JINA LAKE NA NSABU YAKE (A.S).
Jina lake ni Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Husein bin Ally bin abi twalib (a.s).
MAMA YAKE (A.S).
Mama yake ni Ummu Far’wa binti Qaasim bin Mohammad bin abii Bakar.
KUNIA YAKE (A.S).
1- Abu abdillah. 2- Abu ismaail.
MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).
1- Aswaadiq. 2- Aswabir. 3- Al faadhil. 4- Atwaahir. 5- Al kaamil. 6- Al munjiy, na mengineyo.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).
Alizawa tarehe 17 mwezi wa Rabiul awwal mwaka 83 hijiria, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S).
Alizaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah.
WAKEZE (A.S).
1- Fatima binti wa Hussein bin Ally bin Hussein (a.s), na wakeze wengine walikuwa ni vijakazi.
WATOTO WAKE (A.S).
1- Ismaail. 2- Abdallah. 3- Mussa. 4- Is’haaq. 5- Mohammad. 6- Abbas. 7- Ally. 8- Ummu Far’wa. 9- As’maa. 10- Fatima.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S).
Pete yake ilikuwa na Nembo ifuatayo: (Allahu waliyyii wa ismatii min khalqihi), na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.
UMRI WAKE (A.S).
Ali ishi kwa muda wa miaka 65.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 34.
WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).
Ali ishi katika zama za watawala wa aina mbili, 1- Watawala wa banii umayyah, 2- watawala wa bani Abbas.
Watawala wa banii Umayyah: 1- Haashim bin Abdul milk. 2- Ibrahiim bin Waliid. 3- Mar’wan Al himaar. Ama watawala wa bani Abbas: 1- Abul Abbas Assaffah. 2- Abuu jaafar Al mansuur Dawaaniqiy.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi tarehe 25 mwezi wa shawwal mwaka 148 hijiria, na zimetajwa tarahe nyingine tofauti na hizi.
SEHEMU ALIPO FIA (A.S).
Ali kufa shahidi katika mji wa madinatul munawwarah.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Aliuwawa (a.s) kwa kulishwa sumu katika zama za khalifa wa bani Abbas aitwae Mansuur Dawaaniqiy.
SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikwa katika makaburi ya Baqii yaliyoko katika mji wa madinatul munawwrah.