ulinganifu wa matamko kwa mujibu ya maamrisho ya Allah swt  atakavyo.

 


UDANGANYIFU NA KHIANA

 

1192.  Urafiki haupo kamwe katika uongo.

1193.  Kwa kubadilisha maana halisi ya jambo kuna haribu asili yake.

1194.  Kusema uongo kunaharibu habari.

1195.  Kusema uongo panapostahili,kutamlindia heshima za mtu.

1196.  Kusema uongo na unafiki kunadhalilisha nidhamu na heshima ya mtu.

 

 


UKIASI NA UFUJAJI.

 

1197.  Aliyebarikiwa ni yule ambaye anaelewaye vyema thamani yake na asiyevuka mipaka.

1198.  Kwa kupima kiasi ni nusu ya hifadhi.

1199.  Ufujaji unapotea kabla ya njaa.

1200.  Ufujaji unapoteza uwema na sadaka.

1201.  Tamaa ya mali kunaharibu ukiasi alionao mtu.

1202.  Kiasi kwa uangalifu kinabakia zaidi ya kile kilicho fujwa.

1203.  Hakuna ufahari katika ufujaji.

1204.  Kupima kiasi ni njia ya usalama na ya amani.

 


UWEMA ( HISANI )

 

1205.  Heshima na ukukuzi hauwezi kamwe kulinganiswa na ubaya,sio yenye wema.

1206.  Mwenendo wa mtu ni diraja ya akili yake.

1207.  Urithi ulio bora kabisa ni uungwana wa mtu.

1208.  Hakuna chochote kile chenye thamani dhidi ya uungwana.

 


KUWAHESHIMU WAZAZI

 

1209.  Kuwatazama wazazi ni fardhi iliyo kuu kabisa.

1210. Kuwatunza na kuwastahi wazazi wako (kuwalea) na malezi ya watoto wako, ndiyo yatakayo kulea wewe na kukustahi.

 


PUPA

1211.  Hakuna ushindi uliopo katika pupa.

1212.  Lawama huwa ni daima kwa yeyote aendeleae kwa pupa

 


HUSUDA

1213.  Husuda humwibia mtu raha zake.

1214.  Silaha ya husuda ni malalamiko na mapingamizi.

1215.  Husuda huitafuna uwema kama vile moto iharibuavyo mbao.

 


KAZI

1216.  Matendo ndiyo matokeo ya nia.

1217. Uwemwaminifu katika kazi zako, kwami majaribio ya Allah swt  yako macho sana juu yako.

1218.  Siku ya mwisho ni siku ya Qiyamah na wala si siku ya kufanya kazi.

1219.  Shauku ya uaminifu ni uharibifu mambo mema.

1220.  Upande ulio mgumu wa tendo, ni kuhifadhi utukufu wa jambo.

1221.  Bila ya uaminifu , kazi zote hazitakuwa na thamani yeyote ile.

1222. Itakuwa ni wema iwapo mambo mema yawe rafiki yako na matilaba, adui yako.

1223.  Elimu kiasi kidogo huharibu mienendo na tabia.

1224.  Kazi nyingi zenye tamaa, zitaharibu zingine zote.

1225. Hakuna aheshimiwaye zaidi kuliko wengine ila ni yule mwenye kufanya ibada.

1226.  Hakuna usalama ulio bora kuliko ibada .

1227.  Kumtii Allah swt ni sehemu ya busara ya mtu.

1228.  Ibadi ni pahala palipobora pa kujihifadhia.

1229.  Ibada ni mahala palipo bora pa kujihifadia.

1230.  Kujionesha au kujidai kunaharibu na pia kuighasi ibada.

 

 


KUFANYA GHIBA.

 

1231.  Hakuna uwema au uamnifu katika kufanya ghiba.

1232.   Yeyote yule asikilizaye ghiba basi ndiye mfanya ghiba mwenyewe.

1233.   Yeyote yule awasemae wengineo kwako, ndivyo vivyo hivyo ujue wazi wazi kuwa ndivyo akusemaye wewe kwa wengineo.

 


KUCHEKA

1234. Kucheka kwa wastani (bila kutoa sauti) ni mcheko ulio bora kuliko vyote.

1235.  Kucheka kwa kupita kiasi kutamharibia mtu heshima yake.

1236.  Kucheka kwa kupita kiasi kunaiuwa bongo.

 


SIFA

1237.  Majivuno yanadhihaki sifa na pia kuiharibu.

1238.  Uwema na ukarimu kunavuna sifa njema.

1239.  Yeyote yule akusifuaye ndiye akuuae.

 


MISEMO.

 

1240.  Utakatifu huambatana na busara.

1241.  Kutoridhika  kwa mtu kutamfutia utulivu.

1242. Saumu ya akili ni kuiepusha kutoka matamanio yote yaliyo maovu.

1243.  Uoga ni kutokana na moyo uliodhoofika na usio na uimara.

1244.  Vitu vinavyotuharibu sisi ni karibu tu tutakavyo ungana navyo.

1245.  Kufuatilia mateso na matatizo yamkabiliayo mtu, yanadhihirisha ukubwa wake na ustahimilivu na uwema wake.

1246.  Yeyote asemaye maneno na misemo ya wale wenye busara, basi ndivyo anavyojivisha utukufu wao.

1247.  Maisha marefu hukutana na matatizo mengi.

1248.  Ardhi ni msafishaji bora.

1249.  Makabiliano ndiyo yanayomsaidia sana mtu.

1250.  Ukweli na mabishano ndiyo yaliyo bora kabisa.

1251.  Mtu ajigambaye basi ndiye ajidhalilishaye yeye nafsi yake.

1252.  Mtu mwenye mafanikio bora kabisa.

1253.  Yeyote yule mwenye kuhofu ndiye abakiaye salama.

1254. Tajiri hasemwi kwa kuongezeka kwa uwema na kuiendeleza subira.

1255.  Uso wenye mcheko (mcheshi) huuepusha kutoka moto wa uadui.

1256.   Kwa kukatalia zawadi ndiko kunamaanisha kutokuwa na shukrani.

1257. Hakuna chochote mbali na kule kufanya Tawbah ila ni kujipunguzia ule mwenendo unaofutilia.

1258.   Usiligeuze tumbo lako likawa ni kaburi la wanyama.

1259.   Ugonjwa ni moja wapo ya aina mbili za kifungo.

1260.   Kuzuzuliwa kwa ghadhabu ni dhambi pia.

1261.  Ndugu huongezea na kufurahikia furaha zetu na hutuondolea na kutuponya yale maumivu tuliyonayo.

1262.  Ubongo (akili) huwa ni mfano wa ghala (stoo) ambayo ilifungwa kabisa na maswali tu ndio zifunguazo kutoka humo.

1263.  Hata kama pazia itaondolewa mbele yangu ,basi hakuna chochote kile kitachoongezeka katika imani yangu.

1264.   Pale Allah swt ampendeleapo Mja wake yeyote,Yeye humshugulisha katika mapenzi yake.

1265.  Nywele za kijivu huelezea kuwa ni hatua ya kuikaribia mauti

 


BAADHI YA DUA’ ZA IMAM ALI (A.S.)

 

1265.  Ewe Allah swt,mbariki yule ambaye hazina yake kuu ni imani na silaha zake ni machozi.

1266.  Ewe Allah swt, wewe ni mkuu kabisa kwa kumwangamiza yule  ambaye umeshakwisha kumtukuza hapo awali.

1267.  Sala ni silaha ya mumini.

1268.   Je kuna yeyote yule ambaye anaelewa vyema uwezo wa Allah swt na tena asimwogope Allah  swt?

1269.  Je kuna yeyote akuelewaye vile wewe ulivyo na tena asiwe na khofu yako?

1270. Ewe Allah swt, ngozi hii yangu hafifu, haitaweza kustahimili moto mkali wa Jahannam.

1271. Mishale yote hailengi penye kuheshimiwa na kwa kupatwa na shida na majaribio.

1272. Ewe muumba ,wewe upo pekee mwenye kuheshimiwa na mwenye kudumu daima milele na umelazimishia viumbe vyako kwa kifo na kwa kupatwa na shida na majaribio.

1273.   Ewe muumba, nisamehee madhambi yangu pasipo mimi kujua kwangu .

1274.   Ewe mola , unisamehe madhambi yangu yale ambayo yanayoweza kuniteremshia juu yangu laana na adhabu na ghadhabu zako.

1275.  Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale yanayoweza kuwa sababu ya kuharibu na kuzighasi zile baraka zako zilizo juu yangu.

1276.  Ewe mola, nisamehe madhambi yangu ambayo ndiyo yanayozuia na kuzipoteza ibada zangu kabla ya kukufikia wewe.

1277. Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale ambayo inanikatiza mimi katika imani yangu.

1278. Ewe mola, mimi nakukaribia wewe kupitia kwa kukukumbuka  wewe .

1279. Ewe mola, mimi nakuomba wewe uniweke furaha na niwe nimeridhika na yale  wewe uliyonijaalia maishani mwangu na katika bahati yangu  (kwa ajili yangu).

1280. Ewe mola wewe ni mwepesi  sana wa kubariki na kurehemu, msamehe yule ambaye hana chochote ila ni ibada na sala zako tu. 

1281. Ewe Allah swt !, Je wewe utauachilia Moto uzikumbe nyuso ambazo ziko zimeangukia mbele yako kwa unyenyekevu?

1282.   Ewe Allah  swt, zipatie nguvu mikono na miguu katika kutekeleza wajibu na huduma katika kazi zako.

1283.   Na uzipatie nguvu mbavu zangu ili nipate hali ya kukufikia wewe.

 


 

DUA.

 

1284.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Bihar al-Anwaar, J. 91, Uk.6:

“Ewe Mola wetu sisi kwa hamu kubwa utujaalie haki, Serikali ya Kiislam, (ambayo kwa hakika ipo uadilifu serikali ya Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s., tunamwomba Allah swt atuharakishie kudhihiri kwake). Kwa kupitia hii serikali takatifu, uihamasishe na kuipenda Islam na wafuasi wake ambao na papo hapo kuwadhalilisha unafiki na wanafiki.  Na, katika kipindi hicho utuweke sisi miongoni mwa wale watu wanaowaita wengine katika utiifu wako na kuwaongoza katika njia yako utukufu; na, utujaalie heshima na ukuu katika dunia hii na Akhera.

 

Aamin Ya Rabbal ‘Alamiin.


 

 

1285.  Kuna aina nne ya watu:

  • Wale wanaokula na kuwalisha wengine
  • Wale wanaokula na kuwanyima wengine
  • Wale hawali wenyewe na wala hawawapi wengine wale
  • Wale wanaowanyan’ganya wengine ili wale peke yao

 

1286.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa:

“Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

 

1287.  Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Moyo ulio msafi- halisi ni ule  ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt  tu”

 

1288.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa:

“Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake.”

 

1289.  Allah swt abatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

“Na anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt).” (50:33)

 

1290. Qur’an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11,  inatuambia:

“ Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye anayemwamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu”

 

1291.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Ar-Raa’d, 13, Ayah 28:

“Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia.”

 

1292.  Na vile vile mwishoni mwa Surah al-Fajr, 89, Ayah 28 twaabiwa

“Ewe nafsi yenye kutua”!

“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika, na umemridhisha.”

 

1293.  Allah wt amesema katika Qur'an,Surah, Hajj , 22 , Ayah 32:

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayeziheshimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.

 

1294.  Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 54:

“Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao. Na hakika Allah swt ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka.”

 

1295. Allah wt amesema katika Qur'an, Surah, Ash-Shams, 91,   Ayah 9-10:

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)”  Qur’an Tukufu Tukufu inatuelezea:

 

Qur’an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1 – 2:

“Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”.

 

1296.  Twaambiwa katika Qur’an Tukufu Surah, Ash-Shams, 91,   Ayah 8:

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake” 

 

1297.     Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283,  inazungumzia kulipa kwa amana:

“Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia dhambini.”

 

1298.  Anaelezea Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

“Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka.”

 

1299.  Allah swt katika Quran: :

“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

 

1300.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46:

“Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka.

 

1301.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi.”

 

1302.   Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Al I’mran, 3, Ayah 7:

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi........”

 

1303.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13:

“Kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache na miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt hawapenda wafanyao wema.”

 

1304.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah, Al H’adiid, 57, Ayah 16:

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa  Kwa hivyo nyoyo zao zikiwa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.”

 

1305.  Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah At Tawba, 9, Ayah 45:

“Nyoyo zao zina shaka; kwa hivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao.”

 

1306.   Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Mut'ffifiin, 83, Ayah 14:

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.”

 

1307.  Twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa:

“Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Allah swt’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

 

1308.  Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53  kuhusu Mtume Yussuf a.s., inazungumziwa Nafsi :

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu”

 

Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Yusuf, 12, Ayah 53: 

 

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu”

 

1309.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2,

       uk.330

“Zipo aina tatu za dhuluma:

  • Kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya
  • pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya
  • tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi.”

 

 


 


ZAKA

 

1310.  Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al –Tawbah, Ayah

34 – 35 :

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya.

 

1311.  Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran, 3 , Ayah 180 :

Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Allah swt katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao. La ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyoyafanyia ubakhili – Siku ya Qiyamah.

 

1312.  Imeandikwa katika Minhaj-us-Sadiqiin kuwa imeelezwa katika Hadith kuwa :

‘Yeyote yule aliyebarikiwa na Allah swt kwa mali na utajiri, lakini kwa sababu za ubakhili wake hakutoa Zaka na malipo mengine yaliyofaradhishwa kwake, basi Siku ya Qiyamah mali hiyo itatokezea kwake katika sura ya nyoka, ambaye atakuwa mwenye sumu kali kwani hatakuwa na unywele wowote juu ya kichwa chake na atakuwa na alama mbili za rangi nyeusi chini ya macho yake na hii ndiyo dalili ya kutambulisha kuwa nyoka huyo ni mkali sana na hatari kabisa. Basi nyoka huyo atajiviringisha shingoni mwa mtu huyo kama mnyororo. Katika hali ya kumsuta, nyoka huyo atasema: ‘Mimi ni mali yako ile ambayo wewe ulikuwa ukijivuna na kujifakharisha duniani.’

 

1313.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasail-as Shiah, mlango 3, J.6, Uk. 11:

“Mtu yeyote ambaye hatatoa na kulipa Zaka ya mali yake basi Siku ya Qiyamah Allah swt atamwadhibu kwa miale ya mioto katika sura ya nyoka wakubwa ambao watakuwa wakinyofoa na kula nyama yake hadi hapo hisabu yake itakapokwisha.”

 

1314.  Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Tafsir Minhaj as-Sadiqiin kuwa :

“Iwapo mtu aliye na mali na utajiri atakapoijiwa na ndugu au jamaa yake kwa ajili kuomba msaada kutokea mali na utajiri huo alionao, na yeye kwa sababu ya ubakhili wake akimnyima, basi Allah swt atamtoa nyoka mkubwa kabisa kutokea mioto ya Jahannam ambaye huizungusha ulimi wake mdomoni ili kwamba mtu huyo amwijie ili aweze kujiviringa shingoni mwake kama mnyororo mzito.”

 

1315.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah, Zakat,mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 11 na Al-Kafi :

“Mtu yeyote anayemiliki dhahabu na fedha na asipotoa Zaka yake iliyofaradhishwa (au Khums, kama vile inavyoelezwa katika Tafsir al-Qummi), basi Allah swt atamfunga kifungo katika mahala pa upweke na atamwekea nyoka mkubwa kabisa ambaye atakuwa amedondosha nywele zake kwa sababu ya sumu kali aliyonayo, na wakati nyoka huyo atakapotaka kumshika basi mtu huyo atakuwa akijarbu sana kukimbia lakini atkaposhindwa hatimaye na atakapotambua kuwa hataweza kujiokoa basi atamnyooshea mikono yake mbele ya nyoka huyo. Lakini nyoka huyo atazitafuna mikono hiyo kama vile anavyotafunwa mtoto mdogo wa ngamia na atajiviringisha shingoni mwake kama mnyororo. Na hapo Allah swt anatuambia kuwa ‘Yeyote yule anayemiliki mifugo, ng’ombe na ngamia na siyetoa Zaka ya mali yake, basi Allah swt Siku ya Qiyamah atamfunga kifungo cha upweke na kila mnyama atamwuma na kila mnyama mwenye meno makali atampasua na yeyote yule ambaye hatoi Zaka kutokea mitende, mizabibu na mazao yake ya kilimo, basi huyo siku ya Qiyamah basi atafungwa shingoni mwake kwa mnyororo wenye urefu wa takriban magorofa saba.”

 

1316.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah Mlango 3, J.6, Uk.11 :

“Allah swt amefaradhisha Zaka pamoja na Sala. Ameamrisha kutekeleza Sala na kutoa Zaka hivyo iwapo mtu atasali bila ya kutoa Zaka, basi atakuwa hakukamilisha Sala.”

 

1317. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Wasa’il as-Shiah, Zakat,mlango 3, Hadith 13, J.6, Uk. 11: amesema kuwa :

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia katika Masjid an-Nabawi, na aliwataja watu watano kwa majina yao na akasema kuwa inukeni na mtoke humu Msikitini na wala msisali kwani nyinyi hamutoi Zaka.

(Wasiolipa Zaka wamefukuzwa kutoka Msikitini !)

 

1318. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT,mlango 3, Hadith 24, J.6, Uk 14 :

“Mtu yeyote asiyelipa Zaka ya mali yake basi yeye wakati wa mauti yake atataka kurudishwa humu duniani ili aweze kutoa na kulipa Zaka, kama vile Allah swt anatuambia: ‘Ewe Allah swt nirudishe tena ili nikafanye mema niliyokuwa nimeyaacha !’ Yaani wakati wa kifo chake atasema kuwa arudishwe humu duniani ili akaitumie mali aliyoilimbikiza katika njia njema, lakini atajibiwa kuwa kamwe haitawezekana hivyo kurudi kwake.”

 

1319. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameelezea tafsir ya Ayah isemayo kuwa : ‘Allah swt atawaonyesha matendo yao katika hali ya kusikitisha mno kuwa wao hawatatoka nje ya Jahannam’ kama ifuatavyo katika Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk 21 :

 

“Mtu yule ambaye anakusanya na kulimbikiza mali yake na anafanya ubakhili katika kuitumia katika mambo mema na kwa kutoa zaka n.k., basi anapokufa huku amewaachia mali hiyo wale ambao watatumia mali hiyo katika utiifu wa Allah swt au kwa kutenda madhambi, basi iwapo itatumiwa katika utiifu wa Allah swt basi atakuwa mtu wa kujivuna na iwapo itatumiwa katika maasi na madhambi basi itamdhalilisha.”

 

1320. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk21 :

“Hakuna kitu kinachokimaliza Islam kama Ubakhili na njia ya Ubakhili ni sawa na njia ya sisimizi ambayo haionekani na yenyewe ipo kama Shirk ambayo inayo aina nyingi.”

 

1321. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amesema katika Safinat al-Bihar, J.1 Uk. 155 :

“Watu watakapokataa kutoa Zaka, basi baraka itakuwa imeondolewa kutoka ardhini kwa kutoa mazao na matunda kutoka mashamba yao,na madini.”

 

1322.  Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema katika Wasa’il as-Shiah, Mlango 1, Hadith  13 :

“Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka na mutokomeze balaa, maafa kwa Du’a na muhifadhi mali zenu kwa kutoa Zaka.”

 

1323.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 10, J.6, Uk23 :

“Allah swt anazo mahala pengi humu ardhini ambazo huitwa ‘kilipiza  kisasi’ hivyo Allah swt anapomjaalia mtu mali na utajiri, na huyo mtu haitumii kwa kutoa malipo aliyofaradhishiwa, basi huwekewa nafasi mahala hapo. Mali ambayo anakusanya kwa mbinu zake zote,inapomtoka na anaiachia wengine.”

