HISTORIA  FUPI  YA MTUME (S.A.W)

JINA  LAKE NA NASABU  YAKE.

Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul mutwalib bin hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim  (A.S)

MAMA  YAKE.

Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin zuhra bin kilaab.

KUNIA YAKE NI:

Abul qaasim, pia Abuu Ibrahiim.

JINA  LAKE  MASHUHURI.

1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa  ndani ya Qur’ ani tukufu kama:

2- Khaatamun nabiyyiin. 3- Al ummiyyi. 4-  Al muzammil. 5- Al mudathir. 6-  Al mubiin. 7-Al kariim.

8- An nuur. 9- An niima. 10-  Ar rahmaan. 11- Ash shaahid. 12- Al mubashir.13-  An nadhiir. 14- Abdur rauuf.    15- Ar rahiim. 16- Ad daai  na mengine mengi.

TAREHE  YA KUZALIWA KAKE.

Alizaliwa tarehe  17 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka  wa tembo sawa na mwaka  571 H.D.kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashie, na kauli nyingine inasema ya kuwa alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Rabiul awwal mwaka huo huo.

SEHEMU  ALIPO  ZALIWA.

Alizaliwa katika mji wa makkatul  mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.

KUPEWA  KWAKE  UTUME.

Ali pewa rasmi utume tarehe  27 mwezi wa rajab katika mji wa makka baada ya kutimiza miaka  40 ya umri wake mtukufu.

MAFUNDISHO  YAKE.

Mtume (s.a.w) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe wote, na alikuwa akilingania udugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye Dini ya ki islaam, kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu alizo zipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika,  kisha waislaam wakazipokea kutoka kwa Mtume (s.a w).

MIUJIZA  YAKE.

Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’ ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi sana kwani hai hesabiki.

WITO  WAKE.

Mtume (s.a.w) ali walingania  watu  kwenye   upweke wa Mwenyezi Mungu katika mji wa makka na kwa njia ya siri kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia ya wazi kwa muda wa miaka kumi.

KUHAMA KWAKE.

Alihama kutoka katika mji wa makka kwenda madina  mwanzoni mwa mwezi wa rabiul awwal baad ya kupita miaka  13 tangu kupewa utume, na kuhama huko kulitokana na maudhi mengi ya makuraishi, mushrikina na mkafiri  kumuelekea yeye na maswahaba wake.

 VITA  VYAKE.

Mwenyezi Mungu alie takasika  alimpa idhini ya kuwapiga vita mushrikina na makafiri na wanafiki, na baada ya idhini hiyo aliweza kuingia kwenye mapambano na watu hao kwenye vita vingi sana, na kati ya hivyo vilivyo  kuwa mashuhuri ni  Badri, Uhudi, Khandaq (Al ahzaab) Khaibar, na  Hunain.

WAKEZE  MTUME (S.A W).

 Mtume alikuwa na wanawake kadhaa: Wakwanza ni  Khadija binti Khuwailid (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake),na huyu ndie mwanamke wa kwanza wa Mtume (s.a.w), ama wengine ni : 2-Sauda binti zum’a, 3- Aisha binti abi baker, 4- Ghuzya binti dudaan (ummu shariik) 5- Hafswa binti omar, 6- Ramla binti abii sufyan (ummu habiibah), 7- Ummu salmah binti umayyah, 8-  Zainab binti Juhsha,  9- Zainab  binti Khaziimah,  10- Maimuna bintil Harithi, 11- Juwairia bintil Haarithi, 12- Swafia binti Hayyi bin Akhtwab.

WATOTO  WAKE MTUME (S.AW).

Watoto wake ni kama wafuatao:  1- Abdallah.  2- Qaasim.  3- Ibrahiim (a.s)  4- Fatimatuz  zahraa (a.s).na kuna kauli zingine zisemazo kuwa  Zainab, Ruqayya, na ummu kulthum  ni wanawe pia.

BABA  ZAKE WADOGO.

Mtume (s.a.w) ana  baba wadogo  tisa (9), nao ni watoto wa abdul mutwalib   kama wafuatao:  1- Al haarith. 2- Zubair. 3- Abu twalib. 4- Hamza. 5- Al ghidaaq, 6- Dharaar  Al muqawwim, 7- Abu lahab. 8- Al abbas.

SHANGAZI  ZAKE  MTUME (S.AW).

Mtume (s.a.w) alikuwa na shangazi sita kutokana na akina mama tofauti nao ni kama wafuatao: 1- Umaimah.  2- Ummu hakiimah.  3- Burrah.  4- Aatikah. 5- Swafiyyah.  6- Arwy.

MAWASII   WAKE  MTUME (S.A.W).

Mawasii wake ni kumi na mbli,nao ni kama wafuatao: 1- Amirul muuminnina  Ally bin abii twalib (a.s).  2- Hassan bin Ally (a.s)  3- Hussein bin  Ally  (a.s)  4- Ally bin Hussein (a.s).  5- Mohammad bin Ally ( a.s)   6- Jaafar bin Mohammad (a.s) 7- Mussa bin Jaafar (a.s)  8- Ally bin Mussa  (a.s)   9- Mohammad bin Ally  (a.s)   10- Ally bin Mohammad (a.s)  11- Hassan bin Ally  (a.s)  12- Al hujjat binil Hassan   (Mohammad mahdii )  (a.s).

MLINZI WAKE.

Mlinzi wake alikuwa ni Anas.

WAIMBAJI  MASHAIRI WA  MTUME (S.A.W).

1 – Hassan bin Thabiti.  2- Abdallah bin Rawaha.  3- Kaab bin Maalik.

WAADHINI    WA MTUME (S.A.W).

1- Bilal  Al –habashi   2- Ibnu ummu makhtuum.  3- Saad Al-qurt.

NEMBO  YA PETE YA MTUME (S.A.W).

Nembo  ya pete yake ilikuwa ni  (( Mohmmad  rasuulu llah)).

UMRI  WAKE (S.A.W).

Ali ishi kwa muda wa miaka 63.

MUDA  WA UTUME  WAKE (S.A.W).

Utume wake ulidumu kwa muda wa miaka 23.

TAREHE YA KUFARIKI  KWAKE  (S.A.W).

Alifariki dunia tarehe 28 mwezi  wa  safar mwaka wa 11 hijiria.

SEHEMU ALIYO FIA (S.A.W).

Mtume alifia katika mji wa madinatul munawwarah.

SEHEMU  ALIYO ZIKIWA (S.A.W).

Alizikiwa katika mji wa madina ndani ya nyumba  yake tukufu.

Kwa  ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu  Buharul an’waar  juzuu ya 15-16,kwa wale wenye kufahamu lugha ya kiarabu.