UWAHHABI

Asili na kuenea kwake

( Uchambuzi wa kihistoria ) 

 

Kimekusanywa na kutarjumiwa na

AMIRALY M. H. DATOO

Bukoba  Tanzania

 

                                  Y A L I Y O M O

 

       

MANENO MACHACHE............................................................................... 3

(1) UWAHHABI : ASILI NA KUENEA KWAKE................................... 4

(2) MISHENI YA KWANZA YA MAWAHHABI................................. 14

(3) WAISLAMU WA TA’IF WAPORWA NA KUUAWA................... 16

Muujiza....................................................................................................... 20

(4) UDHALIMU WA MAWAHHABI KATIKA MAKKAH............... 21

(5) MAWAHHABI  HUKO  MADINA..................................................... 28

Muujiza....................................................................................................... 30

(6) WAUTHMANIYYA WAKOMBOA MIJI........................................ 33

 

 

 

 

 

 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

MANENO MACHACHE

KWA JINA LA ALLAH SWT MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 

Natoa shukurani zangu kwa Allah swt, Mtume Muhammad s.a.w.w. pamoja na Ahli Bayt tukufu ya nyumba yake a.s. kwa kunijaalia uwezo wa kukikusanya na kukitarjumu kitabu hiki.

 

Allah swt amewatuma Mitume a.s. kuja kutuongoza na kutuletea maamrusgo Yake ili tusihangaike kwa kutapa huku na huko tukitafuta kipi ni kweli na sahihi. Lakini wapo watu wenye uchu wa kujitakia dunia kwa hali yoyote ile, hivyo wanawasahau Mitume a.s. na ujumbe waliokuwa wametuletea katika miaka yote hiyo. Kwa tamaa na uroho wao wanachafua dunia na desturi za amani.Wanawatesa na kuwateketeza watu bila ya kujali kuwa wao wafanyavyo si haki.

 

Mtume s.a.w.w. alisema kuwa, “Ummah wangu utagawanyika katika makundi sabini na tatu, ni kundi moja tu litakaloingia Peponi.” Hivyo makundi sabini na mbili , kama zilivyobainishwa, zitaingia Motoni kwa sababu za itikadi zao potofu, na kwa hakika hayo yamshakwisha tokea. Makundi haya sabini na mawili si makundi ya makafiri kwa kutojua ilimu sahihi ya Qur’an na Hadith, lakini wataingizwa Motoni kwa sababu wao wamediriki kuubadilisha Uislamu.Na hao wanaitwa ahl al-bid’a au -dalala , wakaidi. Wakaidi, kwa sababu wao ni Waislamu, na hapo mbeleni watatolewa kutoka Jahannam na kupelekwa Peponi. Mbali na hao, wapo wale ambao ni Waislamu lakini wanakuwa katika jitihada za kuubadilisha kwa ilimu yao potofu na kipeo chao kidogo, hivyo wanatoka nje ya Uislam. Kwa hakika hao watabakia Motoni kwa milele. Nao ni Zindiq na wachafuzi.

Leo, watu waitwao la-madhhabi wanatumia mamilioni ya madola kwa kueneza imani zao potofu katika kila nchi humu duniani. Ni jambo lakusikitisha mno kuona kuwa hawa waroho wa mapesa wamekuwa wakivutiwa mno katika imani zao potofu na za kufitini, huku nyuma wakiachia hazina kubwa waliyoachiwa na Ahl al-Bayt a.s. ya Nyumba ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Maulamaa wa Ahl-as-Sunna. Hao Mawahhabi wamejaribu kwa jitihada zao zote kuwadanganya Waislamu kuwa vitabu vya Maulamaa wao vinawapotosha. Wao wametayarisha vitabu na propaganda zao dhidi ya Islam halisi iliyokuja kwetu kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w.,kwa maandiko ya Mawahhabi yaliyojaa upotofu na vitisho na ulghai.

 

Kwa hakika Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab na kizazi chake wamekuwa wakitoa imani zao potofu kwa kuchapa vitabu ambavyo vimekuwa vikiwapotosha Waislamu kwani walikuwa wakizitumia Ayah za Qur’an tukufu dhidi ya Waislamu wenyewe. Wao hata walithubutu kuwaita Wailsamu kuwa ni Makafiri kwa kuelezea kiuongo Ayah na Hadith. Na jambo hili ndilo limenifanya mimi nijiandae kukitoa kitabu hiki ambacho kitafichua uasili wao.

 

Kijitabu hiki kilicho mikononi mwenu ni sehemu moja ya kitabu kamili juu ya Mawahhabi. Sehemu hii inazungumzia vile Mawahhabi walivyotokezea, vile walivyo enea vile majahili na makatili waliojiingiza katika Uwahhabi ili kujipatia mali na cheo wamewateketeza na kuwaua Waislamu na kuzipora mali zao.

 

Vile vile ninakitayarisha kitabu kingine ambacho kitazungumzia imani za Mawahhabi na kuzichambua moja baada ya pili ili Waislamu wajue waziwazi kuwa wao wanadanganywa juu juu tu. Vitabu vingi vimeandikwa juu ya Mawahhabi, lakini kuna haja ya kutoboa mambo yao ili uasili wao ujulikane.

 

Hivi karibuni rafiki yangu mmoja Msunni, ambaye alikuwa akitoa mihadhara dhidi ya  wauaji wa Imam Hussain a.s. huko Karbala, Iraq, nimesikia amejiunga na Mawahhabi hawa. Hivyo natumai atakapoisoma habari zilizoandikwa humu, labda atajifikiria.

 

Jambo la pili, nimebishana na rafiki yangu mmoja ambaye ni shabiki mkubwa wa mpira. Mimi nilimwambia kuwa katika siku atakazokuwa yeye akiangali mechi za footbal za Kombe la dunia 1998,Ufaransa,mimi nitakitayarisha kitabu kimoja.Hivyo tuone yule anayeupoteza muda na yule anayeutumia muda kwa ajili ya manufaa ya wengine.

 

Tunamwomba Allah swt awasaidie Waislamu wasiteleze kutumbukia katika mitego ya Mawahhabi.

 

 

Amiraly  M. H. Datoo

P.O.Box 838

BUKOBA

9 June 1998

 

 

 

 

SEHEMU YA KWANZA

(1) UWAHHABI : ASILI NA KUENEA KWAKE

Katika zama za utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire), tawala zote ambazo zilikuwapo katika bara la Uarabu, kila jimbo lilikuwa na maofisa waliokuwa wameteuliwa kutoka serikali kuu. Baadaye, kila mkoa isipokuwa Hijaz ilikuwa mikononi mwa wale walioweza kuzinyakua na kuwa tawala za Kifalme.

 

Imani za Mawahhabi zilizoenezwa na Muhammad ibn ‘Abd al - Wahhab zilikuwa zimeshabadilika kuwa katika sura za kisiasa katika kipindi kifupi katika mwaka 1150 A.H.( 1737) na zilienea Bara zima la Arabia. Baadaye, kwa amri za Khalifa wa Istanbul, Muhammad ‘Ali Pasha, Gavana wa Misri, aliikomboa Arabia kwa msaada wa majeshi ya Misri.

 

‘Abd al-‘Aziz ibn Muhammad, aliyewaamini Mawahhabi, alitangaza vita kwa mara ya kwanza katika 1205 A.H. (1791) dhidi ya amir wa Makkah, Sharif Ghalib Effendi. Wao walikuwa wamekwisha eneza Uwahhabi kisirisiri hadi hapo. Wao waliwaua na kuwatesa Waislamu wengi mno, kuwachukua wanawake na watoto wao mateka na kuzipora mali zao zote.

 

Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alitokana na kabila la Bani Tamim. Alizaliwa katika kijiji cha Uyaina karibu na mji wa Huraimila huko katika jangwa la Najd, mwaka 1111 A.H.(1699) na kufa 1206 A.H.( 1792). Hapo awali alikuwa na nia ya kufanya biashara, hivyo alisafiri hadi Basra, Baghdad, Iran, India na Damascus, ambako kote huko alijipatia sifa la jina kama Sheikh wa Najdi kwa sababu za ujanja na tabia yake.Yeye aliona na kujifunza mambo mengi katika sehemu hizi na hivyo akawa na hamu ya kuwa kiongozi mkubwa. Hivyo ili kutaka kutimiza hamu yake hiyo ilimbidi abuni njia moja iliyokuwa tofauti na njia zinginezo ili aweza kutimiza malengo yake, na kwa kujitayarisha kwa hayo, alianza kuhudhuria mihadhara ya maulamaa wa Kihanbali waliokuwapo katika Mji Mtukufu wa Madinah na baadaye huko Damascus kwa kipindi fulani. Wakati aliporejea Najd, alianza kuandika makala juu ya maudhui ya dini kwa ajili ya wanakijiji wake.Katika kuandika makala hayo,yeye alikuwa akiongezea fikara zake alizokuwa amezipata kutoka makundi ya bid’a ya Mu’tazila na wengineo. Wanakijiji wengi waliokuwa masikini majahili, hususan wakazi wa Dar’iyya na chifu wao jahili, Muhammad ibn Sa’ud, walikuwa wakimfuata Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab. Waarabu walikuwa wakiheshimu mno ukabila na kwa kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa si kutoka kabila maarufu, basi alimtumia Muhammad ibn Sa’ud kama chombo kwa kuutangaza fitna yake mpya aliyokuwa ameiita Uwahhabi. Yeye alijitambulisha kama Qadhi (mkuu wa mambo ya dini ) na Muhammad ibn Sa’ud kama Hakim (mtawala). Kwa hila zake alikwishafanya mabadiliko katika katiba yao kuwa wao hawatarithiwa na mtu yeyote yule isipokuwa watoto wao tu.

 

Katika mwaka 1306 (1888) wakati ambapo kitabu kiitwacho Mir’at al-Haramain kilipoandikwa, kiongozi wa Najd alikuwa ‘Abdullah ibn Faysal, kutokea kizazi cha Muhammad ibn Sa’ud, na Qadhi pia alikuwa ametokana na kizazi cha Muhammad ibn ‘Abd al-Wahhab.

 

Baba yake mzazi wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, ‘Abd al-Wahhab, ambaye alikuwa ni mcha Mungu, ‘alim halisi katika Madina, ndugu yake Sulaiman ibn ‘Abd al-Wahhab na waalimu wake walikuwa wamekwisha tambua kutoka maneno, matendo, ishara na mawazo yake, ambayo mara kwa mara alikuwa akidhihirisha katika sura ya maswali alipokuwa mwanafunzi huko Madina, kuwa atakuwa mpotofu ambaye ataidhuru mno Islam kwa undani katika kipindi kifupi kijacho. Wao wote kwa pamoja walimuasa na kumnasihi aache mawazo yke hayo ya upotoshi na vile vile walikuwa wakiwashauri Waislamu wote kwa ujumla wasimfuate na wajiepushe na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab. Lakini katika muda mfupi tu walikumbana na jambo walilokuwa nalo khofu, na yeye alianza kueneza uzushi wake huo kidhahiri kwa jina la Uwahhabi. Kwa ajili ya kuwapotosha majahili na wapumbavu, yey alijitokeza kwa mawazo ya kurekebisha na kuzua mambo ambayo hayakubaliani na vitabu vya maulamaa wa Islam. Yeye alithubutu kwa kishindo kuwatuhumu Waislamu wa Ahl as-Sunnah wal Jama’a kuwa ni makafiri. Yeye alikuwa akiamini kuwa ni shirk kumwomba Allah swt kwa kupitia Mtume Muhammad s.a.w.w. au Mitume mingine a.s. au ma-Awliya’’ na kuzuru makaburi.

 

Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa akimwona mtu yeyote yule anayesali na kuomba karibu na kaburi kuwa ni Mushrik. Yeye alisisitiza kuwa Waislamu wasemao kuwa mtu fulani au kitu fulani mbali na Allah swt kimefanya hivi au vile,kwa mfano, kwa kusema kuwa dawa fulani na fulani zimeponyesha au mimi nimeweza kupata kile nilichokuwa nikihitaji kwa kupitia Wasila wa Mtume Muhammad s.a.w.w. au au mawali fulani fulani basi hao wote ni Mushrik. Ingawaje waraka wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab hazikuwa chochote isipokuwa ni uongo na fitina tu, lakini majahili hawakuweza kutofautisha baina ya ukweli na uongo, wale wasiokuwa na kazi, wazururaji, majahili, wenye kuvizia bahati na wenye nyoyo ngumu walizipokea mawazo yake na kujiweka bega kwa bega pamoja naye na kuamini wale Waislamu waliokuwa katika njia sahihi kuwa wote kwa pamoj ni makafiri.

 

Wakati Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alipowaomba ruhusa watawala wa Dar’iyya kutaka kueneza imani zake za uzushi kwa kupitia utawala wao, wao walimpokea kwa mikono miwili kwa matumaini ya kupanua eneo la utawala na kuzidi kwa nguvu zao.  Wao walijitolea kwa hali na mali kueneza imani hizo kila mahala.  Wao hata walithubutu kutangaza vita dhidi ya wale wote waliokuwa wakimkataa na kumpinga. Watu  Mahayawani na  wateka nyara wa jangwani walikuwa wakishindana katika kujiunga na jeshi la Muhammad ibn Sa’ud wakati pale iliposemwa kuwa ni halali kumwua na kupora mali za Waislamu. Katika mwaka 1143 ( 1730 ), Muhammad ibn Sa’ud pamoja na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab wakishirikiana kwa pamoja walifikia maafikiano kuwa wale wote ambao hawata kubalia Uwahhabi, basi watakuwa ni makafiri na Mushrik, na hivyo ilikuwa ni halali kwao kuwaua na kutaifisha mali yao yote, na walitangaza rasmi amri hiyo miaka saba iliyofuatia.  Hapo ndipo Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alipoanza kutunga uzushi wa ijtihad pale alipokuwa na umri wa miaka thelathini na miwili na aliitangaza kidhahiri pale alipokuwa na umri wa miaka arobaini.

 

As-Sayyid Ahmad ibn Zaini Dahlan, Mufti wa Makkah, akielezea katika somo la Al-fitnat al-Wahhabiyya (kitabu cha Al-Futuhat al-Islamiyya) kuhusu imani za Uwahhabi na dhuluma na maafa zinazowapata Waislamu kutoka kwa Mawahhabi. Yeye anaandika:  Ili kutaka kuwadanganya ma’ulamaa wa Ahl as-Sunnah katika miji ya Makkah na Madinah, wao waliwatuma watu wao katika miji hizo, lakini watu wao walishindwa kujibu maswali ya Maulamaa wa Kiislamu. Imekuwa dhahiri kuwa wao kwa hakika walikuwa ni wazushi majahili. Kulipitishwa sharia ikiwasema kuwa ni makafiri na kuenezwa kila mahala. Shariff Mas’ud ibn Sai’d, Amir wa Makkah, aliamrisha kuwa Mawahhabi watiwe mahabusu. Baadhi ya Mawahhabi walikimbilia Dar’iyya na kuelezea yale yaliyowapata.”

