HADITH ZA MTUME s.a.w.w. NA MA-IMAMU a.s. 

 

UTANGULIZI. 4

MUWE TAHADHARI ENYI WASOMAJI. 6

1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH.. 11

2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH: 15

3.  HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI: 20

4.    SABABU ZA UCHELEWESHO KATIKA UANDISHI WA HADITH: 26

HADITH NI NINI ?. 28

ALQAAB. 40

MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE?. 41

AINA ZA AHADITH.. 43

HADITH ZILIZOTOLEWA.. 44

 

SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH.. 51

HADITH YA UFUNGUZI. 52

KUMJUA ALLAH SWT, UKUU NA BARAKA ZAKE.. 53

SALA  NA  ATHARI ZAKE.. 55

SALA ZA USIKU WA MANANE.. 59

KUMWAMINI ALLAH NA KUIPATA FURAHA YAKE.. 61

TAQWA NA UMUHIMU WAKE KWA WAISLAMU.. 62

K U O M B A   D U A.. 65

AHLUL BAYT a.s. 68

MAPENZI YA AHLUL-BAYT a.s. 70

SIFA NA TABIA ZINAZOKUBALIKA.. 71

WAFUASI HALISI WA AHLUL-BAYT a.s. NA SIFA ZAO.. 74

 

MADHAMBI NA ATHARI ZAKE.. 76

ELIMU NA THAMANI YAKE.. 79

ILIMU NA FADHILA ZA KUJIFUNZA.. 81

ILIMU NA FADHILA ZA  KUIFUNDISHA.. 83

ELIMU – HEKIMA – MA’ARIFA. 84

UMUHIMU WA MAARIFA.. 85

KUTAFUTA ELIMU. 86

AKILI. 86

UJAHILI: 93

UTUKUFU NA UMUHIMU WA WANAZUONI. 94

KUWA MAKINI KUHUSU AKHERA.. 97

JANNAT. 98

JAHANNAM... 108

T A W B A.. 121

KULINDA HESHIMA YA WAUMINI. 123

M A T E N D O  M E M A.. 124

 

DHULUMA NA UONEVU.. 126

HAKI ZA WAISLAMU WENZAKO.. 128

SALAAM -- KUSALIMIANA.. 130

KUTENDA MEMA NA KUZUIA KUTENDA MABAYA. 132

ULIMI NA MAOVU YAKE. 136

KUSENGENYA NA KUTAFUTA KOSA. 137

UHARAMISHO WA KUSEMA UWONGO 139

KUSEMA UONGO.. 162

MARAFIKI NA URAFIKI. 164

MARAFIKI WASIO WEMA.. 167

KUWAHUDUMIA WATU.. 169

KUTOA MIKOPO.. 171

KUWASAIDIA WENYE SHIDA.. 172

ZAWADI NA KUWAFURAHISHA MUUMIN.. 173

SADAKA NA MISAADA.. 174

 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

 

Zimekusanywa na kutarjumiwa na

AMIRALY M.H.DATOO

BUKOBA - TANZANIA


YALIYOMO

 


UTANGULIZI

 

Allah swt anatuambia katika Al-Qur’an tukufu: Sura al-Nahl, 16,

Ayah 43

Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.

 

Sura Al-Ambiya, 21, Ayah 7

Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (ufunuo). Bas waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.

 

Ayah hii Tukufu inawasihi Waumini kujielekeza kwa Ahl-Dhikr yaani watu wenye busara na Wanazuoni wa Ummah ili kuweza kubainisha baina ya haki na batili, wakati ambapo Waumini wanapokumbana na shida au ugumu katika masuala mbalimbali, kwa sababu Allah swt baada ya kuwafundisha ilimu, aliwachagua hao kwa hayo. Hivyo, wao wamebobea katika ilimu na ambao ndio watu halisi wanaoielewa, kuifundisha na kuitekeleza kwa usahihi mafunzo ya Qur’an.

 

Ayah hii iliteremshwa kwa ajili ya kuwatambulisha Ahlul-Bayt a.s. nao ni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Fatimah  a.s., Al-Imam Hassan ibn Abi Talib a.s. na Al-Imam Husayn ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. , ambao kwa ujumla wanaitwa Watukufu watano au ‘Al-i-‘Aba ambapo pamoja na hao wameongezeka Ma-Imamu a.s. wengine tisa kutokea kizazi cha al-Imam Husayn ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.mara nyingi katika nyakati mbalimbali aliwatambulisha hao kuwa ni Ma-Imam waongozi, nuru katika kiza, na ni wale ambao wamebobea katika ilimu na bila shaka Allah swt amewajaalia Ilimu ya Kitabu Kitukufu.

 

Ukweli huu, kama ilivyorejewa mahala pengi katika Ahadith mbalimbali kuanzia zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.kuanzia ufunuo hadi leo hii, na vile vile wanazuoni wengi na Wafasiri kutokea Ahl-Sunnah wamekiri waziwazi katika vitabu vyao kuwa Ayah hizi za Qur’an zilikuwa zimeteremshwa hususan kwa ajili ya kuelezea na kuwatambulisha Ahl-ul-Bayt a.s.  Baadhi ya mifano ya vitabu vyenyewe ni kama ifuatavyo:

1.      Imam Tha’labi katika tafsiri ya kitabu chake juu ya Ayah hiyo ya 42 kutokea Sura An-Nahl, namba 16

2.      Tafsir ibn Kathir, j.2, Uk.591

3.      Tafsir at-Tabari, j.14, Uk.75

4.      Tafsir-i-Alusi, ijukanavyo kama: Rahul-Bayan , j. 14, Uk. 134

5.      Tafsir-i-Qartabi, j.11, Uk. 272

6.      Tafsir-i-Hakim, au Shawahid-ut-Tanzil,  j. 1, Uk. 334

7.      Tafsir-i-Shabistrary, au: Ihqaq-ul-Haq,  j.3, Uk.482

8.      Yanabi’-ul-Muwaddah, cha Ghanduzi Hanafi, Uk. 119

 

Kwa kutegemea ukweli huu, sisi lazima tujielekeze kwa Wananyumba ya Ahlul-Bayt a.s., na kutekeleza maneno yatuongozayo ili kuelekeza maisha yetu mema. Kwa sura hii, Imam-ul-Hadi a.s. anasema katika  Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na ‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha :

“Maneno yenu yenye busara yanatupa nuru, maamrisho yenu ni hidaya kwa watu na usia zenu ni Taqwa na usawa.”

 


MUWE TAHADHARI ENYI WASOMAJI

Kwa kupitia  Watukuu hawa ndipo sisi tunaweza kuokoka humu duniani na Aakhera na maisha yetu yakawa mema na salama.

Twapata katika  Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na ‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha :

“Ni kwa sababu yenu Allah swt ametutoa nje ya upotofu (wa ukafiri), ametufanya huru kutoka huzuni na masikitiko, na kutuchukua pa usalama dhidi ya maangamizo ya dunia na mioto ya Jahannam pia.”

 

Katika katika  Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na ‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha  twasoma :

“Ni kwa sababu ya Ukuu na uongozi wenu kuwa Allah swt ametufundisha ilimu ya kanuni za Dini , na kuweka sawa na vyema yale yote yaliyovurugika na kufasidika katika dunia. (Naye ametuepusha na umasikini, udhalilifu na ujahili, na kututunukia ilimu, heshima na hadhi.)

 

Kwa hakika, iwapo sisi tutawaacha hawa watukufu waliobarikiwa na kutukuzwa na Allah swt, basi hakuna shaka kuwa tutatumbukia katika upotoshi na maangamizi katika kila hali.  Ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.amesema :

“Mfano wa Ahlul-Bayt a.s. yangu ni sawa na Safinah ya Mtume Nuhu a.s. Yeyote yule atakaye ipanda basi kwa hakika ameokoka na yeyote yule  atakayekhilafu kuipanda, basi kwa hakika amezama na kutokomea mbali.” [1]

 

Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. :

“Inawezekana nikaitwa hivi karibuni nami nikaitikia. Hivyo, mimi ninawaachieni miongoni vitu viwili vilivyo vizito (vyenye thamani na maana kubwa mno) : Kitabu cha Allah swt (yaani Qur’an) ni kamba iliyovutika kutoka mbinguni hadi ardhini , na Ahlul-Bayti a.s.yangu;  kwa hakika Allah swt, Mrehemevu, Mwenye kuwa Makini, amenijulisha kuwa kamwe, kamwe vitu hivi viwili havitatengana hadi kukutana na mimi hapo Hawdh-Kauthar  (Chemchemi ya milele). Hivyo, muwe waangalifu mutakavyojishikiza navyo wakati ambapo mimi sitakuwapo.”

 

Na vile vile katika Hadith nyingineyo imeongezeka:

“Kamwe, kamwe, hamtapotoka iwapo mutakuwa mumeshikamana navyo hivi vitu viwili.” [2]

 

Hivyo, je ni heshima gani itakayopita kuliko Qur’an , Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.na Ahlul-Bayt a.s. vikawa ni mifano yetu, waalimu na viongozi wetu ?

 

Na kwa sababu hizi ndipo sisi kwa moyo halisi na unyenyekevu tunasema:

 

Sisi tumefadhilika kwa sababu sisi ni wafuasi wa Madhehebu ambayo muasisi wake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.(mja ambaye amekombolewa kutokana na minyororo ya udhalili na kuchaguliwa kuwa mkombozi wa binadamu wote kutoka utumwa mbali na ule wa Allah swt ) kwa kufuata mwongozo kutoka Allah swt.

 

Sisi tumetukuzwa kwa kuwa na kitabu kitakatifu cha Nahjul-Balagha, ambacho ni kitukufu baada ya Qur’an Tukufu, chenye maandiko matukufu kwa ajili ya maisha yetu wanaadamu, ni kitabu kikubwa kwa ajili ya ukombozi wa mwandamu na maelekezo yake ya kiroho na kisiasa yanayo thamani kubwa kwa ukombozi na kimeandikwa na Ma’sum Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

Vile vile tumebarikiwa kwa Imam Al-Mahdi a.s. atokanaye na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.yu bado hai na kwamba anahabari na kujua habari zetu zote.

 

Sisi tumebarikiwa kuwa na Doa ambazo ndizo zilizofunzwa na Ma-Imam a.s. kama Dua za Sha’baniyyah, Dua ya ‘Arafah ya al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Sahifa-i-Sajjadiyah ya al-Imam Zayn-al-‘Aabediin a.s. , na Sahifa-i-Fatimah.

 

Vile vile sisi tumebarikiwa kuwa na Mwanazuoni mkubwa katika zama zetu ambaye hawezi kueleweka kwa watu wengine isipokuwa Allah swt, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.na Ma-Imamu a.s. kwa sababu ya kipaji chake kikubwa cha ilimu na hekima.

 

Vile vile sisi tumebarikiwa kwa kuitwa Madhehebu ya Ja’afariyyah na kwamba Fiqh  ambayo ni bahari isiyo na mwisho ( ya ilimu ), ambayo ni mchango mmojawapo wa Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.Vile vile sisi tunafakhari kubwa sana kwa kuwa na Ma-Imamu a.s. wote, na tunawafuata kikamilifu.

 

Sisi tumebarikiwa kwamba Maimam a.s. wetu walikuwa wameteswa, kuwekwa mahabusu na vile vile kutolewa makwao kwa sababu wao walikuwa daima wamejitolea muhanga kuutetea ubinadamu na kuinua hali ya Dini ya Islam na kuyatekeleza maamrisho ya Qur’an  yakiwemo maamrisho ya kutengeneza Serikali adilifu na hatimaye hao Ma-Imamu a.s. waliuawa katika harakati zao za kutokomeza serikali dhalimu na Taghuti katika kila zama. [3]

 

Sasa, ewe mpenzi kaka na dada !

Wewe ni shahidi wa macho, katika dunia hii ndogo, ndogo zaidi kuliko kijiji katika ulimwengu, unajionea kuwa hali ya binadamu inaendelea ipo inateketea katika jangwa la dhuluma na pasi na haki, wakati mwanadamu huyo yupo anatumbukia chini zaidi katika matingatinga ya kutokuhurumiwa na kukosekana kwa uadilifu.

 

Wale wote wanaojidai kuhusu uhuru na raha ya mwanadamu wanashuhudia kwa makini kumomonyoka kwa maadili katika mazingira waliyoyaumba wao wenyewe. Wao hawana tena uwezo wa kudhibiti hali hiyo isipokuwa kuangamia kwa binadamu na ubinadamu. Lakini, je ni kweli kuwa huo ndio mwisho wa mstari huo ?

 

Jibu kwa kushangaa litakuwa  ndiyo, hadi hapo mwanadamu atakaporejea katika uumbwaji kwake wa kiAllah swt, akimulika makosa na kasoro zake zilizopita kama ndiyo tochi kwa maisha yake ya mbeleni na akiitumia Islam kama ndiyo dawa ya matatizo yake yote.

 

Katika zama hizi, Islam ambayo ndiyo tukufu, na bora kabisa katika kutuongoza, bora katika katika historia, imetoa mikono yake kwa ajili ya kumnusuru mwananadamu ili asije akazama na kughalibiwa na maovu na kwa baraka za Allah swt, imesimama imara kumtibu mwanadamu dhidi ya magonjwa maovu kabisa ya maovu.

 

Islam ipo kwa ajili ya kutuliza kiiu cha mwanadamu anayezurura katika majangwa ya chumvi kali zisizo na taqwa kwa kumnywisha maji matamu na baridi ya itikadi zilizonurishwa kwa ilimu na maarifa na utukufu wa Ahlul-Bayt a.s. , ambayo ndiyo sura halisi ya tafsiri kamili ya ufunuo ambayo kamwe haikuwa na kosa au kasoro ya aina yoyote ile. Inatoa mwanga kwa hali zote na kimwili na kiroho ya maisha ya mwanandamu. Hivyo, imefungua milango kikamilifu kwa mwanadamu kukamilika kikamilifu.

 

Lakini Ewe rafiki mpendwa

NI jambo la muhimu na kwanza kabisa kwa kutaka kujua habari za shule yoyote ile pamoja na mafunzo yake, inatubidi sisi kutazama kwa undani maandiko na kuelewa mazungumzo na maneno ya viongozi wake. Na kwa njia hii ndipo sisi tutakapoweza kujua kuhusu itikadi na imani na malengo ya shule hiyo kuhusu dunia na matatizo yake na hivyo kuweza kufikia maamuzi na makisio ya upeo wake.

 

Al-Imam ‘Ali  ar-Ridha a.s. amesema katika  Bihar al- Anwar j.2, uk.40; Ma’aniy-ul-Akhbaar, cha Saduq, uk.180; na  Was’il al-Shiah’, j. 27, uk. 92

“Rehema za Allah swt zimfikie mja ambaye huisha maamrisho yetu”  Nami nilimwuliza ni vipi mtu anaweza kuziweka hai maamrisho yenu ?  Imam a.s. alijibu “Yeye anaweza kujifunza ilimu na maarifa yetu na kuwafundisha wengineo. Kwa hakika, iwapo watu watazijua faida na mema za miihadhara na misemo yetu, basi kwa hakika watazifuata kuzitekeleza.”

 

Matumaini mema

 

Twategemea kuwa msomaji kwa kuyasoma na kuyazingatia maneno yenye thamani isiyosemekana, kuwa kwa kupitia maneno na maongozao ya Ahlul-Bayt a.s. vizazi vyetu hususan vijana wataongoka na kamwe hawatapotoka wala kuvutiwa na mavutio yanayotuongoza kuelekea maangamizo ya milele na kwamba utamaduni wetu hautamomonyoka siku baada ya siku na badala yake tutatengeneza utamaduni wetu uwe utamaduni wa Kiislamu  kwa baraka na miongozo za Ahlul-Bayt a.s. na kwamba tutakuwa washupavu na maaskari kulinda imani na Din ya Islamu dhidi ya maadui wake walio ndani na nje. Tutakuwa Waislamu bora na mfano kwa watu wote.

 

Amani na Salaam ziwafikie wale wote waliongoka.

 

 

 


1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH

 

Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni.  Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili.  Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith.  Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika.

 

Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?"  Al-Harith ibn al-A' war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake.[4] Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

 

Imam Hassan ibn Ali ibn Abi Talib a.s. ameripotiwa akiwashauri watoto wake kama ifuatavyo:-

"Nyinyi sasa ni watoto wa Ummah ambao katika maisha ya mbeleni mtakuwa wakubwa wao.  Jielimisheni Elimu; na yeyote yule miongoni mwenu atakayeweza kuhifadhi (kukariri) elimu (yaani Hadith), basi aiandike na kuiweka nyumbani mwake."[5]

 

Imeripotiwa kuwa Hujr ibn Adi, mmoja wa Sahaba wa Mtume s.a.w.w. na Imam Ali ibn Abi Talib a.s., aliziandika Hadith za Imam Ali ibn Abi Talib a.s. katika kitabu na kuzirejea pale alipohitaji msaada wa mwongozo katika masuala mbalimbali [6] Mifano hii inadhihirisha umuhimu aliokuwa ameuambatanisha Imam Ali ibn Abi Talib a.s., watoto wake na Sahaba wake katika uandikaji wa Hadith.  Mifano miwili ifuatayo itaonyesha dhahiri vile Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alivyokuwa akisisitiza umuhimu wa Hadith na kuzihifadhi.

 

Umar ibn Ali anaripoti kuwa mtu mmoja alimwuliza Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ni vipi kuwa yeye (i.e. Ali) aliweza kunakili na kusimulia Hadith nyingi za Mtume s.a.w.w. kuliko Sahaba wengineo.  Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alijibu: "Hii ni kwa sababu daima nilipokuwa nikimwuliza swali Mtume s.a.w.w., alikuwa akinijibu maswali yangu.  Na pale nilipokuwa nikiwa kimya, basi Mtume s.a.w.w. alianzisha mazungumzo mwenyewe." [7]

 

Ali ibn Hawshab anaripoti kutoka Makhul, mwanachuo kutokea Syria, kuwa Mtume s.a.w.w. aliisoma Ayah  (69:12)

 

Na hapo alimwambia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. "Mimi nimemwomba Allah swt kuwa masikio hayo yawe ni yako."  Baadaye Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema:  "Mimi kamwe sikusahau Hadith yoyote au chochote kile kilichosikilizwa na sikio langu kikisemwa na Mtume s.a.w.w. [8]

 

Umar ibn al-Harith anasema: 

"Wakati mmoja Ali  a.s. aliuelekeza uso wake kuelekea mbinguni na kuurudisha chini akisema:"Mwenyezi Mungu na Mtume wake s.a.w.w. wamesema kweli." "Je, kilikuwa nini?"  Kikundi cha watu kiliuliza.  Imam Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Mimi ni mpiganaji wa vita na vita vinarithishia mtu ulaghai. Vivyo hivyo, ninaweza kukubali iwapo nitaporomoka kutokea mbinguni kwa ajili ya kunaswa na ndege kuliko kumsingizia uwongo Mtume wa Allah swt. Kwa hivyo fuateni chochote kile mukisikiacho kikitoka kwangu........" [9]

 

Kauli juu ya uandishi wa Hadith pia zimenakiliwa kutoka Maimamu wengine.

Al-Imam al-Sadiq a.s. alisema:

"Andikeni na kuieneza elimu yenu miongoni mwa ndugu zenu, na iwapo mtafariki basi watoto wenu watarithi vitabu vyenu.  Itafika siku ambapo patatokea machafuko na hapatakuwapo na mtu wa kumfanya rafiki na wala hapatakuwa na chochote cha kuweza kutegemewa isipokuwa ni vitabu tu....[10]

 

Al-Imam al-Sadiq a.s. pia amenakiliwa kwa kusema:  "Hifadheni vitabu vyenu kwani mutakuja kuvihitaji hivyo siku moja."  Vile vile ameripotiwa akisema kuwa nguvu za moyo na kuhifadhi akilini inategemea mno juu ya maandishi.[11]

 

Abu Basir anaripoti kuwa aliambiwa na Imam al-Sadiq a.s.: "Baadhi ya watu waliotoka Basrah walikuwa wakija na kuniuliza kuhusu Hadith na waliziandika.  Je, kwa nini nawe hauziandiki?"  Na aliongezea kusema, "Elewa wazi wazi kuwa wewe kamwe hautaweza kuhifadhi Hadith bila ya kuiandika."[12]

 

Idadi kubwa ya mapokezi yanaonyesha kuwa Maimamu a.s. walikuwa navyo vitabu na maandishi ambavyo walirithi kutoka vizazi vilivyowatangulia.[13]

 

Katika riwaya nyingine Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ameripotiwa akiwa amesema:  "Ikamateni elimu (kwa kuiandika),"  ambavyo aliirejea mara mbili [14] Imeripotiwa kutoka Ja'bir kuwa Abu Hanifa alikuwa akimwita al-Imam al-Sadiq a.s. "Kutubi" (yaani mwenye vitabu) kwa sababu ya kutumia mno vitabu, na Imam a.s. alifurahishwa kwa jina kama hilo.  [15]

 

Vile vile imeripotiwa kuwa al-Imam Muhammad ibn Ali al-Baqir a.s. ameziandika Hadith za Mtume s.a.w.w. ambazo zilikuwa zikinakiliwa na Jaabir ibn Abdullah Ansaari. [16]  

 

(Ingawaje taarifa hii inaonyesha kuwa siyo ya ukweli kwani Jaabir alikuwa ameshakwisha kufariki wakati Imam a.s. alikuwa na umri wa miaka mitano tu, labda inawezekana kuwa Hadith ziliandikwa na mjumbe).

 


2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH:

 

Kwa kuwa riwaya (desturi) ya uandishi wa Hadith ilikuwapo miongoni mwa Shia tangia mwanzoni, wao walikuwa wanaongoza katika uandishi wa Hadith na Fiqh. Dr. Shawqi Dayf anaandika:

"Mwelekeo na umuhimu wa Mashia katika uandishi wa Fiqh umekuja daima ni madhubuti mno. Sababu nyuma yake ilikuwa ni imani yao katika Maimamu wao ambao walikuwa ni kiongozi wao (haad) na wakiwa wameo ngozwa na Allah swt (mahdi) na fatawa zao zimekuwa zimeshikamana. Kwa hivyo, wao walipatiwa uzito na umuhimu katika misemo ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Na kwa sababu hiyo, mkusanyiko wa kwanza ulifanywa na Mashia, ulifanywa na Sulaym ibn Qays al-Hilali, katika zama za al-Hajjaj." [17]

 

Al-Allamah al-Sayyid Sharaf al-Din anaandika:

“Imam Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na wafuasi wake walitilia mkazo na kufuatilia swala la uandishi kuanzia mwanzo kabisa.  Jambo la kwanza kabisa lililotiliwa mkazo na kufuatiwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ilikuwa ni kuiandika Quran nzima, ambayo aliifanya baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. kwa kuiandika kimpangilio wa ufunulio wa Aya za Qurani.Katika Qurani hiyo pia alikuwa ameonyesha ni aya zipi zilizokuwa 'amm au khass, mutlaq au muqayyad, muhkam au mutashabih. Baada ya kukamilisha hayo, aliendelea na kazi ya ukusanyaji wa kitabu kwa ajili ya Fatimah, ambacho kilikuwa kikijulikana kwa vizazi vyao kama Sahifat Fatimah. Baada ya hayo, aliandika kitabu juu ya diyat (fidia) ambacho kilijulikana kama Sahifah.  Ibn Sa'id amenakili hivyo katika musnad kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. mwishoni mwa kazi yake mashuhuri al-Jami.'  Mtunzi mwingine wa Kishia ni Abu Rafi, ambaye alikusanya maandiko yakiitwa kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya. [18]

 

Marehemu Sayyid Hassan al-Sadr anaandika kuwa Abu Rafi, aliyekuwa mawla wa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyekuwa wa kwanza miongoni mwa Mashia kwa kukikusanya kitabu. [19]  al-Najashi katika Fihrist ameelezea kuwa Abu Rafi alikuwa ni mtunzi katika kizazi cha kwanza cha Mashia.  Mfuasi wa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Abu Rafi alishiriki katika vita vya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na alikuwa ni mwangalizi wa hazina ya Serikali huko Kufah. Kitabu chake kilichokuwa kikiitwa Kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya, ambacho kilikuwa kimeanza kwa sura izungumziayo Salat, kufuatiwa na sura juu ya Saumu, Hajj, Zakat, kutolewa kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. katika Kufah, Kitabu hiki kilinakiliwa na Zayb ibn Muhammad ibn Ja'afer ibn al-Mubarak katika nyakati za al-Najashi.

 

Ali ibn Abi Rafi, mwana wa Abu Rafi, aliye tabi't na Mshia khalisi ameweza vile vile kukusanya kitabu kilichokuwa na sura mbali mbali juu ya mambo ya Sheria kama vile wudhuu, Salaat, n.k.  [20]

 

Kama ilivyoelezwa hapo awali, abu Hanifa alimwita al-Imam al-Sadiq a.s. kutubi (akisema 'innahu kutubi' ) sifa ambayo ilimtambulisha na wengineo.  Wakati Imam a.s. aliposikia kuhusu hayo, alicheka na kusema,  "...... lakini kila alichokisema kuwa kwangu suhufi ni kweli; mimi nimesoma suhuf (vitabu) vya mababu zangu." [21] Riwaya hii inaonyesha kwa wazi wazi kuwa Imam a.s. alikuwanavyo vitabu fulani ambavyo alipewa na mababu zake, na hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Ahl al-Sunnah walikuwa hawakutilia mkazo katika uandishi wa Hadith.

 

Miongoni mwa mapokezi ambayo inatuonyesha kuwa ma-Imam a.s. walikuwa navyo vitabu kama hivyo, ni mojawapo iliyoripotiwa na Muhammad ibn 'Udhafir al-Sayrafi anasema:

"Mimi nilikuwa pamoja na al-Hakam ibn Utaybah na tulimtembelea al-Imam al-Baquir a.s. Al-Hakam alimwuliza swali Imam a.s. Abu Ja'afer a.s. alikuwa akimstahi sana. Wao walitofautiana juu ya swala fulani na hapo Abu Ja'afer alisema: "Mwanangu (mtoto wake), inuka na ukilete kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Huyo mtoto alimletea kitabu kikubwa, ambacho Imam a.s. alikifungua, na kulipitishia macho hadi kulipata swala walilokuwa wakilizungumzia. Na hapo Abu Ja'afer a.s. alisema:  "Haya ni maandishi ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na yaliyosemwa na Mtume s.a.w.w..........."[22]

 

Katika riwaya nyingineyo ameripotiwa Imam al-Baquir a.s. akisema: "Katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. nimepaona ambapo Mtume s.a.w.w. akisema: 'Wakati zakat itakapokuwa hailipwi, basi baraka itapotea kutoka ardhi."  [23]

 

Vile vile ipo imeripotiwa kuwa Imam al-Sadiq a.s. amesema:

Baba yangu alisema:  "Mimi nimesoma katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume s.a.w.w. ameandika mkataba baina ya Muhajirun na Ansar na watu wengineo wa Yathrib ambao waliungana naye, ikisemwa humo hivi:  "Jirani ni sawa na mtu mwenyewe; asitendewe visivyo haki au kutendewa madhambi. Utukufu wa jirani wa mtu ni sawa na ule utukufu wa mama yake." [24]

 

Katika riwaya nyingine al-Imam al-Sadiq a.s. amesema:

Imeelezwa katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. "Mfano wa dunia ni sawa na mfano wa nyoka: ngozi yake nyororo mno, lakini ndani yake ni sumu kali mno. Mtu aliye mwenye busara hujiweka naye mbali, lakini jahili anafanya kila aina ya jitihada ya kutaka kuikaribia." [25]

 

Kwa mujibu wa riwaya nyingineyo, habari ifuatayo imetoka katika kitab adab Amir al-Muminiin:

Mtu yeyote asijaribu kurejea katika mithali katika masuala ya Din, kwani amri ya Allah swt haiwezi kutambuliwa kwa mithali.  Watatokezea watu ambao watakuwa wakirejea katika mithali, na hao watakuwa na uadui pamoja na Din. [26]

 

Zurarah anaripoti:

Nilimwuliza al-Imam al-Baquir a.s. kuhusu hisa ya babu katika urithi.  Imam a.s. alijibu: "Sijawahi kumwona mtu yeyote yule akilisemea swali hili bila ya kuongezea mawazo yake ya kibinafsi, isipokuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s.." Mimi nilimwuliza: "Na jee alisema nini?" Imam a.s. alinijibu: "Njoo kesho, mimi nitakusomea kutoka kitabuni." Mimi nilisema, "Mimi niwe fidia juu yako, naomba uiseme katika mtungo wa Hadith kwani Hadith zako ni afadhali kwangu kuliko kukisoma kitabu." Imam a.s. alisema: "Tafadhali usikilize kile nilichokuambia. Njoo kesho na mimi nitakusomea kutoka kitabu hicho." Siku ya pili mimi nilimwendea Imam a.s. wakati wa adhuhuri. Jaafer ibn Muhammad mwanae Imam a.s. alinikaribia na Imam a.s. alimwambia kunisomea kitabu hicho........[27]

 

Katika riwaya nyingine, Imam al-Sadiq a.s. anasema:  "Ipo imeelezwa katika Kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa mtu anywaye pombe na mwenye kumsaidia aliyelewa (muskir) basi wote wanastahili kuadhibiwa, ambavyo ni sawa katika sura zote mbili." [28]

 

Muhammad ibn Muslim, Sahaba wa Imam al-Baquir a.s. asema:  "Abu Jaafer alinisomea kitabu kitab al-faraidh, ambacho yalikuwemo yaliyosemwa na mtume s.a.w.w. na kuandikwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s.." [29]

 

Habari zote zilizotajwa hapo juu, ambazo ni chache sana kutokea riwaya nyingi mno kama hizo, zinatudalilisha kuwa desturi ya Mashia ya kuandika Hadith imetangulia mawaidha ya ma-Imam a.s. kwa sahaba wao kuhusu uandishi wa Hadith.  Ilikuwa ni desturi ambayo ilianzia katika zama za Mtume Mtukufu s.a.w.w. na ilikuwa imeanzishwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Zipo Hadith, nyingi katika desturi ya Mashia ambazo zimetimiza kanuni za tawatur, na vile vile yapo marejeo katika Sunni ambazo zinathibitisha na kushuhudia Hadith kama hizo.

 

Mambo yote hayo yanakuelekeza katika uimara na uhakikisho wa usahihi wa Hadith zilizonakiliwa na Mashia.  Hii ni kwa sababu pamoja na kuendelea na maongozo ya Maimamu a.s. hadi kufikia katikati ya karne 3 A.H./9 A.D., Hadith za Mashia zilitoa watunzi wengi mno na ambao maandishi yao kuanzia kipindi cha al-Imam al-Sadiq a.s. yamekuwa kwa hakika ni katika idadi kubwa sana.  Iwapo mtu ataweza kutupia macho Rijal al-Najashi, basi huyo ataweza kuona kuwa wafuasi wa Imam a.s. wametupatia kazi kubwa ambazo zimetumika kama misingi ya Fiqh katika Ushia.

 

Ukweli ni kwamba, Mashia idadi yao ndogo kwa upande mmoja na maisha ya hatari waliyokuwa wakiishi kwa upande wa pili ambayo iliwazuia watu waovu na wenye kuvizia majukumu kuingia katika Ushia pamoja na umuhimu uliosisitizwa na Maimamu a.s. na wafuasi wao katika uandishi, ndivyo vilivyoleta matokeo ya utajiri na usahihi wa Fiqh ya Kishia.  Haya ndiyo faida ambazo hazikupatikana kwa Ahl al-Sunnah kwani, kwanza, wingi wa idadi yao, pili, kwa kuwa madhehebu ya Sunni ndiyo iliyokuwa Dini ya utawala wa Dola, na tatu, kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa kwa Waislam kwa ujumla kuyafuatilia yale yanayotokana na ukweli wa misingi ya kihistoria.

 


3.  HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI:

 

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D.  Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H.  kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio.  Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa.  Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake.

 

Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith.  Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana.

 

Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith.  Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith.  Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith.

 

Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani.  Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili.  Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao,"  wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.

 

Wao walizihifadhi Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu).  Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao.  Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo.  Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.

 

Al-Zuhri anasema:

"Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo.  Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga."

 

Al-Zuhri anaendelea kusema:

"Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao.  Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza):  Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?" [30]

 

Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote.  Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Talib a.s. waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo.  Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith.[31]

 

'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. [32] Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtume s.a.w.w. [33]  Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm: "Andika Hadith yoyote ile ya mtume s.a.w.w. uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka."  [34] Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtume s.a.w.w. [35]

 

Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo.

 

Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa.  Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia.

 

Hadith za kusemwa mdomoni tu  (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza  kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D.  Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo.

 

Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.)  Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith.[36]

 

Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D.  Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah.  Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.[37]

 

Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." [38]  Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. [39]  Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtume s.a.w.w.  Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." [40]

 

Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.

 

Ibin Hajar anasema:

“Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba, wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji.  Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam. [41]

 

Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. [42] Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili:  Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili.  Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo:

 

“Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo.  Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith.  Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika.  Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa.  Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas.  Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah.  Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida. [43]

 

Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa.  Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi  na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi.  Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D.

 

Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. [44]  Yahya al-Hamani [45] huko Kufah na al-Musd [46] huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

 


4.      SABABU ZA UCHELEWESHO KATIKA UANDISHI WA HADITH:

 Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif).   Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtume s.a.w.w. kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtume s.a.w.w. , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa.  Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

 

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah Mtume s.a.w.w. Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume s.a.w.w. , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume s.a.w.w. hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao.  Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

 


HADITH NI NINI ?

Mawaidha na Nasiha maneno aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Hadith kwa kifupi, maneno yoyote yaliyotoka mdomoni kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mbali na ayah za Qur'an Tukufu, ama yale aliyoyatenda kuonyesha, hayo yote ni Hadith. Vile vile maneno na matendo yote ya Ma’asumin a.s. pia ni Hadith yaani yataingizwa katika Hadith. Kutokana na Hadith sisi tunaweza tukajua na kufuatilia na kutekeleza mambo ambayo ni usuliFuru’, Sunnah na faradhi.

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa maisha yake yote alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. popote pale alipokuwa akiwapa watu nasiha na mawaidha katika mambo mbalimbali na kuwaongoza katika masuala mbalimbali basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. daima alikuwa akinufaika na hayo yaliyokuwa yakisemwa na kutendwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ndivyo alivyosema “Sisi ndio dalili za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile ndio Sahaba wake halisi, na sisi ndio ufunguo wa hazina yake ya ilimu na mlango wa mji wake wa ilimu[47] alioutangaza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mtu yeyote hawezi kuingia katika nyumba au mji isipokuwa kwa kupitia mlango wake.”

 

Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi nina ilimu na ma’arifa ya Utume na maneno ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Sisi Ahlul Bayt a.s. ni milango ya hekima na kwa hakika sisi ndio tunayo nuru ya hukumu za Allah swt. (Nahjul Balagha).

 

Katika historia tunapata habari kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ndio aliyekuwa mtu ambaye amekusanya na kuwa na hazina kubwa ya Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Tumepata kuona kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye daima alikuwa akiziandika Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuzielewa na kuzikariri vyema kabisa. Na kwa amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndipo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alitayarisha kitabu kimoja ambamo kumeandikwa Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Sunnah zake, na kitabu hicho kinaitwa Sahifat Jami’a na kitabu kingine kinaitwa Kitabul Faraidh, ambamo katika vitabu hivyo vyote viwili kumeandikwa Ahkam za Sharia.  Vitabu hivyo vimenakiliwa katika vitabu vingine mfano Sahih Buhari amenakili kwenye kitabu chake ambao ni upande wa Masunni. Na upande wa Mashi’ah Ma’ulamaa wa Kishi’ah Sheikh Sadduq a.r. amenakili katika kitabu kinachoitwa Manla yahdharulfaqih na Sheikh Tusi a.r. kinachoitwa Tahdhib na Thiqqatul Islam Quleyni r.a amenakili katika Al Kafi.

 


SHIAH NA HADITH [48]

Kwa hakika Mashiah wana mchango mkubwa sana katika uandishi wa Hadith na katika hali ambayo ni sahihi. Na wa kwanza kabisa ni mchango Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambao hauna kifani wala usioelezeka, je litakuwa ni kosa gani iwapo wafuasi wake watamfuata yeye katika kuzidumisha na kuzihifadhi sirat na sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Katika historia vile vile tunapata mambo yaliyowazi kabisa kuwa kulikuwa na baadhi ya Ma-sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambao walikuwa wakikataa kabisa kusiandikwe Hadith kwa sababu ya visingizio kuwa vilikuwa vikigongana na ayah za Qur'an Tukufu. Na wapo Ma-Sahaba wengine pia wameadhibiwa vifungo na adhabu mbalimbali kwa ajili ya kunakili na kusambaza Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Kwa hakika Ibn Hajar anaandika katika Futuh al-Bari utangulizi wake jambo moja la kustaajabisha, kuwa yeye anasema,

“Mwanzoni mwa Waislam kulikuwa na utata katika uandishi wa Hadith, kwa sababu baadhi yao walikuwa wanasema kuwa ni karaha kuziandika. Na katika wale waliokuwa wakisema kuwa ni makuruh alikuwepo ‘Umar bin Al Khattab, Ibn Masoud na Abu Sai’d Al Khudhri. Na katika upande wa pili ambao walikuwa wakieneza Hadith kwa usahihi walikuwa ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na vile vile Anas alikuwapo.  Na kwa hakika Mashi’ah wamekuwa mbele katika kueneza Hadith zilizokuwa sahihi na miongoni mwao nawaletea majina yao:

 

1.   Mtumwa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyekuwa akiitwa Abu Rafi’, na ambaye alikuwa miongoni mwa wale Waislam wa mwanzoni kabisa.

Bwana ‘Abbas mjomba wake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndiye aliyekuwa amempa zawadi huyo, na wakati huyo mtumwa alipompa habari Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mjomba wake huyo Bwana ‘Abbas ameukubalia Uislam, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kusikia hiyo habari njema alimfanya huru huyo mtumwa kwa sababu ya kuleta habari hizo njema. Katika fadhila zake tunaona kuwa yeye alifanya Hijra mara mbili, na amesali katika Qibla zote mbili na amefanya Bay’a ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mara mbili.

 

Na vile vile ameshiriki katika vita vya Jihad vingi sana pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., na baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. yeye hakumwacha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na daima alikuwa naye pamoja. Alikwenda na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. hadi Kufa, Nchini Iraq na alishiriki naye katika vita vitukufu vyote vilivyotokea na alikuwa ni mtu mmoja aliyekuwa akiaminiwa sana na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kiasi kwamba yeye alikuwa akitunza Baitul Maal pia. Yeye alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na tano. Na yeye ni miongoni mwa Rawi wa Kishi’ah [49] wanaoaminiwa na kusadikiwa, naye ameandika kitabu kimoja ambamo ameandika riwaya za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kinachoitwa Kitabu Sunan Wal-ahkam Wal-Qadhaya. Katika vitabu vya ‘ilmul Rijal kitabu hiki ni muhimu sana na chenye faida kubwa sana.

 

2.   Bwana Salman Muhammad (Al Farsi) ambaye baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliandika habari za Jasliq kwa niaba ya Mfalme wa Roma

 

3.   Asbagh bin Nabata, aliandika usia wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alioumfanyia Bwana Malik Ashtar, vile vile aliandika Nasiha alizomfanyia mtoto wake Muhammad. Asbagh bin Nabata alikuwa ni mmoja wa Ma-Sahaba wa karibu sana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.

 

4.   Suleim bin Kais Al Hilali yeye ameandika kitabu chenye Ahadith ambacho kinatumika mpaka sasa hivi na kwa mara ya mwisho kilikuwa kimechapwa huko Najaf Al Ashraf, nchini Iraq. Hadith zake zimetokana na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe na vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ; Miqdad, Salman, Abudhar na wapenzi wa Ahlul Bayt a.s.

 

5.   Mitham al-Tammaar yeye alikuwa mmoja wa Ma-Sahaba mashuhuri na mshupavu wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye naye ameandika kitabu ambacho Sheikh Sadduq amekitumia katika ‘Aamali na vile vile Tabari ametumia katika Basharatul Mustafa.

 

6.   Zaid bin Wahab Aljahni ambaye ametunga kitabu kimoja ambamo ameandika hotuba zote za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alizokuwa akizitoa siku za Ijumaa na Idi, kwa hakika ameufanyia ‘umma huu ihsani kubwa sana. Ibn Hajar na Ma’ulamaa wengine wanasema kuwa huyu bwana Zaid bin Wahab Thiqqah na wanampa Ukuu. Yeye amefariki katika mwaka takribani 96 Hijriyyah.

 

7.   Mkusanyiko mkubwa kabisa wa semi na Dua za Ma’sumin a.s. yanayojulikana kama Sahifa al-Kamila na vile vile inajulikana kama Zaburi Al Muhammad. Kitabu hicho kimekuwa tangia uhai wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na humo kumeandikwa semi zao n.k. ambayo yalikuwa yamesimamiwa kikamilifu na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ndiye aliyefanya mpango huo.

 

8.   Jabir bin Yazid bin Al Harith Al Jaufi, yeye ameziandika yaani yeye katika nuru ya ahadith za Masumin a.s. ameandika Tafsiri, vita vya Jamal, Siffin, na Naherwaan, na vile vile ameandika kuuawa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  Yeye amefariki katika mwaka 128 Hijriyyah.

 

9.   Bwana Abu Hamza Thumali (aliyefariki mwaka 150 Hijriyyah) alikuwa mmoja Sahabi mashuhuri mwaminifu kabisa wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na ameweza kutunga kitabu kiitwacho Annawadir Wa-Dhuhud. Vile vile amefanya tafsiri ya Qur'an Tukufu pia.

 

10. Vile vile miongoni ma Ma-Sahaba wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alikuwa akiitwa Muhammad bin Keis Al Bijalli ambaye ameandika kitabu kiitwacho Qadhaya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

11. Aban bin Taghlib (aliyefariki mwaka 141 Hijriyyah) ni kwamba wote wanaafikiana kuwa yeye ameishi katika zama za Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na Hadith zao alizozileta huyu Aban bin Taghlib zinasemwa kuwa ni Asili. Yaani inamaanisha kuwa Hadith zake hizo yeye alizoziandika zimetoka moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s. na si kwa kupitia watu wengine walizozisikia inamaanisha kuwa ni yeye mwenye amezisikia hizo.

 

12. Takriban waliosomea ilimu ya Hadith ilifikia elfu nne au na zaidi kuanzia katika zama za Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Siku moja Hassan bin Ali Alwashakhi yeye alikutana na wale watu waliokuwa wakizoea kuzisema Hadith si chini ya mia tisa katika Masji Al-Kufa, na wengi wa wale waliokuwa wakizisema hizo Hadith walikuwa wakisema tumeambiwa Hadith hii na Ja’afar bin Muhammad yaani zilikuwa ni Hadith asili ambazo huyo mtu amezisikia moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s.

 

13. Ibn Nadhir katika kitabu chake Fahrist amemwandikia yule Yunusu bin ‘Abdul Rahman na habari zake kuwa ni mtu mmoja mwaminifu na mwenye kutegemewa kabisa ambaye miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Musa al-Kadhim a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. Kwa hakika kitabu hiki ni chenye manufaa sana kiitwacho Jawamiul Aasar.