 

1324. Zipo riwaya nyingi ambazo zinazumngumzia kukufurishwa kwa mtu asiyetoa Zaka kwa sababu za ubakhili wake. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah,mlango 4, Hadith 2, J.6, Uk 18 :

“Bila shaka Allah swt amewawekea hisa mafukara na wenye shida katika mali za matajiri ambayo imefaradhishwa. Faradhi ambayo inapotimizwa inakuwa ni yenye kuwafakharisha matajiri hao na ni kwa sababu ya kutoa huko Zaka kunakoharamisha kumwagwa damu yao na wanaolipa zaka wanaitwa Waislamu.”

 

1325. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk 18 :

“Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata lau kwa kiasi cha Qirat (1.20 Dinar yaani punje nne za Shayiri) basi huyo si Mumin wala si Mwislamu na watu kama hawa ndivyo alivyoelezea Allah swt  kuwa watakuwa wakitaka warudishwe humu duniani ili watekeleze

mema.”

 

1326.  Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameeleza katika Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk 18:

“Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata kwa kiasi cha Qirat moja (sawa na punje nne za Shayiri) basi huyo atakuwa  bila imani na kufa kwa mauti ya Myahudi au Mnasara.”

 

1327.  Amesema vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. katika Wasa’il as-Shiah, Zakat, mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 19 na  Kafi :

“Allah swt ameruhusu kumwagwa damu ya watu wa aina mbili ambapo hukumu hii itatekelezwa pale atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, Sahibuz-Zamaan, a.s. na hivyo mmoja miongoni mwa watu hao wawili ni yule anayefanya zinaa ilhali anayo mke wake hivyo atauawa kwa kupigwa mawe hadi kufa kwake na wa pili ni yule asiyetoa Zaka, huyo atakatwa kichwa.”

 

1328.  Vile vile amesema, katika Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 8, J.6, Uk 20 :

“Mali haipotei katika majangwa na Baharini isipokuwa ile isiyolipiwa Zaka na atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, Sahibuz-Zamaan, a.s. basi wale wote wasiolipa Zaka watasakwa na kukamtwa na watakatwa shingo zao.”

 

1329. Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Fussilat, 41, Ayah

6–8 : 

“Ole wao wanaomshirikisha, ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Aakhera.” 

 

1330. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , katika  Al-mustadrak :

“Kwa kiapo cha Allah swt ambaye anayo roho ya Mtume Wake katika kudura yake, kuwa hakuna mtu anayemfanyia khiana Allah swt isipokuwa Mushrikina kama hawa ambao hawatoi Zaka kutoka mali zao.”

 

1331. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., katika Al-Khisal, Uk. 450, Mlango Kumi :

“Ya Ali ! Katika Ummah wangu wapo makafiri wa makundi kumi :

Mfitini na mchonganishi

Mchawi

Dayyuth yaani mwanamme yule ambaye anajua kuwa mke wake anazini lakini hajali bali anapuuzia,

Mwanamme yule ambaye anauroho wa kiharamu wa kutafuta wanawake mbalimbal kwa kulawiti,

Anayewalawiti wanyama 

Anayezini pamoja na wale walioharamishwa kwake yaani ambao ni mahram kwake,

Anayechochea na kuzidisha moto wa fitina na chuki miongoni mwa watu, 

Anayewasaidia makafiri kihali na mali kupigana dhidi ya Waislamu,

Asiyetoa Zaka

Asiye Hijji ilhali ana uwezo kamili na kutimiza masharti yake na akifa katika hali hiyo.”

 

1332.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika kuzungumzia faida za utoaji wa Zaka, katika Kafi na Wasail, Mlango 1, Hadith 9 :

“Bila shaka Zaka imefaradhishwa kwa ajili ya kuwajaribu (mtihani) matajiri na wenye mali na kuwatimizia mahitaji ya wenye shida na kwa yakini, iwapo watu wangalikuwa wakitoa Zaka ipasavyo, basi kusingalikuwapo na Waislamu masikini na wenye shida na wala kusingalikuwa na mmoja kumtegemea mwingine na wala kusingalikuwapo na wenye kuwa na njaa au wasiokuwa na nguo. Lakini taabu na shida zote walionazo masikini ni kutokana na wenye mali na utajiri kutotimiza wajibu wao wa kutoa Zaka na Sadaka. Hivyo Allah swt humtenga mbali na neeema na baraka Zake yule ambaye hatimizi wajibu wake huo. Nami naapa kwa kiapo cha Allah swt ambaye ameumba viumbe vyote na anawapatia riziki zao, kuwa hakuna kinachopotea katika mali katika nchi kavu au majini isipokuwa ile isiyotolewa  Zaka.

 

Faida ya tatu, Nafsi yetu inatoharishwa kwa udhalilisho wa ugonjwa sugu wa ubakhili na hivyo inatubidi sisi lazima tuutibu ugonjwa huu unaoangamiza na kutumaliza.

 

1333.  Hivyo Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al-Tawba, Ayah 103 :

“Chukua Sadaka katika mali yao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Sadaka zao na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Kwa hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu, na Allah swt ndiye asikiaye na ajuaye.”

 

1334.  Vile vile Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah

al – Hashri, 59,  Ayah 9:

“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa waliyopewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.  Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.”

 

1335.  Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al –Baqarah, Ayah 28 :

“Allah swt huongezea katika Sadaka”

 

1336.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah al – Sabaa, 34, Ayah 39 :

‘Chochote kile mtakachokitoa (katika njia yake), basi Atawalipeni (humu humu duniani) malipo yake, Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.’

 

1337.  Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al –Rum, 30,  Ayah 39 :

‘Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Allah swt . Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Allah swt, basi hao ndio watakaozidishiwa.’

 

1338.  Amesema Bi. Fatimah az-Zahra a.s. bintie Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba aliyoitoa kuzungumzia Fadak katika Bihar al-Anwaar, J.8, Uk 109 :

“Kwa ajili ya kujitakasa na dhambi la Shirk, Allah swt ametufaradhishia kuikamilisha imani yetu (yaani mtu yeyote anayetaka kujitakasisha na unajisi basi inambidi kuleta imani kwa moyo wake kamilifu), na Sala inamwepusha na magonjwa ya kiburi na kujifakharisha, na Zaka inamwepusha mtu kwa magonjwa ya ubahili ili mwanadamu awe mkarimu na mpenda kutoa kwa ajili ya mema ili atakasike) na hii pia ndiyo sababu kuu katika kujiongezea riziki .”

 

1339.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. ameripotiwa akisema katika

  Al-Kafi:

“Yeyote yule anayetumia kutoka mali yake katika njia ya kheri, basi Allah swt anamlipa mema humu duniani na kumwongezea katika malipo yake.”

 

1340.  Vile vile ameripotiwa akisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  katika Wasa’il as-Shiah : Mlango Sadaka, Hadith 19, J.6, Uk. 259 :

“Tafuteni riziki yenu kwa kutoa Sadaka.”

 

1341.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa katika Kitab ‘Uddatud-Da’i kuwa  alimwuliza mtoto wake :

“Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi?”

 

Naye alimjibu :

“Zipo Dinar arobaini tu.” 

Imam a.s. alimwambia

“Dinar zote hizo zigawe Sadaka.”

Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam a.s.

“Ewe Baba ! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote.”

Imam a.s. alimwambia :

“Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaka kwani ni Allah swt tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaka ( kutolea

mema ).”

 

Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaka Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam a.s. alitumiwa Dinar elfu nne.

 

Hapo Imam a.s. alimwambia mwanae :

“Ewe Mwanangu ! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah swt ametupa Dinar elfu nne badala yake.”

 

1342.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amesema katika Nahjul Balagha kuwa :

“Mtu anapokuwa masikini au mwenye shida basi fanyeni biashara pamoja na Allah swt kwa kutoa Sadaka.”

 

1343.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Zakat-i-Fitrah inakamilisha saumu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”

 

1344.  Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al – Tawbah,  9, Ayah 60 :

“Wa kupewa Sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Allah swt , na wasafiri. Huu ni wajibu uliofaradhiwa na Allah swt . Na Allah swt ni Mwenye kujua Mwenye hikima.”

 

1345.  Vitu saba vina Zaka Sunnah :

  • Mali ya biashara au mtaji

Mali ambayo mtu anataka kuitumia katika kufanyia biashara

  • Aina za nafaka :

Mfano mchele, dengu, dengu iliyoparazwa. Lakini mbogamboga kama vile biringanya, matango, matikimaji, maboga hayana Zaka.

  • Farasi jike
  • Vito vya dhahabu na mawe

Vitu vilivyotengezwa vya kuvaa na mawe kama almasi n.k.

  • Mali iliyozikwa au kufichwa

Iwapo mtu atakuwa na mali aliyoizika au aliyoificha ambayo hawezi kuitumia basi kwa misingi ya uwezo inambidi kutoa Zaka ya mwaka mmoja.

  • Kukwepa kutoa Zaka

Iwapo mtu atauza sehemu ya mali kiasi fulani kabla ya kuisha kwa mwaka kwa misingi ya kukwepa kulipa Zaka, basi itambidi uanzapo mwaka mpya, alipie Zaka sehemu hiyo aliyokuwa ameuza kwa ajili ya kukwepa Zaka yake.

  • Mali ya kukodisha

Mtu anayepokea malipo kutokana na kukodisha majumba, maduka, mashamba, mabustani au hamaam (mabafu yanayotoza malipo kwa kutumia ).

 


KHUMS

1346. Allah swt anavyotuelezea katika Qur'an Tukufu, Surah al-Anfaal, 8, Ayah 41 :

NA JUENI ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Allah swt na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Allah swt na tuliyoteremsha kwa mja wetu(Muhammad) siku ya kipambanuo (katika Vita vya Badr), siku ( Waislamu na Makafiri ) yalipokutana majeshi mawili. Na Allah swt ni Muweza wa kila kitu.

 

1347.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Man la yahdhurul Faqih, J.2, uk.41

“Kwa kuwa Allah swt ametuharamishia Zaka sisi Ahlul-Bayt a.s.hivyo ametuwekea Khums kwa ajili yetu na hivyo Sadaka pia ni haram kwetu na zawadi imeruhusiwa kwa ajili yetu.”

 

1348.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Usuli Kafi, J. 1, Uk.545 :

“Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kununulia chochote kutoka kifungu ambacho Khums haijalipwa na hadi pale wasipoifikisha kwa wanaostahiki kwetu.”

 

1349.  Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Al-Kafi, J.1, Uk. 546 :

“Siku ya Qiyamah wakati ule utakuwa mgumu kabisa pale wanaostahiki Khums watakapotokezea kudai haki zao kutoka wale wasioilipa.”

 

1350. Miongoni mwa marafiki tajiri mmoja kutokea Uajemi alimwandikia barua Al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. na alimwomba Imam a.s. ruhusa ya kuitumia ile mali ambayo khums haijatolewa. Basi Imam a.s. alimwandikia majibu kama ifuatavyo : Imenakiliwa kutoka Al-Wafi, Al-Kafi na Tahdhib

“Bila shaka Allah swt ni Wasi’ na Mkarimu na amechukua dhamana ya kumlipa thawabu na malipo mema yule mtu ambaye atatekeleza hukumu zake na ameweka adhabu kwa yeyote atakayekwenda kinyume ya hayo. Bila shaka mali iliyo halali kwa ajili ya mtu ni ile ambayo Allah swt ameihalalisha na kwa hakika Khums ni dharura yetu na ni hukumu  ya Dini yetu na ni njia ya kujipatia kipato kwa jili ya riziki sisi na wenzetu na imewekwa kwa ajili ya kulinda hishima zetu dhidi ya wapinzani wetu. Hivyo kamwe musiache kutoa na kulipa Khums. Na kila inapowezekana kusijikoseshe Du’a zetu na kwa hakika kwa kutoa Khums kunazidisha riziki yenu na  kutoharisha na ni hazina kubwa kwa ajili ya Siku ile ambayo kutakuwa na taabu tupu na mateso (Siku ya Qiyamah). Na kwa hakika Mwislamu sahihi ni  yule ambaye amemwahidi Allah swt kwa ahadi na ‘ibada, basi atimize kwa ukamilifu. Na iwapo atakubali kwa mdomo tu ilhali moyoni anakataa na kupinga basi atambue kuwa yeye si Mwislamu.

 

1351.  Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144  kuwa :

“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaka.”

 

1352.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia :

“Nasikitika mno na ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake.”

 

1353.  Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu  Surah al- Ma’arij,70, Ayah 24 – 25 :

Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.

Na mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba…

 

1354.  Al Imam Musa bin Ja’afer a.s. amepokelewa riwaya kuwa  :

“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa na mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umri uliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikini.

 

Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

 

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

 

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilolifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake.

 

Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

 

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikini na uwe na uhusiano mwema pamoja nao. Na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

 

Mtu huyo alizingatia na kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika wakati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

 

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa : ‘Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.’”

 

1355. Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al –Al-An-‘Aam 6, Ayah 141 :

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisiyo tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana. Kileni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

 


 

1356.  Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

 

1357.  Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika  Al-Wafi :

“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt anamhisabia deni hilo katika Sadaka hadi kuja kulipwa kwake.”

 

1358.  Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa :

“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidi katika Qur'an Tukufu adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wenye shida wanapokuja kuazima vitu vya nyumbani, basi inabidi  kuwa azima vitu vya nyumbani.”

 

1359.  Abu Basir amemwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa

“Majirani zetu wanapokuja kuazima vyombo au vitu vingine vya nyumbani, na tunapo waazima basi huvunja vunja na kuviharibu vitu vyetu na hivyo sisi tunalazimika kuwakatalia kwa misingi hiyo, sasa je kuwakatalia huku ni dhambi ?”

 

1360.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :

“Iwapo watu hao wanatabia kama hiyo, basi si dhambi kuwanyima.”

 

1361. Inabidi kuwapa muda au kuwasamehe madeni wale ambao hawana uwezo wa kuyalipa madeni hayo. Na kuhusiana na swala hili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Iwapo mtu anataka asidhalilishwe Siku ambayo hakuna mwingine wa kuwaokoa isipokuwa Allah swt , basi inambidi awape muda wa kulipa madeni wadaiwa wake au kuwasamehe madeni yao.”

 

1362.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Yeyote yule atakayempa muda wa kulipa madeni ambaye hana uwezo wa kulipa ( basi kwa ajili yake ) thawabu zake mbele ya Allah swt  ni sawa na thawabu za kutoa Sadaka kila siku kwa kiasi hicho hadi atakapolipwa.”

 

1363.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliambiwa kuwa :

“Abdur Rahmaan bin Sababah anamdai deni marehemu mmoja, nasi twamwambia yeye kuwa amsamehe lakini yeye anakataa kata kata kumsamehe deni lake.”

 

1364.  Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema :

“Ole wake, je haelewi kuwa iwapo atamsamehe marehemu deni lake basi Allah swt atamlipa Dirham kumi kwa kila Dirham yake moja. Na iwapo hatamsamehe basi atalipwa Dirham moja kwa Dirham yake moja.”

 

1365.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.2,Uk. 204 :

“Mtu yeyote atakayemsaidia Mumin kwa mavazi wakati wa baridi au joto basi Allah swt atamjaalia mavazi ya Jannat (Peponi au Paradiso ) na atampunguzia shida kali wakati wa kutoa roho yake (wakati anapokufa ) na atampanulia kaburi lake na Siku ya Qiyamah atakapotoka nje ya kaburi lake atakuwa akitoka katika hali ya furaha kwa kuonana na Malaika.”

 

1366.  Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J.2, Uk.205 :

“Iwapo Mwislamu yeyote atamsaidia mtu asiye na mavazi kwa mavazi au aliye na dhiki ya mali, akasaidiwa ( nyumba,mali n.k ) basi Allah swt anamwekea Malaika elfu saba hadi Siku ya Qiyama kwa ajili ya kumwombea maghfirah kwa kila dhambi lake.”

 

1367.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Wafi, al-Kafi na kunakiliwa pia katika Tahdhiib :

“Baada ya kufariki kwa mtu, huongoka  kwa mambo matatu

  • Sadaka ambayo aliitoa humu duniani na ambayo inaendelea baada yake,
  • Sunnah ambayo aliitekeleza kwa mfano Adhan ambayo baada ya kifo chake ingali ikiendelea,
  • Kuacha mtoto mwenye tabia na mienendo mizuri ambaye atakuwa akimwombea dua na usamehevu kwa ajili yake ( na akifanya mema kwa niaba ya baba yake, kama inavyoelezwa katika vitabu vingine.

 

 


RIBA

1368.  Dhambi la riba ni miongoni mwa Madhambi Makuu.

 

1369.  Kwa mujibu wa Qur’an tukufu, kuchukua riba ni dhambi ambalo linasababisha adhabu kali kabisa kutoka kwa Allah swt.  Adhabu za kuchukua na kutoza riba ni kali kabisa kuliko madhambi mengine. Kama ilivyoelezwa katika Surah Aali Imran, 3, : 130 - 131:

‘Enyi Mlioamini! Msile riba, mkizidisha mara dufu kwa mara dufu; na mcheni Allah ili muweze kuwa na ufanisi’

 

‘Na ogopeni moto wa Jahannam ambao umetayarishiwa makafiri.’

 

1370.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah al Baqarah, 2, Ayah 275 :

‘Wale wanaokula riba, hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye Shaitani kamzuga kwa kumsawaa; na haya ni kwa sababu wamesema, ‘biashara ni kama riba’, Allah ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba.  N a aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.’

 

1371. Ayah hiyo inatuthibitishia kuwa wale wanaochukua riba watabakia kwa milele katika Jahannam (Motoni) na kamwe hakutakuwa na uwokovu kwa ajili yao. Allamah Muhammad Husain Tabatabai (a.r.) katika Tafsiri ya Al-Mizan , anasema:

“Adhabu aliyoiweka Allah swt kwa ajili ya mla riba ni kali kabisa kwani hakuna mahala pengine palipozungumzwa kwa ajili ya wale wavunjao kutoka Furu-i-Diin. Kosa lingine ni lile la kulea urafiki pamoja na maadui wa Islam. Athari za riba zipodhahiri na bayana kwetu sote. Kukusanya na kuficha mali ndiko kunako ongezea tofauti kati ya  tabaka la masikini na tajiri. Umasikini ni ugonjwa ambao unamdhalilisha na kumshusha hadhi mgonjwa wake, unateketeza uthamini wake na kuharibu maadili yake. Na haya yanaelekeza katika mutenda maovu, uizi, ubakaji na mauaji. Walanguzi ndio watu wanaowajibika kwa kuteketea kwa usawa wa kijamii, ambao wamejilimbikizia mali kupita kiasi kwamba haiwafikii wanao hitaji na wenye dharura. Kwa kuvunjika kikamilifu kwa mshikamano wa kijamii unaweza kuzua na kukuza vita vya wenyewe kwa wenyewe au vita vya ndani na kuendelea hadi kuzuka kwa vita vya dunia ambavyo hatima yake itakuwa ni mauaji na maangamizo. Katika ulimwengu wa sasa ikiwa na silaha za kisasa za teknolojia ya hali ya juu na ya maafa makubwa katika nuklia na kemikali, vita vinapozuka si kwamba vinaleta mauaji ya wanaadamu tu bali humgeuza yeye kuwa ni picha tu, mgonjwa na asiye na uwezo wowote na ameharibika kimwili kwa vizazi na vizazi vijavyo.

 

1372.  Katika kitabu ‘Islam and World Peace’ imeandikwa:

“Islam inasema kuwa mapato ya mtu yatokane na kiwango cha juhudi na kazi iliyofanyika.” Kwa sababu  uwekezaji wenyewe haufanyi kazi wala jitihada ya aina yoyote ile. Hivyo, mali ya matajiri haitakiwi kamwe kuongezeka kwa kutokana na riba.”

 

1373.  Mtume Muhammad s.a.w.w. anasema katika Hadith moja, katika Wasa’il al-Shiah  :

“Ibada inayo sehemu sabini. Na muhimu kabisa ni mtu kujipatia kipato chake kilicho halali.”

