HISTORIA  FUPI  YA  IMAM  MOHAMMAD  JAWAAD (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S).

Jina lake  tukufu ni Mohammad bin Ally bin Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin abi Twalib (a.s).

MAMA  YAKE (A.S)

Mama yake alikuwa ni mjakazi  alie kuwa akiitwa  Sakinah Marsiyya, na inasemekana ya kuwa alikuwa akitwa  kwa jina la  Khaziiran, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

KUNIA YAKE (A.S)

1- Abu Ally.  2- Abuu Jaafar.  3- vile vile huitwa kwa kuniya ya Abuu Jaafar Athani, ili kumtofautisha au kumpambanua na imam Baaqir (a.s).

MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S)

1- Al jawaad.  2- Attaqiyyu. 3- Az zakiiyyu. 3- Al qaaniu. 4- Al murtadhaa.  5- Al muntakhab, na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S)

Alizaliwa tarehe 10 mwezi wa Rajab mwaka 195 hijiria, na kuna kauli nyingine kuhusiana na kuzaliwa kwake tofauti na hii.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S)

Alizaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah, ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.

WAKEZE  (A.S)

1- mkewe wa kwanza alikuwa ni mjakazi  alie kuwa  akitambulika kwa jina la Simarah. 2-  Ummul fadhli  binti Maamuun.

WATOTO WAKE (A.S)

1- Imam Al haadii (a.s). 2- Mussa. 3-  Fatima.  4- Umamah.

NEMBO YA PETE YAKE (A.S)

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Niimal qaadirilllah).

UMRI WAKE (A.S)

Aliishi kwa muda wa miaka  25.

MUDA WA  UIMAMU  WAKE (A.S)

Uimamu wake  ulidumu kwa muda wa miaka 17.

WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).

Imam ali ishi katika zama za makhalifa wafuatao wa  kibani Abbas: 1- Maamuun. 2- Muutaswim.

TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).

Alikufa shahidi mwishoni mwa mwezi wa dhil qaadah mwaka 220 hijiria.

SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).

Ali kufa shahidi katika mji wa Baghdaad, nchini Iraaq.

SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).

Aliuwawa kwa kulishwa sumu katika zama za khalifa wa bani Abbas aitwae Al muutaswim.

SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).

Imam alizikiwa kwenye  makaburi ya maquraishi, katika mji wa Kaadhimiyyah, pembezoni mwa babu yake Imam Kaadhim (a.s).