 

14. Ibn Nadiim katika kitabu chake Fahrist amewaandika watoto wawili wa Sa’id bin Himad ambao ni Hussein na Hassan na vile vile ameandika habari zao pia, kuwa hawa watu walikuwa ni hodari kabisa katika ‘ilimu ya Hadith,Fiq-h na Manaqib. Hao wote walikuwa wana kitabu walichokitunga juu ya Hadith na walikuwa ni miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Muhammad Taqi Al Jawad a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.

 

15. Fadhl Bin Shaazan Nishapouri (aliyefariki 260 Hijriyyah) yeye amewahi kuwa Sahaba wa Maimam watatu a.s. ambao ni, Al Imam Muhammad at-Taqi a.s., Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. na Al Imam Hassan al-'Askari a.s.  Naye ameandika vitabu vitatu:

·         Cha kwanza Kitabul Faraidh Al Akbar,

·         cha pili Kitabu Faraidh Al Awsat,

·         cha tatu Kitabu Faraidh Al-Asghar  ambacho ni mashuhuri.

 

16. Na baada ya hapo hii kazi ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulikuwa umeendelezwa na Ma-Sahaba na wazee na wameweza kuleta kazi nne zilizo kubwa kabisa. Kazi hizo nne ambazo mpaka leo zinajulikana kwa jina la mashuhuri Kutub Al-‘Arbi’a yaani inajulikana kwa jina la vitabu vinne. Kitabu Cha kwanza kabisa ni Al Kafi, ambacho kimetayarishwa na kuandikwa na Thiqqatul Islam Al Quleyni a.r. (amefariki mwaka 329 Hijriyyah) katika kitabu hiki zipo Hadith takribani elfu kumi na sita.  Vile vile kuna kitabu kingine kinachoitwa Man la haydharul faqih ambacho kimeandikwa na Bwana Abu Ja’afer As-Sadduq humo takribani Hadith elfu sita zinapatikana. Vile vile kulikuwa na kitabu chake kingine kijulikanacho kwa jina Madinatul ‘Ilm ambacho Shahid a.r. amekizungumzia.

 

Na kwa kutokana na fitina za zama hizi kitabu hiki hakipo yaani hakipatikani  Na Sheikh Sadduq a.r. katika mwaka 381 Hijriyyah.

 

      Vile vile tunapata vitabu viwili mashuhuri na vyenye faida sana ambavyo vinavyoitwa Tahdhibul Ahkam na kingine Al-Istibsaar vyote vikiwa vya Sheikh Taifah Bwana Ja’afer Muhammad bin Hassan Tusi (aliyefariki mwaka 460 Hijriyyah).  Kwa kuunganisha vitabu vyote viwili zipo Ahadith elfu kumi na nane zilizo andikwa.

     

Kwa hakika katika zama zote hizi ilimu hii ya Hadith na katika nuru ya Ayah za Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ‘ummah umeweza kuwatambua na kuwafuata Ahlul Bayt a.s. na kuweza kujipatia ma’arifa yao na Ma-Sahaba. Katika kila zama kazi zilikuwa zikifanyika kwa kiwango fulani katika kuendeleza jitihada hizi za Hadith lakini katika mwaka wa 11 Hijriyyah kulifanywa kazi moja kwa kiasi kikubwa sana cha kutungwa kwa kitabu kiitwacho Bihar Al Anwar ambacho kilitungwa na Muhaqqiq ‘Allama Majlisi a.r. (aliyefariki 1111 Hijriyyah), kitabu hicho ambacho kilikusanya Hadith kwa wingi. Kwa hakika kitabu hiki kimoja yaani Bihar Al Anwar sisi hatujakipa heshima kiasi inavyotakiwa na wala sisi hatujafaidika nacho kiasi tunachotakiwa kufaidika nacho. Bihar Al Anwar ni kitabu ambacho Hadith ambazo hazikuandikwa katika Kutub Al-‘Arbi’a basi hizo Hadith zinapatikana katika kitabu hiki cha Bihar Al Anwar. Kwa hakika kitabu hiki kina Juzuu ishirini na sita lakini katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Beirut wamejaribu kukipanga katika vitabu vidogo zaidi ambavyo vimefikia Juzuu mia moja na kumi, ambavyo hata mimi ninavyo. Katika zama hizi vitabu hivyo na vingine vingi vinapatikana kwa urahisi katika CD za compyuta ambavyo mtu hana haja ya kujitwisha vitabu hivyo na inakuwa rhisi kutafuta masuala atakayo.

 

Kwa hakika Maulamaa wamefaidika sana na Hadith zilizo andikwa katika Bihar Al Anwar na vile vile inadhihirisha vile wanavyoonyesha kuisifu na kuiheshimu kazi hiyo na hapa nimejaribu kuwaletea baadhi ya majina yao ambao wamekuwa katika zama zake hizo na mmoja miongoni mwao kama Marhum ‘Allamah Majilisi alipewa ruhusa ya kunakili yaani ‘ijaza ya riwaya.

 

1.   Muhammad bin Hassan Hurri ‘Aamili aliyefariki mwaka 1104 na mwandishi wa kitabu kinachoitwa Wasa’il as-Shi’ah, nacho kimechapwa si chini ya Juzuu ishirini.

 

2.   Mullah Muhsin Faiz Khashani aliyefariki 1091 na ambaye ni mwandishi wa Al-wafi  Kitabu hiki kina Juzuu kumi na nne kinazungumzia juu ya Usul, Furu’, Sunan, na Ahkam.

 

3.   Mulam ‘Abdullah bin Nurullah Bahrani mwandishi wa kitibu kiitwacho Al Awalim kitabu hiki kiko katika Juzuu mia moja. 

 

4.   Sheikh Muhammad Ridha bin Abdul Latif Tabrizi, aliyefariki mwaka 1158 na ni mwandishi wa kitabu kiitwacho As-Shifa’.

 

 

Sote kwa pamoja tunaomba kwa Allah swt nguvu zetu na jitihada zetu hizi azikubalie. Iwapo kumetokezea au kumebakia kasoro zozote katika kutarjumu basi tunamwomba Allah swt atusamehe na ninawaomba Wanazuoni na wenye Ilimu wajaribu kusaidia turekebishe kwa sababu katika kukitarjumu kitabu hiki hapakuwapo na matayarisho kamili kuanzia awali.

 

Na kazi hii imefanywa kwa nia njema kwa matarajio kuwa itatumika kwa nia njema na itafaa kutukupeleka mahala pema. Inshallah.

 

Naomba kazi yangu hii niiweke mbele kwa idhini ya Allah swt.

 

Na kuiweka mbele ya Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. iwe ni kama zawadi kwake.

 


UTAMBULISHO WA MA’SUMIIN A.S.

KATIKA AHADITH: KUNIYYAT  NA  ALQAAB

 

Mara nyingi tunaposoma vitabu vya riwaya tunapata majina mengine yaliyotofauti na majina ya asili.  Hivyo tunaona katika Ahadith kuwa Ma’asumiin a.s. wanatambulishwa kwa majina yanayoitwa Kuniyyat au Iaqab, kwa mfano: Qala Abul Hasan ( yaani amesema Abul Hasan ) au Qala Abu ‘Abdillah (yaani amesema  Abu ‘Abdillah) n.k. na hapo ndipo tunakuwa hatuelewi ni Ma’sum a.s. yupi ambaye amesema hayo.

 

Waarabu wanayo desturi ya kuwaita wazee wao si kwa majina yao bali kwa majina mengineyo yaan Kuniyyat au Alqaab.  Hivyo inatubidi tupate ufafanuzi zaidi kuhusu majina hayo yanayotumiwa kwa ajili ya Ma’sumiin a.s zaidi ya mara moja.  Na hivyo Maulamaa wetu wametuelewesha ilivyo sahihi kabisa.

 

Wakati wa kujaribu kufafanua juu ya Laqab au Kuniyyat kunatiliwa maanani kuhusu maneno na maana ya Hadith, zama za kusemwa na habari za wale wanaoziripoti, ndipo hapo panapoweza kutambuliwa kwa Alqaab au Kuniyyat katika Hadith hiyo kunatambulishwa Ma’sumiin a.s. yupi.

 

Hivyo kuelezea hayo na mengineyo, maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa mwanga katika swala hili kwa ujumla:

 

1.  ABUL QASIM

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Imam al-Mahdi a.s. Iwapo  kutaripotiwa riwaya kuwa Abul Qasim tu, basi ijulikane kuwa ni Imam al-Mahdi a.f

 

2.  ABU MUHAMMAD

 Zipo Hadith chache mno zinazojulikana kuwa Imam Hasan a.s. Hata hivyo hiyo ndiyo Kuniyyat yake.

 

3.  ABU ‘ABDILLAH

 Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hussein a.s na vile vile inatumika kwa ajili ya Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

 

4.  ABUL HASAN

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam Musa ibn Ja’afer a.s., Imam Ali ibn Musa al-Ridha a.s. na Imam Ali an-Naqi a.s. Iwapo kutakuwapo na Abul Hasan tu katika riwaya, basi kutatambuliwa Imam Musa ibn Ja’afer a.s. Na iwapo kutaandikwa Abul Hasan Thani (Abul Hasn wa pili) basi kutakuwa kumefanywa ishara ka Imam Ali ar-Ridha a.s. na pale panapoandikwa Abul Hasan Thalith (Abul Hasan wa tatu) basi tujue kuwa kunamaanishwa Imam Ali an-Naqi a.s.

 

5.  ABU MUHAMMAD

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam  Hasan a.s., Imam Zaynul Aabediin a.s na Imam Hasan al-‘Askari a.s. lakini iwapo kutaandikwa riwaya kwa Abu Muhammad tu tutatambua kuwa riwaya hiyo ni kutoka Imam Hasan al-‘Askari kwa sababu riwaya za Imam Zaynul Aabediin a.s. zinatajwa kwa jina lake tu, bali zipo riwaya chache mno tu kwa Kuniyyat yake.

 

6.  ABU IBRAHIM

Katika Hadith Kuniyyat hii inatumika hasa kwa ajili ya Imam Musa ibn Ja’afer a.s.

 

7.  ABU IS-HAQ

Kuniyyat hii inatumika kwa kumtambulisha Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

 

8.  ABU JA’AFER

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Imam Muhammad Taqi a.s

 

Lakini iwapo kutakuwapo na Abu Ja’afer tu au Abu Ja’afer Awwal, (Abu Ja'afer wa kwanza) basi ijulikane kunamaanishwa kwa Imam Muhhammad al-Baquir a.s.

 

Na iwapo kutaandikwa Abu Ja'afer Thani (Abu Ja'afer wa pili) basi kutambuliwe kuwa ni Imam Jawad a.s.

 

Kwa mara chache mno Abul Hasan inatumika kwa ajili ya Imam Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. lakini mahala pengi mno kunatumika Kuniyyat yake mahsusi ya Abul Hassanain.

 

 

 

 

 


ALQAAB.

Wakati pale utakapoona riwaya zinanakiliwa kutoka kwa ‘Aalim, Sheikh Faqih au ‘Abdi Salih, basi mutambue kuwa kunamaanishwa kwa Al Imam Musa al-Kadhim a.s.

 

Vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anajulikana kwa alqaab zifuatazo: Abu ‘Abdillah, Faqih na ‘Aalim.

 

‘Allamah Majlisi a.r. anasema kuwa mahala pengi mno katika riwaya kunapotajwa Faqih basi kunamaanishwa kwa Imam ‘Ali an-Naqi a.s. na kwa mara chache mno kunatumika kwa ajili ya Imam Hasan al-‘Askari a.s na Imam al-Mahdi a.s.

 

Naqi, Mazii, Sahibul ‘Askar na Hajjul kunamaanisha Imam Hasna al-‘Askari a.s.

 

Sahib na Sahibuddaar zinatukika makhsusi kwa ajili ya Imam al-Mahdi a.s. Lakini Sahibun Nahiyah inapokuja, basi kwa mara nyingine hutumika kwa ajili ya Imam ‘Ali an-Naqi a.s. au Imam Hasan al-‘Askari a.s.

 

‘Allamah Majlisi anasema kuwa mara nyingine katika Ahadith hutumika maneno Ghaib, ‘Alil au Gharim basi inatubidi kuelewa Imam al-Mahdi a.s.

 

Iwapo kutakuwapo bi ahadihima (kwa mojawapo) basi itatubidi tuelewe kuwa ni ishara kwa Imam Muammad al-Baquir a.s. au Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

 

Na iwapo tutakuwa bi ‘Askariyyen, tuelewe kuwa ni Imam Alian-Naqi a.s. na Imam Hasan al-‘Askari a.s.

 

Vile vile iwapo tutaona bi Kadhimain basi kunamaanishwa Imam Musa al-Kadhim a.s. na Imam Mahammad at-Taqi a.s.

 

Kwa mukhtasari, zipo alqaab nyingi ambazo zinajulikana kimakhsusi kwa ajili ya Ma’sumiin a.s. kama vile Amir al-Muuminiin, Mujtaba Shahid, Zaynul Aabediin, Baquir, Sadiq, Kadhim, Ridha, Jawad, Hadi, ‘Askari, na Sahibuz Zamaan (salaam ziwe juu yao wote).

 

 

MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE?

Kwa hakika somo hili ni kubwa na lenye kwenda kwa undani zaidi, lakini kwa ajili ya wasomaji, tunawaleteeni habari hizi kwa kifupi ili kuwafaidisha.

 

Katika lugha ya Kiarabu, mtu anayeripoti riwaya huitwa Rawi na sifa zake zimeelezwa na kubainishwa na Ma’ulamaa walio mabingwa wa ilimu ya Ahadith:

 

1. Rawi lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu. Riwaya zozote zitakazotolewa katika hali ya  kuwehuka au kurukwa na fahamu, basi hazitathaminika au kukubalika.

 

2. Ni lazima Rawi awe amebaleghe na Mukallaf, yaani shariah za Dini ziwe zimeshakwisha kuwa faradhi juu yake. Hapa inawajumuisha vijana na watoto na wale wote ambao bado hawajabaleghe lakini wanaweza kutofautisha baina ya wema na ubaya. Aina hii ya vijana hao huitwa Mumayyiz na hivyo riwaya zao zinapotimika masharti mengineyo, huweza kukubalika na kusadikika.

 

3. Ni lazima Rawi awe Mwislamu.  Riwaya za mtu asiye Mwislamu haziwezi kuaminiwa au kusadikiwa.

 

4. Rawi lazima awe ni Mwislamu mfuasi wa Madhehebu ya Sh’iah Ithna-Asheria.  Lakini iwapo kutakuwa na riwaya kutokea Mwislamu mfuasi wa Madhehebu mengine, basi kwa uzito wa dalili zinginezo na kufanya uchunguzi iwapo huyo Rawi ni mtu aaminiwaye katika historia.

 

5. Uadilifu wa Rawi pia ni sharti mojawapo, yaani asiwe akifanya madhambi makuu (ghunah-i-Kabira) na wala asiwe akirudiarudia madhambi madogo madogo (ghunah-i-saghirah).

 

   Sheikh Tusi a.r. ametilia mkazo swala hili kwa kuelezea kuwa kuna tofauti katika uadilifu wa Rawi na mtoa ushahidi.  Iwapo Rawi ni fasiki na iwapo itathibitika kuwa yeye katika riwaya yake na habari zake ni mkweli bila ya udanganyifu, basi riwaya yake inaweza kufuatwa.

 

6. Rawi asiwe msahaulivu, bali awe ni mtu mwenye kukumbuka vyema na udhibiti wake, (yaani haimaanishi kuwa Rawi asiwe akisahau kama mtu wa kawaida) yaani Rawi anapotaka kuelezea riwaya au Hadith, basi asiwe na mushkeli wa kuikumbuka.


 

AINA ZA AHADITH

Sayyid Ibn Taus a.r. (amefariki 673 Hijriyyah) na ‘Allamaha Hilli a.r. (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-‘arbi’ah ambazo ni kama zifuatazo:

 

1. HADITH SAHIH

    Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma’sumiin a.s.

 

2. HADITH HASAN

   Riwaya ambazo Rawi wake ni Mashiah na ambapo hapakufanywa uchunguzi wowote juu ya uadilifu wao.

   Hadith kama hizo zinajulikana kama hasan kwa sababu Rawi amepokelewa kwa misingi ya husn-dhan yaani kwa dhana njema.

 

3. MUTAWATH-THAQ

   Yaani Rawi wote wawe wakiaminiwa lakini miongoni mwao si wote ambao ni Mashiah.

 

4. DHAIF

   Ni riwaya zile ambazo hazina sifa hata mojawapo za hapo juu.

 

   Tanbih lipo jambo moja la kuzingatia, kuwa Ma’ulamaa wanakubaliana na Hadith zilizo Sahih, Hasan na Muwath-thiq.  Ama kuhusu Hadith zilizo dhaif ni kwamba iwapo atayamkinika kuwa Rawi hao si watu wa kutegemewa lakini maelezo na maana yake ni sawa na maana ile ya Ma’sumiin a.s. na katika sura hii, itaweza kukubalika, na wakati Ma’ulamaa wanaozisimulia basi nia yao huwa juu ya Hadith, bali huwa ni kutoa ushahidi tu.

 


HADITH ZILIZOTOLEWA

Kwa mujibu wa kanuni hizi nne, mmefahamu kuwa Hadith inapoangukia kuwa dhaifu haimaanishi kuwa ni Hadith ya uongo, yenye mfululizo dhaifu, na kwa dalili zinginezo na kwa nyenzo zinginezo inaweza kuthibitika kuwa Hadith hiyo inaweza kukubalika, Lakini inapokuwa imekosewa kabisa basi huitwa Kidhb (uongo) au Iftira’ (tuhuma).  Yaani utaratibu uliotumiwa wa kuwanasibisha Ma’sumiin a.s. haupo wenye ukweli, bali tunaweza kusema kuwa ni tuhuma.  Hadith hizo ni uzushi mtupu.  Katika historia ya ilimu ya Hadith, utaratibu huu mmoja ni tatizo kubwa mno kuling’amua iwapo Hadith hii ni uzushi au la.

 

Sayyid Murtadha ‘Alamal Hudaa a.r. anasema:

“Zipo baadhi ya sehemu za Hadith katika Mashia na Waislamu wote kwa ujumla ambazo zimejazwa makosa na uzushi ambazo zinatufanya kuzichukulia kuwa ni Hadith za uongo.  Katika Hadith hizo kuna mambo fulanifulani ambazo kwa hakika si rahisi kukubalika kiakili na ni pingamizi mtupu.  Kwa mfano imani juu ya jabr (ushurutisho) yaani mwanadamu ameshurutishwa na Allah swt katika matendo ya madhambi na uasi, au siku ya Qiyamah Allah swt ataonekana n.k. na hivyo inamaanisha kuwa kunahitajika uchuguzi na utafiti mkubwa katika kuthibitisha ukweli wa usahihi wa Hadith kama hizo.”

 

Imam Ali a.s. amesema: “Mtume Muhammad s.a.w.w. alisema

“Enyi watu, kumekithiri mno kuninasibishia mambo ya uzushi, hivyo mutambue kuwa mtu yeyote kwa makusudi ataninasabisha na uongo au uzushi wowote, basi hakuna mahala pale pengine isipokuwa ni Jahannam tu.”

 

Katika zama hizi ni lazima kufahamu ‘Ilmul Hadith na Rijal yaani kujua habari za wale wenye kuleta riwaya.  Kazi hii ni ya wale mabingwa katika fani hii na wala si ya wale wenye ilimu kidogo ambao wamejua Kiajemi na Kiarabu kidogo hivyo wakaanza kuwapotosha watu.

 

Sasa tuangalie ni kwa sababu gani kumetokezea haja ya kutaka kuzichuja Ahadith na tuwaangalie watu mbalimbali ambao wamefanya juhudi za kuingiza uongo na uzushi na tuhuma katika Ahadith.

 

(1).  Baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kulizuka mgogoro kuhusu ukhalifa ambapo kulitokezea makundi mawili.  Kundi moja likidai kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amekwisha elezea ni nani atakaye kuwa Khalifa baada yake na kundi la pili likaanza kuzua Hadith kuwa swala hilo liachiwe ‘ummah wa Kiislamu kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema kuwa ukhalifa baada yake hautatokana na Bani Hashim (uzushi mtupu).

 

(2). Wakati Uthman alipouawa, basi Ma’uwiya bin abi Sufiyan kwa hila zake alitupa tuhuma za mauaji yalilengwa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Hapo kuliibuka Hadith za kuzuliwa katika kuwatukuza Bani Umayyah, umadhulumu wa Uthman na hukumu juu ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  katika mauaji ya Uthman.  Si hayo tu, bali Hadith zile zilizokuwa zikielezea fadhila za Imam Ali a.s. pia zilianza kubadilishwa na kupotoshwa.  Mfano, ipo ayah ya Qur’an tukufu: ‘wa minanaasi manyashrii nafsahubtighaa mardhatillah’ Aya hii inatoa shuhuda ya tukio lililotokea katika usiku wa Hijrah ambapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  alijitolea nafsi yake kwa ajili ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Kwa amri za Mu’awiyah, Hadith hii ikageuzwa kuwa imeteremka kwa ajili ya Ibn Muljim kwa sababu yeye alikuwa ameiweka nafsi yake hatarini katika kumwua Imam Ali a.s.

 

(3).  Makhariji walizua Hadith chungumzima kuhusu akida zao na Waislamu kwa ujumla pia walizizua  Hadith nyingi mno katika upinzani wao

 

(4).   Ma’ulamaa wa Kiislamu walianza kuzua na kutumia hizo Ahadith katika kuzieleza na kuziendeleza fikra, nadhiri na akida zao.  Mu’tazila, Tasawwuf, Gulat na Ash-Ari na wengineo wote wakaanza kuzua Hadith katika kueneza imani zao.  Iwapo utabahatika kukisoma kitabu kiitwacho Ihyaul Ulumiddiin basi ndipo utakapokuja kujua hali halisi ya uovu huu wa kuzua Ahadith za kiuongo dhidi ya Ma’sumiin a.s. ambazo kwa hakika hazikubaliki kuwa zimesemwa nao.  Kwa kutoa mfano, tunawaleteeni chache ili muweze kuziangalia:

 

(a).   Ahmad bin Mansur anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Baina mikono miwili ya Allah swt kuna maandiko fulani ambamo kuna majina ya wale watu ambao wanaitikadi kuhusu kuwapo kwa uso na kuonekana kwa Allah swt siku ya Qiyama.  Na Malaika wanaona fakhari kwa majina hayo!

 

(b).  Mamun bin Ahmad Harwi anamnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema:

“Kuna mtu mmoja katika ‘Ummah wangu ambaye ni hatari hata kuliko Shaytani, na jina lake ni Muhammad bin Idris (yaani Imam Sahfi’i) na vile vile kuna mtu mwingine ambaye yuko sawa na nuru kwa ‘Ummah wangu, na jina lake ni Abu Hanifa.”

 

Tanbii: Mwandishi wa Lisanul Mizaan anaandika kuwa sababu kubwa ya kuizua Hadith hii ni kwamba huko Khurasan, wafuasi wa Imam Shafi’I walikuwa wengi.

 

(c). Ahmad bin Nasr anasema kuwa siku moja alimwota Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika ndoto akimwambia;

“Itakuwa wema kwako kumtii Shafi’i kwani anatokana nami na Allah swt yu radhi naye”

 

(d). Kwa hakika jambo lakusikitisha mno ni kwamba hawa wataalamu wa kuzua (wazushi) ni watu ambao wameilimika vyema katika masomo ya Qur’an na Hadith.  Mafunzo ya Qur’an hayakuwa yenye maana kwao bali wametilia mkazo masilahi na ulafi wa dunia hii.

 

Ayatullah al-Khui r.a. anaandika katika kitabu chake Al-Bayan fi tafsiril Qur’an, Uk. 28 kuwa kuna rundo kubwa kabisa la riwaya za uongo na zilizozuliwa, ambamo hawa wazushi wamechukua tahadhari kuwa kusije kukapunguzwa fadhila za Qur’an, basi wamezua Hadith zao binafsi; na wamezirembesha kwa fadhila mbalimbali kiasi kwamba zinapopimwa kwa kauli za Allah swt zinajulikana kuwa ni za uongo mtupu.  Mfano Abu Ismah Faraj bin Abi Maryam al-Maruzi, Muhammad bin Akasha al-Kirmani, Ahmad bin Abdillah Juibarri na wengineo wengi.

 

Wakati mtu mmoja alipomwuliza Abu Ismah kuwa amezitoa wapi Hadith chungu mzima kutokea kwa Ikramah na Ibn ‘Abbas kuhusu fadhila za Sura moja moja za Qur’an tukufu ?  Alianza kusema: “Mimi niliona kuwa watu wameanza kuipa mgongo hiyo Qur’an na badala yake wanajishughulisha mno na fiqhi ya Abu Hanifa,  watu wamejishughulisha kuisoma Maghazi  ya Muhammad bin Is-Haq, basi mimi nimezusha Hadith hizo juu ya Qur’an kwa kutaka furaha ya Allah swt ………….!

 

(e).  Wakati kulikuwapo utawala wa Bani ‘Abbas, basi Ma’ulamaa wenye tamaa ya dunia walizizusha Ahadith nyingi mno katika kuelezea fadhila za watawala hao.  Katika Tarikhul Khulafa anaandika as-Sayyuti:

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa yeye alipoona kuwa Bani Marwan wanachezea Mimbar yangu, basi hapo mimi nilisikitishwa mno.  Na hapo baadaye nikaona Bani ‘Abbas pia wanachezea, na kwa hayo mimi nilifurahishwa  mno.”

 

Abu Hurairah ananakiliwa riwaya moja kuwa siku moja Mtume Muhammad s.a.w.w. alitoka nje, na hapo alikutana na Baba mkubwa ‘Abbas, na alimwambia: “Ewe Abul Fadhl ! Je nikupe habari njema ?

 

‘Abbas alisema:

“Naam, Ewe Mtume wa Allah swt !” Ndipo Mtume Muhammad s.a.w.w. aliposema: “Allah swt ameitengeneza swala hili (yaani Dini hii ya Islam) kwangu na kuishia kwa ‘Ummah wangu.” Na akaendelea kusema: “Wakati kizazi chako kitakapoishi Iraq, watakuwa na usukani huu wa Islam kwa muda mpaka atakapodhihiri Mtume Isa a.s. na kumkabidhi.”

 

Tanbihi: Ni jambo la kushangaza mno kuwa huyu huyu as-Suyuti ameandika kitabu kimoja juu ya masuala ya uzushi kiitwacho Al-Lulil mansukh (Lulu bandia) na amewatahadharisha Waislamu kujitahadharisha na Hadith kama hizo za uzushi, pamoja na hayo yeye mwenyewe amenakili riwaya nyingi mno zilizo bandia na Ahadith zilizo zuliwa na hivyo ameshiriki kikamilifu katika kuifikishia Islam jeraha kubwa.

 

(f).  Baadhi ya makafiri na maadui wa Islamu wamekuwa wakiishi miongoni mwa Waislamu na kujihusisha katka harakati za kueneza sumu hii miongoni mwa Waislamu kwa hila na njama mbalimbali.  Wao ili kutaka kutimiza mikakati yao hiyo ya kueneza upotofu, wamekuwa wakijishughulisha na uzushi wa Ahadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. na Ma’sumiin a.s. na walikuwa wakizileta mbele ya watu. Ibn Abil Awjah amekiri mwenyewe kuwa yeye ameingiza kiasi cha Ahadith zipatazo elfu nne zilizozuliwa miongoni mwa Ahadith zilizo za kweli.

( ! )

 

(g).  Katika kipindi cha mwanzo cha Islam, watu walikuwa na shauku kubwa ya kusikiliza visa na masimulizi mbalimbali na katika hali hii kuliibuka wasimulizi wengi wa masimulizi kama hayo na hivyo wao walikuwa wakifanya kila jitihada za kukusanya habari na porojo za kila aina na walikuwa wakiongezea chumvi na pilipili ili kwamba mazungumzo yao yalete ladha nzuri na kuwavutia watu.  Matokeo yakawa ni kwamba Mayahudi walikuwa wamezusha visa na hadithi nyingi kuhusu mitume yao, hivyo mazushi hayo yakapata soko kubwa miongoni mwa Waislamu, na rundo kubwa hili linajulikana kwa jina la Israiliyyaat [50] Hadith zilizozushwa juu ya Mitume a.s. inapatikana katika Tarikhul Ambiya’ na hususan katika tafisiri za Ayah ambazo zinazungumzia habari za Mitume a.s.

 

Ibn Jawzi anaandika kuwa Imam Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu’in walikuwa wakisali Msikitini na wasimuliaji wakaja wakatandika mikeka yao tayari kuanza masimulizi yao mbele ya halaiki kubwa ya mashabeki wao.

 

Wasimulizi wakiendelea na masimulizi yao, wakasema: “Mimi binafsi nimemsikia Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu’in kuwa wao wamewasikia Rawi fulani fulani kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Mtu yeyote atakaye sema La ilaha Illallaah basi Allah swt atamwumba ndege mmoja ambaye mdomo wake utakuwa wa dhahabu na macho ya marjaan………”  Hivyo wao walizielezea habari za ndege huyo, na kama tukianza kuziandika tutaandika kurasa ishirini zinginezo.

 

Kwa hakika watu walipoyasikia haya walianza kuyumba na kwa kutoa shukurani zao walianza kuwatupia mapesa hao wasimulizi, nao walibakia kimya kwa muda zaidi kidogo ili waendelee kupata zawadi zaidi, na hapo ndipo Yahya bin Mu’in alipojitokeza na kumwita aje mbele yake.  Msimulizi alikuja mbio mbio hapo mbele kwa kutarajia kupata zawadi nono, ndipo Yahya alipomwuliza: “Je habari zote hizi zisizo na miguu umeyatoa wapi?” Akajibu: “Nimemsikia Yahya bin Mu’in na Ahmad bin Hambal.”

 

Yahya na Ahmad bin Hambal walishikwa na bumbuwazi na walibakia wakitazamana, na hapo ndipo Yahya kwa hasira alimgeukia msimulizi na kumwambia: “Je hauoni aibu? Wewe umethubutuje kuzusha uongo dhidi yetu ilhali tukiwa mbele yako ? Jina langu ni Yahya bin Mu’in na huyu ndiye Ahmad bin Hambal.”

 

Yule msimulizi alianza kusema: “Mimi daima nimekuwa nikisikia kuwa Yahya bin Mu’in ni mtu mpumbavu na mjinga kabisa, na kwa hakika nimepata uthibitisho huo leo hii, kwa hakika ni ajabu kubwa !.  Je dunia hii nzima ina Yahya bin Mu’in na Ahmad bin Hambal nyie wawili tu na wala haina wengine?  Kwa kusema ukweli mimi nimewanakili riwaya mbalimbali Yahya bin Mu’in sabini na Ahmad bin Hanbal sabini.” Kwa kusema hayo msimulizi alijiondokea zake.

 

(h).  Kulizuliwa Ahadith nyingi mno katika kutukuza makabila na Miji ya Kiislamu. Tazameni mfano mmoja.  Imeripotiwa kuwa al-Imam ar-Ridha a.s. amesema kuwa Mji mtukufu wa Qum umeitwa hivyo kwa sababu hapo ndipo Safina ya Mtume Nuh a.s. iliposimama baada ya kuisha kwa tufani.  (Katika lugha ya Kiarabu neno Qum linamaanisha kusimama).

 

(i).   Katika zama za Makhalifa watu walikuwa wakijishughulisha mno katika kuzusha Hadith za uongo au kuzigeuza maana ili waweze kupata zawadi, hongo au kutukuzwa miongoni mwa watu.  Katika zama za Mahdi ‘Abbasi ambaye alikuwa khalifa wa Bani ‘Abbas, aliijiwa na mtu mmoja aitwaye Ghiyas Bin Ibrahim ambaye aliwakuta njiwa wengi mno katika kasri ya khalifa, na kwa hayo alisema: “Ipo riwaya kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. kuwa imeruhusiwa mashindano matatu tu yaani ngamia, farasi na njiwa.”

 

Kwa hayo, khalifa alimpa zawadi na wakati alipokuwa akiondoka, khalifa alimwambia:

“Mimi nashuhudia kuwa huyu aliyetupa mgongo amemnasibishia Mtume Muhammad s.a.w.w. uongo.”

 

 


SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH

Ili kuweza kuzitambua ni Hadith za aina gani zilizo za uongo, Ma’ulamaa wetu wametupatia dalili ambazo zitakazotujulisha usahihi na ukweli wa Hadith hizo na masharti ni kwamba mtu yeyote asijitumbukize katka kuzieneza na kuzisherehesha Hadith hadi hapo atakapoweza kuthibitisha kuwa zinastahili hivyo.  Hapa tunawaleteeni kwa mukhtasari:

 

(1). Habari zilizoelezwa katika Hadith zisiwe zikipingana na Ayah za Qur’an tukufu, yaani zisipingane na maamrisho ya Allah swt.  Angalieni kuwa mara nyingi ‘Aam, khaas, mutlaq, muqayyad – kwa kutokujua mambo haya watu wanafikia uamuzi wa kusema kuwa Hadith fulani inakwenda kinyume na Ahadith, kunaleta hatari kubwa ya kupotosha maana sahihi ya Hadith.

 

(2). Hadith kamwe isiwe kinyume na akili bali iwe kwa mujibu wa akili.

 

(3). Iwapo Hadith itakuwa ni salama kwa Dini na Madhehebu, basi ipokelewe.

 

(4). Kwa kuitambua Hadith mambo yafuatayo yanatosha:

(a). Ujue lugha ya Kiarabu na kanuni zake kwa ukamilifu,

(b). Zaidi ya hayo inabidi Lisan-i-Suduur yaani kujua maarifa na ubalagha wa lugha ya Ma’sumiin a.s.

(c).Inabidi kuwa mjuzi wa historia ya Kiislamu na sirah za Ma’sumiin a.s.

(d). Ni lazima ajue Madhehebu na mwanzo wao na kuzijua itikadi zao kwa vyema.

(e). Itabidi mtu huyo awe amejiepusha na ta’assub yaani chuki za aina yoyote ile kwani hapo ndipo hapo atakapoweza kushughulikia bila ya upendeleo au ushawishi wa aina yoyote ile.

 

 


HADITH YA UFUNGUZI

 

1.   Amesema al-Imam as- Zayn al-‘Aabidiin a.s., katika Bihar

al- Anwar, j. 90, uk 187 na Sahifah as-Sajjadiyyah, uk. 572:

“Sifa zote ni za Allah swt, na kusiwa Kwake ni haki Yake: sifa zisizo na kifani ndizo zinazomstahiki Yeye. Na mimi najiepusha kwa msaada wake dhidi ya shari za nafsi yangu: Kwa hakika mwanadamu yupo katika kutenda madhambi isipokuwa wale waliobarikiwa na Mola wao. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya maovu ya Shaytani ambaye daima ananiongezea dhambi moja juu ya lingine. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya watawala waovu, watawala katili, na maadui wa nguvu.”

 

“Ewe Mola ! Naomba unifanye mimi kuwa mmoja wa Majeshi yako, kwa sababu kwa hakika Majeshi Yako tu ndiyo yenye kushinda; na unifanye miongoni mwa wanachama Wako, kwani kwa hakika, chama Chako tu ndicho kitakachofanikiwa; na unikubalie kama mmoja wa wapenzi Wako, kwani kwa hakika, wapenzi wa Allah swt hawana hofu na kamwe hawatahuzunika.”

 

“Ewe Mola ! Naomba uniimarishie Dini kwa ajili yangu, kwani hiyo ndiyo hifadhi ya matendo yangu yote; na unitengenezee Aakhera yangu,  kwa sababu hakuna shaka kuwa hiyo ndiyo mwisho wangu wa kudumu na kuepukana na watu wenye dharau na dhihaka, na uyafanye maisha yangu yawe ya kuniongezea mema, na mauti yangu yawe ndiyo kujitoa huru kutokana na kila aina ya kasoro za magonjwa.”

 

“Ewe Mola ! Mbariki Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mtume wa mwisho katika jamii ya Mitume yote, na Ahli Bayti a.s. tukufu, na vile vile Masahaba wake wema, na naomba unijaalie mahitaji matatu kwa leo: Usinibakizie dhambi lolote lile isipokuwa umenisamehe na wala huzuni yoyote ile isipokuwa umeniondolea, wala kusikwapo na adui isipokuwa wewe umemwondosha kwa jina lako tukufu la Allah ambayo ni jina bora kabisa i.e.Bismillah, Mola wa Mbingu na Ardhi …..”


KUMJUA ALLAH SWT, UKUU NA BARAKA ZAKE

 

2.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Al-Khisal,

322:

“Enyi Watu ! Kwa hakika hakutakuwapo na Mtume baada yangu, na wala hakutakuwapo na Ummah baada yenu (Waislamu). Hivyo, Muwe waangalifu katika kumwabudu Allah swt, musali sala tano za siku, mufunge saumu katika mwezi uliowekwa (Ramadhaan al-Mubarak), mufanye Hijja ya Nyumba ya Allah swt (Al-Ka’aba huko Makkah al-Mukaramah), mutoe Zaka kutoka mali zenu kwa ajili ya kuitakasisha nafis zenu kwa hayo, na mutii amri za Wale wenye mamlaka, ili muweze kuingia Pepo ya Mola wenu.”

 

3.   Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema, katika Nahjul-

Balagha, Semi na.129:

“Kwa kuwa na tasawwuri ya Ukuu wa Mola wako basi itakufanya wewe utambue udogo wa viumbe katika mitazamo yako.”

 

4.   Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema, katika Bihar

al- Anwar, j. 77, uk. 289:

“Tawba ni kwa ajili ya yule ambaye ametakasisha kwa ajili ya Allah swt matendo, ilimu, mapenzi, bughudha, kuchukua, kutoa, misemo, ukimya, matendo na asemavyo.”

 

5.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., katika Bihar

al- Anwar, j. 70, uk. 25:

“Moyo ni mahala pa takatifu ya Allah swt, hivyo, basi hakikisha hapawi kitu kingine chochote isipokuwa Allah swt tu.” (Moyo mtukufu ni wa Allah swt tu. Hivyo mapenzi ya dunia isivyo sahihi, lazima iwekwe mbali.)

 

6.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., katika Bihar

al- Anwar,j. 93, uk. 162:

“Wafuasi wetu ni wale ambao wanapokuwa peke yao, wanamkubuka Allah swt kwa kupita kiasi.”  (Kwa hivyo, wao hujiepusha kutenda madhambi wanapokuwa peke yao wakati ambapo kuna hakuna kizuizi cha kuwazuia wao wasitende madhambi na badala yake humkumbuka Allah swt kwa kupita kiasi.).

 

7.   Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., katika Al-Kafi,

J.2, Uk. 426:

“Kwa kiapo cha Allah swt ! Yeye, aliyetukuka, huwategemea kwa mawili:wao waungame na kushukuru Kwake kwa neema  ili Yeye awaongezee wao; na waungame kwa madhambi yao ili kwamba Yeye awasamehe madhambi yao.”

 

8.   Amesema al-Imam Husayn ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib

a.s., katika Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 180:

“Kwa hakika, Allah swt, aliye Mkuu, hakuwaumba wanadamu isipokuwa kwa kumjua Yeye na baada ya kumjua Yeye kumwabudu kwa kumjua Yeye; na wakati wanapomwabudu basi kusikuwepo na haja tena ya kumwabudu yeyote mwingine isipokuwa Yeye peke yake.”

 

9.   Amesema al-Imam Zayn-al-‘Aabediin a.s., katika Safinat-ul-

Bihar, uk. 517:

“Hakuna maangamizo (Jahannam au Motoni ) kwa ajili ya Mumiin aliye na sifa tatu : Kuungama na kukubali kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa Allah swt tu peke yake, pekee ambaye hana mshiriki; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni mtetezi; ukubwa usio na kipimo cha Rehema za Allah swt.”

 


SALA  NA  ATHARI ZAKE

 

10.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., katika

Man la Yahdhurul Faqihi, J.1, Uk. 206:

“Mtu yeyote aichukuliaye sala pasi na uzito wake, basi si hatokani nami. Hapana, Kwa kiapo cha Allah swt, mtu kama huyo hatafikia chemchemi ya Haudh Kawtha. “

 

11.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., katika Bihar

al-Anwaar, Juzuu 82, Ukurasa 236: 

 “Iwapo kutakuwapo na mto unaopita nyumbani mwa mtu ambamo mtu huyo anaoga mara tano kwa siku, je kutabakiapo aina yoyote ya uchafu mwilini mwake ?  Kwa hivyo sala ndivyo ilivyo mfano wa mto huo. Mtu ambaye anasali sala zake basi hujiondolea madhambi yake yote isipokuwa kutabakia madhambi yale ambayo yanamtoa katika Imani yake.

 

12.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., katika

Bihar-ul-Anwaar, J.99, Uk. 14:

“Sala iliyofaradhishwa kwa Allah swt ni sawa na kutimiza Hajj elfu moja na ‘Umrah elfu moja ambazo ni sahihi na zilizokubalika.”

 

13.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., katika

Bihar-al-Anwaar, J.83, Uk. 14:

“Kamwe musizipoteze sala zenu, kwa hakika, mtu yeyote anayezipoteza nyakati za sala zake atainuliwa pamoja na Qarun na Hamaan na itamwia haki Allah swt awatumbukize katika moto wa Jahannam pamoja na Munafiqiin (wanafiki).

 

14.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , katika

Bihar-ul Anwaar, Juzuu 69, Uk. 408:

“Musali sala zenu kama kwamba hiyo ndiyo sala yenu ya mwisho”

 

15.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

     Abi Talib a.s. katika Tasnif-I-Gurar ul-Hikam,  Uk.175:

“Iwapo mwenye kusali angalikuwa akifahamu kiasi alichozungukwa na rehema za Allah swt, basi kamwe asingaliinua kichwa chake kutoka hali ya kusujudu”

 

16.   Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir a.s., katika 

   Bihar al-Anwaar, J.7, Uk. 267:

“Siku ya Qiyama, jambo la kwanza litakalo hisabiwa ni kuhusu sala; kwa hivyo, iwapo itakuwa imkubaliwa, basi matendo mengine pia yatakuwa yamekubaliwa (amasivyo matendo yake mengine mema hayatamnusuru)”.

 

17.   Amesema Al-Imam Al-Sadiq a.s. , Bihar Al-Anwaar, J.82,

Uk. 236:

Katika siku za mwishoni mwa maisha yake, Imam As-Sadiq a.s. aliwaita Jama’a na wafuasi wake na kuwaambia “Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye sala kiepesi (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima)”

 

18.   Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir a.s. ,

Al-Khisaal cha Sadduq, Uk. 432:

“Yapo mambo kumi ambayo mtu atakapokutana na Allah swt siku ya Qiyama ataingia Peponi:

§         Kuamini na kukiri kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa Allah swt,

§         Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah swt

§         Kukiri na kuamini kuwa kile kilichoteremshwa juu ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.w.kutokea Allah swt ni Qur’an tukufu,

§         Kutimiza sala

§         Kutoa Zaka

§         Kufunga saumu mwezi wa Ramadhani,

§         Kuhiji Makkah,

§         Kuwatendea mema wale wampendao Allah swt,

§         Kujiepusha na maadui wa Allah swt,

§         Na kujiepusha mbali na ulevi wa kila aina.