 

1374. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Muhajjatul Baidha :

“Mfanyabiashara mwaminifu atahesabiwa pamoja na Mitume a.s. Siku ya Qiyama. Uso wake utakuwa uking’ara kama mbalamwezi.”

 

 

1375.  Qur’an Tukufu inarejea kutuambia katika Qur'an Tukufu, Surah al-Baqarah, 2 Ayah  275 :

‘‘Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.’

 

1376.  Ayah ya hapo juu ya Qur’an inaendelea Qur'an Tukufu, Surah al-Baqarah, 2 Ayah 276 :

‘Allah huyafutia (baraka mali ya ) riba: na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaqa . Na Allah hampendi kila kafiri (na) afanyaye dhambi.’

 

1377.  Qur’an Takatifu inatuambia Surah al-Baqarah, 2, Ayah 278  :

‘Enyi Mlioamini ! Mcheni Allah, na acheni yaliyobakia katika riba, ikiwa mmeamini.’

 

1378.  Ushahidi wa imani ya mtu katika utiifu wa Hukumu za Allah swt, ayah hiyo hiyo inaendelea : Qur'an Tukufu, Al-Baqarah, 2,

        Ayah 279

‘Na kama hamtafanya hivyo, basi fahamuni mtakuwa na vita na Allah na Mtume Wake….’

 

1379. ‘Na mkiwa mmetubu, basi matapata rasilimali zenu; msidhulumu wala msidhulumiane.’

 

1380. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amezungumzi katika hotuba yake huko Makkah :

“Muelewe kuwa riba iliyokuwa imekusanywa katika zama za ujahiliyya sasa imesamehewa kabisa. Kwanza kabisa mimi binafsi nina wasameheni ile riba ( iliyopo shingoni mwenu) ya (mjombangu) '‘Abbas ibn Abdul Muttalib."

 

1381.  Imeripotiwa kutoka Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. kuwa, katika

     Al-Kafi :

“Kuchukua Dirham (au pesa moja) kama riba ni vibaya sana machoni mwa Allah swt kuliko kuingiliana na mwanamke aliyeharamishwa kwako.”

 

1382.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Wasa’il al-Shiah :

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amemlaani vikali yule ambaye anayekubali riba, anayelipa riba, aneyeinunua riba, anayeiuza riba, yule anayeandika mikataba ya riba na yule anayekuwa shahidi wa mikataba hiyo.”

 

1383.  Ibn Baqir anaripoti kuwa  Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. alijulishwa kuhusu mtu mmoja aliyekuwa akitoza na kupokea riba kama ndiyo halali kama vile ilivyo halali maziwa ya mama. Kwa hayo, alisema Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. katika 

        Al-Kafi :

“Iwapo Allah swt atanipa uwezo mimi juu ya mtu huyu, basi nitamkata kichwa.”

 

1384.  Sama’a anasema kuwa yeye alimwuliza Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. je ni kwa nini Allah swt ametaja kuharamishwa kwa riba mahala pengi katika Qur’an.

 

Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. alimjibu, Wasa’il al-Shiah :

‘Ili kwamba watu wasiache tendo la kutoa misaada (kama vile kutoa mikopo bila ya riba).”

 

1385.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Shughuli mbaya kabisa ni ile ambayo inahusisha riba.”

 

1386.  Zurarah anasema kuwa yeye alimwuliza Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. kuhusu  Ayah ya Qur’an isemayo  katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Baqarah,2, Ayah 276:

‘‘Allah huyafutia (baraka mali ya ) riba: na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaqa .’

 

1387.  Na akaongezea kusema :

“Lakini mimi ninaona kuwa mali na utajiri wa watoza riba inaendelea kuongezeka tu kila siku.”

 

1388.  Amesema Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Loh ! hasara inawezekana kuwa kubwa sana ? Kwa merejeo ya Dirham moja yeye anaipoteza Dini yake.  Na iwapo yeye atafanya Tawba humu duniani basi kutafikia mwisho kwa mali aliyoichuma humu duniani kwa njia iliyo haramu na hivyo kuwa fukara.”

 

1389.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika  Mustadrakul Wasa'il :

“Yule anayechukua riba basi Allah swt atalijazatumbo tumbo lake kwa moto kiasi hicho hicho. Iwapo yeye amechuma zaidi kwa kutokana na mapato ya riba, basi Allah swt hatakubalia matendo yake mema. Hadi kwamba kiasi cha punje moja kama kitabakia ambacho kimepatikana kwa njia ya riba. Allah swt pamoja na Malaika Wake wataendelea kumlaani huyu mtu.”

 

1390.  Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

“Usiku wa Mi’raj Mimi niliwaona baadhi ya watu waliokuwa wakijaribu kusimama lakini hawakuweza kufanikiwa kwa sababu ya matumbo yao makubwa, niliuliza, ‘Ewe Jibraili ! Je ni watu gani hawa ?’

 

1391.  Jibraili alijibu :

“Hawa ndio wale waliokuwa wakichukua riba. Sasa wao wanaweza kusimama tu kama wale waliokamatwa na Mashetani.”

 

1392.  Mtume Muhammad s.a.w.w. aliendelea,

“Na hapo nikawaona wao wakikusanywa katika njia za wafuasi wa Firauni. Kwa kuona uchungu wa joto la Moto mkali, wao walipiga kelele : ‘Ewe Allah swt ! Je Qiyama itakuwa lini ?’

(Hivyo imekuwa dhahiri kuwa Moto unaozungumziwa katika riwaya hii ni adhabu katika Barzakh ).

 

1393.  Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema, katika Mustadrakul Wasa'il :

“Wakati zinaa na riba vitakapokuwa ni vitu vya kawaida katika mji wowote basi Allah swt huwapa ruhusa Malaika kuwaangamiza wakazi wake.”

 

1394.  Ipo riwaya nyingine isemayo kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika  Mustadrakul Wasa'il  kuwa :

“Utakapofika wakati Ummah wangu utaanza kutoza na kupokea riba, basi mitikisiko na mitetemeko ya ardhi yatakuwa yakitokea mara kwa mara.”

 

1395.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, Wasa’il al-Shiah  :

“Iwapo mtu atazini pamoja na mama yake katika Al-Ka’aba tukufu, basi dhambi hili litakuwa hafifu mara sabini kuliko tendo la kutoza na kupokea riba.”

 

1396.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Katika macho ya Allah swt, kuchukua Dirham moja ya riba ni mbaya kabisa hata kuliko matendo thelathini ya kuzini pamoja na maharimu wake yaani baba kuzini pamoja na binti yake.”

 

 


 


USAMEHEVU

 

1397.  Kwa upande mmoja Uislamu unawasisitiza Waislamu kutafuta nyenzo za kujipatia mahitajio yao ya kila siku katika maisha yao kwa njia zifuatazo:

 

1398.  Ibada ni za aina saba, na mojawapo ni kule kujitafutia mahitaji ya kila siku kwa njia zilizo halalishwa katika Dini. [17]

 

1399.  Yeyote yule aliye na maji pamoja na ardhi katika uwezo wake, na wala halimi katika ardhi hiyo, na iwapo atakumbwa na hali ya kukosa chakula cha kujilisha yeye pamoja na familia yake, basi atambue wazi kuwa huyo amekosa baraka za Allah swt. [18]  

 

1400.  Moja ya matendo yaliyo bora kabisa ni kilimo kwani mkulima anajishughulisha katika kilimo na upandaji wa mazao ambayo yanawafaidisha wote bila ya kuchagua iwapo huyu ni mwema au mwovu. [19]  

 

1401.  Yeyote yule asiyejitafutia mahitaji yake ya maisha basi kamwe hatakuwa na maisha ya mbeleni kwani atateketea.

 

1402.  Na yeyote yule anayejitahidi kwa bidii kubwa kwa kujipatia mahitaji kwa ajili ya familia yake basi huyo ni sawa na yule ambaye anapigana vita vya Jihad. [20] 

 

1403. Kwa upande wa pili, Islam inaamini kuwa iwapo mtu atakuwanavyo mali na milki, kilimo na viwanda, utajiri na starehe lakini bila ya Taqwa ya Allah swt  kama vile imani juu ya Allah swt na Mitume a.s, Imani juu ya siku ya Qiyama, thawabu, na adhabu na bila ya kuwa na tabia njema na kuuthamini ubinadamu kama vile msamaha, ushirikiano katika mambo mema, moyo wa utoaji, kuonea huruma n.k. basi kamwe haviwezi kumpatia maendeleo.

 

1404.   Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu Surah Al A’S’R,

           103 : Ayah 1-3

  • ‘Naapa kwa alasiri.’
  • ‘ Hakika mwanadamu yumo hasarani !’
  • ‘ Ila wale ambao wameamini wakatenda mema na wakausiana kwa haki na subira.’

 

1405.   Imam Hussein a.s. amenakiliwa akisema:

“Kama kwa kweli kuna milki ya mali ya mtu humu duniani, basi hiyo ni  kuwa na tabia njema. Iwapo watu wote watakufa, basi kifo jema kabisa mbele ya Allah swt ni kule kujitolea mhanga katika njia ya Allah swt.”

 

1406.   Usamehevu upo wa aina mbili:

·         Sisi tunamsamehe mtu pale tunajikuta kuwa hatuna uwezo wa kulipiza kisasi. Kwa hakika aina hii ya usamehevu unatokana na subira na kuvumilia na kamwe si kusamehe. Kwa maneno mengine, ni aina mojawapo ya kutoweza kujisaidia na udhaifu.

·         Sisi tunamsamehe mtu ingawaje tunao uwezo wa kulipiza kisasi. Aina hii ya usamehevu ndio unaofundishwa na Islam pamoja viongozi wetu.

 

1407.  Amesema Al-Imam Ali as. :

“Mtu anayestahiki kusemehe wengine ni yule ambaye ni mwenye uwezo mkuu  zaidi katika kuwaadhibu wengine.”[21]

 

1408.  Katika wusia wake wakati akiongea na Harith Hamdani, Al- Imam Ali a.s. alisema:

“Tuliza ghadhabu zako na kumsamehe mtu aliyekukosea wakati wewe ukiwa na uwezo au cheo chako.” [22]

 

“Wakati wewe utakapomzidi nguvu adui yako, basi zingatia kumsamehe ikiwa ndiyo shukurani ya kupata uwezo huo.” [23]

 

1409.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s.

“Kuwasamehe wengine wakati mtu yupo katika madaraka ni sambamba na tabia na desturi za Mitume a.s pamoja waja wema.” [24] 

 

1410.  Baadhi ya Ayah za Qur’an tukufu zizungumziazo maudhui haya:

Qur'an Tukufu, Sura  Al- A’araf  (7) Ayah ya 199,

Uchukulie kusamehe na kuamrisha mema na kujiepusha na majaheli[25]

 

Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura A’araf ( 7 ) Ayah ya 200,

‘Na iwapo wasiwasi wa Shaitani utakusumbua basi jikinge kwa Allah, Yeye ndiye Asikiaye na Ajuaye yote.’

 

1411.  Qur'an Tukufu, Sura  Aali ‘Imran  (  3 )  Ayah  134

Wale wanaotumia wakiwa katika hali nzuri na dhiki na ambao huzuia ghadhabu zao na kusamehe (makosa ya) watu ; kwani Allah huwapenda wafanyao mema.  [26]

 

1412.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Aali ‘Imran

( 3 ) Ayah ya 159 kuwa: [27]

Hivyo kutokana na Rehema itokayo kwa Allah  kuwa wewe umekuwa mlaini kwao na kama ungalikuwa mkali na mwenye moyo mgumu bila shaka wangalikukimbia. Basi uwasamehe wewe na uwaombe msamaha na ushauriane (kwa kuwaridhisha tu ) nao katika mambo. Na unapoazimia mtegemee Allah, Hakika Allah huwapenda wamtegemeao.

 

Aya hii tukufu imewateremkia kuhusu wale ambao walikwenda kinyume na amri ya Mtume Muhammad sa.w.w. katika Vita vya Uhud ambapo kulisababisha Waislamu kushindwa.  Watu hao walikuwa ni hamsini na wawili (52) kwa idadi ambao waliwekwa na Mtume s.a.w.w. kulinda pakuingilia huko bondeni na aliwaambia : “ Iwapo sisi tutashinda au kushindwa, nyinyi kamwe musisogee wala kuondoka  hata hatua moja kutoka sehemu hii iliyo nyeti.”

 

Mbinu hii ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ikiwa pamoja na baraka za Allah swt na moyo wa kujitolea mhanga wa vijana wa Kiislamu wenye imani halisi, iliwafanikisha kuwashinda maadui ambao walikimbia. Wailsamu baada ya maadui kukimbia, walianza kukusanya mali iliyopatikana vitani hapo katika uwanja wa mapigano.

 

Mara hawa watu hamsini na wawili walipopata habari kuwa Waislamu wameshinda na wanakusanya mali iliyopatikana vitani, wote, isipokuwa kumi na wawili tu, waliacha ngome zao wazi na kukimbilia mali huku wakiwa wamevunja amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. iliyokuwa imewakataza wasiondoke hapo walipo katika sura yoyote ile ama iwe ya ushindi au kushindwa.  Kwa kuona haya, Khalid ibn Walid, ambaye alikuwa ni kamanda wa jeshi la makafiri, alikwenda hapo bondeni akiwa na jeshi la wapanda farasi mia mbili (200 ) wakiwa wamejiandaa kwa silaha. Makafiri hao waliwashambulia kwa ghafla Waislamu kumi na wawili na kuwaua wote na wakatokezea kwa nyuma kushambulia jeshi la Waislamu. Katika mapigano haya, Mashujaa sabini ( 70 ) wa jeshi la Waislamu waliuawa, akiwemo Hamzah ush-Shuhadaa ( kiongozi wa mashahidi).  Na Mas’ab ibn Umair vile vile wapiganaji wengi walijeruhiwa akiwemo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  Kwa hakika kuvunja amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa hao wachache kulileta maafa makubwa kwa upande wa Waislamu.  Watu walitegemea kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. atatoa amri kali kabisa dhidi ya hawa wachache; lakini sivyo na badala yake kuliteremka Ayah tukufu ikisema:

 

1413.  Qur'an Tukufu, Sura Aali ‘Imran ( 3 ), Ayah ya 159, kuwa:

‘…Basi uwasamehe wewe na uwaombe msamaha na ushauriane (kwa kuwaridhisha tu ) nao katika mambo….’

 

1414. Kwa kuiteremsha Ayah hii, Allah swt alimwamuru Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. atoe msamaha kwa waliokuwa wamekosa.

 

1415.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Bora ya tendo lililo mbele ya Allah swt ni kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima. “ Na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliisoma Ayah hii ya Qur’an:

 

1416.  Qur'an Tukufu, Sura  Al- A’araf  (7) Ayah ya 199,

‘Uchukulie kusamehe na kuamrisha mema na kujiepusha na majaheli’  [28]

 

1417. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika mkataba aliokuwa amemwandikia Malik-i-Ashtar, aliandika:

Zijazeni nyoyo zenu kwa  huruma, uwema na kuwapenda waliochini yenu. Na kamwe musitendee kama wanyama walafi na waroho, kujifanya kama munawalea kwa kuwatenga, kwani wao wapo wa aina mbili: ama wao ni nduguzo katika imani au wapo sawa katika kuumbwa. Wao wanapotoka bila ya kujua na kasoro zinawaghalibu, wanakosa makosa ama kwa makusudi au bila kukusudia.  Kwa hivyo nawe pia uwasamehe  kwa kutegemea naye Allah swt atakusamehe, kwani wewe umekuwa na uwezo dhidi yao, na Yule aliyekuchagua wewe yu juu yako, na Allah swt  yupo juu ya yule aliyekuweka katika wadhifa huu.” [29]

 

1418.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. :

Kusikitika baada ya kutoa msamaha ni afadhali ya kufurahi baada ya kuadhibu.” [30] 

 

1419.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika  Hadith ‘Arbain, ananakili Marehemu Deilami:

“Siku ya Qiyama, mpiga mbiu atasimama na kusema: ‘Yeyote aliye na malipo yake kwa Allah swt basi asimame.’  Lakini hakuna watakao simama isipokuwa wale tu ambao walikuwa ni wasamehevu.  Anaendelea kusema ‘Je hao hawakusikiaga ahadi iliyokuwa imetolewa na Allah swt :

 

1420.  Qur'an Tukufu,Surah Ash-Shuura  ( 42 ), Ayah 40, [31]

‘Na malipo ya uovu mfano wa huo. Lakini anayesamehe na kusahihisha; ujira wake uko kwa Allah swt. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.’

 

1421.  Qur'an Tukufu,Sura An-Nahl (16) Ayah 126,

‘Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoonewa, na kama mkisubiri basi hiyo itakuwa bora kabisa kwa wafanyao subira’.

 

1422.  Baada ya ufunuo wa Ayah hiyo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema : “mimi nitakuwa mwenye subira.” [32]

 

1423.  Qur'an Tukufu, Surah  Fat-h   (48 ) Ayah 1-2,

‘Bila shaka tumekwishakupa kushinda kuliko dhahiri. Kwamba Allah  alinde kwa ajili yako (dhidi) ya yale yaliyopita kabla ya (wafuasi wako) kasoro zako na yale yanayokuja …’ [33]

 

1424.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliisoma Ayah ifuatayo :

Qur'an Tukufu, Surah Bani- Israil (17 ) Ayah 81,

‘ Na sema : ‘Ukweli umefika; na uongo umetoweka; Kwa hakika uongo ndio wenye kutoweka.’ [34]

 

 

1425. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimsamehe mtumwa wa Kihabeshi, Wahshi, ambaye ndiye aliyekuwa amemwua Bwana Hamza, babake mkubwa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. . Alimsamehe wakati ambapo alikuwa na uwezo kamili wa kumwadhibu na kulipiza kisasi. Kwa hakika hii ndiyo iliyokuwa kanuni ya mtu ambaye alikuwa akiwaambia watu wote kuwa huruma ipo imefungamana katika tabia tatu:

    • Kumsamehe yule aliyekutendea yasivyo sahihi.
    • Kudumisha mshikamano wa udugu pamoja na jamaa ambaye ameuvunja uhusiano pamoja nawe.
    • Kumsamehe yule ambaye amekudhulumu au kukunyima haki yako.

 

1426. Qur’an tukufu inawatakata Wailsamu waigize tabia na mwnenendo kama Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ndiye awe kiigizo chao :

 

1427.  Qur'an Tukufu, Surah  Ahzab (33 ) Ayah 21,

Kwa hakika mnao mfano mwema kwa Mtume wa Allah, … [35]

 

Kwa mujibu wa Ayah hiyo, iwapo sisi tutapenda kuwa Waislamu wema, basi itatubidi kuzifuata tabia na mienendo yote ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. .

 

1428.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s.

“Allah swt hakubakiza chochote kile ambacho waja Wake watakihitaji hadi Siku ya Qiyama, isipokuwa vyote vipo katika kitabu kitakatifu cha Qur’an na ambayo yote yamefikishwa kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. Yeye amewekea mipaka kwa kila kitu, na kuweka uthibitisho kwa ajili yake.  Kwa wale watakaopita mipaka yake, Allah swt ameainisha adhabu za kutubu za Kidini.” [36]

 

1429.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema :

“Tofauti baina ya Waislamu na jamii zingine ni kwamba watu wote ni sawa mbele ya Shariah za Allah swt.  Islam haitofautishi baina ya tajiri na masikini, au baina ya mwenye nguvu na mnyonge.  Kwa kiapo cha Allah swt ! Lau Fatima binti ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. angalikuwa amefanya uizi, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. angalimkata mkono wake pia.” [37]

 


 


AHADITH MCHANGANYIKO

 

1430.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk. 584 na  485 :

“Mimi ni mbora wa Manabii na Ali a.s. ni mbora wa Mawasii. Mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili. Wa kwanza wao ni Ali a.s. na wa mwisho wao ni Mahdi a.s.”