 

Maulamaa wa Hijaz, wanaotokana na Madhehebu yote manne, akiwemo Sulaiman ndugu yake Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab  na waalimu wake waliokuwa wamemfundisha, walivisoma vitabu vya Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab  na wakatayarisha katika sura ya vitabu majibu ya maandiko yake, yenye kuleta utenganishi na kuidhuru Islam, kwa ajili ya kuwatanabahisha Waislamu, wajitahadhari na kujitenga na upotoshi wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab.

 

Kwa hakika vitabu hivi havikuweza kusaidia zaidi na badala yake ziliongeza hasira na chuki za Mawahhabi dhidi ya Waislamu na kumzuzua zaidi Muhammad ibn Sa'ud awashambulie Waislamu na kusababisha umwagikaji mwingi wa damu. Yeye alitokana na kabila la Bani Hanifa, kabila ambalo alitokamo mzushi wa Utume Musailamat al-Kadh-dhab. Muhammad ibn Sa'ud alikufa katika mwaka 1178 (1765), na hivyo kwa mujibu wa katiba waliyokuwa wametunga, mwanake ‘Abd al-‘Aziz alimrithi.  ‘Abd al-‘Aziz aliuawa kwa kupigwa kisu tumboni, katika msikiti wa Dar’iyya katika mwaka 1217 (1803). Na hapo mtoto wake Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz ndiye aliyekuwa chifu wa Mawahhabi.  Hawa wote watatu walijitolea kimabavu kama kwamba walikuwa wakishindana, katika kumwaga damu ya Waislamu ili waweze kuwadanganya na kuwapotosha Waarabu na kueneza Uwahhabi.

 

Mawahhabi wanadai kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa akihubiri mawazo yake kwa ajili ya    kujipatia utukufu katika imani yake katika upweke wa Allah swt na kuwakomboa Waislamu wasitumbukie katika Shirk.  Wao wanadai kuwa Waislamu wamekuwa wakitenda dhambi la Shirk kwa karne sita mfululizo na hivyo yeye alikuja kuirejesha upya dini ya Waislamu. Yeye anazitoa Ayah za Qur’an Tukufu nambari 5 ya Surah al-Ahqaf, Ayah 106 surah  Yunus, Ayah 14 sura al-Ra’d ili kwamba Waislamu wote wakubaliane na mawazo yake. Hata hivyo, zipo Ayah nyingi kama hizo, na Maulamaa wanasema kuwa hizo Ayah zimekuwa zikiwazungumzia makafiri waliokuwa wakiabudu miungu na masanamu au waliokuwa washirikina.

 

Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, Mwislamu anakuwa Mushrik pale anapoomba kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. , au kwa Mtume a.s. mwingine, au wali au mcha Mungu karibu na kaburi au mbali kutoka hapo, yaani, iwapo anapomwomba msaada wa kutokana na shida aliyonayo, au anapoomba kutetewa mbele ya Allah swt kwa kutaja jina  lake au anapotaka kuzuru kaburi lake.  Allah swt anatuambia  kuhusu makafiri wanaoabudu miungu na masanamu katika Ayah ya tatu ya surah al-Zumar, lakini Mawahhabi wanaonyesha Ayah hii kama ndio waraka wa kuhalalisha utumiaji wao wa neno la Mushrik kwa ajili ya Waislamu waombao kwa kuwaweka Mitume a.s. au Mawalii kama ndio watu walio baina yao na Allah swt.  Wao wanasema kuwa hata Mushrik waliokuwa wakiabudu miungu pia awaikuwa wakijua kuwa vyote vilikuwa vimeumbwa na Allah swt. Wao wanasema kuwa Allah swt amebainisha:  Na kama ukiwauliza, Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema, Allah (Surah Ankabut, ayah ya 61na Sura Zukhruf, Aya ya 87 ). Wao wanadai kuwa hao Mushrik walikuwa hivyo makafiri Mushrik si kwa sababu walikuwa wakiamini hivyo bali wao walizungumza kama ilivyosemwa katika Ayah ya 3 ya Surah az-Zumar: Wale wanaofanya marafiki na wale  mbali na Allah wanasema, “Wao wanatusaidia kutufikisha karibu (ya Allah swt) kwa kututetea mbele  Allah’”  Wao wanadai kuwa Waislamu wanaoomba katika makaburi ya Mitume, ma-Awliya’ kwa utetezi na misaada basi wanakuwa Mushrik kwa kusema hivyo.

 

Ni jambo la kipumbavu kabisa kwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab kuwasema Waislamu wanakuwa makafiri na Mushrik kwa Ayah hiyo. Kwa sababu, makafiri wanawaambudu masanamu ili kwamba ni masanamu hayo tu ndiyo yatakayowasaidia kuwatetea wao; wao wanamwacha Allah swt  na badala yake wanakluwa na imani moja tu ya kuwaomba miungu na masanamu hiyo kuwa watetezi wao.  Lakini ni uhakika uliyo bayana kuwa Waislamu kamwe hawawabudu Mitume a.s. au Ma-Awliya’ lakini wanayo imani kuwa kila kitu kinatoka kwa Allah swt. Sisi tunapenda kuwa hao ma-Awliya’ wawe ni Wasila wetu.  Makafiri wanaamini kuwa miungu na masanamu yao inawaombea chochote kile wakitakacho na kumfanya Allah swt kuwatimizia chochote kile wakitakacho.

 

 Wakati ambapo, Waislamu wanaomba msaada  wa Awliya’ ambao wanawajua kuwa hao ndio watumwa wapenzi  wa Allah swt, kwa sababu Allah swt ameahidi katika Qur’an tukufu kuwa Yeye atawaruhusu waja wake wapenzi kuwatetea na atakubali utetezi wao na Sala na kwa sababu Waislamu wanaamini ubashiri mzuri katika Qur’an. Kamwe huwezi kulinganisha baina ya kafiri anayeabudu miungu na masanamu na Waislamu wakiomba msaada wa Awliya’.  Waislamu na Makafiri wote ni binadamu  kwa  miili, na wanafanana kwa kuonekana, lakini Waislamu ni marafiki wa Allah swt na watakuwa Peponi kwa milele wakati ambapo Makafiri ni maadui wakubwa wa Allah swt  na watakuwapo kwa milele katika Motoni.  Kujionesha kwao hakumaanishi kuwa watabakia vivyo hivyo daima.  Wale wanaowaabudu masanamu na miungu ambao ndio maadui wakubwa wa Allah swt, yatawafikisha hadi kuingia Jahannam. Lakini wale wanaowafanya marafiki wa Allah swt kuwa marafiki wao, basi Allah swt atawabariki na kuwarehemu.  Ipo Hadith isemayo: Rehema za Allah swt zinateremka pale waja wake wapenzi wanapotajwa, nayo pia inatuonyesha kuwa Allah swt ataonyesha rehema zake na misamaha yake pale Mitume a.s. na Awliya’  wanapoombwa.

 

Waislamu wote kwa pamoja wanatambua waziwazi kuwa Mitume a.s. na Awliya'  si watu wa kuabudiwa na wala si washiriki wa Allah swt.  Waislamu wanatambua vile vile kuwa wapo waja wa Allah swt ambao hawastahili kuombwa na papo hapo wapo waja wengineo ambao maombi yao hukubaliwa Kwake.  Katika surah Maidah, Ayah ya 35 tunaambiwa: “Tafuteni Wasila wa kunifikia Mimi” Allah swt anamaanisha kuwa Yeye atakubalia ibada za waja wake halisi na kuwapatia kile wakiombacho.  Tunapata Hadith sharif iliyonakiliwa na al-Bukhari, Muslim na katika Kunuz ad-daqaiq, isemayo: “Kwa hakika, wapo wacha Mungu halisi wa Allah swt ambapo Yeye anawaumbia kile walacho kiapo; kamwe hawasingizii.” Waislamu wanawachukulia Awliya'  kama Wasila na kutegemea maombi na msaada wao kwa sababu wao wanaamini Ayah na hadith za hapo juu.

 

Ingawaje wapo baadhi ya makafiri wanaowaabudu masanamu wakidai kuwa ingawaje masanamu wao si waumbaji lakini Allah swt tu ndiye muumba, hivyo wao wanaamini kuwa masanamu wao wanastahili kuabudiwa kwa sababu masanamu hao wananao uwezo wa kumfanya allah swt awatimizie kile wakiombacho. Wao wanawashirikisha masanamu wao pamoja na Allah swt. Iwapo mtu yeyote atakayemwomba yeyote yule ambaye ameshirikishwa na Allah swt kwa ajili ya maombi yake basi huyo mtu atakuwa kafiri.  Lakini yule asemaye kuwa: “Kwa hakika maombi yangu hayatakubaliwa kwa amri yake. Yeye ni sababu tu. Allah swt anawapenda wale ambao wanaojiimarisha katika njia Yake. Ni yeye anaumba kwa matokeo ya sababu. Mimi namwomba msaada huyu mtu kwa sababu ya kuwa imara katika njia ya Allah swt, lakini nategemea maombi yangu kukubaliwa na Allah swt. Mtume Muhammad s.a.w.w. alikuwa ni mja wake mpenzi na mimi ninazifuata Sunnah zake katika utiifu Wake,” basi atapata thawabu. Iwapo maombi yake yatakubaliwa basi atamshukuru Allah swt; na kama sivyo, basi itabidi aridhike kwa amri ya Allah swt. Kuabudu masanamu na miungu kwa Makafiri si sawa na vile Waislamu wawaombavyo Awliya'  kwa maombi, utetezi na misaada. Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atasema kuwa makundi mawili haya yako sawa bali atasema kuwa makundi haya mawili yapo tofauti kabisa. Hakuna muumba isipokuwa Allah swt pekee.

 

Mushrik na Makafiri, hata hivyo, huwachukulia masanamu wao kuwa ni ilah ( miungu ) au ma’bud ( anayestahili kuabudiwa ) na huwa wanawaabudu ingawaje wao wanatambua waziwazi kuwa masanamu kamwe hawawezi kuwaumbia chochote. Baadhi yao wanakuwa mushrik  kwa kuwachukulia masanamu wao kuwa ni ilah ambapo wengine kwa kuwaabudu au kuwachukulia kama ma’abud.  Watu hao sio Mushrik kwa sababu wanasema kuwa masanamu yao itawatetea na kuwafanya karibu zaidi ya Allah swt, bali wao ni Mushrik kwa sababu wao wanawachukulia kama ma’bud na kwa sababu wanawaabudu.

 

Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, “Utafika wakati ambapo Ayah zilizoteremshwa kuhusu Makafiri zitatumika dhidi ya Waislamu.” na “Ninayo khofu sana kuwa watu watakuja kuzitumia Ayah za Qur’an kwa matumizi ambayo Allah swt hazikubalii.  Hadith hizi mbili  zinadalilisha kuwa watu wasio na dini watatokezea na kuzibandika Waislamu Ayah zile zilizoteremshiwa Makafiri na hivyo kuichezea Qur’an.

 

Waislamu wanazuru makaburi ya wale, wanaowaamini kuwa wanapendwa na Allah swt. Wao wanamwomba Allah swt kwa kuwapitia waja wake wanaopendwa naye. Mtume Muhammad s.a.w.w.  pamoja na ma-Sahaba watukufu pia walifanya hivyo na sisi pia tumeambiwa kufanya hivyo.

 

Mtume Muhammad s.a.w.w. baada ya kumlaza kaburini mama yake na Imam Ali a.s. Fatimah bint Asad na aliomba: “Ewe Mola wangu ! Mrehemu Mama Fatima bint Asad ! Mrehemu mno kwa mapenzi ya Mtume Wako na Mitume waliyokuwa wamenitangulia mimi !”

 

Mtu mmoja kipofu alimwomba Mtume Muhammad s.a.w.w. amwombee duaa ili apone upofu wake. Mtume Muhammad s.a.w.w. alimwambia aombe hivi: “Ewe Mola wangu! Kwa hakika mimi ninakuomba na ninaelekea kwako kupitia kwa Mtume wako Mtume wa Rehma, Ewe Muhammad! Kwa hakika mimi naelekea kwa Mola wangu kupitia kwako katika haja yangu ili ikubaliwe, ewe Mola wangu ! Mfanye Muhammad kuwa muombezi  wangu.”

 

Mtume Adam a.s. aliomba: “Ewe Mola wangu! Naomba nisamehe kwa mapenzi ya mwanangu Mohammad s.a.w.w.!” wakati alipoteremka katika kisiwa cha Serandib (Ceylon) baada ya kula tunda la mti alilokuwa amepigiwa marufuku na Allah swt. Na Allah swt alibainisha: “Ewe Adam ! Mimi ningalikuwa nimekubali utetezi wako iwapo ungekuwa umeomba msamaha kupitia Muhammad kwa ajili ya viumbe vyote vilivyopo duniani na mbinguni.”

 

Umar alimchukua ‘Abbas (r.a.) kwa ajili ya kuomba mvua kwa nia ya kumchukua kama Wasila, na maombi yake yalikubaliwa.

 

Katika historia kuna matukio na habari nyingi zielezeazo ruhusa kuzuru makaburi na kuhusu kuwataja watu waliokwisha kufa kuwafanya Wasila katika kuomba duaa.

 

Muhammad ibn Sulaiman Effendi anadondoa kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa mwovu na aliyepotoka na kwamba alikuwa na tabia ya kutumia Ayah za Qur’an na Hadith visivyotakiwa. Yeye ameandika:“Ewe Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab! Usiwatukane Waislamu ! Mimi ninakushauri kwa kiapo cha Allah swt. Mwambie ukweli yeyote yule asemaye kuwa kuna muumba mwingine mbali na Allah swt!  Msahihishe huyo kwa kumtolea uthibitisho ulio sahihi!  Wasilamu kamwe hawawezi kuitwa Makafiri! Wewe pia u Mwislamu pia.  Inawezekana ukamwita mtu mmoja kuwa ni Kafiri kuliko kuwaita mamilioni.  Kwa hakika ni dhahiri kuwa yeyote yule ajitoaye nje ya jumuiya yake basi anaangukia hatarini. Katika surah an-Nisa, Ayah ya 115 tunaambiwa: “Na atakayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam; napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia.” Kwa hakika Ayah hii inawasema wale waliojitoa katika madhehebu ya Kiislamu.

 

Zipo Hadith nyingi mno zinazoelezea kuwa imeruhusiwa kuzuru makaburi. Ma-Sahaba walikuwa wakiizuru kaburi ya Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa mara nyingi mno kwa ajili ya kutaka kupata baraka, na kumeandikwa makala na vitabu vingi mno juu ya baraka za kuzuru hapo.

 

Kamwe haidhuru kuomba kwa kupitia Mawali’ (Wasila), kuomba kwa kutaja majina yao. Ni imani potofu kuamini kuwa mtu atajwaye atakuwa akimwathiri mwombaji na atamfanyia chochote kile atakacho na atakuwa akijua mambo asiyoyajua.Waislamu kamwe wasituhumiwe kwa mambo kama hayo kwani wao hawaamini hivyo. Waislamu wanaomba kwa kupitia waja wake wapenzi wa Allah swt wawe kama watetezi wao, wawaombee wao. Sifa ya kuumba kile kiombaccchwo ni kwa ajili ya Allah swt tu peke yake na wala hakuna mwingine. Allah swt anawataka waja wake wamwombe Yeye kama vile alivyoamrisha katika Surah al-Maidah, Ayah 27: Allah huwakubalia (ibada,duaa n.k.) wale awapendao. Watu waliokufa hawatakiwi kutimiza kile walichoombwa bali wanakuwa ni watu wa kati kwa Allah swt kuwatimizia kile walichomuomba Allah swt kutimiziwa.  Hairuhusiwi kuwaomba wafu kitu chochote na Waislamu hawafanyi hivyo.  Inaruhusiwa kuwataka wawe watu wa kati katika kutimiziwa maombi yao. maneno Istighatha, Istishfa’ na tawassul vyote hivyo vinamaanisha kuomba kwa Wasila .