 

 

19.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s., katka Nahjul Balagha, Msemo 136:

“Kwa kila mwenye kusali, sala ndiyo sababu kubwa ya kumfanya amkaribie Allah swt,; na kwa yule aliye dhaifu, Hajj – kuhijji Makkah – ni sawa kabisa na Jihadi – kupigana katika njia ya Allah swt. Kwa kila jambo kuna zaka yake, na hivyo zaka ya mwili ni saumu. Jihadi ya mwanamke ni kuwa mwenzi mwema wa mume wake.”

 

20.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , ‘Irshad-

ul-Qulub, Uk. 53:

“Hakuna usiku unaopita isipokuwa Malaika wa Mauti huwaita ‘enyi watu wa maqaburi!’ na huwauliza kile kinachowasikitisha kwa siku hiyo kwa yale waliyoyaona na maisha yajayo. Kwa hayo wafu husema ‘kwa hakika, sisi twasikitika na kuwaonea wivu muminiin wale ambao wapo misikitini mwao ambapo wao wapo wansali wakati sisi hatusali; wao wanatoa zaka wakati sisi hatutoi; wao wanafunga mwezi wa Ramadhan wakati ambapo sisi hatufungi; wao wanatoa misaada kwa kile walichonacho ziada ya familia yao, wakati sisi hatufanyi hivyo; ….”

 

21. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mustadrak-

ul-Wasa’il, J.3, Uk.102:

“Kwa kila wakati uliyofanywa muayyan kwa ajili ya sala , mimi huwa ninamsikia mpiga mbiu ambaye huita na kusema ‘Enyi wana wa Adam ! Dumisheni sala ili muweze kuuzima moto ambao nyinyi wenyewe muliuwasa kwa ajili yenu (kwa kutenda madhambi).”

 

22.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar-ul-

Anwaar, J.82, Uk.202:

“Lazima muwe waangalifu wa Sala, kwani siku ya Qiyama Allah swt atakapomsimamisha mja wake (kwa hisabu) basi jambo la kwanza la kuulizwa litakuwa ni kuhusu Sala. Iwapo mtu atakuwa amekujanayo kamilifu, basi atakuwa miongoni mwa watu waliookoka, ama sivyo, atatupwa Motoni (Jahannam).”

 

23.   Abu Basir Amesema kuwa yeye alimtembelea Umm-i-

Hamidah (mama yake Imam Musa ibn Ja’afar a.s.),

kwa ajili ya kumpa pole kwa kifo cha Ja’afar ibn Muhammad a.s.  Yeye alilia na hivyo yeye pia alilia kwa sababu ya kilio cha mama huyo.  Baadaye, mama yake al-Imam a.s. alisema,  Wasa’il-ush-Shiah, J.4, Uk. 26:

“Ewe Aba Muhammad ! Iwapo ungalikuwa umemwona Ja’afar ibn Muhammad alipokuwa kitandani wakati wa kufariki, basi ungalikuwa umejionea mambo ya ajabu kabisa : Yeye alifumua macho yake na kutaka maJama’a wote wakusanywe.’  Na hapo yeye aliendelea kusema kuwa maJama’a wote walikusanyika bila ya kubaki mtu. Hapo al-Imam a.s. alisema kwa kuwaangalia wote: “Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye Sala kiepesi  (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima)”    

  

24.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar-ul-

Anwaar, J.84, Uk.258:

“Ibada ya yule mtu ambaye mapato yake yanatokana na njia zilizo haramu ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga."

 


SALA ZA USIKU WA MANANE

 

25.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar-ul-

Anwaar, J. 77, Uk. 20:

“Heshima ya Mumiin ipo katika kukesha kwake usiku na utukufu wake upo katika kujitawala  mwenyewe miongoni mwa watu.”

 

26.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

 Abi Talib a.s. , Ghurar-ul-Hikam, Uk. 289:

“Yeyote yule alale zaidi wakati wa usiku, lazima atapoteza kitu mujimu kabisa katika matendo yake (i.e. sala ya usiku) ambayo hataweza kuipata wakati wa mchana.”

 

27.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar ,

J. 13, Uk. 329:

Allah swt katika ufunuo wake kwa Mtume Musa a.s., mwana wa ‘Imran a.s. alisema: “Ewe Mwana wa ‘Imran !  Wale tu ambao wanadai kunipenda mimi, wasema uongo, kwani usiku unapoingia wao hulala huku wakiniacha mimi.”

 

28.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar ,

J.83, Uk. 127:

“Kamwe usiikose Sala ya usiku wa manane ! Kwa sababu, ukweli ni kwamba, mpotezaji ni yule anayeikosa (faida zake) Sala za usiku wa manane.”

 

29. Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Khisal cha Sadduq,

Uk. 72:

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alimwambia Jibrail amwambie chochote, naye alimwambia: “ Ishi utakavyo huku ukitambua kuwa utakuja kufa; penda chochote kile utakacho lakini utatengana nacho; tenda utakavyo lakini utakutana nacho ( na kulipwa malipo yake). Heshima ya Mumin ni Sala yake ya Layl (usiku wa manane), na utukufu wake upo katika kujiepusha (na kuangamiza) sifa za watu.”

 

30.  Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar , 
   J
. 75, Uk. 107:   

“Vipo vitu vitatu ambavyo ndivyo sifa za Muumin na ndivyo vito vya thamani kwake humu duniani na Aakhera. Navyo ni: Sala katika sehemu ya mwisho wa usiku (Salat ul-Layl), kutotamani au kuwa na wivu kwa kile kidogo kilicho mikononi mwa watu, na mapenzi (na uongozi ) wa Imam kutokana na kizazi cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

 

31.   Amesema al-Imam Muhammad ibn Ali al-Jawad ul-

‘A’immah a.s. , Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 79:

“Yeyote yule aliye na imani kamili juu ya Allah swt, anaona furaha; na yeyote amwaminiaye, basi anatosheleza matendo yake.”

 


KUMWAMINI ALLAH NA KUIPATA FURAHA YAKE

 

32.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar,  

J. 71, Uk. 208:

“Baba yangu aliniambia kuhusu baba yake kuwa mtu mmoja kutoka mji wa Kufa alimwandikia baba yake viz. Al-Husayn ibn  Ali a.s., akimwuliza a.s. kumjulisha yeye kuhusu mema ya dunia hii na mema ya Akhera.  Kwa hayo Imam a.s. alimwandikia (katika majibu): “Kwa jina la Allah,aliye Rahmaan na Rahiim’. Baadaye akiendelea ‘Kwa hakika yeyote yule atakaye furaha ya Allah swt hata wakati wa kutokuwafurahisha watu, Yeye humtosheleza katika masuala ya watu. Lakini, yule ambaye hutaka furaha za watu wakati anamuudhi Allah swt, basi Allah swt humwachia watu ( na yeye atakuwa mbali na baraka za Allah swt), Wassalaam’.”

 

33.   Amesema Al-Imam Zayn Al-Abedin a.s. , Al-Kafi, J. 2,

Uk.81:

“Yeyote yule atendaye matendo yake kwa mujibu wa vile alivyoamrisha Allah swt, ni miongoni mwa watu bora.”

 

34.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J.2,

Uk. 124:

“Yeyote yule aliye na mapenzi ya Allah swt,anachukia kwa ajili yake Allah swt, na anatoa msaada kwa ajili ya Allah swt, basi huyo ni miongoni mwa wale ambao Imani yao imekamilika.”

 

35.   Amesema Al-Imam Al-Hasaan Al-Askari, Imam wa Kumi

na Moja, a.s. , Bihar al-Anwaar, J.17, Uk. 218:

“Hakuna sifa zaidi ya hizi mbili: Kuwa na Imani kwa Allah swt na kuwa mwenye manufaa kwa Waislamu.”

 


TAQWA NA UMUHIMU WAKE KWA WAISLAMU

 

36.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar

al- Anwar, J. 71, Uk. 373:

 “Miongoni mwa kitu kilicho muhimu kabisa kwa kuwafikisha watu hadi kufikia Peponi ni taqwa na tabia njema.”

 

37.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar

al- Anwar , J.77, Uk. 130:

 “Wakati wa kutoa uamuzi wa kitu, fikiria matokeo yake. Iwapo ni nzuri kwako wewe kuendelea na maendeleo, fuata hivyo, lakini iwapo inakupotosha, uiachilie mbali …..”.

 

38.   Aliulizwa Al-Imam As - Sadique a.s. kuhusu maana ya

Taqwa, na alijibu , Safinat ul-Bihar, J.2, Uk.678:

“Allah swt hakukosi mahala pale alipokuamrisha wewe uwepo, na hakuoni pale ambapo amekuharamishia wewe kuwepo.”

 

39.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mustadrak

Al-Wasa’il-ush-Shi’h, J.8, Uk.466 no. 10027:

 “Onyesha heshima zako kwa ajili ya Allah swt kama vile utakavyoonyesha heshima zako mbele ya mtu mwema miongoni mwa ukoo wako.”

 

40.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. , Ghura-ul-Hikam, Uk. 321:

“Kwa mtu kuinamisha macho yake kutamwia kama kizuizi dhidi ya matamanio (shahwa) yake.”

 

41.   Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib

a.s. amewaambia wana wake Al Imam Hassan ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. wakati ‘Abdur Rahman ibn Muljim (Allah amla’ani) alipokuwa amempiga dharuba ya upanga kichwani mwake, katka Nahjul Balagha, Barua no. 47:

“Ninawasihini nyote mumwogope Allah swt na nyinyi wala musiwe na uchu wa starehe za dunia hii hata kama itawakimbilia nyinyi. Wala musikisikitikie kitu chochote cha dunia hii ambacho mumekikosa. Semeni ukweli na mutende (kwa kutumai) malipo. Muwe adui wa mdhalimu na msaidizi wa mdhulumiwa.”

 

42.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. , Nahjul Balagha, Barua no. 31:

“Ninawauusieni kumwogopa Allah swt, Ewe mwana wangu, kubakia katika Amri Zake, kuujaza moyo wako kwa ukumbusho Wake na kubakia katika kumtegemea Yeye tu. Hakuna Hakuna ushikamano unaotegemewa kuwa madhubuti baina yako na Allah isipokuwa wewe iwapo utaishikilia menyewe.

 

43.   Abi Osama Amesema kuwa alimsikia Al Imam Ja'afer as-

Sadiq a.s.  akisema, Al-Kafi, J.2, Uk. 77

“Muwe nakhofu za Allah, taqwa, ijtihadi, kusema ukweli, uaminifu katika amana, tabia njema na ujirani mwema. Muwaite wengine kwenu (kwa tabia zenu njema), wala si kwa maneno tu. Muwe watu wenye kupendeza na kamwe musiwe watu wa kutuaibisha. Ninawausieni murefushe rukuu’ na sujuda zenu.  Kwani kila mmoja wenu anaporefusha rukuu’ na sujuda basi Shaytani hulia nyuma yenu kwa kusea ‘ Ole wako ! yeye ametii; amesujudu na mimi nilikataa.”

 

44.   Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein bin Al Imam ‘Ali

ibn Abi Talib a.s.  Amesema, Bihar al- Anwar , J.69, Uk. 277:

 “Kwa hakika marafiki wa Allah hawatakuwa na khofu yoyote juu yao wala hawatakuwa watu wenye kuhuzunika) iwapo watadumisha yaliyofaradhishwa na Allah swt, wakafuata Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.wakajiepusha na yale yaliyoharamishwa na Allah swt, wakawa wacha Allah swt wema katika kile walichonacho katika utajiri na wadhifa wa humu duniani, wakajitahidi kujitafutia kile kilicho halali, wakaamua kutojifakharisha wala kutojilimbikia katika mali na utajiri isipokuwa katika kutoa misaada na kutoa malipo ya kulipa yaliyofaradhishwa kwake. Basi kwa hakika hao ndio waliobarikiwa katika mapato yao na watalipwa mema kwa yale waliyoyatanguliza huko Aakhera.”

 

45.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ,

Mustadrak al-Wasa’il, J. 12, Uk. 89:

 “Kwa hakika Wana wa Adam wapo sawa na meno ya kitana kuanzia zama za Mtume Adam a.s. hadi leo, na wala hakuna utukufu wa Mwarabu juu ya asiye Mwarabu, wala Mwekundu juu ya Mweusi isipokuwa kwa Taqwa.”

 

46.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 2, Uk.

76:

“Kwa hakika, tendo dogo kabisa lifanywalo pamoja na Taqwa ni bora kabisa kuliko tendo kubwa (au matendo mengi) lifanywalo bila Taqwa.”


K U O M B A   D U A

 

47.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2,

Uk.493:

“Dua yoyote inayoombwa kwa Allah swt, inakuwa imezuiwa na mbingu hadi hapo iwe imeshirikishwa na Salawat i.e. kumsaliwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.pamoja na Ahlil Bayt a.s.”

 

48.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Al-Kafi J.2,

Uk.491:

“Muminiin waombao Dua zao hazikukubaliwa humu duniani watatmani kuwa dua zao hata moja zisingelikubaliwa pale watakapoonyeshwa hapo Aakhera, mema kupita kiasi ya thawabu (akipewa yeye kwa kutokujibiwa Dua zake na kwa mateso na shida alizozipata akiwa humu duniani).”

 

49.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. Bihar al- Anwar , J.93, Uk. 295:

“Tendo lipendwalo sana mbele ya Allah swt humu duniani ni Dua na ibada iliyo bora kabisa mbele Yake ni unyenyekevu na ucha-Allah swt.”

 

50.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. Al-Khisal cha Sadduq, Uk. 302:

“Milango ya Peponi ipo wazi kwa nyakati tano: wakati mvua inyeshapo;  wakati wa Vita vitukufu; wakati wito wa Sala utolewapo (wanapotoa Adhaan) ; wakati wa kusoma Qur’an Tukufu wakati ambapo jua linazama  na linachomoza alfajiri.”

 

51.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. Bihar al- Anwar , J.93, Uk. 343:

“Mujiweke tayari kuomba Dua katika nyakati tano: Wakati usomwapwo Qur’an; Wakati utolewapwo Aadhaan; Wakati unaponyesha mvua; Wakati wa kwenda kupigana katika vita vitakatifu kwa ajili ya kuwa shahidi; Wakati madhulumu anapoomba dua, kwa sababu yeye hana kizuizi cha aina yoyote chini ya  mbingu.”

 

52.    Amesema Al Imam Hussain ibn ‘Ali bin Abi Talib a.s. ,

katika Dua-i-‘Arafah:

“Ewe Mola Wangu ! Wewe U karibu kabisa wa kuombwa; Na mwepesi wa kujibu;  na Wewe Mkarimu wa kutoa;  na unamtosheleza umpaye; unamsikia vyema akuulizae; Ewe Uliye Rahmaan wa dunia na Aakhera na Mremehevu kote !”

 

53.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. , Nahjul Balagha, Msemo 135:

“Anayejaaliwa vitu vinne hanyimwi vinne: Anayejaaliwa kuomba Dua hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kufanya Tawba hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kuomba msamaha  hanyimwi kusamehewa kwake; anayejaaliwa kutoa shukuurani zake hanyimwi kuongezewa kwake.”

 

54.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Bihar al- Anwar ,

J. 78, Uk. 216:

“Siku ya Qiyama, Allah swt atazihesabu Dua zote alizokuwa akiziomba Mja wake na kuuzibadilisha katika matendo mema na kwa hayo atawapandisha daraja katika Jannat (Peponi).”

 

55.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. At- Tahdhib, J. 4,

Uk. 112:

“Ponyesheni magonjwa yenu kwa kutoa Sadaka[51] na mujiepushe na balaa za kila aina kwa Dua

 

56.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Wasail-ush-Shi’ah 

J. 7, Uk. 60:

“Mwombe Allah swt maombi yako na daima uwe ukisisitiza katika kumwomba kwani Allah swt mwenyewe anapenda mno kubakia kwa kumsisitiza miongoni mwa waja wake Muminiin.”

 

57.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Al-Kafi, J. 2, Uk.

467:

“Ninakuusieni muombe Dua’, kwa sababu hamtaweza kumkaribia Allah swt kwa vinginevyo kama hivyo.”

 

58.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. Ghurar-ul-Hikam, Uk. 185:

“Inawezekana kuwa wewe umemwomba Allah swt Dua ya kitu fulani ambacho yeye hakukujaalia kwa sababu yeye anataka kukupa kitu kilicho bora zaidi ya kile ulichokuwa umekiomba, hapo mbeleni(unatakiwa kufanya subira - mtarjum).”

 


AHLUL BAYT a.s.

 

59.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar

al- Anwar , J.27, Uk. 113:

 “Mfano wa Ahlul-Bayt yangu kwa Ummah wangu ni sawa na Safina ya Mtume Nuh a.s. Wote wale watakaoipanda ndani yake basi wameokolewa na wote wale waupingao, basi wamezama na kupotea ……….”

 

60.    Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., Imam wa

tano, Bihar al- Anwar , J. 2, Uk. 144 :

“Ahadith zetu (za Alhul Bayt) zinahuisha nyoyo.”

 

61.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar

al- Anwar , J.38, Uk. 199:

 “Muhuishe mikutano na mikusanyiko yenu kwa makumbusho ya Ali ibn Abi Talib a.s.”

 

62.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Ikmal-ud-

    Din, J. 1, Uk.253: na yenye maana yakaribiayo katika Yanabi-ul-

Muwaddah, uk. 117:

 Ipo riwaya kupitia Jabir-il-Ju’fi iliyopokelewa kutoka Jabir-ibn-Abdillah isemayo: Mimi nilisema: Ewe Mtume wa Allah swt, sisi tunamwelewa Allah swt na Mtume wake s.a.w.w. Sasa jee hawa ‘Ulul-Amr ni wakina nani ambao utiifu wao umefardhishwa sawa na wako ?

 

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alisema:

“Ewe Ja’abir ! Wao ni, baada yangu, Makhalifa wangu na Ai’mmah wa Waisilamu; wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib a.s.; atafuatia (Imam) Hassan, na (Imam) Husayn; atafuatia Ali ibn il Husayn; atafuatia Muhammad ibn Ali; ajulikanaye katika Tawrati kama Baqir, ambaye utakutana naye, Ewe Ja’abir ! Pale utakapomtembelea, umpe salaam zangu. Baada yake Musa ibn Ja’afar; atafuatia Ali ibn Musa, atafuatia Muhammad ibn Ali; atafuatia Ali ibn Muhammad, atafuatia Hassan ibn Ali; na baada yake (atakuja) Al-Qaim, ambaye jina lake ni sawa na jina langu. Yeye ndiye atakaye kuwa Mamlaka Ya Allah swt juu ya ardhi hii na Aliyebakia miongoni mwa Waja wake. Yeye ndiye mwana wa (Al-Imam) Hassan ibn Ali ( al-‘Askari). Huyu ndiye shakhsiyyah ambaye Allah swt atafungua Dhikiri zake Mashariki na Magharibi na huyu ndiye Shakhsiyyah ambaye atakuwa ghaibu kwa wafuasi na wapenzi wake ambavyo hakuna nyoyo zozote zile zinazoweza kukubali isipokuwa nyoyo za wale tu ambao Allah swt ameshakwishakuzijaribu kwa ajili ya Imani.”

 

Ja’abir alisema: “Mimi nilimwuliza ‘Ewe Mtume wa Allah swt ! Je wafuasi wake watafaidika naye wakati akiwa ghaibu ? Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alijibu: ‘Naam. Kwa kiapo cha Yule aliyenichagua kuwa Mtume, wao watafaidika kwa nuru yake na watafaidika kwa ibada akiwa ghaibu kama vile kufaidika kwa watu kutokana na (nuru ya ) jua hata pale linapofunikwa kwa mawingu…….’”

 

63.    Amesema Malik ibn Anas kuhusu mema ya Imam

As-Sadique a.s. , Bihar al- Anwar  J. 47. Uk. 28:

“Hakuna macho yaliyowahi kuona, hakuna masikio yaliyokwisha kusikia, na wala hakuna moyo uliyokwisha  shtushwa kwamba kunaweza kuwapo na mtu yeyote aliye bora zaidi kuliko (Imam) Ja’afar as- Sadique  (a.s.) katika Taqwa, elimu, ibada na Ucha-Allah swt.”

 

64.    Amesema Al Imam Hussain ibn ‘Ali bin Abi Talib a.s.,

Al-Irshaad, Uk. 204:

“Kwa roho yangu, hakuna Imam isipokuwa ni Hakimu kwa Kitabu, anaimarisha uadilifu, anaamini katika Dini ya Ukweli, na anajizuia nafsi yake pamoja na njia ya Allah swt.”

 


MAPENZI YA AHLUL-BAYT a.s.

 

65.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Al-Jami’-

ul-Saghir, J. 1 Uk. 14:

“Wafunzeni watoto wenu vitu vitatu: Mapenzi ya Mtume wenu, Mapenzi ya Ahlul-Bayt, usomaji wa Qur’an.”

 

66.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar ,

J. 74, uk. 354:

“Mtu yeyote ambaye hawezi kutufanyia wema wowote sisi Ahlul-Bayt basi wawafanyie mema wafuasi wetu walio wema; na yeyote yule asiyeweza kutuzuru, basi wanaweza kuwazuru wafuasi wetu walio wema ambavyo thawabu za kutuzuru sisi zitaandikiwa yeye.”

 

67.     Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., Al-Kafi, J.1,

Uk. 187:

“Kwa kile kilicho bora kabisa kwa mja kumkaribia  Allah swt ni utiifu kwake Allah swt, utiifu kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. na utiifu kwa ulil Amr.”

 

Aliendelea kusema:

“Mapenzi yetu (ya Ahlul-Bayt) ni Imani na chuki dhidi yetu ni kufr.”

 

68.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Bihar al- Anwar ,

J.27, Uk.91:

“Kwa hakika zipo daraja za ibada, lakini mapenzi yetu , Ahlul-Bayt, ni ibada iliyo bora kabisa.”

 


SIFA NA TABIA ZINAZOKUBALIKA

 

69.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Al-Kafi,

J.2, Uk.235:

 “Je niwatambulisheni Mu’miin ni nani? Muumin ni yule ambaye waumini wengine wanamwamini kwa nyoyo zao na mali pia. Je niwatambulisheni Mwislamu ni nani ? Mwislamu ni yule ambaye Waislamu wengine wanakuwa wamehifadhika kwa ulimi na mikono yake….. Ni haramu kwa Mumiin kumfanyia ubaya mumin mwenzake, au kumwacha katika hali ya shida, au kumsengenya au kumkataa kwa ghafla.”

 

70.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Usul-i-Kafi, J.2,

Uk. 374: 

“Haimpasi Mwislamu kuhudhuria au kushiriki katika mikutano au mikusanyiko ambapo Sharia za Allah swt zinavunjwa na kwamba yeye (huyo Mwislamu) hana uwezo wa kuyazuia hayo.”

 

71.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. Khisal  cha

Sadduq, J. 1, Uk. 88:

“Yeyote yule kwa tabia yake husema  ukweli, basi matendo yake yametakasika; Na allah swt humwongezea riziki yule aliye na nia njema; na yeyote yule awatendeaye mema familia yake, Allah swt humwongezea umri mrefu.”

 

72.   Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib

 a.s., Safinat ul-Bihaar, J.1, Uk.599:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alijiwa na mtu mmoja aliyeomba kufundishwa tendo kwayo ataweza kupendwa na Allah swt pamoja na watu, utajiri wake utaongezeka, mwili wake utakuwa na siha nzuri, umri wake utaongezeka na atainuliwa Siku ya Qiyama pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w..

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alimjibu: ‘Hizi ndizo njia sita zinazohitaji sifa sita:

Iwapo wataka Allah swt akupende, lazima umwogope na ujiepushe na madhambi,Iwapo wataka watu wakupende, lazima uwe mkarimu kwao na ukatae walichonacho mikononi mwao, Iwapo wataka Allah swt akuongezee utajiri wako, hunabudi kutoa malipo yaliyofaradhishwa kwako i.e. Zaka, Khums, na zinginezo.

 

Iwapo wataka Allah swt aupatie mwili wako afya njema, basi uwe ukitoa sadaqa kila mara iwezekanavyo, Iwapo wataka Allah swt aurefushe umri wako, basi uwe ukiwajali maJama’a zako,

 

Iwapo wataka Allah swt akuinue pamoja nami Siku ya Qiyama, basi ni lazima urefushe sujuda zako mbele ya Allah swt, aliye Pekee na Mmiliki.”

 

73.   Amesema Al-Imam Ar-Ridhaa a.s. Imam wa Nane,

‘Uyun-ul-Akhbaar ur-Ridhaa, J.1, Uk.256:

“Mumin hawezi kuwa mumin kamili hadi hapo atakapokuwa na mambo matatu: Sunna za Allah swt, Sunna za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w..  na Sunna za Imam a.s. wake. Ama Sunna za Allah swt ni kuzificha siri zake; kama vile Allah swt anavyosema katika Sura Al-Jinn, 72, Ayah 26 & 27.

 

 Yeye ndiye mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,

Usipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyumba yake.

 

 Na ama Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.ni kule kupatana na kuelewana na watu, wakati ambapo Allah swt alimtuma Mtume wake kuwapenda  watu na Amesema: ‘Uzoee usamehevu na uwafundishe mema na ujiondoe kutoka majaheli

 

Ama kuhusu Sunnah za Imam a.s. (kuwa imara na) mwenye subira katika siku nzuri na siku mbaya na nzito, ambavyo Allah swt anatuambia katika Sura Al-Baqara, 2, Ayah 177.

Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Allah  swt na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, Jama’a na mayatima na masikini na wasafiri, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.

 

74.    Amesema Al Imam Muhammad al-Taqi a.s. (al-Jawad

Imam wa Tisa),  Muntah al-‘Amal, Uk.229:

“Mumin anahitaji mambo matatu: mafanikio yatokayo kwa Allah swt, mwenye kujipa mawaidha, kukubaliwa na yule ampaye nasiha.”

 

75.   Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Imam wa Nne,

aliulizwa  “Ewe mwana wa Mtume ! Huanzaje siku  yako ?”  Na Imam a.s. alijibu, Bihar al- Anwar, J.76, Uk. 15:

“Mimi huanza siku yangu huku nikitakiwa kutimiza mambo manane (8): Allah swt ananitaka nitimize yaliyafaradhiwa juu yangu; Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. ananitaka nitimize yale yaliyo Sunna yake; Familia yangu inanitaka mimi niwatimizie mahitaji yao kama chakula n.k.; Nafsi yangu inanitaka niitimizie matamanio yangu; Shaytani aninitaka mimi nitende madhambi; Malaika wawili wanaonihifadhi wananitaka mimi nitende matendo kwa moyo halisi, Malaika wa Mauti anataka roho yangu na Kaburi inautaka mwili wangu. Basi mimi ndivyo nilivyo baina ya mzunguko wa matakwa hayo.”

 

76.    Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. , Bihar al- Anwar ,

J. 67 Uk.305:

“Kwa hakika kila kitu kinashawishiwa na Mumin kwa sababu Dini ya Allah swt inamfanya yeye awe ni mtu mwenye nguvu, na wala yeye kamwe hashawishiwi na kitu chochote kile, na kwa hakika hii ndiyo dalili ya kila Mumin.”

 


WAFUASI HALISI WA AHLUL-BAYT a.s. NA SIFA ZAO

 

77.    Al Imam Muhammad al Baqir a.s. alimwambia, Ja’bir,

Al-Kafi, j. 2, Uk. 74:

“Je inatosheleza kwa mtu kujiita Shia na mfuasi wetu ati kwa kudhihirisha mapenzi yetu, Ahlul Bayt ? Kamwe sivyo hivyo !, Kwa kiapo cha Allah swt, huyo mtu kamwe hawezi kuwa mfuasi wetu isipokuwa yule ambaye amejawa khofu ya Allah swt na kumtii ipasavyo. Ewe Ja’abir! Wafuasi wetu hawawezi kutambuliwa isipokuwa kwa sifa zifuatazo watakazokuwanazo kama unyenyekevu, kujitolea; uadilifu; kumsifu Allah kupita kiasi; kufunga saumu na kusali; kuuwatii wazazi; kuwasaidia masikini, wenye shida, wenye madeni, na mayatima wanaoishi karibu naye; kusema ukweli; kusoma Qur’an; kuuzuia ulimi kusema chochote kuhusu watu isipokuwa kwa mapenzi; na kuwa mwaminifu kwa maJama’a kwa maswala yote …….”

 

78.    Amesema Sulayman Ibn Mahran kuwa

Yeye alimtembelea Imam Ja’afer as-Sadique a.s. wakati ambapo baadhi ya wafuasi (Mashiah) walikuwa karibu naye na alimsikia Imam a.s. akiwaambia, Al-Amali, cha Saduq, Uk. 142:

“(Mujiheshimu) muwe kama vito vya thamani kwa ajili yetu na wala kamwe musiwe wenye kutuaibisha sisi. Waambieni watu kuhusu mema, na muizuie ndimi zenu zisizungumze mneno maovu na mambo yasiyo na maana.”

 

79.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2,

Uk. 56:

“Kwa hakika, sisi huwapenda wale walio na busara, wenye kuelewa, wenye elimu, wenye kufanya subira, waaminifu na wenye imani. Kwa hakika Allah swt aliwajaaliwa Mitume a.s. kwa tabia njema. Kwa hivyo yeyote yule aliye na sifa hizo basi amshukuru Allah swt, lakini yule ambaye hana hayo basi amlilie Allah swt, Aliye Mkuu na Mwenye uwezo, na amwombe hayo. “Ja’abir kwa unyenyekevu alimwuliza Imam a.s. ndiyo yapi hayo”, na Imam a.s. alimjibu: “Nayo ni: Ucha-Allah swt, kutosheka, subira, kushukuru, kuvumilia, tabia njema, furaha, hima, bidii, shauku, mkarimu, mkweli na mwaminifu katika amana.”

 

80.   Amesema Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi,

J. 2, uk.75:

“Yeyote yule anamtii Allah swt basi ni mpenzi wetu, na yeyote yule asiyemtii Allah swt basi ni adui wetu (sisi Ahlul-Bayt)…..”

 


MADHAMBI NA ATHARI ZAKE

 

81.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar

    al- Anwar, J. 77, Uk. 79 na Mustadrak Al-Wasail, J.11, Uk. 330:

 “Msitazame udogo wa dhambi, lakini muangalie mliyemuasi (Allah swt).”

 

82.    Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn

Abi Talib a.s. Bihar al- Anwar, J. 70, Uk.18:

“Iwapo mtu anapenda kujiona vile alivyo mbele ya Allah swt, basi ajitathmini kwa madhambi na maasi yake mbele ya Allah swt; basi kwa kipimo hicho ndivyo alivyo huyo mtu mbele ya Allah swt.”

 

83.    Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. aliwauliza watu ni kwa nini

wanamwudhi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Basi mmoja wa watu alimwuliza Imam a.s. vipi, naye Imam a.s. aliwaambia, Usul-i-Kafi , J.1, Uk. 219 :

“Je hamujui kuwa matendo yenu yapoyanajulishwa kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na pale aanapoona madhambi dhidi ya Allah swt miongoni mwao, basi husikitishwa mno. Kwa hivyo musimuudhi Mtume wa Allah swt na badala yake munatakiwa kumfurahisha (kwa kutenda mema).”

 

84.    Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Ghurur al-

Hikam, Uk. 235:

“Kukosa kusamehe ni kasoro moja kubwa kabisa na kuwa mwepesi katika kulipiza kisasi ni miongoni mwa madhambi makubwa kabisa.”

 

85.   Kutokea Asbaghi bin Nabatah kutokea kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Al-Khisal,cha as-Sadduq, J. 2, Uk. 360:

“Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. kuwa Allah swt anapoikasirikia Ummah na kama hakuiadhibu basi bei za vitu vitapanda juu sana yaani maisha yatakuwa ghali, maisha yao yatakuwa mafupi, biashara zao hazitaingiza  faida, mazao yao hayatukuwa mengi, mito yao haitakuwa imejaa maji, watanyimwa mvua (itapungua), na watatawaliwa na waovu miongoni mwao.”

 

(Yaani Hadith hiyo juu inatubainishia kuwa iwapo kutakuwa na jumuiya ambayo imejitumbukiza katika madhambi basi wanabashiriwa kupatwa na mambo saba hayo yaliyotajwa.)

 

86.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema kuwa amekuta

katika kitabu cha Al-Amir al-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. akisema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.Amesema, Safinat –ul-Bihar, J. 2, Uk.630:

“Wakati zinaa  itakapokithiri katika jumuiya basi idadi za mauti za ghafla zitakithiri; na patakapokuwa na uovu basi Allah swt atawatumbukiza katika maisha ya ghali na hasara. Wakati watu watakapoacha kulipa zaka , basi ardhi itazinyakua baraka zake kutokea mazao, matunda, madini na vitu vyote kama hivyo. Wakati watakapotenda bila haki kwa mujibu wa Shariah, basi itakuwa sawa na kumsaidia dhalimu na ugaidi. Na watakapozikiuka ahadi zao, basi Allah swt atawafanya maadui wao kuwasaliti na kuwakandamiza. Wakati watakapoacha uhusiano pamoja na ndugu na Jama’a zao, basi yote yale wayamilikiayo yatakwenda mikononi mwa waovu. Na wakati watakapojiepusha na kutoa nasiha ya mambo mema na kuyakataza maovu na kama hawatawafuata waliochaguliwa Ahl-ul-Bayt a.s., basi Allah swt atawasalitisha kwa walio wenye shari miongoni mwao na katika hali hii, wataomba duaa lakini hazitakubalika.”

 

87.    Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al- Anwar

, J .70, Uk. 55:

“Machozi hayaishi illa kwa nyoyo kuwa ngumu, na nyoyo haziwi ngumu illa kukithiri kwa madhambi.”

 

88.    Allah swt alimwambia Mtume Dawud a.s.: Ithna-

Ashariyyah, Uk. 59:

“Ewe Dawud ! Wabashirie habari njema wale watendao madhambi kuhusu msamaha wangu, ambayo inajumuisha kila kitu kilichopo humu duniani, ili wasikate tamaa ya msamaha wangu; na waonye wale watendao mema kwa adhabu zangu ili wasije wakajifanyia ufakhari kwa utii wao, kwani ufakhari ni dhambi mbaya kabisa.”

 


ELIMU NA THAMANI YAKE

 

89.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar

al- Anwar , J. 2, Uk. 25:

“Waalimu pamoja na wanafunzi wanashirikiana katika kuulipwa mema wakati watu wengine hawabahatiki..”

 

90.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar

al- Anwar , J. 2, Uk. 121:

“Yeyote yule aienezaye Din kwa watu bila ya yeye mwenyewe kuwa na ilimu ya kutosha, basi anaidhuru Din zaidi kuliko vile anavyoitumikia.”

 

91.   Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. , Nahjul Balagha,

semi No. 482:

“Thamani ya kila kitu ni katika ubora wake.”

 

Yaani thamani ya mtu ni katika ilimu yake. Cheo na utukuzo wake utakuwa katika kiwango cha ilimu aliyonayo. Macho yetu hayaangali sura, urefu ukubwa wa mwili wa mtu bali humthamini kwa kufuatana na kiwango cha ilimu aliyonayo. Hivyo inatubidi sisi sote tujitahidi katika kutafuta na kuipata ilimu kwa kiasi tuwezacho.

 

92.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika

Bihar al- Anwar, J. 2, Uk.36:

“Elimu ni amana ya Allah swt juu ya ardhi hii na wanazuoni ndio wenye amana hii. Hivyo yeyote yule atebdaye kwa mujibu wa ilimu yake, basi kwa hakika ameiwakilisha amana vile ipasavyo …”

 

93.    Al-Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:, Bihar al- Anwar ,

J. 78, uk. 189:

“Jitafutieni ilimu kwa sababu kujifunza ni matendo mema na kusoma kwenyewe ni ‘ibada.”

 

94.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema:, Bihar al- Anwar

, J. 1, Uk. 179:

“Mtu ambaye anatafuta ilimu, ni sawa na mpiganaji vita katika njia ya Allah swt.”

 

95.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika Bihar al-

Anwar , J. 2, Uk. 92:

“Uichunge sana ilimu yako na utazame ni kwa nani unaitoa.”

 

96.     Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Al-Kafi,

J.1, Uk.36:

“Muitafute ilimu na kuipamba kwa subira na ukuu ; na uwe mnyenyekevu kwa yule ambaye anaitafuta ilimu kutoka kwako”

 

97.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Al-Kafi,

J. 1, Uk. 35:

“Yeyote yule ajifunzae ilimu na kutenda vilivyo, na kuifundisha kwa ajili ya Allah swt, basi Malaika watatmukuza mbinguni .”

 

98.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwar , J.1, Uk. 204:

“Wema wa duniani humu pamoja na Aakhera ni pamoja na ilimu.”


ILIMU NA FADHILA ZA KUJIFUNZA

 

99.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika, 

Bihar al- Anwar , J. 1, Uk. 184:

 “Yeyote yule atafutaye ilimu ni sawa na mtu anayefunga saumu mchana na akikesha macho usiku kucha akifanya ibada. Iwapo atajifunza ilimu kwa sehemu fulani, basi itakuwa kwake ni afadhali kabisa hata kuliko kuwa na dhahabu ya ukubwa wa mlima Abu Qubais na ambayo itagawiwa sadaqa katika njia ya Allah swt.”

 

100.   Al-Imam Zaynul ‘Aabediin a.s. Amesema katika, Usul-i

-Kafi, J. 1, Uk. 35:

“Iwapo watu wangalikuwa wakitambua kile kilichopo ndani ya kutafuta ilimu, basi wao wangaliitafuta hata kama itawabidi kusafiri na hata kuhatarisha maisha yao katika kuipata.”

 

101.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Qurar-ul-Hikam,

Uk. 348:

“Kutafuta ilimu haitawezakana wakati mwili unastareheshwa.” (yaani mtu hataki kutaabika)

 

102.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Bihar al-

Anwar, J. 2, Uk.152:

“Hifadhini maandiko  na vitabu vyenu kwa sababu hautapita muda mutakapovihitaji.”

 

103.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika, Al-Kafi,

J. 1, Uk. 30:

“Kwa hakika, kukamilika kwa Din ni kule kuitafuta ilimu na kuitekeleza ipasavyo, na muelewe waziwazi kuwa kutafuta ilimu ni faradhi zaidi kwenu nyinyi kuliko kutafuta mali na utajiri.”

 

104.  Amesema al-Imam al-Hassan ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika, Bihar al- Anwar, J. 78, Uk. 111:

“Wafundisheni watu wengine ilimu muliyonayo na mujaribu kujifunza ilimu waliyonayo wengineo.”

 

105.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

 Bihar al- Anwar , J. 1, Uk.167:

 “Fadhila za ilimu zinapendwa zaidi na Allah swt hata kuliko fadhila za ibada.”

 

 


ILIMU NA FADHILA ZA  KUIFUNDISHA

 

106.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Ithna-Ahariyyah, Uk. 11:

 “Mtu yeyote aliyekuwa na ilimu kuhusu swala fulani na akaificha pale atkapoulizwa basi Allah swt  atamkasirikia kwa ghadhabu za moto.”

(yaani mtu anapokuwa na habari ambazo zitamsaidia mtu aliyepatwa na shida na ikaweza kumsaidia kuimarisha hali yake, badala ya kumsaidia yeye akaificha, basi hapo kwa hakika ametenda dhambi kubwa.)

 

107.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

 Bihar al- Anwar, J. 92, Uk. 19:

 “Qur’an Tukufu ni chuo kikuu ; hivyo jielimisheni kiasi muwezavyo kutokea chuo hiki.”

 

108.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Sunnahn-i-ibn-Majah, J. 1, Uk.88:

“Kwa hakika, kile kitakachoendelea kumfikia mtu hata baada ya kufa kwake, miongoni mwa matendo yake mema ni : ilimu ambayo yeye amewafundisha na kuieneza  kwa wengineo, mtoto mwema aliyemwacha, kuacha Qur’an Tukufu ikapatikana.”

 

109.   Amesema al-Imam Ali ar-Ridha a.s. katika,  Ma’anil

Akhbaar, Uk. 180  na ‘Uyun-il-Akhbaar –ir- Ridha, J. 1, Uk. 207:

“Rehema za Allah swt ziwe juu ya yule ambaye anazihuisha amri zetu.”

Na halikuwapo mtu akamwuliza Imam a.s. ni vipi wanaweza kuhuisha amri zao, na Imam a.s. alimjibu:

“Anaweza akijifunza ilimu zetu na akawafundisha watu. Kwa hakika, iwapo watu wangelikuwa wamezijua faida na mema ya semi zetu, basi kwa hakika wangalitufuata sisi.”

 


ELIMU – HEKIMA – MA’ARIFA.

 

110.  Elimu ni fidia kwa juhudi za akili.

111.  Wema ni sababu kuu ya elimu.

112.  Kumwogopa Allah swt ni matokeo ya elimu.

113.  Jumla ya utukufu wote, ni elimu au ma’arifa.

114.  Yeyote afundishaye herusi moja, amenifunganisha nae

        minyororo.

115.  Elimu iliyo bora ni ile inayomfaa mwenye kuwa nayo.

116.  Elimu ni hazina na maisha.

117.  Unyenyekevu ni matokeo ya elimu na ma’arifa.

118.  Mtu mwenye elimu yu hai hata kama amekufa.

119.  Dini ni ghala na elimu ni mwongozo wa kuifikia ghala.

120.  Ili kupata ufanisi itikia elimu na kupuuzia ujahiliya.

121. Wengi wanaelezea ma’arifa, lakini ni wachache waiingizayo akilini mwao.

122. Bakhshishi iliyo kamili ya Allah swt ni ile maisha iliyotegemea elimu na hekima.

123.  Wapumbavu wengi mno wanawafanya wasomi kuwa wachache.

124. Aliyeelimika anamwelewa vyema mjinga kwani yeye binafsi alikuwa mjinga awali.

125. Na mtu aliye jahili hataweza kumwelewa mtu aliyeelimika kwani hajaelimika mwenyewe.

126.  Wana elimu wanaishi katika kiwiliwili kilichokufa cha ujahili.

127.  Ma’arifa huuwa ujahili.

128.  Elimu ndiyo iipatiayo maisha Roho.

129.  Ma’arifa chache (ya Allah swt) huharibu mwenendo wa mtu.

130.  Hakuna chochote kile pasi na nuru  ya kweli tu itakayokutakasisha.

131.  Kuwaheshimu waliosoma ni kumheshimu Allah swt.

132.  Ma’arifa ni chanzo cha khofu ya Allah swt    (--inaletwa na )

133. Kile kikomazacho ma’arifa ni matendo kwa kutumia hekima na ma’arifa hayo.

134.  Kufundisha ndiko kujifunza.

 

 


UMUHIMU WA MAARIFA

 

135.    Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alielekea Msikitini na huko akakuta makundi mawili ya Waislamu. Kikundi cha kwanza kilikuwa kikijifunza ilimu ya Dini, na kikundi cha pili kilikuwa kinafanya ‘ibada.