 

1431.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 33,

‘Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume ) na kukutakaseni kabisa kabisa.’

 

1432.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 56,

‘Hakika Allah na Malaika Wake wanamteremshia Rehema Mtume, basi enyi Waumini (Waislamu) msalieni Mtume na muombeeni Amani’

 

1433. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika  Yanabiul Mawaddah, uk 42, 217 :

“Mimi nawaachia nyinyi Makhalifa wawili; Kitabu cha Allah swt : ni kamba iliyonyoshwa kutoka mbinguni mpaka ardhini, na Jamaa zangu wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.)”

 

1434. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 30/31

“Mfano wa Ahlul Bait zangu kwenu ni kama mfano wa jahazi ya Nuh a.s. , mwenye kupanda jahazi hiyo ameokoka na mwenye kuiachilia, kapotea.”

 

1435.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Sahih Muslim, Kitabu Al-Fadhail, mlango wa Fadhail Ali a.s. kwa kiingereza ni : J.4, uk. 1286, Hadith  nambari 5920 :

“….Enyi watu ! …. Ninawaachia nyinyi vizito viwili : Cha kwanza ni Kitabu cha Allah swt chenye uongozi na mwangaza basi shikamaneni na Kitabu cha Allah swt  …. Na watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bait a.s. )”

 

1436.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. Musnad Bin Hanbal, j. 4; uk. 437 :

“Hakika Ali ni kiongozi wa kila Mumiin baada yangu.”

 

1437.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika

At-Tirmidhi, j.5, uk. 66 Na.3786

“Enyi Watu ! Mimi hakika nimekuacheni vitu viwili navyo ni Kitabu cha Allah swt (Qur’an ) na watu wa ukoo wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.). Mkivichika viwili hivyo milele hamtapotea.”

 

1438.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema 

“Mkipata neema chache msirudishe kwa uchache wa shukurani.”

 

1439.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukuf, Sura Al-Imran, 3, Ayah 179 :

‘Wala usidhani wale waliouawa katika njia ya Allah swt kuwa ni wafu, bali wahai wanaruzukiwa kwa Mola wao.’

 

1440.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :

“Changanyikeni na watu kiasi ambacho kama mkifa watawalilia na mkiishi watatamani kuwa nanyi.”

 

1441.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Al-Ghadiir :

“Siku ya Ghadiir Khum ni Idi bora mno kwa Ummah wangu.”

 

1442. Allah swt  amesema katika Qur'an Tukufu, Surah…, …., Ayah….,

‘Shikamaneni na kamba ya Allah na wala msifarakane.’

 

SEMI MCHANGANYIKO

1443.  “Uwe mpole na mwenye huruma kwa wale walioko chini yako au 

       amri yako.”

 

1444. “Uchukue tahadhari na wala usidanganyike na ving’aavyo.”

 

1445. “Umwie ndugu yako kwa uwema hata kama ametokezea kwako

kukudhuru. Yeye anapo puuzia au kuukanusha udugu nawe, umwijie kindugu, utokezee awapo katika shida na ujaribu sana ili uweze kumsaidia katika hali hiyo. Awapo mchoyo au bahili kwako na akupuuzapo pale uwapo na mahitaji ya msaada wa kifedha, uwe mkarimu na umsaidie kifedha kwa kiasi uwezacho. Iwapo yeye ni mjuvi na mkatili kwako, basi wewe uwe mpole na umhali yeye. Iwapo anakudhuru, uyakubalie hoja zake. Uishi nae kama kwamba wewe ni mfaidika. Lakini uwe mwangalifu sana kuwa wewe usiwe hivyo kwa wasio stahiki na walio waovu.  

 

1446. “Usiimarishe urafiki na maadui wa marafiki wako kwani na rafiki yako atakugeuka wewe na kujitokezea mbele yako kama adui pia.”

 

1447. “Umshauri na kumpatia mawaidha mema na bora sana rafiki yako hata kama yeye hatapendelea hivyo.”

 

1448. “Uimarishe vyema na kusawazisha hasira, kwa sababu mimi sijawahi kuona  faida yoyote ile iliyo zaidi kuliko kujizuia hivyo.”

 

1449.  “Usimkorofishe mtu ambaye akufikiriaye wewe kuwa u mzuri na mwema na wala usijaribu kumfanya ajaribu kukugeuka.

 

1450.  “Usiwe mbaya kwa watu wa nyumbani mwako (mke, watoto na wakutegemeao) na wala usiwe kwao kwa ghadhabu na mkatili yungali hai.”

 

1451.  “Usimkimbilie yule akupuuzaye.”

 

1452.  “Kamwe usiwaijie kwa ubaya wale waliokufanyia hisani.”

 

1453.  “Masikini ni yule ambaye hana marafiki. Yeyote yule akunashaye haki na kujiona kuwa maisha yake yanamzonga na zenye kumtatanisha basi ni mtatanishi.”

 

1454.  “Uhasiano ulio bora kabisa ni ule kati ya mtu na Allah swt.”

 

1455.  “Uahirishe matendo yako maovu kwa kipindi kirefu kwani wewe unaweza kuyatenda popote pale utakapo penda (kwa hivyo kwa nini uwe na haraka ya kutenda?)”

 

1456.   “Uchukue mambo mema kutoka kila tawi la elime kama vile nyuki atafutavyo asali (utamutamu) kutoka kila ua  zuri.

 

1457.  “Kumbuka kwa chochote kile kilivyo kidogo ambacho umepatiwa na Allah swt  kitakuwa ni chenye manufaa zaidi na huduma zaidi kwako na ni yenye heshima kwa uwingi usio na maana. Uelewe vyema kuwa kiasi chochote kile mtu mwingine atakacho kukupatia ni sehemu mojawapo ya kiasi alichomjaalia Allah swt .”

 

1458. “Hasara uipatayo wewe kutokana na ukimya wako unaweza kufidiwa kwa urahisi, lakini hasara itakayotokana na kusema kupita kiasi na kusema ovyo itakuwa vigumu kuyarudia. Je hauoni kuwa njia iliyo bora ya kuyalinda maji katika bwawa ni kwa kuufunga mdomo wake ?” 

 

1459.  “Kulinda na kuhifadhi kile ulichonacho na kilicho chako ni afadhali kuliko kuomba na kutamani vile walivyonavyo wengine.”

 

1460.  “Marejeo yatokanayo na kazi za mikono au uhodari wa ufundi kwa njia ya heshima na utukufu ingawaje hata kama ikiwa ni kidogo, ni heri ya utajiri ambao wewe unaweza kuupata/kuulimbika kwa kufanya madhambi maovu.”

 

1461.  “Hakuna mhifadhi bora wa siri zako kuliko wewe mwenyewe.”

 

1462.   “Kwa mara nyingi mtu anajaribu kila njia kujipatia kitu ambacho ndicho chenye kumletea madhara yeye. Na mara nyingi mtu hujitakia mabaya ya madhara mwenyewe.”

 

1463.  “Yule aliyenatabia ya kusema sana, ndiye afanyaye makosa mengi.”

 

1464.  “Yule ambaye huwa na tabia ya kufikiri na kuyadhatiti mambo, huendeleza nguvu zake za kina na fikara na nuru ya macho.”

 

1465.  “Riziki inayopatikana kwa njia isiyo halali ni njia ovu kabisa ya kupata riziki.”

 

1466.  “Kwa kujijumuisha pamoja na awatu wema, wewe utaendeleza uwem katika tabia yako na kwa kujiepusha na makundi ya waovu, basi uwema ilivyo bora.”

 

1467.  “Iwapo huruma au upole wako utatokezea kutendwa kwa ukatili na uonevu basi ukomeshaji na kutilia mkazo mkali ndiyo huruma na uwema ilivyo bora.”

 

1468.  “Kamwe usitumainie uzushi kwani ndizo rasilimali za wajinga au wapumbavu.”

 

1469.  “Busara ndilo jina la mkondo wa kukumbuka uzoefu na kuitumia. Uzoefu uliyo bora zaidi ni ule ambao ukupatiao tahadhari iliyo bora na mawaidha yaliyo bora.”

 

1470.  “Kila mmoja ajaribuaye siye ndiye afanikiwae.”

 

1471. “Yeyote yule atakaeiaga (kufa) hii dunia, basi ajue kuwa  hatarudipo tena.”

 

1472.  Karibuni utakipata kile alichokuidhinishia Allah swt kwa ajili yako.”

 

1473.  Allah swt Amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Az-Zumar, 39 , Ayah 13 - 15 :

“Mimi naogopa adhabu ya siku kama nikimuasi Mola wangu.

Sema: “Namuabudu Allah swt kwa kumuitikadi kuwa yeye tu ndiye Allah swt .”

“Basi nyinyi abuduni mnachopenda kisichokuwa yeye.” (khiari yenu, lakini Allah swt atakulipeni tu); Sema: “Hakika watakao pata hasara ni wale walizotia hasarani nafsi zao na watu wao siku ya Qiyama. Angalieni! Hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.”

 


                             FADHAIL  ZA  IMAM  ALI  a.s.

 

1474. Kutokea ‘Ala, amesema yeye: “Mimi nilimwuliza ‘Aysha kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume s.a.w.w. kuhusu yeye.  ‘Ayesha alijibu, naye akasema kuwa ‘Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu.

 

1475.  Na kutoka ‘Ali ibn Abi Talib a.s., kasema: “Aliniambia Mtume Muhammad s.a.w.w.  ‘Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri’

 

1476. Na kutoka kwa Hudhaifa: “Alisema  Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa ‘ ‘Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri.’

 

1477.  Kutokea kwa  Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: “Alisema Mtume Muhammad s.a.w.w. , ‘uadui, chuki na bughudha dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki.’”

 

1478.  Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. akasema: “ Hakuna ampendaye ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa ni mumiin halisi, na hakuna amchukiaye ‘Ali isipokuwa ni kafiri.”

 

1479.  Na kutokea Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ,  alisema: “Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya ‘Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu ).”

 

1480.  Amesema Al-Imam  Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu a.s. kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii.”

 

1481.  Kutokea Ja’abir, anasema kuwa  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “ Ali ibn Abi Talib a.s. ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri.”

 

1482. Amesema Ibn ‘Abbas kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “ ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wa Hitta [38]   Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri.”

 

1483. Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu “ bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambay yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib a.s. , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1484.  Jami’ bin ‘Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza ‘Ayesha kuhusu daraja la ‘Ali ibn Abi Talib a.s. mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. ?  Yeye alijibu: “ Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w.”

 

Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib a.s. katika macho ya Mtume Muhammad s.a.w.w. . Alijibiwa kuwa “Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. .”

 

1485.  Na kutokea Ibn ‘Umar amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Bora wa mtu miongoni  mwenu ni ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na bora wa vijana wenu ni  Al - Hassan na Al -Husayn

 

1486.  ‘Urwah anaripoti kutoka ‘Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. “Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannam aunguzwe na moto.  ‘Aisha  akasema kuwa “Mimi niliisahau hadith hii siku ya (vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao.”

 

1487.  Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja’abir azungumze chochote kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. .  Ja’abir kasema: “’Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa bora miongoni mwa wanadamu.”  Mimi nilimwuliza tena “Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”  Yeye alinijibu: “Hakuna atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa kafiri.”

 

1488.  Hashim bin Barid alisema kuwa ‘Abdullah ibn Mas’ud alisema : “Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur’an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  na Surah za Qur’an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1489.  Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika  Masjid-i-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah  (laana za Allah swt ziwafikie juu yao )  na akapanda juu ya mimbar na akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib a.s.  kwa kusema: “Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib a.s. kwa mapenzi yake ba dala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake.” Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: “Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu” [39]  Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ?  Hapo Said alijibu: “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema.”

 

1490. Ummi Hani binti Abu Talib a.s. kasema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kasema kuwa: “Bora wa viumbe vya Allah swt  katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib a.s.  na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote.”

 

1491.  Ja’abir anasema kuwa “Hakuna anayeshuku fadhail za ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa “Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w.  isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1492.  Said bin Ja’abir alise kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn ‘Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na aliniambia kuwa nimchukue hapo.

 

Hivyo mimi nilimfikisha kwao.  Kufika hapo alisema “Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt ?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt  amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ?  Na kwa hakika hili limetokea” akasema.  Ndipo alipoendelea kusema: “Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema ‘Yeyote yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi amenikashifu mimi  na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu  Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake.” Na hapo ndipo  Ibn ‘Abbas aligeuka.

 

1493.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. : “Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  kwa dhikr ya ni dhikr zangu na dhikr zangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni ‘ibadah. Na mwenye kufanya ‘ibadah huingia Peponi.”

 

 


MAADILI YA ISLAM:

Nafs  aina na sifa zake

Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni faradhi. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: “Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi kwa hakika ametambua Allah.”

 

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa: “Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

 

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:

 

Hapana shaka kuwa mwanadamu hana nafs zaidi ya moja, lakini hii nafsi au  inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama ‘nafsi ya kujilaumu’ ‘au nafsi ya kuamrisha’ ‘nafsi inayotosheka’ (kama vile vielezwavyo katika Qu’rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

 

1494.  NAFSI SAFI AU THABITI (Thabit.)

 

Katika Qur’an Tukufu, Surah Ash Shua’raa, 26, Ayah 89, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-

“Isipokuwa mwenye kuja kwa Allah swt na moyo safi”

 

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

 

Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: “Moyo ulio msafi- halisi ni ule  ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt  tu”

 

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allah swt tu.

 

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa:

“Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake.”

 

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah swt  na wale wapendwao kwa ajili ya Allah swt (Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  na Ahali yake a.s.)

 

1495.  NAFSI YENYE KUTUBU (al-Nafs al- Muniib).

 

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni kutubu na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Allah swt, Qur’an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

“Anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu), na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt).”

 

Kuwa na khofu ya Allah swt pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah swt kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah swt imo ndani yake thabiti.

 

Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Allah swt yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah swt na wala haitorudi kamwe kwa Allah swt.

 

1496.  NAFSI MWONGOZI (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur’an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia:

“Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah swt. Na anayemuamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.”

 

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah swt, yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

 

1497.  NAFSI ILIYO RIDHIKA (al-Nafs al- Mutmai’na)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni kuridhika. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Ar-Raa’d, 13, Ayah 28

“ Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia.”

 

Na vile vile mwishoni mwa Qur’an Tukufu, Surah al-Fajr, 89, Ayah 28, twaambiwa:

“Ewe nafsi yenye kutua”!

“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika na umemridhisha.”

 

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah swt tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza kumghalibu na kumpotosha yeye.

 

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ma - Imamu a.s. waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

 

1498.  NAFSI YA TAHADHARI YA UADILIFU (al-nafs Al

Muttaqi ):

 

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na ) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali  hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu.

Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 32 :

“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayezihishimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.”

 

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha Taqwa kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allah swt na yale yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, shariah, waumini wake, Makkah, Al-Ka’abah Tukufu n.k. Kwa ufupi chochote kile kinachohusika na Allah swt huwa kina kuwa na umuhimu na

ta‘adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya  taqwa

 

1499.  NAFSI NYENYEKEVU (al- Nafs al- Mukhbit)

 

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu na uvumilivu, yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah swt

 

Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Qur’an Tukufu, Surah al Hajj, 22, Ayah 54:

“Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Allah swt anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka.”

 

Kwa sababu nyoyo hizi hujiinamisha chini mbele ya Allah swt na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allah swt nao kamwe hawavunji maamrisho ya Allah swt na wala hawazisaliti au kuzipinga.

 

1500.  NAFSI HALISI (al-Nafs al-Zakiyyah):

 

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au  iliyo mtakatifu. Katika Qur’an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 9-10, Allah swt anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akiisemea nafsi, anatuambia:

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)” 

 

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwa kuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele.

 

1501.  NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (al-Nafs al- Lawwama).

 

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu  hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa.

Qur’an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1-2,  inatuelezea:

“Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”.

 

Ni dhahiri kuwa iwapo Allah swt akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

 

1502.  NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (al-Nafs al-Mulham):

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Allah swt. Twaambiwa katika Qur’an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 8

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake” 

 

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- Nafsi halisi si ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah swt yatafikia kikomo chake.

 

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

 

1503.  NAFSI YENYE MADHAMBI (al-Nafs al-Aathima):

 

Iwapo nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi.

Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283 inazungumzia kulipa kwa amana:

“Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Allah swt, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi.  Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allah swt ni Mjuzi wa mnayo yatenda.”

 

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

 

1504.  NAFSI ILIYO SINZIA (al-Nafsal-Ghafil)

 

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah swt. Anaelezea Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

“Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka”

 

1505.  NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (al-Nafs al- Matbu’)

 

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho,Amesema Allah swt katika Quran: :

“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

 

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allah swt hadi kudharau na kutokubali ujumbe Wake na maamrisho ya Allah swt ambayo amemwekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo nafsi yake inaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athari yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimia kwa nafsi na kushindwa kwake.

 

1506.  NAFSI ILIYO POFUKA ( al-Nafs al- Amya):

 

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka.

Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22,

 Ayah 46:

“Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikia?  Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka.”

 

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah swt na hazimwoni Allah swt. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah swt na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

 

1507.  NAFSI YENYE MARADHI (al-Nafs al-Maridha):

     Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi. basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo.”

 

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Allah swt) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na Aakhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa anavutiwa navyo kama kwamba ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi iliyokwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

 

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Allah swt katika sala na kutii Sharia Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa hiyo nafsi wake imeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kusita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur’an Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga wa moyo, wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

 

1508.  NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (al-Nafs al-Za’igha):

 

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.

 

Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakumbwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Allah swt. i.e njia iliyonyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu

 

Katika Qur’an Tukufu, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Al I’mran, 3, Ayah 7:

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. lakini hawakumbuki hayo isipokuwa wenye akili.”

 

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih) wa aya za Qur’an Tukufu ili kuitumia Qur’an Tukufu kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

 

1509.  NAFSI YA MOYO MGUMU (al-Nafs al-Qasiya)

 

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili. Katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13

“Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt huwapenda wafanyao wema.”

 

Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu Surah Al H’adiid, 57, Ayah 16:

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu na wengine wao wakawa wapotovu.”

 

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

 

1510.  NAFSI WASIWASI (al-Nafs al-Murtaba):

 

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu ipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya Dini ya Islam kama vile kushuku kuwapo kwa Allah swt, Aakhera, Utume wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  na vile vile Uimamu (wa ma-Imamu a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.

 

Katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 45:

“ Wasio muamini Allah swt na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zina shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao.”

 

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza katika Ayah za Qur'an Tukufu na Ahadith Tufuku za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

 

 

1511.  NAFSI ILIYOPATA KUTU (al-Nafs-al-Ra’ina):

 

Kutu ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha nafsi ambavyo ni sehemu  umuhimu kwa ajili ya Allah swt utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza kurudishwa iwapo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Allah swt.

 

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Allah swt kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Allah swt, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia kutokana kwa Allah swt, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa maana yake. Qur’an Tukufu, Surah Al Mut’affifiin, 83, Ayah 14, ikiwa inatukumbusha kuwa:

 “Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.”

 

Katika aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba (Kipo kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia swala hili kwa marefu na mapana ) mara moja kwa  ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa:

“Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Allah swt’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

 

1512.  NAFSI AMURU (al-Nafs al- ‘Ammara):

 

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matendo ya madhambi bila kiasi. Katika Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 , kuhusu kisa cha Mtume Yussuf a.s., inazungumziwa Nafsi :

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.”

 

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Mtume Yussuf a.s.. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Mtume Yussuf a.s. alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile dhidi ya Mtume Yussuf a.s.. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Mtume Yussuf  a.s. au ni wote vyovyote vile, Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53, inatuambia kuwa:

 

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.”

 

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma’asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, ilimradi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na maana yake; na ile nafsi iliyo ilimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

 

HATIMAYE:

 

Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa Nafsi halisi na Nafsi ridhika n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya kupigwa mihuri au zilizopofuka na zenye maradhi zikiwa ni kama mifano.

