JINA LAKE NA NASABU YAKE.
Jina lake ni Ally bin abi twalib bin abdul mutwalib bin haashim bin abdul manafi.
MAM YAKE.
Mama yake ni Fatima binti asad bin haashim bin abdul manafi.
KUNIA YAKE.
Kunia yake ni 1- Abul Hasssan. 2- Abul Hussein. 3- Abu sibtwain. 4- Abu rihanatayni. 5- Abu turab. na mengineyo.
MAJINA YAKE MSHUHURI.
1- Amirul muuminin. 2- Sayyidul muslimiin. 3- Imamul muttaqiin. 4- Qaidul ghuril muhajjalin. 5- Sayyidul awswiyaa. 6- Sayyidul arab. 7- Al murtadhaa. 8- yaasubud diin. 9- Haydar. 10- Al anzaul batwiin. 11- Asadullah. Na mengineyo.
TAREH YA KUZALIWA KWAKE (A.S).
Alizaliwa tarehe 13 mwezi wa Rajab baada ya mwaka wa tembo kwa miaka 30 baada ya kuzaliwa mtume (s.a.w)
SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S).
Alizaliwa katika mji wa makka (ndani ya kaaba tukufu).
VITA ALIVYO PIGANA (A.S).
Alishiriki katika vita vyote vya Mtume (s.a.w) isipokuwa vita vya Tabuuk kwani Mtume (s.a.w) alimuamuru kubakia katika mji wa madinatul munawwarh na alifanya hivyo kwa ajili ya kusimamia mambo ya mji huo Mtume akiwa hayupo, ama vita ambavyo alivyo viendesha yeye menyewe katika zama za utawala wake ni kama vifuatavyo: 1- Vita vya Jamal. 2- vita vya swiffin. 3- vita vya Nahrawaan.
WAKEZE (A.S)
1- Fatima Zahraa (a.s) binti wa Mtume (s.a.w), 2- Umamah binti Abil Aasi, 3- Ummul baniin Al kilaabiyyah, 4- Laylaa binti Mas’ood, 5- Asmaa binti Umais, 6- Aswahbaau binti Rabiiah (Umm Habiib) 7- Khawlah binti Jaafar. 8- Ummu Saad binti Ur’wah. 9- Makhba’atu binti Imri’il Qaisi.
WATOTO WAKE (A.S)
Wana historia wame tofautiana kuhusu idadi ya watoto wake Imam (a.s) lakini riwaya
zimekuwa zikizungumzia
kati ya 25 na 33, na hapa
tuta taja walio mashuhuri kati
1- Imam Hassan bin Ally (a.s). 2- Imam Hussein bin Ally (a.s). 3- Ummul maswaaib Zainabul Kubraa (a.s). 4- Zainab Assughraa. 5- Al abbas (Abul fadhli) 6- Mohammad Al awsat. 7- Jaafar. 8- Abdallah. 9- Othumaan. 10- Mohammad binil Hanafiyyah. 11- Yahyaa. 12- Ummu Haaniy. 13- Maymuunah. 14- Jumanah (Ummu Jaafar). 15- Nafiisah.
NEMBO YA PETE YAKE (A.S)
Nembo ya pete yake ilikuwa kama ifuatavyo: (Al mulku lillahil waahidul qahaar), na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.
UMRI WAKE (A.S).
Ali ishi kwa muda wa miaka 63.
MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S).
Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 30.
TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Imam Ally alikufa shahidi tarehe 21 mwezi wa Ramadhan mwaka 40 hijiria.
SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).
Alikufa shahidi kutokana na dharuba alilo pigwa na mal uun Abdurrahmaan bin muljim Al muraadiy kwa upanga kichwani kwake (a.s) akiwa katika hali ya sijda kwenye mihraab ya msikiti wa Al kufa.
SEHEMU ALIPO ZIKIWA (A.S).
Alizikiwa katika mji wa (Najaful ashraf ), katika sehemu iitwayo Al harraa.