 

Kwa kuona hayo Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. :

“Vikundi vyote viko katika kheri, ama hawa wanamwomba Allah swt  na hawa wanajifundisha na kuwafundisha wengine wasio na ilimu, kwa hakika hawa ndio bora, nimetumwa kwa watu ili kuwafundisha.”

 

Kisha akakaa pamoja nao.

 

136.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Ewe Kumail ! Hakuna harakati zozote utakazozifanya, ila unahitaji kuwa na maarifa.”

 

137.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Kukosa macho ni jambo jepesi kuliko kukosa mwanga (maarifa)”.

 

138.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

”Usizungumzie usilolifahamu”.

 

139.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Elimu ni msingi wa kila heri”.

 

140.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. :

“ Katika hadith inayotokana na mababa zake, toka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambae ameipokea toka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

 “Watu wengine walio na thamani (qimmah) kwa watu ni wale walio na elimu nyingi kati yao, na wale wenye thamani duni kati yao ni wale wachache wao wa elimu”.

 

 

KUTAFUTA ELIMU.

 

141.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. :

“Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa kila Mwislamu Mwanamme na Mwislamu Mwanamke”

 

142.  Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. :

“ Kujitolea nafsi yake mtu kwa ajili ya kutafuta elimu, mfano wake ni kama anaepigana vita kwa ajili ya Allah  swt.”

 

143.    Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

“Watu ni aina mbili; Aalimu (mwenye elimu) na mwenye kujifundisha, ama watu wengine ni upumbavu na wapumbavu mahala pao ni motoni”.

 

144.  Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. :

“Kuwa mwenye elimu au mwenye kujifundisha elimu, jiepushe kuwa mwenye kupumbazika na kuona ladha ( ya kutojihangaisha kutafuta elimu.)

 

145.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

“ Sikupenda kumwona kijana, kijana kati yenu ila amekuwa kati ya moja ya hali mbili;

Ima awe mwenye elimu au

mwenye kutafuta elimu, na kama hakufanya hivyo basi amepoteza nafasi yake, na aliye poteza nafsi yake amefanya dhambi na anayefanya dhambi ndio amekaa motoni.”

 

 

AKILI.

 

146.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema

“ Hakika heri yote hupatikana kwa akili”.

 

147.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Akili ni jahazi ya elimu.”

 

148.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“ Hakugawa Allah swt kwa waja wake kitu kilicho bora kuliko akili, usingizi wa mwenye akili ni bora kuliko kukesha kwa mtu mjinga, kufuturu (kutofunga) kwa mtu mwenye akili ni bora kuliko Saumu ya mtu mjinga, na kutosafiri kwa mtu mwenye akili ni bora kuliko safari ya mtu mjinga”.

 

149.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  

“ Ubinadamu wa mtu hutokana na akili yake.”

 

150.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.:Kumwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. :

“Ewe Mwanangu! Hakika ya utajiri ni utajiri wa akili na ufakiri mkubwa ni kuwa mtu mpumbavu.”

 

151.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Akili ndio mjumbe wa haki.”

 

152.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Rafiki wa kila mtu ni akili yake, na adui ni ujinga wake”.

 

153.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“ Mwenye kutekeleza (vitendo) kutokana na kile anachojua, Allah swt humrithisha (humjalia) elimu ambayo haijui.”

 

154.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Akili ni kitu cha maumbile,  huzidi kwa elimu na majaribio.”

 

155.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Asiejaribu mambo hudanganyika.”

 

156.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Na majaribio ya muda mrefu ni nyongeza ya akili.”

 

157.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema :

“ Ewe Hisham! Hakika kwa Allah  swt juu ya watu kuna dalili (burhani) mbili: Dalili ya wazi, na dalili ya ndani. Na ama ile ya wazi ni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Manabii na Maimamu a.s. na ama ya ndani ni akili.”

 

158.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema

“Mwenye kuwa nayo akili, amekuwa na  dini.”

 

159.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“ Mwenye kuijua nafsi yake, hakika amemjua Allah swt.”

 

160.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Huzijua mtu aibu za nafsi yake, ni maarifa yenye kunufaisha zaidi.”

 

161.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Na akili ni ngao (ngome) ya majaribu.”

 

162.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema

“ Na kila ujuzi unahitaji majaribio.”

 

163.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Kutafuta elimu ni bora kuliko kufanya ibada. Amesema Allah swt,

Hakika wanaomwogopa Allah swt miongoni mwa waja wake ni wanachuoni.

 

164.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  

“ Hakuna zaka iliyo bora katika elimu kuliko kuifanyia kazi.”

 

165.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“ Mweney kuwa na yakini (uhakika wa Jambo) hufanya amali (kazi) hali ya kuwa yeye ni mwenye kupigania Jihadi.”

 

166.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Lau (mtihani wa Allah  swt) husubiri, na asiyefahamu hakanushi.”

 

167.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Hasubiri mtu yeyote katika uchungu wa haki ila yule anae kuwa na yakini (uhakika) wa matokeo yake.”

 

168.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema  :

“ Hakuna kitu chochote kile ila kina upeo wake,”

akaulizwa” Ni nini upeo wa Yaqini (kuwa na uhakika)?. Akasema “Usiogope kitu chochote.”

 

169.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“ Kutoa majabali kutoka mahali pake ni rahisi kuliko kuutoa moyo kutoka katika chochote.”

 

170.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Haisafiki kazi mpaka isihi (iwe sahihi) elimu.”

 

171.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“ Mwanachuoni katika zama zake, hayamhujumu matatizo.”

 

172.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Aliye kamilika kiakili hayawi mazito kwake matatizo.”

 

173.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“Akili iliyokamilika, ndiyo yenye kuvunja mabaya.”

 

174.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Lengo la elimu ni kufanya kazi vizuri”.

 

MAELEZO 1.

 

Katika nadharia za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Mawasii wake, elimu ni kitu bora kuliko kitu kingine chochote kile, kiasi kwamba jambo hili limeweza kuwastajaabisha watu wengi kutokana na hadithi nyingi zilizo pokewa zinazo sifa ubora wa elimu, hadithi kadhaa zimesikiwa toka kwenye ulimi wake Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Maimamu a.s.  Lakini je! Mshangao huo utabaki mpaka lini? Mshangao mbele ya uhakika wa mambo yalivyo hausaidii kitu. Je hatuamini kwamba maendeleo ya Dunia na Akhera hupatikana kwa elimu?. Jibu liko wazi kwamba kwa elimu hupatikana na maendeleo. Kwahiyo tunajionea wazi kuwa thamani ya elimu iko juu sana.

 

 

MAELEZO 2.

 

Mwanadamu hutokea akajifunza elimu, lakini elimu yake ikawa ni upuuzi mtupu na balaa kwa watu, kutokana na kule kuvuka mpaka kwake na kuitumia elimu yake isivyo ndivyo na kinyume cha mtu mwenye akili, matokeo ya mtu wa ina hii ni kugundua mambo ambayo hayana faida yoyote kwa wengine, elimu kama hii humpoteza yeye mwenyewe na ummah pia katika dunia na akhera, hatimaye mtu huyu hugunduwa utengenezaji wa pombe na mabomu.

 

 

175.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“ Inamtosha mtu kuwa mjinga kwa kutokuzijua aibu zake.”

 

176.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“Enyi watu! Hakuna heri katika dini isiyo na mafunzo ndani yake.”

 

177.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Mfanya ibada bila ya mafunzo ni kama punda mwenye kuzunguka, anazunguka na wala hachoki.’’

 

178.  Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema  :

“Mwenye kueneza elimu basi anao ujira mfano wa mwenye kutekeleza kwa hiyo (kutokana na elimu hiyo).”

 

179.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“ Upingeni ujinga kwa elimu.”

 

180.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema  :

“Katika kuwasifu waja wa Allah swt: Nawakasimamisha masikio yao (kwakusikiliza ) elimu yenye manufaa kwao.”

 

 

181.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema:

“ Nimekuta elimu ya watu iko katika mambo manne:

Kwanza kati ya hayo manne ni kumjua Mola wako,

Pili kujuwa alicho kiumba,

Tatu kujuwa anacho taka kwako,

Nne kujuwa chenye kukutoa katika dini yako.”

 

182.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema  :

“Lau ningeijiwa na kijana miongoni mwa vijana wa ki-Shi’a hajifunzi (elimu ya dini) ninge mtia adabu.”

 

183.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema  :

“ Rafiki wa kila mtu ni akili yake na adui wake ni ule ujinga wake.”

 

184.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Mwenye akili ni kufikiri ataona (kuona muongozo)

 

185.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s.  amesema:

“ Kila kitu kina dalili, dalili ya mwenye akili ni kufikiri na dalili ya kufikiri ni kunyamaza.”

 

186.  Mtume Mtukufu Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Kufikiri kwa muda wa saa moja ni bora kuliko ibada ya mwaka.”

 

187.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“ Kufikiri ni kioo kilicho safi.”

 

188.  Al Imam Hassan al-'Askari a.s.  amesema:

“Haikuwa ibada kwa uwingi wa kufunga na kusali, hakika ya ibada ni kufikiri (na kuzingatia) kuhusu Allah swt.”

 

189. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  amesema:

“Elimu ndio kichwa cha kila heri na ujinga ndio kichwa cha kila shari.”

 

190. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema  :

“ Ujinga ni Umauti.”

 

 

 

 


UJAHILI:

 

191.    Hakuna maumivu ya kupita zaidi ya ujahili.

192.  Watu ni adui kwa kile walichobakianacho jahili.

193.  Fadhila za jahili ni sawa na bustani juu ya chungu cha kinyesi.

194.  Wasi-wasi ni matokeo ya ujinga.

195. Nia kuu ya busara ni kule mtu kukubali na kukiri ujinga wake (iwapo anao).

196. Ni mtu mpumbavu kabisa iwapo atapuuzia umuhimu wake (atajidharau, kujidhalilisha)

197.  Mjinga ni mwenye hasara hata kama akiwa katika hali gani ile.

198.  Ujinga uliodhalilishwa (wa ujinga) ni kule kumtii mwanamke.

 


UTUKUFU NA UMUHIMU WA WANAZUONI

 

199.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika, 

    Bihar al- Anwar , J. 2, Uk. 49:

 “Yapo makundi mawili ya Ummah wangu kwamba wanapokuwa wachaAllah swt, Ummah wangu utakuwa sahihi na wakati watakapokuwa wameingiliwa na ufisadi, basi Ummah wangu utageuka kuwa waovu.”

 

 Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliulizwa kuhusu waliokuwa wakimaanishwa. Alijibu :   “Wanazuoni wa Din na watawala.”

 

200.  Amesema Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika, Bihar

al- Anwar , J. 1, Uk. 222:

“Utakapokuwa umekutana na Mwanazuoni basi uwe mwenye kutaka kujua mengi kuliko kujifanya msemaji zaidi, na ujifunze namna ya kusikiliza na namna ya kuzungumza vyema, na wala usimkatize kauli yake yoyote atakayokuwa akizungumza.”

 

201.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Ithna-

Ashariyyah, Uk. 245:

“Ewe ‘Ali ibn Abi Talib  ! Malaika Jibraili alitaka alitamani kuwa mwanadamu kwa sababu saba zifuatazo:

1.  Sala za Jama’a

2.  Uhusiano pamoja na wanazuoni

3.  Kudumisha amani miongoni mwa watu wawili

4.  Kuwahurumia na kuwahishimu mayatima

5.  Kuwatembelea na kuwajua hali wagonjwa,

6.  Kuhudhuria na kushiriki katika mazishi

7.      Kuwagawia maji mahujjaji

Kwa hivyo nyinyi pia muwe watu wa kuzipenda na kuvitekeleza vitu hivyo.”

 

202.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika, Nahjul

Balagha, Semi No. 265:

“Iwapo matamshi ya watu wenye busara yatakuwa katika malengo yao, basi huwa kama matibabu, lakini yanapokuwa siyo sahihi basi ni sawa na ugonjwa.”

 

203.  Amesema al-Imam Hassan al ‘Askari a.s. katika, Al-

Ihtijaj, J. 2, Uk. 155:

“Maulamaa wa Kishia’h ni walinzi wa mishikamano ya Islam.  Kwa hivyo, yeyote yule katika wafuasi wetu anayechukua jukumu hili basi ni bora kuliko kupigana vita dhidi ya Waroma (kwa sababu huyu analinda mishikamano ya imani zetu).

 

204.  Amesema al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. katika, Bihar al-

Anwar , J. 2, Uk. 5:

“Jihadharini kuwa hakimu wa kidini wa kweli ambaye anapatia watu mema na huruma, na kuwahifadhi dhidi ya maadui wao, kuwazidishia neema za Peponi  na kuwapatia ridhaa za Allah swt kwa ajili yao (kwa kupitia hidaya).”

 

 

205.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Bihar al-

Anwar , J.2, Uk. 43:

“ ….  Malipo kwa Mwanazuoni ni zaidi kuliko malipo ya mtu afungaye saumu nyakati za mchana na kusali nyakati za usiku na akipigana vita vya jihadi kwa ajili ya Allah swt. Na, wakati mwanazuoni anapokufa, basi kutatokezea pengo katika Islam ambalo haliwezi kuzibwa illa kwa aina yake tu.”

 

206.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Nahjul

Balagha,semi No. 147:

“Ewe Kumayil ! Wale wanaojilimbikizia utajiri na mali ni watu waliokwisha kufa hata kama watakuwa bado hai, wakati maulamaa (wanazuoni) wenye elimu watabakia hadi hapo dunia itakapokuwa ikibakia. Hata kama watakuwa lakini mafunzo na mifano yao itabakia mioyoni mwa watu.”

 

 

207.  Amesema al-Imam Husayn a.s. katika, Tuhaful ‘Uqul,

Uk. 172:

“ ….. Kwa hakika, njia ya masuala ya Waislamu na hukumu za Shariah zipo katika mikono ya Wanazuoni wakiAllah swt ambao ndio wenye amana za Allah swt katika mambo ayatakayo na yale asiyoyataka …”

 


KUWA MAKINI KUHUSU AKHERA

 

208.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwar, J. 1, Uk. 203,

“Wafuasi wa Mtume Isa a.s. walimwuliza ni watu gani wawafanye marafiki wao, naye a.s. aliwajibu: “Pamoja na wale ambao wanapokuwa nanyi humkumbusha Allah swt, mazungumzo yao hukuzidishieni ilimu na matendo yao huwavutieni ninyi kutenda matendo mema kwa ajili ya Aakhera.”

 

209.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Qurar-ul-

Hikam, Uk. 335:

“Kusiwepo na shughuli ya aina yoyote ile ambayo itakuzuia kutenda matendo kwa ajili ya Aakhira, kwa hivyo, muda wa kufanya hivyo upo mdogo sana.”

 

210.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Qurar-ul-

Hikam, Uk. 274:

“Yeyote yule atakayeiuza Aakhera yake kwa maisha ya humu duniani, basi kwa hakika amepoteza yote kwa pamoja.”

 

211.  Al-Imam ‘Ali ibn Muhammad al-Hadi a.s. Amesema

katika, Bihar al- Anwar, J. 78, Uk. 370:

“Kumbuka pale utakapokuwa kitandani ambapo mauti imekukalia kichwani na huku umezungukwa na ndugu na maJama’a zako, na hapo hakuna mganga anayeweza kukuepusha na kifo hicho wala hakuna rafiki anayeweza kukusaidia.”

 


JANNAT.

 

212.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema,

Kila mtu katika Jannat atahudumiwa kwa vitu vizuri vya Jannat kiasi kwamba hata atakapopata wageni kwa malaki na malaki lakini hakutapungua chochote… neema nyingi tele…”

 

213.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu :

“Allah swt ni mwadilifu. Iwapo matendo mema ya mwanamme yatakuwa zaidi ya mwanamke, basi mwanamme atapewa fursa kwanza kufanya chaguo na uamuzi iwapo anapendelea kuishi na mke wake au hapana. Na vivyo hivyo iwapo matendo mema ya mwanamke yatakuwa zaidi basi naye atapewa chaguo kama hili yaani iwapo atapenda kuishi na mume wake au hapana. Iwapo mwanamke huyo hatamchagua bwanake awe mume wake hapo Jannat, basi huyo mwanamme aliyekuwa mume wake humu duniani hatakuwa mume wake huko Jannat .”

 

214. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema kuwa Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu Sura-i-Yasin,36, Ayah ya 78

‘Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake – akasema: “Nani atakaihuisha mifupa na hali imesagika ?”

215.  Katika Milango yote 8 ya Jannat kumeandikwa :

Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi,

 

216.  Mlango wa kwanza

Katika mlango wa kwanza wa Jannat kumeandikwa :

Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia riziki ni nnne :

    • kutosheka,
    • kutumia katika njia sahihi,
    • kukana kisasi na
    • kufanya uhusiano pamoja na watu waliookoka yaani katika njia nyoofu.

 

217.  Mlango wa pili

Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia furaha katika maisha ya Aakhera ni nne :

·         Kuonyesha huruma kwa mayatima,

·         kuwawia wema wajane,

·         kuwasaidia wacha-mungu katika kufanikisha malengo yao na

·         kuwaangalia na na kuwasaidia masikini na wasiojiweza.

 

218.  Mlango wa tatu

Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia siha njema katika maisha haya mafupi ni nne :

·         Kuongea kwa uchache,

·         kulala kidogo,

·         kutembea kidogo na

·         kula kidogo.

 

219.  Mlango wa nne

·         Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wageni wake;

·         Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa jirani zake;

·         Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wazazi wake;

·         Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe ni mwenye kusema mema au anyamaze kimya.

 

220.  Mlango wa tano

  • Yeyote yule ambaye hataki kunyanyaswa siku ya Qiyamah, basi naye asimnyanyase mtu yeyote;
  • Yeyote yule ambaye hataki kusengenywa siku ya Qiyamah, basi naye asimsengenye mtu yeyote;
  • Yeyote yule ambaye hataki kudhalilishwa siku ya Qiyamah, basi naye asimdhalilishe mtu yeyote;
  • Mtu yeyote yule ambaye anataka kujishikiza kwa umadhubuti katika maisha haya mafupi na yale ya Aakhera, basi lazima atoe shahada kuwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mja  (Walii) Wake halisi.

 

221.  Mlango wa sita

  • Yeyote yule anayetaka kaburi lake liwe pana na lenye nafasi ya kutosha (kutombana) basi ajenge Misikiti;

 

  • Yeyote yule anayetaka asiliwe na wadudu au minyoo ya ardhini, aifanye Misikiti iwe nyumba yake ( yaani awe akiizuru kwa mara nyingi kama kwamba anaishi humo );

 

  • Yeyote yule anayetaka kubakia freshi, (yaani asipate shida na taabu za kiu katika maisha haya na yale ya Aakhera ambapo kila mtu atakuwa akitafuta hata tone moja la maji ) basi awe akifagia Misikiti;

 

  • Na yeyote yule ambaye anataka kuiona nafasi yake hapo Jannat basi atengeneze sakafu na kuweka mazulia au mikeka katika Misikiti.

 

222.  Mlango wa saba

·         Moyo halisi unapatikana kwa mema manne:

·         Kuwatembelea wagonjwa,

·         kutembea nyuma ya jeneza,

·         kununua sanda kwa ajili ya maiti na

·         kulipa madeni.

 

223.  Mlango wa nane

·         Yeyote yule anayetaka kuingia katika milango hii basi lazima awe na sifa nne zifuatazo :

·         Ukarimu,

·         adabu njema,

·         moyo wa kujitolea na

·         kujiepusha katika kuwadhuru waja wa mungu.

 

224. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. ananakiliwa riwaya na Muhammad ibn Qays katika ukurasa wa 115 wa kitabu

         Al-Mahasin:

 

“Siku moja Shaitani alimwona Mtume Nuh a.s. akisali, basi Shaitani alimwonea wivu Mtume Nuh a.s. na hakuweza kujizuia, akasema. “Ewe Nuh ! Allah swt aliyetukuka, Mkuu, amejenga mwenyewe Bustani ya Eden , akapanda miti na kutiririsha mito ndani mwake. Na kisha akaangalia mandhari hayo na kusema, “Kwa hakika waumini na waongofu ndio washindi ! La, Kwa Utukufu wangu ! Mtu mwenye utovu wa adabu (mwenye madhambi) kamwe hataingia kuishi humu.’”

 

225.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema,

“Mitume yote imekatazwa kuingia Jannat kabla yangu, na mataifa yote yamekatazwa kuingia humo kabla ya waumini watufuatao sisi, sisi Ahlul Bayt a.s., kuingia ndani mwake.”

 

226.  Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amenakiliwa akisema, uk.139, J.8

ya Bihar al-Anwar, akisema, 

“Jannat  inayo milango sabini na moja ya kuingilia : Ahlul Bayt a.s. yangu na wafuasi wao wataingilia milango sabini, wakati ambapo watu wengine wataingilia mlango uliobakia.”

 

Taqwa

 

227.  Qur’ani Tukufu , Sura  al-Maryam ,19 , Ayah 63 :

Hiyo ndiyo Jannat tutayowarithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu.

 

228.  Vile vile twaambiwa katika Qur’ani Tukufu , Sura  al-Hujurat ,

49, Ayah 13 :

Enyi watu ! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa na mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa  Allah swt ni  huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi….

 

229.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Maidah,

5, Ayah 85 :

Basi Allah swt atawalipa, kwa yale waliyoyasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema.

 

230.  Allah swt anasema katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Tawbah,

9, Ayah 111:

Hakika Allah swt amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Jannat. Wanapigana katika Njia ya Allah swt – wanauwa na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na  Qur'an. Na nani atimizae ahadi kuliko Allah swt ? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

231.  Allah swt anasema katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Naziat,79,

 Ayah 40 – 41 :

Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt Mlezi, na akijizuilia nafsi yake na matamanio,

Basi huyo, Jannat itakuwa ndiyo makaazi yake !

 

232. Allah swt atuambia katika Qur’ani Tukufu, Surah

al-Waqia,56,Ayah 10–13 :

Na wa mbele watakuwa mbele. 

Hao ndio watakao karibishwa

Katika Bustani zenye neema.

 

233.  Qur’ani Tukufu , Sura al-Dahar, 76, Ayah 12 :

Na atawajaza Bustani za Jannat na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.

 

234. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Ra’d, 13,

Ayah 24 :

Hao ndio watu wa Jannat, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.(Wakiwaambia) Assalamu ‘Alaikum ! amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno  malipo ya Nyumba ya Akhera.

 

235.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4,

 Ayah 13 :

Na anayemtii Allah swt na Mtume wake, Yeye atamtia katika Jannat zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

236.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Safaat,

37, Ayah 39 – 43 :

Wala hamlipwi ila hayo hayo mliyokuwa mkiyafanya.

Isipokuwa waja wa Allah swt  walio khitariwa.

Hao ndio watakaopata riziki maalumu,

Matunda, nao watahishimiwa.

 

237.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Maidah,

5, Ayah 119 :

Allah swt atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Allah swt amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa.

 

238.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ta-Ha, 20,

 Ayah 75– 76 :

Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu.

Bustani za milele zipitazo mito kati yake,wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.

 

239.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura Ali Imran,

 3,   Ayah 133-136 :

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Jannat ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyowekwa tayari kwa wachamungu,

Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allah swt huwapenda wafanyao wema;

Na ambao pindiwafanyapo uchafu au wakijidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah swt na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao – na nani anayefuta dhambi isipokuwa Allah swt ? – na wala hawapendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.

Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.

 

240.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Rahman,

55,  Ayah 46 :

Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt atapata Jannat (Bustani) mbili

 

241.  Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s. amesema katika Majma’ul Bayan :

“Mtu yeyote ambaye anajua na kutambua wazi kuwa mimi nifanyapo jema au baya, basi Allah swt yupo anashuhudia matendo yangu haya, basi mtu kama huyu daima atakachokuwa akikifanya basi atakuwa mwangalifu mno katika matendo yake na atajiambia kuwa lau nitafanya kazi hii njema basi Allah swt atalipa mema kadha na kadha na lau nitafanya maasi na madhambi, basi Allah swt ataniandikia adhabu kadha wa kadha. Kwa hivyo watu kama hawa wamewekewa Bustani mbili katika Jannat.”

 

242.  Qur’ani Tukufu , Sura al-Mujadilah, 58, Ayah 21 :

Allah swt ameandika : Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Allah swt ni Mwenye nguvu, mwenye kushinda.

 

Tawallah maana yake ni kuwa rafiki wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahl al-Bayt a.s. na

 

Tabarrah inamaana ya kujiepusha na kujiweka mbali na kutokuwa na uhusiano wowote pamoja na wale maadui wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja Ahl al-Bayt a.s.

 

 

243.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Ma’arij,

70,  Ayah 22 -34 :

Isipokuwa wanaosali,

Ambao wanadumisha Sala zao,

Na ambao katika mali yao iko haki maalumu

Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba;

Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,

Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.

Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo

Na ambao anahifadhi tupu zao.

Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi –

Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka.

Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,

Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,

Na ambao wanazihifadhi sala zao.

Hao ndio watakao hishimiwa Jannat.

 

 

244.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.”

 

Sifa nne za watu wa Jannat

 

245.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. :

“Yeyote yule atakayekuwa na sifa nne basi Allah swt ataliandika jina lake miongoni mwa watu wa Jannat :

  • Mtu ambaye mwepesi kwa kutoa shahada kuwa hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu na Mimi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume wa Allah swt.
  • Mtu ambaye anasema: Alhamdu lillaah pale apatapo neema
  • Mtu yule asemayeAstaghfirullah pale atendapo dhambi
  • Na yule asemaye Inna lillaahi wa inna ilayhi rajiun pale apatapo msiba.

 

246.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Mumin masikini na mafukara ndio watakaokuwa wa kwanza kuingia  Jannat kwa miaka arobaini kabla ya Mumin matajiri kuingia Jannat.

(Nitawapeni mfano. Ni sawa na meli mbili zinazopita katika vituo vya ukaguzi wa maofisa wa forodha. Naye baada ya ukaguzi anaona kuwa meli moja haina chochote, ipo tupu, hivyo ataiachilia ipite na kuendelea na safari yake. Na pale anapoikagua meli ya pili, anakuta kuwa imejaa shehena na hivyo huisimamisha na kuanza uchambuzi na ukaguzi.)

 

247.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliulizwa kuhusu Ayah ya

    Qur'an Tukufu : Surah al-Waqiah, 56, Ayah ya  10 , 11 , 12

Na wa mbele watakuwa mbele

Hao ndio watakao karibishwa

Katika Bustani zenye neema

 

248.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema :

“Jibrail a.s. kaniambia: ‘Inamaanisha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. na Mashi’ah. Wao ndio watakao kuwa wa kwanza kabisa kukaribia Jannat , wakiwa wamemkurubia Allah swt , Aliye Mkuu, kwa heshima mahususi waliyojaaliwa.’”

 

249.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Je itakuwaje pale ambapo wewe utakuwa umesimama mbele ya Jahannam, na Daraja (Siraat) litakapowekwa, na watu watakapoambiwa: ‘Vukeni Daraja ( Siraat ) hili.’

 

Na wewe utauambia moto wa Jahannam ‘ Huyu ni kwa ajili yangu, na huyu ni ka ajili yako !’

 

Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. alijibu :

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , je ni nani hao watakaokuwa pamoja nami ?”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamjibu :

“Hao ni Mashi’ah wako, watakuwa pamoja nawe popote pale uwapo.”

 

Amepokewa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema :

“Haki ipo pamoja na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. yupo pamoja na haki.”


JAHANNAM

 

250.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuhusu adhabu katika daraja la tatu

la Jahannam  ( iitwayo Saqar) ni kama ifuatavyo :

“Humo yako Mateso makali mno, inapopumua wakazi wake huungua kuwa majivu kwa kutokana na joto lake, lakini hawatakufa. Nyama yao itaunganikana tena ……… Humo pia kuna kisima kiitwacho Saqar ambayo ni kwa ajili ya wale wajivunao, wakandamizaji na wadhalimu, na walioasi na ambapo mateso yatakuwa makubwa zaidi.

 

Iwapo hii ndiyo itakuwa hali ya daraja la nne la Jahannam  sasa hebu fikiria hali itakayokuwa katika daraja la tano, sita na saba.

 

Tumwombe Allah swt atuepushe na Jahannam  !  Amin.

 

251. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema :

“Muelewe waziwazi kuwa hakuna atakayeishi katika Jahannam  kwa milele isipokuwa kafiri, Munafiki na watendao madhambi na uasi. Ama kwa watu wataomaliza kutimiza kipindi cha adhabu zao, watatolewa huru kutoka Jahannam.”

 

252.  Qur’an Tukufu Surah ya Al-Balad, 90, Ayah ya 19-20 

zisemazo :

Lakini waliokanusha Aya Zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao.

 

253.  Qur’ani Tukufu  Surah al-Humazah, 104, Ayah 5 – 9 :

Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika (Moto unaoitwa) Hutama.  Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini ( Huo Moto unaoitwa ) Hutama ? Ni Moto wa Allah swt uliowashwa (kwa ukali barabara). Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) watafungiwa (wewemo ndani yake ). Kwa magogo marefu marefu

 

254.  Qur’ani Tukufu  Surah al-Mursalat, 77: Ayah ya 32:

"Hakika (Moto huo) hutoa macheche yaliyo kama majumba."

 

Milango ya Jahannam

 

255.  Mlango wa kwanza

  • Yeyote yule atakayekuwa na matumaini katika Allah swt basi daima atakuwa mtu mwenye furaha na mafanikio;
  • Yeyote anayekuwa na khofu ya Allah swt basi anajaaliwa usalama;
  • mtu mwovu na aliyepotoka na mstahiki wa adhabu za Allah swt ni yule ambaye hana matumaini yoyote kwa Allah swt na wala hana khofu ya aina yoyote ile ya Allah swt.

 

256.  Mlango wa pili

  • Yeyote yule asiyetaka kufanywa uchi Siku ya Qiyama, basi awavalishe nguo wale walio uchi humu duniani,
  • Yeyote yule asiyetaka kupatwa na kiu Siku ya Qiyamah, basi awanywishe wale wenye kiu humu duniani,
  • Yeyote yule asiyetaka kupatwa na njaa Siku ya Qiyamah, basi awalishe wale wenye njaa humu duniani.

 

257.  Mlango wa tatu

  • Allah swt huwalaani wale wasemao uongo,
  • Allah swt huwalaani wale walio mabakhili,
  • Allah swt huwalaani wale wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge.

 

258.  Mlango wa nne

  • Allah swt humdhalilisha yule ambaye anaidharau Dini ya Islam, 
  • Allah swt humdhalilisha yule anayewakashifu Ahl ul-Bayt a.s. ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
  • Allah swt humdhalilisha yule ambaye anawasaidia wadhalimu katika kuwadhulumu watu.

 

259.  Mlango wa tano

  • Msiendekeze matamanio yenu, kwani matamanio yanapingana na tendo la kusadikisha;
  • Musiyaongelee zaidi yale yasiyowahusu kwani mtaondoka katika Baraka za Allah swt;
  • Na kamwe msiwe wasaidizi wa madhalimu.

 

260.  Mlango wa sita

  • Mimi nimeharamishiwa kukubalia Mujtahid (hawa ni wale ambao wamefikia upeo wa Ijtihad, uwezo wa kutoa fatwa. Rejea vitabu vya Fiqh ndipo utakapoweza kupata ilimu zaidi katika somo hili).
  • Mimi nimeharamishiwa kukubalia wale wanaofunga saumu.

 

261.  Mlango wa saba

  • Ujihisabie mwenyewe matendo yako kabla hujafanyiwa hisabu ya matendo yako;
  • Uikaripie nafsi yako kabla wewe hujakaripiwa;
  • Na mwabudu, Allah swt aliye Mkuu na aliyetukuka, kabla ya wewe hujafika mbele yake na ambapo hautaweza tena kumwabudu na kumtukuza.

 

 

262.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amenakiliwa katika

uk.145, J.1 ya al-Zamakhshari’s Rabee’ al-Abrar akiwa amemwuliza Malaika Jibrail a.s.,

“Je ni kwa nini mimi kamwe sijamwona Malaika Mikaili a.s. akicheka au kutabasamu?”

 

Malaika Jibraili a.s. alimjibu:

“Mikaili kamwe hakucheka wala kutabasamu kuanzia pale Jahannam  ilipoumbwa. ” 

 

263.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema,

“Katika safari yangu ya usiku wa (‘Israa), mimi nilisikia sauti kubwa mno, hivyo nilimwuliza Malaika Jibrail a.s., ‘Je sauti hii kubwa ni ya nini, Ewe Jibraili ?’

 

Naye alinijibu,

‘Ni jiwe lililotupwa kutokea juu kuangukia ndani mwa Jahannam , na imekuwa ikianguka kwa muda wa vipindi sabini vya baridi, na sasa ndipo ilipofika chini.”

 

264.  Abu ‘Asim ‘Ubayd ibn ‘Umayr ibn Qatadah al-Laythi, Hakimu wa

 Makkah (aliyeariki 68 A.H.), amesema,

“Jahannam  hupumua mara moja kwa sababu yake Malaika na Mitume a.s. yote hutetemeka, kiasi kwamba hata Mtume Ibrahim a.s. hupiga magoti na kusema, “Ewe Mola wangu ! Nakuomba uniokoe!”

 

265.  Abu Sa’eed al-Khudri amenakiliwa akisema,

“Iwapo milima itapigwa kwa rungu mara moja inayotumiwa na Malaika wa Jahannam , basi itavunjika vipande vipande na kuwa vumbi.”

 

266.  Tawoos ibn Keesan al-Khawlani amenakiliwa akisema,

“Wakati Jahannam ilipoumbwa, Malaika walishtushwa mno, na wakati nyie wanaadamu mulipoumbwa, basi walitulia.”

 

267.  Al-Hasan ibn Yasar al-Basir amesema,

“Kwa kiapo cha Allah swt! Hakuna hata mja mmoja wa Allah swt anayeweza kustahimili joto la Jahannam ! Tumeambiwa iwapo mtu atasimama Mashariki na Jahannam  ikawa upande wa magharibi na ikafunuliwa kidogo tu, basi bongo ya mtu huyo aliye Mashariki itachemka. Iwapo kama kiasi cha ndoo moja ya usaha wa Jahannam  ukimwagwa juu ya ardhi hii ya dunia, basi hakuna hata kiumbe kimoja kingalibakia hai.”

 

 

268.  Abu Zar al-Ghaffari, Allah swt amwie radhi, alikuwa akisema,

“Waambieni wale ambao hupenda kulimbikiza utajiri wao kuwa watachomwa nayo juu ya paji la uso wao, pembeni mwao, na migongoni mwao hadi watakapokuwa wamejaa kwa mioto.”

 

269. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, kama vile tuambiwavyo katika uk.243, J.8, ya Bihar al-Anwar,

“Hakuna Mja wa Allah swt mwenye utajiri au mali na hataki kulipa Zaka isipokuwa kwamba atachomwa kwa vipande hivyo vya mapesa vitakavyokuwa vimepashwa moto katika moto wa Jahannam na kwamba watatumbukizwa katika adhabu hizo kuanzia juu ya vipaji vyao vya nyuso zao na migongo yao hadi pale Allah swt atakapokuwa amemaliza kupokea mahisabu na adhabu za waja wake Siku ya Qiyamah, muda ambao ni wa maelfu ya miaka kwa mujibu wa mahisabu yetu. Hapo ndipo watakapotumwa ama kuingia Jannat   au  Jahannam  .”

 

270.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Italetwa mbele yake, naye atachukizwa nayo; na itakapoletwa karibu yake, itauchoma uso wake na kifuvu kitadondoka. Iwapo ataweza kunywa hata kidogo kutokamo, basi matumbo yake yatakatika vipandevipande na kutokezea sehemu za nyuma ya kutokezea haja kubwa.”

 

271.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameripotiwa akisema,

“Sala za mtu anayekunywa pombe hazikubaliwi kwa siku arobaini; na iwapo atakufa huku pombe ikiwamo tumboni mwake, basi Allah swt atamlazimisha anywe sadiid, maji yatokayo kwenye sehemu za uchi wa malaya ambayo yatakusanywa katika birika huko Jahannam  na kupewa watu hawa, na kwayo matumbo na ngozi zao zitachomwa.”

 

272.  Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anavyotupatia picha ya

Jahannam, tumwombe Allah swt asitutumbukize humo :

‘Janga kubwa kwa mtu ni kule kutumbukia katika Jahannam ; yeye atajihisi kuwa anachemshwa mzimamzima, na ataona mateso yake yasiyona mwisho, na kiumbe fulani kinakoroma na kupumua, viumbe vyote vilivyo humo hukosa raha na kamwe hawapati fursa ya kupumzika, na kamwe hawatapata kupumzika kutokana na adhabu zake au mauti ya uhakika. Yeye hasinzii hata kidogo wala hakutakuwa na mapumziko katiko mateso yake : Kutakuwa na maumivu yakudumu kiasi ambacho tunamwomba Allah swt atunusuru na kutusaidia .’  ( Hotuba  83 ).

 

273.  ‘Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa kuliko sehemu yoyote ile,

mahala ambapo mikono ya wakazi wake yanakuwa yamefungwa shingoni mwao, na vichwa vyao vimefungwa na miguu yao kwa minyororo na mavazi yao yametengenezwa kwa  lami. Mashati yao yametengenezwa kwa moto wakati ambapo adhabu zao za moto usiozimika kamwe hazitakwisha kamwe mahala ambapo mlango wake utakuwa umejazwa watu, katika moto mkali kabisa kiasi kwamba sauti zao zinasikitisha na kutisha, na miale ya moto ikipaa na kufikia kila sehemu na wala hakuna kujitoa kutoka humo na wala hakuna muda utakaokwisha,na wala haina mwisho wake kwa wale wanaoteketezwa na kuchomwa humo.’   ( Hotuba 109 ).

 

274. ‘Joto lake ni kali mno, kufikia chini kwake ni mbali mno, sakafu

 yake ni chuma, vinywaji vyake ni usaha.’   (Hotuba 120 ).

 

275.  ‘Siku ya Qiyamah, madhalimu wote wataletwa bila ya kuwapo na mtu yoyote wa kuwasaidia au kuwatetea, na hivyo watatumbukizwa katika moto wa Jahannam na humo atasagwasagwa kama vile machine za kusaga zifanyavyo, hadi hapo atakapojigonga kichwa katika sakafu ya chini kabisa.’ ( Hotuba 164 )

 

276. ‘Iwapo Malik (msimamizi wa Jahannam) atakuwa mkali, husababisha sehemu yake moja kuminyana na sehemu zingine, anapogombeza, milango yake huruka juu na chini (hutema kama volkeno). (Hotuba 183 )

 

277.  Ayah 23 ya Surah al-Fajr, 89 na katika Ayah zinginezo pia :

Basi Siku hiyo italetwa Jahannam. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini ?

 

278.  Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4,  Ayah 140 :

Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnaposikia Aya za Allah swt zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Allah swt atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

 

279.  Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Surah

al-Nisaa, 4 ,  Ayah 145 :

Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahannam, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru.

 

280.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Nisaa, 4,

  Ayah 55 :

Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.

 

281.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Jinn, 72,

 Ayah 23 :

….. Na wenye kumuasi Allah swt na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannam wadumu humo milele.

 

282.  Allah swt antuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 ,

Ayah 115 :

Na anayempinga Mtume baada ya kudhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamwingiza katika Jahannam. Na hayo ni marejeo maovu.

 

283.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Kahaf, 18,

 Ayah 106 :

Hiyo Jahannam ni malipo yao kwa walivyokufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu.

 

284. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu,Sura al-‘A’raf, 7, 

Ayah 179 :

Na tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.

 

285.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-‘A’raf,

7, Ayah 18 :

Akasema : Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

 

286.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura az-Zumar,

39,  Ayah 32 :

BASI NI NANI dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uwongo Allah swt na kuikanusha kweli imfikiapo ?  Je! Siyo katika Jahannam makazi ya hao makafiri?

 

287.  Na vile vile  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu ,

Sura al-A’raf, 7, Ayah 36 :

Na wale watakaokanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa Motoni; humo watadumu.

 

288.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Hud, 11,

  Ayah 113 :

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Allah swt, wala tena hamtasaidiwa.

 

289.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Surah

al-Maidah,5,  Ayah 2 :

…. Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui….

 

290.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Jathiyah,

 45,  Ayah  24 :

Na walisema:Hapana ila huu uhai wetu a duniani – twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa dahar. Laini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadahani tu.

 

291.  Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema Safari ndefu lakini

matayarisho ya safari ni madogo. Tukiwa watumwa wa dunia basi tutatumbukia Jahannam .

 

292.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema katika Mizanul

Hikmah kuwa :

“Mapenzi ya dunia ndiyo chanzo chote cha kila aina ya madhambi.”

 

293. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al- ‘Asra’, 17,

Ayah 18 :

Anayetaka yapitayo upesiupesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannam ; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.

 

294.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Tawbah,

9,  Ayah  34 – 35 :

Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia za Allah swt. Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Allah swt. Wabashirie khabari ya adhabu iliyochungu.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya.”

(Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile ambamo zaka haijatolewa).

 

295.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Anfal, 8,

  Ayah  15 – 16:

Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo.

Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo – isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi – basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Allah swt . Na pahala pake ni Jahannam, na huo ni mwisho muovu.

 

296.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Maida,

 5,  Ayah 32 :

Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika wakiwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

 

297.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Nisaa,4,

 Ayah 93 :

Na mwenye kumuuwa Mumiin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam humo atadumu, na Allah swt amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.

 

298.  Qur’ani Tukufu , Sura al-Ali Imran, 3, Ayah 21 :

Hakika wanaozikataa Ishara za Allah swt , na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.

 

299.  Watu wa Jannat watawauliza watu wa Jahannam kile

kilichowaingiza Jahannam. Nao watawajibu kuwa wao hawakuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Muddathir, 74,  Ayah 39 – 46 :

Isipokuwa watu wa kuliani.

Hao watakuwa katika mabustani, wawe wanaulizana

Khabari za wakosefu:

Ni nini kilichokupelekeni Motoni (Saqar) ?

Waseme : Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali.

Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.

Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu.

Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya malipo.

 

300.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu,Surah

 al-Fussilat,41, Ayah 7 :

Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa akhera.

 

301.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Nisaa, 4,  

Ayah  10 :

Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumoni mwao moto, na watingia Motoni.

 

302. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al- Baqarah,

2, Ayah 275 :

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyosimama aliyezugwa na Shaitani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Allah swt ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Basi aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi,, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyokwisha pita, na mambo yake yako kwa Allah swt. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

Allah swt huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka…

 

303.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Ibrahim,

14,  Ayah 28 – 29 :

Hebu hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Allah swt kwa kukufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo ?

Nayo ni Jahannam ! Wataingia.  Maovu yaliyoje makazi hayo !

 

304. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Surah

al-Mutaffifiin, 83, Ayah 1 – 10 :

Ole wao hao wapunjao!

Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.

Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa

Katika Siku iliyo kuu,

Siku watapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote ?

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.

Unajua nini Sijjin ?

Kitabu kilichoandikwa.

 

305. Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Humaza,

104,  Ayah 1 – 5.

Ole wake kila safihi, msengenyaji !

Aliyekusanya mali na kuyahisabu.

Anadhanim kuwa mali yake yatambakisha milele !

Hasha! Atavurumishwa katika Hutama

Na nani atakujuvya ni nini Hutama ?