 

Hali hii inadhihirisha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

 


 

1513.  Qur’an inatuambia katika, Sura  Ya-Sin, 36; Ayah 79:

Sema: “Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya ) kuumba”

 

1514.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

Kuwazulia uwongo Allah swt  na Mtume Muhammad s.a.w.w. ni Dambi Kuu (dhamb kabirah).”

                            

 


FADHAIL  ZA  IMAM  ALI  a.s.

 

1515. Kutokea ‘Ala, amesema yeye:

“Mimi nilimwuliza ‘Aysha kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume s.a.w.w. kuhusu yeye.  ‘Ayesha alijibu, naye akasema kuwa ‘Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu.”

 

1516.  Na kutoka ‘Ali ibn Abi Talib a.s., kasema:

“Aliniambia Mtume Muhammad s.a.w.w.  ‘Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri”

 

1517. Na kutoka kwa Hudhaifa:

“Alisema  Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa ‘ ‘Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri.”

 

1518.  Kutokea kwa  Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema:

“Alisema Mtume Muhammad s.a.w.w. , ‘uadui, chuki na bughudha dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki.’”

 

1519. Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. akasema:

“ Hakuna ampendaye ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa ni mumiin halisi, na hakuna amchukiaye ‘Ali isipokuwa ni kafiri.”

 

1520.  Na kutokea Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ,  alisema:

“Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya ‘Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu ).”

 

1521. Amesema Al-Imam  Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu a.s. kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii.”

 

1522.  Kutokea Ja’abir, anasema kuwa  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“ Ali ibn Abi Talib a.s. ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri.”

 

1523. Amesema Ibn ‘Abbas kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“ ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wa Hitta [40]   Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri.”

 

1524. Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu

“ bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambay yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib a.s. , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1525. Jami’ bin ‘Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza ‘Ayesha kuhusu daraja la ‘Ali ibn Abi Talib a.s. mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. ?  Yeye alijibu:

“ Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w.”

 

Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib a.s. katika macho ya Mtume Muhammad s.a.w.w. . Alijibiwa kuwa “Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. .”

 

1526.  Na kutokea Ibn ‘Umar amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

“Bora wa mtu miongoni  mwenu ni ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na bora wa vijana wenu ni  Al - Hassan na Al –Husayn”

 

1527. ‘Urwah anaripoti kutoka ‘Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. “Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannam aunguzwe na moto.  ‘Aisha  akasema kuwa

“Mimi niliisahau hadith hii siku ya (vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao.”

 

1528.  Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja’abir azungumze chochote kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. .  Ja’abir akasema:

“’Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa bora miongoni mwa wanadamu.”  Mimi nilimwuliza tena “Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”  Yeye alinijibu: “Hakuna atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa kafiri.”

 

1529.  Hashim bin Barid alisema kuwa‘Abdullah ibn Mas’ud alisema : “Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur’an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  na Surah za Qur’an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1530.  Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika  Masjid-i-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah  (laana za Allah swt ziwafikie juu yao )  na akapanda juu ya mimbar na akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib a.s.  kwa kusema:

“Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib a.s. kwa mapenzi yake ba dala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake.” Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: “Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu” [41]  Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ?  Hapo Said alijibu: “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema.”

 

1531. Ummi Hani binti Abu Talib a.s. kasema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kasema kuwa:

“Bora wa viumbe vya Allah swt  katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib a.s.  na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote.”

 

1532.  Ja’abir anasema kuwa “Hakuna anayeshuku fadhail za ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa

“Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w.  isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

1533.  Said bin Ja’abir alise kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn ‘Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na aliniambia kuwa nimchukue hapo.

 

Hivyo mimi nilimfikisha kwao.  Kufika hapo alisema

“Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt ?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt  amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ?  Na kwa hakika hili limetokea” akasema.  Ndipo alipoendelea kusema: “Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema ‘Yeyote yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi amenikashifu mimi  na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu  Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake.” Na hapo ndipo  Ibn ‘Abbas aligeuka.

 

1534.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. :

“Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  kwani dhikr zake ni dhikr zangu na dhikr zangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni ‘ibadah. Na mwenye kufanya ‘ibadah huingia Peponi.”

 

1535.   Amesema:

“Siri ya ufanisi ni hii, kwamba uhusiano wetu na wengine uwe wa mapenzi badala ya uhasama. Ikiwa mtu hawezi kufanya urafiki na watu wenye tabia nzuri, basi hataweza kabisa kuishi bila kuwa na fazaa!”

 

1536.   Mwanachuoni mmoja amesema:

“Maisha yetu ni kama eneo la milima ambapo ikiwa patapigwa ukelele mmoja, mtu atasikia mwangwi wake ukirudi kwake; hivyo, wale waliojawa na mapenzi ya wengine katika nyoyo zao, wataona hali kama hiyo kutoka kwao. Ni kweli kwamba maisha yetu ya kidunia yamesimama juu ya mabadilishano na malipano. Hatutaki kusema kwamba maisha yetu ya kiroho pia yamesimama juu ya msingi huohuo, lakini vipi inayumkinika kutaraji kuona uaminifu kutoka kwa wengine bila ya wewe mwenyewe kuwa mwaminifu kwao? Na vipi mtu atake apendwe na wengine bila yeye mwenyewe kwanza kuwapenda wao.?”

 

1537.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwakunjulia watu wote moyo wa mapenzi. Upendo wake mkubwa juu ya watu, upole na mvutio wake ulikuwa ukidhihirika kwenye uso wake wa kimalaika. Alikuwa akiwatendea vizuri na kuwakirimu Waislam wote sawasawa. Rawdhatu ‘l-Kafi, uk. 268.

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akiwashughulikia na akigawa wakati wake kati ya masahaba zake sawasawa.”

 

1538.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akikataza tabia mbovu, na alikuwa akisema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 371.

“Tabia mbaya ni kisirani, na mtu mwovu kabisa kati yenu ni yule mwenye tabia mbovu.”

 

1539.   Mahali pengine amesema: Wasa’ilu ‘sh-Shi’ah, jz. 2, uk. 222.

“Enyi wana wa Abdul Muttalib! Ninyi hamtaweza kamwe kuwaridhisha watu kwa mali zenu, hivyo kutaneni nao kwa uso mchangamfu na mwendo mzuri.”

 

1540. Aliyekuwa mtumishi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Anas bin Malik, alikuwa daima akikumbuka hulka nzuri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., na alikuwa akiwaambia watu kwamba katika kipindi cha miaka kumi aliyomtumikia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., hakuwahi kabisa kumwona ameukunja uso wake unaonawiri, wala hakuwahi hata mara moja kumwona amepandisha nyusi zake au ameonyesha uso wa hasira kwa sababu ya kufanya jambo lisilopendeza.

 

1541.   Tabia njema na uchangamfu ni katika sababu zinazozidisha umri wa mtu. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Wasa’ilu ‘sh-Shi’ah, jz. 2, uk. 221.

“Wema na tabia nzuri hustawisha ardhi na huzidisha umri.”

 

1542.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Mustadriku ‘l-Wasa’il, jz. 2, uk. 83.

“Tabia njema ni miongoni mwa ufanisi wa mtu.”

 

1543.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 279.

“Tabia nzuri hupanua riziki na huvuta (nyoyo za) urafiki.”

 

1544.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Watu wenye akili kamilifu kabisa ni wale wenye tabia nzuri kabisa.”

 

1545.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Wasa’ilu ‘sh-Shi’ah, jz. 2, uk. 221.

“Vitakavyowaingiza kwa wingi umma wangu katika Jannat ni ucha-Mungu na tabia njema.”

 

1546.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Jami’u ‘s-Sa’adaat, Jz. 2, uk. 28.

“Chukulia jambo la ndugu yako (wa imani) kwa maana nzuri kabisa mpaka ulione kinyume chake wala usilidhanie vibaya neno analolitoa ndugu yako wakati kuna uwezekano wa kuwa sahihi na kheri.”

 

1547.   Matunda mojawapo ya dhana nzuri ni kupatikana urafiki wa watu wa kuwepo mapenzi na usafi wa moyo. Amirul Muuminin Ali a.s. ametaja matokeo na matunda ya dhana nzuri katika maneno yake mbalimbali, amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 687.

“Mwenye kuwadhania vizuri watu hujifaidia mapenzi yao.”

 

1548.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 378.

“Dhana nzuri humwokoa mwenye kufuata madhambi.”

 

1549.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 376.

“Dhana nzuri ni raha ya moyo na usalama wa dini.”

 

1550.      Dhana nzuri humpunguzia mtu taabu na matukio mabaya. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 377.

“Dhana nzuri hupunguza majonzi.”

 

1551.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 680.

“Mwenye kuwa na matumaini juu yako huwa amekuamini na kukudhania vizuri, hivyo usiharibu dhana yake (ukamvunja moyo).”

 

1552.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 74.

“Dhana ya mtu ni mizani ya akili yake, na kitendo chake ni ushahidi wa kweli kabisa wa dhati yake.”

 

1553.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 676.

“Mwenye kutojali dhana mbaya juu ya ndugu yake, huwa ana akili timamu na moyo mtulivu.”

 

1554.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Usulu ‘l-Kafi, jz. 1, uk. 394.

“Miongoni mwa haki za muumin kwa muumin mwenzake ni……… kutomkadhibisha (kumsadiki).”

 

1555.   Qur'an Tukufu, Surah Al Hujaraat, 49, Ayah 12. inasema waziwazi kwamba dhana mbaya ni dhambi, na inawatahadharisha Waislamu wajiepushe na kudhaniana dhana mbaya:

Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya, kwani kuwadhani watu dhana mbaya ni dhambi.

 

1556.   Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Allah swt amewaharamishia Waislamu vitu vitatu: damu zao, mali zao, na kudhaniana vibaya.”

 

1557.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Nahju ‘l-Balaghah, uk. 1174.

“Si uadilifu kutoa hukumu kwa kutegemea dhana.”

 

1558.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 154.

“Jihadhari na kudhania vibaya, kwani dhana mbaya huharibu ibada na huifanya dhambi kubwa zaidi.”

 

1559.  Vile vile amesema kwamba kuwadhania vibaya watu wanyoofu ni aina moja ya udhalimu: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 434.

“Kumshuku mtu mwema ni dhambi mbaya kabisa na ni udhalimu unaochukiza sana.”

 

1560.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 698.

“Mwenye kutawaliwa na dhana mbaya hakubakii amani baina yake na rafiki yake.”

 

1561.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 433.

“Dhana mbaya hufisidi mambo na huchochea maovu.”

 

1562.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 152.

“Jihadhari na ghera (inayotokana na kushuku) mahali si pake, kwani humtia mzima maradhi na humshuku asiyekuwa na hatia.”

 

1563.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 835.

“Humwoni mwenye kushuku kuwa mzima.”

 

1564.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 712.

“Yule ambaye dhana yake si nzuri humwogopa kila mtu.”

 

1565.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 29.

“Nyoyo zina kumbukumbu mbaya ambazo huchukiwa na akili.”

 

1566.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk.80.

“Mwovu hamdhanii vizuri mtu mwingine kwa kuwa haoni kwake ila tabia yake mwenyewe.”

 

1567.   Qur’an Tukufu, Surah An-Nahl, 16, Ayah 105, inasema wazi kwamba mwongo yuko nje ya jamii ya Waislamu:

Wanaozua uwongo ni wale wasioziamini ayah za Allah swt, na hao ndio waongo (hasa)!”

 

1568.   Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 418.

“Halahala na ukweli, kwani ukweli huongoza kwenye wema, na wema huongoza kwenye Jannat. Mtu haachi kusema ukweli na kutafuta ukweli mpaka aandikwe ni mkweli mbele ya Allah swt. Na jihadharini na uwongo, kwani uwongo huelekeza kwenye ufisadi, na ufisadi huelekeza kwenye Moto. Mtu haachi kusema uwongo na kufuata uwongo mpaka aandikwe ni mwongo mbele ya Allah swt.”

 

1569.   Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 118.

“Watu wenye kuwasadiki upesi wengine ni watu wenye kusema kweli kuliko wengine; na watu wenye kuwakadhibisha zaidi wengine ni watu wenye kusema uwongo kuliko wote.”

 

1570.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 605.

“Lau vitu vingeainishwa (kwa ulingano wao), ukweli ungekuwa pamoja na ushujaa, na uwongo ungekuwa pamoja na uwoga.”

 

1571.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amejata matunda ya kusema kweli katika usemi mfupi huu: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 876.

“Msema kweli hujichumia vitu vitatu:

kuaminiwa,

kupendwa na

kuheshimiwa.”

 

1572.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Usulu ‘l-Kafi, jz. 1, uk. 460.

“Msidanganywe na sala na saumu zao, kwani huenda mtu akawa amezoea kusali na kufunga na endapo ataziacha ataona taabu. Hivyo, wajaribuni katika kusema ukweli na kuweka amana.”

 

1573.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 170.

“Tabia mbaya kabisa ni kusema uwongo.”

 

1574.   Al Imam Hasan Askari a.s. amesema: Jami’u ‘s-Sa’adaat, jz. 2, uk. 318.

“Maovu yote yamewekwa katika nyumba moja, na ufunguo wake ni uwongo.”

 

1575.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 146.

“Jihadharini na wanafiki, kwani wao ni wapotevu na wanapoteza (watu). Nyoyo zao zina maradhi lakini nyuso zao ni safi.”

 

1576.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 60.

“Maneno ya mnafiki ni matamu lakini moyo wake ni maradhi.”

 

1577.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ametoa taswira nzuri ya mnafiki kwa kusema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 562.

“Mfano wa mnafiki ni kama kondoo anayebabaika kati ya makundi mawili ya kondoo.”

 

1578.   Mtume Muhammad s.a.w.w. ametoa alama tatu za kauleni: Biharu ‘l-Anwar, jz. 15, uk. 30.

“Na mnafiki ana alama tatu:

anaposema husema uwongo,

anapotoa ahadi huvunja, na

anapoaminiwa hufanya hiana.”

 

1579.   Al Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: Biharu ‘l-Anwar, jz. 15, uk.172.

“Ni uovu mno kwa mja kuwa na nyuso mbili na ndimi mbili. Humsifu nduguye mbele yake lakini humsengenya nyuma yake. Akifanikiwa humwonea wivu, na akipata mashaka humtupa.”

 

1580.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 88.

“Mnafiki hujisifu mwenyewe na huwakejeli watu wengine.”

 

1581.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amemdondoa Luqman akimwusia mwanawe haya: Biharu ‘l-Anwar, jz. 15, uk. 30.

“Mnafiki ana alama tatu:

ulimi wake hukinzana na moyo wake,

moyo wake hukinzana na vitendo vyake, na

dhahiri yake hukinzana na batini yake.”

 

1582.   Mtu mmoja alimwuliza Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.:

Al-Wafi, jz. 3, uk. 106.

“Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniambia kwamba ananipenda sana. Vipi nitajua kama kweli ananipenda sana?” Imam a.s. akamjibu; “Tahini moyo wako. Ukimpenda, basi anakupenda. Tazama moyo wako. Ukimkataa mwenzako, basi mmoja wenu ana ila.”

 

1583.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 501.

“Dhamiri safi ni ushahidi bora zaidi wa ukweli kuliko lugha fasihi.”

 

1584.   Qur’an Tukufu, Surah Al Hujaraat, 49, Ayah 12, inatoa picha ya maana halisi ya usengenyaji katika jumla ndogo na fasihi:

Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?”

 

1585.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mimi nimetumwa kukukuzieni na kukukumilishieni maadili mema.”

 

1586.   Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 48.

“Ukiwepo katika baraza ambapo mtu mmoja husengenywa, basi

msaidie mtu huyo, au

wakataze wasengenyaji, au

ondoka hapo.”

 

1587.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju  ‘l-Fasahah, uk. 613.

“Mwenye kumtetea nduguye anayesemwa kwa ubaya wakati hayupo, hustahiki kwa Allah swt kuepushwa na Moto.”

 

1588.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema pia: Biharu ‘l-Anwar, jz. 16, uk. 179.

“Mwenye kumsengenya Mwislamu, Allah swt hatazikubali funga na sala zake za mchana na usiku arobaini mpaka asemehewe na msengenywa… Na mwenye kumsema Mwislamu katika Mwezi wa Ramadhani, hatapewa thawabu ya kufunga.”

 

1589.   Mtume Muhammad s.a.w.w. wa Waislamu amewasifu Waislamu kwa sifa hii:

“Mwislamu ni mwenye kuwasalimisha Waislamu kutokana na mikono na ulimi wake.”

 

1590.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 36.

“Kumsengenya ni juhudi za mtu dhaifu.”

 

1591.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Al-Kafi, jz. 2, uk. 247.

“Yatakikana muumin awe ni kiburudisho cha (roho ya) muumin (mwenzake) kama vile maji baridi yanavyokata na kutuliza kiu.”

 

1592.   Al Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: Al-Kafi, jz. 2, uk. 459.

“Inatosha kuthibitisha aibu ya mtu anayeona aibu za watu wengine bila ya kuona yake mwenyewe, au anayewagombeza watu jambo ambalo yeye mwenyewe anashindwa kuliacha, au anayemwudhi rafiki yake kwa jambo lisilomhusu.”

 

1593.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameonyesha nukta muhimu juu ya maudhui hii pale aliposema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 558.

“Mtu bora kuliko wote mbele yako ni yule mwenye kukuonyesha aibu zako na kuisaidia nafsi yako.”

 

1594.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 659.

“Mwenye (kutaka) kutafuta aibu za watu, aanze na zake.”

 

1595.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 559.

“Inatosha mtu kujifanya mpumbavu mwenyewe kwa kutazama aibu za watu wengine huku akizificha zake.”

 

1596.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema maneno matamu na yenye kuvutia kuhusu utambuaji na utibabu wa maradhi ya kinafsi kwa njia ya mtu mwenyewe kujichungua: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 448.

“Ni lazima kwa mwenye akili kuichungua nafsi yake na kuziona dosari zake katika dini, maoni, maadili na adabu; kisha azikusanye (azihifadhi) katika kitabu na achukue hatua ya kuziangamiza.”

 

1597.   Qur’an Tukufu, Surah An-Nisaa, 4, Ayah 32, inasema:

Wala msitamani vile ambavyo Allah swt amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine.”

 

1598.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Mustadraku

‘l-Wasa’il, jz. 2, uk. 428.

“Asili ya kijicho ni upofu wa moyo na ukanyaji wa fadhila na neema za Allah swt. Sifa hizo ni mabawa mawili ya ukafiri. Kijicho humtia mwanadamu katika uchungu wa daima na humwangamiza kabisa kabisa asiokoke kamwe.”

 

1599.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema” Nahju ‘l-Fasahah, uk. 366.

“Watendeeni sawasawa watoto wenu mnapowapa zawadi.”

 

1600.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ametaja madhara ya kimwili ya kijicho: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 494.

“Naustaajabia mghafala wa mahasidi juu ya uzima wa miili yao.”

 

1601.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk.32.

“Kijicho huuangamiza mwili.”

 

1602.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 141.

“Jihadharini na uhasidi, kwani huitia ila nafsi.”

 

1603.   Al Imam Zaynul Abidin a.s. alimwomba Allah swt hivi: Sahifah Kamilah, dua ya 22.

“Ewe Allah swt ! Teremsha rehema na baraka kwa Muhammad na Aali za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.; na nipe kifua kilichohifadhika na uhasidi, ili kwamba nisimwonee wivu yoyote kati ya viumbe Vyako juu ya fadhila Zako; wala nisione kijicho juu ya neema Zako ulizompa yeyote kati ya viumbe Vyako – ziwe ni neema za dini au dunia, afya au takwa, nyingi au nyepesi, ila kwamba nitamani bora zaidi kwa ajili yangu lakini kutoka Kwako peke Yako, (Ewe) usiye na mshirika.”

 

1604.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 355.

“Shindaneni katika maadili yanayovutia, matumaini makubwa na mawazo matukufu ili mpate jazaa kubwa.”

