HISTORIA FUPI  YA IMAM  MOHAMMAD MAHDIY  (MWENYE KUSUBIRIWA).

JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S)

Mohammad bin Hassan bin Ally bin Mohammad  bin Ally bin Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin Abii  twalib (a.s).

MAMA YAKE (A.S)

Mama yake alikuwa ni mjakazi alie kuwa akiitwa  Narjis, na kuna kauli nyingine kuhusiana na mama yake (a.s).

KUNIA YAKE  (A.S)

Kunia yake ni Abul qaasim.

MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S)

1- Al mahdiy. 2- Al muntadhwar.  3- Swahibuz zamaan. 4- Al hujjah. 5- Al qaaim.  6- Waliyyul asri.

7- Aswaahib, na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S)

Alizaliwa tarehe 15 mwezi wa shaaban mwaka 255 hijiria, katika zama za khalifa wa bani Abbas alie kuwa akiitwa Al muutamad.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S)

Alizaliwa katika mji wa Samarrah.

UMRI WAKE (A.S)

Yeye yu hai isipokuwa ametoweka katika macho ya watu (yaani haonekani), na atatokea katika zama za mwisho kwa utashi wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na tuna muomba Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake (a.s) ili aujaze ulimwengu usawa na uadilifu.

MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S)

Muda wa uimamu wake ni mrefu na bado unaendelea, kwa sababu bado yu hai (a.j)

WAWAKILISHI WAKE (A.S)

Imam alikuwa na  wawakilishi wane, na watu walikuwa wakichukua hukumu za Dini kutoka kwao wakati wa ghaibatus sughraa (ghaiba ndogo) nao ni kama wafuatao: 1- Othmaan bin Saiid. 2-Mohammad bin Othmaan. 3- Hussein bin Ruuh. 4- Ally bin Mohammad  As samariy.

KUGHIBU KWAKE (A.S)

Imam anazo ghaiba  mbili,  1- Ghaibatus sughraa (ghaiba ndogo), nayo  ilidumu kwa muda wa miaka 74 na  ilianza mwaka 260 hijiria hadi mwaka 329 hijiria.  2- Ghaibatul kubraa (ghaiba kubwa), ilianza  mwaka 329 hijiria  baada ya kufariki muwakilishi wake wa mwisho (a.s).

ALAMA ZA KUDHIHIRI KWAKE (A.S)

1- kutokea kwa Sufyaan.

Kuuliwa kwa Hassaniy.

3- Kuja kwa bendela nyeusi kutoka Khorasani (iran).

4- Kutokea kwa Al yamaaniy.