Moto wa Allah swt uliowashwa.

Ambao unapanda nyoyoni.

Hakika huo utafungiwa nao

Kwenye nguzo zilionyooshwa.

 

306.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Surah

al-Mumin, 23, Ayah 43 :

Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.

 

307.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu , Sura al-Asra’,

17,  Ayah 27 :

Kwa hakika wabadhirifu ni ndugu wa Masheitani. Na Shaitani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi.

 

308.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Zukhruf,

43,  Ayah 74 :

Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannam

Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.

 

309.  Allah swt anatuambia katika Qur’ani Tukufu, Sura al-Nisaa,

   4,  Ayah 14 :

Na anayemuasi Allah swt na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Allah swt ) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.

 

310.  Allah swt amewaamrisha Malaika kuwa:

Mtu anaponuia kutenda jambo jema wamwamdikie thawabu. Na anapoanza kutembea katika kulifanya tendo jema basi hapo pia anaongezewa thawabu nyingi na pale anapolianza kutenda tendo jema basi huongezewa zaidi ya hayo na anapomaliza kulitenda tendo jema basi hapo analipwa thawabu nyingi mno zisizo na  hisabu.

 

Lakini mtu anaponuia kutenda dhambi basi hapo haandikiwi adhabu, na anajitoa kwenda kutenda dhambi napo pia haandikiwi kwa sababu inawezekana akarudia njiani na anapolianza tendo ovu pia kuna uwezekano wa kutolikamilisha na kwa masikitiko makubwa, anapolikamilisha basi kwa huruma zake Allah swt, huandikiwa dhambi moja tu.

 

 

 


T A W B A

311.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Al-Mahajjat-ul-Baydha:

“Majonzi makubwa ya watu wa Jahannam ni kuahirisha kwao Tawba”

 

312.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika,

Was’il al-Shiah, J.16, Uk.74:

“Yeyote yule anayefanya Tawba ni sawa na yule mtu ambaye hana mzigo wowote wa madhambi ya aina yoyote ile.”

 

313.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Qurar-ul-

Hikam, Uk. 240:

“Wapo waahirishaji ambao huahirisha kufanya Tawba hadi hapo mauti inapowafikia.”

 

314.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., katika Bihar al- Anwar, J. 77, Uk. 63:

“Ewe ‘Ali ! Amebarikiwa yule ambaye anatazwa na Allah swt wakati pale anapolia kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi ambayo hakuna mwingine ajuaye illa Allah swt tu.”

(Baadhi ya Ahadith zinasisitiza kuwa haimpasi mtu kuwaambia watu wengine juu ya madhambi yake mwenyewe. Hivyo inambidi aungame madhambi yake kwa Allah swt tu na wala si kwa mtu mwingine.)

 

315.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwa , J. 3, Uuk. 314:

“Katika kila sehemu ya tatu ya usiku na usiku wa kuamkia Ijumaa kuanzia usiku uingiapo( hadi alfajiri) Allah swt huwauma Malaika mbinguni ili kuita: ‘Je yupo mwenye kuomba ili nimtimizie ombi lake ?’ Je yupo yeyote mwenye kufanya tawba ili nimrejee ? Je yupo aombaye msamaha ili nimsamehe ?’ “

 

Tanbihi: Katika utamaduni wa Kiislamu, tunafundishwa kuwa kulala katika usiku wa kuamkia Ijumaa kunaitwa usingizi wa masikitiko ; kwa sababu Siku ya Qiyama watu watakuwa wakisikitika mno kwa kulala usiku hizo.

 

316.  Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika,  Bihar al-

Anwar, J. 92, Uk. 216:

“Fungeni milango ya madhambi kwa kumwomba Allah swt , na mufungue milango ya utiifuu kwa kusema Bismillah-ir-Rahmaan-ir-Rahiim.”

 

 


KULINDA HESHIMA YA WAUMINI

 

317.   Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika, 

Bihar al- Anwar , J. 74, Uk. 301:

“Ni faradhi kwa kila Mwislamu kusitiri na kuzificha aibu sabini (70) za Mwislamu mwenzake (ili kulinda heshima yake).”

(Makosa na kasoro zake zote zishughulikiwe kibinafsi na wala zisienezwe na kutangazwa kwa watu wengine).

 

318.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Bihar

al- Anwar, J. 74, Uk. 165:

“Kubali msamaha akuombao Nduguyo Mwislamu na kama hakufanya hivyo, jaribu kumvumbulia hivyo.”

 

319.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, 

Mustadrak Al-Was’il al-Shiah’il-ush-Shiah,   J. 12, Uk. 305 na 14155:

“Hali mbaya kabisa ya uhaini ni kutoboa habari zilizo siri.”

 

320.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Ghurar-

ul-Hikam, Uk. 322:

“Kumuonya kwako aliyetenda makosa miongoni mwa au mbele ya  watu ni kumdhalilisha.” (Inakubidi uongee naye katika faragha).”

 

321.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Al-kafi,

J. 2, Uk. 192:

“Katika matendo yote aypendayo Allah swt, ni kule kumletea furaha Mwislamu kwa mfano : kumshibisha, kumwondolea majonzi yake, au kumlipia madeni yake.”

 

 


M A T E N D O  M E M A

 

322.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwar , J. 76, Uk. 43:

“Kwa kufanya usuluhisho na amani miongoni mwa watu wawili (kwa kulinganisha) ni borai kuliko ibada za sala na saumu zake mwenyewe.”

 

323.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Nahjul-

Balagha, Uk. 511 , Semi No. 248;

“Iwapo mtu atakufikia wewe kwa mema, basi inakubidi uhakikishe kuwa fikira zake zinabakia kweli.”

 

324.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

  Bihar al- Anwar , J. 96, Uk. 119:

“Yeyote yule awaongozaye watu kwa taqwa (atalipwa) sawa na yale ayatendayo (aliyeongozwa) hayo matendo mema..”

 

325.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Al-Khisal

cha Saduq, Uk. 323:

“Yapo matendo sita ambayo Mwislamu Momiin anaweza kufaidika nayo hata baada ya kufariki kwake:

·        Kumwacha nyuma mtoto atakaye mwombea maghfira,

·        Kuacha Mus.-hafu sharifu ambao watu watakuwa wakisoma,

·        Kuchimba kisima cha maji kitakachokuwa kikiwafaidisha watu,

·        Mti alioupanda yeye,

·        Sadaka aliiyoitoa katika kusababisha maji yakatirika vyema,

·        Ahadith na Sunnah nzuri atakazokuwa ameacha nyuma yake na zikifuatwa na watu.

 

326.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.katika,

Bihar al- Anwar, J. 76, Uk. 126:

“Iwapo isingalikuwa vigumu kwa Ummah wangu basi ningalikuwa nimewaamrisha kupiga miswaki kwa kila Sala.”

 


DHULUMA NA UONEVU

 

327.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Thawab-ul-A’amaal, Uk. 309:

“Siku ya Qiyama, mwitaji ataita:’ Je wako wapi wadhalimu na wasaidizi wao na wale wote waliowatengenezea wino au waliowatengenezea na kuwakazia mifuko yao au waliowapatia wino kwa ajili ya kalamu zao ? Kwa hivyo, wakusanye watu wote hawa pamoja nao !’ “

 

328.    Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Nahjul-

Balagha, Uk. 347:

“Kwa kiapo cha Allah swt, Iwapo nitapewa umiliki wa nchi sana pamoja na yale yote yaliyomo chini ya mbingu zilizo waz  ili nimuasi Allah swt kwa kiasi cha mimi kunyofoa punje moja ya shairi kutoka kwa sisimizi, basi mimi kamwe sitafanya hivyo.”

 

329.   Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika,

Al-Kafi, J. 2, Uk. 330:

“Zipo aina tatu za dhuluma: moja, ni ile ambayo Allah swt anasamehe, pili, ile ambayo Allah swt haisamehe, na tatu ni ile ambayo Allah swt haipuuzii.

 

Hivyo, dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni ukafiri dhidi ya Allah swt. Na dhambi ambalo Allah swt anaisamehe ni kile mtu anachojifanyia dhidi yake mwenyewe na Allah swt. Lakini dhambi ambalo Allah swt haipuuzii ni ile ambayo inavunja haki za watu. “

 

Ufafanuzi:

Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

 

330.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika, Tasnif

Ghurarul Hikam, J. 2, Uk.36 :

“Dhuluma husababisha miguu kupotoka, inaondoa baraka na kuangamiza umma au taifa.”

 

331.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika, Nahjul-

Balagha, Barua  na 53:

“Hakuna kitu kinachovutia na kuharakisha kuondolewa kwa neema za Allah swt spokuwa kuendekea kwa dhuluma, kwa sababu Allah swt anazisikiliza dua za madhulumu na huwa yuko tahadhari pamoja na madhalimu.”


HAKI ZA WAISLAMU WENZAKO

 

332.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwar , J. 75, Uk. 150 :

“Yeyote yule anayemhuzunisha Mwislamu mwenzake basi kamwe hawezi kumfidia hata kama atamlipa dunia nzima kwani haitatosha (ispokuwa iwapo atatubu na kumfurahisha Mwislamu huyo).”

 

333.   Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. Amesema katika, Bihar

al- Anwar, J. 2, Uk. 75:

“Moja ya faradhi miongoni mwenu  kuelekea Mwislamu mwenzenu ni kutokumficha kitu chochote ambacho kinaweza kumfaidisha humu duniani au Aakhera.”

 

334.    Al-Imam Al-Hassan Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

Amesema katika,

“Watendee watu vile utakavyopenda wewe kutendewa.”

 

335.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Ghurarul-

Hikam, Uk.181:

“Alla swt humrehemu mtu ambaye anahuisha yaliyo haki na kuangamiza na kuteketeza yale yaliyo batili, au hukanusha dhuluma na kuimarisha uadilifu.”

 

336.   Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Tuhfatul-

Uqul, Uk. 277:

“Tabia hizi nne ni kutokea tabia za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. : haki, ukarimu, subira na kuvumilia katika shida, na kusimamia haki ya Mumiin.”

 

337.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika, Nahjul-

Balagha, Barua  na 53 :

“Kwa hakika ni watu wa kawaida ndio walio nguzo za Din, nguvu ya Waislamu na hifadhi dhidi ya maadui.  Hivyo mwelekeo wako daima uwe kuelekea wao na uwanynyekee.”

 

338.    Amesema Al-Imam Ja’afar as-Sadiq a.s.katika, Al-Kafi,

J. 2, Uk. 170:

“Allah swt haabudiwi zaidi ya thamani kuliko kutimiza haki ya Mumiin.”

 

339.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Bihar al- Anwar, J. 67, Uk. 72:

“Yeyote yule anayemuudhi Mumiin, basi ameniudhi mimi.”

 

340.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

Mustadrak al-Was’il, J. 17, Uk. 89:

“Yeyote yule atakayemdhulumu Muumin mali yak pasi na hakie, basi Allah swt ataendelea kumghadhibikia na wala hatazikubalia matendo yake mema atakayokuwa akiyatenda; na hakuna hata mema moja itakayoandikwa katika hisabu zake nzuri hadi hapo yeye atakapofanya tawba na kuirudisha hiyo mali kwa mwenyewe.”

 

 


SALAAM -- KUSALIMIANA

 

341.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika,

  Bihar al- Anwar , J. 76, Uk. 4:

“Pale munapokutana miongoni mwenu basi muwe wa kwanza kwa kutoa salaam na kukumbatiana; na munapoachana, muagane kwa kuombeana maghfirah.”

 

342.  Al-Imam Hussein ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

Amesema katika, Bihar al- Anwar, J. 78, Uk. 120:

“Thawabu sabini (70) ni kwa ajili ya yule ambaye anaanza kutoa salaam na thawabu moja ni kwa ajili ya yule anayeijibu hiyo salaam.”

( Wakati watu wawili wanapoonana, mtanguliaji katika kutoa salaam hupata thawabu zaidi ).

 

343.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema katika, Bihar

al-Anwaar, J. 69, Uk. 393:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwakusanya watoto wa ‘Abdul Muttalib na kuwaambia:  Enyi watoto wa Abdul Muttalib ! muwe waanzilishi wa salaamu, mujali Jama’a zenu, musali sala za usiku wakati watu wengine wanapokuwa wamelala, walisheni vyakula watu, na muongee maneno mazuri na hayo kwa hakika mutaingia Peponi kwa amani.”

 

344.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 12, Uk. 55:

“Yeyote yule anayekuwa ni muanzilishi wa kutoa salaamu basi atakuwa ni mpenzi sana wa Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”.


 


KUTENDA MEMA NA KUZUIA KUTENDA MABAYA.

 

345.    Allah swt anatuambia katika Qur’an Sura Al Imran,

  3, ayah 104.

 Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.

 

346.     Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, 

J. 100, Uk. 92.

“Itakapofika wakati katika umma wangu ambapo Waislam watakuwa wakitekenya wengine wafuate mema na wajizuie na mabaya, basi kwa hakika watakuwa wametangaza vita dhidi ya Allah swt.”

 

347.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema,  Bihar al Anwaar, 

J. 100, Uk. 94.

“Yeyote yule anayeacha kukataza wengine wasifanye maovu kwa maneno na kwa matendo (ni tofauti na kuona maovu yakitendeka) basi huyo ni maiti inayotembea miongoni mwa walio hai.”

 

348.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shi’ah, J. 11, Uk. 278:

“Kumzuia Muislam asitende matendo maovu ni sawa na Allah swt kumlipa thawabu za Hija 70 zilizokubaliwa…”

 

349.   Alisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Nahjul Balagha,

Uk. 392 Barua no. 31:

“Ambizeni miongoni mwenu kutenda mamea; basi mtakuwa miongoni mwa watendao mame.  Muwazuie wengine wasitende maovu kwa maneno yenu, na mujiepushe, na uwezo wenu wote, na yeyote yule anayetenda hivyo.  Mumtumikie Allah swt kama ni wajibu wenu; na angalieni kusiwepo na mulaumiaji au lawama yoyote itakayoweza kuwazuia nyie katika kutekeleza maswala ya Allah swt.  Jitupeni jitumbukizeni katika hatari kwa ajili ya kunusuru ukweli popote pale itakapo hitajika.” 

 

350.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Kafi,

J. 5, Uk.56:

“Kwa hakika kuwaambia watu yaliyoyakweli na kuwazuia kwa yale yaliyo potofu ndiyo sirah ya Mitume a.s. na waja wema. Kwa hakika ni jambo moja kubwa (wajib) kutokana na hiyo mambo mengine mengi yaliyo faradhishwa yanaweza kubakia, Ummah zingigine zinawea kunusurika, maelewano ni halali, dhuluma imekatazwa, na hakikaamani itajaa juu ya ardhi

 hii …”

 

351.    Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Ghurar-ul-

Hikam,Uk. 236:

“Uimara wa dini ni kule kuamrisha yaliyo mema na kukatza yale  yaliyo maovu, na kubakia katika mipaka ya Allah swt.”

 

352.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Wasa'il

    ush-Shi'ah, J. 16, uk. 135

“Yeyote anayeona maovu au mabaya yanatendeka basi ayazuie kwa matendo yake, kama ana uwezo huo, bila shaka; kama hawezi kufanya hivyo, basi azuie kwa ulimi wake, na kama hawezi kufanya hivyo pia basi anaweza kulaani kimomoyo.”

 

353.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ,

At-Tahdhib, J. 6, Uk. 181:

“Yeyote yule katika ‘Umma wangu anayechukua jukumu nakumamrisha mema na kukataza maovu na anaye jihusisha katika ucha-Allah swt,wataishi kwa raha na mustarehe na watakapo acha kufanya hivyo, basi baraka na neema za Allah swt zitaondolewa kwao.”

354.    Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.,  Nahjul

Balagha, Barua No. 47, Uk. 422:  

“Akiwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. wakati Ibn Muljam (Laana za Allah swt zile juu yake) alipompiga dharuba kali katika Masjid Kufa…”Muogopeni Allah swt (Na akasema tena)Muogopeni Allah swt katika mambo ya Jihad, (Jitihada za vita vitakatifu), kwa misaada ya mali, maisha na mazungumzo yenu katika njia ya Allah swt…”

 

Msiache kuamrisha mema na kukataza maovu isije hawa waovuwakachukua nafasi juu yenu, na baadaye(Katika hali hiyo)mtakapo Sali basi salah zenu hazita kubaliwa…

 

355.    Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Mustadrak

    Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 12, Uk. 185:

“Kuamrisha mambo memani jambo mmoja jema kabisamiongoni mwa watu.”

 

356.   Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 100, Uk. 89:

 “Matendo mema yote kwa ujumla, ikiwemu Jitihada za vita vitakatifu vya Jihad katika njia ya Allah swt, kwa kulinganisha na kuamrisha mema na kukataza maubaya, ni sawa na kyasi kidogo cha mate ya kilinganishwa na bahari yenye kina kirefu.”

 

357.   Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi

J. 5, Uk. 56:

“Allah swt alimteremshia Wahyi Mtume Shua’ib a.s

“Mimi nitawaadhibu watu wako kiasi cha laki moja na kati yao arobaini elfu ni waovu na elfu sitini ni katika watendao wema.”

 

Mtume Shua’ib a.s aliulizia hawa waovu wanastahili adhaabu lakini hawa watendao wema je akasema kwa hayo Allah swt alimterenshia wahi tena” Wao(walio wema)wamehusiana na watendao dhambi na hawa kuwa wakali hawa kughadhabishwa kwasabasbuadhabu na khofu zangu. 

 

 

 

 

 

358.   Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il

ush-Shi'ah, J. 16, Uk. 120:

 “Wambieni wenzenu wa tende wemana wajizui na ubaya kwani hamutambui kuwa kwakuamrisha mema kamwe haikaribishi mauti wala kukatisha riziki.

 

359.   Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Mustadrak-ul-

Wasa'il, J. 12, Uk.181:

 “Ole wale  watu ambao hawaisaidi Dini ya Allah swt kwa kuamrisha mema na kwa kutaza maovu.

 


ULIMI NA MAOVU YAKE.

 

360.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar

al-Anwaar, J. 71, Uk.286:

 “Matokeo yatokanayo na ulimi ni mabaya kabisa (yaliyo sabasishwa nayo) kuliko dharuba ya upanga mkali.

 

361.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Bihar

al-Anwaar  J. 71 Uk.277:

“Miongoni mwa mambo yote, ulimi unastahilikuwekwa katika mahabusukwakipindi kirefu zaidi kuliko kitu kinginechochote. (Kwasababu madhambi yetu mengi yana tokana nayo, kama vile kuwasuta watu, kusema uongo, kuzua mambo, kuwadhihaki wengine, na vile vile kuwa tuhumu watu wengi, n.k)

 

362.   Amesema Al Imam Amiril Momineen a.s. Ghurar-ul-

Hikam Uk. 228:

“Fikirieni na mupime kabla hamja ongea ili kwamba muweze kujizuia dhidi ya ( kutenda ) makosa.”

 

363.    Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Waqayi-

ul-Ayyam, Uk. 297:

“Maangamizo ya mtu yako katika mambo matatu “Tumbo lake, matamaniyo yake, na ulimi yake.”

 

364.  Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Bihar al-

Anwaar, J. 78, Uk.178 :

 “Hakuna mtu yeyote aliye salimika kutokana na ulimi wake hadi hapo yeye atakapo udhibiti ulimi wake.” 

 


KUSENGENYA NA KUTAFUTA KOSA.

 

365.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Al-Usul-

i- Kafi, J. 2, Uk. 57:

“Uzushi unafanya kazi dhidi ya Imani ya Mwislamu, Mumim kwa haraka zaidi kuliko ugonjwa wa Ukoma unavyo enea mwilini.”

 

366.    Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Ghurar-ul-Hikam

Uk. 307:

“Msikilizaji wa kile kinacho sengenywa ni sawa na yeye ndiomsengenyaji.”

 

367.   Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Bihar al-

Anwaar, J. 75,  Uk. 261:

“Kuacha tabia ya kusengenya ina thamani kubwa sana mbele ya Allah swt kuliko kusali sala yenye raka’h elfu kumi zilizo sunnah.

 

368.  Amesema ‘Abdul Mu’min-il-Ansari. Bihar al- Anwar ,

J. 75 , Uk. 262:

“Kuwa wakati moja yeye alikuwa mbele ya Imam Abil HassanMusa Ibn Jaffer a.s ambapo Abdillahi Jaffer alikuwa akitokezea na Abdul Mu’min alitoa tabasamu mbele yake. Na hapo Imam a.s alimuuliza Abdul Mu’min iwapo alimpenda Abdillahi Jaffer na alipomjibu Imam kuwa yeye hakumpenda (‘Abdillah ) isipokuwa yeye alikuwa ni Imam wa saba. Hapo Imam a.s alimwambia yeye ni ndugu yako, ni Mu’min na Mu’min moja ni ndugu wa Mu’min mwingine hata kama wazazi wake ni watu tofauti. Hivyo amelaaniwa yule anayemtuhumu ndugu yake wakiislamu, analaaniwa yule anayemgeuka ndugu yake Mwislamu, analaaniwa yule asiyempa muongozo mwema ndugu yake Mwislamu, na analaaniwa yule ambaye anamsengenya Mwislamu mwenzake.”

 

369.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Tara'if-ul-

Hikam, Uk. 182:

“Mwovu miongoni mwa watu ni yule ambaye anatafuta kasoro za watu wengine wakati akiziacha kasoro zake.”

 

370.   Al Imam Musa al-Kadhim a.s. Amesema, Bihar

al-Anwaar, J. 74, Uk.232:

“Amelaaniwa mtu yule ambaye anawasengenya ndugu zake wengine (Waislamu wenzake).”


UHARAMISHO WA KUSEMA UWONGO [52]

 

371.  Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah An-Nahl,16,

Ayah ya 105,

Wanaozua uwongo hawana imani

 

372.  Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

Mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni msema uwongo.”

 

373.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

Allah swt humlaani mwongo hata kama atasema ukweli”

 

374.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Jitahadharisheni, Mimi ninawaambieni dhambi Kuu kabisa katika Madhambi Makuu :

  • Kumshirikisha Allah pamoja na mtu mwingine
  • Wazazi kukufanya Aaq
  • Na kusema uwongo

 

375.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :

“Ugonjwa wa kusema uwongo ndio ugonjwa mbaya kabisa.”

 

376.  Vile vile Imam Hasan al-‘Askari amesema katika Mustadrad al-Wasa'il,Kitabu Hajj, mlango wa 12:

“Maovu yote yamefungwa katika chumba kimoja kwa kufuli, na uwongo ndio ufunguo wake.”

 

377.  Amesema al-Imam Musa ibn Ja'afar a.s. :

“Mtu mwenye busara kamwe hawezi kusema uwongo hata kwa matamanio yake mwenyewe.”

 

378.       Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :

“Itakuwa vyema kwa Waislamu iwapo hawatafanya urafiki na udugu pamoja na Mwongo.”

 

379.       Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika  Al-Kafi, j.2:

“Uwongo unateketeza misingi ya Imani.”

 

380.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema  katika  Al-Mustadrak al-Wasail :

“Mumin anaposema uwongo bila ya shida yoyote,basi Malaika elfu sabini humlaani !!”

 

“Na hutoka harufu mbaya kabisa kutokea moyoni mwake, harufu hiyo hufika hadi ‘arsh .”

 

“Na Allah swt humwandikia kwa dhambi hilo moja, madhambi sabini ya zinaa na zinaa zenyewe si zinaa za kawaida bali zinaa pamoja na mama yake .”

 

381.  Riwaya moja inasema :

‘Uwongo ni mbaya zaidi kuliko ulevi.’

 

382.  Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah

An-Nahl,16, Ayah ya 105,

Wanaozua uwongo hawana imani.

 

383.  Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah

Az-Zumar ,39, Ayah ya 3,

..Bila shaka Allah hamuwongozi aliye mwongo, aliye kafiri.

 

384. Kwa mujibu wa Ayah za Qur'an Tukufu  tunaambiwa kuwa

 mwongo ni mstahiki wa adhabu za Allah swt  na Allah swt huwa daima ameghadhabikia. Kama vile tuonavyo katika Ayah zifuatazo :

Surah Aali-Imran, 3,  Ayah ya 61

‘.. Tutake laana ya Allah swt iwashukie waongo.’

 

385.  Surah An-Nuur ,24 , Ayah ya 7 :

‘… Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.’

 

386.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Baqarah, 2,

Ayah ya 197,  kuwa : ‘Na katika Hajj hairuhusiwi maneno machafu wala ufusuka.’  Katika Ayah hii takatifu neno ‘fisq’ inamaanisha uwongo kwa mfano katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Hujurat , 49, Ayah ya 6, tunaona kuwa uwongo unaitwa kuwa ni ‘ufasiki’. Ayah yenyewe inasema :

Enyi mlioamini ! Iwapo mtaijiwa na mwongo na habari yoyote basi msikubalie tu bali mufanye upelelezi….. 

 

387. Tumepewa hukumu ya kujiepusha na kuabudu masanamu na kutosema uwongo na inasemwa kuwa : ‘Basi mjiepusheni na uchafu (wa mfano wa masanamu) na jiepusheni na maneno ya uwongo.’    Qur'an Tukufu, Surah Al-Haj, 22, Ayah 30, Hapa  qauli dhur  au laghwu  inamaanisha uwongo.

 

388.  Katika riwaya dhambi linaitwa Ithm  au Dhamb kwa Mfano amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. :

Uwongo yote kwa yote ni ithm na dhamb.

 

389.  Mwongo huwa ni mustahiki wa laana na ghadhabu za Allah swt

na  mfano wa kauli isemwayo katika Qur'an Tukufu Surah An-Nuur, 24 , Ayah 7,  isemayo :

… Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.

 

390.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Mustadrak al-Wasail  kuwa

“Jiepusheni na uwongo kwani uwongo huufanya uso wenu kuwa mweusi.”

 

 

391. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Usuli Kafi, Kitabul Iman wal-Kufr, mlango wa uwongo :

Bila shaka Allah swt ametengenezea kufuli  kila dhambi na ufungua wa kufuli hizo ni ulevi ambapo uwongo ni mbaya hata kuliko ulevi.”

 

392. Iwapo ulevi unaangamiza akili na fahamu lakini uwongo si kwamba unaangamiza akili na fahamu lakini unamfanya mtu akose adabu na heshima kiasi kwamba yeye huwa tayari kwa jambo lolote la kishetani. Iwapo mlevi atakapokuwa amelewa, huwa hana uwezo wa kuiharibu jamii kwani anakuwa hana fahamu wala habari zake mwenyewe lakini mwongo akiwa katika fahamu zake timamu huweza kuiharibu na kuiteketeza jamii nzima kwa hila na uwongo wake. Na hivyo kuleta hasara kubwa sana kwa jamii nzima.

 

393.  Zipo riwaya zisemazo kuwa Siku ya Qiyama midomo ya wasema uwongo itakuwa ikinuka harufu mbaya kabisa !.

 

394.  Harufu mbaya iliyozungumzwa hapo juu, itakuwa mbaya kabisa kiasi kwamba hata Malaika Siku ya Qiyama watachukizwa kumkaribia huyo mwongo anayenuka harufu mbaya. Lakini si Siku ya Qiyama tu, bali hata humu duniani pia wanaisikia harufu mbaya ikitoka vinywani mwa wasema uwongo. Ipo Hadith ya Mtume Muhammad s.a.w.w. isemayo :

 

“Wakati mja wa Allah swt anaposema uwongo, basi hutokwa na harufu mbaya kabisa kutoka mdomo wake kiasi kwamba hata Malaika pia wanajiweka naye mbali.”   (Mustadrak al-Wasail.)

 

395. Allah swt  humlaani msema uwongo kama vile Aya ya Mubahila inavyoelezea Qur'an Tukufu, Surah An-Nuur, 24, Ayah ya 7

kama ilivyokwishaelezwa kuwa inadhihirisha waziwazi.

‘… Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.’

 

396.  Imepokelewa riwaya kuwa harufu mbaya inayotoka midomo ya mwongo huifikia mbingu.

 

397.  Imepokelewa riwaya kuwa Malaika walio karibu ya Allah swt pia humlaani msema uwongo.

 

398. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Al-Kafi : “Uwongo ni kiangamizacho Imani.

 

399. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi :

“Mtu yeyote hataweza kuionja imani hadi hapo atakapoiacha uwongo, ama uwongo huo uwe wa kikweli au kimzaha.”

 

ndivyo inavyopatikana kwa mujibu wa riwaya,.

 

400. Ipo katika Hadith moja ya Mtume Muhammad s.a.w.w. isemayo :

 

“Kwa mtazamo wa heshima na kiadabu, mtu aliye chini kabisa ni yule msema uwongo.”

 

401. Imeripotiwa kuwa uwongo ni ufunguo wa kufuli ambayo imepigwa katika nyumba iliyofungwiwa maovu yote.

 

402.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Mustadrak al-Wasail kuwa : “Jiepusheni na uwongo kwani hiyo ni mojawapo ya aina za ufiski, na vyote hivi viwili ni vitu vya Jahannam.”

 

403.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail kuwa : “Zipo alama tatu za mnafiki : kusema uwongo, kufanya khiana na kugeuka ahadi alizozitoa.”

 

404.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail  :

“Ushauri wa mwongo hauna umuhimu wowote.”

 

405.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail:

“Na ugonjwa wa uwongo, ni ugonjwa mbaya kabisa wa kiroho.”

 

406. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Bila shaka Ibilisi hujipaka wanja, huvaa uchawi vidoleni na hutumia vyombo vya kuvutia hewa  puani. Ama wanja wake kufanya ni visingizio na uvivu, ama uchawi wake vidoleni ni uwongo na chombo cha kuvutia puani ni takabari na ghururi !”

 

407.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail :

“Mapato maovu kabisa  ya  mwanadamu, ni uwongo.”

 

 

408. Imeripotiwa katika Al-Mustadrak al-Wasail kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. alijiwa na mtu mmoja aliyeuliza :

“Ewe Mtume Muhammad s.a.w.w. Je ni matendo yapi hasa yanawafanya watu waingine Motoni (Jahannam) ?”

 

409.  Mtume Muhammad s.a.w.w. alimjibu :

“Uwongo ! Iwapo mtu atasema uwongo, basi atakuwa amejiingiza katika dhambi la uasherati, na hivyo amekufuru, na anayekufuru ataingia Motoni (Jahannam).”

 

410.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika  Wasa’il

al-Shiah :

“Kwa hakika mtu ambaye anapindukia kusema uwongo huadhibiwa adhabu ya kumuasi Allah swt ambavyo mojawapo ni ugonjwa wa usahaulivu !” Na hivyo ndivyo ilivyo kuwa mtu husema uwongo na mara husahau kama yeye alikuwa amesema uwongo na hatimaye uwongo wake hukamatwa na hivyo kudhalilika, na katika kujaribu kujitetea na kujihifadhi inambidi azungumze uwongo mmoja baada ya mwingine na hivyo huingia katika machachari ya kutaka kuilinda uwongo wa kwanza. Lakini hatambui kuwa kila asemavyo uwongo mmoja baada ya mwingine, anaendelea kujidhalilisha tu.” 

 

Yaani mara nyingi tunajaribu kuinusuru uwongo mmoja kwa uwongo hata mia, bila hata ya kuona aibu, na hii ndiyo laana ya Allah swt kwa msema uwongo. Hapa roho na akili yake vinamkataza, lakini wasiwasi wa Shaitani unamburuta tu katika kusema uwongo baada ya uwongo kwani yeye anakuwa yu mfungwa wa Shaitani.

 

411. Msema uwongo huadhibiwa kwa adhabu mahususi. Mheshimiwa Rawandi katika kitabu chake  Da’awat anaandika Hadith moja ndefu ya Mtume Muhammad s.a.w.w. katika maudhui haya ambayo inazungumzia vile alivyokuwa akisimulia Mtume Muhammad s.a.w.w. kile alichokiona katika Me’raj, kuwa :

“Nilimkuta mtu mmoja amelazwa juu ya tumbo lake na yupo mtu mwingine ambaye amesimama juu ya kichwa chake na ambaye anayo nyundo ya misumariambayo anakaa akimpiga yule mtu aliyelazwa na kumjeruhi. Uso wake unajeruhiwa kiasi cha kubomokabomoka kabisa katika vipande vipande ! Nyundo inapoinuliwa juu mtu huyo huwa salama na punde inapoteremka chini hujeruhiwa hivyo hivyo na hivyo ilivyo adhabu zake.”

 

Kwa hayo  Mtume Muhammad s.a.w.w. anasema kuwa :

“Mimi niliuliza ni sababu gani ya kuadhibiwa hivi ?” 

 

Alijibiwa :

“Huyu ni yule mtu ambaye alipokuwa akitoka nyumbani kwake, alikuwa akisema uwongo kiasi kwamba watu wa duniani walikuwa wakipata hasara kubwa kutoka na uwongo wake. Basi adhabu hii atabakia nayo hadi Qiyama.”

 

412. Mwongo hukosa sala za usiku wa manane (salatul Layl) na baraka zote zipatikanazo kwa sala hii huzikosa na baraka mojawapo ya sala hii ni kupatikana na kuongezeka kwa riziki. Bwana Sharif, anamnakili Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. akiwa amesema, katika Bihar al- Anwar : “Mtu anaposema uwongo hukosa baraka ya kusali sala za usiku wa manane na kama atakosa baraka za sala hiyo basi na baraka za riziki pia hukosekana !”

 

413. Allah swt Anasema katika Qur'an Tukufu,  Sura Az-Zumr, 39, Ayah 3 :

..Bila shaka Allah hamuwongozi aliye mwongo, aliye kafiri.

 

414.  Mtume ‘Isa ibn Maryam a.s. amesema , katika Al-Kafi : “Mtu ambaye anakithiri kwa uwongo basi ubanadamu wake humwondokea.” Na kwa hayo huwa ana uhusiano na watu kwani na watu wenyewe huwa hawana moyo nae.”

 

415.  Uwongo ni ukhabithi na uchafu mkubwa.

 

416.  Uwongo upo mbali na imani bali tuseme kuwa ni kinyume ya imani.

 

417.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Al-Mustadrak al-Wasail : “Kila kutakavyozidi kusemwa kwa uwongo, basi ndivyo vivyo hivyo imani ya mtu itakwenda ikipungua !”

 

418.  Mwongo ndiye mwenye madhambi mengi kuliko wote.

 

419.  Katika Al-Mustadrak al-Wasail  ipo Hadith ya Mtume Muhammad s.a.w.w. inayosema :

“Mojawapo ya dhambi kuu niya mtu mwenye mazungumzo na uwongo wa mtu kupindukia kiasi.”

 

420.  Mwongo hujiteketeza kwa uwongo wake

 

421. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail 

“Jiepusheni na uwongo hata kama mtaona ufanisi ndani yake, lakini kwa hakika huo si ufanisi bali ni maangamizo ndani yake.”

 

422.  Mwongo hastahiki kuwa ndugu na rafiki wa watu

 

423.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Wasa’il al-Shiah :

 

“Inambidi kila Mwislamu asiufanye uhusiano na kiudugu na urafiki pamoja na msema uwongo aliyekithiri !”  

 

424.  Akaendelea Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kusema :

“Kwani rafiki wake mwongo pia huchukuliwa kuwa ni mwongo ! Kiasi kwamba hata kama atasema ukweli wowote, ukweli huo hautasadikiwa kuwa ni ukweli.”

 

425.  Allah swt hawaongozi wafujaji na waongo

 

426.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu,  Sura Al-Mumin, 40, Ayah ya 28,  kuwa

‘Kwa hakika Allah hamwongozi yule ambaye amepindukia mipaka na mwongo.’ Hivyo inamaanisha kuwa msema uwongo na mfujaji huwa wako mbali na haki na uhakika.

 

427.  Mwongo huonekana kuwa ni binadamu, lakini sivyo

 

428.  Ipo riwaya katika kitabu kiitwacho ‘Uyunil Akhbar ar-Ridhaa a.s.:

Kwa hakika mwongo huonekana kuwa ni binadamu lakini katika hali ya Barzakh hana uso wa kibinadamu. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema akiwa anamwelezea Bi.Fatimah az-Zahra a.s. tukio la Mi’raj,: “Usiku wa Mi’raj mimi nilimwona mwanamke mmoja ambaye kichwa chake kilikuwa kikifanana na kichwa cha nguruwe na mwili mzima uliobakia ulikuwa kama wa punda. Sababu ya hayo ni kuwa yeye alikuwa na tabia ya fitina na alikuwa akisema uwongo.”

 

429.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura An-Nahl,16, Ayah 116 na 117 :

Na msiseme kwa sababu ya uwongo usemao midomo yenu, hili ni halali na hili ni haramu ili msije mkamzulia uwongo Allah. Hakika wale  wanaomzulia uwongo Allah , hawatafanikiwa.

 

430. ‘(Duniani) Kuna faida kidogo tu lakini (Aakhera) watapata adhabu kali ziumizazo.’

 

 

431.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Al-Kafi:

“Msituzulie hata uwongo mmoja kwani kama hivi uwongo utakutoweni nje ya Dini bora kama ya Islam.”  Yaani kwa kuwazulia Maimamu a.s. uwongo hata moja kunatokomeza Nuru ya Imani kutoka moyoni mwa waongo. Iwapo uwongo kama huu utazuliwa kwa Maimamu a.s. katika hali ya saumu, basi saumu inabatilika papo hapo.

 

432.  Ni jambo la kawaida kwetu sisi kusema :

“Allah swt yupo shahidi kuwa kile nikisemacho ni sahihi au Allah swt anajua kuwa kile nikisemacho ni kweli mtupu.”

 

433.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

“ ‘Mtu yeyote atakayesema kuwa Allah swt anajua’ wakati Allah swt anajua asili (yaani kinyume na achojidai huyo mtu kwa kutenda kinyume) basi ‘arsh-i-Ilahi inatetemeka kwa kuona Ukuu wa Allah swt.”

 

434. Vile vile Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika 

Wasa’il al-Shiah ,Kitabul Iman, mlango na.5 :

“Iwapo mtu atasema kuwa ‘Allah swt anajua wakati kwamba ni mwongo’ basi Allah swt anamwambia ‘je ewe haukumpata mwingine wa kumdanganya isipokuwa mimi tu? Ambaye unamzulia uwongo ?”

 

435. Kwa mujibu wa riwaya zinginezo, inasema kuwa wakati mtu

anapomfanya shahidi Allah swt katika uwongo anaouzua, basi Allah swt humwambia :

“Je haujampata mdhaifu mwingine yeyote kuwa shahidi wako katika uwongo na uzushi wako huo isipokuwa umenipata mimi tu ?”

 

 

436.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Kashaful Hujjat :

“Kamwe musinakili Ahadith kutoka mtu ambaye hategemewi kuwa sahihi amasivyo wewe utakuwa umesema uwongo mkubwa kabisa.na mwongo ni mtu aliyedhalilika mbele ya Allah swt na viumbe vyake.”

 

437. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-

Balagha, alimpa nasiha Harith Hamdani kwa barua aliyokuwa amemwandikia:

“Usiwe ukiwaambia watu yale yote uliyoyasikia, kwani kunatosheleza katika kusema uwongo.”

 

438.  Mtume Muhammad s.a.w.w.  amesema, katika Wasa’il

al-Shiah  :

“Mtu yeyote atakachoninasabia kile ambacho sijakisema, basi makao yake yatakuwa ni Jahannam (Motoni) tu.”

 

438. Bwana Nuuri katika kitabu chake Darus-Salaam anaandika

kuwa bwana mmoja aliyeelimika na mwenye matendo, kwa ajili ya kukisanifu kitabu maqame’ alimwendea Bwana Muhammad ‘Ali huko Karmanshah na kusema :

“Mimi nimeota usingizini kuwa ninaiparua nyama ya al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., sasa je nini utabiri wa ndoto hii ?”

 

439.  Bwana  Muhammad ‘Ali aliinamisha kichwa chake na kufikiria,

baada ya punde  akasema : “Bila shaka wewe ni khatibu wa kusoma Majlis na kusoma masaibu.”  Huyo Bwana akajibu : “Naam !”   Akamwambia :

“Ama shughuli hii uiache au usome kwa kutoa maudhui yako kutokea vitabu vinavyoaminiwa na kutegemewa kwa usahihi.”

 

Imeandikwa katika kitabu Shifaus-Suduur kuwa siku moja Shekhe mmoja alikuwa akisoma waadhi mbele ya Ayatullah al-Haj Muhammad Ibrahim Kalbasi. Sheikh huyo alikuwa akionyesha kuwa al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema “Ya Zainab! Ya Zainab !”  kwa kuyasikia hayo Ayatullah Kalbasi akasema kwa sauti ya kupaaza : “Allah swt auvunje uso wako ! Al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. hakusema mara mbili, badala yake alisema mara moja tu !”

 

440. Daraja moja lingine la uwongo ni kule kula kiapo cha uwongo,

kutoa ushahidi wa kiuwongo au kuficha ushahidi katika Mahakama ya Shariah.  Hakuna shaka kuwa  haya ndiyo uwongo ambazo zimo katika Madhambi Makuu. Insha Allah yote hayo yatazungumzwa kiundani ili kueleweka vyema.

 

441.  Amesema al-Imam Zayn-al-‘Aabediin a.s. katika Al-Kafi:

“Jiepusheni na uwongo, ama iwe ndogo au kubwa, au iwe katika hali ya masikitiko au huzuni au katika mzaha.”

 

442.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi :

“Mtu yeyote hawezi kamwe kuionja Imani yake hadi hapo ajiepushe na uwongo, haidhuru kama itakuwa katika huzuni au mzaha.”

 

443.  Imeripotiwa kutoka Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema

katika  Wasa’il al-Shiah :

“Hakuna wema katika uwongo hata kama itakuwa katika hali ya huzuni au furaha. Wala hautakiwi kutoa ahadi za uwongo kwa watoto wako, ahadi  ambazo hauna nia ya kuzitimiza. Kwa hakika uwongo unampotosha mtu kutenda madhambi makubwa makubwa ambayo hatimayake humtumbukiza mtu katika Moto wa Jahannam.”

 

444.  Mtume Muhammad s.a.w.w. alipokuwa akimwusia Abu Dhar

al-Ghaffari,alimwambia :

“Ewe Abu Dhar ! Mtu yeyote atakayejihifadhi dhidi ya uharamisho sehemu zake za siri na ulimi wake, basi ataingia Peponi.  Mtu yeyote atakayetamka uwongo katika mzaha basi uwongo huo katika mzaha utampeleka hadi Jahannam !”

 

“Ewe Aba Dhar ! Ole wake yule mtu ambaye anapozungumza huzungumza kwa uwongo ili aweze kuwachekesha watu.  Vile vile ole wake ! Ole Wake !  Ewe Abu Dhar ! Yule ambaye atakayekaa kimya ataongoka. Hivyo kukaa kimya kwako ni faradhi kuliko kunasibisha uwongo na kusitoke kamwe uwongo hata kiasi kidogo kutoka kinywani mwako.”

 

445.  Bwana Abu Dhar anasema:

“Je tawba ya mwenye kusema uwongo kwa kujua hivyo,

itakuwaje ?”

 

446.  Mtume Muhammad s.a.w.w. alisema  katika Wasa’il al-Shiah ::

“Kufanya Isteghfar na kusali sala tano kwa kutimiza masharti yake ndiyo yanayoweza kuyaosha madhambi hayo."

