JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S).
Jina lake ni Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin abii twalib (a.s).
MAMA YAKE (A.S).
Mama yake ni kijakazi alie kuwa akiitwa: Hamidah, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.
KUNIA YAKE (A.S).
1- Abul Hassan. 2- Abu Ibraahiim. 3- Abuu Ally. 4- Abuu Ismaail na mengineyo.
MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).
1- Kaadhim. 2- Abdusswaleh. 3- Asswaabir. 4- Al amiin na mengineyo.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).
Alizaliwa tarehe 7 mwezi wa safar mwaka 128 hijiria.
SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S).
Alizaliwa katika sehemu iitwayo (Abuwaa), katika mji wa Madinatul munawwarah.
WAKEZE (A.S).
Wakeze wote walikuwa ni vijakazi.
WATOTO WAKE (A.S).
Takriban Imam alikuwa na watoto 37: 1- Imam Ally bin Mussa Ridhaa (a.s). 2- Ibrahiim.
3- Abbas. 4- Qaasim. 5- Ismaail. 6- Jaafar. 7- Haarun. 8- Hassan. 9- Ahmad.
10- Mohammad. 11- Hamza. 12- Abdallah. 13- Is’haaq. 14- Ubaidullah. 15- Zaid. 16- Hassan. 17- Al fadhlu. 18- Sulaimaan. 19- Fatimatul kubraa. 20- Fatimatu sughraa.
Ruqayyah. 22- Hakiimah. 23- Ummu abiiha. 24- Ruqayyah Assughraa. 25- Kulthuum. 26- Ummu Jaafar. 27- Lubaabah. 28- Zainab. 29- Khadijah. 30- Ulayyah. 31- Aaminah. 32- Hasnah. 33- Burayha.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S).
Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: ( Hasbiya llahu), na kuna riwaya zingine tofauti na hiyo zizungumziazo nembo yake.
UMRI WAKE (A.S).
Aliishi kwa muda wa miaka 55.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 35.
WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).
1- Abuu jaafar Mansuur Dawaniiqiy. 2- Mohammad Mahdiy. 3- Mussa Al haadiy. 4- Haarun Rashiid.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi tarehe 25 mwezi wa Rajab, mwaka 183 hijiria, na kuna riwaya zingine zilizo taja tarehe tofauti na hiyo.
SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi katika mji wa Baghdaad huko nchini Iraq.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Ali uwawa kwa kulishwa sumu katika zama za khalifa wa bani Abbas aitwae Haruun Rashiid.
SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikiwa kwenye makaburi ya maquraishi katika mji wa kaadhimiyyah, kaskazini mwa mji wa Baghdaad.