 

Allah swt ndiye pekee muumbaji na ni desturi Yake kumfanya  mja wake kuwa Wasila au sababu ya kuumbwa kwa kitu kingine.  Yeyote yule atakaye Allah swt aumbe jambo basi achukue Wasila ambacho ndiccho kitakachokuwa Wasila wa kuumbwa kitu hicho.  Mitume yote imekuwa ikitumia Wasila katika masuala yao.

 

Allah swt anasifia mno matendo ya kutawassuli na vile vile Mitume a.s. pia wametuamrisha hivyo. Matukio ya kila siku  pia yandalilisha umuhimu wake na inambidi mtu ang’angie ili aweze kufanikiwa katika kutimiziwa haja zake.  Ni muhimu kutambua kuwa Allah swt tu ndiye afanyaye hizo sababu  kuwa sababu za vitu, na huziumba baada ya mtu kuzishikilia kwa madhubuti sababu. Mtu yule anayeamini anaweza kusema: “Nimejipatia kitu hiki kwa kutokana na sababu hiyo.”  Sentenso hii haimaanishi kuwa hiyo sababu ndiyo iliyoumba kitu hicho, bali inamaanisha kuwa Allah swt amekiumba kitu hicho kwa kupitia sababu. Kwa mfano, sentenso, “dawa nilizozitumia zimeniponya”;  “ Mgoonjwa wangu amepona baada ya mimi kuchukua nadhiri ya Sayyidat Fatimah”;  “Supu imenikinaisha,” na “maji yametuliza kiu changu,”  vyote hapo vinamaanisha sababu hizo kuwa ni Wasila. Ni muhimu kutambua kuwa Mwislamu asemaye kauli kama hizi huwa anaamini hivyo.  Wale wanaoamini hivyo kamwe hawawezi kuitwa Makafiri. Mawahhabi nao pia wanasema kuwa inaruhusiwa kuoma kitu kutoka wale walio karibu na hai.  Wao wanaomba mmoja kwa mwinginw na hata kuwaomba maofisa wa serikali kwa mambo mengi.; hata kuthubutu kusema kuwa wanawaomba kuwatimizia maombi yao. Kwao ni shirk kuwaomba waliolkufa au waliombali, bali si shirk kuwaomba walio hai. Hata hivyi iwe wazi kuwa Maulamaa wa Dini hii wanasema kuwa si shirk kwa sababu wa pili hayupo na hakuna tofauti baina yao.  Kila Mwislamu anaamini kuwa kile kilicho faradhi ni faradhi na kile kilicho haraamu ni haraamu tu. Na vile vile ni imani yetu ya msingi kuwa Allah swt ndiye muumba pekee na afanyake kwa kudura zake na wala hakuna mwingine anayeumba wala mwenye uwezo kama Allah swt. Iwapo Mwislamu atasema, “Mimi sitasali,” basi itaeleweka kuwa yeye hatasali wakati huo au katika mahala hapo, au kwa sababu amekwisha kusali.Si haki kwa mtu yeyote kumtuhumu kuwa yeye hatasali kamwe.Kwa sababu, kuwa kwake Mwislamu itawazuia wengine wasimwite kafir au Mushrik.  Hakuna mtu yeyeote mwenye haki kumwita Mwislamu ati ni kafiri au Mushrik kwa sababu amezuru makaburi, awaombaye waliokufa kwa msaada na utetezi au asemaye “Maombi yangu kadhaa wa kadhaa yakubaliwe,” au “Ewe Rasulullah! Tafadhali naomba unitetetee mimi !”  Kuwapo kwake Mwislamu kunadalilisha kuwa maneno na matendo yake yote yapo kwa mujibu wa imani iliyokubaliwa, halali na nia.

 

Imani potofu na maandiko ya Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab yatavunjika na kukanushwa katika misingi yake kwa nguvu za ufahamu na uamuzi kwa kutokana na maelezo yafuatayo. Katika kuongezea, kwa hakika kumeandikwa vitabu[1] vingi mno kwa kuthibitisha kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa ni mtu aliyepotoka, amewatukana Waislamu na amefanya njama zake zote za kuungamiza Uislamu undani mwake.  Sayyid ‘Abd ar-Rahma (r.a.), Mufti wa Zabid, Yemen, ameandika kuwa itatosheleza kabisa kuandika Hadith ifuatayo ili kumthibitishia yeye kuwa alikuwa amepotoka: “Baadhi ya watu watatokezea Mashariki mwa bara la Arabia. Wao watasooma Qur’an tukufu. Lakini Qur’an tukufu haitawashuka kooni mwao. Wao wataiacha Islam kama vile mshale unavyouacha upinde. Wao wananyoa nyuso zao.” Nyuso zao kunyolewa inamaanisha waziwazi kuwa ni wale watu ambao wanasemwa kupotoka ni wafuasi wao.  Hakuna haja ya kupekua vitabu vingine baada ya kuisoma Hadith hii.  Imeamriwa katika kitabu cha Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab  kuwa wafuasi wake wanyoe ngozi ya kichwa pamoja na nywele na pembeni za uso.  Amri kama hii haipatikani katika madhehebu zote sabili na mbili za Kiislamu.

 

MWANAMKE AMNYAMAZISHA IBN ‘ABD AL-WAHHAB

 

Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab vile vile aliwatolea wanawake amri ya kunyoa nywele zao zote. Alitokezea mwanamke mmoja, kwa ujasiri akamwambia: “Nywele ni pambo muhimu kwa mwanamke kama vile ilivyo ndevu kwa ajili ya mwanamme. Je amri hii inataka kuwafanya wanaadamu wajinyime opambo walilojaaliwa na Allah swt ?”  Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab  hakuweza kumjibu mwanamke huyo.

 

Ingawaje kuwa mambo maovu mengi katika imani potofu za Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, zipo imani tatu kuu:

1. Yeye amefundisha kuwa  matendo yanafanya sehemu ya imani na yeyote yule anayepuuzia faradhi (kwa mfano, hajatimiza sala mara moja kwa sababu ya uvivu au hajatoa Zaka kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu ya  ubahili, ilhali anajua kuwa sala na zaka vyote hivyo ni faradhi) basi atageuka kuwa kafiri, na lazima auawe na mali yake yote igawiwe miongoni mwa Mawahhabi.

 

2. Wao wanaamini kuwa ni tendo la shirk kuwafanya Wasila Mitume a.s. na Awliya'’ na kuomba kwa kupitia wao kwa ajili ya kutimizika haja yake au kuwa katika hali ya amani dhidi ya khofu. Wao wanasema kuwa ni haramu kabisa kukisoma kitabu cha sala kiitwacho Dala’il al-Khairat.

 

3. Wao wanasema kuwa ni ushirikina kwa kujenga  misikiti karibu na makaburi ya watu wema, kuwasha taa au vibatari katika misikiti hiyo kwa ajili ya wale wafanyao ibada au kwa kutoa misaada kutoa nadhiri ya kuchinja mnyama kwa ajili ya watu waliokufa. Kwao kila mojawapo la tendo hilo ni katika sura ya ‘ibada ya mtu sambamba na Allah swt.

 

Makaburi yote ya Ahl al-Bayt a.s.,Masahaba wote, ma Awliya'’ na Mashahidi yaliteketezwa isipokuwa lile la Mtume Muhammad s.a.w.w. wakati Sa’us ibn ‘Abd al-Aziz alipoishambulia Makkah na Madinah.Makburi hayakuweza kutambuliwa. Ingawaje wao wamejaribu hila zao za kutaka kuteketeza kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w., kwani wale waliokuwa wameinua mapanga na mashoka, waligeuka kuwa wehu au walipooza miili yao, na hivyo hawakuthubutu kutenda maovu yao hayo. Wao walipoishika Madinah,Ibn Sa’ud aliwakusanya Waislamu na akiwa tuhumu alisema:“Dini yenu kwa sasa imekamilshwa na Mawahhabi na Allah swt ameridhika nanyi.  Wazazi wenu walikuwa makafiri na mushrik. Kamwe musiifuate dini yao! Waambieni watu wote kuwa wao walikuwa ni makafiri. Imeharamishwa kusiomama mbele ya kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. na kuomba. Nyie munaweza kusema: “As-salaamu ‘ala Muhammad” wakati mpitapo katika msikiti. Hamuruhusiwi kuomba utetezi wake mbele ya Allah swt.”

 

(2) MISHENI YA KWANZA YA MAWAHHABI

'Abd al- Aziz ibn Muhammad , ambaye amewaua kikatili Wailsamu wengi kupita kiasi kwa kuueneza Uwahhabi, aliwatuma Mawahhabi watatu kwenda Makkah katika mwaka 1210 A.H. (1795).  Maulamaa wa Ahl as-Sunna walikabiliana nao kwa kuwatolea Ayah za Qur’an Tukufu na Hadith sharifu kiasi kwamba Mawahhabi hao wawakilishi hawakuweza kujibu vyovyote vile. Wao hawakuwa na lolote lile la kuzungumzia isipokuwa kukubaliana na ukweli mtupu uliojitokeza mbele yao.  Hao wawakilishi wa ki-Wahhabi waliandika ilani ndefu mno na kuzitia sahihi zao kuwa Ahl as-Sunna wapo katika njia ya haki na kweli na kwamba wao watatu walikuwa katika njia iliyopotoka, njia ya wendawazimu.  Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba kiongozi wao ‘Abd al-Aziz hakukuyatia maneno ya viongozi wake wa kidini yenye nasiha kwake  masikioni mwake kwani yeye alichokuwa akikitaka ni matakwa yake ya kisiasa na alikuwa amekwishaufanya roho yake kwa ajili ya uchifu. Yeye aliongezea kuwatesa Waislamu siku baada ya siku nyuma ya pazia la kidini. Kwa hakika Waislamu waliangamizwa na kuteketezwa kwa uwezo wake wote.

 

Mawahhabi hao watatu waliweka hoja ishirini za kuwashawishi Waislamu wakazi wa Makkah.  Hoja zao hizo ishirini zimegawanyika katika makundi hayo matatu tuliyoyazungumzia. Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alisema kuwa ni Ijtihad ya Imam Ahmad ibn Hanbal, kuwa ibada ni sehemu ya imani. Hatahivyo, Ijtehad zote za Imam Ahmad ibn Hanbal zilikuwa zimerekodiwa katika vitabu na Maulamaa wa Makkah walikuwa wakizijua zote, hivyo wao waliweza kwa urahisi mno kuwashawishi Mawahhabi hao watatu kuwa shutuma za Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab zilikuwa za uongo na potofu.

 

Mawahhabi hao watatu walikuwa na uhakika kuwa imani ya Maulamaa wa Ahl as-Sunna yalikuwa ni sahihi nao hata walithubutu kusema: “Waislamu wa Makkah wanazuru makaburi ya Mtume Muhammad s.a.w.w., ‘Abdullah ibn Abbas na Mahjub ( Mahjub Sayyid ‘Abd ar-Rahman, alikuwa ni ‘Alim mashuhuri katika zama zake, alifariki katika mwaka 1204 A.H. (1790) na alizikwa katika makaburi ya Mu’alla (makaburi ya Maqureishi) ) na huwa wakisema: ‘Ewe Rasul - Allah !’ au ‘Ewe Ibn ‘Abbas!’ au ‘Ewe Mahjub!’ Hatahivyo, kwa mujibu wa ijtihad ya Imam wetu Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, wale wasemao ‘La ilaha Illallah Muhammadun Rasulullah,’ lakini wanawaomba watu wengine hugeuka kuwa makafiri.  Hivyo ni halali kuwaua na kuzichukua mali zao zote.” Maulamaa wa Ahl as-Sunna waliwajibu: “Kuzuru makaburi ya waja wapenzi wa Allah swt kwa ajili ya kuwafanya tawassul au kuwaomba watuombee, haimaanishi kuwa wao wanaabudiwa. Wao wanapowazuru, hapakuwi na nia ya kuwaabudu bali ni kwa madhumuni ya kumwomba Allah swt wawe wasila, yaani, kuwapitia na kuwafanya watetezi.” Na wao walitoa hoja zao kwa vithibitisho kuwa imeruhusiwa na vile vile ni muhimu kuwachukua hao kama ndio sababu.

 

Zipo dalili na uthibitisho mwingi wa uhalali wa kuzuru makaburi ya Awliya'  kwa ajili ya kuwafanya wasila au kuwaomba wawe wasila wakati wa kumwomba Allah swt hoja zetu: Ayah ya 35 ya Surah al-Maidah inasema, “Enyi Waumini ! Mwogopeni Allah natafuteni Wasila wa kunifikia Mimi !” Vitabu vyote vya tafsiri vinaandika chochote au yeyote apendwaye au akubaliwaye na Allah swt huwa wasila. Ayah ya 80 ya Sura an-Nisa’ inasema: “Yeyote amtiiaye Rasul basi amemtii Allah.”  Hii ni sababu  kwa nini wasila katika Ayah iliyotangulia ni Rasulullah kwa mujibu wa maulamaa’ wengi wa Kiislam. Kwa hivyo, inaruhusiwa kufanya wasila wa Mitume a.s. na warithi wao – Awliya' na waja halisi Waislamu – na kujaribu kumkaribia Allah swt kwa kuwapitia hao. Iwapo ingalikuwa ni ukafiri au ushirikina kwa kuwataja au kuwaomba, wale ambao husali basi wote kwa pamoja watakuwa makafiri; basi  Mawahhabi pia watakuwa makafiri kwa mujibu wa taarifa ya hapo juu – kama ilivyonakiliwa fatwa ya Muhammad ibn Sulaiman, kwani kila Mwislamu anatuma salaam juu ya Rasulullah na dua kwa ajili ya mtukufu Mtume s.a.w.w. katika kila sala kwa kusoma”As-salaamu ‘alaika ayyuhan Nabiyyu wa rahmat-Allah.”