 

447.  Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika  Jihad :

“Laana ya Allah swt inamwia msema uwongo hata kama atasema katika  mzaha”

 

448. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Al-Khisal :

“Mimi ninachukua dhamana ya kumpatia nyumba katika daraja iliyo ya juu kabisa katika Jannat kwa ajili ya mtu yeyote ambaye anajiepusha na ugomvi na vita halafu hata kama yeye atakuwa katika haki. Na nitampatia nyumba mtu yeyote yule katika daraja iliyo ya kati ambaye anajiepusha kusema uwongo hata kama atakuwa katika mzaha. Na vile vile nitampatia nyumba katika bustani za Jannat kwa mtu yeyote yule mwenye tabia njema.”

 

449.  Imepokelewa riwaya kutoka  Safinatul Bihar, j.2, uk. 473

 kuwa Asma’ binti ‘Umays anasema,  :

“Usiku wa kwanza wa ‘Aisha, Mtume Muhammad s.a.w.w. alinipa chombo kimoja cha  mazima akisema ‘wape wanawake wanywe’ 

 

450.  Wanawake wakasema :

“Sisi hatuna njaa’ Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa kuyasikia hayo alisema :’Njaa pamoja na Uwongo musivichanganye kwa pamoja !”

 

451.  Asma’ akauliza :

“Iwapo sisi tutakuwa tukitamani au tukitaka kitu na tukasema kuwa hatukitaki au hatukitamani, basi jee huo ni uwongo ?”

 

452.  Basi Mtume Muhammad s.a.w.w. alimjibu :

“Naam ! Bila shaka kila aina ya uwongo unaandikwa kiasi kwamba hata uwongo mdogo mdogo pia huitwa uwongo.”

 

453.  Ipo riwaya moja kutoka kitabu Bihar al- Anwar , j. 16, mlango wa

 hishima ya ndugu mu’miin …, uk. 241 ipo riwaya ifuatayo :

Siku moja al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. alikuwa ameketi pamoja na mwanae Isma’il, na akaja mfuasi wake mmoja akatoa salaam na akaketi pamoja nao. Wakati Imam a.s. alipoondoka kuelekea nyumbani mwake, basi na yule mtu pia akaondoka kumfuata Imam a.s. hadi kizingitini mwa nyumba ya Imam a.s.  Imam a.s. hapo hapo aliagana nae na kuingia nyumbani mwake, mwana wa Imam a.s., Isma’il alimwuliza babake ni kwa nini hakumkaribisha mtu huyo kuingia nyumbani mwao kama desturi njema ?  Imam  Ja'afar as- Sadique a.s. alimwambia kuwa haikuwa munasibu kwa mtu yule kuingia ndani, kwani mimi binafsi sikuwa nataka huyo mtu aje ndani na wala sikutaka Allah swt anihesabu miongoni mwa watu ambao wanasema nini mdomoni na wanavyo nini moyoni mwao !”

 

454.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa uwongo Mkuu upo

     katika makundi matatu :

·         Kumwita mtu kwa jina mbali na jina la mzazi wa kweli.

·         Kusema ndoto za uwongo ambazo hakuziota,

·         Au aseme kile ambacho mimi (Mtume Muhammad s.a.w.w.) sikusema..

 

455.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika  Bihar al- Anwar,

 j.15, uk. 42 kuwa :

“Uwongo ulio ovu kabisa ni kunakili kwa riwaya zilizo za uwongo.”

 

456.  Siku moja al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwapo

katika baraza la Mua’wiyah na hapo mtu mmoja akaanza kutamka maneno yenye kashfa dhidi ya al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s..

 

457.  Al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu :

“Ewe ‘Umar ibn ‘Uthman ! Tabia yako ina upumbavu ambao wewe hauwezi kuuelewa. Mfano wako ni kama ule wa mbu ambaye akijiona mkubwa aliukalia mtende na wakati wa kutaka kuruka, aliuambia mtende : ‘jizatiti kwa umadhubuti, kwani niko naruka kwa ajili ya kuteremka !’  Kwa hayo mti  ukamjibu : ‘Mimi wala sijui ni kutoka wakati gani umenikalia juu, sasa hebu niambie kuondoka kwako kutaniangusha ?!”

 

458.  Tuelewapo kuwa jambo lililopo ni uwongo basi na kulisikiliza pia

ni haram. Kama vile kuandika na kusomwa kwa uwongo umeharamishwa basi na kunakili uwongo pia umeharamishwa.  Kwa hakika Qur'an Tukufu  imekuwa ikiwalaumu Mayahudi na Makafiri kwa kupeleka habari za uwongo za huku kupeleka  huko na za huko kuleta huku. Qur'an Tukufu  inatuambia :

‘ Enyi wasikilizaji wa maneno ya uwongo….’

 

459.  As-Shayk Sadduq (a.r.) ameinakili riwaya ifuatayo kutoka kwa

al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. kuwa al-Imam a.s. aliulizwa  :

“Je inaruhusiwa kusikiliza uwongo wa waongo kwa makini ?”

 

460. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika  kumjibu (Kitab-i-’itiqadat) :

“Hapana ! Iwapo mtu anamsikiliza kwa hamu na basi huwa anafanya ibada kwa mujibu wake.  Iwapo msemaji anamwamini Allah swt  basi msikilizaji atafanya ibada ya Allah swt .  Na iwapo msemaji anafuata maneno ya Shaitani basi msikilizaji atafanya ibada ya Shaitani.”

 

461. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Haj, 22,

Ayah 30 :

“Mjiepusheni na maneno ya upuuzi”

 

462. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Furqan, 25,

Ayah 72

‘Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo…’

 

463.  Popote pale ambapo kutakuwa na hatari ya maisha, mali au

heshima ya mtu na kama kwa kusema uwongo kutamwondolea hatari hizo basi kunaruhusiwa kusema uwongo katika sura hizo. Hatari hizo ama ziwe kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya mtu mwingine. Hata hivyo imeruhusiwa kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kunusuru hayo. Katika baadhi ya nyakati, ni faradhi kusema na kula kiapo cha uwongo katika kuyanusuru maisha ya mtu, mfano,  iwapo dhalimu atataka kumwua Mwislamu, ataka kumpiga na kumdhuru Mwislamu, au anataka kumdhalilisha na kumkashifu, anataka kumdhulumu na kumnyang’anya mali yake au anataka kumfunga mahabusu. Sasa iwapo huyo mdhalimu akikuomba anwani ya Mwislamu huyo, basi ni faradhi kwako kutompatia anwani yake, halafu hata kama itakubidi useme uwongo na ule kiapo cha kiuwongo kuwa wewe haujui chochote.

 

464.  Sheikh Ansari anawanakili Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na

al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Makasib  kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema , Wasa’il al-Shiah ,Kitab al-Iman, j. 3, mlango na. 12:

"Mnaweza kula kiapo cha uwongo lakini mumnusuru ndugu yenu Mwislamu asiuawe kibure !”

 

465.  Ismail Ibn Sa’ad ambaye Hadith yake ni sahihi anasema katika

Wasa’il al-Shiah , Kitabul Iman, j. 3, nambari 12 :

“Mimi nilimwuliza Al-Imam ‘Ali  ar-Ridha  a.s. kuhusu mtu ambaye amekula kiapo cha uwongo mbele ya mfalme kwa ajili ya kutaka kuinusuru mali yake.”

 

466.  Al-Imam ‘Ali  ar-Ridha  a.s. alimjibu :

“Hakuna shida yoyote.”

 

467.  Mwandishi anasema kuwa yeye alimwuliza tena Al-Imam

‘Ali  ar-Ridha  a.s. :

“Je inaruhusiwa kwa mtu kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kunusuru mali ya Mwislamu mwenzake kama vile alivyokula kiapo cha uwongo kwa ajili ya mali yake mwenyewe?”

 

468.  Al-Imam ‘Ali  ar-Ridha  a.s. alimjibu:

“Naam ! Inaruhusiwa.”

 

469.  Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s.  anasema katika  Faqiyyah :

“Iwapo itambidi Mwislamu kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kumnusuru Mwislamu mwenzake pamoja na mali yake isichukuliwe na mdhalimu au mwizi, basi hakuna shida ndani ya kula kiapo cha uwongo na si hayo tu, bali hatatakiwa kulipa kaffara ya kula kiapo cha uwongo na badala yake atapewa malipo mema kabisa pamoja na thawabu nyingi mno kutoka kwa Allah swt.”

 

470.  Vile vile iwapo ataweza kuvumilia hasara basi ni Sunnah

kuvumilia na hivyo asiseme uwongo.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha,  kuwa :

“Ni alama ya Imani kuwa mtu aseme ukweli tu hata katika wakati wa kupatwa hasara na asiseme uwongo kwa ajili ya kupata faida.”

 

471.  Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. amesema katika Wasa’il al-Shiah,

Kitab Haj :

“Mazungumzo yapo aina tatu :”

·         Ukweli

·         Uwongo

·         Kuwasuluhisha  watu

 

472.  Kuna mtu aliuliza :”Mimi niwe fidia kwako ! Je kuwasuluhisha

 watu ni kitu gani ?

 

473.  Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s.  alimjibu :

“Wewe umsikie mtu mmoja akimzungumza mtu mwingine na ukamwambia mtu mwingine kuwa fulani bin fulani alikuwa akikuzungumza vyema kabisa (ambapo kwa hakika ni kinyume chake kabisa) ”

 

 

474.  Vile vile iwapo bibi na bwana wamekwisha tengana na umefika

wakati wa talaqa basi inambidi mtu azungumze hata uwongo ilimradi aweze kuwasuluhisha, na kwa hakika hili ndilo litakuwa jambo jema kabisa.

 

475.  Mtu anaweza kumwendea mume na kumwambia kuwa “Loh ! Mke

wako kwa kweli anasikitika mno kwa kuachana kwani anakupenda kupita kiasi na hivyo hataweza kuvumilia kuachana kwenu na anaweza kuugua.”

 

476.  Na vivyo hivyo amwendee bibi na kumtengenezea mambo kama

hayo ya uwongo ili kusafishwe mazingira na kuleta usuluhisho na  muungano baina ya bibi na bwana.

 

477.  Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. akiwa

amesema :

“Hakuna tendo lililo bora kabisa baada ya kutimiza yaliyo faradhishwa kama vile kuwasuluhisha watu !  Hii ni kheri ambayo inayoeneza kheri  duniani kote.”

 

478. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa Mtume

Muhammad s.a.w.w. alisema wakati wa usia, katika Wasa’il al-Shiah , Kitab Hajj, mlango 141 :

“Ewe Ali ! Bila shaka Allah swt anapendelea uwongo katika kusuluhisha na hapendezewi ukweli katika kuzua ufisadi na

magomvi !”

479.  Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

“Kusuluhisha miongoni mwa watu, kufikiria usulihisho na kuepusha magomvi ni bora kuliko sala na saumu.”

 

480.  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

“Hakuna uwongo kwa mtu anayesuluhisha.”

 

481.  Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. :

  • “Uwongo ni mwovu na haikubaliki isipokuwa katika sura mbili :
  • Katika kuuondoa shari ya mdhalimu
  • Kuwapatanisha watu.”

 

482.  Mtume Muhammad s.a.w.w. anasema :

“Zipo nafasi tatu ambapo uwongo unapendeza: kudanganya katika vita, ahadi aitoayo mume kwa mke wake na kuwapatanisha watu.”

 

483. Ama kuhusiana na ahadi ya mume kwa mke wake, Islam

inapendelea kuwaona wakiishi kwa raha na mustarehe na waishi kwa kupendana. Hivyo kumwambia mke wako uwongo wa kumtimizia jambo fulani, kama unao uwezo basi vyema kabisa, lakini kama hana uwezo, basi anaweza kumpa ahadi ya uwongo ili kuepukana na ugomvi na kumuudhi mke wake.

 

Kwa mfano, wewe hauna uwezo wa kumtimizia ombi fulani la mke wako, kama kwa mfano anataka nyumba, lakini wewe kwa kutokuwa na uwezo huo, utamdanganya kuwa nitakujengea au kukununulia ili kumridhisha mke wako. Sote tunajua kuwa ukaidi wa mwanamke ni ukaidi mkubwa kabisa  na vile vile Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa “mwanamke ni kama mfupa wa ubavu, upo umepinda, hivyo usijaribu kuunyosha, utavunjika” hivyo tutumie mbinu kama hizi kwa nia njema ili kutuliza mambo nyumbani.

 

484. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi

(ikizungumzia thawabu za Allah swt na juu ya adhabu na matumaini ya kusamehewa) :

“Jiepusheni na kusema uwongo ! Pale mtu anapotarajia kupata  kitu basi anataka akipate tu hicho kitu (basi huwa tayari kufanya kazi yoyote ili aipate) na vile vile mtu anapokiogopa kitu chochote kile, basi hujiweka mbali nacho.”

 

485.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha, :

“Mtu yeyote anayefikiria kuwa yeye anamtegemea Allah swt  lakini matendo yake hayaonyeshi hivyo basi kwa kiapo cha Allah swt aliye Mkuu, mtu huyo ni mwongo.  Ingawaje mtu anapokitegemea kitu basi mwenendo wake hudhihirisha hivyo.  Lakini itawezekanaje yeye amtegemee Allah swt ambapo matendo yake hayadhihiri hivyo ? (mtu kama huyu kwa hakika si miongoni mwa wale wamtegemeao Allah swt  basi anajidanganya mwenyewe).  Vile vile mtu anapokiogopa kitu chochote basi matendo yake yatadhihirisha hali hiyo yaani ataamua kukikimbia kitu hicho. Lakini mtu anapodai kuwa anamwogopa Allah swt na kwa nini sasa hakimbii mbali na madhambi ?”

 

486.  Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s.  amesema katika Misbah

As-Shari’ah :

“Wakati musemapo Allahu Akbar basi muelewe kile kilicho baina ya mbingu za juu na ardhi, vyote ni vidogo mbele ya Allah swt na kwa undani wa moyoni mwenu muelewe kwa sababu Allah swt anapoona kuwa kuna mja wake ambaye hasemi Allahu Akbar kutokea undani mwa moyo wake, basi Allah swt (humwambia) ‘Ewe mwongo ! Wewe unataka kunidanganya basi kwa kiapo cha heshima na Utukufu Wangu basi mimi nitakuepusha na dhikr yangu !’”

 

487. Mtu anaposema kuwa :”Mimi ninayo furaha kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. ni Mtume wangu  na Qur'an Tukufu  ni kitabu Kitakatifu na kuwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni Imamu wangu. Na vyote hivyo vipo kwa ajili ya kuniongoza.” 

 

Ingawaje anatamka kwa mdomo lakini kimatendo utaona kuwa Shaitani na matamanio yake ya nafsi ndio viongozi wake !  Na huvifuata hivyo !  Utaona kuwa yeye havitilii maanani mafunzo na hidaya ya Qur'an Tukufu . Na vile vile hatilii maanani maamrisho na mafunzo yaliyotolewa na Maimamu a.s.  Kwa hivyo mtu kama huyu  ni mwongo.

 

488.  Wakati mtu anapofanya dua na akasema “(Ewe Mola wangu !)

Mimi ninapoziangalia madhambi yangu basi hulia na ninapoangalia ukarimu wako ninajawa na matumaini kuwa Wewe utanisamehea.”

 

Kwa hakika utaona kuwa tunatamka hivyo lakini hatujali madhambi na hata anapotambua kuwa jambo fulani ni dhambi, basi hulitenda bila ya woga wowote ule !  Uso wake haushtuki hata punje kidogo wakati wa kutenda dhambi !  Basi hujitoa katika ukarimu na rehema za Allah swt !  Je mtu kama huyu anapoyatamka maneno kama hayo yalivyo katika dua, anasema ukweli ? Je uwongo wake si upo
wazi !?

 

489. Vile vile mtu anapotamka “Mimi ninalia kwa kutokwa nafsi yangu

na ninalilia maswala ya kaburini na ninalilia khofu ya Qiyama”

 

ingawaje ni dhahiri kuwa hakuna anachokililia kitu kama hicho Huo ni uwongo wake kwani matendo yake hayaonyeshi kama kweli anayo khofu kama hiyo moyoni mwake.  Al-Imam Zaynul ‘Aabediin a.s. amesema katika Dua-i-Abu Hamza Thumali : “Ewe Allah swt !  Labda Wewe umenipata katika ngazi za waongo na kwa hivyo (umeniondolea mtazamo wako wa kirehema) na umeniacha katika hali niliyonayo.”  Yaani mimi nimekuwa nikiyatimiza matamanio ya nafsi yangu na wala sijui nitaangukia katika maangamizo yapi.

 

490. Mfano wa kuwaambia uwongo Maimamu a.s. ni kama vile

tunavyosema katika Ziyarat :

“Enyi Aimma Ma’asumiin a.s.! Mimi nimezikubali kauli zenu na ninayafuata hukumu (na maamrisho) zenu na mimi ni mwenye kuwatiini.” 

 

Sasa iwapo mtu atazisikia kauli na maamrisho ya Maimamu a.s. na asizifuate na badala yake akazifuata matamanio na maamrisho ya nfsi yake basi bila shaka mtu kama huyu ni Shaitani ! Basi inadhihirika waziwazi kuwa huyo ni mwongo kwa Maimamu a.s. !

 

491. Vile vile mfano mwingine wa kusema uwongo upo unapatikana

katika Ziyarat, wakati tusemapo :

“Enyi Aimma watoharifu ! Mtu yeyote aliye na amani pamoja nanyi basi mimi pia nitakuwa na amani pamoja naye na yeyote yule atakayepigana vita pamoja nanyi au kuwapinga basi nami nitakuwa na vita naye na nitampinga vile vile  !”

 

492. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyodai, lakini matendo yetu ni kwamba tunao urafiki mzuri wa kidugu pamoja na maadui wa

Islam ! Na badala yake sisi tunafanya uadui pamoja na wapenzi na wafuasi wa Aimma a.s.. Wakati anaposema

“Enyi Maasumiina.s. ! Mimi ninawaacha wale wanaokukhilafu nyinyi.” 

Lakini kwa hakika haya haytekelezwi kimatendo Sasa jee mtu kama huyu si mwongo mbele ya Maimamu a.s. ?

 

493.  Hivyo sisi tunaweza kusema kuwa muumin hawasemi uwongo

mfano kuwa kila Mumiin anakuwa na khofu ya Allah swt  kama vile tunavyoambiwa katika Qur'an Tukufu  : ‘Kama nyinyi ni mumiin wa kweli basi muwe mukiniogopa Mimi tu’ (Surah Aali-Imran, 3, Ayah ya 175).  

Na vivyo hivyo Mumiin wote ndio wanaomtegemea Allah swt tu na bila shaka wote wanakuwa na khofu ya Allah swt  na matumaini yao pia yanakuwa na ngazi mbalimbali na kamwe haiwezekani zinalingana na za Aimma a.s.

 

494.  Dua-i Abu Hamza Thumali :

“Ewe Allah swt ! Mimi madhambi niliyoyatenda si kwamba nikukupinga wewe na wala sikutenda madhambi hayo kuwa nikichukulia hukumu zako ati ni za kawaida na wala sikutenda madhambi kwa kufikiria kuwa adhabu zako ni ndogo bali  nimetenda kwa kutokana na kasoro zangu za kinafsi na ujeuri wangu..”

 

495.  Du’a :

“Ewe Allah swt ! Nakuomba unipatie yakini ya kweli kwayo ambayo mimi niweze kutii amri zako kikamilifu.” 

 

496.  Inapatikana katika riwaya kuwa “Mtu anapokitaka kitu basi kwa

kufanya jitihada, anakipata tu.”

 

497.  Qur'an Tukufu  katika Surah at-Tawbah, 9, Ayah ya 119 :

‘Muwe pamoja na Wasemao ukweli.’  Katika Ayah hii Allah swt anatuambia kuhusu ‘Sadiqiin’ ambao ndio Ahlul Bait a.s. ya Mtume Muhammad s.a.w.w.’

 


KUSEMA UONGO[53]

 

498.  Anas Ibn Maliki Khisal-i-Sadduq, Uk. 321:

Anaelezea kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema “Chukueni mambo sita kutoka kwangu, na mimi nakubalia, na kutoa dhamana (Ya wewe kuingizwa Jannat)

 1. Usiseme uongo 

  2.Unapo toa ahadi, usivunje

 3. Unapo pewa amana na wengine, basi uwemuaminifu

 4. Tazama chini ( usitende dhambi ).

 5. Chunga heshima yako

 6. Idhibiti mikono yako na ulimi wako.

 

499.    Amesema Imam Al Hassan  al-‘Askari a.s,Bihar

al-Anwaar, J. 72, Uk.263:

“Iwapo maovu yote yatawekwa katika nyunba moja, basi ufunguo

( wa milango yake ) itakuwa ni uongo.”

 

500.   Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. Tuhaful-'Uqul,

 Uk. 201:

“Jiepusheni na kusema uongo hata kama ni uongo mgogo au mkubwa, kama kwa wadilifu au unasema kwa kdhihaki, kwasababu mtu anapo  sema uongo mdogo basi anaweza kudiriki kusema uongo mkubwa pia. 

 

501.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Bihar al-Anwaar, J. 75,

Uk. 196:

Wakati mmoja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliulizwa kuhusu umbali baina ya ukweli na uongo naye akiwa akionyesha umbali huo baina ya macho yake na maskio yake kwa vidole vinne katika kutoa jibu hilo, “Kile majo yako yanayooonani ukweli na mengi na yale yanayo sikilizwa na maskio yako ni sehemu kubwa ni uongo.”

 

502.   Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi,

J. 2, Uk. 339:

“Kwa hakika Allah swt ameyawekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe.”

 

503.   Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 347:

“Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo.”

 

504.  Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi,

J. 2, Uk. 339:

“Kwa hakika Allah swt ameya wekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe.”

 

505.  Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 347:

“Muwe wa sema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo.”

 

 


MARAFIKI NA URAFIKI.

 

506.     Mtume Muhammad  s.a.w.w. Amesema, Bihar

al-Anwaar, J. 74, Uk. 192:

“Mtu anaathirika kwa imani ya marafiki zake.  Kwa hivyo, muwe waangalifu kabisa katika urafiki wenu pamoja nao.[54]

 

507.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Amesema: Bihar

al-Anwaar, J. 76, Uk. 267:

“Uwe rafiki wa yule ambaye atakuwa ndio heshima yako, si wewe uwe heshima yake. (Ufanye urafiki na wale walio juu yako ili wewe uweze kupata maendeleo kutokana na urafiki huo).

 

508.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Bihar

al-Anwaar, J. 74 Uk. 282:

“Ndugu yangu mpenzi ni yule (anayenitambulisha) makosa na kasoro zangu.

509.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Khisal-i-

Sadduq, J. 1, Uk. 88.:

“Kwa hakika kuna marafiki wa aina tatu kwa ajili ya Muislam:

1. Rafiki anayesema mimi niko pamoja nawe iwapo upo hai au umekufa: Na hili ndio matendo yake.

2. Rafiki anayesema mimi nipo rafiki wako hadi ukingoni mwa kaburi na nitakuacha:hawa ni watoto wake.

3. Rafiki anayesema mimi nitakuwa nawe hadi pale utakapo kufa:hii ni mali ambayo ataiacha humu duniani kwa warithi wake baada ya kifo chake.

 

Tanbih

Kutokana na riwaya hii, na kama hizi sisi tunaelewa kuwa kitu ambacho kitakuwa pamoja na huyo mtu aliye kufa na kuaga dunia hii katika siku ya Qiyamah imani na matendo yake mema. Na suala hili limezungumziwa katika ahadithi nyingi sana za Kiislam na vile vile katika ayah za Qur’an tukufu, kwa mfano:

 

510.  Allah swt anatuambia katika Qur’an Sura Ar-Raa;d, 13, ayah

 ya 29.

Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.

 

511. Allah swt anatuambia katika Qur’an Sura Al-Kahf,18, ayah 30.

Hakika wale walio amini na wakatenda mema – hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema.

 

512. Allah swt anatuambia katika Qur’an tukufu Sura Al-Kahf, 18, ayah ya 107.

Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.

 

513.  Allah swt anatuambia katika Qur’an tukufu Sura Maryam,19, ayah ya 96.”

Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi.

 

514.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. , Bihar

al-Anwaar, J. 74 Uk. 187:

“Muwe waangalifu katika kutafuta marafiki wa kweli na mujaribu kuwafanyia majaribio, kwa sababu wao watakuwa ndio msaada wenu pale mnapokuwa katika hali nzuri na watetezi wenu pale mtapokuwa katika shida na matatizo.”

 

515.     Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. , Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 141:

“Kukutana pamoja na wacha Mungut kunawaleteeni mema.”

 

516.     Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. Amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 78, Uk. 151:

“Jitahadharisheni na urafiki wa watendao madhambi, na kuwasaidia madhalimu.”

 


MARAFIKI WASIO WEMA

 

517.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Usul-i- Kafi,

J. 2, Uk. 379:

“Anayetafuta uhusiano na marafiki wa wale wanao wadhalilisha wapenzi wa Allah swt basi watambue kuwa wao wamemuasi Allah swt.”

 

518.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 16, UK. 146:

“Mnapojulishwa kuhusu marafiki zenu wanapotenda maovu, nendeni mumwambie:

Ewe fulani bin fulani ! Ama acha kutenda madhambi au ukae mbali nasi:

Na hapo utengane naye hadi atakapo acha kutenda maovu.

 

519.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili kutoka baba

yake Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. ambaye Amesema kuwa baba yake Al Imam Hussein ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema , Al-Kaf ,  J. 2, Uk. 641:

“Ewe mwanangu ! Jichunge na makundi matano na kamwe usifanye urafiki nao, wala usiongee nao na wala usifanye urafiki pamoja nao.

 

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alimuuliza baba yake

Je ni makundi gani hayo matano. Imam a.s. alimujibu:

 

Jitahadharishe na wala usifanye urafiki pamoja na yule msema uongo kwa sababu yeye ni kama mazua mazua anaye kufanyia vitu vya mbali vikawa karibu, na anakifanya kiwe mbali kile ambacho kiko karibu nawe.

 

Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na mtu ambaye hana tabia njema, kwa sababu atakuuza kwa thamani kwa tonge moja au hata chini ya hiyo.

 

Jihadhari na wala usifanye uhusiano na bahili kwa sababu yeye atakunyima kutoka mali yake pale wewe utakapo hitaji hasa.

 

Jihadhari na usifanye urafiki pamoja na mpumbavu, kwa sababu yeye atataka kukufaidisha wewe lakini kwa uhakika anakudhuru zaidi.

 

Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na yule ambaye hawajali ndugu na maJama’a zake, kwa sababu mimi nimemona mtu kama huyo akilaaniwa katika kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an Tukufu) katika sehemu tatu.

 

Nayo ni:

Sura Al Baqarah, 2, Ayah ya 27; 

Wanao vunja ahadi ya Allah  swt baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Allah  swt kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye Khasara.

 

Sura Al-Raa’d,  13, ayah ya 25

Na wale wano vunja ahadi ya Allah  swt baada ya kuzifunga, na wanakata aliy amrisha Allah  swt yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: Hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.

 

Sura Muh'ammad, 47, ayah 22

Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe Jama’a zenu ?

 

 

520.     Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Mustadrak-ul-

Wasa'il, J. 12, Uk. 197:

“Ewe Kumail ! sema kile kilichopo katika hali yoyote ile. Uwe marafiki pamoja na wacha Allah swt na jiepushe na watendao maovu, jiweke mbali na wanafiki na usiwe pamoja na wadanganyifu na wahalifu na wahaini.”


KUWAHUDUMIA WATU

 

521.     Amesema Mtume Muhammad  s.a.w.w. , Shahab-ul-

Akhbar, Uk. 194:

“Yeyote yule atakaye mpuuzia ndugu yake Muislam mwenzake matatizo na shida za dunia hizi, basi Allah swt atampunguzia shida na matatizo yake huko Akhera.”

 

522.     Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar

al-Anwaar, J. 7, Uk. 318:

“Kwa hakika, maombi ya shida za watu zinazokuijia wewe ni miongoni mwa neema na baraka za Allah swt juu yako.  Hivyo usisikitike kwa sababu ya neema na baraka hizi.”

 

523.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al-Anwaar,

 J. 74, Uk.166:

“Popote pale utakapoona ndugu yako Muislam ana shida, jaribu kuangalia kama utaweza kumusaidia. (Usimpuuze mpaka akutamkie shida zake.)”

 

524.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amenakili

kutoka mababu zake a.s. ambao wamemnakili Mtume Muhammad  s.a.w.w. akisema, Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 382:

“Yeyote yule anayemlisha muumin aliye na njaa akashiba basi Allah swt atamlisha mpaka ashibe kutoka matunda ya Jannah;

Na yeyote yule atakaye mvisha nguo yule aliye na shida za nguo, Allah swt atamvisha nguo zilizofumwa na za hariri, na

yeyote yule atakaye mumalizia kiu muumin basi Allah swt atamjaalia kinywaji kilichopigwa lakiri;

Na yeyote atakaye msaidia muumin kupunguza shida yake, basi Allah swt atamweka chini ya Arshi yake siku ya Qiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha Arshi yake.”

 

525.     Mtume Muhammad  s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 164:

“Watu wanamtegemea Allah swt kwa ajili ya riziki, kwa hiyo mpenzi miongoni mwa watu kwake Allah swt ni yule ambaye anawasaidia wale watu wanaomtegemea Allah swt na kuwafanya watu wa familia ya nyumbani wakawa na furaha.”

 

526.     Amesema Mtume Muhammad  s.a.w.w., Al-Kafi, J. 2, 

Uk. 199:

“Yeyote yule atakaye wasaidia Waislam ndugu zake wakati wa shida, Allah swt atamwondolea shida na matatizo sabini na tatu, moja ambayo ni ambayo iko humu duniani na sabini na mbili zingine zitakazo kuwa wakati wa shida kubwa, ambapo watu watakuwa mashughuli katika mambo yao ya binafsi (katika Akhera).”

 

 


KUTOA MIKOPO

 

527.     Amesema Mtume Muhammad  s.a.w.w., Bihar al-Anwaar,

J. 76, Uk. 369:

“Yeyote yule anayeijiwa na ndugu yake Muislam kwa ajili ya kukopa na kama yeye hampi mkopo, basi Allah swt atamharamishia kuingia Jannat siku ambayo waja mema watakuwa wakilipwa na kufidiwa.”

 

528.     Amesema Mtume Muhammad  s.a.w.w., Bihar al-Anwaar,

J. 76, Uk. 367:

“Yeyote yule anayetakiwa na ndugu yake Muislam kwa kukopeshwa na kama yeye hamkopeshi mkopo, Allah swt atamzuia kuingia Jannat siku ambayo waja wema watakuwa wakilipwa mema yao.”

 


KUWASAIDIA WENYE SHIDA

 

529.     Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w., Tuhaful-'Uqul, Uk.34:

“Waulizeni maswali walio elimika, muongee pamoja na wale wenye hekima, na mujihusishe pamoja na masikini.”

 

530.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Ghurar-ul-Hikam

J. 4, Uk. 190:

“Sababu mojawapo ya kuteketea na kupotea kwa mali na utajiri wa mtu ni kule kutowajali na kutowasaidia wale wenye shida.”

 

531.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al-Hayat, Volume

 2, Uk. 51:

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amemnakili Allah swt kwa kuameambiwa usiku wa Mi’raj: Ewe Ahamad! Mapenzi yangu ni kule kuwapenda masikini. Wafanye masikini wawe karibu nawe na uwaweke karibu nawe ili mimi niweze kukufikia wewe………..”

 

532.     Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. :

“Yeyote yule anayemmalizia muumin njaa yake kiasi kwamba akaridhika kikamilifu, basi hakuna binadamu yeyote miongoni mwetu au miongoni mwa Malaika wanaojua kiasi cha thawabu yake siku ya Qiyamah isipokuwa Allah swt mmiliki wa Malimwengu yote. Na aliongezea: Kumlisha Muislam aliye na njaa ni njia moja kubwa sana ya kuomba Tawba( usamehevu).”

 

 Baada ya hapo alisoma ayah ya Qur'an Tukufu Sura Al-Balad, 90,

 ayah 14 – 16.

Au kumlisha siku ya njaa

Yatima aliye Jama’a,

Au masikini aliye vumbini.

 


ZAWADI NA KUWAFURAHISHA MUUMIN

 

533.     Mtume Muhammad  s.a.w.w. Amesema, Al-Ithna-'Asheriyyah,

Uk. 223:

“Wakati sadaka inapotolewa na mtu kutoka mikononi mwake, basi hiyo sadaka inasema:

Mimi nilikuwa kitu cha kwisha, lakini wewe umenipa maisha;

Mimi nilikuwa sina thamani sasa wewe umenifanya niwe na thamani kubwa;

mimi nilikuwa ni adui nawe umenifanya mie kuwa rafiki;

Wewe ulikuwa daima ukinilinda na kunihifadhi lakini sasa mimi nitakulinda na kukuhifadhi hadi siku ya Qiyamah.”

 

534.     Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar,

J. 74 Uk. 314:

“Yeyote yule atakaye mfurahisha Muumin, basi kwa hakika kwanza kabisa amemfurahisha Allah swt, na pili amemfurahisha Mtume Muhammad s.a.w.w. na tatu ametufurahisha sisi Ahlul Bayt a.s. ”

 

535.     Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha

  Uk. 533, Msemo. 328:

“Allah swt ameweka mahitaji ya wale wasio na uwezo katika mali ya matajiri. Kwa hivyo atakapokuwa mtu asiye na uwezo akabakia katika hali ya njaa basi ni kwa sababu matajiri wamemnyima haki yake.”

 

536.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 75, Uk. 314:

“Kwa kiapo cha Allah swt ! Yeyote yule anayeizuia mali yake isiwasaidie Mumin wenye shida basi siku ya Qiyamah kamwe hawataonja chakula cha Jannat wala Kinywaji kilichopigwa Lakiri.”

 


SADAKA NA MISAADA

 

537.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa :

“Sadaka inalipia madeni na inaongezea katika barakah.”

 

538.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa :

“ Sadaka inamwepusha mtu na ajali mbaya.”

 

539.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Mtu yeyote yule aliye mja wa Allah swt akiwa Mumin akatoa Sadaka, basi Allah swt baada ya kifo chake huyo mtu huwaweka vyema na kuwasaidia wananyumba yake katika hali njema.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaendelea kusema :

“Faida ya kutoa Sadaka ni kwamba inamsaidia kulipia madeni na viile vile kuongezea katika baraka.”

 

540.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kusaidia na kutoa sadaka vyote hivyo vinaondoa umasikini na hurefusha umri wa mtu. Na yule anayetoa huweza kuepukana na aina sabini za ajali mbaya.

 

541. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika kuelezea tafsiri ya aya, ya Qur'an Tukufu, Sura Al-Layl, 92 , Ayah ya 5 na 6 :

Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali

Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu.

 

Ndipo amesema kuwa;

Allah swt ndivyo anavyo walipa wale watendao mema, kwa mema yao mara kumi, au hata mara laki moja na hata zaidi ya hapo.

 

Na vile vile amesema kuwa: anayetoa katika njia ya Allah swt basi Allah swt humjaalia kila aina ya tawfiqi katika kazi hiyo ya khairi.”

 

542. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Mtu yeyote yule ambaye anamwamimi Allah swt kuwa atamlipa na atamwongezea zaidi ya kile anacho kitoa basi huyo mtu kwa moyo mkunjufu na bila aina ya ubakhili wowote atatoa sadaka na misaada kwa wingi kabisa.”

 

543. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Siku ya Qiyama ardhi itakuwa imepata moto kupita kiasi na mumin watakuwa katika kivuli na kivuli hicho itakuwa ni kile alicho kuwa akitoa Sadaka.”

 

544. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema kuwa:

“Enyi watu! Toeni sadaka bila shaka sadaka inaongezea katika mali yenu, na hivyo mtoe sadaka na Allah swt atawarehemu.”

 

545.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema kuwa:

“ Toeni sadaka mjipatie riziki.”

 

546.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Toeni sadaka mjiongezee riziki yenu. Bila shaka anayeamini kuwa Allah swt hulipa mambo yote. Basi yeye huwapa sadaka masikini kwa kupita kiasi. Allah swt humjaalia riziki kwa njia mbalimbali kwa  kile huyu mtu akitoacho katika mali yake.”

 

 

547.  Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema kuwa :

“Kuwa na akida ya Tawhid ni nusu ya sehemu ya dini, enyi watu!  Toeni Sadaka ili mpate riziki zaidi”.

 

548. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.  ametoa riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa :

 “Kuwa mali halisi ya mtu ni ile ambayo yeye ametolea sadaka.”

 

549.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“Toeni Sadaka asubuhi na mapema ili balaa zisiwafikieni katika siku nzima.”

 

550. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa:

“Sadaka ni kinga dhidi ya moto wa Jahannam .”

 

551. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“ Enyi watu muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka.”

 

552. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika Nahjul Balagha amesema kuwa:

“Mnapoona riziki yenu inapungua na kuwa finyo basi muwe mkitoa sadaka ndivyo mtakuwa mkifanya biashara na Allah swt.”

 

553.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Imani ya muumini inakuwa na sifa nne za lazima,

·         Awe na tabia njema,

·         Awe mkarimu na mwepesi wa kutoa

·         Asizungumze zaidi ya yale yanayo takikana (hazungumzi mambo ovyo ovyo)

·         Hutumia kile kiasi kinacho takiwa ,siyo mfujaji ( anaotoa katika njia ya Allah swt ).

 

554.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini.”

 

555.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliijiwa na mtu mmoja

na aliyeuliza,

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi ninazo pesa na utajiri je ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru?”

 

 556.  Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim a.s.  alimjibu kuwa:

“Kuwa mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi.”

 

557.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Maimuna binti Harun, Je Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ‘Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi nimemfanya huru.’

 

 Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia “Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi.”

 

 

558.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini.”

 

559.  Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., naye akawaambia;

“Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa  siku dharura wake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya.”

 

 

560.  Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. aliulizwa na Sahaba mmoja  :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi watoto wangu wawili wamefariki na amebakia mtoto wangu mdogo.”

 

Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. kamwambia:

“Basi toa Sadaka kwa niaba ya mtoto wako huyo.”

 

 Na siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alipomtembelea huyo mtu akamwambia,

“Mwambie mtoto wako huyo atoe Sadaka kwa mkono wake walau kiasi kidogo chochote kile au hata kama kitakuwa ni kipande kidogo tu. Utambue wazi kuwa kiasi chochote kile hata kikiwa kiasi gani kama kitatolewa kwa roho safi  basi mbele ya Allah huwa ni kipenzi, kwani Allah swt ameelezea kuwa:

Qur’an Tukufu, Surah Az-Zilzalah,99, Ayah7 - 8

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona !

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona !

 

561. Vile viel Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alimwelezea kuwa:

“Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Balad,90, Ayah11 - 16

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani ?

Kumkomboa mtumwa;

Au kumlisha siku ya njaa

Yatima aliye jamaa,

Au masikini aliye vumbini

 

“Hivyo ewe Sahabi  uelewe kuwa Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa si watu wote wenye uwezo wa kuwanunua na wenye kufanya huru watumwa hivyo yeye ameweka thawabu hizo hizo kwa wale watakao toa Sadaka au watakao walisha yatima na masikini.”

 

562.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alijiwa mtu mmoja mbele yake na kuelezea habari za mtoto wake, na kwa hayo Al Imam akamjibu :

“Toa Sadaka kwa niaba yake.”

 

Na mtu huyo akajibu kuwa

“Sasa mtoto wake amekuwa na umri  yaani amekuwa kijana.”

 

Basi Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimwambia kuwa

“Mtoto wako atoe Sadaka kwa mkono wake, hata kama itakuwa ni kipande cha mkate, na hapo ndipo Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alisema riwayah ya Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. kuwa:

“Katika Israil alikuwa mtu mmoja aliyekuwa akimpenda mno mtoto wake, na akaona katika ndoto yake anaanmbiwa kuwa, mtoto wako huyo umpendaye mno atakufa usiku wa ndoa yake. Kulipowadia usiku wa arusi baba mzazi wa mtoto huyo, usiku kucha akawa katika wasiwasi na hakupata usingizi na kamwe hakupata raha usiku huo.

 

Na kulipo pambazuka asubuhi na mtoto alipotoka chumbani mwake akiwa hai basi baba yeke alimwuliza

 ‘Ewe mwanangu! Je katika usiku huu wako wa kuamukia leo umefanya mema yoyote?’

 

 Kwa  hayo mtoto akajibu

“Ewe baba yangu! hakuna jambo la maana sana lililotendeka, bali alitokezea masikini mmoja akaja mlangoni kuomba chakula, alikuwa na njaa na kile chakula walichokuwa wameniwekea, mimi nikampa chakula chote huyo mtu aliyekuja kuomba.’

 

 Kwa hayo baba yake akasema

“Kwa sababu hii tu ndiyo Allah swt amekuondoshea balaa kubwa iliyokuwa ikupate wewe usiku huo.”

 

563.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakwambia ‘ewe fulani!  Usitoe Sadaka kamwe.”

 

564.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua”.

 

565. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hadith zake amesema kuwa:

“Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afahali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji.”

 

566.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“Kuna aina tatu ya mikono wa

·         kwanza ni mkono ule wa Allah swt  ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt,

·         mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na

·         mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt  na musikalifishe nafisi zenu”.

 

567.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.  amesema kuwa:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amemfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema.

 

Ewe Allah swt umsaidie Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema: Ama kuhusiana na sadaka tafadhali usiwe na mnunguniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt.”

 

568. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa kuna riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Toeni Sadaka, angalau hata kwa sa’  ya tende, na kama sa’ moja hiyo hamnayo basi mtoe tende kwa kiganja kimoja na hata kama hivyo haitawezekana basi mtoe tende kiasi chochote kile na kama hivyo haitawezekana basi mtoe angalau kokwa moja ya tende, na kama hivyo pia haitawezekana basi yule masikini aliyekuja kuwaomba mumwambie maneno mazuri na matamu na maneno matakatifu katika kumwelezea kuwa hakuna chochote, na hayo pia ni sadaka.

 

Kwa sababu isitokee Siku ya Qiyama kwamba Allah swt atakapo kuuliza hesabu ya neema alizokujaalia akakuambia

‘Ewe mja! Mimi nilikupa mambo chungu nzima, sasa hebu angalia nafsini mwako je kwa kutumia neema hizo wewe umejiandalia nini?’

 

Na hapo wewe utaangalia sehemu zote nne za dunia na utajawa na masikitiko, na utakuta hakuna jambo lolote lile litakalo kuokoa dhidi ya adhabu za Allah swt.”

 

569.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Mtoe tende kiasi fulani kwani itawaokoa na moto wa Jahannam , mpanue riziki zenu na mteremshiwe riziki nyingi kwa kutoa Sadaka na kupitia dua mziondoe balaa na shida zenu.”

 

Mkumbuke kuwa kwa kutoa Sadaka hamtapungukiwa katika mali yenu. Na miongoni mwa jamaa zenu wanapokuwa na shida muwasaidiapo hiyo siyo Sadaka bali hiyo ni wajibu wenu.”

 

570.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Kulikuwa na mja mmoja aliyekuwa akifanya ibada ya Allah swt kwa umri wake wa miaka  themanini.

