HISTORIA  FUPI   YA IMAM ALLY   AL HAADIY (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YAKE  (A.S)

Jina lake tukufu ni Ally bin mohammad bin Ally bin Mussa bin Jaafar bin mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin Abii twalib (a.s).

MAMA YAKE  (A.S)

Mama yake alikuwa ni mjakazi alie kuwa akiitwa  Sumanah, na inasemekana kuwa alikuwa na jina lingine tofauti na hilo.

KUNIA YAKE  (A.S)

1- Abul Hassan. 2- Abul Hassan Athaani.

MAJINA YAKE MAARUFU  (A.S)

1- Al haadiy. 2- Al mutawakkil.  3- Al Fattah. 4- An naqiyyu. 4- Al murtadhaa.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S)

Alizaliwa tarehe  15mwezi wa dhul hajji, mwaka 212 hijiria, na kuna kauli nyingine tofauti na na hiyo.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S)

Alizaliwa katika kijiji cha  (Swaria) ambacho kiko umbali wa maili tatu kutoka mji wa madinatul munawwarah.

WAKEZE (A.S)

Alikuwa na mke mmoja alie julikana kwa jina la Susan, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

WATOTO WAKE (A.S)

1- Imam Hassan Askari (a.s). 2- Hussein. 3- Mohammad. 4- Jaafar.

NEMBO YA PETE YAKE (A.S)

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Hifdhul uhuud min akhlaaqil maabuud), na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

UMRI WAKE (A.S)

Aliishi kwa muda wa miaka 42.

MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S)

Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 33.

WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S)

Aliishi katika zama za wataala wafuatao: 1- Al muutaswim.  2- Al waathiq. 3- Al mutawakkil.

TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)

Alikufa shahidi tarehe 3 mwezi wa rajab, mwaka  254 hijiria.

SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S)

Alikufa shahidi katika mji wa Samarrah.

SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)

Ali uwawa (a.s) kwa kulishwa sumu katika zama za khalifa wa kibani Abbas aitwae  Al mutawakkil.

SEHEMU  ALIPO ZIKIWA (A.S)

Alizikiwa katika mji wa Samarrah ulioko katika nchi ya Iraq.