 

Zipo faida nyingi mno kwa kuzuru makaburi na kumwomba Allah swt kwa kuwafanya Awliya' kama wasila. Kwa sababu Hadith iliyotolewa na Ibn ‘Askari na kunakiliwa katika Kunuz ad-daqaiq inasema, “Mwislamu ni kioo cha Mwislamu ndugu yake.”Tunaelewa kutokana na Hadith hiyo kuwa roho ya Mwislamu mmoja ni kioo cha Mwislamu mwingine. Hivyo zinaonekana ndani mwao. Uwema unatoka kutoka roho ya walii kuingia katika moyo wa  yule mtu ambaye anayemfikiria na kuwa wasila wake wakati wa kulizuru kaburi la wali huyo. Roho iliyo dhaifu inapata nguvu. Huu ni mfano wa vyombo viliwi vinavyounganishwa kwa bomba. Roho iliyo na nguvu au cheo cha juu ndiyo inayopungukiwa.  Iwapo roho ya yule aliye kaburini itakuwa dhaifu basi roho ya aliyemzuru itakuwa imeudhika.Na hii ndiyo sababu kuu ya kuharamishwa kuzuru makaburi hapo katika kipindi cha mwanzoni cha Islam, kwa sababu  makaburi hayo yalikuwa ni ya watu wale waliotoka katika kipindi cha ujahili wakati huo.  Baada ya muda ilitolewa ruhusa kuzuru makaburi kwa sababu palikuwa pamezikwa Waislamu. Mtu atakuwa akifikiria Mtume Muhammad s.a.w.w. au wali atakapokuwa akizuru kaburi lake.  Ipo Hadith sharifu isemayo: “Allah swt huonyesha rehema wakati waja Wake watukufu wanapofikiriwa.” Hivyo imeeleweka kutokana na Hadith hii vile vile kuwa Allah swt humpelekea rehema mtu anayezuru makaburi, na Yeye huzikubalia sala za waja Wake wale ambao huteremshiwa rehema Zake.Hivyo kusema kidhahiri kuwa:“Makaburi yasitembelewe. Awliya' hawawezi kuchukuliwa kama wasila,”  ni maoni yanayotakiwa kupuuzwa. Ipo Hadith tukufu isemayo: “Yeyote yule anayezuru kaburi langu baada ya kutimiza faradhi za Hijja basi atakuwa kama ametembelea mimi pale nilipokuwa hai,” inakanusha imani hii katika misingi yake na hivyo kuonyesha umuhimu wa kuzuru makaburi.  Hadith hii imetolewa kutoka Kunuz ad-daqa’iq.

 

Mawahhabi  nao wanaleta mbele Hadith: “Wanalaaniwa wale wanawake ambao huzuru makaburi na wale wafanyao sala makaburini na wale ambao huwasha mishumaa juu ya makaburi,”  kama kisingizio cha kubomoa makaburi ya shakhsiyyah watukufu.  Wao vile vile wandai kuwa mambo kama hayo hayakuwapo katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w.  na wanatoa Hadith ifuatayo, “Mambo ambayo hayapo katika zama zetu lakini yataletwa mbeleni na wala musiyanasabishe kwetu.” Wawakilishi wa Mawahhabi walikubaliana na Maulamaa wa Ahl as-Sunna kwa sababu majibu ya dai lao la pili yalikanusha madai yao.

 

(3) WAISLAMU WA TA’IF WAPORWA NA KUUAWA

Wakati Maulamaa wa Ahl as-Sunna walipowanyamazisha Mawahhabi katika mwaka 1210 A.H. (1796), Maulamaa wa Makkah walitayarisha waraka na kutia sahihi zao  ambamo waliandika Ayah za Qur’an Tukufu pamoja na Hadith sharif kwa kuthibitisha kuwa Uwahhabi ni njia iliyo tofauti na mbali na Islam, mtego wa hila na njama zilizotengenezwa na maadui wa Islam kwa ajili ya kuuteketeza Uislam undani mwake.  Mawahhabi wale watatu waliokuwa wametubu kwa upotofu wao, walihakikisha na kuthibitisha waraka huo. Nakala za azimio hilo zilitumwa katika nchi zote za Kiislamu.

 

Baadhi ya Mawahhabi wa Makkah walimwendea ‘Abd al-‘Aziz, mtawala huko Darr’iyya, na kumwelezea kuwa wawakilishi wao hawakuweza kuwakabili Maulamaa wa Makkah na kwamba waraka wa azimio lao kuwa Uwahhabi ulikuwa ni upotofu na njama dhidi ya Islam, zimepelekwa kila nchi ya Kiislam.  ‘Abd al-‘Aziz ibn Muhammad ibn Sa’ud na wafuasi wake, waliingiwa na hasira kali kabisa dhidi ya Ahl as-Sunna, waliishambulia Makkah katika mwaka 1215. Amir wa Makkah, Sharif Ghalib ibn Musa’id ibn Sa’id Effendi, aliwakabili vikali. Damu nyingi ilimwagika pande zote mbili.  Sharif Ghalib Effendi hakuwaruhusu hao kuingia Makka, lakini makabila ya Waarabu kuzunguka Makkah walikubali Uwahhabi. Baina ya Idi mbili za mwaka huo huo, Sa’ud alituma jeshi katika mji wa Ta’if. Huko wao waliwatesa na kuwachinja ovyo Waislamu wanawake na watoto wa Ta’if. [2]

 

Mateso na mauaji ya Ta’if wakiwemo wanawake na watoto yalifanyika kwa amri ya adui mkubwa wa Islam, brigadia mwovu kabisa aliyekuwa akiitwa ‘Uthman al-Mudayiqi. Mtu huyu na Muhsin walikuwa wametumwa na Sharif Effendi kwenda Dar’iyya ambapo walitakiwa kuzungumzia mapatano ya awali ya kuwazuia Mawahhabi wasiizingire Madina na kutowatesa Waislamu. Lakini mnafiki huyu alikuwa ni jasusi kwa Sharif Effendi.Yeye alimhadaa mwenzake Muhsin, wakati wanaelekea Dar’iyya kuwa angeliweza kumpatia mafanikio mengi.  Hao wawili  walitoboa siri zao kwa Sa’ud  ibn ‘Abd al-‘Aziz  huko Dar’iyya. Sa’ud,  alipowatambua kuwa wao walikuwa watumwa wake watiifu, aliwaweka waporaji chini ya ukamanda wao.  Wao walikwenda hadi mahala paitwapo  Abila karibu na Ta’if na huko wakampelekea Sharif Ghalib Effendi barua kuwa Sa’ud na wao, wasaliti hao wawili, walikuwa hawatambui uhalali wa maptano ya hapo awali na kwamba Sa’ud alikuwa akijitayarisha kuuzingira mji wa Makka. Sharif Ghalib Effendi aliwajibu katika lugha laini akiwashauri, lakini ‘Uthman mkatili, alikuwa kwa hakika adui mkubwa wa Islam, alizichana barua. Yeye aliwashambulia Waislamu waliokuwa wametumwa na Amir na kuwaghalibu.. Ilimbidi Sharif Ghalib Effendi alirudi hadi ngome ya Ta’if na kuchukua hatua za kujihami. Huyu Mwahhabi katili aliweka kambi za majeshi yake huko Malis karibu na Ta’if mwishoni mwa mwezi wa Shawwal katika mwaka 1217 A.H. (1802). Yeye vile vile alioomba msaada kutoka mkatili Amir wa Bisha, Salim ibn Shakban, ambaye alikuwa na roho katili kuliko jiwe lililojaa uadui dhidi ya Uislamu. Kulikuwapo na tawala za kifalme takriban ishirini katika majangwa na kila falme alikuwa na kikosi cha Mawahhabi mia tano zaidi ya kikosi cha Salim mwenyewe kipatacho elfu moja.

 

Wakazi wa Ta’if wakiongozwa na Sharif Ghalib Effendi, waliwashambulia majeshi ya Mawahhabi huko Malis.  Alifanikiwa kuwaua waporaji elfu moja na mia tano wa Salim ibn Shabkan. Salim pamoja na wafuasi wake walitoroka Malis.  Lakini walikusanyika na wengine na kurejea kuishambulia Malis na waliupora mji mzima. Sharif Ghalib Effendi alikwenda Jeddah kutafuta msaada wa kijeshi. Wakazi wengi wa Ta’if walikuwa wamejaa kwa khofu na walitoroka kwa kisiri siri pamoja na vitu vyao vya majumbani.  Ingawaje wale wakazi wa Ta’if waliokuwa wamejisitiri katika ngome, waliweza kuwashinda majeshi madogo madogo ya Mawahhabi waliokuwa wakijaribu kuwashambulia, wao walipeperusha bendera nyeupe ya kutaka usitihwaji wa vita baina yao kwani Mawahhabi walikuwa wakimiminika majeshi mengi. Wao walikubali kujisalimisha kwa masharti kwamba maisha na heshima zao hazitadhuriwa. Ingawaje maadui pia walikuwa wamekwisha nguvu na kudhoofika kwani nao pia walipata pigo kubwa la kuuawa na wengi walitoroka kutoka majeshi yao na walidhoofika pia, akatokea mwakilishi wa wakazi wa Ta’if, ambaye alikuwa mwovu na msaliti mkubwa, ingawaje alikuwa akiwaona Mawahhabi wanatoroka kwa kukimbia hapo, aliwapigia sauti kubwa kwa kuwaambia, “Sharif Ghalib ametukimbia kwa kuogopa! Na hivyo wana-Ta’if hawana nguvu ya kukabiliana nanyi ! Wao wamenituma kuwaleteeni habarri kuwa wao wapo tayari kujisalimisha na kuisalimisha ngome nzima mikononi mwenu na wanawaombeni muwasamehe. Mimi ninawapenda Mawahhabi. tafadhalini rudini! Nyinyi mumemwaga damu nyingi kupita kiasi na haitakuwa jambo la busra kwenu nyinyi kurudi bila ya kuikamata Ta’if. Ninaapa kuwa wana-Ta’if watajisalimisha wao na ngome hiyo. Wao watakubalia chochote kile mutakacho nyinyi.”  Kwa hakika lilikuwa ni kosa la Sharif Ghalib Effendi katika kuipoteza Ta’if bila maana.  Iwapo angalikuwa amebakia Ta’if pamoja na Waislamu, basi isingalifika maafa hayoo. Kwa sababu waporaji ni waoga, Mawahhabi hakudhani kuwa wana-Ta’if watajisalimisha vile kirahisi. Lakini walipoona bendera ya kutaka amani juu ya ngome, walimtuma jasusi kuja kujua hali halisi iliyokuwapo ndani mwa ngome. Wana-Ta’if walimvuta ndani kwa kamba huyo mjumbe. Mjumbe huyo aliwaambia: “Kusanyeni mali zenu zote hapa na mujisalimishe kama munataka kuishi hai.” Mali zao zote zilikusanywa na kurundikwa mahala pamoja kwa msaada wa Mwislamu mmoja aliyekuwa akiitwa Ibrahim. Mjumbe huyo alisema: “kwa hakika hii haitoshi.” Aliendelea kuseam kuwa “Sisi kamwe hatuwezi kuwasameheni kwa haya tu, lazima mulete zaidi na zaidi!” Yeye aliwapa daftari na kuwaambia “orodhesheni majina ya wale wanaokataa kutoa mali zao! Wanaume wapo huru kwenda popote pale watakapo isipokuwa wanawake na watoto watafungwa kwa minyororo.” Kwa hakika wote kwa pamoja walimwomba awe mlaini mwenye huruma kidogo, basi yeye aliongeza udhalimu na uovu wake.  Ibrahim, alishindwa kuvumilia zaidi ya hapo na hivyo alimpiga kifuani kwa jine na kumwua. Wakati malumbano haya yanaendelea, Mawahhabi waliishambulia na ngome hiyo na hivyo waliweza kukwepa kulengwa mizinga na risasi. Wao walibomoa milango na kufanikiwa katika kuingia ndani ya  ngome.  Mawahhabi waliwaua wanawake, wanaume na watoto wote waliowaona na hata kuthubutu kuwaua watoto wachanga waliokuwa katika masusu yao.  Mitaa ya mji ilijaa kwa mito ya damu. Wao walishambulia kila nyumba na kupora vyote vilivyokuwamo na popte pale walichokipata, wakawa wakishambulia kama vichaa na kikatili hadi usiku ulipoingia.  Wao hawakuweza kuzichukua nyumba za mawe upande wa mashariki wa ngone, hivyo walizishambulia nyumba hizo kwa risasi. Mlaghai moja wa Kiwahhabi  alipiga kelele: “Sisi tunawasameheni! Munaweza kwenda popote pale mupendapo pamoja na wake na watoto wenu,” lakini wao waliyapuuzia bila kujali. Wakati huo Mawahhabi waliwakusanya watu, ambao walikuwa wakijitayarisha kuondoka na kuhama, juu ya mlima na kuzizunguka zile familia halisi wa Waislamu, ambao wamekua katika mapenzi na udugu na wengi wao walikuwa ni wanawake na watoto, na kuwaweka wakafa kwa njaa na kiu kwa muda wa siku saba, na kuwatesa mno kwa visingizio, kupiga mawe na vitisho vya aina mbalimbali. Mawahhabi walimwita mmoja baada ya mwingine na kuwapiga na kuwauliza: “Tuambieni pale mulipoficha mali zenu !” na walipiga makelele, “Siku yenu ya kufa inawadia!” kwa wale walioomba msamaha.

 

Ibn Shakban, baada ya kuyakamdamiza majumba hayo ya mawe kwa muda wa siku kumi na mbili bila ya kufanikiwa kuyabonyeza,  aliahidi kuwa wale wote watakaotoka nje ya nyumba zao na kujisalimisha pamoja na silaha zao, basi watasamehewa. Kwa hayo, Waislamu walimwamini na kutoka nje, lakini, wakiwa wamefungwa mikono yao migongoni mwao, wao waliburutwa na Ibn Shakban hadi juu ya mlima pale ambapo walikuwapo Waislamu wengine waliokuwa wameshikiliwa. Waislamu mia tatu na sitini na saba, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto (Allah swt awarehemu) wote kwa pamoja walichinjwa chinjwa mlimani hapo.  Mawahhabi waliwaachia wanyama wao wawakanyage Waislamu hao na hatimaye kuwaacha hapo bila ya kuwazika ili waliwe na ndege wa kuwinda kwa muda wa siku kumi na sita. Wao walifanya hujuma kubwa ya kupora mali za Waislamu katika kila nyumba, na waliweza kukusanya mali nyingi mno mpaka kukutokea kama mlima mbele ya lango la ngome hiyo na walimtumia Sa’ud asilimia ishirini ya yale yaliyoporwa na iliyobakia waligawana miongoni mwao. Wadhalimu na nvua za masika zilizoa mapesa na vito vya thamani mno na hapo kulibakia kiasi cha rial za dhahabu elfu arobaini tu, katika mikono ya Ahl as-Sunna; kiasi cha rial elfu kumi ziligawiwa miongoni mwa wanawake na watoto, na vitu viliuzwa kwa bei ndogo kabisa.

 

Mawahhabi walizichana nakala za Qur’an tukufu na vitabu vya tafsir, Hadith na vitabu mbalimbali vya Kiislamu walivyovichukua kutoka maktaba, misikiti na majumbani mwa watu, na kuvitupa huku na huko. Wao walithubutu hata kutengenezea viatu kwa ajili miguu yao michafu vya majalada ya dhahabu ya Qur’an na vitabu vinginevyo. Kwa hakika zilikuwapo zimeandikwa Ayah tukufu za Qur’an juu ya majalada hayo. Majani (makurasa) ya Qur’an tukufu zilikuwa zimetupwa ovyo mitaani mwa mji wa Ta’if kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata nafasi ya kuuweka mguu juu ya ardhi ya mji wa Ta’if.  Ingawaje inasemekana kuwa Ibn Shakban alikuwa ametoa amri ya kutokuzichana nakala za Qur’an Tukufu, lakini hao Mawahhabi waporaji wa majangwani hawakujua Qur’an ni nini, na hivyo walizichana chana nakala zote walizozipata na kuzikanyaga kanyaga ovyo. Inajulikana kuwa ni nakala tatu tu za Qur’an Tukufu na nakala moja tu ya Sahih al-Bukhari ndizo zilizo salimika kutokana na hujuma na uporaji wa Mawahhabi katika mji  mkubwa wa Ta’if.