 

Siku moja alimwona mwanamuke mmoja mzuri aliyekuwa akipendeza naye akawa ameingia katika mtego wake.  Yeye alitimiza matamanio yake visivyo halali na mara akatokezea Malakul mauti (malaika anayetoa roho). Ulimi wake ulifunga kuongea na jasho lilianza kumtoka na kutokwa kwa roho na mara hapo alipita masikini akiomba.

 

Basi mtu huyu ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho alimwambia yule masikini kwa ishara kuwa mahala fulani kuna mkate hivyo auchukue hivyo aweze kula huyo masikini, na masikini huyo alivyoelekezwa akauchukua mkate akaondoka zake.

 

Kwa hiyo ikatokea kwamba Allah swt aliibatilisha ibada zake za miaka themanini kwa sababu ya kuzini na ikatokea kwamba Allah swt akamsamehe madhambi yake yote kwa sababu ya kutoa Sadaka kwa moyo mkunjufu.”

 

571.  Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.  amesema kuwa;

“ Katika zama za Bani Israil kuliwahi kutokea baa la njaa ambao uliendelea kwa muda wa miaka mingi. 

 

Katika wakati huo ikatokezea kwamba bibi kizee mmoja akiwa amekabwa na njaa hali ya juu alikuwa ameketi akiwa na kipande kidogo cha mkate huku akitaka kukila kipande hicho, mara akasikia mlangoni sauti ikisema ya masikini aliyekuwa amekuja kuomba:

‘Ewe mja wa Allah swt! Mimi nakufa kwa njaa naomba unisaidie, bibi kizee huyo akajiambia kwa hakika Sadaka ndiyo wakati huu muafaka wa kutoa, na kile alichokuwa akila akakitoa haraka akampa huyo aliyekuwa akiomba.

 

Bibi kizee huyo alikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa amekwenda porini na ghafla kule alishambuliwa na mnyama. Kwa kusikia sauti ya mtoto wake huyo bibi kizee ikimwita, alikimbia kumfukuza mnyama huyo na kwa muujiza wa Allah swt  ni kwamba,  Allah swt alimtuma Malaika Jibrail a.s kwenda kumwokoa mtoto huyo katika mdomo na mabano ya mnyama wa huyo muuwaji, na Malaika Jibraili a.s. akamwambia ‘Ewe bibi kizee ! Je umefurahi sasa? Kwa kile ulichokitoa sadaka basi Allah swt naye amekulipa mema yake.”

 

572.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“ Mfanye mema katika hali ya shida na ufakiri, na wema huo ni Sadaka.

 

Toeni Sadaka kama itakuwa ni kiasi gani kwa udogo wake. Mnaweza kutoa kiasi cha tende mkajiokoa na  Jahannam. Kwa hakika udogo huo siyo hoja na Allah swt ataulea udogo huo kama kwamba nyie mnavyo walea watoto wadogo wanaonyonya maziwa, na siku ya Qiyama wakati mema yenu hayo  ( mliyokuwa mkisema ni madogo) yatakapoletwa mbele yenu mtaona kuwa ni sawasawa na ukubwa wa milima mikubwa sana.”

 

573. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameseama kuwa Allah swt anasema kuwa :

“Hakuna kitu kingine mbali na Sadaka ambacho mtu anaweza kumpatia mtu mwingine kidhahiri, na kwa hakika mimi ndiye wakili wake musitahiki, na mimi ninayepokea kwa mikono Sadaka hiyo halafu hata ikiwa kama ni tende kidogo haidhuru mimi ndiye ninaitunza, kama vile mwanadamu anavyowatunza watoto wake.

 

Siku ya Qiyama huyo mtoa Sadaka atastaajabishwa mno kwa Sadaka zake ndogo alizokuwa akitoa zimekuwa kubwa kama milima ya Uhud, milima mikubwa sana.”

 

574. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa: 

“Toeni Sadaka asubuhi na mapema kwa sababu kunaondoa balaa kwa siku nzima.”

 

575.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka asubuhi na mapema basi mtoa Sadaka huepukana na kila aina ya matatizo na mabaya yote kwa siku nzima.”

 

576.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Toeni Sadaka asubuhi, na kwa mapenzi kabisa, mwenyewe kutoa Sadaka amebahatika. Basi humwomba Allah swt amani kutokana na balaa zote zilizoko ardhini na mbinguni, na kwa hakika Allah swt humjaalia hivyo kwa sababu ya kutoa Sadaka.” 

 

577. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaelezea kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa:

“Ewe Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.! Sadaka huondoa balaa ambazo lazima zitatokezea, na kwa kutenda mema pamoja na ndugu na majamaa kunarefusha umri.

 

Ya Ali! Iwapo jamaa na ndugu ni watu wenye shida, basi kuwapa Sadaka  hao haitakuwa ni Sadaka.

 

Ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.! Kusema maneno bila vitendo ni ya bure hayana maana, na Sadaka  bila kuwa na nia nayo haiwi Sadaka.”

 

578. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa: Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza mtu mmoja

“Je leo umefunga Saumu?”

 

Mtu huyo alijibu

“La hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

 

 Tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:

“Je leo umeshawahi kumtembelea aliye mgonjwa?”

 

 Naye akajibu:

“Hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  aliendelea kumwuliza naye aliendelea kumjibu hapana hakufanya hivyo.

 

579. Mwishoni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliendelea kumwuliza:

“Je umemlisha masikini yeyote?”

 

 Naye akajibu: “Hapana Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.!” 

 

Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwambia huyo mtu :

“Nenda kwa wananyumba wako, nenda ukawatendee  na uwe nao kwa  mema na uwawie wema, basi hayo ndiyo yatakuwa Sadaka  yako kwao.”

 

 

580.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye ameseama:

“kwa baraka za Sadaka Allah swt humwondolea mwenye kutoa Sadaka balaa sabini, ambamo kuna magonjwa, madhara yatokanayo na moto, kuzama maji, kufunikwa na majumba mpaka kufa na atamwepusha ili asiwehuke au asiwe mwehu.”

 

581.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa: 

“Ili kutaka kuepukana na shari za madhalimu basi toeni Sadaka.”

 

582.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaelezea kuwa: Siku moja Myaudi mmoja likuwa akienda kukata miti porini na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwangalia na kuwaambia Ma-Sahaba wake :

 “Myahudi huyu leo ataumwa na nyoka na kifo chake kitasababishwa na sumu ya nyoka. Myahudi huyo kama kawaida yake alikata kuni na alijitwisha kichwani mwake na akarud akiwa salama.

 

Na tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwona Myahudi huyo akamwambia ateremshe mzigo wa kuni huo na auweke chini. Na Myahudi akafanya hivyo alivyoambiwa, na katika mzigo huo wa kuni wakaona kuna nyoka mweusi mwenye sumu kali sana huku akiuma kuni.

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Myahudi yule,’Je wewe leo umefanya jambo gani?’

 

 Myaudi huyo akasema: Mimi nimekata kuni na kuzifunga tu, lakini wakati nilivyokuwa nikirudi nilibakiwa na vipande viwili vya mkate na kipande kimoja mimi nikala na kipande kimoja nikampa masikini Sadaka.

 

 Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema kwa kiapo cha Allah swt ni kwa sababu ya Sadaka  ndiko balaa hii imekuondokea, kwa hakika Sadaka humwepusha mtu na ajali mbaya.”

 

583.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alikuwa pamoja na Ma-sahaba wake katika Masjid Nabawi, na upande mmoja wa ukuta ukaanguka chini. Kulikuwa na mtu mmoja hapo ambaye aliponea chupu chupu tu, kulianguka kizingiti kizito karibu na muguu wake. Lakini yeye bahati nzuri hakupata udhuru wowote.

 

Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliwaambia Ma-sahaba wake, hebu mwulizeni huyu mtu leo amefanya matendo gani? Na wakati alipoulizwa huyo mtu akasema:

 

“Mimi nilipotoka nyumbani mwangu leo nilikuwa na kokwa chache za  tende. Na kukatokezea na masikini mmoja akaniomba basi mimi nikampa kama Sadaka .

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akajibu

“Basi kwa sababu hiyo tu leo, Allah swt amekuepusha na balaa hii ambayo ingekumaliza.”

 

584. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. siku mmoja alimwambia Sahabi wake 

    Mayassari kuwa:

“Ewe Mayassari je wajua kuwa wewe umeisha fikiwa na mauti mara nyingi, lakini Allah swt amekuongezea umri wako zaidi kwa sababu ya wewe kuwa mkarimu na kuwajali jamaa na ndugu zako umewawia wema ndio maanake umri wako umezidi.”

 

 

585.  Al Imam Hasan al-'Askary a.s. anasema kuwa:

“ Wakati mmoja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akiwa pamoja na wenzake walikuwa safari na wenzake hao walikuwa na mali nyingi sana. Na njiani wakapata habari kuwa wako majambazi wanaowapora matajiri mali zao. Kwa kusikia hayo hao matajiri walianza kutetemeka na wakaingiwa na hofu na wakaanza kumwuuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. je tufanyeje sasa?

 

Na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawajibu:

‘Mkabidhini mali yenu yule ambaye ataweza kuifadhi mali yenu, na kwa kweli ataitunza sana na baada la kupungua hata itazidi pia, sio hayo tu na pale mutakapokuingiwa na shida ya mali yenu basi yeye kila siku atawarudishia pamoja na nyongeza yake. ‘

 

Kwa kusikia hayo hao wenzake aliokuwa nao katika safari wakamwuliza :

“Je ni nani huyo?”

 

 Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawajibu:

“Yeye ni miliki wa malimwengu zote Allah swt.”

 

 Basi hao wenzake wakamwuliza je tunaweza kumkabidhi vipi mali zetu hizi? Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawaambia: Toeni Sadaka  muwape wale wanaostahiki. Kwa kusikia hayo wakauliza ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Hapa tulipo tutawatoa wapi hawa masikini na mafakiri tutawatafuta wapi? Basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliwajibu: munuie kuwa  sehemu moja ya mali yenu mtatoa Sadaka basi na msiwe na wasiwasi Allah swt atailinda mali yenu yote.

 

 

“Wale waliokuwa naye pamoja safarini walinuia hivyo kama vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alivyowaambi,a na Imam a.s. akawaambia sasa nyie mko katika amani ya Allah swt, na wakiwa wanaendelea na safari majambazi hao walikumbana nao na kwa kudura za Allah swt wao wakawapita salama usalimini bila ya kudhurika na kusumbuliwa, hadi wakafika mwisho wa safari yao.

 

Waliopofika tu mwisho wa safari yao wao wakatoa sehemu moja walizokuwa wamenuia kama Sadaka na sehemu iliyo bakia walifanyia biashara yao, na Allah swt akawajaalia baraka kiasi kwamba wakapata faida hata zaidi ya mara kumi.” 

 

 

586.  Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa Mina pamoja na Ma-sahaba wake wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na  akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema “mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue”.

 

Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia “Allah swt atakuzidishia” na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na akamwambia Imam a.s. “Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa.” Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam a.s. hakumpa chochote.

 

Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukurani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: ‘Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. ‘Ewe Aba ‘Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri. Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-sahaba wakamwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam a.s. lazima angeendelea kumpa chochote zaidi ya hayo.”

 

587.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“ Mimi nilinunua ardhi pamoja na mtu mmoja. Mtu huyo huyo alikuwa ni mnujumi, kwa hiyo yeye kila alipokuwa akipiga mahesabu yake na elimu ya nyota yake aliyokuwa nayo alikuwa akiangalia saa nzuri ndipo alipokuwa akienda shambani mwake, nami bila kujali kama saa mbaya nilikuwa nikienda shambani mwangu, na sisi tulipokuwa tayari basi ardhi au sehemu yangu ikawa na faida zaidi kuliko sehemu yake.

 

Kwa hivyo yeye bila kusita katika  hali ya kustaajabisha aliniambia mimi sijawahi kuona kama hivi. Mimi kila saa zilizokuwa nzuri nilikuwa nikija shambani mwangu. Na wewe bila kujali saa nzuri au mbaya ulikuwa ukija kwenye shamba lako. Sasa itakuwaje mimi nipate hasara au kasoro?

 

 Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu ngoja nikwambie hadithi moja ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyesema kuwa:

‘Mtu yeyote anayetaka Allah swt amwepushe na maovu na mabaya ya siku nzima basi yeye aianze siku yake kwa kutoa Sadaka, na yeyote anayetaka ajiepushe na balaa na maovu ya usiku basi yeye usiku unapoingia atoe Sadaka na ujue kwamba mimi daima ninapotoka nyumbani mwangu huwa ninatoa Sadaka. Kwa hivyo kufanya biashara na Allah swt hivi afadhali zaidi kuliko elimu yako ya nyota na kupiga ramli.”

 

588.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Mtoe Sadaka  usiku kwa sababu huiondoa ghadhabu ya Allah swt, husamehe madhambi mazito, na hukusababishia hesabu zako siku ya Qiyamah zikaenda vizuri. Kutoa Sadaka  katika siku kunaiongezea mali yako na kuilinda na kunaufanya umri wako uwe mrefu.”

 

589.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Kwa kutoa Sadaka  yaani kunapokucha kunayeyusha madhambi kama vile chumvi inavyoyeyuka katika maji. Na kunapotolewa Sadaka usiku basi kunaondoa ghadhabu za Allah swt.”

 

590. Ibn ‘Abbas amesema kuwa: Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Sura Al-Baqarah,2, Ayah 274  

Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika

 

“Aya hiyo imeteremshwa makhsusi kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa sababu yeye alikuwa anazo Dinar chache ambazo wakati wa usiku yaani baadhi ya Dinar hizo wakati wa usiku na baadhi wakati wa mchana na zinginezo katika hali ya siri na zinginezo zikiwa ni dhahiri alizokuwa akitoa Sadaka katika njia ya Allah swt.”

 

591. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka  kifichoficho ghadhabu za Allah swt hupoa.” 

 

592.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Sadaka inayotolewa kidhahiri basi kuliko hiyo Sadaka  inayotolewa kifichoficho ni afadhali zaidi.”

 

593.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alisema kuwa:

“Mambo yanayomfikisha mtu moja kwa moja kwa Allah swt kama kipitio au (Wasila) ni imani. Na baada yake ni kuwatendea mema ndugu na majamaa zake mtu, ambaye inaongezea baraka katika mali yake na umri wake ukawa  mrefu na Sadaka inayotolewa kifichoficho inamfanya huyo mtu asamehewe madhambi yake, na madhambi aliyokuwa yamemgadhabisha  Allah swt kwa sababu ya kutomtii, yanabadilishwa kuwa mema na baadaye ni tabia njema na uwema, mambo ambayo yanaepusha ajali mbaya na inamfanya huru mtu katika makucha ya udhalilisho.”

 

594.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka  kidhahiri kunaondoa aina sabini za balaa lakini kwa kutoa Sadaka  kifichoficho kunamfanya mtu anusurike  na ghadhabu za Allah swt.”

 

595.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.   amesema kuwa:

“Baba yake Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. kila siku usiku alikuwa akitoka nyumbani pamoja na kifurushi cha fedha mgongoni mwake na mara nyingine alikuwa akichukua kufurushi cha vyakula na alikuwa akiwaendea wale wenye shida na dhiki.

 

Wakati akiwapelekea misaada hii majumbani mwao Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akiufunika uso wake ili wasiweze kumtambua ni nani huyu anayewafikishia misaada mpaka majumbani mwao.

 

Wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipofariki ndipo hapo ikajulikana hawa wanaosaidiwa wenye shida hawapati misaada waliyokuwa wakipata, ndipo hapo wakajua kuwa aliyekuwa anawasaidia mpaka milangoni mwao alikuwa si mtu mwingine bali ni Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s . vile vile wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipolazwa wakati wa kuoshwa baada ya kufariki kulionekana mabegani mwake na mgongoni mwake alama zilikuwa zikionyesha kuwa alikuwa akibeba mizigo mizito kwa muda mrefu.

 

Na katika kipindi kimoja cha baridi kali sana yeye alikuwa amejifunika nguo ambayo ilikuwa inamsaidia asiisikie makali ya baridi wakati alikuwa ametoka nje ya nyumba anakwenda mahala fulani. Njiani alikutana na mtu ambaye alimwomba nguo hiyo ili naye aweze kujistiri na kujizuia dhidi ya makali ya baridi iliyokuwapo. Kwa maombi hayo Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. alimpa hiyo nguo naye akabaki bila nguo ya kujifunika au  kujuzuia na baridi.  Vile vile Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa kila mwaka akijifunika nguo ya kujizuia baridi na kipindi kilipokwisha alikuwa akiiuza na fedha zake zote zilizokuwa zikipatikana alikuwa akitumia katika kuwasaidia wenye kuhitaji misaada.”

 

596.  Vile vile Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alisema kuwa:

“Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  alikuwa akiwasaidia na kuwalisha na kuwatunza familia zaidi ya mia moja katika mji wa Madina. Na alipokuwa akikaa kula mayatima, wazee, wagonjwa na masikini walikuwa wakikaa kula naye pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., na vile vile alikuwa akiwafungia vyakula kwa ajili ya kuwachukulia wale waliokuwa majumbani mwao au kama baba ni mzee alikuja kula huko basi alifungiwa chakula awapelekee mke na watoto zake nyumbani.

 

Vile vile yeye yasemekana kuwa  alikuwa hakai kula pamoja na mama yake juu ya meza moja ya chakula na watu walipomwambia ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wewe ni kigezo cha tabia njema na mfano bora katika Waislamu! Je kwanini hukai pamoja na  mama yako katika kula chakula?.

 

Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s.  aliwajibu kuwa

“Mimi sikai na mama yangu kwa sababu yawezekana mama yangu akiangalia chakula moja labda akataka kuchukua na wakati huo mkono wangu ukawa mrefu kwenda kuchukua chakula hiki itakuwa kweli hiyo ni kitovu cha nidhamu na ndivyo maana yake ninajiepusha kukosa nidhamu mbele ya mama yangu.”

 

597.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Mtu anapotoa Sadaka  ya chakula kwa ajili ya kuwapa masikini na mafakiri basi mujue kuwa aina hiyo ya Sadaka  huondoa ufakiri na humwepusha mtu na kumuondolea ufakiri, na kuurefusha umri wake na humwepusha na aina sabini za vifo vya kutisha (ajali mbalimbali).”

 

598.  Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku ya Qiyamah wakati kutakuwa na jua kali lichomalo basi watu aina saba watakuwa wamepewa kivuli na Allah swt na mmoja wao ni yule anayetoa Sadaka ya vyakula kiasi kwamba mkono wa kushoto haupati habari kuwa mkono wa kulia umetoa Sadaka.”

 

599.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Enyi Waislamu! Je niwaambieni mambo matano ambayo kwa hakika ni mema, maneno hayo yanawapelekeni hadi Jannat.?  

 

Ma-Sahabah wakajibu

“Naam lazima tuambie ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Naomba utuongoze.”

 

600.  Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. akasema:

“Mnapopatwa na misiba basi lazima ufanye subira na mujaribu kuficha, mutoe Sadaka kiasi kwamba mkono wa kulia unapotoa mkono wa kushoto usipate habari, muwatende mema wazazi wenu, na kwa hakika katika mambo hayo ndiyo kuna furaha ya Allah swt na kila mara mwezavyo kusema semeni La Haula wala Quwwata illa billahil ‘Aliyil ‘Adhiim  kwa hakika hiyo ni  hazina moja kubwa katika hazina za Jannat, na vile vile katika nyoyo zenu muwe na mapenzi ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahlul Bayt a.s.

 

601.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. daima ilikuwa akitoka usiku katika kiza huku amejitwisha mafurushi ya mapesa na vyakula kwa ajili ya kwenda kugawa kwa masikini katika mji wa Madina, alikuwa akiwafikishia misaada waitaji walipokuwa. Na siku ambayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliaga dunia, watu wakaona misaada imesimama na watu hawakufikiwa na misaada hiyo ndipo walipokuja kujua kuwa misaada hiyo ilikuwa ikiletwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye daima alikuwa akificha uso wake ili watu wasijue kuwa ni yeye anayewafikishia misaada hiyo.

 

602.  Mu’alla ibn Khuns anasema kuwa:

“Usiku mmoja kulikuwa kukinyesha manyunyu ya mvua, nikamwona Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akielekea katika makazi ya Banu Sai’d nami nikajaribu kumfuata nyuma kisirisiri na mara nikasikia katika giza kizito hicho kama kitu kimedondoka na nikamsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

‘Ya Allah swt! Ninaomba vitu hivi nivipate tena.’

 

Na hapo mimi nikatokezea karibu ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.,  nikatoa salamu. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. baada ya kuitikia salamu akaniambea je wewe ni Mua’alla ?

 

Nami nikamjibu :

‘Ndiyo ewe Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ! Niwe fidia juu yako.

 

Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaniambia:

‘Naomba uniokotee vitu hapo chini unisaidie.”

 

 Mu’alla anasema mimi katika giza kizito hicho nikaanza kupapasa aridhini na nikakuta kumbe ni vipande vya mikate na wakati ninamkabidhi Imam a.s mikate  nilivyo viokota katika giza  kali nilihisi kifurushi alichokuwa nacho migongoni mwake kilikuwa kizito mno na hivyo nilimwomba Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Lakini hakukubali  nimsaidie kubeba kifurushi hicho.”

 

Lakini Imam a.s alikataa akaniambia

“Ninapendelea kuubeba uzito huu mimi mwenyewe kwa sababu huu ndiyo utakao kuwa ufanisi wangu katika siku ya Qiyamah na bora kwangu na hivyo unaweza kuja nami katika safari hii.”

 

Tulipokaribia katika makazi ya Banu Sa’id, Imam a.s. alikwenda kwa kila mmoja ambaye ni mwenye shida akamwekea mikate miwili na akarudi. Na wakati huo akaniambia kwa kutoa Sadaka usiku kunatuliza ghadhabu za Allah swt, na Allah swt usamehe madhambi makubwa, na kusahilisha hesabu katika siku ya Qiyamah.”

 

603.  Zuhri anasema kuwa: 

“Siku moja wakati wa baridi kali mno na ukungu ulikuwa umejaa mwingi mno mimi nilimwona Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. akiwa amejitwisha kifurushi kikubwa cha chakula na mzigo mkubwa wa kuni.

 

Nami sikusita nikamwambia ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je nini haya?’

 

Imam a.s akanijibu nina nia mpango wa safari, na hivyo ndivyo ninavyojitayarisha kwa ajili ya mahitaji yangu.

 

 Zuhri akasema:

‘Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi nakupa mfanyakazi wangu ambaye atakusaidia kukubebea mizigo yako hiyo mizito.”

 

Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. alimkatalia nami nikamwambia,

“Basi nipe mimi mwenyewe nikupunguzie kukusaidia kukupunguzia huu mizigo. Kwa hayo Imam a.s. akajibu, lakini kwa kufanya hivyo mimi sitakuwa nimetoka katika wajibu wa kufika mwisho wa safari yangu vile inipasavyo kufika, kwa hiyo naomba uendelea na shughuli zako uniache peke yangu.”

 

Zuhri anasema:

“Baada ya kufika siku chache mimi nilipomwona Imam a.s nikamwambia,

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi sioni kama wewe ulikwenda safari yoyote ile.”

 

Imam a.s akamjibu:

“Naam ! Vile uchukuliavyo sivyo. Muradi wangu ulikuwa ni safari ya Aakhera. Mimi nilikuwa nikijitayarisha kwa ajili ya safari ya Mauti. Kumbuka kwamba kujikumbusha na kujitayarisha kwa mauti basi mambo mawili ni muhim, kwanza kujiepusha na yaliyo haramishwa na pili ni kutoa muhanga wa mali katika njia ya Allah swt.”

 

604.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika baadhi ya misemo yake

    anasema.:

·         “Toeni Sadaka  kwa basabu kunatuliza ghadhabu za Allah swt

·         Toeni Sadaka  katika njia ya Allah swt mngejariwa kwa sababu ya riziki muliyojaaliwa na Allah swt kwa kufanya hivyo nyinyi mtahesabiwa katka wale wanaopigana katika njia ya Allah swt.

·         Yeyote yule ambaye ana imani kamili kuwa Allah swt hulipiza kile kinachopendwa na Mumin basi huyo mtu lazima ataitia  nafsi yake katika shida na kwa kufanya mema.

·         Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka .

·         Muilinde na  muihifadhi na kulinda mali yenu kwa kutao zaka[55].  

·         Urekebishe matumizi na mahitaji ya maisha yenu ili mweze kupima vyema.

·         Kuwaza na mawazo ni nusu ya uzee unaoletwa nawe.

·         Mwenye matumizi yenye mahesabu yaani anayebana matumizi kamwe hawezi kuwa mwenye shida na dhiki.

·         Kumsaidia yule ni mtu ambaye anaheshima na mkuu na kumsaidia yule ambaye ana madeni haya maneno mawili hayana kifani yoyote.

·         Kila jambo lina mazao yake, kwa hiyo mazao ya mema  na  kuwa na nia  katika  kutumia mali au chochote katika njia ya Allah na kwa ajili ya Allah swt basi mazao yake ni kwamba kufanya haraka kutekeleza azma hiyo na kamwe usifanye kucheleweshwa.

·         Muongezee na mupanue riziki yenu kwa kutoa Sadaka, kabla hamjaijiwa na balaa, mwombe dua na kwa hakika mtaweza kujiepusha  nayo na  kujiokoa nayo.

 

605.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kutoa Sadaka  siku ya Ijumaa kuna thawabu na  fadhila kubwa sana.”

 

606.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Msimkatalie masikini anayeomba siku ya ‘Arafah. Lazima mpeni chochote kile.”

 

607.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mtu yeyote atakaye kuwa ametoa Sadaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, basi yeye atakuwa ameepukana na balaa za aina sabini.”

 

608. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa ameulizwa na mmoja

    wa Ma-Sahaba wake,

“Ewe Mtume wa Allah swt! Ni Sadaka  ipo iliyo bora kabisa  kuliko zote!”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu,

“Sadaka  iliyo bora ni ile ya wakati ule ambapo mtoa Sadaka  yuko salama u salimini, mwenye afya kamili na anayeishi maisha mema bila wasiwasi, na ambaye anauogopa umasikini.

 

Na wala msicheleweshe kiasi kwamba mpaka kwamba mwisho wa maisha yenu yameisha wafikia shingoni, na hapo ndiyo mnaanza kutoa usia kuwa kiasi fulani mpe masikini fulani na fulani mpe kiasi fulani na kadhalika. Kama tunaelewa kuwa mtu fulani kweli ni mstahiki wa msaada au Sadaka sasa kwa nini tusubiri mapaka sisi tunataka kufa ndiyo basi tuseme msaidieni wakati shida alikuwa nayo tangu hapo zamani?”

 

609.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliombwa na mtu mmoja kuwa

     ampatie nasiha, na hivyo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia:

“Tayarisha matayarisho yako ya safari, na matayarisho yako hayo yatume kabla wewe hujaenda safari. Jifanyie matendo yako mwenyewe yaani kama unataka kufanya mema uyatende mema kabisa katika uhai wako na mambo yoyote yale ambayo  unayoona yanafaida kwako uyatende wewe mwenyewe na wala usiwatupie wengine kama unaweza kujitimizia wewe mwenyewe.[56]

 

610.  Kwa kuzungumzia swala tulilozungumziwa hapo No. 2  hapo juu

siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amekwenda katika ghala la mtu mmoja ambaye alikuwa amefanya usia kuwa baada ya kifo chake maghala yake yote yaliyokuwa yamejaa kwa tende yagawiwe Sadaka  kwa masikini. Na baada ya kifo chache ikatekelezwa usia wake na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokwenda kule baada ya kufagia akakuta kokwa moja ya tende imebakia mguuni mwake basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akainama akalichukua kokwa hilo la tende moja  akasema:

“Kama mtu huyu katika uhai wake angelikuwa amegawa kokwa hii moja ya tende basi angepata thawabu zaidi  kuliko hata  mlima mkubwa kabisa wa Uhud.”

 

611.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka kwa

mababu zake a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa   akisema:

“Pale anapokuja mtu yeyote usiku kugonga mlango kwa nia ya kuomba msaada, basi msimvunje moyo, msaidieni na hasa inapokuwa mwombaji aliyekuja ni mwanaume.”

 

612.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Allah swt kwa kila kazi amemweka mweka-hazina ambaye anaweka mahesabu yake isipokuwa Sadaka, ambaye mahesabu yake na utunzaji wake anaweka Allah swt mwenyewe. Baba yangu mzazi wakati alipokuwa akimpa chochote mwombaji alikuwa akikichukua tena na alikuwa akiubusu mkono wa  huyo mwombaji, na alikuwa akiunusa kwa hamu sana, na ndipo baadaye alipokuwa akimrudishia na kumpa kitu hicho hicho.”

 

613.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Allah swt amesema  kuwa mimi nimewateua mawakili kwa kila jambo na ambao ndio wanaosimamia na kuweka ripoti zake isipokuwa Sadaka ambayo mimi mwenyewe ndiye ninayetunza habari zake.”

 

614.  Mu’alla bin Khunais amesema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

alikwenda katika makazi ya Banu Sa’id na wale wote waliokuwa na shida aliwawekea mikate na kuondoka zake. Hapo mimi nilimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.:

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je hawa watu ni marafiki na wafuasi wenu?”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :

“La! Hawa kama wangekuwa marafiki na wapenzi wetu na wafuasi wetu basi ningewaongezea kiasi cha punje ya chumvi”. [57]

 

Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliponielezea kwa uwazi zaidi kwamba siku moja Mtume ‘Isa bin Maryam a.s. alikuwa akipita ufuoni mwa bahari, na akatoa mkate kidogo kutoka kifurushi chake akatupa baharini. Baadhi ya wale aliokuwa nao wakamwuliza!

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je umefanya nini bwana? Nini maana ya kutupa mikate baharini?

 

Mtume Isa a.s akawajibu:

“Katika bahari kuna viumbe vya Allah swt na iwapo kutatokezea na viumbe vyovyote vitakavyo kula humo kutokana na nilichowatupia basi kwa hakika katika ufalme wa Allah swt nitakuwa na thawabu nyingi mno.”

 

615.  Al Imam Muhammad al-Baqir a.s.  amesema:

“Pozeni nyoyo zenu kwa sababu ya kiu kali kwani Allah swt hupendezewa sana na tendo hilo. Kwa hakika amebahatika yule mtu ambaye anawamalizia kiu wanyama kwani yeye siku ya Qiyamah  atapata msaada mkubwa sana atakapokuwa katika hali ya kiu.”

 

616.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa akifunga safari baina ya

Makkah na Madina, akaona kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyejitupa chini ya mti mmoja. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwamwambia mtu mmoja aliyekuwa naye, aende akamwulize hali yake, inawezekana labda alikuwa na kiu kali. Mtu huyo alipomwendea huyo mtu aliyekuwa amelala chini ya mti na kumwuliza hali yake basi ikajulikana kuwa mtu huyo alikuwa na kiu ya maji. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimnywesha maji na akaondoka  kuendelea na safari yao. Yule aliyekuwa naye safarini akasema,

“Ewe  mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. !  Huyu mtu alikuwa ni Mnasara, watu kama hawa pia tunaweza kuwasaidia na kuwapa Sadaka?”

 

 Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu

“Naam ! Katika mazingira kama haya inawezekana.”

 

617. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.

alikuwa pamoja na wafuasi wake nao katika safari, na waliketi kwa ajili ya kula chakula. Na akatokezea swala mmoja ambaye alikuwa akitafuta chakula, Imam a.s. akamwambia huyo

‘Swala njoo karibu, njoo ule nasi! Usiwe na wasiwasi utulie na ujue hapa kwetu hautakuwa na hofu yoyote, upo katika usalama.”

 

Kwa kusikia hayo Swala huyo alimsogelea Imam a.s. na alikula pamoja nao.

 

618. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa Siku moja baba yake alikuwa pamoja na wenzake katika bustani yake na walipoketi  kula  chakula na  mara akatokezea Swala mmoja aliyekaribia.

 

Hapo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. . ambaye ni baba yake na  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. akasema:

“Ewe Swala, jina langu mimi ni Al Imam Zaynul 'Aabediin bin Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na mama yangu Bi Fatima az-Zahra a.s., njoo ushiriki nasi katika kula. Na Allah swt kiasi alichokuwa amemjaalia cha chakula  huyo Swala alikula.”

 

619.  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“Hakuna mtu yeyote mwingine isipokuwa ni Mwislamu tu anayeweza kuchinja wanyama wenu wa dhabihu siku ya Iddi na  Sadaka, na unapotoa Sadaka  katika kutoa humo lazima wapewe Waislamu tu. Na unapotoa Sadaka  katika mali zinginezo unaweza kuwapa Kafir Zimmi  ambao wenye kuhitaji misaada hiyo.”

 

620.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah moja kutoka

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtu mmoja alimwuliza Mutume s.a.w.w. :

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Je ni Sadaka  ipi iliyo bora kabisa?”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:

“Sadaka  ile ambayo watakayo pewa wale jamaa na ndugu ambao hata kama alikuwa amekorofishana nao au amegombana nao au hawana uhusiano nao kwa sababu ya magomvi.”

 

621.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Iwapo wewe unatoa kumi kwa ajili ya Sadaka , basi ili kuwasaidia Mumin toa kumi na nane na yule ambaye hawezi kabisa msaidie kwa ishiririni na kwa ajili ya kuwasaidia jamaaa na ndugu kwa wema  utoe ishirini na nne.”

 

622.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema Riwayah kutokea

 kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kuwa amesema:

“Mtu yeyote atakaye wasaidia jamaa na ndugu zake katika kwenda Kuhijji au ‘Umra, basi Mtume Allah swt atamjaalia thawbu za Hijja mbili na ‘Umra mbili, na yoyote yule atakayemsaidia ndugu yake Mumin basi Allah swt atamlipa kusiko na kifani.”

 

623.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameseama kuwa:

“Iwapo mtu atawasaidia jamaa au ndugu zake ambao wana shida ni muhtaji basi hiyo siyo Sadaka.”

 

624.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah moja ya Mtume

Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema:

“Kwa mtu yeyote yule ambaye atakwenda mwenyewe kwenda kumsaidia jamaa au ndugu yake mwenye shida na kutoa kitu chochote kwenye mali yake na kumsaidia  basi Allah swt atamjaalia ujira wa mashahidi mia moja na kwa kila hatua atakayotembea atamwandikia mema elfu arobaini,  na kiasi hicho hicho cha maovu yake yatasamehewa. Na vile vile kiasi hicho hicho ataongezewa daraja lake mbele ya Allah swt na atamwandikwa miongoni mwa wale waja wake halisi waliofanya ibada yao kwa uhalisi kwa muda wa miaka mia moja.”

 

625.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., aliulizwa na mtu mmoja :

“Ewe Mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Je yeyote yule anayekuja kuomba mlangoni anastahili kupewa Sadaka au badala yake tuwape jamaa na ndugu zetu Sadaka  hiyo?”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwajibu :

“Kwa hakika kuwapelekea msaada Sadaka  jamaa  na ndugu wa mtu zina thawabu nyingi zaidi.”

 

626. Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliandikiwa barua na mtu mmoja akimwuliza,

“Iwapo mtu anaweza kunuia  kuwa mimi katika mali yangu nitatoa sehemu fulani ya mali nitamsaidia mtu fulani na katika kipindi hicho iwapo atakuja kujua kuna mtu katika ndugu na jamaa zake ambaye ni kweli anashida na anahitaji msaada wake basi je huyo mtu anaweza kubadilisha nia yake ya kumsaidia jamaa yake badala ya kumpa mtu aliyekuwa amenuia hapo kabla?”

 

Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. akamjibu kuwa:

“Utaangalia ukaribu wa watu hao na yule aliye karibu nawe katika madhehebu umpatie na lau kama wote wawili kama watakuwa wanatokana na dhehebu  moja tu basi kwa mujibu wa kauli ya Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kuwa kugawanywe kati kati yaani watu wote wawili wapewe nusu kwa nusu, kwa sababu iwapo kutakuwa na jamaa na ndugu ambao wana shida na taabu basi huwezi kutoa Sadaka  na kuwapa wengine. Na kwa hakika kwa kufanya hivyo utakuwa umepata thawabu na fadhila za Sadaka.”

 

 

627.  Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliandikiwa barua na mtu mmoja akimwuliza kuwa:

“Je inawezekana mimi nikatoa Zaka au Sadaka  kutoka mali yangu nikampa mtu ambaye si jamaa wala ndugu yangu?”

 

 Na kwa hayo Imam a.s. alimjibu:

“Usimpe Zaka au Sadaka  mtu yeyote mwingine  isipokuwa wenzako na majamaa zako.”

 

628.  Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliulizwa:

“Je inawezekana kumpa Sadaka  Nasibi (maadui wa Ahlul Bayt

a.s.)?”

 Imam a.s akamjibu kuwa:

“Musiwape Sadaka  wala Zaka maadui wa Ahlul Bayt a.s. na ikiwezekana hata maji pia msiwape.”

 

629.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Je inaruhusiwa kumlisha mtu kama humwelewi kuwa ni Mwislamu au si Mwislamu?”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akajibu kuwa :

“Mtu ambaye humwelewi na kama huelewi chochote kuhusu urafiki au adui, basi yeye unaweza kumpa. Kwa sababu Allah swt anasema tuwatendee watu mema. Lakini yule aliye mpingamizi wa haki au ambaye anaelekea kuhusu upotofu na madhambi au anayewachukua watu kuelekea upotovu na madhambi, huyo msimpe.”

 

630.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Mara nyingi tunaona masikini wanaokuja kuaomba, lakini sisi tunakuwa hatuwafahamu, Je watu kama hawa tunaweza kuwapa?”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwajibu

“Kama wewe moyoni mwako utaingiwa na huruma  kwa ajili ya mtu huyo basi unaweza kumpa, ingawaje hata kama si kamili lakini hata kidogo itafaa.”

 

631.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kidhahiri wapo waombaji wengi ambao (wengi wanatoka vijijini na maeneo karibu ya mji ) hivyo nyie muwape Sadaka watoto, wanawake, wagonjwa, wadhaifu na wazee.”

 

632.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mnapoijiwa na masikini kwa ajili ya kuomba ambao ni wazee kabisa na wanawake na watoto na wasichana wadogo basi muwasaidie Sadaka na vile vile muwasaidie Sadaka  wale mnaoijiwa huruma mioyoni mwenu.”

 

633.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Mijini mwetu wanakuja waombaji wengi sana kutoka vijiji na vitongoji ambavyo viko karibu na mji ambamo humo wamechanganyikana Mayahudi,Manasara, Wakristo na hata Majusi (Wanaohabudu moto) sasa katika sura hii je tunaweza kuwasaidia Sadaka ?”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu :

“Naam ! Mnaweza kuwapa.”

 

634.  Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. aliandikiwa barua na humo akaulizwa:

“Je tunaweza kuwasaidia wale masikini waliopo mitaani ambao hatujui dini na wala Madhehebu zao?”

 

Kwa hayo Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. aliwajibu:

“Kama mtaweza kuwatambua wale maadui na wenye chuki na Ahlul Bayt a.s. na mukiwasaidia basi Allah swt hatakulipeni chochote  ama wale ambao nyie hamuelewi Madhehebu yao basi hakuna matatizo yoyote katika kuwapa Sadaka.  Na muwasaidie masikini wale wowote wanaoomba kama mtaingiwa na huruma mioyoni mwenu. Hata kama hamtaweza kuwaelewa dini na madhehebu zao… Insha-Allah hakuna tatizo lolote katika  kutoa Sadaka  katika sura kama hizi.”

 

635. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia muhudumu wake:

“Yeyote yule anayekuja kuomba nyumbani kwake basi asimruhusu akaondoka hadi pale ahakikishe kuwa amemlisha chakula, hususan siku ya Ijumaa.”

 

Mwandishi anasema kuwa mimi nilimwambia Imam,

“Ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Kila mwombaji huwa si msitahiki.”

 

Kwa hayo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alinijibu

“Ninaogopa kuwa inawezekana mwombaji akawa msitahiki lakini mimi nikamfukuza, isije tukapata matatizo na dhiki iliyo mpata Mtume Ya’aqub a.s na nyumba yake.”

 

636.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Msimvunje moyo mwombaji hata kama atakuwa amekuja kuomba katika usafiri wa farasi.”

 

637.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Iwapo mtoaji atakuwa anajua wema na fadhila za kutoa Sadaka  basi kamwe hatamrudisha mtu yeyote bila ya kumpa kitu chochote.”

 

638.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Kamwe msiwarudishe mikono mitupu waombaji. Iwapo waombaji wengine wasingekuwa waongo na wadanganyifu basi kamwe wengine wasingerudipo.”

 

639.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kamwe hakumrudisha masikini yeyote aliyemwomba asaidiwe Sadaka. Na kama Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa hana chochote cha kumpa basi alikuwa akimwambia kwa lugha tamu Allah swt atakujaalia Insha-Allah.”

 

640.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Mtume Ibrahimu a.s. daima amekuwa akiwahudumia na kuwakarimu wageni, na pale alipokuwa hakuwapata wageni wowote wale, basi alikuwa akifunga mlango wake na akitoka kwenda kuwatafuta wageni.”

 

Na katika hadithi hiyo hiyo tunapata wakati mmoja Malaika Jibrail alimwijia Mtume Ibrahim a.s. na kumwambia :

“Allah swt amenituma safari hii kwa mja wake mmoja ambaye ameweka marafiki Wake kama ni Khalil Wake.”

 

Kwa hayo Mtume Ibrahim a.s. akaingiwa na shauku ya kutaka kumjua na akasema :

“Tafadhali sana naomba unitambulishe huyo umzungumzaye, nami nitapenda kwenda mbele yake.”

 

Jibrail a.s. akasema :

“Ewe Khalil (rafiki)! Ndiwe wewe tu !”

 

Basi Mtume Ibrahim a.s. akamwambia :

“Ewe Jibrail a.s. ! Je kwanini umenifanyia hivyo ?”

 

Hapo Malaika Jibrail a.s. akamjibu :

“Kwa sababu wewe kamwe haujamnyooshea mkono yeyote, na wewe daima haujawahi kumkatalia yeyote aliyekuja kukuomba.”

 

641.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema sema kuwa Mtume Allah swt alikuwa akisema

“Kamwe msimrudishe mikono tupu mwombaji. Hata kama mtakuwa katika hali ya ugumu kiasi gani.

 

642.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa Mtume Musa a.s. wakati alipokuwa akimlilia Allah swt, Allah swt alimwambia :

“Ewe Musa hata kwa ukimpa kidogo mpe ili utunze heshima ya mwombaji,  na kama hicho pia hauna basi kwa maneno matamu na kauli nzuri umwambie na kumwomba msamaha. Kwa sababu miongoni mwa waombaji mara nyingine si lazima atokane na binadamu au Majini bali anakuwa ni Malaika wa Rehema. Kwa hiyo Malaika huyo ndiye anaye wajaribu watu na kile nilicho kushauri ndiyo ujaribu kutegemea kupata jibu lake na huwa anawaombeamo kwa hivyo, ewe mwana wa Imran  angalia vile tabia yako itakavyo kuwa”.    

 

643. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa riwaya kuwa siku moja mtu mmoja alikuja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuomba kwa hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwaangalia Ma-Sahaba wake  na kuwaambia,

“Enyi Ma-Sahaba wangu ! Msaidieni.”