 

1605.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Lau Allah swt angeruhusu kiburi kwa waja wake, basi angewaruhusu Manabii na Mawalii Wake. Lakini Allah swt amewakataza kuwa na kiburi na amewaridhia kuwa na unyenyekevu. Hivyo, huweka videvu vyao juu ya ardhi (kumnyenyekea Allah swt), huzisugua nyuso zao kwenye ardhi, na huwanyenyekea waumini.”

 

1606.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fusahah, uk. 12.

“Jiepusheni na kiburi, kwani mja anapotakabari, Allah swt husema: ‘Mwandikeni mja huyu miongoni mwa waasi.’”

 

1607.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ametaja kwa ufupi asili ya kinafsi ya ndweo na majivuno: Al-Kafi, jz. 3, uk. 461.

“Hakuna mtu anayeugua kiburi ila kwamba amehisi uduni (dhila) nafsini mwake.”

 

1608.   Al Imam Musa bin Jaafar a.s. amesema: Wasa’ilu ‘sh-Shi’ah, jz.1, uk. 74.

“Maringo na majivuno yana vidato; kimojawapo ni kumpambia mja amali yake mbaya akaiona nzuri na akaipenda na kufikiria kwamba amefanya vizuri.”

 

1609.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 147.

“Jihadhari na kujipenda (kujiona) mwenyewe, kwani utazidiwa na wenye kukuchukia.”

 

1610.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk 26.

“Kiburi huharibu akili.”

 

1611.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 651.

“Mwenye kudhoofisha fikra zake huimarisha ghururi yake.”

 

1612.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 102.

“Unyenyekevu ni kiini cha akili, na majivuno ni kiini cha ujinga.”

 

1613.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 478.

“Kibur ni maradhi ya ndani.”

 

1614.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 677.

“Mwenye kuona bora mwendo wake, hushindwa kurekebisha nafsi yake.”

 

1615.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 95.

“Mwenye kujipenda nafsi yake haoni aibu zake, na lau angejua mema ya wengine angetengeneza dosari na hasara zake.”

 

1616.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk.138.

“Jikingeni kwa Allah swt kutokana na ulevi wa utajiri, kwani una nishai (ulevi) inayochelewa kutoka.”

 

1617.   Siku moja tajiri mmoja alikwenda katika baraza la Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Baadaye akaja maskini mmoja na akakaa karibu na tajiri huyo. Tajiri akakusanya nguo zake alipomwona maskini amakaa ubavuni mwake. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia tajiri:

“Unaogopa umaskini wake ukuguse?”

Tajiri akajibu: “Hapana!”

Akamwuliza: “Unaogopa sehemu ya mali yako aipate yeye?”

Akajibu: “Hapana!”

Akamwuliza: “Unaogopa nguo zako ziingie uchafu?”

Akajibu: “Hapana!”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuliza: “Basi kwa nini umezikusanya nguo zako na umekikunja kipaji chako?”

 

Tajiri akasema: “Ewe mtume wa Allah swt! Utajiri wangu na mali zangu zimenifumba macho yangu nisitambue uhakika, na zimenifanya niyaone mazuri yale mabaya yangu. Kwa kufuta kosa hilo lisilofaa, natoa nusu ya mali zangu kumpa maskini huyu.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuliza maskini: “Je, unaikubali tuzo hiyo?”

 

Maskini akakataa, na alipoulizwa sababu yake, akasema: “Naogopa nami pia nisiwe na sifa mbaya kama yake baada ya kuwa na utajiri mwingi.”

 

1618.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 66.

“Wafanyieni uadilifu watoto wenu katika kutoa zawadi kama vile mtakavyopenda wakufanyieni uadilifu kwa mema na mapenzi.”

 

1619.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 8.

“Mcheni Allah swt na adiliana na watoto wenu kama vile mpendavyo wakutendeeni wema.”

 

1620.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Nahaj ‘l-Balaghah, uk. 877.

“Wafanyie (Wamisri) uadilifu, endeana nao kwa upole, changamka nao, na fanya insafu katika kuwatazama pia ili kwamba watukufu wasitazamie dhuluma kutoka kwako wala wanyonge wasikate tamaa ya kuona uadilifu kutoka kwako.”

 

1621.   Mabalozi wa Allah swt ni waasisi wa uadilifu na waratibu wa sera ya ukamilifu wa mwanadamu. Katika zama za ukhalifa wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., siku moja Aqil alikwenda kwa ndugu yake mtawala (yaani Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ). Baada ya kumwelezea matatizo yake na umaskini wake, akamshika nduguye (Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.) ampe karibu mani moja (ratili mbili) ya ngano zaidi kuliko sehemu yake kutoka Baitul Maal (Hazina). Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. badala ya kumkubalia akamsogezea kipande cha chuma kilichopashwa moto ili kumwonya. Aqil akapiga kelele. Hapo Imam a.s. akamwambia:

“Ewe Aqil! Mamako akulilie! Unapiga kelele hivyo kwa kuogopa kipande cha chuma tu kilichopashwa moto na mtu, lakini mimi nitavumilia vipi moto utakaowashwa kwa ghadhabu za Allah swt ? Je, inafaa wewe upige kelele kwa sababu ya kuungua mwili, nami nivumilie adhabu ya roho?”

 

Baada ya ya kusema hayo, akaongeza:

“Wallahi! Hata kama nitapewa dunia nzima pamoja na utajiri wake wote ili kwamba nimnyang’anye siafu ganda la shayiri alilonalo mdomoni mwake, sitafanya hivyo kamwe! Mimi ni duni na haina thamani kuliko ganda hilo hata kutaka kumuudhi siafu.”

 

1622.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 537.

“Kutosamehe ni aibu mbaya kuliko zote, na kulipiza kisasi ni dhambi kubwa kuliko zote.”

 

1623.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amewasifu waungwana wanasamehe makosa ya wengine, kwa kusema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk.768.

“Ni murua wa watukufu kusamehe makosa kwa haraka.”

 

1624.   Mambo mazuri na mabaya hayawi kamwe sawasawa katika dunia hii. Hivyo, ni afadhali kulipa ubaya kwa amali njema kabisa ili kwamba yule aliyekufanyia ubaya na uadui awe ni rafiki yako wa karibu.

     

Msamaha huwa na thamani kubwa sana wakati mtu anapokuwa na uwezo na nguvu za kulipiza. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameihesabu sifa hii tukufu kuwa ni miongoni mwa sifa njema za Mitume na wachaji: Safinatu ‘l-Bihar, jz. 2, uk. 702.

“Msamaha wakati wa (kuwepo) uwezo (wa kulipiza ubaya) ni miongoni mwa mienendo ya Mitume na wacha-Mungu.”

 

1625.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameutaja msamaha kama ni silaha bora kabisa ya kuwapigia wapinzani: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 1150.

“Mlaumu nduguyo kwa (kumfanyia) mema, na jiepushe na shari yake kwa kumfadhili.”

 

 

1626.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amefichua uhakika wa ndani wa maana ya kinyongo na chuki kwa kutoa usemi mfupi: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 178.

“Moyo wa mwenye kinyongo ni mgumu kuliko nyoyo zote.”

 

1627.   Wakati wa adhabu ya roho daima humtesa mwenye chuki. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 85.

“Kinyongo huadhibu nafsi na huzidisha adhabu yake.”

 

1628.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 490.

“Dhamiri zinapotibiwa ndipo siri zinapojitokeza na kuonekana.”

 

1629.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 106.

“Chuki ni moto wa ndani ndani usiozimika ila kwa ushindi.”

 

1630.   Chuki hukoka moto wa hamaki. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 21.

“Chuki huwasha hasira.”

 

1631.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 666.

“Mwenye kuondoa chuki hutuliza moyo na akili yake.”

 

1632.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 399.

“Mja mwenye furaha ni yule ambaye moyo wake hauna chuki wala wivu.”

 

1633.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Usulu ‘l-Kafi, jz. 2, uk. 305.

“Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kuidhibiti hamaki yake hawezi kuitawala akili yake.”

 

1634.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 625.

“Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake.”

 

1635.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto.”

 

1636.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru

‘l-Hikam, uk. 71.

“Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake), na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo.”

 

1637.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ametuusia tuwe na subira na uvumilivu ili tuweze kukabiliana na hasira na hamaki, kwa sababu tunavihitajia hivyo kuepukana na maumivu yake. Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 133.

“Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia.”

 

1638.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 463.

“Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo.”

 

1639.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema: Al-Wafi, jz. 3, uk. 148.

“Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Mungu.?”

 

1640.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ametoa mwongozo mzuri wa kufanya wakati mtu anapopandwa na hamaki: Ahyau

‘l-Ulumu ‘d-Din, jz. 3, uk. 151.

“Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge-kwani moto hauzimiki ila kwa maji.”

 

1641.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema: Al-Kafi, jz. 2, Uk. 162.

“Allah swt hakumruhusu mtu yeyote kwenda kinyume katika mambo matatu:

·         Kuweka amana ya mwema au mwovu;

·          kutimiza ahadi ya mwema au mwovu; na

·          kuwatendea mema wazazi wema au waovu.”

 

1642.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ametaja kuvunja ahadi kama ni alama mojawapo ya unafiki: Biharu ‘l-Anwar, jz. 15, uk. 234.

“Mwenye kuwa na sifa nne (zifuatazo) ni mnafiki; na hata akiwa nayo mojawapo kati ya hizo pia atasifika kwa unafiki isipokuwa aiache:

·         Mwenye kusema uwongo anapozungumza;

·          mwenye kuvunja ahadi anapoahidi;

·         mwenye kufanya hiana anapoaminiwa; na

·         mwenye kufisidi anapogombana.”

 

1643.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameandika: Mustadriku

‘l-Wasa’il, jz. 2, uk. 85.

“Jihadhari usiwasimange raia zako kwa hisani ulizowafanyia, wala usijione bora kwa ajili ya kazi unazowafanyia, na unapowaahidi usiende kinyume na ahadi zako. Hakika masimango huharibu hisani, na kujiona huondoa nuru ya haki, na kuvunja ahadi husababisha kuchukiwa na Allah swt na watu. Allah swt anasema: katika Qur’an Tukufu, Surah Ass’af, 61, Ayah 3

‘Ni chukizo kubwa mbele ya Allah swt kusema msiyoyatenda.’”

 

1644.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 228.

“Kutimiza ahadi hufuatana na uaminifu, nami sikijui kinga kinachokinga vizuri zaidi kuliko kutimiza ahadi.”

 

1645.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l Fasahah, uk. 201.

“Mtu asimwahidi mwanae asipoweza kutimiza.”

 

1646.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameonyesha namna ya mtu kusuhubiana na mwenzake: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 323.

“Ukimchagua mtu kuwa rafiki yako, basi kuwa mtumishi wake na mwonyeshe uaminifu wako wa kweli na moyo safi.”

 

1647.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mwenye furaha kayaya kuliko watu wote ni yule mwenye kuingiliana na watu watukufu na ambaye huendeana na watu bila ya kuwadhulumu, huzungumza nao bila ya kuwadanganya, na huahidiana nao bila ya kuvunja. Hakika mtu kama huyu amekamilisha murua wake, amedhihirisha uadilifu wake, na anastahiki udugu na urafiki wake.”

 

1648.   Allah swt amezitaja sheria alizowatungia waja wake kama ni amana, na amekataza kabisa kufanya khiana ya aina yoyote: katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Anfaal, 8, Ayah 27,

Enyi mlioamini! Msimfanyie khiana Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mkakhini amana zenu na hali mnajua.

 

1649.   Vile vile Allah swt amesema: katika Qur’an Tukufu, Surah An-Nisaa, 4., Ayah 58,

Hakika Allah swt anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenyewe.

 

1650.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 505.

“Ukomo cha khiana ni kumfanyia khiana rafiki mpendwa na kuvunja ahadi.”

 

1651.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 446.

“Mtu mwovu kuliko wote ni yule asiyeamini kuweka amana wala hajizuii kufanya khiana.”

 

1652.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 150.

“Jihadharini na khiana kwani ni dhambi mbaya kabisa; na kwamba mwenye kukhini ataadhibiwa katika Moto kwa khiana yake.”

 

1653.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Safinatu ‘l-Bihar, jz. 1, Uk. 41.

“Halahala na kusema ukweli na kurejesha amana kwa mwema au mwovu, kwani sifa mbili hizi ni ufunguo wa riziki.”

 

1654.   Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Amali as-Sadaq, uk. 149.

“Halahala na kuweka amana. Naapa kwa yule aliyembaathi Muhammad kwa haki kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., kwamba lau mwuaji wa babangu Husayn bin Ali angenipa upanga ule aliomwulia bababngu, kumwekea amana, nisingemfanyia khiana.”

 

1655.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, Uk. 592

“Mwenye kutenda kitendo kiovu atalipwa (hapahapa) duniani.”

 

1656.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 453.

“Uaminifu katika (kuweka) amana ni alama ya usafi wa mwenye imani.”

 

1657.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru

‘l-Hikam, uk. 53.

“Khiana ni dalili ya upungufu wa uchaji na utovu wa dini.”

 

1658.   Al Imam Sajjad a.s. amesema: Al-Wafi, uk. 127.

“Una wajibu wa kumlea (Mwanao) kwa adabu nzuri, kumwongoza kwa Mola wake Mtukufu, na kumsaidia katika kumtii.”

 

1659.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 224.

“Wenye akili huhitajia adabu kama vile shamba linavyohitajia mvua.”

 

1660.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, uk. 549.

“Hakuna jambo linalochukiwa mno katika Uislamu kama uchoyo.”

 

1661.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, uk. 81.

“Mwenye kuwa na raha kidogo kabisa kati ya watu wote ni bakhili.”

 

1662.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, uk. 81.

“Allah swt amrehemu mtu anayebana mengi (ziada) ya maneno yake, na anayetoa ziada ya mali yake.”

 

1663.  Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju ‘l-Fasahah, uk. 8.

“Jihadhari na uchoyo, kwani uchoyo umewaangamiza waliokutangulia, umewafanya wamwage damu zao, na wahalalishe yaliyoharamishwa.”

 

1664.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 497.

“Nashangaa juu ya bakhili mwovu; huuharakisha umaskini anaokimbia na huupoteza utajiri anaotafuta. Huishi katika dunia maisha ya maskini na atahukumiwa katika Akhera kwa hesabu ya matajiri.”

 

1665.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 368.

“Ukarimu wa mtu huwafanya maadui zake wampende, na ubakhili wake humfanya achukiwe na watoto wake.”

 

1666.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 488.

“Uroho na uchoyo umesimama juu ya msingi wa shaka na kutoaminiwa.”

 

1667.   Al Imam Musa al-Kadhim a.s. ameelezea juu ya thamani ya ukarimu: Furu’ al-Kafi, jz. 4, uk. 38.

“Karimu mwenye murua yuko katika ulinzi wa Allah swt; na Allah swt hamwachi mpaka amtie Peponi. Allah swt hamtumi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wala Wasii yeyote ila kwamba huwa ni karimu; wala hakutokea mwema yeyote ila kwamba alikuwa karimu. Babangu hajafariki mpaka aliponiusia ukarimu.”

 

1668.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. ameshabihisha maisha ya mroho na taswira hii: Usulu ‘l-Kafi, Babu ya Huba ya Dunia.

“Mfano wa mwenye tamaa ya dunia ni kama kiwavi cha nondo, kila akizidi kujizungushia nyuzi (za hariri) ndivyo hujifungia mpaka kufa kwa kujisonga roho.”

 

1669.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, uk. 199.

“Jihadharini na uchu wa mali, kwani uliwaangamiza waliokutangulieni. Uchu uliwashawishi mabakhili na wakafanya ubakhili; uliwaamrisha kukata ujamaa na wakakata; na uliwaamrisha ufisadi na wakafanya ufisadi.”

 

1670.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 135.

“Epukaneni na mwenye tamaa, kwani kuingiliana naye huleta udhalili na mashaka.”

 

1671.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 50.

“Mwenye tamaa ni mfungwa wa udhalili na kifungo chake hakifungiki.”

 

1672.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameashiria jambo hili kwa usemi murua: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 255.

“Mtukufu kuliko wote ni yula ambaye hukata tamaa (juu ya watu), hushika ukinaifu na uchaji, na huacha uroho na tamaa, kwani tamaa na uroho ni sawa na umaskini, na kukata tamaa (juu ya watu) na ukinaifu ni utajiri wa dhahiri.”

 

1673.   Anayejifanya mtumwa wa tama na uchu, huutia maradhi mwili na roho yake. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema: Ghuraru

‘l-Hikam, uk. 544.

“Kila mwenye tamaa ni mgonjwa.”

 

1674.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema; Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 77.

“Tamaa huchafua nafsi, huharibu dini (imani) na huondoa uungwana.”

 

1675.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ametaja matatizo yanayotokana na tamaa: Mustadriku ‘l-Wasa’il, jz. 2, uk. 435.

“Mwenye tamaa husumbuliwa na matatizo saba mabaya:

1.                  Fikra inayomdhuru mwili wake na isiyomnufaisha;

2.                  hamu (hima) isiyokwisha;

3.                  tamaa isiyompa raha ila baada ya kufa na wakati wa

                   kupumzika huona taabu zaidi;

4.                  hofu isiyoacha kumhangaisha;

5.                  huzuni inayofanya maisha yake machungu bila ya kuwa

                   na faida;

6.                  hesabu isiyomsalimisha na adhabu ya Allah swt ila

                  asemehewe na Allah swt; na

7.                  adhabu asiyoweza kuikimbia wala kuiepuka.”

 

1676.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru ‘l-Hikam, uk. 16.

“Tamaa humsukuma mtu kwenye mabaya.”

 

1677.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. vile vile amesema: Ghuraru

‘l-Hikam, uk. 360.

“Matokeo ya tamaa ni kumtia mtu katika aibu.”

 

1678.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Nahju

‘l-Fasahah, uk. 633.

“Miongoni mwa (alama za) uungwana ni mtu kunyamaza kimya na kumsikiliza ndugu yake anaposema.”

 

1679.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Na jifunze kusikiliza vizuri kama vile unavyojifunza kusema vizuri, wala usimkatize mtu yeyote anaposema.”

 

1680.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Safinatu ‘l-Bahar, jz. 2, uk. 522.

“Mja hataipata imani halisi mpaka atakapoacha ubishi hata kama ni haki.”

 

1681.   Al Imam Had a.s. amesema:

“Ubishi huharibu urafiki wa muda mrefu, huvunja uhusiano ulio madhubuti, na sehemu ndogo ya kitu kinachopatikana ni mashindano – na mashindano yenyewe ni chanzo hasa cha kutosikilizana.”

 

1682.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: Usulu ‘l-Kafi, jz. 1, uk. 452.

“Epukaneni na mabishano, kwani huunguza moyo, huleta unafiki na husababisha chuki.”

 

1683.   Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema, "Hakika,miongoni mwa dalili za saa, ni kuwa

1.      watu watapuuza sala

2.      watafuata matamanio yao wenyewe

3.      wataelekeza kujipendelea wao wenyewe, watawaheshimu matajiri,

4.      na watauza Dini yao kwa manufaa ya kidunia

5.      wakati huo roho na moyo wa Muumin itayayuka (kwa huzuni) kama chumvi inavyoyayuka katika maji, kwa sababu ataona mambo yaliyoharamishwa na hataweza kuyabadili."

 

Salman akasema: "Haya yatatokea, ewe Mtume wa Allah swt?"

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo, naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

 

"Ewe Salman,

6.      wakati huo watawala watakuwa wadhalimu

7.      Mawaziri watakuwa waasi,

8.      na wadhamini (wale waliopewa amana kwa kuaminiwa) watafanya hiana,

9.      hakika wakati huo maovu yatakuwa mema na mema yatakuwa maovu,

10.  wale wafanyao hiana wataaminiwa na waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;na mwongo atasadikiwa,na msema kweli atahesabiwa mwongo.