Muujiza

Hali ya hewa ilikuwa shwari wakati wa kushambuliwa kwa mji wa Ta’if. Kulikuwa hakuna upepo. Kulitokea kwa tufani kali baada ya waporaji kuondoka, na ilichukua majani (kurasa) yote ya Qur’an Tukufu pamoja na vitabu vinginevyo na baadaye kutulia. Baada ya kutulia, hapakuwapo na hata karatasi moja iliyobakia juu ya ardhi ya mji wa Ta’if. Hakuna ajuaye zimepeperushwa kwenda wapi.

 

Chini ya jua kali, maiti zote za mashahidi zilioza vibaya sana katika kipindi cha siku kumi na sita. Hali ya hewa kuzunguka mji huo ilikuwa yenye kunuka na kuharibu hewa. Waislamu walimwomba, walilia kilio na kumbembeleza Ibn Shakban awaruhusu kuwazika majamaa zao. Hatimaye aliwakubalia, na hivyo walichimba mashimo mawili makubwa, wakatumbukiza katika mashimo hayo maiti zilizooza za wazazi, mababu, jamaa na watoto wao na kuwafukia kwa udongo. Hakuna maiti hata moja iliyoweza kutambuliwa; baadhi ya miili hiyo ilikuwa imebakia miili nusu au robo tu kwani ndege na wanyama pori walikuwa wamesambaza vipande vya miili hiyo huku na huko.Wao walikuwa wameruhusiwa kuvikusanya vipande hivyo vilivyokuwa vimezagaa huku na huko kwa sababu harufu mbaya ya maozo ilikuwa ikiwabughudhi sana hao Mawahhabi. Kwa hakika Waislamu walikuwa hawana lingine la kufanya isipokuwa ni kutafuta na kuokota vipande vya miili ya watu wao na kuzizika katika mashimo hayo mawili.

 

Kwa hakika tendo hili la kinyama la Mawahhabi la kuacha maiti za Mashahidi zibakie bila kuzikwa hadi kuoza zilikuwa ni hatua ya kulipiza kisasi.  Hapa chini ninawaleteeni mashairi juu ya hayo:

 

    ‘Italeta harufu ya manukato, musisikitike enyi mlioanguka,

      Nyumba haijengwi kabla ya kubomoka.’

 

Hali ya mashahidi (Allah swt awarehemu ) mbele ya Allah swt inaongezeka wakati miili yao inapoachwa kuoza na kuliwa na ndege na wanyama pori. 

 

Maharamia hao waliteketeza kabisa makaburi za ma-Sahaba, Awliya' na Maulamaa baada ya kuwaua Waislamu wa Ta’if na kugawana mali waliyokuwa wamepora. Wao hata walithubutu kulichimba kaburi la ‘Abdullah ibn ‘Abbas, Sahaba mpenzi wa Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa ajili ya kutaka kuchoma moto mifupa yake, lakini waliogopa pale waliponusa harufu ya manukato iliyokuwa ikitokea kaburini wakati walipokuwa wamepiga kwa mara ya kwanza kwa sululu. Wao walisema: “Kuna shetani mkubwa kaburini humu. Hivyo inatubidi kulilipua kaburi hili na mabaruti kuliko kupoteza wakkati wetu katika kulichimba.” Ingawaje wao walijaribu kwa jitihada zao zote kwa kujaribu kulilipua kaburi hilo kwa kuweka unga mwingi wa baruti, lakini  halikulipuka na hivyo waliondoka kwa mshangao. Kaburi hilo liliachwa sawa na ardhi kwa muda wa miaka kadhaa, na hapo baadaye, Sayyid Yasin Effendi aliweka uzio mzuri sana na kulihifadhi kaburi hilo lisisahaulike.

 

Mahramia hao hao wamekuwa wakijaribu mara nyingi mno kufumua makaburi ya Sayyid ‘Abd al-Hadi Effendi  pamoja na Maulamaa wengi, lakini wamekuwa wakizuiwa kufanikiwa katika nia zao mbaya kwa karama (miujiza) tofauti tofauti katika kila kaburi. Walipoona kuwa wao hawafanikiwi katika uovu wao huo, hatimaye waliamua kuacha kuendelea na hamu yao ya kufumua makaburi.

 

‘Uthman al-Mudayiqi na Ibn Shakban vile vile walitoa amri za kubomolewa kwa Misikiti pamoja na Vyuo (Madrassah) viende sambamba na kubomolewa kwa makaburi. Yasin Effendi, mwanachuoni wa Ahl as-Sunna aliwauliza: “Je ni kwa nini munataka kubomoa hata Misikiti ambayo imejengwa kwa ajili ya kufanyia ibada za Allah swt  na kusali sala za Jama’a?  Iwapo nyinyi mwataka kuubomoa Msikiti huu kwa ajili ya kaburi la ‘Abdullah ibn ‘Abbas (r.a) lipo hapa, basi ninawaambieni kuwa kaburi lake liko nje ya Msikiti huu mkubwa. Hivyo, si muhimu kuubomoa Msikiti huu” Kwa maneno hayo, Uthman al-Mudayiqi na Ibn Shakban hawakuwa na jibu lolote. Lakini, Matu, mzindiqi miongoni mwao, alitoa kauli ya kashfa: “Chochote kile chenye kushukiwa na kutuhumiwa ni lazima kiteketezwe.” Kwa hayo Yasin Effendi aliuliza: “Je kuna chochote kile kinachoshukiwa kuhusu Misikiti?” na mhalifu huyo hakuweza kujibu chochote.  Baada ya ukimya mrefu, ‘Uthman al-Mudayiqi alisema; “Mimi sikubaliani na nyote wawili,” na aliamrisha, “Msibomoe Msikiti, teketezeni makaburi !.”

 

(4) UDHALIMU WA MAWAHHABI KATIKA MAKKAH

Ingawaje waovu hawa waliishambulia Makkah baada ya kumwaga damu kwa wingi katika mji wa Ta’if, wao hawakuthubutu kuingia mjini Makkah kwa sababu ulikuwa ni wakati wa Hijja. Sharif Ghalib Effendi alikuwa mjini Jeddah katika kutafuta msaada wa kijeshi ili kuwakabili Mawahhabi, na huku wakazi wa Makkah walikuwa na khofu ya matukio ya maafa ya Ta’if, walituma ujumbe kwa kamanda wa Mawahhabi na walimwomba asiwatese wao. Hivyo Mawahhabi waliingia mjini Makkah katika mwezi Muharram 1218 A.H. ( 1803 ) na walizieneza imani zao za Kiwahhabi. Wao walitangaza hadharani kuwa watawaua wale wote watakao kuwa wakizuru makaburi au watakwenda Madinah kuomba mbele ya kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. Baada ya siku kumi na nne wao waliushambulia mji wa Jeddah kwa kutaka kumteka nyara Shari Ghalib Effendi, ambaye aliwashambulia waporaji wa Kiwahhabi kidhahiri na kwa ujasiri kutokea ngome ya Jeddah na aliweza kuwaua wengi wao, wale waliobakia walitorokea Makkah.  Walipoombwa na wakazi wa Makkah, wao walimteua ndugu yake na Sharif Ghalib Effendi, aitwaye Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi kama amir wa Makkah na kurudi Dar’iyya. Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi aliukubalia uamir kwa ajili ya kuwalinda wakazi wa Makkah kutokana na mateso ya Mawahhabi.

 

Sharif Ghalib Effendi alirejea Makkah pamoja na maaskari wa Jeddah na Gavana wa Jeddah, Sharif Pasha, baada ya siku thelathini na nane kuanzia pale maharamia hao waliposhindwa hapo Jeddah.  Wao waliwatokomeza maharamia waliokuwa wamebakia mjini Makkah, na kwa mara nyingine tena alikuwa Amir.  Maharamia hao walizishambulia vijiji vilivyozunguka mji wa Ta’if na kuwaua watu wengi mno kwa kulipiza kisasi cha Makkah.  Wao walimchagua mharamia ‘Uthman al-Mudayiqi kama gavana wa Ta’if.  ‘Uthman aliwakusanya maharamia wote kuuzunguka mji wa Makkah, alipata kundi kubwa mno, mwaka 1220 ( 1805).  Waislamu wa Makkah kwa hakika waliathirika mno kwa mateso na njaa kwa kipindi cha miezi mingi, na hapakuwapo na hata mbwa aliyebakia kuliwa nyama yake katika siku za mwishoni mwa kuzingirwa.  Sharif Ghalib Effendi alifahamu kuwa kwa wakati huo hapakuwa na suluhisho lingine lolote isipokuwa kuingia katika mkataba pamoja na maadui ili kunusuru maisha ya raia wake.  Yeye aliiusalimisha mji wa Makkah kwa sharti kuwa yeye atabakia kama amir wa mji na kwamba mali na maisha ya Waislamu yatakuwa salama.

 

Maharamia hao waliteka miji ya Madinah na Makkah na walipora vito vya thamani kabisa duniani humu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika Khazinat an-Nabawiyya  (Hazina ya Mtume)  kwa zaidi ya muda wa miaka elfu moja. Wao waliwadharau vibaya sana Waislamu kiasi kwamba hakuna maneno hata ya kuelezea. Baadaye, walirudi Dar’iyya baada ya kumteua mtu mmoj aitwaye kwa jina la Mubarak ibn Maghyan kama gavana wa mji.  Wao walibakia mjini Makkah na Madinah na hawakuwaruhusu Mhujjaji wa Ahl as-Sunna kuingia Makkah kwa kipindi cha miaka saba.   Wao waliifunika al-Ka’aba kwa vipande viwili vya kitambaa vyeusi vikiitwa Qailan. Wao walipiga marufuku uvutaji wa hukah  na waliwatendea vibaya mno wale waliovuta. Wakazi wa Makkah na Madina hawakuwapenda hao na daima walikuwa wakijiepusha nao.

 

Ayyub Sabri Pasha alielezea katika juzuu ya kwanza ya kitabu chake Mirat al-Haramain, kilichochapwa katika mwaka 1301 A.H. (1883), kuhusu mateso waliyoyapata Waislamu wa Makkah kama ifuatavyo:

 

“Mateso waliyoyapata Waislamu katika mji mtakatifu wa Makkah na Mahujjaji, kila mwaka, ni vigumu kuyaelezea kwa undani zaidi.

 

“Chifu wa maharamia, Sa’ud, alikuwa akimwandikia barua za vitisho kila mara amir wa wakazi wa Makkah, Sharif Ghalib Effendi. Ingawaje Sa’ud alijaribu kuuzingira mji wa Makkah kwa mara kadhaa, lakini hakuweza kuingia mjini hadi mwaka 1218 A.H. (1802). Sharif Ghalib Effendi, pamoja na gavana wa Jeddah, waliwakusanya viongozi wa misafara ya Mahujjaji kutoka Damascus na Misri katika mwaka 1217 A.H. na kuwaambia wao kuwa maharamia walikuwa na nia ya kuushambulia mji mtukufu wa Makkah, na iwapo wao watakubali kumsaidia yeye, basi  wao kwa pamojawataweza kumteka Sa’ud, chifu wa maharamia. Kwa masikitiko, ombi lake hilo halikukubaliwa.  hapo, Sharif Ghalib Effendi alimteua ndugu yake Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi, kama amir wa Makkah, aliwatuma kwa Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz wanazuoni watano wa Ahl as-Sunnah, waitwao Muhammad Tahir, Sayyid Muhammad Abu Bakr, Mir Ghani, Sayyid Muhammad ‘Akkas na ‘Abd al-Hafiz al-‘Ajami kama ni kamati ya uwema na kusamehe.

 

“Kwa kujibu, Sa’ud alikwenda Makkah pamoja na majeshi yake. Yeye alimteua ‘Abd al-Mu’in kama ndiye Ofisa Mkuu wa jimbo na aliamrisha makaburi yote yavunjwe, kwa sababu kwa mujibu wa imani ya Mawahhabi, wakazi wa Makkah na Madina hawamwabudu Allah swt na badala yake huabudu makaburi. Wao walidai kuwa wakazi wa miji hiyo miwili watamwabudu Allah swt vile iwapasavyo kama makaburi hayo yatakuwa yamevunjwa. Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, Waislamu wote walikufa  kama makfiri  na mushrik kuanzia mwaka wa 500 A.H. (1106); Islam ya kweli na hakika uliteremshiwa yeye, na hivyo haikuruhusiwa kuwazika wale waliokuwa Mawahhabi karibu au pamoja na makaburi ya mushrik na makafiri, wakimaanishwa Waislamu.

 

“Sa’ud aliishambulia Jeddah kwa ajili ya kutaka kumteka Sharif Ghalib Effendi na alitaka kuiteka Jeddah. LAkini, watu wa Jeddah, bega kwa bega pamoja na majeshi ya Uthmaniyyah (Ottoman) kwa uhodari na ushupavu waliwashinda maadui wao na kuwafanya majeshi ya Sa’ud kutoroka.  Sa’ud aliwakusanya wote wale waliokuwa wakitoroka na kurejea nao mjini Makkah.

 

“Ingawaje Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi alijitahidi kubakia kama rafiki wa Mawahhabi ili kuwalinda Waislamu wa Makkah wasiteswe na kuuawa na Mawahhabi wadanganyifu, lakini waovu hawa walizidisha dhuluma na udhia wa kila aina siku baada ya siku. Kwa kuona maovu ya Mawahhabi yamekithiri kupindukia kiasi, yeye alimtumia ujumbe Sharif Ghalib Effendi  kuwa Sa’ud alikuwa Makkah pamoja na jeshi lake lililopiga mahema katika uwanja wa Mu’alla (makaburi ya Maqureishi )na itawezekana kumkamata Sa’ud iwapo atawashambulia hata kwa kikosi kidogo cha majeshi.

 

“Kwa kuupata ujumbe huo, Sharif Ghalib Effendi aliwachukua baadhi ya majeshi waliokuwa wakijulikana pamoja na Gavana wa Jeddah,Sharif Pasha, na aliwashambulia Mawahhabi wakati wa usiku. Yeye alifanikiwa kuzingira mahema yao, lakini Sa’ud aliweza kutoroka akiwa hai. Majeshi yake yalisema kuwa wao walikuwa tayari kujisalimisha iwapo watasamehewa, na ombi lao hilo lilikubaliwa. Hivyo mji mtukufu wa Makkah ulinusurika na watu makatili hawa. Ushindi huu uliwashtusha mno Mawahhabi waliokuwapo huko Ta’if, ambao nao pia walijisalimisha bila hata ya umagikaji wa damu. Mkatili ‘Uthman al-Mudayiqi alitoroka pamoja na maaskari wake kulekea katika milima ya Yemen. Sharif Ghalib Effendi alipopata habari kuwa Mawahhabi waliotoroka baada ya kushindwa wanafanya vitendo viovu vya unyanyaswaji na kupora mali za wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi, aliwatumia ujumbe Ukoo wa bani Saqif na kuwaamuru ‘Nendeni Ta’if na muwashambulie Mawahhabi! Chukueni chochote kile mukipatacho!’ Hivyo kabila la Bani Saqif waliishambulia Ta’if kwa kulipiza kisasi juu ya waporaji, na hivyo Ta’if pia ilinusurika.

