HISTORIA  FUPI  YA FATIMA ZAHRAA  (A.S)

JINA  LAKE  NA NASABU  YAKE (A.S).

Jina lake ni Fatima binti wa  Mohammad  (s.a.w) bin abdallah bin abdul mutwalib.

MAMA  YAKE (A.S).

Mama yake ni  Khadija  binti Khuwailid.

KUNIA YAKE (A.S).

Kunia yake ni 1- ummu  abiiha. 2- Ummul hassanaini. 3-  Ummul aimmah. 4-  Ummur rihaanataini, na mengineyo.

JINA LAKE  MASHUHURI (A.S).

Jina lake mashuhuri ni  1-  Zahraa. 2-  Al batuul.3-  Swiddiiqah. 4-  Mubaraakah. 5- Twahira. 6- Zakiyyah. 7- Radhiyyah. 8- Mardhiyyah.  9-  Al muhaddathah,  na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).

Fatima  Zahraa alizaliwa tarehe 20  jumadal  Aakhir mwaka wa tano wa utume  kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashia, na kuna kauli zingine  zisemazo kuwa alizaliwa katika tarehe tofauti na hiyo.

MAHALA  ALIPO  ZALIWA (A.S).

Alizaliwa katika mji mtukuu  wa makka.

KUOLEWA KWAKE (A.S).

Aliolewa na  Amirul  muuminina Ally bin abii twalib (a.s)

WATOTO  WAKE (A.S)

Ali ruzukiwa  watoto  wafuatao: 1- Hassan (a.s)  2- Hussein (a.s)  3-  Zainabul kubraa.  4-  Zainabu As-sughraa.

NEMBO  YA PETE  YAKE (A.S).

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo:  (Aminal  mutawakkiluun).

MTUMISHI  WKE (A.S).

Mtumishi  wake alikuwa akiitwa    Fidhwah.

UMRI WAKE.

Ali ishi kwa muda wa miaka 18 kutokana  na kauli iliyo mashuhuri. Na kuna kauli zingine tofauti na hiyo.

KUFARIKI  KWAKE.

Alifariki Dunia tarehe 3 jamaadal  Aakhir mwaka wa 11 hijiria, na riwaya nyingine inasema kuwa alifariki tarehe13 jamaadul   ulaa, na kuna kauli nyingine tofauti na hizo.

SEHEMU  ALIPO ZIKIWA.

Alizikwa  katika mji wa madinatul munawwarah, na kuna tofauti  kuhusiana na sehemu ya kaburi lake.

Kwa   ufafanuzi zaidi  rejea katika kitabu Buharul an’waar, juzu ya  39, kwa wenye kufahamu lugha ya kiarabu.