HISTORIA FUPI YA IMAM HASSAN  ASKARI (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YALKE (A.S)

Jina lake ni Hassan bin Ally bin Mohammad bin Ally bin Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin Abii Twalib (a.s).

MAMA YAKE (A.S)

Mama yake ni mjakazi  alie kuwa akiitwa Suusan, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

KUNIA YAKE (A.S)

Alikuwa akijulikana kwa kunai ya Abuu Mohammad.

MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S)

1- Al askari. 2- As siraaj.  3- Al khaaalis.  4- As swaamit. 5- At taqiyyu, na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S)

Alizaliwa  tarehe 8 mwezi wa Rabiul awwal, mwaka 232 hijiria, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S)

Alizaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah.

WAKEZE (A.S)

Mkewe alikuwa ni mjakazi alie kuwa akiitwa  Narjis.

WATOTO WAKE (A.S)

Imam anae mtoto mmoja, na  ambae ni imamu wa zama hizi, na hojja mwenye kusubiriwa (mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).

NEMBO YA PETE YAKE (A.S)

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Subhaana man lahuu maqaalidis samaawati wal ardhi), na inasemekana kuwa kuna nembo nyingine tofauti na hii.

UMRI WAKE (A.S)

Aliishi  kwa muda wa miaka 28.

MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S)

Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 6.

WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S)

1- Al mutawakkil. 2- Al muntaswir.  3- Al mustaiin. 4- Al muutazzu. 5- Al muhtadi  6- Al muutamid.

TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)

Alikufa shahidi tarehe 8 mwezi wa Rabiul awwal, mwaka 260 hijiria, na kuna riwaya nyingine izungumziayo tarehe ya kufariki kwake tofauti na hii.

SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S)

Alifia katika mji wa Samarrah.

SABABU YA KUFA KWAKE (A.S)

Ali uwawa kwa sumu katika zama za khalifa  wa kibani Abbas  alie kuwa akiitwa  Al muutamad.

SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S)

Alizikiwa  ndani ya nyumba yake katika mji wa Samarrah ulioko Iraq.