 

“Uthman al-Mudayiqi aliwakusanya majahili, wauaji wa vijiji vya Milima ya Yemenna, pamoja na Mawahhabi aliokuwa akikutana nao akiwa safarini, aliuzingira mji wa Makkah. Wakazi wa Makkah waliathirika kwa taabu na udhia kwa muda wa miezi mitatu. Sharif Ghalib Effendi alishindwa kuondoa hali hiyo kwani alijaribu kwa mara kumi lakini hakufanikiwa. Akiba ya chakula kilitoweka.  Kulitokea mfumuko wa bei, kwani kila kitu kilikuwa ghali mno kiasi kwamba mkate uliuzwa kwa riali tano na siagi riali sita kwa kipande cha ratili 2.8,  na hapo mbeleni hakuwapo mtu aliyeuza chochote.  Waislamu hawakuwa na njia nyingine isipokuwa kuwala paka na mbwa, ambao nao pia walimalizika. Pia ulifika wakati ambapo iliwabidi wale manyasi na majani.  Ulipofika wakati ambapo kulikuwa hakuna chochote cha kula, Mji wa Makkah ulijisalimisha kwa Sa’ud kwa sharti kwamba hatawatesa wala kuwaua wakazi wa mji huo.  Sharif Ghalib Effendi  hakuwa na makosa katika tukio hili, lakini asingalikuwa ameangukia katika swala kama hili lau angalikuwa ameomba kabla misaada ya washirika wake.  Kwa hakika wakazi wa Makkah walimwambia Sharif Ghalib Effendi , ‘Sisi tunaweza kuendelea kuwakabili Mawahhabi hadi utakapofika msimu wa Hijja iwapo wewe utatutafutia misaada kutoka makabila tunayopendana nao, na kwa hakika tutapata ushindi pale Mahujjaji wa Msiri na Damascus watakapo kuja Kuhiji,’  Sharif Ghalib Effendi aliwaambia, ‘Mimi ningalikuwa nimefanya hivyo kabla, lakini haiyumkinika hivi sasa,’ akikiri kosa lake.  Yeye pia hakutaka kujisalimisha, lakini wakazi wa Makkah walisema, ‘Ewe Amir! Bau yako Mtume Muhammad s.a.w.w. pia alifanya mikataba pamoja na maadui zake. Nawe pia, tafadhali kubaliana na maadui na ututoe sisi katika majanga haya. Wewe utakuwa ukifuata Sunnah ya Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa kufanya hivyo. Kwa sababu Mtume Muhammad s.a.w.w. alimtuma ‘Uthman (kutoka Khudaibiya) kwa kabila la Kiqoreishi katika Makkah kwa ajili ya kufanya mkataba.’  Sharif Ghalib Effendi aliwasihi watu wajiepushe na wazo la kuingia katika mkataba pamoja na Mawahhabi na hadi mwisho alikuwa hakuingia katika mapatano. Yeye alikubali baada ya kushauriwa na kiongozi wa masuala ya dini aitwaye ‘Abd ar-Rahman  wakati ambapo watu walikuwa hawawezi kustahimili shida. Kwa hakika lilikuwa ni uamuzi wa busara wa Sharif Ghalib Effendi kumsikia ‘Abd ar-Rahman na kumtumia kama mpatanishi ili kumzuia Sa’ud asiwatese na kuwaua Waislamu.  Yeye vile vile alijishindia ufadhila wa wakazi wa Makkah na maaskari kwa kusema, ‘Mimi nimekubali kufanya mapatano bila ya kutaka; nilikuwa nikipanga kusubiri mpaka ufike wakati wa Hijja.’

 

“Baada ya kuandikiana masharti na mapatano, Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz aliingia mjini Makkah. Yeye aliifunika al-Ka’ba Tukufu kwa namna ya nguo iliyofanywa kwa kugandamiza manyoya ya wanyama pamoja na sherizi, e.g. ya tarbushi. Yeye alimfukuza kazi Sharif Ghalib Effendi . Alishambulia huku na huko kama Firauni na kuwatesa watu katika hali isiyostahimilika.Kwa sababu kulikuwa hakujawasili misaada yoyote kutoka “Uthmaniyya (Ottoman), Sharif Ghalib Effendi alikuwa amepata uchungu mno.  Yeye alieneza tetesi kuwa sababu kuu ya kuusalimisha mji wa Makkah ilikuwa ni uzembe wa utawala wa ‘Uthmaniyyah(Ottoman Empire) na ilimshawishi Sa’ud kutowaruhusu Wamisri na Mhujjaji kutoka Damascus wasiingie Makkah ili kwamba kuwafanya ‘Uthmaniyya waanze matendo yao dhidi ya Mawahhabi.

 

“Mwenendo huu wa Sharif Ghalib Effendi ulimfanya Sa’ud awe katili zaidi na kuongezea mateso yake. Yeye aliwatesa na kuwaua wengi wa maulamaa wa Ahl as-Sunna na watu wengi matajiri wa mji wa Makkah.Yeye aliwatishia wale ambao hawkubainishwa kuwa wao ni Mawahhabi.Watu wake walipiga makelele masokoni na    mitaani,‘Kubalini dini ya Sa’ud! Jihifadhini katika kivuli chake pana!’ Kwa hakika idadi ya watu waliokuwa wakiweza kuilinda na kuinusuru dini ilikuwa imepungua mno majangwani.

 

“Sharif Ghalib Effendi alipoona hali mbaya iliyojitokeza katika mazingara hayo, aliona kuwa Islam inataka kufutwa katika Hijaz na miji iliyobarikiwa kama vile ilivyokwishatokea katika miji ya majangwani, alimtumia ujumbe Sa’ud, ukisema:’Wewe hautaweza kukabiliana na majeshi ya ‘Uthmaniyya ambayo yatatumwa kutoka Istanbul iwapo utabakia kukalia mji wa Makkah baada ya msimu wa Hijja.  Wewe utashikwa na kuuawa. Usibakie katika mji wa Makkah baada ya Hijja, ondoka zako!’ Kwa hakika ujumbe huu haukuleta uwema wowote bali Sa’us aliongezea ukatili na kuwatesa vibaya sana Waislamu.

 

“Wakati wa kipindi hiki cha uchokozi na utesaji, Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alimwuliza ‘alim mmoja wa ahl as-Sunna,’Jee Muhammad (Mtume Muhammad s.a.w.w. ) yupo hai kaburini mwake? au amekufa kama tunavyoamini watu wengine wanaokufa?’ ‘Alim huyo alimjibu, ‘Yeye yu hai kwa maisha ambayo sisi hatuwezi kujua.’ Sa’ud  alimwuliza swali hili kwa makusudi ili akitarajia jibu kama hilo ili aweze kumtesa na kumwua huyo ‘alim.‘Kama ni hivyo, basi tuonyeshe kama yeye yupo hai kaburini mwake ili tuweze kukuamini. Na lau utashindwa basi tutaelewa kuwa wewe ni mpinzani wa dini yangu. Iwapo utajibu visivyo sahihi, mimi nitakuua,’ alisema Sa’ud. ‘Mimi sitajaribu kukuvutia wewe kwa kukuonyesha jambo moja lisilohusiana na swala hili. Twende pamoja hadi mjini Madinah al-Munawwara na tusimame mbele ya Muwajahat as-Sa’ada. Mimi nitamtolea salaam, na iwapo yeye yu hai basi atanijibu, basi utajionea kuwa bwana wetu Mtume Muhammad s.a.w.w. yu hai kaburini mwake na kwamba husikia na kuwajibu wale wote wanaomsalimia. Iwapo hatutapata  jibu la salaam yangu, basi itajulikana kuwa mimi ni mwongo. Na hivyo utaweza kuniadhibu vile utakavyo,’ alijibu yule ‘alim wa Ahl as-Sunna. Kwa kuyasikia hayo, Sa’ud alighadhabika mno na akamwachia huyo ‘alim aondoke, kwani naye pia angalikuwa kafiri na mushrik kwa mujibu wa imani zake mwenyewe iwapo angelifanya vile alivyotaka ‘alim yule.Yeye alipumbazwa kwani yeye mwenyewe alikuwa si msomi kwa kuweza kutoa majibu. Hivyo ilimbidi amwachie yule ‘alim ajindokee huru kwani asije akajiharibia jina lake.Hata hivyo wao walikuwa ni watu wenye njama mbaya, alimwamrisha askari mmoja amwue huyo ‘alim na kumpelekea habari mara moja. Lakini  huyo askari wa Kiwahhabi hakupata mwanya wa kutekeleza amri hiyo, kwa baraka za Allah swt. Habari hizi mbaya kabisa zilifika katika masikio ya mwanachuoni huyo mujahid, yeye alihama Makkah akifikiri kuwa itakuwa ni wema kwake yeye kuondoka Makkah.

 

“Sa’ud alimtuma muuaji mmoja kwenda kumwua mujahid huyo baada ya kusikia habari za kuondoka kwake. Mwuaji huyo alisafiki usiku na mchana kutwa akidhani kuwa atajipatia thawabu nyingi mno kwa kumwua Ahl as-Sunna. Kwa bahati mbaya, mwuaji alipomfikia mujahid huyo aliyetakiwa kuuawa kwa amri ya Sa’ud, alikuwa ameshakufa kifo cha kawaida punde kabla ya kuwasili huyo mwuaji. Yeye alimfunga mnyama wa mujahid katika mti na kuodoka kwenda kunywa maji.  Wakati aliporudi, akakuta ngamia peke yake bila ya maiti ya mujahid.  Baada ya kurudi kwa Sa’ud, askari huyoo alimwelezea tukio lote. ‘Naam!’  Sa’ud alisema, ‘Mimi nilimwota huyo mtu akichukuliwa juu mbinguni katika Pepo miongoni mwa sauti za dhikr na tasbih.  Watu wenye sura zilizokuwa ziking’ara walimwambia kuwa maiti hiyo ilikuwa ni ya mujahid yule na ilikuwa ikichukuliwa Peponi kwa sababu imani zake zipo sahihi kuhusu Mtume (Mtume Muhammad s.a.w.w. ).’  Kwa kuyasikia hayo, Mwahhabi huyo alisema, ‘Wewe ulinituma kumwua mtu kama huyu aliyebarikiwa! Na sasa wewe hautaki kurekebisha imani zako potofu ilihali umejionea baraka na rehema  za Allh swt zikimfikia huyo mujahid!’.  Na alimlaani Sa’ud. Yeye alitubu.  Sa’ud wala hakuchukua taabu ya kumsikiliza huyo. Yeye alimteua ‘Uthman al-Mudayiqi awe gavana wa Makkah na alirudi Dar’iyya.

 

“Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alikuwa akiishi huko Dar’iyya. Yeye vile vile alifanikiwa kuuteka mji wa Madina.  Mbeleni, yeye aliondoka kwenda Makkah pamoja na wale waliokuwa wakitaka kuhiji na wale waliokuwa wakiweza kuzingumza vyema. Wale viongozi wa dini yao ya Uwahhabi walikuwa ndio katika mstari  wa mbele ambao wangaliweza kuueneza na kuusifu Uwahhabi. Wao walianza kusoma na kuelezea kitabu kilichoandikwa na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab katika Masjid al-Haram huko Makkah siku ya Ijumaa mnamo tarehe 7 ya mwezi wa Muharram, mwaka 1221 (1806). Kwa hakika Maulamaa wa Ahl as-Sunna waliwakanusha wao.[3]  Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alifika baada ya siku kumi. Yeye alifanya kituo chake katika nyumba ya Sharif Ghalib Effendi  katika uwanja wa Mu’alla. Yeye aliiweka kipande cha kile alichojifunika juu ya Sharif Ghalib Effendi kuonyesha urafiki. Na Sharif Ghalib Effendi aliuonyesha urafiki pia. Wote kwa pamoja walikwenda Masji al-Haram na wakafanya tawaf kuuzunguka al-Ka’aba kwa pamoja.

 

“Wakati huo zilifika habari kuwa msafara wa mahujjaji kutoka Damascus walikuwa wakija Makkah. Sa’ud alimtuma Mas’ud ibn Mudayiqi awaendee hao wasafiri na kuwaambia kuwa hawataruhusiwa kuingia Makkah. Mas’ud alionana na msafara huo na kuwaambia, ‘Nyinyi mulipuuzia mikataba na mapatano ya hapo awali. Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz amewatumieni amri pamoja na Salih ibn Salih kuwa nyinyi msije pamoja na majeshi yenu. Lakini tunaona kuwa mnao majeshi yenu! Hivyo kamwe hamtaweza kuingia Makkah, kwa sababu hamkutii amri’ Mkuu wa msafara huo, ’Abdullah Pasha, alimtuma Yusuf Pasha kwenda kwa Sa’ud kumwomba msamaha na idhini ya kuingia Makkah.  Sa’ud alijibu, ‘Ewe Pasha! Mimi ningalikuwa nimekwishawaua nyinyi nyote kama nisingalikuwa na hofu ya Allah swt. Hebu nileteeni magunia ya  sarafu za dhahabu munazozitegemea kuwagawia masikini wa haramain na wanavijiji Waarabu na mara moja muondoke zenu! Mimi ninawaharamishieni nyinyi Hijja ya mwaka huu!  Yusuf pasha alizisalimisha magunia ya sarafu za dhahabu na kuondoka.

 

“Habari za kuzuiliwa na kufukuzwa kwa msafara wa Mahujjaji kutoka Damascus zilienea kwa kasi katika ulimwengu wa Kiislamu.  Wakazi wa Makkah walilia na kusikitika mno kwani walidhani kuwa nao pia wamepigiwa marufuku kwenda ‘Arafat.  Lakini siku iliyofuatia, waliruhusiwa kwenda ‘Arafat kwa masharti kuwa ilikuwa ni marufuku kwao kwenda mahfas au  machela. Kila mmoja, hata mahakimu na Maulamaa, alikwenda ‘Arafat juu ya punda au ngamia.  Khutba ya huko ‘Arafat ilitolewa na Mwahabbi badala ya qadhi wa Makkah. Wao walirejea Makkah baada ya kutimiza mambo ya faradhi katika Hijja.

