JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S)
Jina lake ni Ally bin Hussei bin Ally bin Abii twalib (a.s).
MAM YAKE (A.S).
Mama yake ni Shah Zanaan binti Yazdjard bin Shahriyaar bin Kisraa, na inasemekana kuwa jina lake ni ( Shahri banu).
KUNIA YAKE (A.S).
1- Abuu Mohammad. 2- Abuul Hassan. 3- Abuul Hussin 4- Abuul qaasim.
MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).
1- Zainul aabidiin, 2- Sayyidul Aabidiin, 3- Assajjaad, 4-Dhu thafanaat, Imamul Muuminiin, 5- Al mutahajjid, 6- Azzahid, 7- Al amiin, Azzakiiyyu, na mengineyo.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).
Alizaliwa tarehe 5 mwezi wa Shaaban mwaka 380 hijiria, na imepokelewa pia kuwa alizaliwa tarehe 15 mwezi wa Jamadal Aakhir mwaka huohuo, na kuna kauli zingine tofauti na hizo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA (a.s).
Alizaliwa katika mji wa madinatul munawwarah.
WAKEZE (A.S).
Imepokelewa kuwa alioa wanawake 7, 1- Ummu Abdallah bintil Hussein (a.s) ama wengine sita walio bakia walikuwa ni vijakazi.
WATOTO WAKE (A.S).
1- Imam Baaqir (a.s) (Mohammad bin Ally), 2- Abdallah, 3- Al hassan, 4- Al Hussein, 5- Zaid, 6- Omar, 7- Al Hussein Assughraa, 8- Abdur rahmaan, 9- Sulaimaan, 10- Ally, 11- Mohammadul Asghar, 12- Khadija, 13- Fatima, 14- Aliyyah, 15- Ummu kuluthuum, na wengineo.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S).
Pete yake ilikuwa na Nembo ifuatayo: (Wamaa tawfiiqiy illa billahi), na kuna riwaya zingine zizungumziazo nemboya pete yake tofauti na hii.
VITABU VYAKE (A.S).
1- Swahifatu Sajjadiyyah, 2- Risaalatul Huquuq.
UMRI WAKE (A.S)
Ali ishi kwa muda wa miaka 57.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 35.
WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).
Aliishi katika zama za utawala wa 1- Muawia, 2- Yazid bin Muawia, 3- Muawia bin Yazid, 4- Mar’waan binil Hakam, 5- Abdul malik bin Mar’waan 6- Waliidi bin Abdul malik.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S)
Wana historia wametofautiana kuhusiana na tarehe ya kufa kwake, Baadhi wamesema ya kuwa lifariki tarehe 12 mwezi wa muharram, na wengine wamesema tarehe 18 muharram, na wengine wamesema tarehe 25 muharram mwaka 94 au 95 hijiria.
SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi katika mji wa Madinatul munawwarah.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (a.s).
Ali lishwa sumu katika zama za mtawala wa kibani umayyah Waliidi bin Abdul malik.
SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikwa katika makaburi ya Baqii kwenye mji wa (Madinatul Munwwarah).
Kwa maelezo zaidi rejea kitabu Buharul an’waar, juzu ya 42 kwa wale wenye kufahamu lugha ya kiarabu.