HISTORIA  FUPI YA IMAM HASSAN MUJTABA   (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S)

Jina lake ni Hassan bin Ally bin abi twalib bin Abdul mutwalib.

MAMA YAKE (A.S).

Mama yake ni  Fatima  Zahraa binti wa Mtume  (s.a.w).

KUNIYA  YAKE (A.S) NI.

Abu mohammad.

JINA LAKE MASHUHURI (A.S).

1- Attaqii. 2- Azzakii. 3-  Assibtwi.  4- Atwayyib.  5- Assayyid. 6- Al walii.  Na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA  KWAKE (A.S)

Alizaliwa tarehe 15 mwezi wa Ramadhani mwaka  3 hijiria, na hii ndio tarehe iliyo mashuhuri, na inasemekana ya kuwa alizaliwa mwaka wa  2 hijiria.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S).

Alizaliwa katika mji wa madinatul munawwarah.

VITA VYAKE (A.S)

Alishiriki  katika ukombozi wa nchi za afrika na miji ya faris kati ya mwaka  25- 30 hijiria, na  alishiriki katika vita vyote vya baba yake  Ally bin abii twalib (a.s) kama, Jamal, Swifin, na Nehrawaan.

WAKEZE  (A.S)

1-ummu bashiir binti abi mas’uud  al khazrajiyyah. 2-  Khawla binti mandhuur al fazariyyah. 3- Ummu Is’haaq binti Twalha  Attamiimiy. 4- Juu’da bintil ash-ath.

WATOTO   WAKE  (A.S)

1- Zaidi bin  Hassan. 2-  Hassan bin Hassan. 3- Amru. 4- Qaasim.  5- Abdallah.  6- Abdur rahman. 7- Hussein bin Hassan. 8- Twalha. 9- ummul Hassan. 10- ummul  Hussein  11- Fatima binti Ummu Is’haaq. 12- Ummu Abdallah.  13- Fatima bintil Hassan  14-  Ummu Salamah binti Hassan. 15- Ruqayya binti hassan, na wengineo.

NEMBO YA  PETE YAKE.

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo, (Al izzatu lillahi wahdahu), na inasemekana kuwa kuna nembo nyingine tofauti na hii.

UMRI WAKE (A.S).

Ali shi kwa muda wa miaka 47.

MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).

Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 10.

WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).

Muawia bin abii sufyaan.

TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).

Alikufa  shahidi tarehe 6 mwezi wa Safar mwaka 49 hijiria, na inasemekana  alifariki tarehe 28 safar mwaka 50 hijiria.

SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S).

Alifia katika mji wa  Madinatul munawwarah.

SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).

Alilishwa  sumu na muawia kupitia mkewe   alie kuwa akiitwa  Juudah bintil ash’ath.

SEHEMU ALIPO ZIKIWA (a.s).

Alizikwa kwenye makaburi ya baqii yaliyoko kwenye mji wa Madintul munawwarah.

Kwa ufafanuzi zaidi  rejea kitabu Buharul an’waar juzu ya 39-40 kwa wenye kufahamu lugha ya kiarabu.