 

“Sa’ud  alipowasili Makkah tu alimwachisha kazi Qadhi wa Makkah, Khatib-zada Muhammad Effendi, na alimteua Mwahhabi aliyeitwa ‘Abd ar-Rahma kama Qadhi. ‘Abd ar-Rahman alimwita Muhammad Effendi, Su’ada Effendi, hakimu mkuu wa Madina, na ‘Ata’i Effendi, mwakilishi wa Masharifu huko Makkah na aliwakalisha juu ya sakafu.  Yeye aliwaambia watoe heshima zao kwa Sa’ud. Maulamaa hawa walisema, La ilaha illallah wahdahu la sharika lahu kwa mujibu wa imani ya Mawahhabi na waliketi tena juu ya sakafu. Sa’ud alicheka na kusema, ‘Mimi ninawaheshimuni nyinyi pamoja na msafara wa Mahujjaji wa Damascus na kuwawekeni chini ya uangalizi wa Salih ibn Salih. Salih ni mmoja wa watu wangu wema. Mimi ninamwamini. Mimi ninawaruhusu muondoke kwenda Damascus kwa masharti kwamba mutalipa kurushi 300 kwa kila mahfa- na ngamia aliyebebeshwa mzigo na kurushi 150 kwa kila punda. Kwa hakika huu ni upendeleo mkubwa kwenu kweza kwenda Damasca kwa malipo madogo. Kwa hakika mutaweza kuondoka kwa usalama chini ya ulinzi wangu. Mahujjaji wote watasafiri katika masharti haya. Na huu ndio uadilifu wangu. Mimi nimekwisha mwandikia barua Sultan wa Wauthmaniyya Bwana Salim Khan III. Nimemwandikia kuharamishwa kujenga majengo juu ya makaburi, kufanya machinjo ya wanyama kwa ajili ya waliokufa au kuwaomba kupitia wale waliokufa.’

 

“Sa’ud alibakia Makkah kwa muda wa miaka minne. Muhammad ‘Ali Pasha, Gavana wa Misri, alikuja hadi Jeddah katika mwaka 1227 A.H. (1812) kwa amri ya Sultan wa 'Uthmaniyya Mahmud-i ‘Adli.  Majeshi ya Misri wakishirikiana na majeshi ya Jeddah walifanikiwa kumfukuza Sa’ud kutoka Makkah baada ya vita vikali vya umagikwaji wa damu."

 

(5) MAWAHHABI  HUKO  MADINA

Sulaiman Khan, Khalifa wa sabini na tano wa Ahl as-Sunna na Sultan wa kumi wa Wauthmaniyya, alijenga kuta kuuzunguka mji mtukufu wa Madina; mji ambao haukudhurika kwa mashambulizi ya aina zozote za majambazi kwa muda wa miaka 274 kwa sababu za kuta zake kuwa madhubuti, na Waislamu wa hapo waliishi kwa amani na raha hadi ulipofika mwaka 1222 A.H. (1807) wakati walipoangukia kama windo mikononi mwa Sa’ud.

 

Sa’ud aliwatuma waporaji aliowakusanya kutoka vijiji kwenda Madina baada ya kuiteka Makkah na vijiji vilivyozunguka. Yeye aliwateua ndugu wawili waitwao Baday na Nadi kama makamanda wa vikosi hivyo vya waporaji. Wao walipora vijiji kila walipokwenda na kuwaua Waislamu wengi mno. Vijiji vingi mno kuelekea madina vilichomwa moto na kuteketezwa kabisa. Waislamu waliokuwa na msimamo wa haki kama Maulamaa wa Ahl as-Sunna, waliporwa kila kitu na hatimaye kuuawa. Kwa hakika hali ya uporoja na uteketezwaji wa vijiji kuelekea Madina hauwezi kufanyiwa makisio, hali ilipindukia kiasi. Vijiji vya karibu na Madina vilijisalimisha kwa Mawahhabi kwa hofu ya kuporwa, kuteswa na kuuawa. Na hivyo wote walikuwa ni watumwa na manamba wa Sa’ud. Sa’ud aliwaandikia barua Waislamu wa Madina kwa kumtumia Salih ibn Salih:

Mimi ninaanza kwa jina la Mmiliki wa Siku ya Malipo. Nadhani inafahamika miongoni mwa Maulamaa, maofisa na wafanya biashara wa Madina kuwa amani na raha inapatikana kwa wale tu ambao wanajipatia muongozo.Enyi watu wa Madina! Ninawaiteni katika dini ya haki Ayah ya 19 na 85 ya Surah al-Imran inasema: ‘Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Allah ni Uislam. Na anayetaka dini isiyokuwa basi haitakubaliwa kwake. Naye  Akhera atakuwa katika wenye hasara!’ Mimi nataka mujue hisia zangu kuhusu nyinyi.  Mimi ninawapendeni na ninayo imani n awatu wa Madina. Mimi ninataka kuja kuishi pamoja nanyi katika mji wa Rasulullah.Mimi sitawateseni wala kuwadahalilisha iwapo nyinyi mutanisikiliza na kuzitii amri zangu. Watu wa Makkah wamekuwa wakifaidika na fadhila na huruma zangu tangu nilipoingia mjini humo. Mimi ninawatakeni nyinyi nyote muwe Waislamu kwa upya. Hapo mutasalimika na udhalilisho, mateso na hata mauti iwapo tu mutazitii amri zangu. Allah swt atawalinda na mimi nitakuwa mlinzi wenu.  Mimi ninawatumieni barua hii pamoja na mtu nimthaminiaye mimi, naye ni Salih ibn Salih.  Someni vyema na mufanye maamuzi yenu pamoja naye.! Kile atakachokisema yeye ndicho nikisemacho mimi.”

 

Kwa hakika wakazi wa Madinah walishtushwa mno kwa barua hiyo.  Hivi karibuni wao walikuwa wamesikia mateso na mauaji yaliyowakumba wakazi wa Ta’if wakiwemo wanawake na watoto na hivyo walikuwa wamejaa kwa hofu.  Wao hawakuwa na la kusema ndiyo au hapana kwa barua ya Sa’ud ibn ‘Abd al-’Aziz. Vile vile hawakutaka kusalimisha maisha yao wala dini yao.

 

Kwa kuona hakuna majibu ya barua, kiongozi wa mahramia, Baday mwovu kabisa, aliishambulia mji wa Yanbu, bandari ya Madina. Baada ya kuiteka Yanbu, aliizingira Madina na aliishambuli mara kwa mara kuta za lango la ‘Anbariyya. Ikatokea kuwa siku hiyo Mahujjaji kutoka Damascua walikuja pamoja na kiongozi wao ‘Abdullah Pasha. Pale alipoona mji umezingirwa, Mahujjaji na maaskari walipigana vita vikali dhidi ya maharamia wa Kiwahhabi. Kiasi cha maharamia mia mbili waliuawa katika mapigano ya umwagikaji damu yaliyodumu masaa mawili, waliobakia walifanikiwa kutoroka.

 

Waislamu wa Madina walikaa katika raha na amani hadi pale ‘Abdullah Pasha alipokuwapo Madina kutimiza faradhi zake za Hijja, lakini Baday aliuzingira tena mji wa Madina baada ya kuondoka Mahujjaji wa Damascus.  Yeye aliteka Quba, Awali na Qurban na alijenga maboma mawili ya ng’ombe katika  eneo hilo. Yeye aliweka vizuizi katika barabara zote ziendazo Madina na aliteketeza chemchemi iliyokuwa ikiitwa ‘Ain az-zarqa’.Hivyo Waislamu walikuwa hawana chakula wala maji.

Muujiza

Maji yaliongezeka na kuwa matamu katika kisima cha maji kiitwacho Baghichat ar-Rasul katika Masjid an-Nabi baada ya kuteketezwa kwa ‘Ain az-zarqa’. Maji yalipatikana kwa wingi mjini hapo na hivyo hakuna Mwislamu aliyepata shida ya kiu cha maji.  Hapo awali kisima hiki kilijulikana kuwa na maji ya chumvi.

 

Kuzingira huku kuliendelea kwa muda wa miezi.  Waislamu walikuwa wamedhalilika vya kutosha kwa matumaini kuwa Mahujjaji wa Damascus watakuja tena na hivyo kuwaokoa. Hatimaye Mahujjaji walifika, lakini kiongozi wa msafara, Ibrahim Pasha, aliwaambia, “Salimisheni mji wenu kwao,” kwa sababu yeye alikuwa hana vikosi vya kutosha vya kuweza kupigana nao.Waislamu walikuwa wanadhani kuwa Ibrahim Pasha alikuwa ameshazungumza na kuelewana na Baday na kuwa watakuwa wameahidi kuwa Waislamu hao hawatadhalilishwa wala kuteswa au kuuawa. Hapo wao waliandika barua ifuatayo kwa Sa’ud na kuituma kwa kamati kamati ya watu wanne, waitwao Muhammad Tayyar, Hasan Chawush, ‘Abd al-Qadir Ilyas na ‘Ali:

 

“Sisi tunatoa heshima na kutuma salaamu kwako. Tunamwomba Allah swt akufanye mshindi katika matendo yako ambayo ni kwa mujibu wa uthibitisho wake! Ewe Shaikh Sa’ud! Amir wa Mahujjaji wa Damascus alipowasili hapa na kujionea kuwa mji umezingirwa, barabara zimewekea vizuizi na maji yamekatwa na Baday. Na alijaribu kutafuta sababu ya mambo yote haya na alikuja kujua kuwa hayo ndiyo amri yako.  Kama tunavyoamini kuwa wewe hauna nia ya uadui kuhusu watu wa Madina, na sisi tunadhani kuwa wewe hauna habari na matukio maovu haya yanayotokea. Sisi, viongozi wa Madina, tumekutana na kuamua kukujulisha yale tunayotendewa huku. Sisi sote kwa pamoja tumewachagua watu hawa wanne walio bora, watu watukufu na hivyo tunawatuma kwako kama wajumbe wetu. Tunamwomba Allah swt kuwa wao watarejea kwetu pamoja na habari njema za kufutufurahisha.”

 

Sa’ud aliwatendea vibaya kabisa hao wajumbe baada ya kusoma barua na wala hakuwa na aibu kwa kusema kuwa yeye alikuwa amewakasirikia na kuwachukia watu wa Madina.Wajumbe walimbembeleza mno kuwasamehe na huku wakijitupa hata juu ya miguu yake michafu. Lakini yeye alisema, “Mimi ninadadisi kutokana na barua yenu kuwa nyinyi hamutazitii amri zangu, kwamba hamutaikubalia dini yangu ya kweli, na kwamba nyinyi munajaribu kunidanganya kwa maneno mazuri kwa sababu nyinyi mumezidiwa na kiu, njaa na dhiki na kwamba munanibembeleza kwa nia ya kujitoa katika mambo hayo na wala hamuna nia nyingine. Kwa hakika hakuna njia nyingine isipokuwa kukubali chochote kile nikitakacho mimi. Mimi nitawafanya nyinyi muzomewe na kuteketea kabisa kama vile vilivyowafanyia watu wa Ta;if iwapo nyinyi mutajifanya kuzikubalia amri zangu wakati mutasema au kutenda visivyonipendeza.”Yeye aliwalazimisha Waislamu waache madhehebu yao.

 

Masharti maovu na potofu  zilizotolewa na Sa’ud kwa ajili ya Waislamu wa Madina yameandikwa kwa mapana zaidi katika kitabu kiitwacho Tarikh-i-Wahhabiyan.

 

Wajumbe wa Madina walirudi Madina baada ya kuzikubalia amri za Sa’ud kwa ushurutisho. Wakazi wa Madina, walishtushwa mno kwa matukio hayo, na walionyesha kukubali kwao bila ya kujitakia, kwani yeyote yule aangukaye baharini humshika nyoka. Wao waliisalimisha ngome yao ya Madina kwa watu sabini wa Baday kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sharti la saba la mapatano hayo. Moja ya masharti katika mapatano hayo ilikuwa ni kubomoa makaburi  yaliyopo mjini Madina. Wao walilazimika kutimiza masharti hayo ili waepukane na mateso ya Mawahhabi.  Ingawaje wao walifanya kwa shinikizo, wala si hiari zao, lakini matokeo ya matendo yao yalikuwa mabaya mno.

 

Hakuna jibu lililofika la barua yao ya kuomba msaada kutoka Istanbul. Wakazi wa Madina waliishi katika hali ya kuteswa na kukandamizwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.Ulipofika wakati ambao wao walikata tamaa kabisa wa kuwasili msaada kutoka Istanbul, wao walimwandikia barua Sa’ud ya kuomba msamaha huko Dar’iyya, iliyopelekwa na Husain Shakir na Muhammad Saghayi. Lakini Sa’ud hakuwapokea wajumbe hao kwani alikuwa amekwishapata habari kuwa wakazi wa Madina walikuwa wameomba msaada hapo awali kutoka Istanbul. Sa’ud mwenyewe aliondoka Dar’iyya pamoja jeshi kubwa mno kwenda Madina kuendeleza dhuluma na kuwatesa kuwateketeza Waislamu wa mjini humo.

 

Wakatili na wanavijiji wote wa majangwa ya arabia walikuwa wameshakwisha mtambua Sa’ud kama mtawala wa Najd, ambaye alikuwa akizitilia sahihi barua alizoziandika huku na huko kwa cheo “al-Imam ad-Dar’iyyat al-majdiyya wa ‘l-ahkam ‘d-da’wati ‘n-Najdiyya”.

 

Punde alipoingia mjini Madina, aliwaamrisha wafanyakazi na wahudumu wa makaburini hapo (Qubba) kuzibomoa kwa mikono yao. Ingawaje Waislamu wa hapo walikuwa wamekwisha bomoa maqubba mengi  kwa mujibu wa sharti la tatu waliyokuwa wamepewa na Sa’ud kiasi cha miaka mitatu iliyopita, lakini wao walikuwa hawakuthubutu baadhi ya makaburi ambayo wao walikuwa wakijua kuwa zilikuwa tukufu na zilizobarikiwa. Wafanyakazi na wahudumu hao walianza kazi za kubomoa huku wakilia na kusikitika mno.Mfanyakazi na mhudumu wa kaburi la Bwana Hamza alisema kuwa yeye alikuwa ni mtu aliyezeeka na dhaifu, hivyo asingaliweza kubomoa. Sa’ud alimwamrisha  mtumwa wake mwovu kubomoa. Mtu huyo alipanda juu ya Qubba kutaka kubomoa, lakini alianguka chini na kufa papo hapo, na hivyo kulimfanya Sa’ud aahirishe kubomoa kaburi hilo lakini aliondoka huku ameuondoa mlango wake.Baada ya kusimamia operesheni ya maamrisho yake maovu yenye kuteketeza, alihutubia jukwaa iliyojengwa katika mahala paitwapo Manaha.Yeye alisema kuwa wakazi wa Madina walikuwa hawtaki kumtii lakini wamekuwa wanafiq kwa uwoga wao na kwamba wanataka kuendelea na ushrikina wao kama hapo awali. Na aliongezea kusema  katika sauti mbaya na ufidhuli, kuwa wale wote waliojihifadhi katika ngome mi lazima watoke nje na watoe heshima, na wale ambao watakataa kutoka nje, basi  watakipata kile kiitwacho hukumu ya Mawahhabi kama ilivyotekelezwa mjini Ta’if.

