JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S)
Jina lake tukufu ni Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin Abi twalib (a.s)
MAMA YAKE (A.S).
Fatima binti wa Imam Hassan (a.s).
KUNIA YAKE (A.S).
Abu Jaafar, na nyinginezo.
MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).
1- Baaqir. 2- Baaqirul uluum. 3- Ash-shaakir. 4- Al haadiy, na mengineyo.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).
Alizaliwa tarehe 1 mwezi wa Rajab mwaka 57 hijiria, na inasemekana kuwa alizaliwa tarehe 3 mwezi wa safar mwaka huohuo, na kunakauli zingine tofauti na hiyo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S)
Amezaliwa katika mji wa madinatul munawwarah.
WAKEZE (A.S).
1- Ummu Farwah binti Qaasim. 2- Ummu Hakiim binti Usaid Athaqafiyyah. 3-4- walikuwa ni vijakazi.
WATOTO WAKE (A.S).
1- Imam Swadiiq (a.s). 2- Abdallah. 3- Ibrahiim. 4- Ubaidullah. 5- Ally. 6- Zainab. 7- ummu Salamah.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S).
P ete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Al- izzatu lillahi, na zinginezo.
UMRI WAKE (A.S).
Ali ishi kwa muda wa miaka 57.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 19.
WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).
1- Waliid bin Abdil malik. 2- Sulaiman bin abdul malik. 3- Omar bin Abdul aziiz. 4- Yaziid bin Abdul malik. 5- Haashim bin Abdul malik.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)
Alikufa shahidi tarehe 7 mwezi wa dhul hajji mwaka 114 hijiria.
SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi katika mji wa Madinatul munawwarah.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)
Aliuwawa (a.s) kwa kulishwa sumu kupitia kwa Bwana ibrahiim bin Waliid bin Yaziid katika zama za khalifa wa bani umayya Haashim bin Abdul malik.
SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikiwa katika makaburi ya Baqii katika mji wa Madinatul Munawwarh.