11.  Wakati huo kutakuwapo na utawala wa wanawake,

12.  Masuria watashauriwa,

13.  na watoto watakaa juu ya mimbar,

14.  udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu

15.  na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini;na mateka ya vita (yaani mali ya ummah) yatakuwa kama ni mali ya mtu binafsi;na mtu atakuwa mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema kwa marafiki zake,

16.  na wakati huo kutatokea na nyota zenye mikia (comets)."

 

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?"

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake."

 

"Ewe Salman!

17.  wakati huo mwanamke atakuwa mshiriki wa mumewe katika biashara,

18.  na mvua itakuwa moto sana

19.  na watu wema watabaki katika huzuni;na masikini hawata heshimiwa;na wakati huo masoko yatakaribiana,

20.  Tena huyu atasema,"Mimi sikuuza chochote,na yule atasema, "Mimi sikupata faida yoyote." Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote asiyemlalamikia Allah swt.

 

"Ewe Salman!

21.  tena itatokea iwapo watu watawazungumzia watawala wao, watawaua, na ikiwa watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali yao, watanyimwa heshima zao,watamwaga damu yao na mioyo ya watu itajaa woga;kisha hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga,mwenye khofu,ametishika na ameshstushwa”

 

"Ewe Salman!

22.  Bila shaka wakati huo mambo fulani yataletwa kutoka Mashariki

23.  na mambo fulani yataletwa kutoka Magharibi,

24.  Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) katika Ummah wangu kutokana na hayo; Ole ya Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na huruma juu ya wadogo wao,wala hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa.Miili yao  itakuwa  ya wanadamu,lakini mioyo yao itakuwa ya mashetani."

 

"Ewe Salman!

25.  Wakati huo wanaume watawaashiki wanaume,

26.  na wanawake watawaashiki wanawake;

27.  na watoto wa kiume watapambwa kama wanawake;

28.  na wanaume watajifanya kama wanawake

29.  na wanawake wataonekana kama wanaume;

30.  na wanawake watapanda mipando

31.  Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt juu ya wanawake wa Ummah wangu."

 

"Ewe Salman!

32.  Bila shaka wakati huo Misikiti itapambwa (kwa dhahabu n.k.) kama inavyofanywa katika masinagogi na makanIssa,

33.  na Qur’an zitapambwa (kwa nakshi na rangi za kupendeza n.k.)

34.  na minara (ya misikiti) itakuwa mirefu;na safu za watu wanaosimama katika sala zitazidi,lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao yatatofautiana."

 

"Ewe Salman!

35.  Wakati huo wanaume watatumia mapambo ya dhahabu;kisha watavaa hariri,na watatumia ngozi za chui."

 

"Ewe Salman!

36.  Wakati huo riba itakuwako,

37.  na watu wata- fanyia biashara kwa kusemana na rushwa

38.  na dini itawekwa chini,na dunia itanyanyuliwa juu."

 

"Ewe Salman!

39.  Wakati huo talaqa zitazidi

40.  na mipaka ya Allah swt hayatasimamishwa

41.  Lakini hayo hayatamdhuru Allah swt."

 

"Ewe Salman! 

42.  Wakati huo watatokea wanawake waimbaji,

43.  na ala za muziki

44.  na wabaya kabisa watawatawala Ummah wangu."

 

"Ewe Salman!

45.  Wakati huo matajiri katika Ummah wangu watakwenda Kuhiji kwa matembezi,na walio wastani kwa biashara,na masikini kwa kujionyesha.

46.  Hivyo basi wakati huo watakuwapo watu ambao watajifundisha Qur’an si kwa ajili ya Allah swt na wataifanya Qur’an kama ala ya muziki.

47.  Na watakuwapo watu ambao watasoma dini si kwa ajili ya Allah swt 

48.  na idadi ya wanaharamu itazidi 

49.  watu wataiimba Qur’an,

50.  na  watu watavamiana kwa uroho wa kidunia."  

 

"Ewe Salman!

51.  Haya yatatokea wakati heshima zitakapo- ondoka,na madhambi yatatendwa

52.  na watu waovu watakuwa na uwezo juu ya watu wema,

53.  na uongo utaenea na mabishano (matusi) yatatokea

54.  na umasikini utaenea,

55.  na watu watajiona kwa mavazi yao

56.  na itakuwepo mvua wakati si wake

57.  na watu watacheza dama, kamari na Ala za muziki,

58.  na hawatapenda kuhimizana mema wala kukatazana maovu

59.  na kwa ajili hali itakavyokuwa hata itafikia wakati huo kuwa Muumin atakuwa na heshima ndogo kuliko hata mjakazi

60.  na wanaosoma na wanaotumia wakati wao katika kumwabudu Allah swt watalaumiana.

61.  Hao ndio watu watakaoitwa wachafu na wanajisi katika Ufalme wa mbinguni."

 

"Ewe Salman!

62.  Wakati huo matajiri hawataogopa chochote isipokuwa mtu masikini; hadi kwamba masikini wataendelea kuomba kati ya ijumaa mbili,na hawatamwona mtu yeyote wa kutia chochote mikononi mwao."

 

"Ewe Salman!

63.  Wakati huo itazungumzwa Ruwaibidhah."

 

Salman akauliza:"Ni nini Ruwaibidhah ? Ewe Mtume wa Allah swt, baba na mama yangu wawe fidia kwako."

 

Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akajibu:

64.  "Watu fulani watazungumza kuhusu mambo ya watu ambayo hayakuwahi kuzungumzwa namna hii zamani.

65.  Tena baada ya muda mchache machafuko yatatokea duniani,na kila nchi itafikiri kuwa machafuko yapo katika nchi yao tu."

66.  "Watabaki katika hali hiyo kwa muda ambao Allah swt atapenda wabaki;

67.  kisha ardhi itatapika vipande vya moyo wake dhahabu, fedha na madini mengineyo; (Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.) alinyosha kidole chake penye nguzo, na akasema: "Kama hizi (kwa ukubwa), lakini siku hiyo dhahabu wala fedha hazitamsaidia mtu yeyote. Na hii ndiyo maana ya maneno ya Allah swt 'Hakika dalili Zake zimekuja.'[42]

 

1684.   UBASHIRI WA IMAM JAAFER AS-SADIQ  A.S. 

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq a.s. ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam,Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran.

Imam a.s. alisema:

1 "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki hawatapatikana.

4.      Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.

5.      Kufuata Qur’an kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.

6.      Zitatolewa maana ya Aya za Qur’an kwa mujibu wa matakwa ya watu,hivyo mafhum ya Qur’an itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.

7.      Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.

8.      Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.

9.      Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.

10.  Ulawiti utakuwa ni jambo la kawaida.

11.  Muumin  atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa

12.  Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.

13.  Huruma itakuwa imepotea kabisa.

14.  Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.

15.  Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume wenzao.

16.  Wanawake watawaoa wanawake wenzao.

17.  Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.

18.  Starehe, anasa na zinaa zitashamiri.

19.  Zinaa itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.

20.  Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.

21.  Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.

22.  Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza  fitina na yale wanayozusha.

23.  Ushauri mzuri utakanwa.

24.  Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.

25.  Al-Kaaba haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.

26.  Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah kuhiji.

27.  Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.

28.  Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.

29.  Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao.

30.  Na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara kuma zao.

31.  Wanawake wataunda vilabu vyao,mashirika na umoja wao.

32.  Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.

33.  Wanaume watajirembesha kama wanawake.

34.  Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli.
Na Banu Abbas watalipia ulawiti.

35.  Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume watakuwa hivyo hivyo.

36.  Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.

37.  Riba ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.

38.  Ushahidi wa uongo utakuwa ukIssadikiwa mno.

39.  Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.

40.  Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.

41.  Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.

42.   Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.

43.  Rushwa ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.

44.  Wanaume wata walawiti wake zao.

45.  Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.

46.  Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawake.

47.  Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa.

48.  Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.

49.  Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.

50.  Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa  ulimini.

51.  Pombe na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.

52.  Wanawake wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri,ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.

53.  Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.

54.  Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.

55.  Usomaji na usikilizaji wa Qur’an utakuwa ni bughudha kwa watu.

56.  Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.

57.  Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.

58.  Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.

59.  Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.

60.  Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.

61.  Misikiti itarembeshwa kwa dhahabu.

62.  Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.

63.  Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.

64.  Kumwaga damu ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.

65.  Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi mabaya ili kuwatishia watu wengine.
Imam a.s. aliendelea kusema:

66.  "Watu watakuwa wakipuuzia sala na kutojali.

67.  Watu hawatakuwa wakilipa zaka ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.

68.  Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.

69.  Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

70.  Watu watakuwa wakIssali katika mavazi ya kiajabu.

71.  Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.

72.  Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.

73.  Watu watasali kwa kuonyesha tu.

74.  Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.

75.  Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.

76.  Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali,watasifiwa kwa midomo tu.

77.  Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah na Madina.

78.  Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.

79.  Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.

80.  Matajiri wataigwa.

81.  Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.

82.  Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko,maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.

83.  Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.

84.  Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.

85.  Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume wao.

86.  Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi,basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.

87.   Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.

88.  Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.

89.  Pombe itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.

90.  Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.

91.  Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala.

92.  Misikiti itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.

93.  Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala za jamaa'  na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

 

 


1685.     VIFO VYEUPE NA VYEKUNDU:

Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim a.s. kutatokezea kwa aina mbili za vifo - nyekundu na nyeupe.

Kwa nyekundu kunamaanisha damu yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali.

 

Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafa ya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala."

 

Tanbihi: Kwa vifo vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damu itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia.Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande.  Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n.k. yanavyoua watu kwa mamilioni.


UBASHIRI WA IMAM ‘ALI

 

1686.   Imam Ali ibn Abi Talib  a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake,

  1. Watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa.
  2. Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi.
  3. Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi.
  4. Waislamu wataanza kuchukua riba. 
  5. Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida.
  6. Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa.
  7. Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia.
  8. Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao.[43]
  9. Wanaume watawataka wanawake ushauri na uongozi.
  10. Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu.
  11. Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida.[44]
  12. Mauaji na umwagaji wa damu utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe.
  13. Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na  wadhalimu watakuwa wenye nguvu.
  14. Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu.
  15. Wasufi na wasomaji wa Qur’an watakuwa wapumbavu.
  16. Kutakuwa kukitolewa ushahidi  wa kughushiwa.
  17. Qur’an Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.
  18. Misikiti itakuwa ikijengewa minara mirefu.
  19. Watu waovu watakuwa wakiheshimwa.
  20. Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao.
  21. Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale.
  22. Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume wao  kwa uroho wa mali.
  23. Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana.
  24. Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu
  25. Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa.
  26. Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji.
  27. Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi.
  28. Wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.
  29. Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke)na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme[45].
  30. Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea.
  31. Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.
  32. Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .
  33. Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko  kitu chochote kile.
  34. Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.
    Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema
    "Ewe Bwana, naomba utwambie Dajjal atakuwa ni mtu wa aina gani?"
    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.
  35. Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.
  36. Jua litakuwa pamoja naye.
  37. Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.
  38. Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,
  39. Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.
  40. Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal yatakauka hadi siku ya Qiyama,
  41. Baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."
  42. Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.
  43. Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa,
  44. Wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,
  45. Huyo Dajjal atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria, atauawa siku ya Ijumaa mchana,
  46. Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam Mahdi a.s.
  47. Na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

 

UDONDOZI WA UBASHIRI

 

1687.   Kutoka dalili na mabashiri ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. hapa kuna madondoo machache ambayo yamechambuliwa:

1.      Uasi wa Sufiani,

  1. kuuawa kwa Hasan,
  2. Ikhitilafu baina ya Bani Abbas kwa matakwa ya dunia.
  3. Kupatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani, ikifuatiwa na kupatwa kwa mwezi mwishoni mwa mwezi huo wa Ramadhani.
  4. Beda (mahala baina ya Makkah na Madina) itadidimia ardhini,
  5. Ardhi katika upande wa Mashariki na upande wa Magharibi zitadidimia,
  6. Jua wakati wa asubuhi litaonekana liko papo hapo bila kutembea hadi wakati wa mchana na baadaye litachomoza kutoka Magharibi.
  7. Mcha Mungu atauawa nyuma ya msikiti wa Kufa pamoja na watu sabini wengine.
  8. Mtu mwema kutoka ukoo wa Bani Hashim atachinjwa baina ya Rukn na Makam huko Makkah.
  9. Kuta za Msikiti wa Kufa zitaporomoka.
  10. Bendera nyeusi zitatokezea huko Khorasan.
  11. Mtu kutoka Yemen ataongoza uasi.
  12. Mtu atakayetokea nchi za Maghreb ataonekana huko Misri na ambapo atapata mamlaka makubwa.
  13. Warusi watafika Bara la Arabia,
  14. Wazungu watafika Palestina.
  15. Upande wa Mashariki kutaonekana kwa nyota yenye mkia. Mwanga wake utaonekana kama ule wa mwezi na ncha zake zote zitakuwa moja (zitaungana).
  16. Kutaonekana uwekundu mkubwa sana mbinguni.
  17. Kutazuka moto mkubwa sana katika Mashariki ya kati ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu hadi saba.
  18. Wale wasio Waarabu watawafukuza Waarabu kutoka ardhi zao.
  19. Utawala wa kifalme utakwisha nchini Iran.
  20. Wamisri watamuua kiongozi wao.
  21. Bendera tatu zitakusanyika Syria.
  22. Kutazuka mizozo mikubwa na Syria itateketezwa.
  23. Bendera za Waarabu na Bani Qais zitatoka Misri.
  24. Bendera ya Banu Kinda itapepea Khorasan.
  25. Jeshi kubwa sana litapita Hira.
  26. Mabango meusi yatafika kutokezea Mashariki.
  27. Maji ya mito ya Furat yatafurika katika mitaa ya Kufa.
  28. Kutatokezea watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume.
  29. Sayyid kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imamu Mahdi
  30. Mtu mwenye heshima kubwa kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai karibu na Khankin.
  31. Kutajengwa na daraja katika Baghdad katika sehemu za Kharah.
  32. Kutakuwa na tufani ya upepo mkali katika Baghdad wakati wa asubuhi na kutafuatiwa na kupasuka kwa ardhi ambamo baadhi ya sehemu itadidimia ardhini.
  33. Mauti,vifo na maangamizo yatakithiri huko Iraq kiasi kwamba watu watakuwa kama wamewehuka.
  34. Vikundi vitapigana mno huko Iran.
  35. Sura za jumuia zitachafuliwa.
  36. Watumwa wataanza kutawala nchi za Mabwana wao.
  37. Sura kama ya binadamu itaonekana karibu na jua.
  38. Makaburi yatafumuliwa na
  39. Waliokufa watapewa uhai.
  40. Kutakuwa na mvua itakayonyesha kwa mfululizo wa siku ishirini na nne ambayo itahuisha ardhi iliyokuwa imekufa.  Kwa hakika wakati huo ndio utakuwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s.

MUKHTASARI WA DALILI

1688.  

  1. Baghdad itateketezwa kabisa.
  2. Basra itazama.
  3. Waarabu watatawaliwa na mfalme wa ukoo mmoja tu kwa nguvu.
  4. Msikiti wa Borasa (baina ya Baghdad na Kazmain) utadhoofika.
  5. Kutakuwa na nchi nyingi za Kiislamu na kutakuwa na soko la kawaida
  6. Qum itakuwa ni kitovu cha mafunzo ya Kiislamu, kitakuwa ni kituo kipya kuliko kile cha Najaf (Iraq). Na hapo ndipo kutakuwa kukitolewa ahkamu za dini.
  7. Kutakuwapo na reli kupitia katika nchi za Kiislamu.
  8. Azarbaijan itakumbwa na vita.
  9. Wanawake watakosa heshima kabisa.
  10. Duniani kote kutaenea sheria za kidemokrasia.
  11. Kutakithiri kizazi cha wanaharamu.
  12. Kutakithiri riba na rushwa.
  13. Kuzaliwa kwa wanawake waovu katika familia nzuri.
  14. Watu wenye hali ya chini wataweza kujenga majumba makubwa.
  15. Watu wema na waaminifu watakuwa wakiomba mauti ili waepukane na maudhi wanayoyapata.
  16. Watoto na majahili watapanda juu ya Mimbar, na watajulikana kama khatib.
  17. Wanazuoni watajiingiza katika mambo ya dunia.
  18. Madhumuni ya kutafuta Elimu itakuwa ni kutaka kutafuta pesa.
  19. Badala ya kusalimiana matusi ndiyo yatakayo kuwa yakitumika watu watakapokuwa wakikutana.
  20. Watu watatoka katika dini zao kwa sababu ya ulafi wa vitu.
  21. Dini ya Kiislamu itakuwa dhaifu.
  22. Mambo ya kuingiliana yatakuwa yakifanyika kidhahiri kama vile wafanyavyo wanyama.
  23. Wanawake watasuka nywele zao kama nundu za ngamia.
  24. Kupatwa kwa mwezi na jua na mitetemeko vitatokea Mashariki na Magharibi na baadaye katika Bara la Arabia.
  25. Kutakuwa na ongezeko katika kuzaliwa watoto wa kike.
  26. Ulawiti na pombe vitakuwa ni vitu vya kawaida.
  27. Mitetemeko ya kila mara itaongezeka.
  28. Wanawake watakuwa na taasisi zao.
  29. Wanawake watafanya kazi pamoja na wanaumme katika kutafuta maisha yao.
  30. Usafiri utakuwa wa haraka sana.
  31. Kutakuwa na muongezeko wa ajali za njiani.
  32. Mavazi yatakuwa mafupi.
  33. Mwanamme na Mwanamke watajaribu kuonana sawa kijinsia
  34. Kutakuwa na ndoa za kuoa jinsia yake yaani mwanamme atamuoa mwanamme mwenzake na mwanamke atamuoa mwanamke mwenzake (na mambo haya hasa yanatokea katika nchi za Ulaya).
  35. Wakazi wa Kufa na Najaf watakuwa wamekaribiana sana.
  36. Wakazi wa Makkah na Madina wataongezeka.
  37. Hijab itakuwa imepotea (hijab, bubui).
  38. Maji yataanza kujaa katika ziwa Sawa.
  39. Kutakuwapo na nyota yenye mkia karibu na Capricorn.
  40. Watu wengi sana  watakufa kwa sababu ya kuenea kwa vita
  41. Misikiti na Qur’an itarembeshwa kwa dhahabu.
  42. Kutatokea  na moto mkubwa sana katika mashariki na utaendelea kuwaka kwa siku saba.Na moto huo utatia khofu kubwa sana kwa mioyo ya watu.
  43. Kutakusanyika bendera tofauti tofauti huko Kufa na kusababisha mifarakano mikubwa.
  44. Utawala wa Kifalme utakwisha huko Iran.
  45. Kutatokea na mivurugo katika nchi za Kiaarabu.  Kila nyumba ya mwarabu na nchi zote za Kiislamu zitahusishwa humo.
  46. Kukosa Imani kutaenea kote.
  47. Waislamu wataiga tamaduni na mila za maadui zao.
  48. Vifo vya ajali vitaongezeka.
  49. Ala za muziki zitaenea kiasi kwamba hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayesalimika kwa sauti zao.
  50. Watu wataanza kukataa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.
  51. Kutaonekana sura katika jua, na sauti zao zitasikika duniani kote.
  52. Mwanadamu atafika mwezini.
  53. Sufiani atatokezea na kueneza utawala wake wa vitisho.
  54. Sayyed Hassan atatokezea huko Iran.Na yeye atafika Multan kwa kupitia Kirman huku akiteka sehemu zote. Yeye atamfikia Imam a.s. Yeye atamfikia Imam Mahdi a.s. na kujIssalimisha mbele yake.
  55. Kutatokezea wazushi wa mtume sitini.
  56. Mtume Issa a.s.atateremka kutoka mbinguni.
  57. Maafa, magonjwa ya kuambukiza na ukame utaenea kote.
  58. Nafsi ibn Zakia atauawa katika al- Khaaba (mtu mcha Mungu atauawa katika al-Kaaba).
  59. Jua litachomoza kutoka Magharibi kwa siku moja.
  60. Warusi wataingia Bara la Arabia na watu weupe wataingia Bara la Parestina.Nao baadaye watapambana.
  61. Wachina wataingia Bara la Arabia na kusababisha maangamio na maafa ambayo yatakuwa ni mambo ya kawaida.
  62.  Baadhi ya miji itateketezwa kwa sababu ya maafa na misukosuko.
  63. Sauti ya kutisha itasikika kutoka mbinguni.
  64. Kutokezea kwa Dajjal.
  65. Moto na moshi itakuwa kawaida duniani.
  66. Mvua zitatokezea pasipo na misimu yake.
  67. Kuongezeka kwa joto katika anga za juu.
  68. Kulipuka kwa moto mkubwa katika Aden.
  69. Baadhi ya makundi ya wanaume yatakuwa yamegeuka maumbo.
  70. Kutatokea na mabadiliko ya ajabu katika sayari ya Capricorn
  71. Mkuu wa Dola ya Misri atauawa.
  72. Kutakuwapo na mvua ya mfululizo kwa muda wa siku ishirini na nne(24).Dunia nzima itakuwa imejaa michafuko, maafa na maangamizo n.k. 

