JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S).
Jina lake ni Hussein bin Ally bin abi twalib bin Abdul mutwalib.
MAMA YAKE (A.S).
Mama yake ni Fatima Zahraa (a.s) binti wa Mtume (s.a.w).
KUNIA YAKE (A.S).
Abu abdillah.
MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).
1- Arrashiid. 2- Atwayyib. 3- Assayyid Zakii. 4- Al mubaarak. 5- Attaabiu limardhatillah. 6- Addaliil alaa dhati llah. 7- Assibtwi. 8- Sayyidu shabaab ahlil jannah. 9- Sayyidu shuhadaa. 10- Abuu aimmah, na mengineyo.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S)
Alizaliwa tarehe 3 mwezi wa shaaban mwaka wa 4 hijiria, na kuna kauli nyingine isemayo kuwa alizaliwa tarehe 5 mwezi wa shaaban mwaka huohuo, na kuna kuli zingine tofauti na hizo.
VITA VYAKE (A.S).
Alishiriki pamoja na baba yake Amirul muuminin Ally (a.s) katika vita vya Jamal, na vita vya Swiffiin, na vita vya Nahrawaan. Na alikuwa ni jemedari wa jeshi la Imani dhidi ya jeshi l ukafiri na upotevu katika vita vya karbalaa (yaani tukio la Twaf).
WAKEZE (A.S).
1- Shaah Zanaan binti kisraa. 2- Laylaa binti murrah Athaqafii. 3- Ummu Jaafar Al qadhaaiyyah, 4- Rabaab binti imri’il qaisi Al kilabaiyyah, 5- ummu Is’haaq binti Twalha Attamiimiyyah.
WATOTO WAKE (A.S)
1- Alliyul Akbar, 2- Alliyul Asghar, 3- Jaafar, 4- Abdallah Arradhii’u, 5- Sakiinah, 6- Fatima bintil Hussein, na wengineo.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S).
Inasemekana kuwa nembo ya pete yake ilikuwa ni (Likulli ajalun kitaab) na kuna riway isemayo tofauti na hivyo.
UMRI WAKE (A.S).
Ali ishi kwa muda wa miaka 57.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 11.
WATAWALA WA ZANA ZAKE (A.S)
Ali ishi katika zama za utawal wa Muawia na mwanae Yazid.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi tarhe (10) mwezi wa Muharram mwaka 61 hijiria.
SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi katika mji mtukufu wa Karbalaa huko iraq.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Ali uwawa shahidi kwa kuipigania na kuitetea Dini ya babu yake Mohammd (s.a.w) katika vita vya karbalaa, dhidi ya jeshi la fasiki Yazidi bin Muawia.
MAHALI ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikiwa katika mji mtukufu wa Karbalaa.
Kwa malezo zaidi rejea kitabu buharul an’waar juzu ya 40- 41, kwa wenye kufahmu lugha ya kiarabu.