 

Na mmoja katika Ma-Sahaba wake akamsaidia kifaa cha dhahabu. Aliyekuja kuomba akasema

“Je leo ni --  yako?”

 

Yule Sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akajibu :

Naam ndiyo maana yake”.

 

Yule mwombaji akasema:

Mimi nimekubalia hivyo. Mimi si Jini wala si binadamu; bali mimi ni Malaika niliyetumwa na Allah swt nije nikujaribu na kwa hakika nimekuona wewe miongoni mwa watu wenye kushukuru neema za Allah swt. Mungu akujaalie kila la heri.”

 

644.  Sa’ad bin Musayyab anasema kuwa Siku moja wakati wa swala ya asubuhi yeye alikuwa pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., akatokezea mwombaji mmoja na wakati huo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema:

“Mpeni huyo mwombaji---- kumbukeni kuwa---kamwe msimwondoe mwombaji  katika hali ya kuhuzunika yaani msimwondoe mwombaji bila kumpa chochote”.

 

645.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ananakili riwaya kutoka baba yake

mzazi a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:   

“Mruhusu mwombaji aondoke hata kwa kidogo na kwa  mapenzi na kwa huruma pia. Kwa sababu mara nyingi anayekuja kuomba huwa si kutoka binadamu au Majini bali huwa ni njia moja kwa kuwajaribia nyie kwa ajili ya kuwaongezea neema.”

 

646. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha :

“Masikini anapokuja kwenu basi anakuwa ni mjumbe wa Allah swt na yeyote yule atakaye muudhi na atakayemhudhunisha basi atakuwa amemhudhunisha Allah swt na yeyote yule atakaye kuwa amempa chochote basi ajue kuwa amempa Allah swt”.

 

647.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaripoti kutoka kwa wazazi wake

a.s ambao wamesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Wakati ‘Ummah wangu utakapogeuza uso au utakapo wageuzia uso wale wanao hitaji msaada wao na watakapoanza kutembea kwa maringo basi wakati huo Allah swt atasema: kwa kiapo cha utukufu na ukuu wangu hawa watu watakomeshana wao kwa wao na hivyo ndivyo nitakavyo waonjesha adhabu yao.”

 

648.  Walid bin Sahib anasema kuwa:

“Siku moja mimi nilikuwa kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na hapo akatokezea mwombaji mmoja. Imam a.s alimpa chochote huyo mwombaji na akatokezea mwombaji wa pili naye akapewa chochote. Hivyo hivyo akatokezea mwombaji wa nne basi Al Imam a.s akamwambia Allah atakusaidia upate zaidi njia yako atakupanulia. Na baada ya hapo Imam a.s akasema iwapo mtu atakuwa na Dirham takriban elfu thelathini au arobaini, na akanuia akawa na mpango wa kuzitumia zote ambazo kimatokeo hatabakiwa na chochote basi mtu kama huyo atawekwa miongoni kwa wale watu ambao Allah swt huzitupiliambali dua zao.”

 

Kwa hayo mimi nikasema

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je ni makundi gani ya watu hawa watatu?

 

Kwa hayo Imam a.s akajibu

“Mmoja wao ni yule ambaye ana mapesa na mali na baada ya kutumia vyote anaomba ‘ewe Mola wangu naomba unipe riziki’. Basi  hapo Allah swt anamjibu  ‘Je mimi sikukupanulia njia na kukuwekea sababu za wewe kujiwekea riziki yako?”

 

649.  Ali ibn Hamza anasema kuwa:

“Mimi nilimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. swali kuwa yeye amesikika akisema mwalishe watatu---- na kama mnataka kuwapa chochote zaidi muwape ama sivyo nyie mmeshatimiza haki ya siku yenu hiyo”.

 

650.  Walid bin Sabih daima alikuwa akisema kuwa:

“Mtu yeyote anayetoa Sadaka  na iwapo Sadaka  hiyo itakubaliwa au Sadaka  hiyo itarudishwa basi yule mtoa Sadaka  haruhusiwi kuila au kuitumia tena hiyo Sadaka  kwa ajili yake. Na badala yake hana njia yoyote isipokuwa aigawe Sadaka    kwa mtu mwingine. Hatakuwa na ruhusa kwa vyovyote vile vya kuitumia hiyo Sadaka  isipokuwa Sadaka  itatolewa tena Sadaka  kwa mtu mwingine. Vile vile mfano wake inachukuliwa kuwa mtu anapomfanya huru mtumwa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya kutaka furaha ya Allah swt basi kamwe hawezi kumchukua tena yule mtuma(aliyefanywa huru) akamfanya  mtumwa wake. Na baada ya kumfanya huru mtumwa na mtumwa atakapo rudi kwake basi hawezi kumweka vile alivyokuwa amemweka mwanzoni kabla ya kumfanya huru katika njia ya Allah swt. Na vivyo hivyo ndivyo swala hizi zinausiana na Sadaka pia.”

 

651.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.  amesema:

“Yeyote yule atakayekuwa ametoa Sadaka  na iwapo Sadaka  hiyo itamrejea yeye tena basi yeye mwenyewe hataweza kuitumia wala hataweza kuiuza, kwa sababu kitu hicho kilishatolewa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na hivyo hakuna kitakachoweza kushirikishwa katika swala hilo, na mfano wake pia ni sawa na ule wa kumfanya huru mtumwa hivyo hataweza kurudishwa tena katika utumwa.”

 

652.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema

“Iwapo mtu atanuia kutoa Sadaka kwa ajili ya mtu fulani anayeuhitaji msaada huo na wakati huo akapata kujua kuwa mtu huyo ameshaondoka, basi hawezi kuirudisha na kuichanganya hiyo mali katika mali yake na badala yake itambidi amgawie mtu mwingine.”

                                  

653.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: Kuna mtu

alimwuliza iwapo mtu alimfanya huru mtumwa bado ambaye hajafikia umri wa kubalehe je sheria inasemaje?

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu

“Hakuna tatizo lolote ndani yake lakini sheria itakayotumika hapo ni kama ile ya kutoa Sadaka  (yaani baada ya kumfanya huru mara moja hauwezi kumrudisha katika utumwa tena).”

 

654.  Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:

“Dua ya mtu msiidharau au kusema kuwa haifai chochote. Mara nyingi dua muliyoombewa na Mayahudi au Manasara hukubaliwa. Ingawaje inawezekana kwa dua aliyo jiombea yeye mwenyewe haiwezi kukubalika.”

 

655.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Wakati mnapo wasaidia waombaji, muwaombe wawaombeeni dua hata kama dua zao wenyewe hazikubaliki kwa ajili yao wenyewe, mradi kuna uwezekano mkubwa kwa dua zao kwa ajili yenu zikakubalika.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakiliwa na Abu Basir riwaya moja kuwa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Wakati mtu anapomsaidia fakiri mwenye shida sana asiye na uwezo, na pale fakiri huyo anapomwombea dua, basi dua hiyo lazima inakubaliwa na Allah swt.”

 

656.  Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Wakati mnapowapa chochote waombaji; basi muwaombe wawaombeeni dua, kwa sababu inawezekana kwa sababu ya udanganyifu na ulaghai wake dua zake zenyewe kwa ajili yake zisikubaliwe lakini kwa ajili yenu dua zake zitakubaliwa.”

 

657.  Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.:

“Alikuwa akimwambia mfanyakazi wake, zuia kwa punde kidogo sadaka, ili mwombaji amalize kuomba dua.”

 

658.  Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. Na vile vile amesema:

“Dua ya fakiri na mwombaji kamwe hairudishwi au haitupiliwi mbali.”

 

659.  Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amemwamrisha mfanyakazi wake kuwa:

“Wakati unapowapa chochote waombaji basi muwaambie wawe wakituombea heri.”

 

660.  Al-Imam a.s. amesema:

“Wakati muwapapo chochote masikini na waombaji basi muwe mukiwaomba wawaombeeni dua kwa sababu wanapo waombeeni dua kwa ajili yenu dua zao hukubalika na inawezekana dua zao kwa ajili yao wenyewe hazikubaliki.”

 

661.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo mtu atapewa msaada ikapitia mikono themanini hadi ikamfikia aliye mustahiki basi kila mkono utapata haki sawa sawa ya malipo.”

 

662.  Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Bora ya sadaka zote ni ile ambayo binaadamu baada ya kujitimizia mahitaji yake kwa moyo mkunjufu anatoa sadaka.”

 

663.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Yule atakaye fikisha msaada katika hali nzuri kwa mwenye kustahiki basi huyo mfikishaji wa sadaka atapata thawabu sawa kama za yule atakaye toa sadaka yake – hata kama katika kufikisha msaada huo kwa anayestahiki itachukua mikono elfu arobaini basi wote watapata malipo sawa kabisa kwani Allah swt hana upungufu wala kasoro ya aina yoyote ile, na wale watu wanaofanya Taqwa na kutenda mema basi laiti kama mungeweza kuelewa uhakika wa swala hili.”

 

664. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Watoaji ni wa aina tatu

·         kwanza ni Allah swt mwenyewe ambaye anatoa kwa ajili ya malimwengu zote.

·          Pili ni yule mwenye mali na

·         tatu ni yule msaada unaopitishwa katika mikono yake au ni mtu ambaye anafikisha misaada hiyo.”

 

665.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amenakiliwa riwaya na Abu Basir kuwa amesema:

“Watoaji ni wa aina tatu wa

·        kwanza kabisa ni Allah swt,

·         wa pili ni yule ambaye anatoa kutoka mali yake na

·        tatu ni yule anayefikisha kama msaidizi katika kufikisha msaada huo kwa mustahiki.”

 

666.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Allah swt amefaradhisha kwa waja wake kwa kusisitiza kuwa kama yafuatavyo,

·         kwanza uadilifu na mapenzi yake pamoja na muumini mwenzake kama vile ajipendeavyo yeye kwa ajili yake ndivyo ampendee muumini mwenzake.

·         pili awe ameweka hisa fulani au kiasi fulani katika mali yake kwa ajili ya kutaka kumsaidia muumin ndugu  mwenzake. Na

·          tatu kumukumbuka Allah swt katika kila hali na hapa haimaanishi kuwa kwa kumsifu Allah swt peke yake au kwa kutoa uradi (tasbihi) bali hapa kuna maanisho ya kuwa kufanywe kwa kimatendo kabisa yale yaliyoelezwa katika dini yakiwa ni sehemu ya imani ya mtu.”

 

667.  Aban ibn Taghlib anasema kuwa Siku moja yeye alimwomba Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amwelezee haki za muumini mmoja juu ya muumini mwingine. Kwa hayo Imam a.s. alimjibu :

“Ewe Aban! Achana nayo, usini shurutishe kukujibu ulicho uliza.

 

Nami nikamwambia :

 “Ewe Mola wangu niwe fidia kwako.”

 

Na baada ya hapo niliendelea kumsisitiza Imam a.s. anielezee na ndipo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alipoanza kuniambia :

“Haki ya muumini mwenzako juu yako ni kwamba nusu ya mali yako iwe ni mali yake.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akagundua kuwa rangi ya sura yangu imebadilika na akaniambia,

“Ewe Aban je huna habari kuwa Allah swt ameelezea habari za wale watu ambao wamezipenda nafsi za watu wengine kuliko hata nafsi zao?”

 

Nami nikamujibu

“Bila shaka, niwe fidia juu yako.”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaendelea kujibu,

“Kwa hivyo nyie toeni nusu ya mali yenu muwape ndugu zenu muumini, na kwa hayo pia haitamaanisha kuwa nyie mmethibitisha mapenzi yenu kikamilifu, kwa sababu bado mko mnalingana. Kujitolea mhanga na kufikia kiwango hicho itathibitika pale ambapo hata katika nusu ya mali mliyobakia nayo mkatoa mkawagawia muumini ndugu zenu.”

 

668. Muhammad bin  Ajlan anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na mara akatokezea mtu mbele yao akatoa salamu, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza

“Je ndugu uliowaacha huko nyuma hali zao ziko je?”

 

Basi huyo aliyekuja akawasifu na akatoa sifa zao na akaelezea kuhusu hali zao zilivyokuwa. Kwa hayo Imam a.s. akauliza :

“Je matajiri miongoni mwao wanawatunzaje wagonjwa wao?”

 

Basi huyo mtu akajibu :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. !  Kidogo tu.”

 

Na Imam a.s. akamwuliza

“Je hao matajiri wanaonana mara ngapi na masikini?

 

Basi huyo mtu akajibu :

“Mara chache tu.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza

 “Je hao matajiri wanawasaidia kwa mikono yao hao masikini?

 

Kwa hayo huyo mtu akasema

“Ewe Mawla !  Wewe unaniuliza mambo ambayo katika utamaduni wetu upo mchache sana.”

 

Kwa hayo Imam a.s. alimujibu

“Je wao watajidhaniaje kuwa wao ni Mashi’a wetu?”

 

669.  Abu Ismail anasema kuwa:Yeye alimwambia Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.,

“Ewe Maula niwe fidia juu yako! Kwa sasa hivi huko kuna Mashia wengi.”

 

Kwa hayo Imam a.s. akajibu:

 “Je wanawasaidia na kuwahurumia mafakiri na wenye shida? Je wale wanao watendea mabaya sasa watu hao wema waliofanyiwa mabaya wanawasamehe hao wabaya walio watendea mabaya? Je wanasaidiana miongoni mwao katika kamari ? [58]

 

Kwa hayo yote mimi nikajibu :

“Hapana sivyo hivyo.”

 

Hapo Imam a.s. akasema :

“Kwa hakika hao sio Mashia wetu. Basi mjue wazi kuwa Mashia wetu mienendo yao na desturi na utamaduni wao ni kama vile nilivyoelezea hapo.”

 

670. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. siku moja alimwuliza Sa’id bin Hassan,

“Je inawezekana miongoni mwenu kuwa muumini mmoja akatia mkono katika mfukoni mwa muumini wa pili na akajitolea kiasi cha fedha alizo na shida nazo bila ya kusita au kuogopa na muumini yule aliyetiliwa mkono mfukoni mwake asimzuie?”

 

Said bin Hassan akamjibu

“Ewe Mawla! Kwa hakika mimi sina habari na jambo kama hili.”

 

Kwa hayo Imam a.s. akamwambia

“Kwa hakika hakuna chochote.”

 

Hapo mimi nikamwambia Imam a.s. :

“Je hii inamaanisha kuwa sisi tumeisha teketea na kuangamia?”

 

Imam a.s. kwa hayo akamujibu :

“Sivyo hivyo, miongoni mwenu udugu na upendo bado haujaingia nafsini mwenu.”

 

Na katika maswala ya dua imesha zungumziwa hadithi moja ambamo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema zipo aina tatu za dua ambazo kwa kufika kwa Allah swt hakuna mtu anayeweza kuzizuia. Miongoni mwake moja ni

·         dua ya muumini anayemwombea muumini mwenzake na ambaye ametoa msaada kutoka mali yake kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na Ma’asumiin a.s. Na pili ni

·         dua kwa ajili ya muumini mwenzake ambaye pamoja na uwezo wake anaomba hivyo na ambaye baada ya kujua shida na dhiki kali ya muumini mwenzake hakuipuuzia bali amemsaidia.”

 

671.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa na mtu mmoja :

“Ewe Mawla! Je ni mtu gani mwenzi wako aliyebora kabisa?”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu,

“Ni wale ambao wanawawia na kuwafanyia mema ndugu zao katika imani katika hali ya raha,starehe na shida.”

 

Na aliendelea kueleza kuwa

“Ewe Jamil, yeyote yule aliye nacho kingi basi kutenda kwake mema ni rahisi sana. Kwani Allah swt amewasifu wale walio nacho kidogo na huku wanafanya mema. Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Hashri, 59, Ayah 9:

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

672.  Jamil bin Darraj anasema kuwa:

“Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alitukusanyisha na kutuambia

“Miongoni mwenu bora kabisa ni yule ambaye ni mkarimu na mtenda mema kwa wenzake na mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili na anawawia wengine kwa hali hiyo na bora ya matendo ni kule kutendeana mema pamoja na ndugu zenu na vile vile kuwatimizia haja na mahitaji yao na kwa hakika matendo haya yanamuudhi na kumvunja nguvu Shaitan na kunamwepusha mtu asiingie Jahannam na badala yake aingizwe Jannat. Ewe Jamil! Naomba uwafikishie habari hizi muumin halisi.”

 

673.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa kumwambia:

“Ewe Ali! Nina ku-usia mambo matatu ambayo kwa hakika yanathibitisha imani.

  • Moja ni kwamba wakati wa shida na dhiki kutoa mali au chochote na kuitumia katika njia ya Allah swt
  •  pili kuwawia waadilifu watu
  • tatu ni kuwapa elimu wale wanao tafuta elimu kama wanataka kujifunza elimu.”

 

674.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye amesema:

“Bora ya sadaka ni ile ambayo inatolewa bila ya kuwa na shida yoyote na inatolewa kwa furaha.”

 

Mwandishi anasema hadithi hii inawahusu wale ambao wana watoto, familia na ndugu na majamaa. Yeye anakuwa na majukumu ya kuwauliza na kuwatimizia haja hawa watu wanaomtegemea yeye na hivyo baada ya kumalizana nao anatoa sadaka kwa furaha.

 

675.  Sama’a anasema kuwa:

“Siku moja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.,

“Iwapo mtu atakuwa na chakula cha kumtosha siku moja, je anaweza kumsaidia yule mtu mwingine ambaye hana chochote? Au tuseme kama mtu ana chakula cha kuweza kumsaidia mwezi mmoja anaweza kuwasaidia wengine ambao hawana kiasi hicho au yeye hana zaidi bali ana kiasi kile tu cha kumtosha yeye,na hivyo hawezi kumsaidia mwingine basi mtu kama huyo atakuwa amelaumiwa na kushutumiwa?”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu,

“Katika suala hili yapo mambo mawili, miongoni mwenu kuna watu ambao wao wanawasaidia na kuwapenda wengine zaidi kuliko nafsi zao na ambapo Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

Na jambo la pili ni kwamba yule ambaye ana kiasi kile tu ambacho kinamtosha yeye tu, basi mtu kama huyo hayuko katika lawama.

 

Naam, mkono ulio juu uko afadhali kuliko mkono uliopo chini (yaani yule anayempa mtu mkono wa juu na yule anayepokea ni mkono wa chini)na daima wakati wa kutoa lazima aanzie na wale ambao kwa hakika wako chini ya utunzaji wake (anawajibika kuwatunza na kuwasaidia na kuwatimizia mahitaji yao).”

 

676.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliambiwa na ‘Ali bin Sued Assinani:

“Ewe Mawla! Naomba unifanyie usia”.

 

 Kwa hayo Imam a.s. alimwambia

“Fanya Taqwa. Na umwogope Allah swt”.

 

Na hapo Imam a.s. alinyamaza kimya, basi yeye akasema :

“Ewe Imam a.s.! Nina shida kubwa sana. Mimi nimeshindwa kabisa sina uwezo wowote, yaani fikiria kwamba sina nguo yoyote juu ya mwili wangu iwapo fulani ibn fulani asingenivulia nguo zake akanipa na kunivalisha mimi.”

 

Katika kumjibu Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimujibu,

“Funga saumu na utoe sadaka.”

 

Naye kwa kunyenyekea alisema:

“Je nitoe katika yale ambayo mimi ninasaidiwa na watu? Na nitoe kiasi gani kutoka humo?”

 

Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimjibu

 “Chochote kile Allah swt anachokufikishia katika riziki yako toa humo sadaka, kwa kufanya hivyo acha nafsi yako ivumilie kidogo kwa ajili ya kuwatolea wengine walio na shida pia.”

 

677.  Abu basir ananakili riwaya moja ama kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Yeye aliuliza, bora ya sadaka zote ni ipi?”

 

Imam a.s. akamujibu,

“Sadaka bora ni kutoka ile mali ambayo mtu hana nyingi (kitu ambacho unacho kidogo au cha kukutosheleza tu wewe, unatoa humo sadaka), je wewe huna habari

Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

 

678.  Hakika hadithi moja ndefu Masufi walileta dalili moja mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

Je hii ayah inamaanisha kuwa mtu atoe yote yale na afilisike kabisa?”

 

Imam a.s. aliwajibu

“Kwa ayah hiyo ni ufafanuzi ambavyo watendaji walikuwa wakitenda kama Allah swt alikuwa ameruhusu. Hakuna aliye wazuia hao, na ujira wao pia upo kwa Allah swt, lakini hiyo ni amri ya Allah swt ambayo ni kinyume na matendo yao.

 

Na sababu ya kufanya hivyo ni kwamba Allah swt anamwonea huruma muumin ili huyo muumin asiweze kuwaletea shida na kuwadhuru nafsi za wananyumba katika familia yao watoto – dhaifu na watoto wadogo, wote walio dhaifu, na ambao hawawezi kustahimili njaa, wazee waume kwa wanawake.

 

Iwapo mimi nitakuwa na kipande kimoja cha mkate na nikagawa sadaka, basi wale wote wanaonitegemea mie wataangamia na kuteketea.

 

Ndyio maana Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, iwapo mtu atakuwa na kokwa tano za tende au mikate mitano au Dinar tano au Dirham tano na yeye anataka kuzitumia zote, basi itakuwa ni vyema kabisa iwapo yeye azitumie kwa ajili ya wazazi wake, na baadaye kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake na tabaka la tatu kwa ajili ya ndugu na jamaa zake ambao wana shida na wanahitaji msaada wake, na baada ya hapo awasaidie majirani ambao ni mafakiri, na mwishoni kabisa atumie kwa ajili ya kuwasaidia wengineo katika njia ya Allah swt.

 

Na baadaye akaendelea kusema kuwa siku moja ilitokea mtu mmoja kutokea Ansaar alifariki(kufa). Kwa mujibu wa usia wake yeye alikuwa na watumwa watano au sita ambao wote walifanywa (kwa mujibu wa usia huo) huru na wakaondoka zao na huko nyuma familia yake hakuwaachia chochote watoto wadogo wadogo na wana nyumba yake wote wakawa ni muhtaji, wakawa wao sasa wanategemea misaada kutoka wengine ilhali huyu bwana alikuwa na watumwa watano au sita.

 

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipojulishwa habari hizo alisikitika mno na akasema,

“Laiti kama nyie mngelikuwa mmenijulisheni kabla kuwa mtu huyo amewafanya watoto na wenye nyumba yake kuwa muhtaji (ni watu wenye kuhitaji misaada na sadaka) basi mimi kamwe nisingelikubali mtu huyu azikwe katika makaburi ya Waislam.’

 

Hlafu anaedelea kusema kuwa wazee wetu wamenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtoaji sadaka inambidi kwanza awatimizie mahitaji ya wale wanao mtegemea yeye; na wale ndugu na jamaa walio wakaribu zaidi ndio awape kwanza (yaani wazazi, mke, watoto na ndugu zake na majamaa wanaofuatia wa karibu zaidi) na baada ya hapo majamaa na ndugu wenye uhusiano wenye ujamaa nao wa mbali ndio wapewe”.

 

679.  Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. Amenakiliwa hadithi yake moja isemayo kuwa:

“Wakati muwapapo sadaka masikini muwaombe wawaombeeni dua, na akaendelea kusema, baadaye kuubusu mkono wa yule uliyemsaidia (uliyempa sadaka) kwa sababu sadaka unayoitoa kwanza inakwenda katika mikono ya Allah swt ndipo inapoingia katika mikono ya mwombaji.

 

Kama vile Allah swt anavyosema katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:

Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali Sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

680.  Ahmad bin Fahad anaandika katika kitabu chake kuwa:

“ Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. wakati wa kutoa sadaka alikuwa akiubusu mkono wake mwenyewe, na mtu mmoja alimwuuliza sababu ya kufanya hivyo na Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. alimjibu,

“Kwa sababu kufanya hivyo ni kwamba sadaka kwanza inakwenda katika mkono wa Allah swt ndipo baadaye huishia katika mkono wa mwombaji.”

 

681.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Sadaka inayotolewa na muumin kwa hakika inafika mikononi mwa Allah swt na baadaye ndio anapewa aliye mwombaji. Na akaendelea kuelezea ayah ya Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:

Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali Sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

682.  Jabir Al J’ufi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad

al-Baquir a.s. kuwa  Al Imam Amir al-Muuminiin ‘Ali bin Abi Talib a.s. amesema kuwa:

“Siku moja nilitoa sadaka ya Dinar moja, hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akaniambia,

“Je unajua sadaka inapotolewa na mkono wa muumin kabla yake yeye anakuwa amejitoa nje ya mitego ya masheitani sabini? Na kabla ya yule mwombaji hajapokea hiyo sadaka inakwenda katika mikono ya Allah swt?

 

Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:

Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali Sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

683.  Mu’alla bin Hunais ananakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Kila kitu Allah swt amekiwekea mtunza hesabu wake, isipokuwa sadaka tu, kwamba yeye ndyeo mwenyewe anayeishughulikia. Na baba yangu a.s. alipokuwa akimpa masikini au mwombaji sadaka yoyote, alikuwa akiichukua tena akawa akiinusa na kuibusu na tena alikuwa akimrudishia mwombaji mikononi mwake kwa heshima na adabu.

 

Kwa sababu sadaka anayopewa mwombaji kwanza inakuwa imepitia katika mikono ya Allah swt ndipo inapoishia katika mikono ya yule anayeomba. Kwa hiyo mimi pia nimependelea kukibusu kitu kile ambacho kimeshaingia katika mikono ya Allah swt ndipo kikaenda katika mkono wa mwombaji!”

 

684.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kwa kila kitu isipokuwa sadaka tu Allah swt amemweka Malaika kutunza habari zake – na sadaka ameiweka katika usimamizi wake mwenyewe.”

 

685.  Muhammad bin Muslim ameripoti riwaya moja ama kutokea Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. kila alipokuwa akimpatia sadaka mwombaji basi alikuwa akiibusu mikono ya mwombaji huyo. Na alitokezea mtu akauliza sababu ya kufanya hivyo naye akajibu kwa sababu inatoka kwenye mikono ya Allah swt na inaingia katika mikono ya mwanadamu huyo mwombaji.”

 

686.  Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. amesema:

“Ujue kuwa uso wako unaong’ara kwa heshima na adabu, na wewe wakati unapokwenda kuomba na ukarefusha mikono yako kwa ajili ya kuomba basi heshima na adabu hiyo inayeyuka na kuanza kudondoka kutoka usoni mwako. Sasa ni kuangalia uyeyukaji huo unamdondokea nani ndio wewe unatakiwa ujue uangalie na ujue.”

 

 

687.  Ibn Fahad ameripoti riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Shi’a wetu hata kama watakuwa wakifa kwa njaa basi kamwe wakati wowote ule hawatainyoosha mikono yao kwa mbele ya watu kwa ajili ya kuomba.”

 

688.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mtu yeyote anayenyoosha mkono wake na kufungua kiganja chake kwa ajili ya kuomba, basi ushahidi wake utupiliwe mbali.”

 

689.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo mwombaji angelikuwa akijua yale majukumu na wajibu walio nao katika kufanya hivyo, basi kamwe asingeomba chochote kwa mtu yeyote. Na vile vile na kutokumpa mwombaji pia kuna majukumu na wajibu mkubwa sana iwapo watu wangelijua basi kamwe wasingeli wakatalia kuwasaidia watu.”

 

690.  Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwaambia Ma-Sahaba wake:

“Ni kwa nini hamfanyi bay’a yangu (utiifu wangu)?”

 

Basi Ma-Sahaba wakamjibu:

“Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tumeshakwisha kufanya bay’a yako tangu mwanzoni. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema, mfanye bay’a katika swala ambalo mle kiapo kuwa nyinyi kamwe hamtanyoosha mikono yenu kwa wengine kwa ajili ya kuomba. Na baada ya kula viapo hivyo ikaonekana mandhari tofauti kabisa miongoni mwa Ma-Sahaba kiasi kwamba hata mtu alipokuwa akidondosha mkongojo wake basi alikuwa akiteremka kutoka usafiri wake wa mnyama kama ngamia n.k. kuteremka chini na kujiokotea mkonojo wake, na kamwe alikuwa hamwambii mtu mwingine amwokotee na kumpa hiyo bakora yake iliyoanguka”

 

691.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo mtu atakwenda mbio mbio msituni akakata kuni na mzigo huo akauchukua kuja nao kwa hiyo atakuwa ametunza heshima na hadhi yake, basi jambo hilo ni afadhali kuliko udhalilisho wa kuomba.”

 

692.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Yeyote yule aliyetuomba sisi tunampa na yeyote yule aliyetoa na yeyote yule aliye shukuru basi Allah swt atamfanya awe tajiri.”

 

693.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kwa kuwaomba watu mahitajio yako ni kuteketeza na kuangamiza heshima yako ni sawa na kuteketeza na kuangamiza heshima yako, na vile vile ustahi wako pia unamalizika. Na kwa hakika kile walichonacho wao utajiri wao inambidi mtu akate tamaa asitegemee chochote yaani asiwe na tamaa ya aina yoyote na hakika hii ndio inayo hesabika kuwa ni heshima kubwa ya muumin. Kumbukeni kuwa tamaa ni ufakiri wa aina mojawapo.”

 

694.  Ja’bir amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Allah swt ameweka karaha kwa wale wanao omba kwa kung’angania na kwa kufuatilia.”

 

695.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Enyi watu! Msiombe wakati watu wanapokuwa katika makundi, isitokee kwamba kwa sababu ya ubahili wao ikawawia nyie machungu.”

 

696.  Mufadhdhal bin Kais bin Rumman anasema kuwa:

“Yeye siku moja alikuwa katika huduma ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na mimi nikamdokezea kidogo kuhusu matatizo niliyokuwa nayo. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia kijakazi wake:

Naomba ule mfuko. Na akaniambia Abu Ja’afar (Manthur) amenitumia hizi Dinar mia nne kwa ajili ya msaada, hivyo chukua wewe. Na uende ukamalize shida na dhiki uliyo nayo.”

 

Nami nikamwambia:

“Hapana! Kwa kiapo cha Allah swt mimi niwe fidia juu yako – mimi sina nia hivyo – mimi nilikuwa natarajia kuwa wewe uniombee dua kwa Allah swt ili shida na dhiki niliyonayo isiniwie ngumu bali iwe nyepesi.”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema,

“Pamoja na mimi kukuombea dua, kamwe usiwaambie mbele ya umati wa watu shida zako kwani kwa kufanya hivyo wewe utapoteza heshima na hadhi yako.”

 

697.  Harith Hamdani anasema kuwa yeye amesikia hadithi ya

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kutokea kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa:

“Maombi ni amana za Allah swt katika vifua vya watu na yeyote yule atakayeficha siri hiyo basi atapata thawabu za ibada.”

 

698.  Kulayni anasema kuwa Bwana Luqman alikuwa akimpa mafunzo mwanake kwa kumwambia:

“Ewe mwanangu, mimi nimeisha kunywa dawa na magamba yaliyo chungu kabisa, lakini mbele ya shida na dhiki hakuna kitu kinachozidi uchungu wake. Iwapo wewe utapitia katika hali kama hiyo, basi kamwe usiseme maombi yako mbele ya watu, kwa sababu wewe katika macho yao utaanguka heshima na taadhima yako, na watu hao hawawezi kukufaidisha chochote na badala yake nakuomba umwombe yule ambaye anakujaribu kwa mitihani ya aina hiyo, na bila shaka ni yeye tu anayeweza kukuondolea matatizo na dhiki iliyokukabili, hivyo umwombe yeye tu (Allah swt). Yeye ni nani duniani ambaye amemwomba Allah swt na akarudi mikono mitupu, na yupo ambaye aliweka matarajio na matumaini yake kwa Allah swt na akajikuta ametoka mtupu?”

 

699.  Imeripotiwa kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Ewe 'Ali! Allah swt ameweka ni amana miongoni mwa waja wake katika hali ya shida na ufukara, na yeyote yule atakayeweza kuificha hiyo amana basi ajue kuwa yeye ni mtu ambaye amedumisha ‘ibada na anapata fadhila za wale walio dumisha ‘ibada na wanao funga saumu, lakini yeyote yule ambaye anaitoboa na kuitangaza hiyo amana ya Allah swt kwa kudhihirisha na kufanya bayana siri ya shida na ufukara wake kwa wengine, na hao watu baada ya kumsikiliza hawamsaidii basi mjue kuwa huyo mtu kwa hakika wamemuua. Mauaji haya sio kwa upanga au kwa mkuki bali ameuawa kimoyo.”

 

700.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt.”

 

700.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt.”

 

 



[1]  Hadith hii imeelezwa na Masahaba nane wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. na wafuasi wanane wa Masahaba, na wanazuoni sitini walio mashuhuri, na waandishi zaidi ya 90 kutokea Ahl Sunna,  imeelezwa katika Mishkat-ul-Masabih, uk. 523 kutoka Ahmad-ibn-Hanbal; ; Faraidh-us-Simtayn, j. 2, uk. 242; As-Sawai’q-ul-Muharaqah, uk. 234 ;  ‘‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha-ul-Akhbar, j.1, uk. 211; na wengine wengi kwa kunakiliwa vitabu, na iwapo utapenda kuvijua basi tafadhali rejea Nafahat-ul-Azhar, j. 4, uk. 127.

[2] Hadith hii imeelezwa na watu zaidi ya sitini kutokea Masahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. vile vile imeelezwa na waelezaji zaidi ya 185 ambao wameelezwa katika Sahih Muslim, j. 2, uk. 238 na Musnad Ahmad Ibn-Hanbal, j.5, uk. 181, 182 ; Sahih-i-Tirmidhi, j.2, uk. 220, nawengiine kutokea vitabu vingine ambavyo iwapo utapenda kuona, vimeelezwa katika ukurasa 199 hadi 210, j. 1 katika Nafahat-ul-Azhar fi Khulasat-i-‘Abaqat-ul-Anwar.

[3] Sehemu ya semi za Al-Imam a.s. kutoka Sahifah Inquilab.

[4] *Tabaqat al-Kubra , j. 6, uk.168,; Taqyid al-'ilm , uk. 89,90; Kanz al-‘ummal, j. 10, uk. 156; Rabi’

    al-Abrar, j.. 3 , uk. 294

[5] Bihar al- Anwar, vol. 2 uk. 152; al- Taratib al - idariyyah vol. 2, uk. 246; Sunan al - Darimi, vol 1, uk.

   130; Ilal al - Hadith, vol. 2, uk. 438; Taqiyyad al - Ilm, uk. 91; Jami’bayan al - ‘ilm, uk.99; Kanz

    jumat al - Imam al - Hasan min Tarikh Dimashq, uk. 167.

[6] Al - Tabaqat all- Kubra, vol. 6 uk.220.

[7] Ansab al - ashraf, vol. 2 uk.98; na Hadith no. 1980 kutokea maisha ya Imam Ali (a.s.) katika Tarikh

  Dimashq Historia ya Damascus); Bihar al- Anwar, vol.2 uk. 230; al - Fadhail ya Ibn Hanbal, Hadith

   no. 222.

[8] Ansab al - Ashraf, vol. 1, uk. 121; Tarikh Dameshq, vol. 38, uk. 202; Hilyat al - awliya, vol. 1, uk. 67;

   Shawahid al - tanzil, Hadith no. 1009.

[9] Ansab al - Ashraf, vol. 2, uk. 145.

[10] Bihar al - Anwar, vol. 2 uk. 50 kutoke  ashf al - Mahajjah.

[11] Bihar al - Anwar, vol. 2, uk. 152.

[12] Bihar al - Anwar, vol. 2, uk 153.

[13] Kwa ajili ya kutaka kuelezwa zaidi juu ya Hadith zizungumziazo swala hili urejea Makatib al –

   Rasul, vol. 1, uk. 71 na 89 iliyoandikwa na Ali Ahmad Miyanji.

[14] Taqyid al - ilm, uk. 89.

[15] Rawdhat al - Jannat, vol. 8, uk. 169.

[16] Taqyid al - Ilm, uk. 104.

[17] Tarikh al - adab al - ‘ Arabi, “al -’ Asr al - Islami”, uk. 453, ambapo masimulizi kama hayo hayo

   yametolewa na Mustafa Abd al - Razzaq; rejea  Tamhid li - tarikh al - falsafah al - Islamiyyah,

   uk.202,203.

[18] Al-Muraja’at , uk. 305,306, iliyochapishwa na al-’Alami,Beirut.

[19] Ta’asis al-Shiah li-ulum al-Islam, uk.280, iliyochapishwa na al-Alami, Beiru.

[20] Rijal al-Najishi, uk.3,4, iliyochapiswa Qum.

[21] Qamus al-Rijal, chini ya maisha ya Muhammad ibn Abd Allah ibn al-Hassan;Rawdhat al Jannat

     vol. 8,uk. 169.

[22] Rijal al-Najashi,uk. 3,4, iliyochapishwa Qum.

[23] Fur’ al - Kafi, vol.2, uk.666; kwa mifano mingine rejea  Fur al-Kafi, vol.7 uk.77.

[24] Wasa’il al-Shiah, sura juu ya Zakati; rejea Makatib al-Rasul vol. 1, uk.73.

[25] Was’il Shiah, sura juu ya  Jihad (vita vitukufu); Makatib al-Rasul, uk.176.

[26] Wasa’il al-Shiah, sura juu ya Qadha.

[27] Furu al-Kafi, vol.7, uk 94.

[28] Was’il al-Shiah, sura juu ya al - Hudud.

[29] Furu al - Kafi, Vol. 7. uk.98.

[30] Al-Tabaqat all-kubra, vol 2. uk. 389; al-Musnaf ya Abd al-Razzaq, vol. 1, uk. 285; Taqyid al-Ilm. uk

    107.

[31] Jami’bayan al-Ilm, vol.1, uk.92.

[32] Al-Musannaf ya Abd-Razzaq, vol.7, uk.337.

[33] Al-Tabaqat al-Kubra, vol.7, uk 447.

[34] Sunan al-Darimi, vol.1,uk.126; Taqyid al-Ilm uk. 105,106.

[35] Sunan al Darimi, vol.1. uk. 126; Akbhar Isbahan, vol 1, uk. 312; Tadhrib al-rawi, uk. 90  ya al-

    Siyuti..

[36] Al-Jarh wa al-ta’dil, vol. 1, uk.184.

[37] Tarik al-Khulafaa, uk. 261 ya al-Suyuti.

[38] Tadhkirat al-Huffadh, vol. 1, uk. 169,170,191,203.

[39] Jami’bayan al-Ilm, vol. 1, uk.88,91.

[40] Jami’bayan al-Ilm, vol. 1, uk.92.

[41] Muqaddamata Fath al-Bari, uk.4,5.

[42] Tadhkirat al-Huffadh, vol.1, uk.160.

[43] Kashf al -zunun, vol. uk. 237.

[44] Tadhkirat al-huffadh, vol. 1, uk.419.

[45] Ibid., vol.uk. 423 (kama hapo 44)

[46] Tadhkirat al-huffadh, vol.1, uk.423; Tadrib al-rawi uk. 88,89.

[47] Ipo Hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa “Mimi ni mji wa elimu na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wake” na vile vile amesema “Mimi ni hazina ya elimu na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni ufnguo wake.” Na zipo Hadith nyingi kama hizo.

[49] Nimetarjumu orodha ya Rawi 100 wa Kishi’ah wanaojuikana na walio ma’arufu katika vitabu vya Ahl as-Sunnah. Kwani wengi wa Masunni wanadai kuwa Mashi’ah ni Rafidhi  (walio asi ) na wengine majaheli kuthubutu kusema kuwa Mashi’ah ni Makafiri. Hivyo itakuwa vyema iwapo utapata makala hayo ukayasoma.

[50] Msomaji anaombwa kujaribu kusoma kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya Kiswahili kwa jina la Tadhwin al-Hadith (Uchunguzi juu ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith) ambamo swala hili limezungumzwa kwa marefu na mapana.

[51] Nimetarjumu maandiko juu ya sadaqah na hivyo utaweza kupata mengi katika kitabu nilichokiipa jina la Dhambi Kuu la Kutokulipa Zaka, Khums na Sadaqah

[52]  Hiki kitabu ni juzuu ya pili katika maudhui haya na kwa kuliona swala

    hili ni nyeti katika jamii yetu, ndiyo maana nimekitayarisha hiki kitabu cha

   juzuu ya pili..

[53] Ndugu msomaji maudhuhi haya yaku sema uongo nime tarjumu vitabu viwili mbalimbali ambavyo nimevipa jina Dhambi kuu katika Islam uharamisho wa uongo. Uongo ni moja katika madhambi makuu katika Islam hivyo ukitaka kusoma zaidi kuhusu uongo nakuomba utafute vitabu hivo viwili juzu ya kwanza na juzu ya pili utayaweza kuona mengi katika somo hiyo.

[54]  Kwa hakika tunaona leo vijana hata wazee wameathirika sana katika jamii kwa sababu ya marafiki kijana anakuwa na marafiki wabaya walevi atakuwa mlevi wavuta bangi atakuwa anavuta bangi wenye kutumia madawa ya kulevya naye atatumia madawa ya kulevya wakiwa wanaenda kwenye mambo ya uasherati na watoto watakuwa waasherati n.k. vivyo hivyo utaona hawa vijana wanajitenga na utamaduni wa nyumbani kwao kwa sababu ya kuathirika shauri ya urafiki wa wenzao wengine hata wanathubutu kutoroka nyumbani n.k. Ndio kwa sababu hiyo utaona Uislam unatia umuhimu sana katika suala hili la kuwachukua marafiki ambao wana tabia nzuri ili maingiliano yetu nao yasitutoe katika dini na utamaduni wetu utaona wengine wakati wa kusali ndio wanapenda kwenda kupiga masoga mabarazani kwa hiyo nasi pia tunaacha kusali tunakalia kupiga soga na wana mbinu nyingi sana za kutupotosha sisi ili maadili yetu yavuje yamomonyoke tuwe na majina ya Waislam lakini tusiwe na tabia na desturi za Kiislam.

[55] Ndugu msomaji kitabu hiki kinazungumzia mambo ya sadaqah  na kuna kitabu kimoja nimekitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia dhambi kuu, kutokulipa zaka na sadaqah. Kwa hiyo ili kutaka kusema habari zaidi kuhusu zaka naomba usome kitabu hicho hutapata kulipa mambo marefu na mapana juu ya zaka.

[56] Mara nyingi sisi hatufanyi mambo mema hatutoi Sadaka, hatusali hatufungi saumu na tunafanya usia wakati wa kufa tunategemea tuache usia kwamba kazi fulani nilikuwa nataka kuifanya mtoto wangu aifanye, Sadaka fulani nilikuwa nataka kuitoa mtoto wangu aitoe, siku fulani sikusali mtoto wangu anisalie, saumu sikufunga mtoto wangu anifungie saumu zangu nk. Kwa hakika mambo kama hayo hayana dhamana kuwa yatatimizwa hivyo unaweza kukosa wewe vyote na ukawa  umestahiki wa ghadhabu na adhabu za Allah swt siku ya Qiyamah.

 

[57] Yaani Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa anamaanisha hapa kuwa angewaongezeapo kidogo.

[58] Nimekitarjumu kitabu juu ya kamari :  Katika Islam Uharamisho wa Kamari. Na kimechapwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, DSM, Box 200333