 

Kila mtu aliogopa wakati malango ya ngome zilipofungwa na kulitolewa ilani katika kila mitaa kuwa watu wote wakusanyike mahala palipokuwa pakiitwa Manaha. Wao walidhani kuwa yale tote yatawapata waliyoyapata watu wa Ta’if, mateso na kuuawa. Wao waliagana kwa machozi pamoja na wake na watoto wao kwani walijua kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wao.Wanawake na wanaume walikuwa wamekusanyika katika makundi mawili huku shingo zao zikiinama chini kuelekea qubba la kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. Mji wa Madina haukuwahi kukumbwa na huzuni na siku nyeusi kama hiyo hapo kabla. Sa’ud alikuwa mwenye chuki dhidi ya Waislamu. Lakini Allah swt kwa baraka za Mtume Muhammad s.a.w.w.aliulinda mji mtukufu wa Madina usipakwe damu kama rangi. Baada ya kuwadhalilisha Waislamu kwa matendo na maneno maovu yaliyo kinyume na heshima, Sa’ud aliwaamrisha maharamia wake waishi katika ngome ya Madina. Yeye alimteua Hasan Chawush, mlaghai mkubwa aliyeaminiwa mno, kuwa gavana wa Madina na yeye mwenyewe alirejea Dar’iyya. Yeye alirudi Madina baada ya kutimiza Hijja huko Makkah katika msimu wake. Yeye alitoka nje ya pango lake na kwenda katika baraza lake wakati ambapo msafara wa Mahujjaji wa Damascus walipokuwa wameshaondoka kwa umbali wa siku mbili au tatu kutoka Madina. Yeye hakushtushwa na moyo wake mweusi na mgumu hata kuliko jiwe, aliwaachia maharamia wake wapore vito vya thamani, kazi za nakshi muhimu katika ukumbusho wa historia, vito vingi vilivyokuwa vimechovya katika dhahabu na kurembeshwa kwa jawhari na mawe yenye thamani na nakala zilizokuwa zimekusanywa za Quran Tukufu pamoja vitabu ambavyo vilivyokuwa havipatikani kwa urahisi, vitu vyote hivi vilikuwa vimewekwa katika jumba la kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. na vilikuwa katika hazina ya Masjid an-Nabawi ambavyo vilikuwa vimetumwa kama vilivyochaguliwa na heshima kama zawadi kutoka Masultani Waislamu, makamanda, wasanii na Maulamaa kutokea sehemu zote za ulimwengu wa Kiislamu kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja. Moto wa uadui uliokuwa unawaka undani mwake dhidi ya Waislamu haukupoa hata baada ya matendo yake ya kuaibisha, yeye aliendelea na azma yake ya kubomoa makaburi yaliyobakia ya ma-Sahaba na Mashahidi.Yeye amejaribu sana kubomoa nyumba ya kabruri la Mtume Muhammad s.a.w.w. lakini alishindwa kwa sababu za sauti za Waislamu kupinda kitendo chake hicho, lakini aliweza kubomoa Shabakat as-Sa’ada, kwa bahati nzuri kutokugusa kuta.Yeye aliamuru kuta zizungukazo mji wa Madina zifanyiwe ukarabati.Yeye aliwakusanya wakazi wa MAdina katika Masjid an-Nabi. Alifunga milango ya Masjid na kutoa hotuba ifuatayo juu ya jukwaa:

 

“Enyi mliokusanyika! Nimekuiteni hapa kwa kutaka kuwapa nasiha na kuwaonyeni kuwa muzifuate amri zangu. Enyi watu wa Madina! Dini yenu ndiyo sasa imekamilika. Kuanzia sasa nyinyi ndio Waislamu.Nyinyi mmemfurahisha Allah.Kamwe musiipende dini ya potofu ya baba na mababu zenu. Wala kamwe musimwombe Allah swt awarehemu! Wao wote walikuwa kama mushrik.Na kwa hakika wote walikuwa mushrik. Mimi nimewaelezeeni vile mutakavyo mwabudu Allah katika vitabu vyangu nilivyowapa watu wenye mamalaka ya dini. Mutambue waziwazi kuwa mali yenu yote, watoto, wake na damu zenu ni mubah kwa maaskari wangu iwapo nyinyi hamutowajali watu wangu wenye mamlaka ya dini. Wao watawafungeni kwa minyororo nakuwateseni nyinyi nyote hadi kufa. Imeharamishwa katika dini ya Uwahhabi kusimama mbele ya kaburi la Mtume kwa nia ya kutoa heshima kwa kusema salat na salaam kama vile mababu zenu walivyofanya. Haiwapashi nyinyi kusimama mbele ya kaburi, lakini munaweza kupita na kusema As-salaamu ‘ala Muhammad, wakati munapokuwa mukipita. Kwa mujibu wa Ijtihad ya imam wetu Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, heshima kiasi hiki kinamtosha Mtume”.

 

Sa’ud, baada ya kutoa kashfa na kauli mbayambaya ambayo sisi hatuna hima ya kuzitoa, aliamrisha milango ya Masjid as-Sa’ada ifunguliwe. Yeye alimteua mwanake ‘Abdullah kama gavana wa Madina na alirejea Dar’iyya. Baada ya hapo ‘Abdullah ibn Sa’ud hakuacha kuwatendea Waislamu wa Madina madhila na mateso ya kila aina.

 

(6) WAUTHMANIYYA WAKOMBOA MIJI

 

Katika miaka hiyo, Serikali ya Wauthmaniyya ilikuwa imeshughulika na masuala ya nje na ilikuwa ikijaribu kuuzima moto wa upinzani uliochochowa na chama chenye utaratibu maalum wa siri (freemasons). Wakati ukatili na mateso ya Sa’ud kwa ajili ya Waislamu yalipofikia hali isiyohimilika katika mwaka 1226 A.H. (1811), Khalifa wa Waislamu, Sultan Mahmud Khan ‘Adli II, alimwandikia barua Gavana wa Misri, Muhammad ‘Ali Pasha, awaadhibu hao mahamia. Kwa kupata barua hiyo, Muhammad ‘Ali Pasha alituma majeshi yake kutokea Misri katika mwezi mtukufu wa Ramadhani chini ya ukamanda wa mwanake Tosun Pasha. Tosun Pasha aliikomboa mji wa Yanbu, bandari ya Madina, lakini alishindwa katika vita vikali baina ya sehemu ya bonde la Safra na mpitio wa Judaida wakati akiwa anaendelea Madina katika siku za mwanzoni mwa mwezi wa Dhul Hijja, mwaka wa 1226 A.H. Ingawaje Tason Pasha mwenyewe alikuwa hakudhurika lakini Waislamu wengi wa ‘Uthmaniyya walikuwa mashahidi. Muhammad ‘Ali Pasha alipopata habari hizi alihuzunika sana kwa bahati mbaya hiyo na hivyo alitokeza na jeshi kubwa la maaskari wenye silaha nzito nzito pamoja na mizinga kumi na nane, mabunduki makubwa tatu na silaha nyingi zinginezo. Wao walipita bonde la Safra na mpitio wa Judaida katika mwezi wa Sha’ban 1227 A.H. (1812). Wao walizikomboa vijiji vingi bila ya kupigana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Muhammad ‘Ali Pasha, kama vile alivyokuwa ameshauriwa na Sharif Ghalib Effendi, alitenda kwa busara kabisa katika kujipatia ushindi kwa kugawa riali 118,000 kwa vijiji ambazo zimejisalimisha kwa ajili ya mapesa. Iwapo Tosun Pasha angekuwa amemtaka ushauri Sharif Ghalib Effendi kama vile alivyofanya baba yake, basi bila shaka asingaliweza kupoteza jeshi lake kubwa kiasi hicho. Sharif Ghalib Effendi alikuwa amir wa mji wa Makkah kama alivyokuwa ameteuliwa na Mawahhabi; lakini moyoni mwake alikuwa na nia ya kuja kuikomboa Makkah kutoka makucha ya maharamia wa Kiwahhabi.  Muhammad ‘Ali Pasha piia alifanikiwa kuikomboa Madina bila ya umwagaji wa damu mwishoni mwa mwezi wa Dhul Qa’da. Habari hizi za ushindi zilitumwa Misri ili ziweze kufikishwa kwa Khalifa.  Watu wa Misri walisherehekea ushindi huo kwa siku tatu (usiku na mchana)  na habari hizo zilienezwa katika nchi zote za Kiislamu.  Muhammad ‘Ali Pasha alituma kikosi kwenda Makkah kwa kupitia Jeddah. Kikosi hicho kiliwasili huko Jeddah mwanzoni mwa mwezi wa Muharram 1228 A.H. na kuelekea mji wa Makkah.  Wao waliingia kwa urahisi mjini Makkah kwa msaada wa mpango wa siri uliotolewa na Sharif Ghalib Effendi. Wakati huo maharamia wa Kiwahhabi pamoja na viongozi wao walikuwwa wamekwishautoroka mji wa Makkah pale walipopata fununu zakikosi cha Wauthmaniyya walipokuwa wakiukaribia mji huo.

 

Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alirejea katika pango lake la uchochezi, Dar’iyya, katika mwaka 1227 A.H., baada ya kumaliza Hijja na kuzuru Ta’if ambapo damu nyingi mno ya Waislamu ilikuwa imemwagwa. Kwa hakika alishtushwa mno punde alipowasili Dar'iyya kwa kusikia kuwa miji ya Makkah na Madina imekombolewa na majeshi ya 'Uthmaniyya. Katika siku hizo hizo, majeshi ya 'Uthmaniyya yalishambulia mji wa Ta’if lakini hawkukumbana na upinzani wowote, kwani nduli wa Ta’if, ‘Uthman al-Mudayiqi pamoja na maaskari wake walikuwa wamekwisha toroka kwa hafu ya kushindwa na kushikwa. Habari hizo nzuri ziliwasilishwa mbele ya Khalifa wa Waislamu huko Istanbul, Sultan Mahmud Khan ‘Adli, ambaye alifurahishwa mno na alimshukuru kwa moyo wake wote Allah swt kwa baraka zake.Yeye alimtumia salaam za pongezi na shukrani na mazawadi mengi gavana huyo Muhammad ‘Ali Pasha na alimwamuru aende Hijaz tena kwa ajili ya kukagua na kuwadhibiti vyema hao maharamia wa Kiwahhabi.

 

Muhammad ‘Ali Pasha akiitii amri ya Sultan Mahmud Khan, aliondoka Misri kuelekea Hijaz. Wakati huo, Sharif Ghalib Effendi alikuwa Ta’if  pamoja na maaskari wa 'Uthmaniyya ,wakimsaka mkatili ‘Uthman aliyejaa damu ya Waislamu waliouawa kwa mikono yake. Baada ya mipangilio ya utafutaji sahihi, ‘Uthman alipatikana na kukamatwa na kupelekwa Misri na baadaye Istanbul. Muhammad ‘Ali Pasha alipowasili Makkah alimpeleka Sharif Ghalib Effendi kwenda Istanbul na kumteua ndugu yake Yahya ibn Mas’ud Effendi kuwa amir wa Makkah. Katika mwezi Muharram 1229 A.H. Mubarak ibn Maghyam, haramia mwingine alikamatwa na kutumwa Itanbul. Maharamia hawa wawili, kwa hakika walikuwa wamemwaga damu ya Waislamu kwa mamilioni, na wakaadhibiwa adhabu waliyostahiki na wakatembezwa katika mitaa ya Istanbul ili watu wawaone na kuwajua. Sharif Ghalib Effendi ambaye alitumikia cheo cha amir kwa muda wa miaka 26 alikaribishwa kwa makaribisho makubwa na yaliyojaa kwa mapenzi, na alipelekwa Salonika ambapo alipumzika hadi alipofariki katika mwaka 1231 ( 1815 ). Qubba ya kaburi lake liko Salonika na ipo wazi kwa wale wafanyao ziyara.

 

Kikosi kilkuwa kimetumwa kusafisha mahala mbali hadi Yemen baada ya kuwafagia maharamia nje ya miji mitukufu ya Hijaz. Muhammad ‘Ali Pasha alikwenda kukisaidia kikosi hiki pamoja na maaskari wake na aliisafisha wilaya nzima. Yeye alirejea Makkah na kuishi huko hadi Rajab 1230, wakati alipomteua mwanake Hasan Pasha kuwa gavana wa Makkah na alirudi Misri. Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz alikufa katika mwaka 1231 na mwanake, ‘Abdullah ibn Sa’ud alimrithi yeye. Muhammad ‘Ali Pasha alimtuma mwanake Ibrahim Pasha pamoja na kikosi  dhidi ya ‘Abdullah ibn Sa’ud.  ‘Abdullah alikuwa ametiliana saini na Tosun Pasha kuwa yeye atakuwa mttifu kwa 'Uthmaniyya iwapo yeye atapewa ugavana wa Dar’iyya, lakini Muhammad ‘Ali Pasha alikataa kuutabua mkataba huo. Ibrahim Pasha aliondoka Misri mwishoni mwa mwaka 1231 na aliwasili Dar’iyya mwanzoni mwa 1232. ‘Abdullah ibn Sa’ud alipambana na Ibrahim Pasha kwa vikosi vyake vyote, lakini alishindwa na kukamatwa baada ya kutokea vita vikali vya kumwagika damu katika mwezi wa Dhul Qa’ada  1233 A.H. (1818).  Habari nzuri za kufurahisha za ushindi zilipokelewa huko Misri kwa maelfu ya sauti za mizinga kutokea boma na kulikuwapo na sherehe kwa muda wa mcha na usiku saba mdululizo. Mitaa yote ilijaa kwa mabendera. Takbir na qasida zilisikika kutokea minara.

 

(7) KAZI ZILIZOFANYIKA BAADA YA UKOMBOZI

 

 



[1] Baadhi ya kazi zilizotokezea katika Kiswahili, kwa ajili ya wasomaji wa Afrika

  Mashariki na Kati, mimi ninazo nakala za vitabu vifuatavyo:

   1.Upotofu wa Madhehebu ya Wahabi,Ahmad Mohammad al-Huseiny(Badawi),Mombasa

     Kenya.

   2. Historia ya Uwahabi na Hatari zake, Khalifa M.Hamisi Mohamed (El-Qadiriy), DSM

     1987.

   3. Upotovu wa Madhehebu ya WAHHABI na hatari zake, Khalifa M.Hamisi Mohamed,

       DSM 19987 & 1988

   4. Fitina za Wahhabi zafichuliwa,Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Bilal Muslim Mission of

       Tanzania., 1997

   5. Uchunguzi juu ya Uwahhabi, Sheikh Ja’afar Subhani, Ahlul Bayt a.s. Assembly of

       Tanzania.,

        DSM 1997

   6. Uwahhabi: kukanushwa na Ahl As-Sunna, mkusanyaji na mtarjum  Amiraly

        M.H.Datoo,Bukoba, Bila Muslim Mission of Tanzania, DSM 1998

[2] Kwa kutaka habari zaidi kuhusu udhalimu na mauaji yasiyostihimilika moyoni, tazama

   kitabu cha Ahmad ibn Zaini Dahlan kiitwacho Khulasat al-kalam (chapa ya Istanbul,

  1395/1975) na Tarikh-i-Wahhabiyyan cha Ayyub Sabri Pasha (Instanbul, 1296 A.H.

  (1879)

[3] Kwa habari zaidi tazama Saif al-Jabbar, mkusanyiko wa makanusho ya Maulamaa wa Makkah dhidi ya Mawahhabi, iliyochapwa baadaye katika Pakistan; na kuchapwa tena Istanbul katika 1395 A.H. (1975).