 

1689.    Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo:

"yeyote yule atakayekufa bila ya kumtambua na kumjua Imam wa zama zake basi mtu huyo atakufa mauti ya ujahili 

(yaani atakufa kifo cha ukafiri)."

 

1690.   HADITH YA PILI

Madhehebu yote ya Islam kwa pamoja yanaelezea Hadith ifuatayo na ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa Kiislamu na vile vile Sahih Bukhari na vitabu vingine vyote vya Hadith pia vinaelezea kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema:

  "Baada yangu watakuwapo Maimamu kumi na wawili ambao watatokana na Maqureish."

 

1691.   HADITH YA TATU

‘Allamah Syed Jamal ud-Din Muhaddath ambaye ni mwachuoni mkubwa wa Ahli Sunna,anaandika katika kitabu chake Rawdhat ul-Ahbaab   kwa kumnakili Sahaba Ja'abir ibn ‘Abdullahi Ansari wakati Allah swt alimfunulia Aya hii Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.:-

"Enyi mlioleta Imani! Mtiini Allah swt na Mtume wake na vile vile mumtiini  'ulil Amr'."

 

"Basi mimi (anaendelea Bwana Ja’abir) niliuliza "Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tunaelewa  Allah swt pamoja na Mtume wake.Lakini jee ni wakina nani hao ambao wanajulikana kama 'ulil Amr" ambao utiifu wao umefaradhishwa kwetu sisi?"

 

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitoa majibu haya yafuatayo:

"Wao watakuwa Makhalifa baada yangu na wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib na amfuataye atakuwa ni mwanae Hasan  na atamfuatia Hussein na baadaye atafuatia  Ali ibn al-Hussein na baadaye Mohammad ibn Ali na anatambulika katika Tawrati kwa umashuhuri wa jina la Baqir na ewe Jaabir! Karibu utafikia zama zake na hapo tafadhali naomba unifikishie salamu zangu. Baada yake atakuja Ja'afer as-Sadiq bin Mohammad na baadaye Musa ibn Ja'afer na baadaye Ali ibn Musa na baadaye Muhammad ibn Ali na baadaye Ali ibn Mohammad na baadaye Hasan ibn Ali na baadaye  Muhammad ibn al-Hasan  ambaye atakuwa juu ya ardhi hii kama  hujjatillah  na  bakiyallah  katika wamchao Allah swt. Huyo ndiye atakayepata ushindi wa mashariki hadi wa magharibi wa dunia hii. Na yeye mwenyewe ambaye atakuwa hayupo mbele ya wafuasi  (Mashiah) wake na wale wampendaye hadi kwamba hao hawatabakia katika itikadi ya Uimamu illa wale tu ambao Allah swt ameshawachukulia mitihani ya nyoyo zao."

 

Ja’abir  r.a. anaelezea kuwa:  Mimi sikusita kumwuliza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

"Ewe Mtume wa Allah swt! Je katika zama za Ghaibat,  wafuasi  (Mashiah)  wake wataweza kufaidika naye?"

 

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:

 "Naam ! Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amenituma nikiwa Mtume wake,kuwa katika zama zake za  Ghaibat  ,Mashiah wake watang'arika kwa nuru yake na kufaidika kwa Ukhalifa wake kama vile  watu wanavyofaidika na jua hata kama litakuwa limejificha katika mawingu."

 

1692.    HADITH  YA  NNE

Imam bu Dawud ameandika katika kitabu chake  Sunan  na Imam Tirmidhi anaandika katika Sahih Tirmidhi  kwa kumnakili Abu Said Khudhri,kuwa:" Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

' Mahdi anatokana nami na mwenye uso unaong'aa na pua yake iliyo ndefu ataijaza ardhi kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imeshajaa kwa dhuluma na ufIssadi, na atatawala kwa kipindi cha miaka saba.' "

 

1693.   HADITH  YA  TANO

Imam Abu Dawuud katika  Sunan amendika kwa kumnakili Sayyidina Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.:

"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa iwapo kwisha kwa dunia hata kama ni siku moja itakayobakia,hivyo pia Allah swt atamtuma mtu mmoja kutokana na Ahlul Bayt yangu  (kizazi changu) humu duniani ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi."

 

1694.    HADITH  YA  SITA

Imam Abu Dawud amemnakili Ummul Moominiina kufuatilia mfululizo huo wake kuwa:

Mtume Mtukufu s.a.w.w amesema kuwa

'Mahdi atatokana na Itrati  (kizazi) yangu,yaani atatokana na kizazi cha Fatimah az-Zahra a.s.'  "

 

1695.   HADITH  YA  SABA

Imam Bukhari katika  Sahih Bukhari , Imam Muslim katika  Sahih Muslim  na Kadhi ibn Mas'ud Baghawi katika Tasnif Sharh al-Sunnah. Wote wanamnakili Abu Hurayrah akisema:

"Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

 

'Je hali yenu itkuwaje wakati Mtume Issa a.s. atakapoteremka kwenu na Imam wenu atakuwapo ametokea miongoni mwenu?'"

 

1696.   HADITH  YA  NANE

Imam Tirmidhi katika  Sahih Tirmidhi  na Imam Abu Dawud katika  Sunan Abu Dawud  wanamnakili Abdullah Ibn Mas'ud akinakili riwaya:

Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

“Kuwa dunia haitakwisha hadi hapo mfalme wa Kiarabu  hatatokea kutokana na kizazi changu,na ambaye jila lake litakuwa kama jina langu."

 

1697.    HADITH  YA  TISA

Imenakiliwa na Maimamu wa Ahli Sunna katika Sahih  zao,riwaya ifuatayo: Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

"Atatokezea mtu mmoja katika Ahlul Bayt yangu,atakayetawala na jina lake litakuwa kama jina langu."

 

1698.    HADITH  YA  KUMI

Imam Abu Is-haq  Tha'alabi katika  tafsir  yake anamnakili  Anas bin Malik kuwa:Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa

"Sisi wana wa Abdul Muttalib ni viongozi wa watu wa Jannah,yaani mimi , Hamza, Ja'afer  na Ali na Hasan , Hussein na Mahdi."

 

1699.  Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. :

“Hakuna watu wanaopoteza utajiri wao isipokuwa kwa kutokana na madhambi yao, kwani Allah swt kamwe hawadhulumu viumbe vyake.”

 

1700.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Wale wote wanaotukuzwa na kuheshimiwa kwa woga wa maovu yao, kwa hakika wao watakuwa miongoni mwa watu waovu kabisa siku ya Qiyama.”

 

 

1701.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kudhibiti hamaki yake hawezi kuitawala akili yake.”

 

1702.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake.”

 

1703.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto.”

 

1704.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake); na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo.”

 

1705.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia.”

 

1706.   Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo.”

 

1707.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Allah swt.”

 

1708.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge-kwani moto hauzimiki ila kwa maji.”

 

1709.   Mtu mmoja alimwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  na kusema:

“Mimi mpaka hivi punde tu nilikuwa nikiamini kwamba wewe na baba yako ni watu wabaya kabisa, lakini sasa ninahisi kwamba huo moyo wangu uliokuwa umejaa chuki na uadui dhidi yenu, sasa umejaa mapenzi na ikhlasi. Hakika hakuna mwingine anayestahiki cheo hiki kitukufu isipokuwa wewe tu.

 

1710.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

”Jiepusheni na ghadhabu, kwani huleta mashaka.”

 

 



[1]  Nimetarjumu kitabu juu ya Sadaqah ambacho kinazungumzia kwa undani zaidi.

[2] Ninajiandaa kukitarjumu kitabu juu ya maudhui haya.

[3]  Nimekikusanya na kukitarjumu kitabu kiitwacho Majina kwa ajili ya Watoto Waislamu.

[4]  Hii ni kasumba katika desturi zetu watu kuwa mwanamke anapokuwa mrembo sana ndio utaona wengine wana mahari makubwa kwa sababu ni mrembo sana kwa hiyo ndio Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema kila mwanamke akiwa mrembo na mahari yake yakiwa madogo basi huyo mwanamke ni bora kabisa katika umma wake.

 

[5]  Sisi imekuwa ni kasumba kuwa kabla ya kuoa lazima tutengeneze vitu vya thahabu Pete, hereni, Kidani, n.k. na hii ni kasumba ya kishetani na mara nyingi utawaona watu wanaotaka kuoa hawana uwezo lakini watakopa hata watauza vitu vyao vingine ili waweze kutimiza haya mambo ambayo hawana uwezo nao lakini ili kuonyesha ati kuonyesha desturi na mila ambazo ni potofu. Hapa tumeona Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. anasema hata kama ana pete ya chuma basi uoe sio mpaka iwe dhahabu.

[6] Mara nyingi tunaona kuwa mwanamke hafikirii wala haoni umuhimu wowote katika masuala kama hayo. Mume anapobisha hodi tu na kukaribia mlangoni, basi mwanamke anapoufungua mlango tu anaanza mashambulio yake kwa kila aina ya silaha alizonazo. Kwa hakika hii ni tabia mbaya mno kwani mume wake ametoka wapi na ameyapitia yapi hayajui. Hivyo inatakiwa kumkaribisha vyema na kumpa angalau bilauri moja ya maji. Lakini iwapo mwanamke atakuwa na tabia kama hii basi ugomvi utaweza kuzuka baina yao na hata mwanamke kuchapwa kibao kwa kutokana na hasira za mume wake.

[7] Leo dunia imekuwa ya uwazi zaidi. Mwanamme anapokuwa na mali na hivyo wanawake wanapoona kuwa mwanamme huyo ana mali na utajiri basi wengi huanza kumtemelea huyo mwanamme na wanaanza kutamaniana. Hivyo kama nilivyoelezea hapo nyuma kuwa wanawake wanakuwa na tabia ya kujiweka kiovyo wanapokuwa nyumbani yaani hawavai vizuri wala kuwavutia wanaume zao na hujiweka kama vijakazi, hivyo mwanamme anapowaona wasichana na wanawake nje ya nyumba yake wamevaa vizuri na kuvutia basi hutumbukia katika mitego ya mapenzi ambavyo tumeona mara nyingi huwapokonya waume wengine. Hatimaye utasikia kuwa bwana anataka kumpa talaka mke wake au mke anataka kumpa talaka mume wake si kwa sababu nyingine bali ni kutaka kuolewa na mwanamme au mwanamke mwingine kwa sababu ya urembo au mapesa. Talaka na ndoa zinamasharti yake. Kuwepo na uadilifu. Lakini talaka na ndoa kama hizo katika Islam zimeharamishwa kabisa.

[8]  Mimi nimekitarjumu kitabu kimoja cha Ayatullah Sayyed Dastaghib Shiraz kinacho zungumzia Tawba kwa kirefu na mapana kwa hiyo ukitaka kusoma zaidi kuhusu Tawba tafadhali sana tafuta kitabu hicho ambacho kitakufaidisha sana.

 

[9] Kipo kitabu kimoja nilichokitarjumu ambacho kinazungumzia visa katika Qur'an, na kisa hiki pia kipo kimezungumziwa kwa marefu.

[10]  Msomaji anashauriwa kukisoma vyema kijitabu nilichokitayarisha mimi kinachozungumzia Ummah wa Mtume Lut a.s. kwa makini kwani kinazungumzia vyema juu ya hali ilivyokuwa na ilivyokuja kuharibika na mafunzo tuyapatayo  kwa kukisoma kisa hicho. Kama hukipati basi wasiliana kwa anwani yangu iliniweze kukusaidia.

[11]  Tunaona mara nyingi sisi katika biashara tunaapa kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu hiki kitu bwana hivi…………. tunaapa uongo na ukweli ‘mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu fulani alinunua angalia wakati yeye hakununua kwako. Na mara nyingi tunajua hiki kitu ni kibaya lakini tunamwambia mtu uongo ili anunue kwa hiyo ndiyo uongo huo umeharamishwa katika Uislam na hata kitu kibaya sisi tutakisifu kweli kiasi kwamba mnunuzi anaweza kutuamini akanunua

 

Lakini tunapotaka kununua sisi tunaanza kutafuta kasoro aah kitu hiki hivi na kitu hiki vile Wallahi nakuapia Mungu niliwahi kutumia kitu hiki ikawa hivi kumbe hayo yote ni uongo kwa sababu tunataka yule mtu mwisho atuuzie kwa bei iliyo ya chini kabisa.

 

Allah swt swala kama hili pia amelikemea katika Qur'an Tukufu Sura Mutaffifina anasema ole wao wale watu wanapopimiwa vitu wanataka wapimiwe kamili ukinunua kilo moja ya sukari upate kilo moja kamili lakini unapouza unataka uuze ikiwa kasoro upunguze hata gram kidogo lakini uuze kitu ambacho kiko kasoro, kwa watu kama hawa kwa hakika wanalaaniwa.

 

[12] Yaani kuachiwa wewe mwenyewe ujitegemee maana yake baraka na rehema Allah swt hazitakuwa pamoja nawe naye hatakuwa mwenye kukunusuru na kukusaidia kwa hiyo matendo yako hayo yatakufanya wewe ujitoe katika rehema, neema na uhifadhi wa Allah swt.

 

[13]  Ndugu wasomaji naona jambo hili liko wazi kabisa kwa sababu dunia hii inatuvutia kwa kila aina ya raha na mazuri ambayo ndani mwake kuna maangamizo yetu wenyewe ni mfano wa nyoka unamwona mzuri ukianza kumchezea anaweza kukuuma ukapata sumu na kufa ukaangamia na vivyo hivyo ndivyo ilivyo dunia, hawa leo tunaona hata vijana pamoja na kuwa na fahamu zao kamili na akili timamu na watu wamesoma na watu wanajua mazuri na mabaya lakini wanajifanya wapumbavu kiasi kwamba wanajiingiza katika madawa ya kulevya ambazo ni raha za muda na athari zake zinateketeza maisha yao wanayaona wanayasikia lakini utaona bado wenyewe wanajitumbukiza katika maangamizo hayo. Vile vile tunaona vijana wanaume vijana kwa wazee wanavutiwa na malaya wanaojiremba wamevaa nguo nzuri T-shirt na masuruali lakini hawafikirii busara ni nini wao wanavutiwa nao na wanakwenda wanafanya uasherati nao na wanakumbwa na magonjwa maovu  kabisa ambayo yanawaua na wengine wanafilisiwa pia kiasi cha kwamba wanapoteza heshima yao na kupoteza uhusiano na jamaa zao. Kwa hivyo tujaribu kuangalia kilicho kizuri tuangalie na undani wake ili tuweze kujua kile tukifanyacho kina hekima gani.

[14]  Kuna msemo usemao: Mali bila daftari hupotea bila habari !

[15]  Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. yeye ni Imam wa kumi na mbili katika mfululizo wa Imam ambao wanaaminiwa na Mashi’a. Kwa hakika Imam sio kwamba ni Mashi’a tu wanafuata Mashi’a ndio wanamfuata kweli kwa sababu wao ndio wanafuata kauli na Sunnah za Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. kwani Imam Mahdi a.s. yeye ametajwa katika vitabu vyote vya Masunni na Mashi’a na dalili zake zote na maisha yake na dalili za Kudhihiri yametajwa katika vitabu vyote hakuna madhehebu ya katika Islam iwe katika upande wa Masunni au Mashi’a wanaoweza kukana kuwapo kwa Imam Al Mahdi a.s. habari zaidi zinapatikana katika vitabu vya Tarikh vile vile mimi nimekikusanya na kukitarjumu kitabu kimoja kinacho zungumzia Dalili za Qiyamah na kudhihiri kwa Imam Al Mahdi a.s. hivyo msomaji unaweza kutafuta kitabu hicho kikakusaidia na ukajua dalili za Qiyamah na dalili za kudhihiri kwa Imam Al Mahdi a.s. kuhusu maswala ya Imam Mahdi a.s. katika vitabu vya Waislam utavipata usiache kufanya utafiti.

[16] Ni jambo la kusikitisha kabisa kuona wanawake wa siku hizi ambao wana tabia za kutembea nje ya nyumba iwe kikazi au kimatembezi Wao wanapokuwa nyumbani wanavaa nguo zilizochakaa na chafu na utakuta nywele na nyuso zao zimechakaa na kiasi kwamba utakapomwona hautamtamani lakini iwapo atakuwa akitaka kwenda nje basi utafikiria kuwa bibi harusi yupo nyumbani kwako kwani wataoga na kuvaa mavazi mazuri na kujipaka vipodozi na manukato kiasi kwamba watakapo pita mtaa mzima hujawa kwa manukato mazuri. Hapo ni kwa ajili ya kwenda nje. Hivyo inamaanisha kuwa amejiandaa hivyo kwa ajili ya wengine na wala si kwa ajili ya mume wake aliye nyumbani. Jambo hili Islam inakataa na kupinga. Wavae vizuri nyumbani na wanapotaka kwenda nje. Mume apewe kipaumbele !

[17] Tuhaf ul-Qaul , uk.26

[18] Chuo cha Wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , j.1, uk. 13

[19] Safinat ul-Bihar, j. 1, uk. 549

[20]  Chuo cha Wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , j.1, uk. 11

[21] Nahjul Balaghah, uk. 266

[22] Nahjul Balaghah, uk. 142

[23] Nahjul Balaghah, uk. 103

[24]  Safinat ul- Bahar, j.2, uk. 207

[25] Al-Quran, Sura ‘Aaraf, Ayah 199 - 200

[26] Al-Quran, Sura Ali Imran, Ayah 134

[27] Al-Quran, Sura Ali Imran, Ayah 159

[28] Al-Mizan al - ‘i’tidal, j.8, uk. 402,

[29] Nahjul Balaghah, uk. 94

[30] Safinat ul- Bahar, j.2, uk. 207

[31] Safinat ul- Bahar, j.2, uk. 208

[32] Muntahi al-A’mal, j.1, uk. 62

[33] Surah  Fath (48 ) Ayah 1-2

[34] Surah  Bani-Israil (17 ) Ayah 81

[35] Surah   Ahzab (33 ) Ayah 21

[36] Hudud Wasail, uk.311

[37] Islam na Fikara za kibinadamu, uk. 670

[38] Rejea al-Qur’an Sura 2 : 55  na  7 : 161

[39]  Rejea Al-Qur’an Sura 18 : 35

[40] Rejea al-Qur’an Sura 2 : 55  na  7 : 161

[41]  Rejea Al-Qur’an Sura 18 : 35

[42] Habari hizi tazama Day of Judgement ,Sayyid Saeed Akhtar Rizvi,Bilal Muslim Mission of Tanzani,DSM,chapa ya pili,1978,uk.44.,naye amenakili kutoka Bihar-ul-  Anwar,j.III.

[43] Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!

[44]  Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya  mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya  misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.

[45]  Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6.30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza  k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.

Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.